Top headlines and developing stories from Tanzania, Kenya, Uganda and the wider region, gathered from the leading local and international newsrooms and updated throughout the day.
Makala hii inaeleza namna uwepo wa kambi za kijeshi za mataifa ya kigeni barani Afrika unavyoibua mjadala kuhusu usalama, uhuru wa mataifa na ushindani wa madola makubwa duniani. Mazingira ya usalama barani Afrika yanazidi kuwa na uwepo wa majeshi ya mataifa mbalimbali ya kigeni, huku serikali zikikabiliwa na changamoto ya kusawazisha mahitaji ya usalama wa…
DAR ES SALAAM; Chama cha Mafundi Rangi na Ujenzi Tanzania (CHAMARAUTA) kimeiomba Serikali na wadau wa sekta ya ujenzi kuwapa mafundi nchini fursa za kushiriki katika miradi mbalimbali ya ujenzi ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi na kuboresha maisha yao. Mwenyekiti wa CHAMARAUTA, Juma Chakusaga, ametoa wito huo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kusitishwa kwa…
Madini muhimu, nishati, miundombinu, teknolojia, njia za biashara, ushirikiano wa kiusalama na ushawishi wa kisiasa vinazidi kuwa sehemu ya ushindani wa mataifa yenye nguvu kutafuta ushirikiano mpana zaidi barani Afrika. Afrika imekuwa miongoni mwa maeneo muhimu katika ushindani wa kisiasa na kimkakati duniani, huku Marekani, China, Russia na Umoja wa Ulaya wakizidisha jitihada za kujenga…
DAR ES SALAAM: Sera ya muda mrefu ya Tanzania ya kutofungamana na upande wowote inakabiliwa na mtihani mpya wa kijiografia kutokana na kuongezeka kwa ushindani kati ya mataifa yenye nguvu duniani, ikiwamo Marekani, China, Russia, India na mataifa mengine, ambao unazidi kuenea barani Afrika. Badala ya kuchagua upande mmoja wa nguvu za kisiasa duniani, mfumo…
KUGUNDULIWA kwa mamia ya miili katika makaburi ya kina kifupi katika Msitu wa Shakahola, Kaunti ya Kilifi, kuanzia Machi 20, 2023, ulifichua mkasa uliotokana na miaka mingi ya itikadi kali za kidini. Kiini cha mkasa huo kilikuwa mhubiri Paul Mackenzie, aliyeaminisha wafuasi wake kuwa kufunga hadi kufa kungewasaidia kukutana na Yesu. Mackenzie alianzisha kanisa la Good News International (GNI) mnamo 2003 ila likasajiliwa rasmi mnamo 2010. Mnamo 2012, huduma hiyo ilisajili kampuni ya Good News Media (K) Limited, iliyoendesha kituo cha televisheni cha Times TV mjini Malindi. Kwa miaka mingi, shughuli zake ziliibua wasiwasi kuhusu itikadi kali, elimu ya watoto na kukataa matibabu ya kisasa. Wafuasi waliitwa Wateule na kufundishwa kuachana na mali za dunia, huku serikali ikisawiriwa kama adui. Mnamo 2017, Mackenzie alikabiliwa na mashtaka yaliyohusiana na kueneza itikadi kali na kuendesha taasisi ya elimu isiyosajiliwa. Katika kesi moja, aliachiliwa baada ya makubaliano na upande wa mashtaka na kuamriwa kudumisha tabia njema. Katika kesi nyingine, aliachiliwa kwa dhamana na hatimaye akaachiliwa huru mnamo 2021. Mnamo mwaka huo huo, watoto 43 wenye umri wa kati ya mwaka mmoja na 13 waliokolewa kutoka katika majengo ya GNI eneo la Mayungu. Ripoti zilisema baadhi yao walizuiliwa, kunyimwa elimu na kufundishwa dini. Mahakama iliagiza wapate ushauri nasaha na matibabu kabla ya kurejeshwa kwa familia zao. Mnamo 2019, Kamati ya raia wa Mahakama ya Kaunti ya Kilifi ilijadili malalamishi kuhusu kuenezwa kwa itikadi kali kwa watoto kupitia kanisa na televisheni ya Mackenzie. Mamlaka ya Mawasiliano baadaye ilifuta leseni ya Times TV. Mackenzie pia alishtakiwa kwa kusambaza filamu zisizokaguliwa na kuendesha studio bila leseni. Mnamo Novemba 10, 2023, alipatikana na hatia ya makosa hayo na kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na miezi sita, lakini akaachiliwa huru kuhusu shtaka la kuchochea watu kukiuka sheria. Wakati huo, baadhi ya wafuasi wake walikuwa wameanza kuhamia Shakahola mnamo 2019, huku idadi ikiongezeka wakati wa janga la Corona. Upande wa mashtaka ulisema walifundishwa kufunga hadi kufa ili waende mbinguni, huku watoto wakitarajiwa kufa kwanza, wakifuatiwa na wanawake kisha wanaume. Mackenzie na washukiwa wenzake 30 baadaye walishtakiwa kwa mauaji ya watoto 191. Wote walikana mashtaka. Mahakama Kuu ya Malindi iliamuru mnamo 2024 mashtaka hayo yapunguzwe yasizidi 12, lakini Mahakama ya Rufaa ilirejesha mashtaka yote 191 Aprili 11, 2025. Kesi ilianza kusikilizwa Agosti mwaka jana baada ya mvutano wa kisheria, na hukumu ikatolewa katika Mahakama Kuu ya Mombasa Jumatatu. Baada ya mkasa huo kufichuliwa, JSC ilisema ingechunguza jinsi kesi za awali za Mackenzie zilivyoshughulikiwa ili kubaini iwapo kulikuwa na mapungufu katika utoaji wa haki. Mkasa wa Shakahola umeibua maswali kuhusu jinsi mamlaka zilivyoshughulikia tahadhari kadhaa za awali na iwapo kuchukuliwa kwa hatua za mapema zingeweza kuzuia vifo hivyo.
DODOMA: THE Parliamentary Standing Committee on Administration, Constitution and Legal Affairs has called for intensified public education on FAIDA Fund to boost participation among public servants, saying greater awareness could help workers grow their savings, improve their financial security and prepare for home ownership. The call follows the fund’s growth in net asset value to…
VYAMA vya kisiasa vinaendelea kuongezeka nchini huku viongozi wakijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu wa Agosti 2027, hali inayoibua maswali kuhusu iwapo miungano hiyo inasukumwa na sera au maslahi ya kisiasa. Afisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa (ORPP) imetoa vyeti kamili vya usajili kwa vyama vingine sita na kufikisha jumla ya vyama vilivyosajiliwa kikamilifu 107. Zaidi ya vyama 30 vingine vina usajili wa muda, ikilinganishwa na vyama 90 vilivyokuwepo kabla ya uchaguzi wa 2022. Wachanganuzi wanasema baadhi ya viongozi wanaanzisha au kupata umiliki wa vyama ili kudhibiti tiketi za uteuzi, kuimarisha nafasi zao katika mazungumzo ya miungano na kupata manufaa ya kifedha. Miongoni mwa vyama vipya ni Mwongozo Mpya Party (MMP), Imarisha Uchumi Party (IUP), United Super Alliance Party (USAP), Forward Kenya Party (FKP), People’s Prosperity Party (PPP) na Freedom and Opportunity Party (FOP). Aliyekuwa Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Eliud Owalo, aliyeanzisha PPP, amesema chama hicho kitalenga urais na pia kusimamisha wagombeaji katika nyadhifa zote za uchaguzi. Msajili wa Vyama vya Kisiasa, John Cox Lorionokou, amevitaka vyama kuzingatia katiba zao na kuhakikisha vijana pamoja na watu wenye ulemavu wanapata nafasi sawa za kushiriki katika shughuli za kisiasa. Vyama vingine vilivyoibuka ni Democracy for the Citizens Party (DCP) kinachohusishwa na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, People’s Renaissance Movement cha Caleb Amisi na United Progressive Movement (UPM) kinachohusishwa na Boni Khalwale. Viongozi wengine waliamua kupata umiliki wa vyama vilivyokuwapo badala ya kuanzisha vipya. Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna amejipatia The Equitable Party (TEP), huku Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino akijipatia Muungano Party na kukibadilisha jina kuwa Mwananchi Party (TMP). Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro amepata People’s Party of Kenya (PPK), huku Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya akihusishwa na United Democratic Party. Umiliki wa chama huwapa viongozi mamlaka ya kisheria ya kusimamia uteuzi wa wagombeaji na kuamua tiketi zitakazotolewa. Vyama pia hukusanya ada za uteuzi, ambazo zinaweza kufikia Sh50,000 kwa kila wadhifa. Aidha, vyama vinaweza kupata fedha kutoka kwa Hazina ya Vyama vya Kisiasa kulingana na matokeo ya uchaguzi. Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Kisiasa ya 2022 yaliongeza vyama vinavyoweza kunufaika na mgao kutoka kwa hazina hiyo. Asilimia 70 ya fedha hizo hugawanywa kulingana na kura zilizopatikana, asilimia 15 kwa kuzingatia wawakilishi waliochaguliwa kutoka makundi maalumu, huku asilimia 10 ikitegemea idadi ya wawakilishi waliochaguliwa. Asilimia tano hutumiwa na ORPP kwa usimamizi. Vyama pia hupata nafasi za uteuzi katika Bunge la Kitaifa, Seneti na mabunge ya kaunti.
SERIKALI za kaunti zinatarajiwa kupokea Sh71.09 bilioni zaidi katika mwaka wa kifedha wa 2026/2027, baada ya Rais William Ruto kutia saini sheria mpya inayolenga kuimarisha uwajibikaji katika matumizi ya fedha za umma. Rais alitia saini Mswada wa Fedha za Ziada kwa Serikali za Kaunti 2026 kuwa sheria katika Ikulu ndogo ya Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu, jana kabla ya maadhimisho ya Siku ya Mashujaa leo. Fedha hizo zimeongezeka kwa Sh425.6 milioni kutoka Sh70.67 bilioni zilizotengewa kaunti katika mwaka wa kifedha wa 2025/2026. Sheria hiyo mpya pia inamtaka Waziri wa Hazina ya Kitaifa kuchapisha ripoti kila baada ya miezi mitatu kuhusu fedha zilizohamishiwa kwa serikali za kaunti. Ripoti hizo zinapaswa kutolewa ndani ya siku 30 baada ya kumalizika kwa kila robo mwaka. Mswada huo ulidhaminiwa na Seneta Ali Roba, mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Seneti kuhusu Fedha na Bajeti. Ulichapishwa Machi 16, 2026, na kusomwa kwa mara ya kwanza katika Seneti Aprili 2. Seneti iliupitisha pamoja na marekebisho Juni 17, kabla ya Bunge la Kitaifa kuupitisha pia kwa marekebisho Agosti 4. Seneti ilikubaliana na marekebisho ya Bunge la Kitaifa Oktoba 6, na hivyo kupisha mchakato wa Rais kutia saini mswada huo. Kati ya fedha hizo, Sh56.38 bilioni ni mgao wenye masharti unaofadhiliwa kupitia mikopo na ruzuku kutoka kwa washirika wa maendeleo. Nazo Sh12.73 bilioni zitatokana na mgao wa mapato ya serikali ya kitaifa, huku Sh1.83 bilioni zikitokana na mirabaha ya madini inayostahili kaunti.
