RAIS William Ruto jana aliwateua makamanda wapya wa Jeshi na Kikosi cha Jeshi la wana Anga kisha kuwaidhinisha maafisa 21 wapandishwe vyeo katika huduma ya jeshi.
Mabadiliko hayo yalitangazwa kufuatia mapendekezo kutoka kwa Baraza la Ulinzi ambalo ni taasisi ya juu zaidi ya kufanya maamuzi yanayohusu Jeshi la Ulinzi Nchini (KDF).
Meja Jenerali David Kipkemboi Ketter alipandishwa cheo kuwa Luteni Jenerali na kuteuliwa Kamanda wa Jeshi la Nchi Kavu.
Ni hatua kuu kwa taaluma ya Luteni Jenerali Ketter katika KDF kwa kuwa 2023 alikuwa miongoni mwa maafisa wa jeshi waliotunukiwa na rais. Wakati huo alipandishwa cheo na kuteuliwa kuwa Naibu Kamanda wa Jeshi la Nchi Kavu.
Luteni Jenerali Ketter amechukua nafasi ya Luteni Jenerali David Kimaiyo Chemwaina Tarus, ambaye amepelekwa katika Chuo Kikuu cha Ulinzi Kenya ili kuhudumu kama naibu chansela.
Hadi uteuzi wake mpya, Luteni Jenerali Ketter alihudumu vilevile kama Naibu Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi aliyesimamia wafanyakazi na mipangilio.
Hatua ya kumtaja Luteni Jenerali Ketter kama Mkuu wa Jeshi la Nchi Kavu ina maana ndiye mtu wa tatu kwenye foleni ya kuwa mkuu wa jeshi nchini. Hii ni kwa kufuata mzunguko wa kuyatoa mamlaka kwenye uteuzi wa mkuu wa jeshi, kulingana na sheria zilizowekwa na Jenerali Mstaafu Daudi Tonje.
Wengine katika daraja hilo ni pamoja na Luteni Jenerali Tarus na Luteni Jenerali Juma Shee Mwinyikai (Kamanda wa Chuo cha Kitaifa kuhusu Mafunzo ya Ulinzi).
Uteuzi wa kuwa mkuu wa jeshi nchini, hata hivyo, unazingatia masuala mengine, ukiwemo umri.
Jenerali Charles Kahariri anatoka kikosi cha jeshi la wanamaji naye Jenerali Francis Ogolla aliyeaga dunia Aprili mwaka jana, alitoka kikosi cha Jeshi la Anga.
David Ketter apandishwa cheo, sasa kusimamia Jeshi la Nchi Kavu
This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
EducationalKitui school gets new irrigation project as govt announces 7 more under KRISE programme
The government commissioned a micro-irrigation project at Kangalu School in Kitui County, benefiting 2,400 people as seven more projects are planned.
EducationalNyumbu kupata miundombinu bora ya shule
KIBAHA: MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Kibaha, Dk.Nicas Mawazo, ameahidi kushirikiana na Baraza la Madiwani pamoja na wataalamu wa halmashauri hiyo kuhakikisha miundombinu ya elimu katika Shule ya Sekondari na Msingi Nyumbu inaboreshwa, ili kuimarisha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji. Ahadi hiyo ameitoa wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua miundombinu ya shule hizo…
EducationalKenyan Form 4 boy shreds his trouser, shirt after finishing KCSE exams: “Amekafunga in style”
A Kenyan Form 4 student celebrated finishing the 2026 KCSE exams by cutting his school trousers into tassels in a viral video shared by Nairobi Juice online.
EducationalUniversity of America challenges NUC over illegal operations
By Ibrahim Hassan-Wuyo The National Universities Commission (NUC) and the University of America, Curaçao, have disagreed over the legality of the institution’s academic operations in Nigeria, with the commission warning prospective students against seeking admission into its programmes. The NUC had declared the institution’s operations in Nigeria illegal, alleging that it was admitting students, running […]