Wanafunzi 156,201 wanufaika ufadhili wa elimu

Habari Leo
Published: May 29, 2025 13:28:33 EAT   |  Educational

JUMLA ya wanafunzi 156,201 wamenufaika na ufadhili wa elimu kuanzia sekondari hadi shule ya upili kupitia Mpango wa ufadhili wa kwa wanafunzi wa kike chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali CAMFED Tanzania. Akizungumza leo Mei 29 Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa CAMFED, Nasikiwa Duke, amesema shirika hilo limelenga kusaidia watoto wa kike wanaotoka mazingira …

JUMLA ya wanafunzi 156,201 wamenufaika na ufadhili wa elimu kuanzia sekondari hadi shule ya upili kupitia Mpango wa ufadhili wa kwa wanafunzi wa kike chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali CAMFED Tanzania.

Akizungumza leo Mei 29 Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa CAMFED, Nasikiwa Duke, amesema shirika hilo limelenga kusaidia watoto wa kike wanaotoka mazingira magumu kutimiza ndoto zao kwa kumaliza kuwazuia kumaliza elimu.

“Kwa mwaka huu pekee, tumefadhili wanafunzi 36,424 kutoka shule 493 wanaosoma kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita,” amesema Nasikiwa.

Aidha ameongeza kuwa katika elimu ya ufundi, CAMFED imefadhili wanafunzi 217 wanaosoma katika vyuo vya VETA na FDC, vilivyoko katika maeneo mbalimbali nchini.

Kwa upande wa elimu ya juu, amesema wanafunzi 6,302 wamefikiwa na ufadhili, ambapo kwa mwaka wa masomo wa sasa, wanafunzi 576 wanasoma katika vyuo mbalimbali 67 nchini.