MAHAKAMA Kuu jana ilimpata mhubiri matata Paul Mackenzie na washukiwa wenzake 30 na hatia ya kushirikiana, kutekeleza na kudumisha mfungo uliosababisha vifo vya mamia ya watoto na watu wazima katika msitu wa Shakahola, Kilifi. Katika uchambuzi wake wa mashtaka 191 ya mauaji, Jaji Diana Kavedza alisema vifo hivyo vilisababishwa na vitendo na uzembe usio halali wa watu waliotekeleza na kudumisha mfungo huo, badala ya kuwa matokeo yasiyokusudiwa ya shughuli za kidini. “Baada ya kuzingatia ushahidi wote, mahakama hii imebaini kuwa washtakiwa ambao ushiriki wao binafsi umethibitishwa walitenda kwa pamoja utekelezaji wa lengo moja lisilo halali la kuanzisha na kudumisha mfungo uliosababisha vifo vya watu wengi Shakahola,” akasema Jaji Kavedza. Jaji huyo alibaini kuwa ingawa kila mshtakiwa alikuwa na jukumu tofauti, vitendo vyao vilikuwa sehemu ya mpango mmoja wa uhalifu. Hata hivyo, kila mmoja alipaswa kuwajibishwa kwa msingi wa ushahidi unaoonyesha ushiriki wake na nia yake ya kutenda uhalifu. Kabla ya kuchambua mashtaka ya mauaji, mahakama pia ilibainisha kuwa ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka uliibua maswali kuhusu uwezekano wa vitendo hivyo kuchukuliwa kama uhalifu dhidi ya binadamu. Jaji Kavedza alikataa hoja kwamba watoto waliofuata maagizo na kuendelea kufunga hadi kufa walikuwa wameamua kufanya hivyo kwa hiari yao wenyewe. Alisema watoto wenye umri wa kati ya miaka sita na 10 hawakuwa na uwezo wa kutafakari kwa kina na kuelewa kuwa kifo ni cha kudumu. Mawazo yao, tabia ya kutenda bila kufikiria na uelewa wao mdogo viliwafanya kuwa rahisi kudanganywa. “Kwa hivyo, inawezekana watoto katika kundi hili, kutokana na msisimko wa shahidi huyu, licha ya kuonekana kama mifupa iliyofunikwa kwa ngozi, waliamini kuwa kifo kinaweza kubatilishwa,” akasema . Alibaini kuwa watoto hao hawangeweza kutoa ruhusa ya hiari, yenye ufahamu na inayokubalika kisheria ya kujinyima chakula hadi kufa. Mahakama ilisema kutokupinga maagizo au kukubali mafundisho hayo hakumaanishi kuwa watoto walikuwa wameamua kufa kwa hiari. Badala yake, mwenendo wao ulipaswa kuangaliwa katika mazingira ya imani za kidini, utegemezi kwa watu wazima, mamlaka ya wazazi, udanganyifu, hofu na shinikizo. “Mahakama imebaini kuwa vifo vilivyosababishwa na njaa vilitokana na vitendo au uzembe usio halali wa wale waliotekeleza mfumo wa mfungo,” akasema Jaji Kavedza. Mashahidi wa upande wa mashtaka walisema kuwa katika mikutano ya maombi chini ya miti Shakahola, Mackenzie aliwaambia wafuasi kuwa Yesu hangekuja kuwaelekeza kufunga hadi kufa ili waende mbinguni. Ushahidi ulionyesha kuwa wazazi waliagizwa kuwanyima watoto wao chakula, kabla ya kuanzishwa kwa mfungo mkavu uliokataza wafuasi kunywa maji. Maagizo hayo yalihusu waumini wote, wakiwemo watoto ambao hawakuwa na uwezo wa kuelewa kikamilifu matokeo yake. Jaji alisema maagizo hayo yalikuwa ya lazima, huku juhudi zikifanywa kuzuia wafuasi kuacha mfungo. Hali hiyo ilikuwa muhimu katika kutathmini nia ya washtakiwa. Alisema maelezo ya kidini yaliyotolewa kuhalalisha mfungo hayangeondoa moja kwa moja nia ya kutenda uhalifu. Mahakama ilipaswa kuchunguza nia ya vitendo hivyo, kwani lengo la kiroho halimaanishi kuwa mtu hawezi kuwa na nia ya kusababisha kifo. Vifo vilivyoendelea kutokea na hali ya wafuasi kudhoofika kimwili pia vilizingatiwa. Mfungo uliendelea licha ya dalili za wazi za madhara yake. Mahakama pia ilichunguza ushahidi kwamba nguvu zilitumiwa kuwalazimisha wafuasi kutii na kuwazuia watu wa nje kuwafikia waliokuwa wakifunga. Njia za kuingia katika baadhi ya makazi zilifungwa kwa matawi na miiba, huku wahanga waliodhoofika kwa njaa wakiachwa bila msaada. Mnamo Machi 23, 2023, shahidi wa upande wa mashtaka aliingia msituni akiwa na waandishi wa habari. Alisema Julius Katana alimtishia, huku mshtakiwa mwingine akimshika shingoni na kumkandamiza chini.Wengine walidaiwa kumpiga na kumsababishia majeraha kichwani na kwenye mbavu. Washukiwa hao wanatarajiwa kurejea mahakamani Novemba 6 kwa ajili ya kusikilizwa kwa hoja kuhusu hukumu watakazopewa. Shahidi mwingine alithibitisha tukio hilo, ambalo liliripotiwa katika Kituo cha Polisi cha Lango Baya. Upande wa mashtaka pia uliwasilisha ushahidi kuhusu kushambuliwa kwa afisa wa Shirika la Huduma kwa Wanyamapori Kenya (KWS) aliyeingia msituni. Jaji alisema matukio hayo yalikuwa muhimu katika kutathmini iwapo mfungo ulidumishwa kwa vitisho, vizuizi na vurugu, na kama washukiwa walielewa matokeo ya vitendo vyao. Ushahidi kutoka kwa Msajili wa Mashirika ulionyesha kuwa Mackenzie alikuwa mkuu wa Good News International Ministries, huku mshtakiwa wa pili akiwa katibu. Mashahidi walisema Mackenzie aliongoza mikutano chini ya miti Shakahola na kutoa maagizo kwa waumini. Baada ya kanisa na kituo cha televisheni cha Times Television kufungwa, aliwaambia wafuasi kuwa kanisa lilikuwa likihamia Shakahola, akitaja eneo hilo kama “Kanisa Jangwani”. Mackenzie alihusishwa na maagizo ya kuwalazimisha wafuasi kufunga, huku baadhi ya mashahidi wakieleza kuhusu kupigwa na matumizi ya mijeledi dhidi ya waliopinga. Baada ya kutathmini ushahidi wote, jaji alisema washukiwa ambao ushiriki wao binafsi ulithibitishwa walitenda kwa pamoja kutekeleza na kudumisha mfungo uliosababisha vifo hivyo. “Nimeridhika kuwa upande wa mashtaka umethibitisha kesi yake bila kuacha shaka ya msingi. Kwa hivyo, kila mshtakiwa anapatikana na hatia katika mashtaka yote 191 ya mauaji na anatiwa hatiani kama alivyokuwa ameshtakiwa,” akasema Jaji. Washukiwa hao wanatarajiwa kurejea mahakamani baadaye kwa ajili ya kusikilizwa kwa hoja kuhusu hukumu watakazopatiwa.
By Chioma Obinna As competition in Nigeria’s non-alcoholic beverage market continues to evolve, Maltina, one of the country’s longstanding malt drink brands, has unveiled a refreshed visual identity to mark its 50th anniversary, retaining its familiar taste while introducing redesigned packaging across its product range.The new identity, unveiled by Nigerian Breweries Plc last week, features […]
“The CityBoy Movement, to all of you, you have done something new in Nigeria politics. You did not just gather people; you built a structure, millions of real, verifiable members,” the President said.
MVUTANO kati ya Rais William Ruto na Gavana wa Trans Nzoia, George Natembeya kuhusu kutenga vibanda katika Soko la Masinde Muliro, Kitale, ulichacha jana huku polisi wakitumwa kulinda usalama na wafanyabiashara wakilalamikia kupoteza mapato. Maafisa wenye silaha kutoka Kikosi cha Kukabili Fujo (GSU) na Polisi wa Utawala (AP) walitumwa katikati ya mji wa Kitale, huku baadhi ya barabara zikifungwa na wafanyabiashara kufunga maduka yao kutokana na hofu ya ghasia. Hali ya wasiwasi pia ilizuka katika makao makuu ya kaunti ya Trans Nzoia baada ya polisi kuvuruga mkutano wa maombi uliokuwa ukiendelea. Gavana Natembeya amesema ataomba Seneti na mahakama kuingilia kati kutatua mzozo huo, akisisitiza kuwa suala hilo linahusu ugatuzi na mamlaka ya serikali ya kaunti. “Nataka Seneti iingilie kati na kusaidia kutatua mzozo huu. Seneti iliundwa kuwa mtetezi wa ugatuzi, na sasa ni wakati wa Bunge hilo kuingilia kati,” alisema Natembeya wakati wa ibada ya kanisa Jumapili. Soko hilo lenye thamani ya zaidi ya Sh800 milioni lilijengwa na serikali ya kaunti kwa usaidizi wa Benki ya Dunia. Hata hivyo, mchakato wa kugawa vibanda umesababisha mzozo kati ya viongozi wa kitaifa na wale wa kaunti. Rais Ruto amepinga mchakato wa ugavi uliofanywa na serikali ya kaunti na kusema vibanda vilivyosalia vitagawiwa kwa njia ya bahati nasibu. Bw Natembeya, kwa upande wake, amedai kuwa wafanyabiashara kutoka Uganda walipewa vibanda vingi ingawa madai yake hayajathibitishwa. Mwenyekiti wa Chama cha Kitaifa cha Wafanyabiashara Kenya (KNCCI) katika kaunti hiyo, Titus Kilong’i, alizua maswali kuhusu mamlaka ya kamishina wa kaunti kuhusika katika ugavi wa vibanda. “Je, kamishina wa kaunti ndiye aliyejenga soko hili kiasi cha kuingilia kati na kugawa vibanda? Baada ya kuvigawa, ndiye atakayekusanya mapato? Je, sheria inamruhusu kufanya hivyo?” aliuliza. Bw Kilong’i alisema orodha za mgao ina utata, akidai kuwa jina la mtu mmoja lilionekana hadi mara nane katika orodha tofauti za masoko. “Tunatakiwa kulipa ushuru, lakini kuna mkanganyiko na tunatishwa. Tutawezaje kuendelea kuishi?” akauliza. Mkurugenzi mtendaji wa KNCCI, Antony Masika, alisema wafanyabiashara wameathirika tangu Alhamisi, huku baadhi yao wakikadiria hasara kutokana na biashara kuvurugwa. Mfanyabiashara Belinda Nakhumicha alisema kufungwa kwa maduka na hali ya wasiwasi imewaathiri wafanyabiashara wanaotegemea mapato ya kila siku. Hata hivyo, washirika wa Rais wameunga mkono miradi yake ya maendeleo katika eneo hilo. Aliyekuwa Waziri wa Afya Susan Nakhumicha alisema wakazi wanafurahia hatua za serikali ya kitaifa kuhusu miradi ya maendeleo na kuingilia kati katika kutenga vibanda sokoni humo. “Tunafurahia yale ambayo Rais ametufanyia, ikiwemo ziara yake katika kaunti wiki iliyopita. Sisi kama wakazi wa Trans Nzoia tunamshukuru sana,” akasema
DODOMA: KATIBU Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Faris Buruhani, amekiomba Chama hicho kuchunguza tuhuma za rushwa zinazodaiwa kuwakabili baadhi ya vijana ili ukweli ubainike na haki itendeke. Buruhani ametoa ombi hilo leo Oktoba 19, 2026 jijini Dodoma alipozungumza na vijana waliojitokeza kumpokea katika Ofisi za Makao Makuu ya UVCCM, kufuatia…
IKUNGI, SINGIDA: Taasisi ya Kuzuia ya Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Singida imekuja na mbinu mpya ya kutumia ngoma za asili kuelimisha wananchi madhara ya rushwa na umuhimu wa uadilifu katika jamii. Hayo yamedhihirika wakati wa tamasha la la ngoma za asili lililofanyika katika kata ya Iyumbu, wilayani Ikungi, Singida mwishoni mwa juma ambapo vikundi…
The Christian Association of Nigeria (CAN) has mourned former Delta State Governor, Dr Emmanuel Eweta Uduaghan, praising his commitment to dialogue and confidence-building during a period of heightened political tension in Nigeria.
