ARUSHA: NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii anayeshughulikia Maliasili Kamishna wa Polisi, Benedict Wakulyamba amesema Wahasibu wa Wizara hiyo na Taasisi zake ni chachu na nguzo muhimu ya kufanikisha malengo ya Wizara na Serikali kwa ujumla, kutokana na jukumu la ukusanyaji, usimamizi na udhibiti wa matumizi ya fedha za umma
Wakulyamba ameyasema hayo leo Februari 13 jijini Arusha wakati akifungua kikao kazi cha kuwajengea uwezo wahasibu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zake ambapo amesema licha ya mafunzo hayo kuwaongezea uwezo pia yatawasaidia katika kuwaongezea ujuzi na maarifa ya usimamizi wa mambo ya fedha katika taasisi na wizara kwa ujumla
“Ni matarajio yangu kuwa mafunzo haya yatakua endelevu kila mwaka ili kuwajengea uwezo katika utekelezaji wa majukumu yao na kupelekea kufanikisha matarajio ya serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye mbeba maono makubwa katika kukuza sekta ya utalii kwa vitendo,” amesema CP. Wakulyamba
Picha ya pamoja kwenye kikao kazi cha kuwajengea uwezo wahasibu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zake
Katika hatua nyingine, C.P Wakulyamba amewataka wahasibu wakuu wa Wizara hiyo na Taasisi zake kuwa washauri wazuri kwa viongozi wao ili kuepukana na changamoto za kikanuni za matakwa ya kifedha kulingana na miongozo kwa kubainisha mapungufu wakati wa ufungaji wa hesabu na kasoro katika kujibu hoja za ukaguzi wa ndani na hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
“Sisi kama viongozi tunawategemea sana nyinyi ili tusiharibu, tunategemea ushauri wenu kwa kusimamia sheria, kanuni na taratibu zaa fedha katika kusimamia matumizi ya Serikali,” amesema CP. Wakulyamba
SOMA: Wahasibu wapewa kipaumbele katika uchumi
Kwa upande wake Mhasibu Mkuu wa Wizara hiyo, Paul Kabale amepongeza uongozi wa Wizara na wahasibu na Taasisi zake kwa kuendelea kupata hati safi kwa ukaguzi wa mwaka wa fedha 2022/2023 kutokana na usimamizi bora wa fedha za umma na makusanyo ya maduhuli ya serikali ndani ya wizara
“Na hii inatokana na ushirikiano na mahusiano mazuri baina yetu katika utekelezaji wa majukumu ikiwemo uandaaji mzuri wa taarifa za fedha na hesabu za majumuisho na kujibu kwa ufasaha hoja za ukaguzi.” Amesema Kabale
Moja ya washiriki akichangia kwenye kikao kazi cha kuwajengea uwezo wahasibu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zake
Wakizungumza nje ya kikao hicho baadhi ya washiriki wa kikao hicho licha ya kushukuru uongozi wa wizara hiyo kwa kuwapatia mafunzo hayo wamesema mafunzo hayo yatawaongezea uwezo mkubwa katika usimamizi wa fedha na kuwa washauri wazuri kwa viongozi wao katika usimamizi wa fedha za umma na uwekezaji
Kikao hicho kilichoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kimeendeshwa na wawezeshaji kutoka Wizara ya Fedha na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kikilenga kuwakumbusha wahasibu wa Wizara hiyo na Taasisi zake wajibu wao wa kuzingatia Sheria ya Fedha Sura Na.348 inayoelezea jukumu la usimamizi wa fedha za umma kwa lengo la kuhakikisha udhibiti na ufanisi.
The post Naibu Katibu Mkuu Maliasili awanoa wahasibu appeared first on HabariLeo.
Naibu Katibu Mkuu Maliasili awanoa wahasibu

This story was originally published by Habari Leo.
Read the full story at Habari LeoRelated stories
TravelMiss World Kufungua Milango ya Utalii
ZANZIBAR imeendelea kujitokeza kama moja ya vivutio muhimu vya utalii nchini, safari hii ikipokea ugeni wa Miss World 2026, Joheirry Molla aliyewasili visiwani humo Novemba 19, 2026, akiwa ameambatana na warembo kutoka mabara sita.
TravelAskari Tanapa, TFS mbaroni mauaji ya wabeba mkaa
KAGERA; Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera linawashikilia askari 13, wakiwemo wa wanyamapori wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), askari wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na askari mgambo, kwa tuhuma za mauaji ya watu wanne yaliyotokea Kijiji cha Kanyamika, Kata ya Karambi, Tarafa ya Kimwani, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera. Taarifa…
TravelNgorongoro scoops continental gong
ACCRA: THE Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA) has won the Excellence in Sustainable Tourism and Conservation Management Award at the Africa Business Forum & Awards 2026. The award recognises Ngorongoro’s contribution to biodiversity conservation, sustainable tourism development and the protection of its outstanding natural and cultural heritage. The awards ceremony was held in Accra, Ghana,…
TravelDk Kijaji: Mashindano makubwa gofu Afrika kufanyika Serengeti
MARA; Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Ashatu Kijaji, amesema Uwanja wa Gofu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti utawezesha Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano makubwa ya gofu ya Afrika na kimataifa, hatua inayotarajiwa kuongeza idadi ya watalii, mapato na kuitangaza nchi kupitia utalii wa michezo. Akizungumza leo Oktoba 18, 2026, wakati wa uzinduzi wa…