Fisi auawa, ameandikwa jina kwenye paja

Habari Leo
Published: Feb 21, 2025 13:38:42 EAT   |  Travel

Askari wa Mamlaka ya wanyamapori kwa kushirikiana na askari kutoka Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA) na Jeshi…

The post Fisi auawa, ameandikwa jina kwenye paja appeared first on HabariLeo.

Askari wa Mamlaka ya wanyamapori kwa kushirikiana na askari kutoka Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA) na Jeshi la Polisi wamemuua fisi ambaye amekutwa ameandikwa jina katika eneo la paja lake katika Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu.

Askari wa vikosi hivyo wapo wilayani humo kwenye operesheni maalumu ya kuwasaka fisi kwenye makazi ya wananchi ambapo hivi karibuni wamesababisha vifo vya watoto.

Fisi huyo ameuawa katika Kijiji cha Kimali kilichopo Kata ya Nyamalapa ambapo kwa mshangao wa wengi fisi huyo amekutwa na alama ya jina kwenye paja lake la kushoto.

Jina hilo lisomeka ‘MALLA N 7’ na kwamba bado haijajulikana maana yake.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwamigagani kata ya Mwalushu, Mkuu wa wilaya ya Itilima, Anna Gidarya  amewataka wananchi wote wanaomiliki nyara za serikali kinyume chaa sheria za wanyamapori wilayani humo kuzisalimisha haraka iwezekanavyo kwa wahusika wa uhifadhi kabla ya hatua kali hazijachukuliwa dhidi yao.

Kumekuwa na matukio ya fisi kushambulia watoto kuanzia majira ya saa moja usiku katika maeneo tofauti katika wilaya ya itilima ambapo mpaka sasa fisi 16 wameuwawa na kikosi kazi cha askari wa TAWA, TANAPA na jeshi la polisi Wilayani humo.

The post Fisi auawa, ameandikwa jina kwenye paja appeared first on HabariLeo.