DODOMA: DISCIPLINE, courage and professionalism in carrying out international peacekeeping duties are among the qualities demonstrated by Tanzania Immigration Department officers who served in the United Nations Interim Force in Lebanon (UNIFIL). Their participation contributed to international efforts to maintain peace and security while representing Tanzania with distinction on the international stage. The commendation was…
SHAMBA la kahawa la Kiganda lenye ukubwa wa hekta 65 eneo la Gatanga, Kaunti ya Murang’a, limekuwa la kwanza Barani Afrika kupata cheti cha Rainforest Alliance Regenerative Agriculture Standard baada ya kubadili namna linavyolima kahawa kwa kuzingatia afya ya udongo, uhifadhi wa maji na mazingira. Shamba hilo, lililokodishwa na kusimamiwa na Coffee Management Services (CMS), hutumia mbolea ya mifugo hasa samadi, mabaki ya matawi yaliyopogolewa kama matandazo, mimea inayoongeza Nitrojeni kwenye udongo na mbinu asilia kudhibiti wadudu. Meneja Mkuu wa CMS Martin Ngare anasema Kiganda huzalisha kati ya tani 110 na 120 za kahawa mbichi kwa mwaka, sawa na karibu makontena sita, ambazo nyingi huuzwa Ulaya na Amerika. “Taji na utambuzi huu unajiri wakati mabadiliko ya tabianchi yanaathiri sekta ya kilimo, yakiweka shinikizo kwa uzalishaji wa kahawa kufuatia kuongezeka kwa kiwango cha joto, mvua isiyotabirika na kuongezeka kwa wadudu na magonjwa,” anasema. Anasema kilimo endelevu kinasaidia kufanya shamba kustahimili changamoto hizo huku likidumisha uzalishaji na ubora. “Mjadala ni kuhusu uboreshaji wa afya ya udongo, kuhifadhi maji, kuongeza bioanuwai na kuhakikisha mazingira mazuri kwa wafanyakazi na watu wanaoishi karibu na shamba,” Ngare anaelezea. Kiganda hufanya vipimo vya udongo ili kubaini virutubisho vinavyokosekana kabla ya kutumia mbolea. Mwaka uliopita, 2025, takriban malori 85 ya samadi yaliwekwa shambani ili kuongeza rutuba na kuboresha uwezo wa udongo kustawisha kahawa. Matawi yanayopogolewa (pruned) huachwa ardhini ili kuoza na kurejesha virutubisho. [caption id="attachment_193144" align="aligncenter" width="300"] Paul Kabubi, meneja wa Kiganda Farm Estate, akiweka chokaa (lime) kwenye mkahawa mnamo Agosti 27, 2026, katika eneo la Gatanga, Kaunti ya Murang’a. Picha|Sammy Waweru[/caption] Miti kama Albizia, Ngare anasema hutumika kutoa kivuli, kuupa udongo Nitrojeni na kusaidia kuleta virutubisho. Katika uhifadhi wa maji, udongo ulioinuliwa unazunguka mikahawa na husaidia kuelekeza maji kwenye mizizi, baada ya umwagiliaji wa juu kusababisha upotevu mkubwa wa maji wakati joto linapofikia nyuzijoto 33 hadi 35. Udhibiti wa wadudu Kiganda Farm pia umebadilika. Badala ya kunyunyizia dawa shamba lote, wafanyakazi hufuatilia miti ili kubaini maeneo yaliyoathirika. Mbinu za kibayolojia hutumiwa pamoja na maadui wa kahawa kama vile wasps na ladybirds, huku dawa zikitumika kwa miti iliyoathirika pekee. Julius Ng’ang’a, Mkurugenzi Mkuu wa Impact Programmes in East and Southern Africa at the Rainforest Alliance, anasema shamba la Kiganda kutambuliwa Barani Afrika ni hatua muhimu kwa sekta ya kahawa. “Hali ya hewa inabadilika, joto linaongezeka, wadudu magonjwa ya mimea yanaongezeka. Mashamba lazima yabadilike, yabadilishe mifumo yake ya uzalishaji chakula na kukumbatia ile bora na salama kwa afya ya watu,” anasisitiza. Karugu Macharia, Mwenyekiti wa Kenya Coffee Platform, anasema kilimo endelevu si mbinu mpya. “Unapoweka samadi kwenye udongo, unaongeza rutuba na kuufanya uwe hai,” anasema, akiongeza kuwa mbinu hizo zinaweza kutumiwa hata na wakulima wadogo. [caption id="attachment_193145" align="aligncenter" width="300"] Nyasi zilizotandazwa shambani kama matandazo, mojawapo ya teknolojia za kilimo endelevu zinazotumiwa na Kiganda Farm Estate kukuza kahawa katika eneo la Gatanga, Kaunti ya Murang’a, Agosti 27, 2026. Picha|Sammy Waweru[/caption] Dkt Tony Maritim, Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kahawa, ndio Coffee Research Institute inayohudumu chini ya Shirika la Utafiti wa Kilimo na Mifugo (KALRO), anasema aina za kahawa zinazostahimili athari za tabianchi kama vile ukame na wadudu zitakuwa muhimu. “Watafiti pia wanatengeneza na kutathmini aina zinazoweza kustawi katika maeneo mapya yanayolimwa kahawa,” anasema. Kahawa inayohimili mikumbo ya tabianchi itasaidia kuongeza kiwango cha uzalishaji ambacho kimeshuka kwa zaidi ya asilimia 100 ikilinganishwa na miaka 30 na 40 iliyopita. Samuel Mwau, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Kiufundi na Ushauri katika Coffee Board of Kenya, anadokeza kuwa uzalishaji wa kahawa nchini sasa ni karibu tani 50,000. “Uzalishaji wa kahawa kwa mkulima mdogo, ambao kihistoria ulikuwa kilo moja hadi mbili kwa mti, sasa unafikia kilo tatu na zaidi katika baadhi ya mashamba kufuatia mikahawa inayostahimili athari za tabianchi,” anasema. Mwau anasema wakulima sasa wanapata Sh120 hadi Sh125 kwa kilo, ikilinganishwa na Sh50 hadi Sh60 miaka mitano iliyopita, hali inayochochea kurejea kwa baadhi ya wakulima katika kilimo cha kahawa.
One person has died and 41 others have been hospitalised following suspected food poisoning in Singida Region after they reportedly consumed a traditional meal and a locally prepared drink while working at a private residence. The deceased has been identified as Ridhiwan Ayoub Omari, 13, who died while receiving treatment at Moyo wa Yesu Dispensary in Singida Municipality. According to a police statement, the incident occurred on October 17, 2026, at around 2pm in Unyambwa Ward, where the victims had been invited to perform work at a private home. They were reportedly served makande, a traditional dish made from maize and beans, and togwa, a locally prepared fermented drink, as payment for their work. Singida Regional Police Commander Matride Kuyeko said the victims began experiencing stomach pains and weakness the following morning. “On October 18, 2026, at around 11am, the deceased and 41 other people began experiencing stomach pains and weakness,” she said. Two children were initially taken to Moyo wa Yesu Dispensary in Mangumitongo, while the other 40 victims were referred to Singida Municipal Hospital for further treatment. Police said the condition of those receiving treatment was improving. Two people are being held for questioning as investigators seek to establish the cause of the suspected poisoning and the circumstances under which the food and drink were prepared and consumed. The incident has drawn attention to communal labour arrangements practised in parts of Tanzania, particularly in the central regions, where households mobilise neighbours to assist with agricultural and domestic activities in exchange for food and drinks. Such arrangements are common during cultivation, harvesting, millet threshing, roofing traditional houses and constructing livestock enclosures, with meals and beverages often forming part of the compensation. However, the involvement of children among those affected raises questions about the nature of the work they were invited to perform and the circumstances surrounding the incident. Police had not identified the suspected contaminant or established whether the food or drink caused the illnesses. Medical findings and further investigations will be needed to determine the cause of the incident and whether any criminal responsibility arises.
MVUTANO wa kisiasa kati ya Rais William Ruto na Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya umechacha huku washirika wao wakipigana vikali kuhusu miradi ya maendeleo na uchaguzi wa 2027. Bw Natembeya ametaka ufafanuzi kuhusu ufadhili wa miradi iliyotangazwa na Rais, akitishia kuzuia mradi wa hospitali ya Sh1 bilioni huku akipinga kile anachokitaja kuwa serikali ya kitaifa kujipatia sifa kwa miradi ya kaunti. Mvutano huo uliongezeka baada ya Rais kutembelea kaunti hiyo mara kadhaa wiki iliyopita, akimkosoa gavana kuhusu huduma za afya na kuwatambulisha wanasiasa wanaoweza kumpinga katika uchaguzi ujao. Rais alielezea Hospitali ya Rufaa ya Wamalwa Kijana kama hatari kwa wagonjwa, akidai imepewa jina la “Shakahola” kwa sababu wagonjwa wanaoenda kutafuta matibabu humo hawarudi wakiwa hai. “Viongozi wanapaswa kupanga kuhusu afya, wala si mazishi ya wananchi wao,” alisema Dkt Ruto, akitangaza kujenga hospitali mpya ya vitanda 300 ndani ya miezi minane. Hata hivyo, Bw Natembeya amehoji umuhimu wa kujenga hospitali nyingine bila kuweka wazi mipango ya ufadhili, akisema vituo vilivyopo vinapaswa kuimarishwa. Washirika wa Rais, akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani Kipchumba Murkomen na Seneta wa Trans Nzoia Allan Chesang, wamemkosoa gavana na kuahidi kuwarai wapigakura kumwondoa mamlakani 2027. Rais pia aliwatambulisha Mbunge wa Kiminini Kakai Bisau, aliyekuwa mbunge Chris Wamalwa na mwakilishi wa Kenya katika Umoja wa Mataifa Susan Nakhumicha kama viongozi wanaoweza kushindana na Bw Natembeya. Mgogoro mwingine unahusu Uwanja wa Kitale ambao ujenzi wake umekwama. Rais alisema serikali ya kitaifa itachukua jukumu la kuukamilisha. “Ingawa nimejenga viwanja 32 kote nchini, uwanja wenu umekwama kwa miaka mingi. Gavana wenu ameshindwa kuukamilisha, nami nitachukua jukumu la kuumaliza,” akasema Rais. Bw Natembeya alijibu kwamba alikuwa ameidhinisha mazungumzo na maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Kenya kuhusu kukamilisha mradi huo kwa fedha za serikali ya kitaifa. Alidai mradi haujaanza kwa sababu amekataa kujipendekeza kisiasa kwa Rais. Kuhusu soko la kisasa la Masinde Muliro mjini Kitale, Dkt Ruto alisema serikali ya kitaifa imetumia karibu Sh1 bilioni kulijenga na akaagiza wafanyabiashara 1,500 walioathiriwa na ujenzi wapewe kipaumbele katika ugawaji wa vibanda. Kila mmoja alipewa Sh10,000 za kuendeleza biashara yake. Bw Natembeya ameapa kufuatilia ugawaji huo ili kuhakikisha wafanyabiashara wa eneo hilo hawabaguliwi na watu kutoka nje. Mvutano umeongezeka zaidi baada ya walinzi wa gavana kuondolewa kwa mara ya pili. Ameitaka Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja kueleza sababu za hatua hiyo, akisema usalama ni haki wala si mapendeleo. Gavana amehusisha hatua hiyo na tofauti zake za kisiasa na serikali ya kitaifa, ingawa madai hayo hayajathibitishwa kwa njia huru. Vuta nikuvute ilidhihirika pia katika mazishi ya Afisa Mkuu Msaidizi wa Inspekta Jenerali wa Polisi Lazarus Simiyu Opicho huko Maili Saba ambapo Bw Natembeya na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna walikutana na washirika wa Rais. Kaulimbiu za “Wantam” zilivuruga shughuli na kuzuia baadhi ya viongozi wa upinzani kuhutubia waombolezaji. Baadaye, polisi walitumia gesi ya kutoa machozi kutawanya mkutano wa viongozi wa upinzani mjini Kitale. Huduma ya Kitaifa ya Polisi ilisema maafisa wawili walijeruhiwa na magari mawili ya serikali kuharibiwa, huku uchunguzi ukianzishwa.
