WAZAZI wanakabiliwa na changamoto ya kuhakikisha watoto wao watakuwa salama wakiwa na shughuli za kuwaendeleza kiakili wakati wa likizo ndefu ya takriban siku 70, bila kutumia pesa nyingi.
Kwa mujibu wa kalenda ya Wizara ya Elimu ya mwaka 2026, muhula wa tatu unamalizika Oktoba 23, huku likizo ikiendelea hadi Januari 1, 2027. Baadhi ya wanafunzi watafanya mitihani ya kitaifa katika kipindi hiki.
Wataalamu wa malezi wanashauri wazazi kusawazisha mapumziko, michezo, kusoma na muda wa familia, badala ya kugeuza nyumba kuwa madarasa ya ziada.
Mwenyekiti wa Chama cha Kitaifa cha Wazazi, Silas Obuhatsa, amewataka wazazi kuwajibika kwa usalama wa watoto wao, ambao hawatakuwa chini ya usimamizi wa walimu.
“Wazazi lazima wawahudumie watoto na kuwaelekeza ipasavyo. Tumesikia kuhusu watoto wanaozama wanapoenda kuogelea. Lazima wazazi wawachunge watoto wao wakati wote wa likizo,” alisema.
Pia aliwaonya wazazi dhidi ya kuwahusisha watoto walio chini ya miaka 18 katika mikutano ya kisiasa na kampeni, akisema wanapaswa kulindwa dhidi ya shughuli zisizowafaa.
Alikosoa pia tabia ya baadhi ya wazazi kuwatuma watoto kufanya kazi ngumu sokoni badala ya kuwapa nafasi ya kupumzika baada ya mihula mitatu ya masomo.
Bw Obuhatsa anasema likizo ni fursa ya watoto kujifunza stadi za maisha, kama kupika, kufanya kazi za nyumbani na kuwajibika, huku wazazi wakihakikisha wanakamilisha kazi walizopewa shuleni.
Hata hivyo, alipinga kuwapeleka watoto katika masomo ya ziada ya kulipia, akisema walimu tayari wamekamilisha silabasi na kutoa kazi za likizo.
Wazazi wanaweza kuwaweka watoto katika shughuli za kuwajenga bila kutumia pesa nyingi. Kusoma vitabu, kuchora, kupika pamoja, kulima bustani, kucheza michezo na kutembelea maktaba ni baadhi ya njia zinazopendekezwa.
Mtaalamu wa malezi Juliet Chepkemoi anasema watoto wanahitaji muda wa kupumzika na kupona kutokana na shinikizo za masomo.
“Likizo huwapa nafasi ya kupumzika, kutafakari yaliyowafika na kupata nafuu kihisia,” alisema.
Hata hivyo, anaonya kuwa watoto wanaoachwa bila uangalizi kwa muda mrefu wanaweza kuathiriwa na marafiki wabaya, matumizi ya dawa za kulevya na maudhui yasiyofaa kwenye mitandao ya kijamii.
Anashauri wazazi kupanga shughuli za likizo pamoja na watoto, kulingana na umri, vipaji na uwezo wa kifedha wa familia.
Pia, wazazi wanapaswa kudhibiti muda wa watoto kutumia simu, televisheni na vifaa vya michezo ya kielektroniki ili shughuli hizo zisiathiri usingizi, mazoezi na mawasiliano ya kifamilia.
Bi Chepkemoi anasisitiza umuhimu wa mawasiliano ya wazi, akisema watoto wanapaswa kujihisi huru kuwaeleza wazazi changamoto zao bila kuogopa kuhukumiwa.
Lengo, anasema, si kuwashughulisha watoto kila dakika, bali kuwapa mazingira salama ya kupumzika, kucheza, kujifunza na kufurahia likizo.
Jinsi ya kuhakikisha usalama wa watoto wakiwa likizoni

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…