ARUSHA: LICHA ya mikoa ya Kanda ya Kaskazini kuwa na utoshelevu wa chakula lakini bado kunachangamoto kubwa ya udumavu ,utapiamlo na lishe duni. Kufuatia changamoto hiyo wataalamu wanatoa elimu nzuri ya kilimo na aina za vyakula vinavyopaswa kuliwa. Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amesema hayo wakati akifungua Maonesho ya 31 Kilimo na Ufugaji…
Nilikosa alama za kujiunga na chuo kikuu. Familia yangu inanilazimisha nijiunge na chuo cha kiufundi nisome ualimu lakini mimi nataka kuwa DJ. Naomba ushauri? Ni jukumu la mzazi kukushauri ila ikiwa kipaji chako kiko kwenye muziki, tafuta njia ya kuonyesha kuwa unaweza kuwa DJ mwenye nidhamu na mafanikio. Jaribu kupata mafunzo rasmi au hata kozi ili uridhishe familia na moyo wako. Tunajuana mtandaoni na tayari ataka tuoane! Nilikutana na mwanamume mtandaoni na tukapendana sana. Hatujawahi kukutana ana kwa ana. Sasa anataka tufunge ndoa. Ni sawa kumuamini? Mapenzi ya mtandaoni yamejaa vizingiti. Kumjua mtu kwa ujumbe si sawa na kumjua ana kwa ana. Kabla ya kufikiria ndoa, jitahidi mkutane, ujue familia yake, marafiki zake, na maisha yake halisi. Usikimbilie harusi kwa sababu ya emojis. Kazi nje ya nchi au ndoa? Ninapewa nafasi ya kuenda kufanya kazi nje ya nchi miaka mitano, lakini mchumba wangu hataki niende. Je, ndoto zangu ni muhimu kuliko ndoa? Ndoto zako ni sehemu yako. Kama mchumba wako anakupenda kwa kweli, atakuvumilia na kukusubiri. Usikubali kufunga ndoto zako kwa sababu ya hofu ya kumkosa mtu. Ni sawa kuishi kwa mavyaa? Hujambo shangazi. Nimeolewa lakini bado tunaishi na mama mkwe kwa sababu mume wangu hana uwezo wa kulipa kodi ya nyumba. Je, ni aibu kuishi kwa wazazi baada ya ndoa? Si aibu kuishi kwa mama mkwe ikiwa ni hali ya muda mfupi na kutokana na sababu halali kama ukosefu wa pesa. Aibu huwa pale mume anakosa mipango ya kujitegemea na kutegemea mamake.
DAR ES SALAAM; Dk Cosmas Mwaisobwa, Msaidizi wa Makamu wa Rais (hotuba) amepokea Kitambulisho cha Uandishi wa Habari (Presscard) kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) Wakili Patrick Kipangula. Dk Mwaisobwa alipokea kitambulisho hicho jana Agosti 6, 2025 baada ya kukidhi vigezo vinavyohitajika kisheria, ambapo yeye ana elimu…
ARUSHA: Shule ya Msingi ya Highridge imesema imejiandaa vyakutosha kuelekea mashindano ya vijana kwa nchi za Afrika Mashariki ‘Chipukizi Cup’ yatakayofanyika Desemba 15 hadi 21 mwaka huu. Mkurugenzi na kocha wa Highridge, Adam Washokera amesema maandalizi yanaendelea vizuri ikiwemo kuwaandaa vijana wao ili kuwakilisha vizuri taifa. Amesema wamekuwa na mipango mbalimbali shuleni ukiacha elimu wanayoitoa…
ARUSHA: Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) nchini Tanzania imewata wafanyabiashara kuendelea kuzingatia sheria ,kanuni na taratibu kwa kuuzaa bidhaa kwa usahihi kama ilivyoelekezwa. Meneja wa EWURA, Kanda ya Kaskazini, Lorvii Long’idu amesema hayo katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Arusha ambapo mamlaka hiyo imefika kwa ajili ya kutoa elimu kwa…
BUKOBA: Taasisi ya Utafiti ya Kahawa mkoani Kagera (TACRI) imewapa elimu wakulima wa kahawa mkoani humo huku ikiwapa amri nane za kuongeza tija la zao hilo. Aidha, lengo ni kuzalisha tani 200,000 ifikapo mwaka 2030. Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Kanda ya Kagera, Dk Nyabisi Ngho,ma amesema utafiti uliofanywa kwa wakulima wa zao la kahawa mwaka…
IDARA ya Habari – MAELEZO imeandaa mwongozo kwa vyombo vya habari uonavitaka viepuke maudhui ya chuki, ubaguzi, kashfa, matusi na kuchochea vurugu katika kuripoti Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu. Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Egbert Mkoko amesema mwongozo huo pia unawataka waandishi wa habari kuchapisha habari za kweli, sahihi na…
DAR ES SALAAM: Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule amewataka viongozi wa serikali za mitaa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu utunzaji wa ardhi na uhifadhi wa mikoko katika wilaya hiyo ili kuwa na mazingira bora. DC Mtambule ameeleza hayo leo jijini Dar es Salaam eneo la Kilongawima katika wilaya hiyo wakati wakipanda miti ya…
USIMAMIZI wa Shule za Kabarak umekanusha kuwa ulikataa kuruhusu vitukuu wawili wa Rais Mstaafu Daniel arap Moi wajiunge na Shule ya Msingi ya Moi Junior na kuenda kinyume na amri ya korti. Naibu Chansela wa Chuo Kikuu cha Kabarak, Prof Henry Kiplagat ambaye pia ni katibu wa Wakfu wa Chuo Kikuu cha Kabarak, alitetea taasisi hiyo kuwa ilipuuza amri ya korti kwa kukataa vitukuu hao wawili wajiunge na shule ya Moi Junior. Akiwa mbele ya Hakimu Mwandamizi Kipkurui Kibelion baada ya kuagizwa afike kortini, alipuuza madai hayo na kusema Shule ya Moi Junior haikuwa imepokea barua kutoka kwa wazazi wa mtoto huyo ya kutaka kusomea shuleni humo. Alisisitiza kuwa kuna mchakato wa kufuatwa katika kujiunga na shule hiyo na wa kwanza ni kujaza na kuwasilisha fomu za kutuma maombi. “Hatujapuuza amri ya korti na hakuna maombi au ombi lolote ambalo limetumwa kwa mpango wowote wa masomo. Shule ya Msingi ya Moi Junior haijapata ombi lolote,” akasema. Pia naibu chansela huyo alisema kuwa shule hiyo haipendelei au kutoa huduma bora kwa mwanafamilia yeyote ya Rais Moi akisema kuwa maombi yote lazima yafuate mchakato uliowekwa. Prof Kiplagat alikuwa ameagizwa kwa nini hajafuata amri ya korti na kuruhusu watoto hao wajiunge na shule ya Moi Junior. Hii ni kufuatia madai ya Collins Kibet, mjukuu wa Moi kupitia mawakili wake kuwa alikuwa akipata ugumu kuhakikisha wanawe hao wanajiunga na shule hiyo. Mnamo Februari, mahakama iliamrisha Bw Kibet ahakikishe watoto wake wawili wanajiunga na mojawapo ya shule zinazosimamiwa na Kabarak na pia awajumuishe kwenye mpango wa bima ya matibabu. Kwa kukosa kutimiza amri hii, Bw Kibet alizuiliwa kwa wiki mbili kuanzia Julai 9 kabla ya kuachiliwa kwa dhamana ya Sh1 milioni. Ijumaa iliyopita, Bw Kibet aliamrishwa aanze mchakato wa kuhakikisha kuwa watoto hao wanajiunga na shule ya Kabarak. Fomu hizo ziliwasilishwa na Prof Kiplagat kortini. Bw Kibet amekuwa kwenye mvutano na aliyekuwa mkewe Gladys Jeruto Tagi ambaye amemshutumu kwa kukosa kujukumikia malezi ya watoto wao wawili. Bi Jeruto aliwasilisha kesi akitaka Bw Kibet aadhibiwe kwa kupuuza amri ya korti 2022. Amri hiyo ilimtaka agharimie elimu ya watoto hao, gharama ya matibabu na pia sehemu ya buradani, pesa zote zikiwa Sh1.5 milioni kwa mwaka. Alidai Bw Kibet alikuwa amefeli kutekeleza majukumu hayo na kumwacha na mzigo wa kutimiza maslahi ya watoto hao.