PWANI: KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, amewaonya watumishi wa umma wanaojiona wako juu ya chama hicho, akisisitiza kuwa hakitavumilia uzembe katika utekelezaji wa majukumu yao. Kihongosi alisema CCM itaendelea kuwafuatilia watumishi wazembe na kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa viwango vinavyotakiwa, bila…
DAR ES SALAAM; Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linatarajia kuwa mwenyeji wa kikao cha Kamati ya Wataalamu wa Kimataifa ya uandaaji wa viwango vya nafaka na mazao ya jamii ya kunde, kitakachofanyika jijini Dar es Salaam Oktoba 20- 21, 2026. Akizungumza kuhusu kikao hicho, Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dk Ashura Katunzi, amesema Tanzania imepata heshima…
DAR ES SALAAM: PUBLIC investment is justified by the benefits it brings to citizens, not merely by the money allocated, contracts signed or funds disbursed. The Vice-President, Deogratius Ndejembi’s concerns over delays in infrastructure projects in Mbeya Region therefore raise an important question: Are taxpayers getting value for money? During his working visit, Mr Ndejembi…
SERIKALI imesema imefaulu kwa asilimia 99 kuwafuatilia watu waliotagusana na mgonjwa wa kwanza wa Ebola nchini pamoja na jamaa zao, huku idadi ya visa vilivyothibitishwa vikifikia saba. Kati ya visa hivyo, vinne ni vya watu ambao tayari walikuwa wametengwa kwa ajili ya kufuatiliwa. Maambukizi hayo yamesababisha kifo kimoja hadi sasa. Katibu wa Idara ya Afya ya Umma Mary Muthoni alisema maafisa wa afya wameimarisha ufuatiliaji na hatua za kuzuia ugonjwa huo usisambae katika jamii. Wizara ya Afya pia imezitaka serikali za kaunti kuandaa vituo vya karantini iwapo idadi ya maambukizi itaongezeka. Vifaa vya kujikinga dhidi ya maambukizi vimetumwa katika maeneo yaliyo hatarini, hasa kaunti zinazopakana na nchi jirani na sehemu kuu za kuingilia nchini. Bi Muthoni aliwataka Wakenya kuzingatia usafi, kuepuka kugusana na majimaji ya mwili yanayoweza kuwa na virusi na kuripoti watu wanaoshukiwa kuwa na ugonjwa huo haraka. Alisisitiza umuhimu wa kunawa mikono, kuepuka ngono bila kinga na watu walioambukizwa au wanaoshukiwa kuwa na Ebola, pamoja na kuepuka kupeana mikono na kupigana busu na wagonjwa wanaoshukiwa kuwa na maambukizi. Serikali imewahimiza wananchi kutokuwa na hofu, ikisema kugundua ugonjwa mapema na kupata matibabu yanayofaa ni muhimu katika kuudhibiti. Wizara pia imehusisha asasi za kidini katika kampeni ya kuelimisha umma na kupambana na habari potovu. Viongozi wa makanisa wametakiwa kuwahimiza waumini kuripoti dalili za ugonjwa mapema, kuzingatia usafi na kuepuka kugusa majimaji ya mwili wa wagonjwa au wanyama wa porini walio wagonjwa au waliokufa. Nairobi imeitenga Hospitali ya Mama Margaret Uhuru Kenyatta iliyoko Kariobangi Kaskazini kuwa kituo cha karantini. Gavana Johnson Sakaja alisema kaunti imeimarisha ufuatiliaji na inashirikiana na serikali ya kitaifa kuwalinda wakazi. Alisema wahudumu wa afya wamepewa mafunzo kuhusu matumizi sahihi ya vifaa vya kujikinga, kuwahudumia wagonjwa kwa usalama na kusafisha magari ya wagonjwa ili kuzuia maambukizi.
SERIKALI imeanzisha shughuli ya kuwahesabu wafanyakazi katika utumishi wa umma ana kwa ana kufuatia uchunguzi wa madai ya ulaghai wa Sh6.2 bilioni kupitia mfumo wa ulipaji mishahara ya serikali. Shughuli hiyo itaanza katika Wizara ya Elimu na linalenga kubaini wafanyakazi hewa, ajira zisizo halali na dosari katika rekodi za wafanyakazi wanaolipwa na serikali. Hatua hiyo inafuatia ukaguzi uliofichua visa vya wafanyakazi wanaodaiwa kushiriki akaunti za benki, rekodi za ajira zisizoaminika na mishahara kulipwa kwa watu ambao hawana taarifa halali za akaunti za benki. Katika ilani ya Oktoba 16, 2026, Katibu katika Wizara ya Elimu, James Kianda aliwaagiza wakuu wa idara kuhakikisha wafanyakazi wote walio chini yao wanahesabiwa ana kwa ana. Wafanyakazi walitakiwa kufika katika majengo ya Jogoo House kuanzia Oktoba 19 hadi Jumatano wakiwa na vitambulisho vya kitaifa, vyeti vya nambari ya siri (PIN) vya Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru nchini (KRA), barua zao za kwanza za ajira na barua za sasa za uteuzi. Shughuli hiyo itawahusisha wafanyakazi wote, wakiwemo waliolazwa hospitalini na walio katika likizo ya mwaka, ugonjwa, uzazi au likizo nyingine zilizoidhinishwa. Bw Kianda alionya kuwa mishahara ya wafanyakazi ambao hawatathibitishwa katika zoezi hilo itasitishwa. Alisisitiza kuwa maagizo hayo ni ya lazima na yanapaswa kutekelezwa bila kuchelewa. Waziri wa Utumishi wa Umma Geoffrey Ruku alisema uchunguzi uliofanywa na Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) umewahusisha wasimamizi 84 wa wafanyakazi katika Idara ya Magereza, Huduma ya Polisi na Wizara ya Afya na ukora wa ulaghai kuhusu ulipaji wa mishahara. Maafisa hao wanadaiwa kuhusika katika udanganyifu wa mishahara na kutokana na hilo wamepokonywa haki ya kuingia katika mfumo wa malipo na kuagizwa kujitenga na majukumu yao kwa siku 30 za kazi ili kuruhusu uchunguzi kuendelea. Serikali imewateua maafisa wengine kusimamia majukumu yao ili shughuli za kawaida zisiathirike. Bw Ruku alisema washukiwa wanatarajiwa kukamatwa kabla ya muda huo kukamilika, akitaja hasa maafisa wa Idara ya Magereza. Uchunguzi wa awali umebaini dosari za kutia shaka katika rekodi za ajira. Baadhi ya wafanyakazi wana rekodi zinazoonyesha waliajiriwa kabla ya kuzaliwa, huku wengine wakionekana kuanza kazi kabla ya kufikisha umri wa miaka 18. Pia, kuna visa vya wafanyakazi wengi kutumia akaunti moja ya benki kupokea mishahara. Serikali inatarajia kuwa zoezi hilo litasaidia kubaini dosari katika mfumo wa malipo, kuwachukulia hatua wanaohusika na kulinda fedha za umma dhidi ya matumizi mabaya.
With the Federal Government’s debts to power generation companies hitting the N6 trillion mark at the end of 2025, the government has gone to the bond market to raise funds to make up for its inability to fund electricity subsidies from the national budget. NERC, in its 2025 industry report, put the Federal Government’s gross […]
SENETA wa Nairobi Edwin Sifuna na baadhi ya viongozi wa Linda Mwananchi wamewakosoa baadhi ya viongozi wa ODM kwa kumkosea heshima mjane wa Raila Odinga, Mama Ida pamoja na familia ya waziri huyo mkuu wa zamani. Akizungumza katika ibada ya kanisa, eneobunge la Embakasi Mashariki jana, Bw Sifuna alisema kuvurugwa kwa maadhimisho ya kwanza ya kifo cha Raila eneo la Bondo kulipangwa na viongozi wa eneo hilo waliopinga mwaliko wa viongozi wa Linda Mwananchi. “Watu wale wale waliokuwa wameapa kuwa hawatakula kabla Raila hajatoa maagizo wamemsahau na sasa wanaimba wimbo wa mtu mwengine. Wanamtukana mjane wake na hata watoto wake,” akasema Bw Sifuna. Bw Sifuna alisema mrengo wake utailinda familia hiyo na kuendeleza maono na uanaharakati wa Raila, ikiwemo kuhakikisha demokrasia. Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino naye aliishutumu serikali kwa kukaa kimya huku ufisadi ukiharibu Jiji la Nairobi. Aliahidi kuwa akichaguliwa kuwa gavana, ataboresha barabara, kuhakikisha wanafunzi wanapata busari bila malipo, kusafisha jiji na kuunda nafasi za ajira kwa vijana.
ODINGA Junior ameapa kubaki katika chama cha ODM na kumuunga mkono Rais William Ruto katika azma yake ya kuchaguliwa tena mwaka ujao, licha ya tofauti za kisiasa zinazozidi kujitokeza katika familia ya Odinga. Jana, Raila Odinga Junior aliungana na viongozi wakuu wa ODM na Waziri wa Madini Hassan Joho katika mkutano wa kumbukumbu ya Raila Odinga uliofanyika Garissa. Haya yanatokea huku dadake Winnie Odinga akiendelea kuwakashifu baadhi ya maafisa wa chama hicho akidai walikodisha wahuni kuvuruga maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kifo cha baba yao yaliyofanyika katika uwanja wa Migwena, Bondo, wiki iliyopita. “Aaah, inafurahisha sana kuwaona viongozi wote wazuri wa ODM wakiadhimisha kumbukumbu ya kwanza ya Baba.Walipokuwa Dubai, sisi tulipokea zawadi zao kutoka Afgoonistan! Asante. Ni lazima nasi tulipe kwa namna hiyo hiyo,” Winnie aliandika ujumbe uliofasiriwa kuwa kejeli katika ukurasa wake wa Instagram. Aliambatanisha ujumbe huo na video iliyowaonyesha Waziri wa Madini Hassan Joho, Gavana wa Homa Bay ambaye pia ni mwenyekiti wa ODM Gladys Wanga, Mbunge wa Dagoretti Kaskazini Beatrice Elachi, Mbunge wa South Mugirango Silvanus Osoro, Kiongozi wa Wengi Kimani Ichung’wah na Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Kitaifa Junet Mohamed wakisafiri kwa ndege ya kibinafsi kutoka Eldoret hadi Garissa. Mkutano wa Garissa ni miongoni mwa shughuli zilizoandaliwa na ODM katika kipindi cha “Mwezi wa Baba”, kwa heshima ya aliyekuwa Waziri Mkuu ambaye aliongoza chama hicho kwa miaka 20. Bw Junior, ambaye ametangaza nia ya kuwania kiti cha ubunge cha Kibra, alisema atatumia tiketi ya ODM kuwania kiti hicho huku akipigia debe muhula wa pili wa Dkt Ruto. Pia ameahidi kumuunga mkono ami yake Dkt Oburu Oginga, katika kukiongoza chama hicho. “Nitabaki ODM hadi mwisho na nitaendeleza kampeni za kusaka uvumishaji Rais Ruto kote nchini anapotafuta kuchaguliwa tena, huku nikigombea ubunge wa Kibra kupitia ODM,” alisema katika mahojiano na Taifa Leo. Alisema hataathiriwa na jamaa zake wanaochagua mwelekeo tofauti wa kisiasa, akisisitiza kuwa anajenga safari yake ya kisiasa mbali na kumuunga mkono Rais. “Baba alituacha katika Serikali Jumuishi na hapo ndipo nitabaki. Nawarai watu wetu wamuunge mkono Rais achaguliwe tena. Nina Rais hadi mwisho,” akasema. Kauli yake inajiri wakati ambapo tofauti zinaongezeka katika familia ya Odinga kuhusu mwelekeo wa ODM na ushirikiano wake na serikali ya Kenya Kwanza. Shangazi yake, Mwakilishi wa Kike wa Kisumu, Ruth Odinga, amesema yuko tayari kuondoka ODM ikiwa kufanya hivyo kutasaidia kutetea haki na demokrasia. Akizungumza katika uwanja wa Migwena wakati wa maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kifo cha kaka yake, alisema, “Ikiwa kusimama na ODM kunamaanisha kujitolea kila kitu kulinda haki, basi iwe hivyo. Nikilazimika kujiunga na chama kingine ili kuhakikisha haki inapatikana Kenya, nitafanya hivyo.” Winnie naye amekosoa baadhi ya misimamo ya uongozi wa ODM na kutangaza kuwania kiti cha useneta wa Nairobi kinachoshikiliwa na Edwin Sifuna. “Isiwe uvumi tena; Edwin Sifuna anapotafuta wadhifa wa juu, mimi nimeona nafasi. Ndiyo maana nitawania useneta wa Nairobi. Hata hivyo, sitaenda peke yangu; ninaenda na vijana,” akasema. Kuhusu azma ya Winnie, Bw Junior alisema ana haki ya kidemokrasia kuwania kiti hicho lakini akamtaka kutafuta tiketi ya ODM kwa kushindana na Mbunge wa Lang’ata, Phelix Odiwuor almaarufu Jalang’o, katika uteuzi wa chama. Bw Junior amekuwa akimuunga mkono Jalang’o, akisema ODM inapaswa kumuunga mkono atakayeshinda uteuzi. Tofauti hizo pia zimeibua mjadala kuhusu nani anayefaa kuendeleza urithi wa kisiasa wa Raila. Bw Junior alipinga hatua ya baadhi ya wazee wa jamii ya Luo kumtawaza Winnie kuwa mrithi wa kisiasa wa babake. Siku ya kutawazwa kwa Bi Winnie, Bw Junior na Jaoko Oburu, anayelenga ubunge wa Bondo, walikutana na Waziri wa Ushirika Wycliffe Oparanya, aliyeahidi kuwaunga mkono kisiasa. Bw Junior pia amemtetea mamake Ida Odinga dhidi ya ukosoaji kuhusu maandalizi ya maadhimisho hayo, akisema kamati ilihusika na mialiko kwa kushauriana na familia.
