Fedha za mitihani zarejeshwa baada ya raia kukemea serikali

WAZAZI wa watahiniwa wanaotarajiwa kufanya mitihani ya kitaifa mwaka huu sasa wamepata afueni baafa ya Bunge la Kitaifa kutenga Sh5.9 bilioni za mitihani hiyo katika shule za msingi, shule za sekondari msingi na sekondari pevu.
Hii ni kufuatia kilio kutoka kwa wadau mbalimbali na Wakenya kwa ujumla baada ya makadirio ya awali ya bajeti kutotengea Baraza la Kitaifa la Mitihani (KNEC) fedha za kugharamia mitihani ya kitaifa katika shule zote.
Mitihani hiyo itakayoanza kufanywa Novemba mwaka huu ni Mtihani wa Kitaifa wa Gredi ya Sita (KPSEA), Mtihani wa Kitaifa wa Sekondari Msingi (KJSEA) na Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne (KCSE).
Sasa Kamati ya Bunge kuhusu Elimu imependekeza kutengwa kwa Sh5.9 bilioni kutoka mgao wa idara zingine ili kufadhili mitihani ya kitaifa.
Pendekezo hilo sasa liko mbele ya Kamati ya Bunge la Kitaifa kuhusu Bajeti (BAC).
Haya yanajiri baada ya Waziri wa Fedha John Mbadi kutangaza kuwa serikali itaangalia upya mfumo wa usimamizi wa mitihani ya kitaifa na wale ambao serikali inapasa kuwalipa ada za mitihani ya kitaifa.
“Tunapendekeza ugavi wa Sh5.9 bilioni za kugharamia usimamizi wa mitihani ya kitaifa, pesa ambazo hazikuwa zimetengwa kwenye makadirio ya bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2025/2026,” kamati hiyo ikasema kwenye ripoti yake kuhusu bajeti hiyo ya mwaka ujao wa kifedha.
Pesa hizo zitapatikana kutoka mgao wa fedha za matumizi ya kawaida za Sekondari ya Msingi (Sh2 bilioni), Shule za Sekondari (Sh3 bilioni) na Shule za Msingi (Sh900 milioni).
Bajeti ya jumla inayohitaji kufadhili mitihani ya kitaifa ya KPSEA, KJSEA na KCSE ni Sh12.58 bilioni.
Makadirio ya bajeti yaliyowasilishwa bungeni mwezi Aprili yalionyesha kuwa sekta ya elimu ilipunguziwa kima cha Sh62 bilioni. Vitengo mbalimbali katika sekta hiyo viliathirika kinyume na ilivyopendekezwa katika Taarifa ya Sera Kuhusu Bajeti (BPS).
Kwa mfano, kulingana na makadirio hamna pesa zilizotengewa mitihani ya kitaifa na usimamizi wa mitihani hiyo ambayo kwa jumla inahitaji Sh12.5 bilioni.
Aidha, Sh1.8 bilioni zilipunguzwa katika mgao wa kufadhili masomo katika shule za msingi za umma huku Sh21.85 bilioni zikiondolewa kwenye mgao wa fedha za kufadhili elimu katika shule za upili.
Awali, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge kuhusu Elimu Julius Melly alikuwa ameapa kuwa kamati yake haingeandaa ripoti ya bajeti hadi fedha za mitihani zirejeshwe.
IMETAFSIRIWA NA CHARLES WASONGAWAZAZI wa watahiniwa wanaotarajiwa kufanya mitihani ya kitaifa mwaka huu sasa wamepata afueni baafa ya Bunge la Kitaifa kutenga Sh5.9 bilioni za mitihani hiyo katika shule za msingi, shule za sekondari msingi na sekondari pevu.
Hii ni kufuatia kilio kutoka kwa wadau mbalimbali na Wakenya kwa ujumla baada ya makadirio ya awali ya bajeti kutotengea Baraza la Kitaifa la Mitihani (KNEC) fedha za kugharamia mitihani ya kitaifa katika shule zote.
Mitihani hiyo itakayoanza kufanywa Novemba mwaka huu ni Mtihani wa Kitaifa wa Gredi ya Sita (KPSEA), Mtihani wa Kitaifa wa Sekondari Msingi (KJSEA) na Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne (KCSE).
Sasa Kamati ya Bunge kuhusu Elimu imependekeza kutengwa kwa Sh5.9 bilioni kutoka mgao wa idara zingine ili kufadhili mitihani ya kitaifa.
Pendekezo hilo sasa liko mbele ya Kamati ya Bunge la Kitaifa kuhusu Bajeti (BAC).
Haya yanajiri baada ya Waziri wa Fedha John Mbadi kutangaza kuwa serikali itaangalia upya mfumo wa usimamizi wa mitihani ya kitaifa na wale ambao serikali inapasa kuwalipa ada za mitihani ya kitaifa.
“Tunapendekeza ugavi wa Sh5.9 bilioni za kugharamia usimamizi wa mitihani ya kitaifa, pesa ambazo hazikuwa zimetengwa kwenye makadirio ya bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2025/2026,” kamati hiyo ikasema kwenye ripoti yake kuhusu bajeti hiyo ya mwaka ujao wa kifedha.
Pesa hizo zitapatikana kutoka mgao wa fedha za matumizi ya kawaida za Sekondari ya Msingi (Sh2 bilioni), Shule za Sekondari (Sh3 bilioni) na Shule za Msingi (Sh900 milioni).
Bajeti ya jumla inayohitaji kufadhili mitihani ya kitaifa ya KPSEA, KJSEA na KCSE ni Sh12.58 bilioni.
Makadirio ya bajeti yaliyowasilishwa bungeni mwezi Aprili yalionyesha kuwa sekta ya elimu ilipunguziwa kima cha Sh62 bilioni. Vitengo mbalimbali katika sekta hiyo viliathirika kinyume na ilivyopendekezwa katika Taarifa ya Sera Kuhusu Bajeti (BPS).
Kwa mfano, kulingana na makadirio hamna pesa zilizotengewa mitihani ya kitaifa na usimamizi wa mitihani hiyo ambayo kwa jumla inahitaji Sh12.5 bilioni.
Aidha, Sh1.8 bilioni zilipunguzwa katika mgao wa kufadhili masomo katika shule za msingi za umma huku Sh21.85 bilioni zikiondolewa kwenye mgao wa fedha za kufadhili elimu katika shule za upili.
Awali, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge kuhusu Elimu Julius Melly alikuwa ameapa kuwa kamati yake haingeandaa ripoti ya bajeti hadi fedha za mitihani zirejeshwe.
IMETAFSIRIWA NA CHARLES WASONGA