UKATILI wa wanafunzi kwa wenzao unaweza kutokea mahali popote, na kwa mtoto yeyote. Hata hivyo, kwa mujibu wa utafiti mpya, baadhi ya watoto wako katika hatari kubwa zaidi ya kudhulumiwa kuliko wengine. Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Nebraska, mjini Lincoln, waligundua kuwa wanafunzi wanaopokea huduma za elimu maalum kwa matatizo ya tabia, pamoja na wale walio na ulemavu unaoonekana wazi (kama matatizo ya lugha au kusikia), wana uwezekano mkubwa wa kuwa waathiriwa wa ukatili wa wanafunzi wenzao kuliko wale wa elimu ya kawaida. Zaidi ya hayo, watoto hawa pia wanaweza kuwa na uwezekano mkubwa wa kuwadhulumu wenzao.Utafiti uliochapishwa katika Journal of School Psychology ulifuatilia zaidi ya wanafunzi 800 wa elimu maalum na ya kawaida, wenye umri wa kati ya miaka tisa hadi 16, katika shule tisa za msingi, kati na upili. Matokeo yalionyesha kuwa watoto wanaopokea elimu maalum walikuwa na uwezekano mkubwa si tu wa kudhulumiwa, bali pia wa kuwadhulumu wengine. Asilimia 67 ya wanafunzi hao waliripoti kuwa wamewahi kudhulumiwa, huku zaidi ya theluthi moja (asilimia 38.1) wakikiri kuwa wamewahi kuwadhulumu wanafunzi wenzao. Waandishi wa utafiti huo wanaeleza kuwa watoto wenye ulemavu unaoonekana wanaweza kuwa waathiriwa wa ukatili kwa sababu huonekana kuwa rahisi kudhulumiwa. Pia wanapendekeza kuwa baadhi ya watoto hao wanaweza kujihusisha na ukatili kama njia ya kulipiza kisasi. Kwa mujibu wa matokeo, wanafunzi wa elimu maalum pia walikuwa na uwezekano mkubwa wa kupelekwa ofisini kwa mwalimu mkuu kwa sababu ya masuala ya nidhamu. Utafiti pia ulibaini kuwa tabia ya ukatili sio kwa jinsia moja pekee. Wasichana na wavulana wote walionekana kuathiriwa kwa kiwango sawa. “Tumesoma habari za kusikitisha kuhusu watoto na vijana waliokatiza maisha yao baada ya kukumbwa na ukatili wa mara kwa mara na wa kudumu. Mbali na vifo hivyo vya kuhuzunisha, kuna athari nyingine nyingi za ukatili ambazo huenda haziripotiwi mara kwa mara lakini ni muhimu sana kushughulikiwa,” asema mtafiti na mtaalamu wa malezi Dkt Debbie Glasser. Anatoa mfano wa watoto wanaodhulumiwa akisema wanaweza kuanza kukumbwa na wasiwasi, huzuni, na matatizo ya kiafya.Wazazi, walimu na wataalamu wengine wanapaswa kufahamu viashiria vya hatari na dalili za ukatili. Baadhi ya ishara kwamba mtoto anaweza kuwa anadhulumiwa ni:Kukosa usingizi au kuwa na ndoto mbaya mara kwa mara, mabadiliko ya tabia ya kula, kutafuta visingizio vya kuepuka kwenda shule, majeraha yasiyoelezeka, kupoteza au kuharibu vitu vya thamani (kama pesa, iPad, simu), kupungua kwa hali ya kujiamini, kuongezeka kwa malalamishi ya maumivu ya kichwa au tumbo na kushuka kwa ghafla kwa alama za mitihani. Hata hivyo, kuwepo kwa tabia hizi hakumaanishi moja kwa moja kwamba mtoto anadhulumiwa. Ikiwa mzazi au mlezi ana wasiwasi kuhusu mtoto wake, anapaswa kutafuta msaada kutoka kwa mtaalamu. Watafiti wanatoa mapendekezo kadhaa kulingana na matokeo yao. Wanashauri kuwa mipango ya kuzuia ukatili inapaswa kutekelezwa kwa wanafunzi wote wa elimu maalum na ya kawaida, ili kukuza ujuzi wa kijamii. Wanatumai kuwa wanafunzi wenye ujuzi wa kijamii wanaweza kuwa mfano mwema kwa wenzao.Pia, wanapendekeza kuwa walimu na wafanyakazi wa shule wawasaidie wanafunzi wenye ulemavu unaoonekana katika madarasa ya elimu ya kawaida ili kusaidia kupunguza visa vya ukatili.
GEITA; KAMPUNI ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) imeanza utekelezaji wa mpango wezeshi kufanikisha mazingira rafiki ya afya ya uzazi kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Geita. Mpango huo unatekelezwa kupitia mradi wa usambazaji wa taulo za kike kwa wanafunzi waweze kujisitiri wakati wa hedhi pamoja na ufadhili wa mafunzo ya…
DAR-ES-SALAAM : TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi imezitaka taasisi na asasi za kiraia zilizopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura kuzingatia sheria, kanuni na maelekezo ya Tume wakati wa utekelezaji wa majukumu yao katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
DAR-ES-SALAAM : VIWANGO vya unyonyeshaji wa maziwa ya mama nchini Tanzania vinaendelea kuimarika, huku asilimia ya watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya mama pekee ikiongezeka kutoka asilimia 58 mwaka 2018 hadi asilimia 64 mwaka 2022.
A total of 734 farmers from 17 Agricultural Marketing Cooperative Societies have successfully completed training under the Elimu Tija initiative, a programme spearheaded by the Kilombero Community Charitable Trust in collaboration with Kilombero Sugar Company Limited
RAIS William Ruto amehakikishia Wakenya kwamba utawala wake unachukulia kwa uzito mkubwa ufadhili wa elimu bila malipo licha ya hofu ya mgao kwa shule kupunguzwa. Akizungumza Jumapili, Julai 27, 2025 katika kanisa la Kianglikana la St Martins, Kariobangi, Nairobi, Rais alisisitiza kwamba elimu ingali nguzo kuu ya kitaifa. “Nataka kuhakikishia kila mtu kwamba elimu haitaborongwa. Hatuwezi kuhatarisha upatikanaji wa elimu ya ubora wa juu na hatuwezi kudhalilisha umuhimu wa elimu,” akasema. Matamshi yake yanajiri wakati kuna mjadala mkubwa uliosababishwa na kukiri mbele ya Bunge kwa Waziri wa Fedha John Mbadi kwamba serikali imepunguza mgao wa fedha kwa kila mwanafunzi kutoka Sh22,244 hadi Sh16,428 (upungufu wa Sh5,340) huku pia akisema Serikali inalemewa kufadhili Elimu Bila Malipo kikamilifu.
Wazazi wana mitazamo tofauti kuhusu watoto wao wadogo na utazamaji wa runinga. Huku baadhi ya wazazi wakikosa kuruhusu kabisa watoto wao kutazama runinga wakiwa na umri mdogo, wengine huwaruhusu watoto wao kutazama vipindi maalum mradi tu vinafunza maadili au vina thamani ya kielimu. Hii si makala ya kuamua iwapo mtoto wako anapaswa kutazama runinga au la – huo ni uamuzi wa kibinafsi unaotegemea familia husika. Kwa wazazi wanaoruhusu watoto wao kutazama runinga, makala hii inalenga kuwasaidia kuhakikisha wanapata manufaa ya kweli kutokana na kile watoto wao wanachotazama. Vipindi vya watoto vinavyolenga elimu mara nyingi huishia kufaidi mtoto kuhusu maisha – kama vile kuwa na nidhamu, kuishi kwa amani na familia, au kuwatendea mema marafiki. Hii ndio sababu vipindi hivi huvutia sana wazazi wengi. Hata hivyo, watoto wanaweza kushushuhudia migogoro au tabia hasi miongoni mwa wahusika. Ili mtoto aelewe somo kuu la hadithi ya runinga, anahitaji kuwa na uwezo wa kufikiri kwa undani – kuunganisha mwanzo, kati na mwisho wa simulizi, kuelewa sababu ya changamoto na matokeo yake, na kwa nini tabia njema ni chaguo bora. Tatizo ni kuwa uwezo huu wa kufikiri bado huwa unaendelea kukua kwa watoto. Hii inamaanisha kuwa, licha ya kujifunza maadili mazuri, kuna uwezekano pia wanaiga baadhi ya tabia hasi wanazoona kabla ya kupata ujumbe chanya. Katika utafiti uliochapishwa hivi karibuni kwenye Journal of Applied Developmental Psychology,watafiti waligundua kuwa vipindi vya kielimu kwa watoto vinaweza kwa bahati mbaya kufundisha baadhi ya tabia mbaya pia. Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Iowa State na Chuo Kikuu cha Buffalo, New York, waliwachunguza watoto wa chekechea darasani na kwenye uwanja wa michezo katika vituo tofauti vya kulelea watoto. Walikusanya pia taarifa kutoka kwa walimu na wazazi. Waligundua kuwa watoto waliotazama vipindi vya kielimu walionyesha tabia za "unyanyasaji wa uhusiano" kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na wale wasiovitazama. Huu si unyanyasaji wa kimwili, bali ni ule wa kihisia kama vile kusema: “Wewe si rafiki yangu tena” au “Hutakaribishwa kwenye sherehe yangu ya kuzaliwa.” Ingawa lengo la vipindi hivi ni kufundisha watoto jinsi ya kutatua migogoro ya uhusiano, si watoto wote wanaweza kutofautisha kati ya somo linalofundishwa na tabia wanayopaswa kuiga. Kabla hujapiga marufuku kabisa vipindi vya watoto, kuna hatua kadhaa za kuchukua Weka muda wa kutazama Hakikisha mtoto anapata muda wa kucheza, kutangamana na marafiki au familia, na kushiriki mazoezi. Shughuli hizi mara nyingi hufundisha mambo muhimu zaidi ya yale yanayoonyeshwa kwenye runinga. Chagua kwa makini Angalia kwa makini maudhui ya vipindi anavyotazama mtoto wako. Si kila kipindi cha watoto kinafaa. Tazama mamoja na mtoto Kuwa sehemu ya utazamaji. Zungumza naye kuhusu anachoona.Mweleze ni kwa nini tabia hasi katika kipindi haikuwa sahihi na jinsi ilivyomwathiri mhusika mwingine. Vilevile, muonyeshe matokeo mazuri ya tabia njema.