By Dapo Akinrefon Former Delta State Governor, Chief James Ibori, has mourned prominent Niger Delta leader Patrick Dele Cole, praising his commitment to the struggle for true federalism and resource control. Cole, who was born on August 4, 1940, in Abonnema, in the Kalabari Kingdom of present-day Rivers State, died in London at the age […]
…Foundation inducts 81 new scholars By Steve Oko UMUAHIA — Abia State Governor, Alex Otti, has increased the annual scholarship award of the Alex Otti Foundation (AOF) from ₦250,000 to ₦350,000 per beneficiary and rewarded six first-class graduates with ₦500,000 each. Otti announced the increase on Saturday at the Foundation’s 2026 Scholarship Banquet, held at […]
MOROGORO; Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro, Dk Mussa Ali Mussa amesema ongezeko la maambukizi mapya ya VVU Manispaa ya Morogoro na halmashauri ya Mji Ifakara kunatokana na kuwepo kwa wageni wengi. Dk Mussa amesema hayo mbele ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya Ukimwi, Dk Zeyana Abdallah Hamid,…
By Victor Ahiuma-Young The Nigeria Union of Petroleum and Natural Gas Workers, NUPENG, has expressed profound sorrow over the deadly tanker explosion at Oluku, along the Benin-Lagos Highway in Ovia North-East Local Government Area of Edo State, raising fresh concerns over road safety, deteriorating highway conditions and the persistent dangers associated with scooping spilled fuel […]
MANYARA: TAKWIMU rasmi zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) zina umuhimu mkubwa katika kupanga na kutekeleza shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii, huku zikisaidia pia kutambua maeneo yenye fursa za uwekezaji. Meneja wa Takwimu wa NBS Mkoa wa Manyara, Gidioni Mokiwa, amesema ongezeko la idadi ya watu katika maeneo mbalimbali ni miongoni mwa…
WAZAZI wanakabiliwa na changamoto ya kuhakikisha watoto wao watakuwa salama wakiwa na shughuli za kuwaendeleza kiakili wakati wa likizo ndefu ya takriban siku 70, bila kutumia pesa nyingi. Kwa mujibu wa kalenda ya Wizara ya Elimu ya mwaka 2026, muhula wa tatu unamalizika Oktoba 23, huku likizo ikiendelea hadi Januari 1, 2027. Baadhi ya wanafunzi watafanya mitihani ya kitaifa katika kipindi hiki. Wataalamu wa malezi wanashauri wazazi kusawazisha mapumziko, michezo, kusoma na muda wa familia, badala ya kugeuza nyumba kuwa madarasa ya ziada. Mwenyekiti wa Chama cha Kitaifa cha Wazazi, Silas Obuhatsa, amewataka wazazi kuwajibika kwa usalama wa watoto wao, ambao hawatakuwa chini ya usimamizi wa walimu. “Wazazi lazima wawahudumie watoto na kuwaelekeza ipasavyo. Tumesikia kuhusu watoto wanaozama wanapoenda kuogelea. Lazima wazazi wawachunge watoto wao wakati wote wa likizo,” alisema. Pia aliwaonya wazazi dhidi ya kuwahusisha watoto walio chini ya miaka 18 katika mikutano ya kisiasa na kampeni, akisema wanapaswa kulindwa dhidi ya shughuli zisizowafaa. Alikosoa pia tabia ya baadhi ya wazazi kuwatuma watoto kufanya kazi ngumu sokoni badala ya kuwapa nafasi ya kupumzika baada ya mihula mitatu ya masomo. Bw Obuhatsa anasema likizo ni fursa ya watoto kujifunza stadi za maisha, kama kupika, kufanya kazi za nyumbani na kuwajibika, huku wazazi wakihakikisha wanakamilisha kazi walizopewa shuleni. Hata hivyo, alipinga kuwapeleka watoto katika masomo ya ziada ya kulipia, akisema walimu tayari wamekamilisha silabasi na kutoa kazi za likizo. Wazazi wanaweza kuwaweka watoto katika shughuli za kuwajenga bila kutumia pesa nyingi. Kusoma vitabu, kuchora, kupika pamoja, kulima bustani, kucheza michezo na kutembelea maktaba ni baadhi ya njia zinazopendekezwa. Mtaalamu wa malezi Juliet Chepkemoi anasema watoto wanahitaji muda wa kupumzika na kupona kutokana na shinikizo za masomo. “Likizo huwapa nafasi ya kupumzika, kutafakari yaliyowafika na kupata nafuu kihisia,” alisema. Hata hivyo, anaonya kuwa watoto wanaoachwa bila uangalizi kwa muda mrefu wanaweza kuathiriwa na marafiki wabaya, matumizi ya dawa za kulevya na maudhui yasiyofaa kwenye mitandao ya kijamii. Anashauri wazazi kupanga shughuli za likizo pamoja na watoto, kulingana na umri, vipaji na uwezo wa kifedha wa familia. Pia, wazazi wanapaswa kudhibiti muda wa watoto kutumia simu, televisheni na vifaa vya michezo ya kielektroniki ili shughuli hizo zisiathiri usingizi, mazoezi na mawasiliano ya kifamilia. Bi Chepkemoi anasisitiza umuhimu wa mawasiliano ya wazi, akisema watoto wanapaswa kujihisi huru kuwaeleza wazazi changamoto zao bila kuogopa kuhukumiwa. Lengo, anasema, si kuwashughulisha watoto kila dakika, bali kuwapa mazingira salama ya kupumzika, kucheza, kujifunza na kufurahia likizo.
MAMA Ida Odinga amekemea vikali vurugu zilizoshuhudiwa wakati wa maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kifo cha mumewe, Raila Amolo Odinga, akisema matendo kama hayo yalionyesha dharau kwa familia yake na kumbukumbu ya mwanasiasa huyo. Katika taarifa iliyotolewa Jumamosi, Oktoba 17, 2026, Ida alisema anasikitishwa na tabia ya baadhi ya waliohudhuria hafla ya kumbukumbu iliyofanyika Bondo kuzomea, kufoka na kuwatisha wageni walioalikwa. Alisema taarifa kwamba baadhi ya watu huenda walilipwa na kusafirishwa hadi hafla hiyo kwa lengo la kuvuruga shughuli na kuwatisha wageni ni za kutia wasiwasi. “Vitendo hivyo vinaonyesha dharau kubwa si kwa familia yetu pekee, bali pia kwa kumbukumbu ya Raila na maelfu ya watu waliofika kwa amani,” alisema. Ida aliomba radhi wageni waliofanyiwa vitendo hivyo, akisema walifika kufariji familia wakati mgumu na walistahili kupokelewa kwa heshima, ukarimu na upendo. Alionya viongozi wa kisiasa kuwa wana jukumu maalumu la kujizuia na kuhakikisha wafuasi wao wanaheshimu utu wa wengine, hata pale ambapo kuna tofauti za kisiasa. Alisisitiza kuwa mwaliko wa familia haupaswi kutumiwa kama nafasi ya kuendeleza uhasama wa kisiasa. “Mahali Raila alipopumzishwa hapapaswi kamwe kugeuzwa uwanja wa mapambano ya kisiasa. Wala majonzi ya familia yetu hayapaswi kutumiwa kama fursa ya kulipiza kisasi cha kisiasa,” alisema. Ida, ambaye alikuwa kwenye ndoa na Raila kwa zaidi ya miaka 50, alisema mumewe aliamini katika uhuru wa kutofautiana, mazungumzo na maridhiano. Alisema Raila aliweza kukabiliana na mamlaka na kupitia mateso ya kisiasa, lakini alielewa umuhimu wa watu wenye misimamo tofauti kuketi pamoja na kutafuta maelewano. Aliwataka wanaotaka kumuenzi Raila kuendeleza maadili hayo badala ya kutumia kumbukumbu yake kuchochea migawanyiko. Ida pia alifafanua kuwa kila mgeni aliyealikwa alikuwa amekaribishwa na familia ya Odinga haikuwa na ugomvi na yeyote kati yao. Alisema kutohudhuria kwa mtu hakupaswi kutafsiriwa kuwa kutokubaliana na familia. Aidha, alishukuru kamati ya maandalizi ya kumbukumbu ya Raila, viongozi wa dini, wasanii, walijitolea na wote waliochangia kufanikisha maadhimisho hayo. Alimshukuru Rais William Ruto kwa msaada wake kwa familia, hasa katika ujenzi wa kaburi la kumbukumbu la Raila. Ida aliwashukuru maelfu ya Wakenya na wageni kutoka Afrika na kwingineko waliofika Bondo kuomba na kushiriki kumbukumbu za Baba. Alisema Raila alikuwa wa familia yake, lakini pia alikuwa wa Kenya, Afrika na watu wengi ambao maisha yao aliyagusa. Aliwataka viongozi na wafuasi wao kuheshimu familia, wageni na mahali Raila alipopumzishwa, akisema Wakenya wanapaswa kuenzi kumbukumbu yake kwa kuishi kwa heshima licha ya tofauti zao.
Augie also raised concerns about the relationship between politics and the administration of justice, warning against the manipulation of legal institutions
TANGAZO la Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) Winnie Odinga kuwa atawania useneta wa Nairobi unatarajiwa kuvuruga muungano wa Linda Mwananchi na upinzani siasa za 2027 zikishika kasi. Seneta wa sasa wa Nairobi, Edwin Sifuna, ametangaza kuwa hatatetea kiti chake na analenga uongozi wa nchi ili kumwondoa Rais William Ruto. Akiongea wakati wa maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kifo cha babake Raila Odinga, Winnie alisema kuwa sasa analenga kiti cha useneta wa Nairobi lakini hakuweka wazi iwapo atafanya hivyo kupitia ODM. “Najua watu wengi wamekuwa wakiuliza mahali nipo na mahali naenda. Leo nataka kuwajibu ili isiwe uvumi tena,” akasema mbunge huyo wa EALA, Alhamisi. “Ifahamike kuwa Edwin Sifuna akisaka afisi nyingine, kuna nafasi katika kiti cha useneta Nairobi na ndiyo maana nimeamua kuwania useneta wa Nairobi. Siendi peke yangu bali naenda na vijana,” akaongeza. Kambi ya Linda Mwananchi ambako Winnie anaegemea, pamoja na viongozi wa upinzani kwa jumla wamekuwa wakisukuma wito wa umoja ambapo wanalenga ushirikiano katika kugawa viti kwenye baadhi ya maeneo hasa Nairobi na Mombasa. Iwapo kutakuwa na muafaka kati ya Linda Mwananchi na upinzani kuhusu kugawana viti Nairobi basi huenda Winnie akajipata pagumu kwa sababu tayari Linda Mwananchi imetangaza kuunga mkono Babu Owino kuwania ugavana. Kizingiti cha pili kinachomchongea Winnie zaidi ni kwamba ni vigumu sana kwa viti vya ugavana, ubunge, uwakilishi wa kike na useneta kushikiliwa na jamii moja Nairobi. Tangu uchaguzi wa 2013 viti hivyo vimeshikiliwa na viongozi kutoka jamii tofauti. Tatu, iwapo Linda Mwananchi itashirikiana na upinzani kugawana viti Nairobi basi itakuwa vigumu kuachiwa ugavana na useneta au mbunge mwakilishi wa kike. Katika mrengo wa upinzani tayari Mbunge wa Embakasi Kaskazini James Gakuya ametangaza kulenga ugavana kupitia DCP. Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua na kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka mnamo Novemba 2025 walisema vyama hivyo vitagawana nyadhifa za ugavana, useneta na mbunge mwakilishi wa kike wa Nairobi. Nne, tangazo la Winnie linajiri wakati nduguye, Raila Junior, tayari alikuwa amemuidhinisha Mbunge wa Lang’ata Phelix Odiwuor maarufu Jalang’o, kugombea useneta wa Nairobi. Jalang’o amekuwa akiandamana na Rais William Ruto katika ziara mbalimbali jijini Nairobi ambapo amekuwa akirejelewa kama seneta. Baada ya Winnie kutangaza azma yake ya useneta Jalang’o aliandika kwenye mitandao ya kijamii kwamba “Niko tayari’. “Ningependa kumwambia mheshimiwa Jalas hongera sana kwa kusimama. Sisi tuko nyuma yako kama ODM,” akasema Raila Junior katika hafla moja ya viongozi wa ODM jijini mapema mwezi huu. Tano, kwa kuwa Winnie anaonekana kuegemea mrengo wa Linda Mwananchi ambao unapinga kuchaguliwa tena kwa Rais Ruto, binti huyo wa mwendazake Raila Odinga atakuwa na kibarua kikali kushawishi wanachama wa ODM wamuunge mkono katika azma yake ya 2027.
