
Waziri Ndumbaro awasili New York mkutano uwindaji kitalii
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amewasili Jijini hapa New York, Marekani leo tarehe 18 Januari 2022 kwa ajili ya kushiriki mkutano wa 50 wa mwaka wa Uwindaji wa Kitalii ( Annual Hunting Convention) ulioandaliwa na Jumuiya ya Uwindaji ya Kimataifa.



















