DC Tanga awataka wananchi kujiepusha na vitendo vinavyochochea uharibifu wa mazingira

Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Japhari Kubecha, amewataka wakazi wa Amboni kujiepusha na vitendo vinavyochochea uharibifu wa mazingira, akisisitiza umuhimu wa kutunza hifadhi ya Amboni ili iendelee kuwa kivutio chenye hadhi kwa maendeleo endelevu. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Diko la Amboni iliyoandaliwa na Hifadhi ya Ngorongoro, Kubecha alisisitiza kuwa juhudi za kulinda mazingira […]
The post DC Tanga awataka wananchi kujiepusha na vitendo vinavyochochea uharibifu wa mazingira first appeared on Millard Ayo.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Japhari Kubecha, amewataka wakazi wa Amboni kujiepusha na vitendo vinavyochochea uharibifu wa mazingira, akisisitiza umuhimu wa kutunza hifadhi ya Amboni ili iendelee kuwa kivutio chenye hadhi kwa maendeleo endelevu.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Diko la Amboni iliyoandaliwa na Hifadhi ya Ngorongoro, Kubecha alisisitiza kuwa juhudi za kulinda mazingira ni sehemu ya mpango wa kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuutangaza utalii wa Tanzania.
“Ni jukumu letu sote kuhakikisha tunalinda hifadhi ya Amboni ili ivutie watalii wengi zaidi, hivyo kuimarisha uchumi wa jamii zetu na taifa kwa ujumla,” alisema Kubecha.
Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Hifadhi ya Ngorongoro, Mariam Kobelo, amesema kuwa kuna mipango inayoendelea ili kuhakikisha mapango ya Amboni yanakuwa sehemu salama kwa watalii.
Alieleza kuwa hatua mbalimbali za kuboresha miundombinu ya eneo hilo zinafanyika ili kuongeza idadi ya watalii na kukuza mapato.
“Tunalenga kuboresha miundombinu ya Amboni ili wageni wafurahie mandhari na historia ya eneo hili. Pia tunapanga kutumia nishati ya gesi kwenye Diko la Amboni ili kupunguza madhara ya kiafya na kutunza mazingira,” alisema Kobelo.
The post DC Tanga awataka wananchi kujiepusha na vitendo vinavyochochea uharibifu wa mazingira first appeared on Millard Ayo.