ARUSHA: VIJANA wametakiwa kuchangamkia fursa za masomo nje ya nchi ili waweze kujiendeleza zaidi kielimu kupitia vyuo vikuu mbalimbali duniani. Akizungumza katika Maonesho ya Elimu ya Vyuo Vikuu nje ya nchi yaliyofanyika Arusha, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Education Link LTD, Abdulmalik Mollel alisema kazi kubwa wanayoendelea kuifanya ni kuwapa fursa vijana wa kitanzania…
Wadau wa elimu wamekasirika vikali baada ya serikali kutangaza kuwa haiwezi kufadhili kikamilifu mpango wa elimu bila malipo, wakionya kuwa sekta ya elimu ya msingi nchini iko katika hatari kubwa kufuatia kupunguzwa kwa mgao wa serikali kwa wanafunzi. Katika hotuba yake mbele ya Kamati ya Elimu ya Bunge la Taifa, Waziri wa Fedha John Mbadi alikiri kuwa serikali haina uwezo wa kugharamia kwa ukamilifu mipango ya Elimu ya Msingi Bila Malipo (FPE) na Elimu ya Sekondari Bila Malipo (FDSE). Chini ya mpango wa FPE, kila mwanafunzi anatakiwa kupata Sh1,420 kwa mwaka, wale wa Sekondari Msingi Sh15,042, na wanafunzi wa sekondari Sh22,244. Hata hivyo, Bw Mbadi alifichua kuwa mgao kwa wanafunzi wa sekondari umepunguzwa kutoka Sh22,244 hadi Sh16,428 kwa mwaka, na kusababisha pengo la Sh5,340 kwa kila mwanafunzi. Hii imewaacha wakuu wa shule wakikabiliwa na madeni kwa wasambazaji wa bidhaa na mishahara ya wafanyakazi wasio walimu. Hatua hiyo imezua hofu ya ongezeko la wanafunzi wanaoacha shule na mwisho wa sera ya elimu ya msingi bila malipo. Chama cha Walimu Wakuu wa Shule za Sekondari (KESSHA) kimeitaka serikali kuruhusu wazazi kugharamia elimu, kutokana na kupungua kwa mgao huo wa serikali. “Mkuu wa shule anatarajiwa kuendesha shule bila pesa za kutosha huku akizuiwa kushirikiana na wazazi kuziba pengo la kifedha. Hali hii haiwezi kudumu,” alisema mwenyekiti wa KESSHA, Bw Willy Kuria. Pia alitaka serikali itoe ruzuku ya dharura kufidia upungufu uliopo kwani shule zilifanya maamuzi ya kifedha kwa msingi wa ahadi ya kupata mgao kamili. “Hata wakati mgao ulikuwa Sh22,244, bado haukutosha kwani kiwango hicho kilitekelezwa zaidi ya miaka minane iliyopita bila kuzingatia mfumuko wa bei na gharama zilizoongezeka. Thamani halisi ya kiasi hicho imepungua sana, na kufanya iwe vigumu kutoa elimu bora katika mazingira ya sasa,” aliongeza Bw Kuria. Chama cha Kitaifa cha Wazazi (NPA) kilionya kuwa kupunguzwa kwa ufadhili kunaweza kusababisha janga jipya katika sekta ya elimu, na kuwalazimu maelfu ya wanafunzi kuacha shule. “Hii ni habari ya kushtua kwa wazazi. Wakati huu ambapo wengi bado wanapambana na kupoteza ajira na kupungua kwa mapato, serikali ilipaswa kuongeza mgao, si kuupunguza,” alisema mwenyekiti wa NPA, Bw Silas Obuhatsa. Chama cha Wadau wa Elimu Kenya (ESAK) kilitoa wito kwa serikali kuitisha mkutano wa kitaifa wa dharura kujadili changamoto ya ufadhili wa shule. Katibu wa ESAK, Ndung’u Wangenye, alionya kuwa iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa, elimu ya mamilioni ya watoto iko hatarini.Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu wa Shule za Sekondari (KUPPET), Akelo Misori, alikashifu serikali kwa kushindwa kushughulikia pengo la fedha katika elimu ya sekondari na kuonya dhidi ya kuhamisha mzigo huo kwa wazazi waliolemewa tayari. Hata hivyo, Waziri wa Elimu Julius Ogamba alipinga madai kuwa serikali imefuta sera ya elimu bila malipo, akisema kuwa wamepunguza kiasi cha mgao kutokana na changamoto za bajeti pekee.
MWANZA: Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP) kwa kushirikiana na Taasisi ya Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET) ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam kinatarajiwa kufanya kongamano la kitaaluma kesho mkoani Mwanza, linalolenga kufanikisha Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Mwaka 2050. Mkuu wa Idara ya…
NAIROBI : SERIKALI ya Kenya imetangaza kushindwa kumudu gharama za kufadhili elimu ya bure kwa shule za msingi na sekondari, hatua itakayoathiri maelfu ya wanafunzi na kuongeza mzigo kwa wazazi.
MAHAKAMA ya Leba jijini Nairobi imeidhinisha kufutwa kazi kwa mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Murang’a kwa kuhusika katika uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi, ikisisitiza kuwa tabia kama hiyo ni ukiukaji mkubwa wa maadili ya kazi. Mahakama ilibaini kuwa mhadhiri huyo, Bw NKB, alikuwa na uhusiano usiofaa na mwanafunzi aliyekuwa akisomea Shahada ya Biashara (Bachelor of Commerce), huku yeye akiwa mhadhiri katika Idara ya Uhandisi wa Umeme na Elektroniki. Jaji Mathews Nduma aliamua kuwa tabia hiyo ilikiuka kanuni za maadili za Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Murang’a, na kufutwa kazi kwa NKB mwezi Machi 2020 kulifanywa kwa misingi halali. Mahakama ilitupilia mbali madai ya mhadhiri huyo ya kutaka arejeshwe kazini na dai lake la fidia ya Sh22 milioni kwa hasara ya ajira, kuharibiwa kwa sifa yake na madai ya ukiukaji wa haki zake za ajira. "Mahakama imeridhika kuwa ushahidi uliowasilishwa na shahidi wa mshtakiwa wa kwanza kwa mizani ya uwezekano, unaonyesha kuwa mlalamishi alikuwa na uhusiano wa kingono na mwanafunzi katika chuo kikuu alikokuwa akifundisha. Alimletea usumbufu, mateso ya kihisia na kiakili, hali iliyohitaji ushauri nasaha ambapo tabia hiyo isiyofaa ilifichuliwa," alisema Jaji Nduma. Mahakama ilieleza kuwa NKB alipitia mchakato wa kinidhamu na alipewa nafasi ya kujitetea lakini alishindwa kujinasua dhidi ya tuhuma za utovu wa nidhamu. Mwanafunzi huyo alitoa ushahidi kuwa alijiunga na chuo hicho mwezi Agosti 2018 kupitia mpango wa kazi na masomo. Alikutana na NKB mwezi Agosti 2019 karibu na maabara ya umeme ambapo alikuwa akifanya kazi. Alitambulishwa kwake na msimamizi wake. Walibadilishana nambari za simu na kuanza kuzungumza. Mwanafunzi huyo alisema kuwa NKB alimrai kwa maneno matamu na kwa muda akaanza kumwamini. Alisema kuwa alitembelea nyumba ya NKB mjini Murang’a mara tatu kati ya Agosti na Septemba na kulala huko. Asubuhi, angepewa Sh100 kama nauli ya kurudi chuoni. Baadaye, alisema, Bw NKB alimtambulisha kwa mpenzi wake lakini akaendelea kumsumbua kwa kumfuatilia kila mara hadi ikawa vigumu kwake kustahimili. Aliripoti suala hilo katika ofisi ya ushauri nasaha ya chuo ambapo alihudumiwa na Bi Ronoh Goretti. Mahakama iliambiwa kuwa Bi Goretti alimshauri aripoti suala hilo kwa Naibu Chansela, baada ya hapo mwanafunzi aliandika barua rasmi kuelezea masaibu yake. Akipinga kufutwa kazi kwake, Bw NKB alidai kuwa hakuruhusiwa kumhoji mwanafunzi huyo ili kuthibitisha ukweli wa madai yake. Alisema kuwa mwanafunzi huyo hakuwahi kuwasilisha malalamishi rasmi wala kiapo, na hakuna ripoti yoyote ya polisi iliyowasilishwa kuhusu madai hayo. Katika utetezi wake, alidai alikuwa tu akimsaidia mwanafunzi huyo ikiwemo kumlipia dawa na kumtumia pesa mama yake. Alisema mchakato wa kinidhamu ulikiuka haki asili na haki za kikatiba. Hata hivyo, Afisa Mkuu wa Usalama wa Chuo Kikuu cha Murang’a, Bw Felix Kimotho, alitoa ushahidi kuwa kesi hiyo iliripotiwa kwa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) Murang’a, Bw NKB aliitwa mwezi Februari 2021 kuandika taarifa baada ya mwanafunzi kudai kubakwa. Hakuna mashtaka ya jinai yaliyofunguliwa dhidi yake. Katika uamuzi wake, mahakama ilibaini kuwa kufutwa kazi kwa Bw NKB kulifanyika kwa utaratibu unaofaa. Alikuwa na nafasi ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo, alisikilizwa wakati wa mchakato, na rufaa yake ilikataliwa kwa kukosa mashiko. "Mshtakiwa (Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Murang’a) kwa kutumia ushahidi ulio thabiti, amethibitisha kwa mizani ya uwezekano kuwa mlalamishi alikuwa na uhusiano usiofaa na mwanafunzi, kinyume na kanuni za maadili za taasisi hiyo," alihitimisha Jaji Nduma.
