KIONGOZI wa People’s Prosperity Party (PPP), Eliud Owalo, ametangaza kuwa chama hicho kimepata usajili kamili, hatua inayokiruhusu kutangaza wagombea katika nyadhifa zote za uchaguzi mkuu wa 2027.
Bw Owalo, ambaye ananuia kutafuta tiketi ya chama hicho kuwania urais, alisema Afisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa (ORPP) imekipatia PPP cheti cha usajili kamili.
Hatua hiyo inakiwezesha chama hicho kujiandaa kushiriki uchaguzi wa urais, ubunge, ugavana na uwakilishi katika mabunge ya kaunti kote nchini.
"Kazi sasa ni kuvumisha chama, kuelekea maeneo mbalimbali ya nchi na kusaka uungwaji mkono. Binafsi usajili huu sasa unanipa motisha ya kusaka uungwaji mkono kwa Wakenya nikiwaeleza kile ambacho nitafanya nikipewa uongozi wa nchi," akasema Bw Owalo kwenye mahojiano na Taifa Leo.
"Nawahakikishia wawaniaji wote kuwa uteuzi utakuwa huru na haki na wananchi ndio wataamua nani anawahi tikiti ya chama chetu katika nafasi zote za uongozi. Kampeni zetu zitajikita katika kuhakikisha kwamba tunawahakikishia Wakenya kuwa tunayoahidi kinatimizwa," akaongeza Waziri huyo wa zamani wa Teknolojia na Mawasiliano.
Katika taarifa yake, PPP ilisema imetimiza masharti ya kisheria yanayohitajika ili kupata usajili kamili chini ya Sheria ya Vyama vya Kisiasa ya mnamo 2011.
Chama hicho kilipatiwa cheti cha usajili wa muda Juni 26, 2026, na kupewa siku 180 kutimiza masharti yaliyowekwa ili kupata usajili kamili.
Miongoni mwa masharti hayo ni kuwa na angalau wanachama 1,000 waliosajiliwa katika kila moja ya angalau kaunti 24.
Wanachama hao wanapaswa kudhihirisha uwakilishi wa kieneo na kikabila, uwiano wa kijinsia na uwakilishi wa makundi maalum, yakiwemo vijana, wanawake, watu wenye ulemavu na jamii za wachache.
Chama hicho pia kilitakiwa kuwa na makao makuu ya kitaifa, afisi za matawi katika angalau kaunti 24 na kamati ya utendaji katika ngazi ya kaunti.
PPP ilisema imetimiza masharti hayo na kuanzisha miundo ya chama katika kaunti 30, pamoja na makao makuu yake yaliyoko Muchai Drive, Nairobi.
Bw Owalo anatarajiwa kutumia tiketi ya PPP kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa Agosti 10, 2027.
Chama hicho pia kinapanga kusimamisha wagombea katika nyadhifa nyingine za uchaguzi kote nchini, kikiwa na lengo la kupanua uwepo wake kitaifa kabla ya uchaguzi huo.
Usajili huo unafanyika huku vyama vya kisiasa vikikabiliwa na makataa kadhaa yaliyowekwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Agosti 10, 2027.
Vyama vilitakiwa kuwasilisha kwa tume majina na saini za mfano za maafisa wao walioidhinishwa kufikia Oktoba 15, 2026. Kanuni za uteuzi wa wagombea zinapaswa kuthibitishwa na Msajili wa Vyama vya Kisiasa kufikia Oktoba 30 na kuwasilishwa kwa IEBC kufikia Novemba 6.
Ratiba ya uchaguzi pia inavitaka vyama kuwasilisha orodha za wanachama na maelezo ya wanaotaka kuwania nyadhifa mbalimbali kupitia mchujo wa vyama kufikia Machi 16, 2027.
Mchujo huo pamoja na utatuzi wa migogoro ya ndani kuhusu uteuzi wa wagombea unapaswa kukamilika kufikia Mei 8, 2027. IEBC itafanya uteuzi rasmi wa wagombea kati ya Mei 29 na Juni 11.
Owalo sasa kupambana na Ruto 2027 baada ya chama chake cha PPP kusajiliwa rasmi

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…