NAIBU Rais, Kithure Kindiki jana alisema kuwa uchaguzi mkuu wa 2027 utakuwa mashindano kati ya maendeleo na kelele za kisiasa.
Akikosoa upinzani kwa kukosa mwelekeo na kujihusisha na siasa za migawanyiko, Profesa Kindiki alionya kuwa viongozi wasio na rekodi ya maendeleo watashindwa uchaguzi huo.
Alisema serikali inalenga kutekeleza miradi ya maendeleo ili iwe na mafanikio ya kuwasilisha kwa Wakenya itakapoomba kura mwaka ujao.
Akizungumza katika soko la Riakiania alipokuwa akizindua miradi ya barabara na umeme, Profesa Kindiki alisema viongozi lazima wawe na rekodi inayoonekana ya maendeleo ili kupata uungwaji mkono wa wapigakura.
“Ni vigumu kwa viongozi kusimama mbele ya wananchi mwaka ujao na kuzungumzia siasa ikiwa hawana rekodi ya maendeleo. Wananchi hawali kelele, matusi na mapigano. Wanataka maendeleo, amani na umoja,” akasema.
Alishutumu upinzani kwa kuendeleza siasa za chuki, migawanyiko na uchochezi badala ya kuelekeza nguvu katika maendeleo.
Profesa Kindiki alisema serikali iko katika harakati za kutekeleza manifesto yake na kuahidi kuwa miradi yenye manufaa kwa wananchi itaendelea.
Pia alionya kuwa ghasia za kisiasa hazitavumiliwa nchini, akisema Kenya inahitaji amani na umoja.
Alitaja uchaguzi wa 2002, ambapo marehemu Mwai Kibaki na Uhuru Kenyatta walishindana kuwania urais bila ghasia na uharibifu wa mali, akiwataka viongozi wa sasa kuiga mfano huo.
“Ushindani wa kisiasa si uadui. Tuenzi siasa zilizokomaa zisizo na ghasia wala chuki,” akasema.
Pia aliwaonya viongozi wa upinzani dhidi ya matusi na tabia zisizofaa, akisema huenda wakalaaniwa na wazee waliompa hadhi ya kuwa kinara wa eneo la Mlima Kenya katika hafla ya Kirigiti.
Kuhusu maendeleo, Profesa Kindiki alisema tangu 2022, nyumba 32,000 katika Kaunti ya Kirinyaga zimeunganishwa na umeme. Serikali imetenga Sh845 milioni kuunganisha nyumba nyingine 10,800.
Eneobunge la Gichugu linafaidika na miradi 28 ya kusambaza umeme katika hatua ya mwisho, inayolenga nyumba 2,100 kwa gharama ya Sh75 milioni.
Alisema ujenzi wa barabara ya kilomita 53 inayounganisha Piai, Mbiri, Ngiriambu, Kiamutugu, Muchagara, Karumandi, Thumaita, Kamugunda, Kamweti, Kavote na Kimunye unaendelea kwa gharama ya Sh2 bilioni.
Barabara hiyo ni sehemu ya kilomita 571 zilizotengewa Sh42 bilioni kwa ajili ya kuwekwa lami Kirinyaga. Kazi ya kuweka lami kilomita 472 inaendelea kwa gharama ya Sh37 bilioni.
Kindiki: Kura ya 2027 itakukuwa mashindano kati ya kelele (upinzanini) na maendeleo (serikali)

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…