BUKOBA: WAZAZI na walezi katika Halmashauri ya Bukoba wametakiwa kuhakikisha wanatanguliza eliku kwa watoto wao kuliko kufikiria kutoa vitu vya gharama kama simu aina ya Iphone ili kuwafurahisha. Wito huo umetolewa leo Julai 23, 2015 na Ofisa Elimu ya Msingi wa Halmashauri ya Bukoba, Julius Shulla wakati akizungumza na wazazi kwenye mahafari ya 14 ya…
DAR ES SALAAM: UFARANSA kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili ( MUHAS ) wanaendelea kuboresha uhusiano wao ambapo sasa wanafunzi wa chuoni hapo watapata nafasi kwenda nchini humo kujifunza masuala mbalimbali ya afya. Sambamba na hilo, walimu na wanafunzi kutoka Ufaransa pia watapata nafasi ya kuja Muhas kufundisha na kujifunza…
MOROGORO: CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimeanzisha mitaala mipya sita ya Ualimu wa Amali inayolenga kuinua ubora wa elimu na kukidhi mahitaji ya walimu kufuatia mabadiliko makubwa ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita. Mitaala mipya hiyo inalenga kuwaandaa walimu wa…
GEITA; KAMPUNI ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) imejitosa kudhamini programu ya mashindano ya michezo kwa shule za sekondari, Halmashauri ya Manispaa ya Geita ili kukabiliana na tatizo la utoro. Hatua hiyo imekuja kufuatia Manispaa ya Geita kuripoti changamoto ya mdondoko wa wanafunzi 2,547 wa shule za sekondari kipindi cha mwaka 2021 hadi 2023…
MAANDALIZI ya mashindano ya kitaifa ya Shirikisho la Michezo ya Shule za Upili Nchini Kenya (KSSSA) yamepamba moto mjini Kakamega kipenga cha mwanzo kikitarajiwa kupulizwa Jumamosi. Viwanja vimekaguliwa huku timu zikiendelea na mazoezi makali tayari kwa mashindano hayo ya wiki nzima yatakayoanza Julai 26 hadi Agosti 2. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa KSSSA Kanda ya Magharibi, Quinto Musungu, viwanja vyote vitakavyotumika tayari vimekaguliwa na viko katika hali nzuri. “Tunahakikisha kila kitu kiko sawa kulingana na mipango yetu ya kuandaa mashindano. Timu zote zinatarajiwa kuwasili kufikia Julai 26 kabla ya uzinduzi rasmi kesho yake katika Shule ya Upili ya Kakamega,” alisema Musungu mnamo Jumatatu. Kauli yake inajiri baada ya mwanafunzi wa kidato cha tatu kuaga dunia ghafla wakati wa mashindano ya soka baina ya madarasa katika shule hiyo ya Kakamega High. Polisi wanafanya uchunguzi kubaini kiini cha kifo hicho cha ghafla. [caption id="attachment_175327" align="alignnone" width="2560"] Maryann Jepkemoi (kushoto) wa Itigo Girls ya Nandi na Merab Keya wa Nasokol Girls ya Pokot Magharibi wakati wa Michezo ya Shule za Upili Kanda ya Bonde la Ufa, jijini Eldoret mnamo Julai 11, 2025. PICHA | JARED NYATAYA[/caption] Mitanange ya shule za upili wikendi hii itahusisha mechi kali kutoka kwa timu bora katika soka, voliboli, mpira wa pete (netiboli), mpira wa vikapu kwa wachezaji watatu kila upande (3x3), raga ya wachezaji saba kila upande, na tenisi. Mabingwa watetezi wa kitaifa Butere Girls na Madira Girls watatetea heshima ya Kanda ya Magharibi kwenye soka ya wasichana, huku timu maarufu ya The Scorpions kutoka Musingu Boys ikiongoza upande wa wavulana. Washindani wapya Bishop Sulumeti Girls kutoka Lugari watawakilisha kanda kwenye voliboli ya wasichana, nao Malava Boys waliowahi kushinda taji la kitaifa watalenga kurejesha ufalme wa voliboli nyumbani. Katika michezo mingine, Bukokholo itapeperusha bendera ya kanda kwenye netiboli, huku Sirakalu Secondary na Tigoi Girls zikishiriki vikapu vya wasichana. Sigalame Boys na St Peter’s Mumias zitawania taji la wavulana kwenye mpira wa vikapu. [caption id="attachment_175331" align="alignnone" width="2560"] Lydia Furaha (kushoto) wa St Joseph’s Girls kutoka Trans Nzoia achomoka na mpira akiandamwa na Mitchel Mmboga (kulia) wa Itigo Girls kutoka Nandi mechi ya raga ya 7s wakati wa Michezo ya Shule za Upili Kanda ya Bonde la Ufa, jijini Eldoret mnamo Julai 11, 2025. PICHA | JARED NYATAYA[/caption] St Peter’s Mumias, Bungoma High, Musingu Boys na Koyonzo Boys watawakilisha kanda hiyo ya Magharibi katika raga, huku mabingwa watetezi kitengo cha wasichana St Maurice Mwira pamoja na Eregi Girls, Madira Girls na Kimobo Girls pia wakishiriki. Shule limbukeni Agai Secondary School itaongoza Kanda ya Nyanza kuwania taji la soka ya wavulana huku Kobala Mixed wakiwakilisha wasichana. St Mary’s Yala na Sigoti Complex Girls zitawania taji la raga, huku mabingwa wa zamani wa netiboli kitaifa Oyugi Ogango Girls High wakiendea taji hilo tena. Gogo Secondary watakuwa wakisaka ubingwa wa voliboli ya wavulana, huku Nyakongo Secondary wakivaana katika voliboli ya wasichana. St Joseph’s Boys High wataongoza mavizio ya soka ya wavulana kutoka Bonde la Ufa, huku Nasokol Girls kutoka Pokot Magharibi wakipigania taji la wasichana. [caption id="attachment_175332" align="alignnone" width="2113"] Dennis Mukhwana (kulia) wa Friends Bwake Boys ya Trans Nzoia akiandamwa na Lawi Kipkurui wa Kapsabet Boys ya Nandi mechi yao ya raga kwenye Michezo ya Shule za Upili Kanda ya Bonde la Ufa, jijini Eldoret mnamo Julai 09, 2025. PICHA | JARED NYATAYA[/caption] St Joseph’s Girls Kitale watashiriki netiboli huku Bwake Boys, St Joseph’s Girls na Itigo Girls zikiwakilisha Bonde la Ufa katika raga. Mabingwa wa zamani wa kitaifa na Afrika Mashariki wa voliboli Cheptil Boys wataongoza mawindo ya Bunde la Ufa kwa upande wa wavulana, nao Kesogon Secondary watabeba matumaini katika kitengo cha wasichana. Kwa mujibu wa Musungu, raga itachezwa katika uwanja wa Kakamega Bull Ring, huku soka ikifanyika katika viwanja vitatu shuleni humo pamoja na Mukumu Boys. Voliboli, netiboli, tenisi ya mezani, na badminton zitachezwa katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Masinde Muliro (MMUST), huku badminton ikifanyika pia katika shule ya upili ya Kakamega High. Kaunti ya Kakamega pia itakuwa mwenyeji wa makala ya 22 ya Michezo ya Shule za Upili za Afrika Mashariki (FEASSSA) mnamo Agosti 14-25. -Imetafsiriwa na Geoffrey Anene
ASILIMIA 30 ya wanafunzi wa Gredi ya Sita wanaosomea katika shule za umma nchini hawawezi kusoma kitabu cha Kiingereza cha kiwango cha Gredi 3, kulingana na ripoti moja iliyotolewa juzi. Kulingana na ripoti hiyo ya utafiti kuhusu Hali ya Elimu nchini Kenya iliyotolewa na Wakfu wa Zizi Afrique na Shirika la Usawa Agenda, ni asilimia 40 pekee ya wanafunzi wa Gredi 4 wanaoweza kusoma. Aidha, ripoti hiyo inaeleza kuwa wanafunzi katika maeneo ya mashambani na maeneo kame ndio waathiriwa wakubwa. Kwa mfano, wanafunzi wawili kati ya wanafunzi 10 wa Gredi 4 Kaskazini Mashariki mwa Kenya ndio wanaweza kusoma na kuelewa hadithi ya Kiingereza ya kiwango cha Gredi 3, tofauti na wenzao wanaosomea shule za mijini. “Viwango vya masomo viko chini zaidi. Ni wanafunzi wanne pekee wa Gredi ya 4 wanaweza kusoma na kuelewa hadithi ya Kiingereza ya kiwango cha Gredi 3; wanafunzi 3 kati ya 10 wa Gredi 6 hawangeweza kusoma na kuelewa hadhi ya Kiingereza ya kiwango cha Gredi 3,” ripoti inasema. Inaongeza, “Wanafunzi katika maeneo kame na ya mashambani ndio waathiriwa zaidi kuliko wenzao wanaosomea katika maeneo ya mijini. Katika eneo la Kaskazini Mashariki ni wanafunzi wawili pekee wa Gredi 4 wanaweza kusoma na kuelewa hadithi ya Kiingereza ya kiwango cha Gredi 3." Hii ina maana kuwa maelfu ya wanafunzi wanapanda ngazi katika mfumo wa elimu bila kupata uwezo hitajika wa kusoma kwa manufaa yao katika elimu ya juu na wakiwa watu wazima. Ripoti hiyo inahusisha hali ya wanafunzi kutoweza kusoma vizuri na udhaifu katika masomo ya chekechea.Kulingana na ripoti hiyo, idadi kubwa ya wanafunzi wenye matatizo ya kusoma, ni wale waliojiunga na shule za msingi kabla ya kusomea shule za chekechea. Ripoti hiyo inasema kuwa watoto waliosomea katika shule za chekechea wanaweza kufanya vizuri katika somo la Hisabati na somo la Kiingereza ikilinganishwa na wenzao ambao hawahudhuri shule za chekechea. “Watoto waliohudhuria shule za chekechea kabla ya kujiunga na shule za msingi wako na uwezekano wa asilimia tisa wa kufanya vizuri katika hisabati na asilimia 18 ya wanafunzi katika somo la Kiingereza kuliko wale ambao hawakuhudhuria shule za chekechea,” ripoti hiyo inaeleza. Licha ya hayo, idadi ya watoto wanaopata nafasi ya masomo ya shule za chekechea ni ndogo katika maeneo mengine ya nchi. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa kitaifa, asilimia 7.4 ya watoto waliosajiliwa katika Gredi 1 hawakuwa wamepata nafasi ya kuhudhuria shule za chekechea. Katika maeneo ya mashambani asilimia 8.4 ya wanafunzi waliojiunga na Gredi 1 hawakupata nafasi ya kuhudhuria shule za chekechea. Na katika maeneo ya mijini, ni asilimia 6.2 ya wanafunzi wa Gredi 1 hawakuhudhuria shule za chekechea.