KIONGOZI wa chama cha Democracy for the Citizens Party (DCP), Rigathi Gachagua, anatarajiwa kurejea nchini wiki ijayo baada ya ziara ya takriban miezi miwili Amerika, wakati ambapo anakabiliwa na changamoto zinazoweza kuathiri mwelekeo wa safari yake ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Gachagua aliondoka Kenya Agosti 26 na ametembelea majimbo mbalimbali yakiwemo Spokane, Portland, Kansas, Dallas na Boston. Alimaliza mikutano yake na Wakenya wanaoishi ughaibuni Oktoba 9, kabla ya kutangaza kuwa angeendelea na mashauriano ya kisiasa kwa siku nyingine 15 katika shamba lake la kibinafsi Texas. Alipoulizwa tarehe ya kurejea, alisema hakuwa ameamua siku kamili, ingawa alikuwa amefunga virago na Wakenya walikuwa wakimtaka aharakishe kurejea kwa sababu, kwa maoni yao, msukumo wa upinzani ulikuwa ukipungua. Atakaporejea, atakuta serikali imeongeza shughuli zake za kisiasa katika eneo la Mlima Kenya, ngome ambayo DCP inajaribu kupata uungwaji mkono mkubwa. Mbunge wa Naivasha Jane Kihara, mshirika wa karibu wa Gachagua, anadai serikali ina mikakati mitano ya kupunguza ushawishi wake katika eneo hilo. Mikakati hiyo, alisema, ni kugawanya umoja wa Mlima Kenya kupitia vyama na viongozi inaofadhili; kutoa zawadi au miradi ya kisiasa ili kupata uungwaji mkono; kutumia vita dhidi ya pombe haramu na dawa za kulevya kupinga kampeni za DCP; kuongeza shughuli za Naibu Rais Kithure Kindiki, hasa Mlima Kenya Magharibi; na kumjenga Mbunge George Kariuki katika siasa za eneo hilo. Gachagua pia atarejea akikabiliwa na wito wa Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano (NCIC), iliyomtaka kufika mbele yake Agosti 27 kujibu madai ya matamshi ya chuki. Kupitia kampuni ya mawakili ya Kiragu Wathuta, alikataa kufika, akisema alikuwa na safari ya nje iliyopangwa kuanzia Agosti 26 hadi Oktoba 20. Tume hiyo ilitaja matamshi aliyotoa Februari 23 katika Uwanja wa Gusii, Kisii; Juni 12 Luanda, Kaunti ya Vihiga; na wakati wa ziara yake Meru kati ya Julai 25 na 28. Bado haijulikani ikiwa Gachagua atafika mbele ya tume hiyo na hatua zitakazochukuliwa iwapo atakosa kufanya hivyo. Changamoto nyingine ni mizozo ya ndani ya chama chake, ambapo hatua za kinidhamu na malalamishi kuhusu uteuzi zimeibua maswali kuhusu umoja wake. Mwaniaji wa ubunge wa Gichugu Njeri Mbogo amesimamishwa kwa siku 180 kutokana na madai ya kuhusika katika tukio ambapo chupi za wanawake zilizokuwa na majina ya Seneta wa Kirinyaga Kamau Murango na Mwakilishi wa Wanawake Njeri Maina zilionyeshwa na waandamanaji. Maina alidai chupi hizo zililetwa kwa nia ya kumchafua kisiasa. Mwenyekiti wa watu mashuhuri wa chama cha DCP, Maina Kamanda, alidai chama hicho kimeingiliwa na watu wanaofanya kazi kwa niaba ya serikali na akaonya kuwa hawatapewa tiketi za uteuzi. Kiongozi wa vijana kaunti ya Kiambu Isaac Mungai pia alifukuzwa kwa sababu za kinidhamu baada ya kutofautiana na Seneta Karungo Thang’wa na kuonekana kumuunga mkono Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro. Wakati huohuo, chama hicho kimemuonya Seneta wa Nakuru Tabitha Keroche dhidi ya kuendesha shughuli zake nje ya miundo ya chama baada ya kuondoka UDA Oktoba 9, 2026, akilenga kiti cha ugavana wa Nakuru. Baadhi ya wanaowania nyadhifa wameibua malalamishi kuhusu haki katika uteuzi, wakidai viongozi wakuu wamekuwa wakionyesha upendeleo kwa wagombeaji fulani kabla ya mchakato rasmi. Gachagua pia atalazimika kukabiliana na mjadala kuhusu kuunda muungano wa upinzani na wakati wa kutangaza mgombeaji mmoja wa urais. Amesisitiza kuwa DCP inapaswa kwanza kujenga miundo yake katika kaunti, kuimarisha uanachama na kujitambulisha kabla ya kuingia katika muungano rasmi. Pia amependekeza kuwa mgombeaji wa pamoja wa upinzani atangazwe Mei 2027, akisema tangazo la mapema litampa Rais William Ruto nafasi ya kumlenga na kudhoofisha kampeni zake. Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa upinzani, akiwemo Kalonzo Musyoka, Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino na aliyekuwa Waziri wa Utumishi wa Umma Justin Muturi, wametaka jina hilo litangazwe mapema. DCP pia inakabiliwa na mahitaji makubwa ya tiketi za uteuzi, huku kamati ya fedha ya chama ikisema inahitaji takriban Sh5 bilioni kwa bajeti yake. Kaimu Katibu wa DCP John Methu hata hivyo amepuuzilia mbali hofu kuhusu changamoto hizo, akisema Gachagua ni mwanasiasa aliyejijenga na amewahi kukabiliana na changamoto kubwa, ikiwemo kuondolewa madarakani kama naibu rais. Alisema Gachagua atarejea akiwa na nguvu mpya kuendeleza ajenda yake ya kisiasa na kushughulikia masuala yaliyoibuka akiwa ughaibuni.
RAIS mstaafu Uhuru Kenyatta alifuta ziara yake ya Bondo kuhudhuria kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga kufuatia wasiwasi kuhusiana na usalama. Timu ya maandalizi ya Bw Kenyatta ilikuwa tayari imewasili Bondo na kiti chake kutengwa katika jukwaa la wageni mashuhuri. Ndege yake pia ilikuwa tayari kuondoka kutoka Uwanja wa Wilson jijini Nairobi Alhamisi asubuhi, lakini hakufika. Msemaji wake Kanze Dena-Mararo alisema kulikuwa na mabadiliko ya ratiba na suala lililohitaji kushughulikiwa, bila kufafanua zaidi. Hata hivyo, hafla hiyo iligeuka jukwaa la malumbano ya kisiasa huku viongozi wakitofautiana kuhusu urithi wa Raila na uhusiano wao na Rais William Ruto. Naibu kiongozi wa ODM Simba Arati alimshutumu Uhuru kwa kufadhili upinzani, huku Waziri wa Kawi Opiyo Wandayi akiwataka wakazi wa eneo hilo kumuunga mkono Rais Ruto. Kutohudhuria kwa Uhuru kulivutia umakini kutokana na uhusiano wake wa kisiasa na Raila, hasa baada ya maridhiano yao ya Machi 2018 na uungwaji mkono wake kwa azma ya Raila kuwania urais mwaka 2022. Kiongozi wa wachache katika Bunge la Kitaifa Junet Mohamed alisema hakuhudhuria kwa sababu ya uwepo wa jina la aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kwenye orodha ya walioalikwa. Gachagua naye hakuhudhuria kwa sababu alikuwa Amerika. Mjane wa Raila, Ida Odinga, alisema familia haikuwa na kinyongo na walioalikwa lakini wakakosa kufika. Hata hivyo, alikashifu vitendo vya kuzomea, kupiga kelele na kutisha wageni wakati wa hafla hiyo. Bi Ida alionya dhidi ya kugeuza eneo la mazishi ya Raila kuwa uwanja wa mapambano ya kisiasa, akisema urithi wake ni mkubwa kuliko tofauti za viongozi.
RAIS William Ruto ameanzisha kampeni za kuimarisha uungwaji mkono wake katika Bonde la Ufa, akilenga kuongeza idadi ya wapiga kura kutoka 5.4 milioni waliojisajili mwaka 2022 hadi zaidi ya milioni saba kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027. Hatua hiyo inajiri huku kukiwa na malalamishi miongoni mwa wakazi wa eneo hilo kwamba Rais amewapuuza kwa miaka minne na sasa amerejelea akitafuta uungwaji mkono kwa muhula wa pili. Washirika wake wanahofia kuwa kutoridhika kwa wapiga kura kunaweza kusababisha wengi kukosa kujitokeza kupiga kura, hali inayoweza kuathiri juhudi zake za kuchaguliwa tena. Rais pia anakabiliwa na kupungua kwa uungwaji mkono katika eneo la Mlima Kenya, ambalo lilichangia pakubwa ushindi wake wa 2022. Wakati huohuo, anatafuta kuimarisha uhusiano na maeneo yaliyokuwa ngome za aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, yakiwemo Nyanza, Magharibi, Pwani na Nairobi. Wabunge wanasema zaidi ya wakazi 1.8 milioni wa Bonde la Ufa hawajajisajili kupiga kura, huku wengi wakikosa vitambulisho vya taifa. “Urais hushindaniwa kwa kura. Tuna uwezo wa kusajili wapiga kura zaidi ya milioni saba. Tafadhali pateni vitambulisho na mjisajili kupiga kura,” alisema Rais alipokuwa Moiben, Kaunti ya Uasin Gishu. Hii ni mara ya pili ndani ya mwaka mmoja kwa Rais kuwataka wakazi wa Bonde la Ufa kupata vitambulisho na kujisajili. Awali alitoa ombi hilo katika kaunti za Bomet na Narok. Mkuu wa Utumishi wa Umma, Felix Koskei, amesema uchaguzi wa 2027 utakuwa na ushindani mkubwa, akiwataka wafuasi wa Rais kuhakikisha wanajiandaa mapema. Kiongozi wa Wengi katika Seneti, Aaron Cheruiyot, amesema chama cha UDA kinahamasisha wakazi wote wanaostahili kujiandikisha ili washiriki uchaguzi. Katika uchaguzi wa 2022, Bonde la Ufa lilikuwa na wapiga kura 5.34 milioni waliojisajili. Ruto alipata kura milioni 2.6, huku Raila akipata takriban 1.1 milioni, hasa kutoka Narok, Kajiado na Turkana. Takwimu za Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) zinaonyesha kuwa wapiga kura wapya 671,958 walikuwa wamejisajili katika eneo hilo wakati wa zoezi la mwaka huu. Bonde la Ufa liliongoza kwa idadi ya waliojisajili, likifuatiwa na Mlima Kenya lililokuwa na wapiga kura wapya 399,220. Katika ziara yake ya siku 10 Kaskazini mwa Bonde la Ufa, Rais amekuwa akizindua na kutangaza miradi ya barabara, afya, umeme, masoko na nyumba za gharama nafuu, huku akiwaomba wakazi kumuunga mkono kwa muhula wa pili. Hata hivyo, chama cha Democracy for the Citizens Party (DCP) cha aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kinaimarisha shughuli zake katika baadhi ya maeneo, yakiwemo Nakuru na Narok. Seneta wa Kajiado Samuel Seki na Mbunge wa Kajiado Kaskazini Onesmus Ngogoyo ni miongoni mwa viongozi waliojiunga na Gachagua. Vincent Rotich, kiongozi wa DCP eneo la Emurua Dikirr, anasema ushindi wa chama hicho katika kiti cha uwakilishi wadi cha Narok Town na kupata zaidi ya kura 10,000 katika uchaguzi mdogo wa Emurua Dikirr kumezua wasiwasi serikalini. Mchambuzi wa siasa Profesa Tom Nyamache wa Chuo Kikuu cha Turkana anasema wito wa Rais kwa wakazi kupata vitambulisho na kujisajili kupiga kura ni sehemu ya maandalizi ya mapema ya uchaguzi. Anasema ushindani unaanza kutoka matamshi ya kisiasa hadi mikakati ya kusajili na kuhamasisha wapiga kura. Ruto pia analenga maeneo yanayozungumza lugha ya Maa na Turkana, ambayo yalimuunga mkono Raila katika chaguzi zilizopita. Amechukua hatua kama kukabidhi usimamizi wa Hifadhi ya Wanyamapori ya Amboseli kwa Kaunti ya Kajiado na hati ya umiliki wa Msitu wa South West Mau kwa Kaunti ya Narok. Hata hivyo, anakabiliwa na upinzani kutoka kwa baadhi ya viongozi wa eneo hilo, wakiwemo Seneta Seki na Mbunge Ngogoyo, wanaohusishwa na Gachagua. Katika Kaunti ya Baringo, mvutano kati ya Rais na mwenyekiti wa Kanu Gideon Moi pia unaongeza changamoto za kisiasa kwa UDA. Hivyo, kurejea kwa Ruto Bonde la Ufa kunahusu zaidi ya kutangaza miradi ya maendeleo. Ni juhudi za kuimarisha ngome yake ya kisiasa, kuongeza idadi ya wapiga kura waliojisajili na kukabiliana na upinzani unaojaribu kujipenyeza katika eneo ambalo kwa muda mrefu limekuwa ngome yake.
