WATU 108 waliotangamana na wagonjwa wa Ebola nchini wako karantini katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH) na Hospitali ya Huduma za Polisi, huku nchi ikiwa na vitanda 211 vya kuwahudumia wanaogua maradhi hayo.
Ripoti ya kuhusu Ebola nchi ya Oktoba 14 inaonyesha kuwa watu 128 waliotangamana na mgonjwa wa kwanza walifuatiliwa. Kati yao, 108 wako karantini, huku 20 wakiwa nje ya karantini. Ufuatiliaji wa watu 15 unaendelea, huku watano wakiwa nje ya nchi.
Kenya ina visa viwili vilivyothibitishwa vya Ebola na kifo kimoja. Mgonjwa wa kwanza alikuwa Mkenya aliyesafiri kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupitia Uganda na kufariki Oktoba 5.
Mgonjwa wa pili, mwanaume mwenye umri wa miaka 39, alipata homa, uchovu na maumivu ya viungo akiwa karantini Oktoba 13. Vipimo katika maabara mbili vilithibitisha kuwa na Ebola na anapokea matibabu.
Jumla ya sampuli 324 kutoka kaunti 18 zimepimwa. Wakati huo huo, wasafiri 685,027 wamechunguzwa katika vituo 26 vya kuingia nchini.
Kenya pia imepokea vifaa vya kujikinga na kudhibiti maambukizi yenye thamani ya Sh61.1 milioni kutoka Amerika na mataifa mengine washirika wake. Vifaa hivyo ni pamoja na barakoa 3,600 za N95, chupa 9,000 za kusafisha mikono, viatu 1,080 vya kujikinga na mifuko 60 ya kuhifadhia miili kwa mazishi salama.
Katibu Mkuu katika Idara ya Afya ya Umma, Mary Muthoni Muriuki, alisema vifaa hivyo vitalinda wahudumu wa afya, wagonjwa na familia zao.
Wahudumu 4,917 wamefunzwa kuhusu Ebola, huku wataalamu 343 wakiwa tayari kupelekwa maeneo yatakayohitaji msaada. Serikali inatayarisha mpango wa kusambaza vifaa hivyo katika kaunti zilizo katika hatari kubwa ya maambukizi.
Watu 108 karantini Kenya ikipokea vifaa vya Sh61 milioni

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…