SHULE tano za sekondari katika kaunti za Bomet na Kericho zimefungwa ndani ya wiki moja iliyopita baada ya wanafunzi kuzua fujo. Miongoni mwa malalamishi yao ni uhuru wao kudhibitiwa, vyakula kupikwa vibaya na madai ya baadhi yao kudhulumiwa kingono na walimu. Katika Kaunti ya Kericho, shule zilizoathirika ni pamoja na Shule ya Upili ya Wasichana ya Moi Tea, Shule ya Upili ya Wavulana ya Litein, Shule ya Upili ya Wasichana ya Kipsigis na Shule ya Wavulana ya Kiptewit. Katika Kaunti ya Bomet, Shule ya Upili ya Wasichana ya Kaplong ilifungwa Ijumaa wiki jana baada ya kuharibu madirisha ya madarasa na gari la shule. Fujo hizo zilichochewa na madai kuwa mwalimu mmoja alimpachika mimba mwanafunzi mmoja. Kufuatia fujo hizo, wanafunzi walishauriwa kwenda nyumbani baada ya kuharibu mali ya shule. Thamani ya hasara haijabainishwa. “Uchunguzi kuhusu kisa hicho unaendeshwa na Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu,” akasema Mkurugenzi wa Tume ya Huduma kwa Walimu (TSC) kaunti ya Bomet, Dkt William Yator. Dkt Yator alisema tume hiyo inachukulia kwa uzito tuhuma zinazohusiana na madai ya mwalimu mmoja kuhusiana kimapenzi na wanafunzi wa kike. Alisema ikiwa mshukiwa atapatikana nahatia, hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake. Wanafunzi wa Shule ya Upili ya Wasichana ya Kaplong walidai kuwa kulikuwa na njama ya kuzima kisa hicho kupitia uhamisho wa mwalimu mshukiwa hadi eneo lingine. Baadhi ya wanafunzi walidai visa kama hivyo vimewahi kutokea katika shule hiyo miaka ya nyuma na hatua haikuchukuliwa dhidi ya walimu washukiwa. Hatimaye, wanafunzi waliodhulumiwa waliteseka kivyao baadhi yao wakilazimika kukatiza masomo yao.
SHULE tano za sekondari katika kaunti za Bomet na Kericho zimefungwa ndani ya wiki moja iliyopita baada ya wanafunzi kuzua fujo. Miongoni mwa sababu zilizochangia wanafunzi kuzua fujo ni pamoja na uhuru wao kudhibitiwa, vyakula vilipikwa vibaya na madai ya baadhi yao kudhulumiwa kingono na walimu. Katika kaunti ya Kericho, shule zilizoathirika ni pamoja na Shule ya Upili ya Wasichana ya Moi Tea, Shule ya Upili ya Wavulana ya Litein, Shule ya Upili ya Wasichana ya Kipsigis na Shule ya Wavulana ya Kiptewit. Katika ilifungwa Ijumaa wiki jana baada ya kuharibu madirisha ya madarasa na gari la shule. Fujo hizo zilichochewa na madai kuwa mwalimu mmoja alimpachika mimba mwanafunzi mmoja. Kufuatia fujo hizo, wanafunzi walishauri kwenda nyumbani baada ya kuharibu mali ya shule. Thamani ya hasara haijabainishwa. “Uchunguzi kuhusu kisa hicho unaendeshwa na Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu,” akasema Mkurugenzi wa Tume ya Huduma kwa Walimu (TSC) kaunti ya Bomet Dkt William Yator. Dkt Yator alisema tume hiyo inachukulia kwa uzito tuhuma zinazohusiana na madai ya mwalimu mmoja alihusiana kimapenzi na wanafunzi wa kike. Alisema ikiwa mshukiwa atapatikana na hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake. Wanafunzi wa Shule ya Upili ya Wasichana ya Kaplong walidai kuwa kulikuwa na njama ya kuzima kisa hicho kupitia uhamisho wa mwalimu mshukiwa hadi eneo lingine. Baadhi ya wanafunzi walidai visa kama hivyo vimewahi kutokea katika shule hiyo miaka ya nyuma na hatua haikuchukuliwa dhidi ya walimu washukiwa. Hatimaye, wanafunzi waliodhulumiwa waliteseka kivyao baadhi yao wakilazimika kukatiza masomo yao.
DAR ES SALAAM: SHIRIKA la Utangazaji Tanzania (TBC), Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara ya Elimu wameandaa shindano la uandishi wa insha kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kumbukizi ya miaka 26 tangu kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Akizungumza na waandishi wa habari…
WATU wengi wanapofikiria kuhusu ustawi wa kifedha, mawazo yao huenda moja kwa moja kwenye kipato: Je, ninapata kipato cha kutosha? Je, ninaweka akiba ya kutosha? Lakini ustawi wa kifedha ni zaidi ya hayo. Ni hali ya kuwa na usalama wa kifedha, uwezo wa kukabiliana na mambo yasiyotarajiwa, na maandalizi ya maisha ya baadaye. Kuna misingi…
TAKRIBAN shule 3,100 za sekondari za umma zenye idadi ndogo ya wanafunzi huenda zikaunganishwa, serikali inapochunguza njia za kutumia rasilmali kwa ufanisi zaidi katikati ya changamoto za kifedha zinazoongezeka, Taifa Leo imefahamu. Katibu wa Elimu ya Msingi, Dkt Julius Bitok, alidokeza kuhusu mpango huo katika hafla moja, akisema kuwa hatua hiyo inachochewa na matokeo ya zoezi la ugawaji wa zaidi ya wanafunzi 1.2 milioni wa Darasa la 9 wanaoendelea na masomo ya sekondari pevu chini ya mtaala mpya wa Umilisi na Utendaji (CBE). Ilibainika kuwa zaidi ya nusu ya shule 9,750 za sekondari nchini hazikuchaguliwa na wanafunzi wanaojiunga na Gredi ya 10 chini ya mtaala mpya. Uchambuzi wa kina unaonyesha kuwa zaidi ya shule 3,000 za sekondari zina wanafunzi wasiozidi 150, hali inayoonyesha kuwa hazina rasilmali za kutosha kujiendesha. “Tutawaita wadau wote kuanzisha mjadala wa kitaifa kuhusu uendelevu wa baadhi ya shule zetu, ili tuweze kuhakikisha rasilmali zinatumiwa kwa ufanisi,” alisema Dkt Bitok. Katibu huyo alisema ingawa sababu za kutokuchaguliwa kwa baadhi ya shule hazijafafanuliwa kwa kina, huenda miundombinu duni, matokeo ya kitaaluma, maeneo zilipo shule, na hadhi ya shule zilichangia maamuzi ya wanafunzi na wazazi. Kwa shule ambazo hazikuchaguliwa, maana yake ni kwamba hazitapokea fedha za ruzuku kutoka kwa serikali. Kila mwanafunzi katika shule ya sekondari anastahili kupokea Sh22,244 kila mwaka kama ada ya masomo, ambapo Wizara ya Elimu inatakiwa kupeleka fedha hizo kwa awamu tatu kwa uwiano wa asilimia 50:30:20. Hata hivyo, uwiano huu haujazingatiwa mwaka huu, na kusababisha upungufu wa Sh18 bilioni hali inayotesa kifedha shule nyingi huku walimu wakuu wakisema kuwa imeathiri hali ya masomo. Kati ya deni hilo, Sh7.5 bilioni ni kwa muhula wa kwanza na Sh10.5 bilioni ni kwa muhula wa pili, hali ambayo imesababisha shughuli nyingi kukwama na madeni kuongezeka katika shule mbalimbali. Chama cha Wakuu wa Shule za Sekondari (KESSHA)wiki iliyopita kilionya kuwa shule za sekondari za umma, hasa za kutwa, ziko hatarini kufungwa kutokana na kucheleweshwa kwa fedha kutoka Wizara ya Fedha. Dkt Bitok alibainisha kuwa katika mikutano ya mashauriano na wakuu wa shule za sekondari katika kaunti ya Elgeyo Marakwet, ilidhihirika kuwa kuna changamoto zinazopaswa kujadiliwa kitaifa. “Tulipowauliza wakuu wa shule sababu ya kutokuchaguliwa kwa baadhi ya shule, tuligundua kuwa zaidi ya shule 3,000 kati ya 9,750 zina wanafunzi chini ya 150 – yaani ni shule ndogo sana,” alisema. Ufichuzi huu unazua maswali muhimu kuhusu uendelevu na ufanisi wa kuendesha maelfu ya shule ndogo wakati huu uchumi umedorora na ucheleweshaji wa fedha za serikali.
