TANGAZO la Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) Winnie Odinga kuwa atawania useneta wa Nairobi unatarajiwa kuvuruga muungano wa Linda Mwananchi na upinzani siasa za 2027 zikishika kasi.
Seneta wa sasa wa Nairobi, Edwin Sifuna, ametangaza kuwa hatatetea kiti chake na analenga uongozi wa nchi ili kumwondoa Rais William Ruto.
Akiongea wakati wa maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kifo cha babake Raila Odinga, Winnie alisema kuwa sasa analenga kiti cha useneta wa Nairobi lakini hakuweka wazi iwapo atafanya hivyo kupitia ODM.
“Najua watu wengi wamekuwa wakiuliza mahali nipo na mahali naenda. Leo nataka kuwajibu ili isiwe uvumi tena,” akasema mbunge huyo wa EALA, Alhamisi.
“Ifahamike kuwa Edwin Sifuna akisaka afisi nyingine, kuna nafasi katika kiti cha useneta Nairobi na ndiyo maana nimeamua kuwania useneta wa Nairobi. Siendi peke yangu bali naenda na vijana,” akaongeza.
Kambi ya Linda Mwananchi ambako Winnie anaegemea, pamoja na viongozi wa upinzani kwa jumla wamekuwa wakisukuma wito wa umoja ambapo wanalenga ushirikiano katika kugawa viti kwenye baadhi ya maeneo hasa Nairobi na Mombasa.
Iwapo kutakuwa na muafaka kati ya Linda Mwananchi na upinzani kuhusu kugawana viti Nairobi basi huenda Winnie akajipata pagumu kwa sababu tayari Linda Mwananchi imetangaza kuunga mkono Babu Owino kuwania ugavana.
Kizingiti cha pili kinachomchongea Winnie zaidi ni kwamba ni vigumu sana kwa viti vya ugavana, ubunge, uwakilishi wa kike na useneta kushikiliwa na jamii moja Nairobi. Tangu uchaguzi wa 2013 viti hivyo vimeshikiliwa na viongozi kutoka jamii tofauti.
Tatu, iwapo Linda Mwananchi itashirikiana na upinzani kugawana viti Nairobi basi itakuwa vigumu kuachiwa ugavana na useneta au mbunge mwakilishi wa kike.
Katika mrengo wa upinzani tayari Mbunge wa Embakasi Kaskazini James Gakuya ametangaza kulenga ugavana kupitia DCP. Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua na kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka mnamo Novemba 2025 walisema vyama hivyo vitagawana nyadhifa za ugavana, useneta na mbunge mwakilishi wa kike wa Nairobi.
Nne, tangazo la Winnie linajiri wakati nduguye, Raila Junior, tayari alikuwa amemuidhinisha Mbunge wa Lang’ata Phelix Odiwuor maarufu Jalang’o, kugombea useneta wa Nairobi. Jalang’o amekuwa akiandamana na Rais William Ruto katika ziara mbalimbali jijini Nairobi ambapo amekuwa akirejelewa kama seneta.
Baada ya Winnie kutangaza azma yake ya useneta Jalang’o aliandika kwenye mitandao ya kijamii kwamba “Niko tayari’.
“Ningependa kumwambia mheshimiwa Jalas hongera sana kwa kusimama. Sisi tuko nyuma yako kama ODM,” akasema Raila Junior katika hafla moja ya viongozi wa ODM jijini mapema mwezi huu.
Tano, kwa kuwa Winnie anaonekana kuegemea mrengo wa Linda Mwananchi ambao unapinga kuchaguliwa tena kwa Rais Ruto, binti huyo wa mwendazake Raila Odinga atakuwa na kibarua kikali kushawishi wanachama wa ODM wamuunge mkono katika azma yake ya 2027.
Vizingiti vinavyokabili azma ya useneta ya Winnie Odinga

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…