KAGERA: UJENZI wa Mradi wa Maji wa Miji 28 wa Rwakajunju, wilayani Karagwe, mkoani Kagera, umefikia asilimia 79, huku huduma ya maji safi na salama ikitarajiwa kuanza kutolewa mwishoni mwa Desemba mwaka huu. Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi, Mathew Kundo amesema mradi huo wenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 63 ni mkombozi kwa wananchi…
KAGERA: WIZARA ya Afya imeitambulisha rasmi taasisi ya kimataifa ya Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation (EGPAF) kuwa mdau mpya wa kuratibu na kuendeleza afua za VVU na UKIMWI mkoani Kagera na mikoa mingine saba. Hatua hiyo ni kufuatia kumalizika kwa shughuli za uratibu zilizokuwa zikitekelezwa na shirika lisilo la kiserikali la Management and Development for…
DAR ES SALAAM; Gavana Mstaafu wa Benki kuu ya Tanzania (BoT) Profesa Florens Luoga, amesema utawala wa kodi ni kiungo muhimu kati ya serikali na wananchi katika kukusanya rasilimali za maendeleo na kutoa huduma za umma. Almesema hayo wakati wa uzinduzi wa kitabu Cha Utawala wa Kodi Tanzania (Administration of Income Tax in Tanzania) kllichozinduliwa…
KIONGOZI wa People’s Prosperity Party (PPP), Eliud Owalo, ametangaza kuwa chama hicho kimepata usajili kamili, hatua inayokiruhusu kutangaza wagombea katika nyadhifa zote za uchaguzi mkuu wa 2027. Bw Owalo, ambaye ananuia kutafuta tiketi ya chama hicho kuwania urais, alisema Afisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa (ORPP) imekipatia PPP cheti cha usajili kamili. Hatua hiyo inakiwezesha chama hicho kujiandaa kushiriki uchaguzi wa urais, ubunge, ugavana na uwakilishi katika mabunge ya kaunti kote nchini. "Kazi sasa ni kuvumisha chama, kuelekea maeneo mbalimbali ya nchi na kusaka uungwaji mkono. Binafsi usajili huu sasa unanipa motisha ya kusaka uungwaji mkono kwa Wakenya nikiwaeleza kile ambacho nitafanya nikipewa uongozi wa nchi," akasema Bw Owalo kwenye mahojiano na Taifa Leo. "Nawahakikishia wawaniaji wote kuwa uteuzi utakuwa huru na haki na wananchi ndio wataamua nani anawahi tikiti ya chama chetu katika nafasi zote za uongozi. Kampeni zetu zitajikita katika kuhakikisha kwamba tunawahakikishia Wakenya kuwa tunayoahidi kinatimizwa," akaongeza Waziri huyo wa zamani wa Teknolojia na Mawasiliano. Katika taarifa yake, PPP ilisema imetimiza masharti ya kisheria yanayohitajika ili kupata usajili kamili chini ya Sheria ya Vyama vya Kisiasa ya mnamo 2011. Chama hicho kilipatiwa cheti cha usajili wa muda Juni 26, 2026, na kupewa siku 180 kutimiza masharti yaliyowekwa ili kupata usajili kamili. Miongoni mwa masharti hayo ni kuwa na angalau wanachama 1,000 waliosajiliwa katika kila moja ya angalau kaunti 24. Wanachama hao wanapaswa kudhihirisha uwakilishi wa kieneo na kikabila, uwiano wa kijinsia na uwakilishi wa makundi maalum, yakiwemo vijana, wanawake, watu wenye ulemavu na jamii za wachache. Chama hicho pia kilitakiwa kuwa na makao makuu ya kitaifa, afisi za matawi katika angalau kaunti 24 na kamati ya utendaji katika ngazi ya kaunti. PPP ilisema imetimiza masharti hayo na kuanzisha miundo ya chama katika kaunti 30, pamoja na makao makuu yake yaliyoko Muchai Drive, Nairobi. Bw Owalo anatarajiwa kutumia tiketi ya PPP kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa Agosti 10, 2027. Chama hicho pia kinapanga kusimamisha wagombea katika nyadhifa nyingine za uchaguzi kote nchini, kikiwa na lengo la kupanua uwepo wake kitaifa kabla ya uchaguzi huo. Usajili huo unafanyika huku vyama vya kisiasa vikikabiliwa na makataa kadhaa yaliyowekwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Agosti 10, 2027. Vyama vilitakiwa kuwasilisha kwa tume majina na saini za mfano za maafisa wao walioidhinishwa kufikia Oktoba 15, 2026. Kanuni za uteuzi wa wagombea zinapaswa kuthibitishwa na Msajili wa Vyama vya Kisiasa kufikia Oktoba 30 na kuwasilishwa kwa IEBC kufikia Novemba 6. Ratiba ya uchaguzi pia inavitaka vyama kuwasilisha orodha za wanachama na maelezo ya wanaotaka kuwania nyadhifa mbalimbali kupitia mchujo wa vyama kufikia Machi 16, 2027. Mchujo huo pamoja na utatuzi wa migogoro ya ndani kuhusu uteuzi wa wagombea unapaswa kukamilika kufikia Mei 8, 2027. IEBC itafanya uteuzi rasmi wa wagombea kati ya Mei 29 na Juni 11.
WATU 108 waliotangamana na wagonjwa wa Ebola nchini wako karantini katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH) na Hospitali ya Huduma za Polisi, huku nchi ikiwa na vitanda 211 vya kuwahudumia wanaogua maradhi hayo. Ripoti ya kuhusu Ebola nchi ya Oktoba 14 inaonyesha kuwa watu 128 waliotangamana na mgonjwa wa kwanza walifuatiliwa. Kati yao, 108 wako karantini, huku 20 wakiwa nje ya karantini. Ufuatiliaji wa watu 15 unaendelea, huku watano wakiwa nje ya nchi. Kenya ina visa viwili vilivyothibitishwa vya Ebola na kifo kimoja. Mgonjwa wa kwanza alikuwa Mkenya aliyesafiri kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupitia Uganda na kufariki Oktoba 5. Mgonjwa wa pili, mwanaume mwenye umri wa miaka 39, alipata homa, uchovu na maumivu ya viungo akiwa karantini Oktoba 13. Vipimo katika maabara mbili vilithibitisha kuwa na Ebola na anapokea matibabu. Jumla ya sampuli 324 kutoka kaunti 18 zimepimwa. Wakati huo huo, wasafiri 685,027 wamechunguzwa katika vituo 26 vya kuingia nchini. Kenya pia imepokea vifaa vya kujikinga na kudhibiti maambukizi yenye thamani ya Sh61.1 milioni kutoka Amerika na mataifa mengine washirika wake. Vifaa hivyo ni pamoja na barakoa 3,600 za N95, chupa 9,000 za kusafisha mikono, viatu 1,080 vya kujikinga na mifuko 60 ya kuhifadhia miili kwa mazishi salama. Katibu Mkuu katika Idara ya Afya ya Umma, Mary Muthoni Muriuki, alisema vifaa hivyo vitalinda wahudumu wa afya, wagonjwa na familia zao. Wahudumu 4,917 wamefunzwa kuhusu Ebola, huku wataalamu 343 wakiwa tayari kupelekwa maeneo yatakayohitaji msaada. Serikali inatayarisha mpango wa kusambaza vifaa hivyo katika kaunti zilizo katika hatari kubwa ya maambukizi.
By Ayo Taiwo Much of Oluwatobiloba Mide-Ibrahim’s management work comes down to two things: reviewing financial work and helping people understand the decisions behind the figures. At the Association for Diagnostic and Laboratory Medicine, she oversees the close, the financial statements and the records behind them. At FinServe Pro, where she is Chief Operating Officer, […]
NAIBU Rais, Kithure Kindiki jana alisema kuwa uchaguzi mkuu wa 2027 utakuwa mashindano kati ya maendeleo na kelele za kisiasa. Akikosoa upinzani kwa kukosa mwelekeo na kujihusisha na siasa za migawanyiko, Profesa Kindiki alionya kuwa viongozi wasio na rekodi ya maendeleo watashindwa uchaguzi huo. Alisema serikali inalenga kutekeleza miradi ya maendeleo ili iwe na mafanikio ya kuwasilisha kwa Wakenya itakapoomba kura mwaka ujao. Akizungumza katika soko la Riakiania alipokuwa akizindua miradi ya barabara na umeme, Profesa Kindiki alisema viongozi lazima wawe na rekodi inayoonekana ya maendeleo ili kupata uungwaji mkono wa wapigakura. “Ni vigumu kwa viongozi kusimama mbele ya wananchi mwaka ujao na kuzungumzia siasa ikiwa hawana rekodi ya maendeleo. Wananchi hawali kelele, matusi na mapigano. Wanataka maendeleo, amani na umoja,” akasema. Alishutumu upinzani kwa kuendeleza siasa za chuki, migawanyiko na uchochezi badala ya kuelekeza nguvu katika maendeleo. Profesa Kindiki alisema serikali iko katika harakati za kutekeleza manifesto yake na kuahidi kuwa miradi yenye manufaa kwa wananchi itaendelea. Pia alionya kuwa ghasia za kisiasa hazitavumiliwa nchini, akisema Kenya inahitaji amani na umoja. Alitaja uchaguzi wa 2002, ambapo marehemu Mwai Kibaki na Uhuru Kenyatta walishindana kuwania urais bila ghasia na uharibifu wa mali, akiwataka viongozi wa sasa kuiga mfano huo. “Ushindani wa kisiasa si uadui. Tuenzi siasa zilizokomaa zisizo na ghasia wala chuki,” akasema. Pia aliwaonya viongozi wa upinzani dhidi ya matusi na tabia zisizofaa, akisema huenda wakalaaniwa na wazee waliompa hadhi ya kuwa kinara wa eneo la Mlima Kenya katika hafla ya Kirigiti. Kuhusu maendeleo, Profesa Kindiki alisema tangu 2022, nyumba 32,000 katika Kaunti ya Kirinyaga zimeunganishwa na umeme. Serikali imetenga Sh845 milioni kuunganisha nyumba nyingine 10,800. Eneobunge la Gichugu linafaidika na miradi 28 ya kusambaza umeme katika hatua ya mwisho, inayolenga nyumba 2,100 kwa gharama ya Sh75 milioni. Alisema ujenzi wa barabara ya kilomita 53 inayounganisha Piai, Mbiri, Ngiriambu, Kiamutugu, Muchagara, Karumandi, Thumaita, Kamugunda, Kamweti, Kavote na Kimunye unaendelea kwa gharama ya Sh2 bilioni. Barabara hiyo ni sehemu ya kilomita 571 zilizotengewa Sh42 bilioni kwa ajili ya kuwekwa lami Kirinyaga. Kazi ya kuweka lami kilomita 472 inaendelea kwa gharama ya Sh37 bilioni.
SERIKALI imepokea maombi 800 kutoka kwa wakulima wanaotaka kununua nyati wa kufuga kwa ajili ya kukamuliwa maziwa. Haya yanatokea wakati ambapo Kenya ikikabiliwa na uhaba wa maziwa unaochangiwa na ukame wa mara kwa mara na gharama ya juu ya malisho ya mifugo. Katibu katika Idara ya Ustawi wa Mifugo, Jonathan Mueke, alisema serikali imekamilisha masharti ya vyeti vya afya ya mifugo vinavyohitajika kuagiza nyati hao kutoka India na sasa inakamilisha makubaliano kuhusu bei na gharama za usafirishaji. Mpango huo ulijadiliwa kwa mapana wakati wa Mkutano wa kwanza wa Mabadiliko ya Kilimo na Mifumo ya Chakula wa 2026, uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri vya Shirika la Kilimo la Kenya (ASK) kuanzia Oktoba 7 hadi 9. Rais William Ruto alimwagiza Katibu Mueke kuandaa mpango wa kuanzisha ufugaji wa nyati hao kupiga jeki sekta ya maziwa nchini. Rais alisema wakulima wanakabiliwa na changamoto za uzalishaji kutokana na ukame na gharama kubwa ya chakula cha mifugo. Pia alieleza wasiwasi kuhusu Kenya kutegemea bidhaa zinazoagizwa kutoka nje, zikiwemo soya na alizeti zinazotumika kutengeneza chakula cha mifugo. Bw Mueke alisema serikali imekuwa ikishauriana na wakulima kuhusu mpango huo kwa mwaka mmoja na nusu na kuanzisha ushirikiano na India, ambayo ina uzoefu mkubwa wa kufuga nyati kwa ajili ya maziwa. Alisema nyati hao wapatao milioni 203 wanafugwa duniani na maziwa yao yana kiwango cha mafuta kinachokaribia mara tatu ya maziwa ya ng’ombe wa kawaida. Kiwango hicho cha mafuta huyafanya maziwa ya nyati kufaa kutengeneza bidhaa zenye thamani kubwa kama jibini, mtindi, siagi na samli. Kenya huagiza baadhi ya bidhaa hizo kutoka nje, hivyo uzalishaji wa ndani unaweza kupunguza mtindo huo. Serikali inalenga kuagiza nyati aina ya Murrah kutoka India, inayosifika kwa uzalishaji wa maziwa. Bei ya nyati hao nchini India inakadiriwa kuwa kati ya Sh102,572 hadi Sh410,289, kutegemea umri, afya na kiwango cha maziwa anayozalisha. Bw Mueke alifafanua kuwa nyati wanaozungumziwa ni wa kufugwa, wala si nyati wa porini wanaopatikana Afrika. Ujumbe wa Kenya unaojumuisha wakulima, wataalamu na waundaji sera unapanga kutembelea India Novemba kujifunza mbinu za ufugaji na uzalishaji wa kibiashara. Misri pia ina nyati milioni tano wanaofugwa kwa ajili ya maziwa. Mbali na maziwa, nyati hao wanaweza kutoa nyama na ngozi kwa matumizi ya viwandani. Hata hivyo, mafanikio ya mpango huo yatategemea upatikanaji wa maji, chakula cha mifugo cha bei nafuu, mbinu bora za ufugaji na masoko.