KAMA wewe ni mzazi wa tineja, tayari unafahamu kuwa mwanao wa kiume au wa kike hutumia saa nyingi kila siku akiwa amezingirwa na vifaa vya kiteknolojia. Unachoweza kuwa hukifahamu ni kwamba michezo ya video inayochezwa kwa muda mrefu na mazungumzo ya mara kwa mara mtandaoni vinaweza kuathiri uwezo wake kupata usingizi mzuri usiku. Kwa mujibu wa watafiti kutoka Kitengo cha Afya ya Vijana na Taasisi ya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC), vijana wanaotumia saa mbili au zaidi kwa siku kwa kompyuta au kucheza michezo ya video kwa madhumuni yasiyo ya masomo wana uwezekano mdogo wa kupata usingizi wa kutosha ikilinganishwa na wenzao wasiopendelea teknolojia sana. Aidha, wanafunzi wa shule ya upili wanaofanya mazoezi ya mwili kila siku wana nafasi kubwa ya kupata usingizi mzuri wa usiku kuliko wale wasiofanya mazoezi mara kwa mara. Matokeo haya yalichapishwa katika jarida la American Journal of Preventive Medicine, baada ya uchunguzi wa kitaifa uliowahusisha zaidi ya vijana 15,000.Wataalamu wanashauri kuwa mwanafunzi wa shule ya upili anahitaji kati ya saa 8 hadi 9 na nusu za usingizi kila usiku. Hata hivyo, vijana wengi hulala saa 5 hadi 6 au hata chini ya hapo. Katika kipindi cha utineja, melatonini—homoni inayozalishwa katika ubongo—huzalishwa kwa kuchelewa zaidi usiku ikilinganishwa na wakati wa utoto. Hali hii huathiri mzunguko wa jinsi mwili unavyojiendesha na kuchelewesha muda wa kijana kuhisi usingizi.Usingizi hutoa manufaa muhimu kwa watu wa rika zote. Kwa matineja, ukosefu wa usingizi unaweza kusababisha matatizo ya kusoma shuleni, kudhoofika kwa kinga ya mwili, hasira zisizoeleweka, na hata msongo wa mawazo. Huwezi kumlazimisha kijana wako ahisi usingizi kabla hajawa tayari, lakini unaweza kuongeza nafasi yake kupata usingizi mzuri kuweka mipaka ya matumizi ya vifaa vya dijitali. “ Ingawa matineja na teknolojia ni kama ndugu, ni muhimu kuweka mipaka ya busara inayofaa familia yako. Zungumza na mwanao kuhusu mipaka hiyo na eleza kwa nini ni muhimu kwa afya na ustawi wake. Hakuna haja ya kuacha teknolojia kabisa—tafuta uwiano bora kati ya muda wa kuitumia na shughuli nyingine,” asema, Dkt Debbie Glasser, mtaalam na mtafiti wa malezi dijitali. Vijana wengi, asema, wana kifaa kimoja au zaidi cha kielektroniki katika chumba chao cha kulala. Wengine wana hadi vinne au zaidi. Vifaa hivi vinaweza kuvuruga usingizi. Hamisha baadhi ya vifaa hivyo hadi chumba kingine ili chumba cha kulala kibaki kuwa mahali pa usingizi, si matumizi ya teknolojia.
Walimu kote nchini wanatarajiwa kupokea nyongeza ya mishahara kati ya asilimia 5 hadi 29.6 kufikia mwisho wa mwezi huu, kufuatia kutiwa saini kwa makubaliano mapya kati ya Tume ya Huduma kwa Walimu (TSC) na vyama vitatu vikuu vya walimu — Chama cha Walimu wa Shule za Sekondari (KUPPET), Chama cha Kitaifa cha Walimu (KNUT), na Chama cha Walimu wa Mahitaji Maalum (KUSNET). Makubaliano hayo, yatakayotumika kwa muda wa miaka minne, yatagharimu serikali jumla ya Sh33.8 bilioni, ambazo zitagawanywa kwa usawa kila mwaka, huku walimu wakipokea nyongeza kila mwaka. Kwa mujibu wa viongozi wa vyama vya walimu, hatua hiyo ni ushindi mkubwa unaorejesha heshima ya taaluma ya ualimu na kuondoa tofauti za muda mrefu katika viwango vya malipo. Makubaliano hayo yalitiwa saini Ijumaa katika Taasisi ya Elimu ya Mahitaji Maalum (KISE) mtaa wa Kasarani, Nairobi, baada ya mazungumzo yaliyochukua muda mrefu hadi usiku. Mabadiliko hayo si tu ya kifedha, bali pia yanahusisha sera mpya kama vile mchakato wa haraka wa pensheni, na ulinzi kwa walimu wa kike wanaonyonyesha.Marekebisho ya mishahara yataanza kutekelezwa Julai 1, 2025, huku mishahara ya mwezi huo ikitarajiwa kuakisi viwango vipya mwishoni mwa mwezi. Kwa upande wa KNUT, chama kinachowakilisha hasa walimu wa shule za msingi, nyongeza ya mishahara itakuwa kati ya asilimia 12 hadi 29.5, huku walimu wa ngazi za chini wakipata ongezeko kubwa zaidi. Katibu Mkuu wa KNUT, Bw Collins Oyuu, alisema kuwa makubaliano hayo ni kati ya nyongeza muhimu zaidi kuwahi kupatikana katika miaka ya hivi karibuni. “Walimu wa ngazi za chini sasa wana kila sababu ya kutabasamu. Wamepewa kipaumbele. Na suala tata zaidi — mwongozo wa maendeleo ya kazi — sasa utapitiwa upya,” alisema Bw Oyuu. Aidha, alisema kuwa maeneo yenye mazingira magumu yaliyotangazwa awali hayataathiriwa, na pensheni kwa walimu wanaostaafu itashughulikiwa kwa haraka zaidi. Alisisitiza haja ya kuwepo kwa sheria mpya kupitia Mswada wa Marekebisho ya Tume ya Huduma kwa Walimu, ili kuimarisha mazungumzo ya baadaye.
