Kutokana na uchumi mgumu unaoendelea kushuhudiwa nchini, wazazi wengi wamekuwa wakilemewa kumudu karo ya kuwasomesha watoto wao.
George Wasonga, 57 afisa wa polisi amekuwa na kibarua kuwalipia watoto wake karo chuoni. Kama mzazi amekuwa akijituma sana kuhakikisha wanatimiza kiu chao cha kupata elimu ya juu ili wajitegemee siku za baadaye.
Nuru ilimwaangazia Wasonga wiki hii baada ya dua yake kutimia na akashinda Sh11 milioni kwenye ubashiri wa Sportpesa Midweek Jackpot.
“Nimekuwa nikipambana sana kuwasomesha watoto wangu na nia yangu imekuwa wasikose chochote maishani ili nao wawe na msingi wa kusaka kujizimbulia riziki siku zijazo,”akasema Wasonga, akiwa mwingi wa furaha baada ya kushinda hela hizo nyingi alizokiri zitasaidia kubadilisha maisha yake.
Alikuwa akiongea mtaa wa Shauri moyo viungani mwa jiji la Nairobi alipopokezwa hundi kutokana na ushindi wake ambao sasa unaashiria mwanzo wa ufanisi na maisha mazuri.
“Kupitia mapenzi ya mwenyezi Mungu sasa mambo yataimarika na wanangu watasoma na kufikia viwango vya juu vya elimu nchini. Sasa sina shaka kwa sababu kila kitu wanachohitaji, nitawatimizia,” akaongeza.
Kando na kuwasomesha wanawe, afande huyo tayari ameweka mikakati ya kupanua biashara zake kisha kufanyia nyumba yake ukarabati.
Wasonga amekuwa akibashiri mechi na Sportpesa tangu 2016 na amewahi kushinda Sh15,000 mapema mwaka huu.
Hata baada ya kushinda Sh11 milioni kuwahi bonasi ya 12 kwenye Mega Jackpots ameapa kuwa ataendelea kushiriki huku akilenga Mega Jackpot. Jumamosi hii Mega Jackpot ilikuwa imefika Sh420,655,592.
“Kwa wengine wanaobashiri jikazeni kwa sababu dua yenu itatimia. Nami nitaendelea kwa sababu nalenga fedha za juu zaidi kwenye Mega Jackpot,” akasema.
Afisa wa Polisi ashinda Sh11 milioni Sportpesa Midweek Jackpot
This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
EducationalKitui school gets new irrigation project as govt announces 7 more under KRISE programme
The government commissioned a micro-irrigation project at Kangalu School in Kitui County, benefiting 2,400 people as seven more projects are planned.
EducationalNyumbu kupata miundombinu bora ya shule
KIBAHA: MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Kibaha, Dk.Nicas Mawazo, ameahidi kushirikiana na Baraza la Madiwani pamoja na wataalamu wa halmashauri hiyo kuhakikisha miundombinu ya elimu katika Shule ya Sekondari na Msingi Nyumbu inaboreshwa, ili kuimarisha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji. Ahadi hiyo ameitoa wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua miundombinu ya shule hizo…
EducationalKenyan Form 4 boy shreds his trouser, shirt after finishing KCSE exams: “Amekafunga in style”
A Kenyan Form 4 student celebrated finishing the 2026 KCSE exams by cutting his school trousers into tassels in a viral video shared by Nairobi Juice online.
EducationalUniversity of America challenges NUC over illegal operations
By Ibrahim Hassan-Wuyo The National Universities Commission (NUC) and the University of America, Curaçao, have disagreed over the legality of the institution’s academic operations in Nigeria, with the commission warning prospective students against seeking admission into its programmes. The NUC had declared the institution’s operations in Nigeria illegal, alleging that it was admitting students, running […]