MAMA Ida Odinga amekemea vikali vurugu zilizoshuhudiwa wakati wa maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kifo cha mumewe, Raila Amolo Odinga, akisema matendo kama hayo yalionyesha dharau kwa familia yake na kumbukumbu ya mwanasiasa huyo.
Katika taarifa iliyotolewa Jumamosi, Oktoba 17, 2026, Ida alisema anasikitishwa na tabia ya baadhi ya waliohudhuria hafla ya kumbukumbu iliyofanyika Bondo kuzomea, kufoka na kuwatisha wageni walioalikwa.
Alisema taarifa kwamba baadhi ya watu huenda walilipwa na kusafirishwa hadi hafla hiyo kwa lengo la kuvuruga shughuli na kuwatisha wageni ni za kutia wasiwasi.
“Vitendo hivyo vinaonyesha dharau kubwa si kwa familia yetu pekee, bali pia kwa kumbukumbu ya Raila na maelfu ya watu waliofika kwa amani,” alisema.
Ida aliomba radhi wageni waliofanyiwa vitendo hivyo, akisema walifika kufariji familia wakati mgumu na walistahili kupokelewa kwa heshima, ukarimu na upendo.
Alionya viongozi wa kisiasa kuwa wana jukumu maalumu la kujizuia na kuhakikisha wafuasi wao wanaheshimu utu wa wengine, hata pale ambapo kuna tofauti za kisiasa.
Alisisitiza kuwa mwaliko wa familia haupaswi kutumiwa kama nafasi ya kuendeleza uhasama wa kisiasa.
“Mahali Raila alipopumzishwa hapapaswi kamwe kugeuzwa uwanja wa mapambano ya kisiasa. Wala majonzi ya familia yetu hayapaswi kutumiwa kama fursa ya kulipiza kisasi cha kisiasa,” alisema.
Ida, ambaye alikuwa kwenye ndoa na Raila kwa zaidi ya miaka 50, alisema mumewe aliamini katika uhuru wa kutofautiana, mazungumzo na maridhiano.
Alisema Raila aliweza kukabiliana na mamlaka na kupitia mateso ya kisiasa, lakini alielewa umuhimu wa watu wenye misimamo tofauti kuketi pamoja na kutafuta maelewano.
Aliwataka wanaotaka kumuenzi Raila kuendeleza maadili hayo badala ya kutumia kumbukumbu yake kuchochea migawanyiko.
Ida pia alifafanua kuwa kila mgeni aliyealikwa alikuwa amekaribishwa na familia ya Odinga haikuwa na ugomvi na yeyote kati yao. Alisema kutohudhuria kwa mtu hakupaswi kutafsiriwa kuwa kutokubaliana na familia.
Aidha, alishukuru kamati ya maandalizi ya kumbukumbu ya Raila, viongozi wa dini, wasanii, walijitolea na wote waliochangia kufanikisha maadhimisho hayo.
Alimshukuru Rais William Ruto kwa msaada wake kwa familia, hasa katika ujenzi wa kaburi la kumbukumbu la Raila.
Ida aliwashukuru maelfu ya Wakenya na wageni kutoka Afrika na kwingineko waliofika Bondo kuomba na kushiriki kumbukumbu za Baba.
Alisema Raila alikuwa wa familia yake, lakini pia alikuwa wa Kenya, Afrika na watu wengi ambao maisha yao aliyagusa.
Aliwataka viongozi na wafuasi wao kuheshimu familia, wageni na mahali Raila alipopumzishwa, akisema Wakenya wanapaswa kuenzi kumbukumbu yake kwa kuishi kwa heshima licha ya tofauti zao.
Ida akemea waliopanga vurugu wakati wa kumbukumbu ya Raila Bondo

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…