Mahakama ya Nairobi imeamuru bilionea mfanyabiashara Peter Munga afurushwe kutoka ardhi ya ekari 75 inayomilikiwa na kampuni ya Del Monte Kenya Limited, iliyoko Kaunti ya Murang’a, kwa kukiuka mkataba wa kuikodisha. Bw Munga alipata pigo jingine baada ya Jaji wa Mahakama ya Mazingira na Ardhi, Anne Omollo, kuagiza Shule ya Kimataifa ya Pioneer – taasisi ya kifahari ya elimu inayohusishwa naye – kuondolewa ardhi hiyo. Jaji Omollo alielekeza kuwa shule hiyo ihamishwe kufikia mwisho wa mwaka huu. Aidha, shule hiyo imepewa hadi Desemba 20, 2025, kukamilisha shughuli zake za masomo bila kutatizwa, kabla ya kuondoka kabisa katika ardhi hiyo. “Ninazingatia maslahi bora ya mtoto kwa kuruhusu kalenda ya masomo ya mwaka huu ikamilike kabla ya masomo ya wanafunzi kusitishwa,” alisema Jaji Omollo. Hata hivyo, alielekeza kuwa shule hiyo iendelee kulipa kodi ya kila mwezi kwa Del Monte hadi itakapohama. Del Monte ililaumu kampuni ya Goshen Gardens Limited kwa kuhamisha mali na mkataba wa kukodisha ardhi hiyo kwa Shule ya Kimataifa ya Pioneer bila kuijulisha, na baadaye taasisi hiyo ikashindwa kulipa kodi, hali iliyosababisha mmiliki wa ardhi kuvunja mkataba. Kabla ya shule hiyo kuingia, Del Monte ilikuwa tayari imetoa notisi ya kuvunja mkataba wake na Goshen Gardens kwa sababu ya kutolipa kodi. Del Monte iliwasilisha kesi kortini mnamo 2016, ikitaka miongoni mwa mambo mengine, shule hiyo ifurushwe kutoka ardhi hiyo na kuondoa majengo yote pamoja na mali nyingine. Mahakama pia iliagiza Kamanda wa Kituo cha Polisi cha Ngati, mjini Murang’a, kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa. Kwa mujibu wa Del Monte, Goshen Gardens ilikodi ekari 75 za ardhi hiyo kwa miaka minane kuanzia Septemba 3, 2013, kwa kodi ya kila mwezi ya Sh550,000. Hata hivyo, kufikia Februari 2015, kampuni hiyo ilikuwa imeshindwa kulipa kodi, na ikapewa notisi ya kuhama. Baada ya kuendelea kukaidi malipo, Del Monte ilisitisha mkataba na kuamuru kampuni hiyo kuondoka. Lakini Goshen Gardens ilishtaki, ikidai Del Monte ilikiuka makubaliano ya mkataba kwa kupunguza ukubwa wa ardhi kutoka ekari 100 hadi 75, na pia kuingia kwenye ardhi hiyo bila idhini, hali ambayo ilisababisha hofu ya usalama ikiwemo kung’olewa kwa ua shuleni. Mahakama ilielezwa kuwa Februari 2, 2015, watu wasiojulikana walivamia majengo ya shule hiyo na kuiba mali ya thamani ya Sh1.6 milioni. Kesi hiyo baadaye ilielekezwa kwa upatanisho, ambapo Goshen Gardens iliruhusiwa kuendelea kutumia ardhi hiyo kwa muda, ikisubiri uamuzi wa mzozo huo.
MOROGORO; WANAFUNZI wawili wa kidato cha nne wa Shule ya Morogoro Sekondari, Lusajo Mwang’onda (18) na Ghalib Omary (18) wakazi wa Kata ya Kihonda Maghorofani , Manispaa ya Morogoro wamefariki dunia kutokana na ajali ya bodaboda iliyowabeba kwenda shule kuparamia lori barabara kuu ya Morogoro- Dodoma. Dereva wa bodaboda hiyo, Baraka Sijawaza Sajio (22) pia…
DAR ES SALAAM; RAIS mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk Jakaya Kikwete amesema Tanzania imepiga hatua kubwa kuhakikisha watoto wanapata elimu na kusaidia kupunguza idadi ya watoto wa mtaani. Akizungumza Julai 14, katika shule ya Kibasala jijini Dar es Salaam kwenye ziara iliyohusisha Shirika la GPE (Global Partnership Education) na Taasisi ya Malala Fund inayojihusisha…
WANAFUNZI watatu Alhamisi, Julai 10, 2025 walifaruju na wengine kupata majeraha baada ya choo kuanguka katika Shule ya Msingi ya Queen of Angels, Kaptebee, Kaunti ya Uasin Gishu. Ilibainika wanafunzi hao walikwama wakati ukuta wa choo cha shule hiyo kiliporomoka kutokana na mvua kubwa ambayo imekuwa ikinyesha eneo hilo. [caption id="attachment_174788" align="alignnone" width="1600"] Afisa wa upelelezi wa jinai akirekodi matukio katika shule ya Queen of Angels Mission School mjini Turbo baada ya watoto watatu kufariki kwa kuporomokewa na choo. Picha|Jared Nyataya[/caption] Kamishina wa Polisi wa Uasin Gishu Dkt Edison Nyale alisema kuwa walikuwa wakitumia choo hicho wakati kiliporomoka. Sakafu ya choo hicho iliporomoka na watoto hao wakakwama ndani,” akasema Dkt Nyale. Watoto wanne waliondolewa ndani ya choo hicho huku watatu wakifa wakipelekwa katika Hospitali ya Kaunti ndogo ya Turbo. Juhudi za uokoaji zilizoshirikisha maafisa kutoka Huduma ya Kitaifa kwa Vijana (NYS), wasamaria wema na idara ya zimamoto kutoka Kaunti ya Uasin Gishu, zilikuwa zikiendelea. Watoto walionusurika walipelekwa hadi Hospitali ya Kaunti ya Turbo huku uchunguzi ukiendelea.
DAR ES SALAAM: MSAFARA wa wataalamu kutoka Jiji la Chengdu Mkoa wa Schuan nchini China umetembelea Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kuanzisha uhusiano wa kibiashara, elimu, kilimo na masuala mengine. Ugeni huo umeongozwa na Naibu Mkurugenzi wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Chengdu na Naibu Meya, Wang Pingjiang na kupokelewa na Mkuu…
ARUSHA: MKURUGENZI wa Jiji la Arusha, John Kayombo amezitaka klabu na vyama vya michezo kuwasilisha mipango kazi yao ili viweze kusaidika kwa maendeleo ya michezo. Akizungumza katika bonanza la michezo la Sabasaba lililofanyika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Baraa iliyopo Moshono jijini hapa, Ofisa Michezo na Utamaduni jiji la Arusha, Benson Maneno ambaye alimuwakilisha…
LUGHA ni chombo kikuu cha binadamu cha kueleza maana – kwa maneno au bila maneno. Inatumika kwa malengo mengi: kujenga madaraja, kuunganisha jamii, kuhimiza amani, kueneza furaha na kukuza upendo. Hata hivyo, lugha pia inaweza kugawanya, kuchochea chuki na hata kuhalalisha vurugu ikiwa itatumiwa vibaya. Kwa kuwa ni chombo chenye nguvu, matumizi ya lugha yanahitaji uangalifu na uwajibikaji mkubwa. Kiswahili, kama lugha ya mawasiliano ya pamoja, kina uwezo wa kipekee wa kuwaleta watu pamoja kutoka makundi tofauti ya kikabila, kidini, kiumri na kijamii. Ni tanuri linaloyeyusha tamaduni mbalimbali na kutumika kama nyenzo ya kuleta usawa, kwa kuunganisha jamii licha ya tofauti zao. Tangu kizaliwe Afrika Mashariki, Kiswahili kimevuka mipaka ya kieneo na kufika mataifa ya mbali kama Japan, Amerika na Finland. Leo hii, kinazungumzwa na watu zaidi ya milioni 250 duniani kote na kinawakilisha ishara ya mshikamano na utambulisho wa kina. Katika takriban nchi 15 za Afrika, Kiswahili ni lugha kuu ya biashara na mawasiliano. Umuhimu wake wa kimataifa ulithibitishwa na UNESCO iliyotangaza tarehe 7 Julai kuwa Siku ya Kiswahili Duniani (SIKIDU), ikitambua Kiswahili kama nyenzo muhimu ya kukuza mazungumzo ya kitamaduni na utofauti. Mwaka huu, chini ya kauli mbiu “Kiswahili kwa Umoja, Amani, na Ustawi,” Chuo Kikuu cha Eldoret kitaadhimisha leo nafasi ya Kiswahili katika kuendeleza amani, mshikamano na mazungumzo ya kitamaduni. Tukio hilo linatufundisha kuwa Kiswahili si lugha tu, bali ni chombo cha amani, maendeleo na ustawi endelevu. Chuo Kikuu cha Eldoret kitaungana leo na jumuiya ya kimataifa kuadhimisha Siku ya Kiswahili. Tunasihi wote kukumbatia Kiswahili katika ngazi zote – kujifunza shuleni, kukitumia nyumbani, kukitumia katika biashara na kukijumuisha katika taasisi. Wito wetu mkubwa ni kutumia Kiswahili kukuza ujumuishaji wa kijamii na kupunguza migogoro. Kupitia Idara yake ya Lugha na Fasihi, Chuo Kikuu cha Eldoret kimejikita katika kukuza Kiswahili. Chuo kimezalisha wahitimu wengi wa Kiswahili wanaohudumu katika sekta mbalimbali ndani na nje ya nchi. Hivi majuzi, chuo kilizindua Taasisi ya Kiafrika ya Masomo ya Maendeleo, taasisi ya umahiri inayolenga lugha za asili za Kiafrika, ambapo Kiswahili kina nafasi ya kipekee. Hapa, Kiswahili si somo tu – ni njia ya kubadilishana maarifa, kukuza maelewano ya kitamaduni, na kuimarisha amani na ustawi. Mwandishi ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Eldoret
