Kamati: Rombo ipewe kipaumbele mpango matumizi ya ardhi

MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi Maliasili na Utalii, Timotheo Mzava imeiomba serikali kupitia Wizara ya Ardhi…
The post Kamati: Rombo ipewe kipaumbele mpango matumizi ya ardhi appeared first on HabariLeo.
MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi Maliasili na Utalii, Timotheo Mzava imeiomba serikali kupitia Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuipa kipaumbele Halmashauri ya Wilaya ya Rombo katika mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Mzava amesema hayo Machi 15, 2025 katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Kisale Msalanga katika ziara ya kamati kukagua mradi wa upangaji wa matumizi ya ardhi mkoani Kilimanjaro.
“Eneo hili nikubwa na nilazima litumike na jamii ilikuleta maendeleo ya nchi pamoja na mtu mmoja hivyo naomba serikali kupitia wizara hii itoe kipaumbele kwa halmashauri hii katika mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa mwaka huu wa fedha,”amesema Mzava
Aidha, Mzava amekabidhi jumla ya hakimiliki za kimila 390 kwa wananchi hao ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ibara ya 74 inayoelekeza kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi, kuandaa mipango kina katika kuimarisha salama za miliki kwa kuwezesha utoaji wa hati za hakimiliki za kimila kwa wananchi.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Geophrey Pinda amesema, jukumu la upangaji wa matumizi ya ardhi katika vijiji 24 kati ya 68 vya Halmashauri ya Wilaya ya Rombo ni suluhisho la migogoro ya Ardhi na mipaka katika vijiji hivyo kwani tayari vimekwisha wekewa mpango wa matumizi bora ya Ardhi.
Pinda amekemea vikali vitendo vya baadhi ya wenyeviti wa vijiji wasio waadilifu kwa kujishughulisha na uuzaji wa maeneo ya vijiji kiholela na hivyo kuchochea migogoro ya ardhi.
Katika Mwaka wa fedha 2024/25 Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi iliidhinishiwa jumla ya Sh bilioni 5 ili kuweza kutekeleza kazi za Maendeleo kupitia mradi wa upangaji matumizi ya ardhi katika vijiji 280 vilivyopo maeneo yaliyopitiwa na miradi ya bwawa la Julius Nyerere, mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki na reli ya mwendokasi pamoja na maeneo yenye migogoro katika vijiji 975 vyenye maelekezo ya baraza la mawaziri vilivyopo mipakani mwa nchi.
The post Kamati: Rombo ipewe kipaumbele mpango matumizi ya ardhi appeared first on HabariLeo.