MAADHIMISHO ya mwaka mmoja tangu kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga yalifichua mivutano kuhusu urithi wake wa kisiasa, huku wanafamilia wakionekana kuelekea katika kambi tofauti kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027. Katika uwanja wa Migwena, Bondo, mjane wake Ida aliwapokea viongozi kutoka makundi hasimu, binti yake Winnie akatangaza azma ya kuwania useneta wa Nairobi, huku mwanawe Raila Junior akisisitiza uaminifu wake kwa chama cha ODM. Wakati huo huo, dadake Raila, Mbunge Mwakilishi wa Kike wa Kisumu Ruth Odinga, alitishia kuondoka ODM akilalamikia kupotoka kwa chama hicho kutoka kwa misingi yake. Hatua hizo zimeibua maswali kuhusu iwapo familia hiyo imeamua kuweka dau katika pande tofauti ili kuhifadhi ushawishi wake, au iwapo kila mmoja anafuata malengo yake binafsi. Kuna mihimili miwili inayoibuka na kundi moja linaegemea kwa Rais William Ruto, Kiongozi wa ODM Dkt Oburu Oginga na Raila Junior, wanaounga mkono ushirikiano wa ODM na serikali. Kundi jingine linahusisha Winnie, Ruth na vuguvugu la Linda Mwananchi linaloongozwa na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, ambalo limepinga ushirikiano huo. Dkt Oginga amepinga madai kuwa kufanya kazi na Ruto ni kusaliti misingi ya ODM. Anasema chama hicho lazima kihamie kutoka kutetea Katiba ya 2010 hadi kutekeleza masharti yake kuhusu usawa wa kiuchumi, ugatuzi na uadilifu wa taasisi. “Hatuwezi kutekeleza maadili yetu ya maendeleo tukiwa pembezoni,” alisema katika hotuba yake ya maadhimisho, akisisitiza kuwa ODM inapaswa kutumia idadi ya wafuasi wake na mtandao wake wa kisiasa ili kuunda serikali ijayo. Ushirikiano huo umewawezesha baadhi ya wanachama wa ODM kupata nyadhifa serikalini. Ida, kwa mfano, aliteuliwa kuwa balozi na mwakilishi wa kudumu wa Kenya katika Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) Februari mwaka huu. Hata hivyo, Winnie alituma ujumbe tofauti alipotangaza kuwania useneta wa Nairobi, akionekana kuhusisha azma yake na kambi ya Sifuna. “Edwin Sifuna anapotafuta nyadhifa nyingine, nafasi ya useneta wa Nairobi iko wazi, na ndiyo sababu nimeamua kuwania kiti hicho. Sitaenda peke yangu, nitaandamana na vijana,” akasema. Mchangunuzi wa siasa Profesa Obora Okoth anasema kauli za Winnie na Ruth zinapaswa kuchukuliwa kwa uzito, akizitafsiri kama ishara ya kutoridhishwa kwa sehemu ya familia na ushirikiano na Ruto. Anasema kauli ya Winnie inaashiria uwezekano wa kujiunga na Linda Mwananchi, huku akionya kuwa wanafamilia wanaowania nyadhifa za kisiasa hawataweza kutegemea jina la marehemu Raila pekee. “Ukoo wa kisiasa iliishia kwa Raila. Mmoja au wawili wanaweza kuchaguliwa, lakini itategemea uwezo wao binafsi,” akasema. Bi Ruth naye alionya kuwa yuko tayari kuondoka ODM ikiwa kubaki kwake kutamaanisha kusaliti misingi ya haki na demokrasia aliyotetea kaka yake. “Ikiwa itamaanisha mimi, Ruth Odinga, kupoteza kila kitu ili kusimama na ODM, nitafanya hivyo. La sivyo, nitahamia chama kingine kwa sababu ninataka haki iendelee kuwepo nchini Kenya,” akasema. Kauli hiyo ilizua majibu kutoka kwa naibu kiongozi wa ODM Simba Arati, aliyewaambia wanaotaka kuondoka kuwa wako huru kufanya hivyo. Alidai kuwa baadhi yao wamenunuliwa, huku akisisitiza kuwa ODM bado ina nguvu eneo hilo. Kwa upande wake, Raila Junior alisisitiza kuwa ODM ndicho chama alichoachiwa na baba yake. Alisema siasa za Raila zililenga kutetea wananchi wa kawaida, wanyonge, ugatuzi na umoja wa kitaifa na analenga ubunge wa Kibra kupitia ODM. Ida, ambaye aliwataka Wakenya kudumisha maridhiano na uvumilivu, pia alionya kuhusu wanasiasa wanaotumia jina la Raila kwa manufaa yao binafsi. “Wengi wataendelea kulitaja jina lake kwa sababu najua Wakenya walimpenda sana. Baadhi watafanya hivyo kwa mapenzi ya kweli, lakini wengine kwa kujinufaisha,” akasema. Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Luo, Ker Odungi Randa, aliitaka familia kubaki katika ushirikiano na serikali ya Ruto, akisema Raila alikuwa na sababu za kuchagua njia hiyo. “Naiomba familia ibaki imara katika serikali jumuishi alikowaachia. Wasitawanyike kwa kushawishiwa na wimbi la sasa. Nyasi zinaweza zisiwe za kijani zaidi upande mwingine,” akasema. Kwa jumla, mivutano hii inaonyesha kuwa urithi wa Raila si suala la nani atarithi jina lake pekee, bali pia ni nani atakayefafanua mwelekeo wa kisiasa aliouacha. Familia inaweza kuwa na nafasi katika pande tofauti kwa sasa, lakini kadri uchaguzi wa 2027 unavyokaribia, itakabiliwa na shinikizo la kuweka wazi misimamo yake. za Winnie na Ruth zinaonyesha kutoridhishwa na njia ya sasa ya ODM, huku Dkt Oginga na Raila Junior wakisisitiza umuhimu wa kubaki ndani ya chama na kuendeleza mkondo wa ushirikiano.
The High Court has ruled in favour of lawyers representing Chadema chairman Tundu Lissu in a constitutional petition challenging restrictions on their consultations with him at Ukonga Prison, finding that prison officers violated regulations protecting lawyer-client confidentiality. In a judgment delivered on Friday, October 16, 2026, the court found that the lawyers had proved their claims that prison officers could overhear their legal consultations with Lissu, who is being held on treason charges. The court ruled that the practice contravened Regulation 13 of the Prisons Regulations, 1968, and undermined the conditions necessary for preparing Lissu’s defence. It ordered prison authorities to allow his lawyers to meet and consult him privately, while maintaining security supervision without compromising the confidentiality of their communications. The court also directed the Commissioner General of Prisons to issue and circulate a circular to all prison heads across the country within 60 days, instructing them to protect prisoners’ and remand inmates’ right to consult their lawyers without their conversations being overheard. The judgment was delivered by Justice Amir Mruma on behalf of Justices Angelo Rumisha and Evaristo Longopa. The constitutional petition, numbered 7300/2026, was filed by lawyers Kulwa Maduhu, Nashon Nkungu and Paul Kisabo, who identified themselves as Lissu’s legal advisers in the criminal cases against him. They were represented by John Seka. The respondents were the Attorney General, the Commissioner General of Prisons, the Officer-in-Charge of Ukonga Prison and Lissu. The Tanganyika Law Society (TLS), which joined the proceedings as an interested party, was represented by Ferdinand Makore. Lawyers challenge restrictions The lawyers challenged restrictions they said had been imposed by the Officer-in-Charge of Ukonga Prison whenever they sought to consult Lissu in the facility’s remand section. They argued that the prison authorities had failed to comply with Regulation 13, which provides for confidential consultations between prisoners or remand inmates and their legal advisers. Mr Maduhu told the court that prison officers had, on several occasions, prevented the lawyers from meeting Lissu or delivering important documents relating to his cases. He said the Officer-in-Charge had informed them that the restrictions were based on instructions from the Commissioner General of Prisons. Mr Nkungu and Mr Kisabo told the court that, even when they were allowed to discuss legal matters with Lissu, prison officers stood close enough to overhear their conversations. The lawyers asked the court to declare that the conduct violated Regulation 13 and constitutional and legal provisions guaranteeing fair trial rights and privacy. The Attorney General raised a preliminary objection, arguing that the petition was improperly filed because the applicants had other legal avenues through which to obtain the relief they sought. The objection was based on Section 8(2) of the Basic Rights and Duties Enforcement Act, commonly known as BRADEA. Court rejects government objection Justice Mruma dismissed the preliminary objection, ruling that the applicants had no alternative legal remedy capable of providing the relief sought under the circumstances other than a constitutional petition. On the merits, he said the court had considered the pleadings and submissions from both sides and was satisfied that the lawyers had proved their claims. He explained that Regulation 13 allows prison officers to maintain visual supervision while inmates consult their lawyers but requires them to remain beyond hearing distance. The judge acknowledged that prisons were security institutions where supervision was necessary to prevent escapes and the introduction of prohibited items. However, he said the regulation sought to balance security requirements with the rights of people in custody. Citing decisions from courts in Kenya, Zambia and South Africa, he underscored the importance of protecting confidential professional communications between lawyers and their clients. The respondents confirmed that prison officers were present during consultations for security reasons but failed to demonstrate that they stood far enough away to prevent them from hearing the discussions. The court noted that no evidence had been presented establishing the distance between the officers and the lawyers. On documents brought into the prison, Justice Mruma said authorities could inspect them for security purposes but were not permitted to read them to establish their contents or confiscate them. “Therefore, we find that the consultations between the second and third applicants and their client took place in circumstances in which prison officers could hear them, contrary to the provisions of Regulation 13 of the Prisons Regulations,” he said. The judge added that Lissu’s decision to conduct his own defence did not extinguish his right to consult his lawyers on legal matters. Missing name on visitors’ list not enough The court also considered Mr Maduhu’s complaint that he had been denied access to Lissu because his name was not on a visitors’ list provided by the Chadema leader. Justice Mruma ruled that the omission of his name was not, in itself, sufficient legal grounds to deny him access because the requirement was not prescribed by law. He noted that Mr Maduhu had demonstrated that other lawyers and individuals whose names were not on the list had been allowed to meet Lissu. Referring to Article 13(6) of the Constitution, the judge said people facing criminal proceedings, particularly those that could result in severe punishment, must have access to proper legal representation and confidential consultations with their lawyers. He also cautioned against the misconception among some officials within the justice system that they had the authority to determine whether suspects were guilty. Under Article 107A(1) and (2) of the Constitution, he said, the administration of justice is vested in the courts. Although the court had no records establishing the precise extent to which Lissu had been affected, Justice Mruma said the evidence showed that prison conditions and restrictions on communication with his lawyers had undermined his rights. The court consequently found that allowing prison officers to remain within hearing distance during consultations violated Regulation 13 and was inconsistent with several constitutional provisions, including Articles 13(1), 13(3), 13(6)(a), 15, 16(1), 22, 26(1) and 29(2). In its final orders, the court directed the Commissioner General of Prisons to issue and circulate the circular to all prison heads within 60 days, requiring them to comply with Regulation 13 and safeguard prisoners’ and remand inmates’ right to communicate privately with their lawyers.