RAIS mstaafu Uhuru Kenyatta alifuta ziara yake ya Bondo kuhudhuria kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga kufuatia wasiwasi kuhusiana na usalama.
Timu ya maandalizi ya Bw Kenyatta ilikuwa tayari imewasili Bondo na kiti chake kutengwa katika jukwaa la wageni mashuhuri. Ndege yake pia ilikuwa tayari kuondoka kutoka Uwanja wa Wilson jijini Nairobi Alhamisi asubuhi, lakini hakufika.
Msemaji wake Kanze Dena-Mararo alisema kulikuwa na mabadiliko ya ratiba na suala lililohitaji kushughulikiwa, bila kufafanua zaidi.
Hata hivyo, hafla hiyo iligeuka jukwaa la malumbano ya kisiasa huku viongozi wakitofautiana kuhusu urithi wa Raila na uhusiano wao na Rais William Ruto.
Naibu kiongozi wa ODM Simba Arati alimshutumu Uhuru kwa kufadhili upinzani, huku Waziri wa Kawi Opiyo Wandayi akiwataka wakazi wa eneo hilo kumuunga mkono Rais Ruto.
Kutohudhuria kwa Uhuru kulivutia umakini kutokana na uhusiano wake wa kisiasa na Raila, hasa baada ya maridhiano yao ya Machi 2018 na uungwaji mkono wake kwa azma ya Raila kuwania urais mwaka 2022.
Kiongozi wa wachache katika Bunge la Kitaifa Junet Mohamed alisema hakuhudhuria kwa sababu ya uwepo wa jina la aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kwenye orodha ya walioalikwa.
Gachagua naye hakuhudhuria kwa sababu alikuwa Amerika.
Mjane wa Raila, Ida Odinga, alisema familia haikuwa na kinyongo na walioalikwa lakini wakakosa kufika. Hata hivyo, alikashifu vitendo vya kuzomea, kupiga kelele na kutisha wageni wakati wa hafla hiyo.
Bi Ida alionya dhidi ya kugeuza eneo la mazishi ya Raila kuwa uwanja wa mapambano ya kisiasa, akisema urithi wake ni mkubwa kuliko tofauti za viongozi.
Uhuru alikosa kuhudhuria makumbusho ya Raila kwa sababu ya hofu ya kiusalama

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…