UBALOZI wa Tanzania nchini Sweden ukishirikiana na jumuiya za Watanzania waishio nchini humo, umeandaa na kufanikisha maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani jijini Stockholm. Maadhimisho hayo hufanyika duniani Julai 7 kila mwaka na yalianza mwaka 2022 kutekeleza azimio lililopitishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO). Akizungumza katika maadhimisho hayo,…
LEO ni maadhimisho ya Siku ya Lugha ya Kiswahili Duniani ambayo hufanyika kila Julai 7, tangu mwaka 2022 kutokana na azimio lililopitishwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO). Ni siku ya kipekee kwa Tanzania ambayo tangu kupigania uhuru, Kiswahili kimekuwa lugha ya umoja, utamaduni na ukombozi. Baada ya uhuru,…
Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden ukishirikiana na Jumuiya za Watanzania waishio nchini humo, umeandaa na kufanikisha sherehe za maadhimisho makubwa ya Siku ya Lugha ya Kiswahili Duniani yaliyofanyika Julai 5, 2025, jijini Stockholm. Maadhimisho hayo hufanyika Julai 7 kila mwaka kuanzia mwaka 2022 kufuatia Azimio lililopitishwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja…
DAR ES SALAAM: Mkurugenzi wa Taasisi ya Miriam Odemba Foundation (MOF) Miriam Odemba amesisitiza Watanzania kuchangia fedha kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa vyoo na baadhi ya miundombinu katika Shule ya Misingi Mwendapole iliyopo Kibaha mkoani Pwani. Hatua hiyo ni juhudi za taasisi hiyo katika kuiunga mkono serikali kuhakikisha wanafunzi wanapata miundombinu bora na imara…
Shule mbalimbali nchini zimetuma ujumbe kwa wazazi, zikiwashauri kutowapeleka watoto wao shuleni kesho, Julai 7, kutokana na hofu ya ghasia zinazotarajiwa wakati wa maadhimisho ya Saba Saba. Wakuu wa taasisi hizo walitaja sababu za kiusalama kwa wanafunzi na walimu, wengi wakisema watasubiri hali itulie kabla ya kurejelea shughuli za kawaida. Maandamano hayo, ambayo yamekuwa yakishika kasi katika miji mikuu nchini, yanatarajiwa Jumatatu, siku ya kumbukumbu ya maandamano ya kihistoria ya Saba Saba mnamo 1990 yaliyolenga mageuzi ya kidemokrasia nchini Kenya. “Kwa sababu ya maandamano yanayotarajiwa siku ya Jumatatu 7/7/25, tunawaomba wanafunzi wabaki nyumbani na warudi shuleni Jumanne 8/7/25, kama kawaida. Asanteni,” ulisema ujumbe kutoka shule zaidi ya 10. Hatua hii ya pamoja inajiri huku kukiwa na hofu kwamba, maandamano hayo yanayoopangwa na wanaharakati wa kizazi cha Gen Z pamoja na mashirika ya kijamii yanaweza kusababisha vurugu katika miji mikuu na barabara kuu. Wadau wa elimu wameeleza wasiwasi wao kuhusu usumbufu unaoendelea kwa masomo kutokana na maandamano ya kitaifa, wakitaka serikali kuhakikisha usalama wa wanafunzi na walimu wakati wowote maandamano kama hayo yanapotokea. Katika taarifa iliyotolewa Jumamosi, Chama cha Wadau wa Elimu Kenya kilisema kuwa maandamano ya hivi majuzi, ambayo mara nyingi huandamana na vurugu na makabiliano ya kikatili kati ya waandamanaji na maafisa wa usalama, yamesababisha hofu kubwa kwa wazazi na kusababisha kufungwa kwa shule kote nchini. “Jana, wazazi walianza kupokea ujumbe mfupi kutoka kwa shule ukieleza kuwa watoto hawapaswi kuripoti shuleni Jumatatu Julai 7 2025 (Saba Saba) kutokana na maandamano yanayotarajiwa, ambayo wakati mwingine hugeuka kuwa vurugu na makabiliano ya kikatili kati ya waandamanaji na maafisa wa usalama,” alisema Ndung’u Wangenye, Katibu Mkuu wa Chama cha Wadau wa Elimu Kenya. “Wiki iliyopita, Jumatano Juni 25 2025, wazazi walipokea taarifa kama hiyo kutoka kwa shule mbalimbali,” aliongeza.Chama hicho kilionya kuwa, usumbufu wa mara kwa mara unahatarisha kalenda ya masomo ambayo tayari ni dhaifu, hasa wakati huu ambapo shule bado zinapambana kutekeleza mtaala wa Umilisi (CBC). “Inapaswa kufahamika kuwa shule bado zinajaribu kujenga misingi imara ya utekelezaji wa CBC na usumbufu wa mara kwa mara wa shughuli za shule utaathiri kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa mtaala huu mpya,” alisema. Aidha, alieleza kuwa sekta ya elimu bado haijapona kutokana na usumbufu wa awali kama vile kufungwa kwa shule kwa muda mrefu kutokana na janga la COVID-19 kati ya mwaka 2021 na 2022, migomo ya walimu hasa wanachama wa KUPPET mwaka jana, na mafuriko ya kitaifa yaliyoathiri maelfu ya wanafunzi. Wadau sasa wanaitaka serikali kuweka mbele usalama na uendelevu wa elimu kwa kuhakikisha kuna ulinzi wa kutosha kwa shule wakati wa maandamano, na kuwalinda wale waliotaja kama 'waathirika halisi' wa vurugu hizi ambao ni watoto wa shule.Mnamo Juni 25, watu wasiopungua 16 walipoteza maisha na zaidi ya 400 kujeruhiwa.
SIGARA, dawa za kutibu maambukizi ya bakteria na dawa za kutibu malaria, bidhaa za urembo na ngozi ni miongoni mwa zinazoghushiwa zaidi nchini Kenya. Kwa mujibu wa ripoti mpya, hali hii inazua wasiwasi kuhusu kupotea kwa mapato na hatari za kiafya na usalama kutokana na bidhaa hizo feki kuenea sokoni. Ripoti hiyo mpya ilizinduliwa na Mamlaka ya Kukabiliana na Bidhaa Ghushi (ACA), ikifichua kuenea kwa bidhaa ghushi katika sekta kuu kama vile kilimo, famasia, pombe, vipodozi, na vifaa vya kielektroniki.Sekta ya tumbaku inaongoza sigara, zikichangia asilimia 89.47. “Dawa za kutibu maambukizi ya bakteria na dawa za malaria zinachangia asilimia 89.28 ya bidhaa feki, jambo ambalo linaweka afya ya umma hatarini kwa kupunguza ufanisi wa matibabu na usalama wa wagonjwa,” ilisema ACA. Sekta ya kilimo iliathirika kwa asilimia 89.16 huku waliohojiwa wakitaja mbolea na dawa za kuua wadudu kama bidhaa zinazoghushiwa zaidi, zikifuatiwa na vipuri vya magari kwa asilimia 81.89. Wakenya pia wananunua bidhaa ghushi bila kujua kama vile vipodozi, dawa za meno, karatasi za choo, nepi, shampoo, nywele bandia na bidhaa za nywele ambazo zinachangia asilimia 88.32 ya bidhaa bandia.Asilimia 81.89 ya washiriki walitaja vipuri vya magari ya magurudumu manne kuwa bidhaa ghushi zaidi katika sekta ya magari. Katika kilimo, zaidi ya nusu ya waliohojiwa walisema mbolea (asilimia 54.29) na chakula cha mifugo (asilimia 45.6) haziidhinishwi ipasavyo. Utafiti huo ulifanyika mwezi Agosti mwaka jana kwa ushirikiano kati ya ACA na Chuo Kikuu cha KCA, ukihusisha watu 2,185 kutoka kaunti nane zikiwemo Mombasa, Nairobi, Nakuru, Nyeri, Machakos, Kisumu, Garissa, na Busia.Mbegu (asilimia 34.9) na vifaa vya kilimo (asilimia 13.66) pia vimeathiriwa. “Uwepo wa pembejeo bandia unatishia utoshelevu wa chakula na maisha ya wakulima. Sheria kali zaidi, adhabu kali, na kampeni za uhamasishaji wa umma zinahitajika kupunguza athari za bidhaa feki katika sekta hii muhimu,” ilisema ACA. Utafiti huo ulifanyika mwezi Agosti mwaka jana kwa ushirikiano kati ya ACA na Chuo Kikuu cha KCA, ukihusisha watu 2,185 kutoka kaunti nane zikiwemo Mombasa, Nairobi, Nakuru, Nyeri, Machakos, Kisumu, Garissa, na Busia. ACA ilitaja maeneo kadhaa ya kutoa na kuuza bidhaa ghushi ikiwa ni pamoja na Hong Kong (China), Singapore, na Umoja wa Falme za Kiarabu, ambazo zinahusishwa na biashara ya bidhaa ghushi. Waliohojiwa walieleza wasiwasi kuhusu usalama wa vinywaji visivyo na kileo kama vile juisi na soda ambazo zilichangia takriban asilimia 75.89 ya bidhaa bandia.
TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) imeendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu matumizi sahihi ya nukta nundu (BRAILLE) kwa masomo ya wanafunzi wasioona. TEA inatoa elimu hiyo katika maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Saba Saba) lengo ni kuongeza uelewa kwa jamii. Mhakiki wa maandishi ya nukta nundu wa TET, Hadija…
MADRID, UHISPANIA : WIMBI la joto kali limeikumba sehemu kubwa ya bara la Ulaya, likisababisha shule nyingi kufungwa na vifo vya watu kuripotiwa katika nchi za Uhispania, Ufaransa na Ureno.