Top headlines and developing stories from Tanzania, Kenya, Uganda and the wider region, gathered from the leading local and international newsrooms and updated throughout the day.
RC MTANDA AWAKALIA KOONI WAKANDARASI WA UJENZI MRADI WA MAJI BUSEGA Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Saidi Mtanda, amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi mkubwa wa maji wilayani Busega na kuwabananisha…
SERIKALI imeunda kikosi cha asasi mbalimbali ili kuharakisha utekelezaji wa agizo la Mahakama Kuu linalohitaji kuwekwa kwa kanuni mpya za kusimamia maandamano ya umma na mienendo ya polisi. Kikosi hicho kinajumuisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wizara ya Usalama wa Ndani, Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS), Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu (KNCHR), Tume ya Huduma kwa Polisi (NPSC), Mamlaka Huru ya Usimamizi wa Polisi (IPOA) pamoja na mashirika mengine. Hatua hiyo ilibainika wakati mahakama ilipopewa taarifa kuhusu utekelezaji wa uamuzi wa Machi 25, 2026, ulioitaka serikali kuchapisha kanuni za maandamano, maandamano ya kutumia au kupita barabarani na matumizi ya nguvu ya polisi dhidi ya waandamanaji kwa muda wa siku 90. Agizo hilo lilielekezwa kwa Inspekta Jenerali wa Polisi, NPS na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Mahakama iliambiwa kuwa kamati hiyo imeandaa mpango wa utekelezaji na pia inasaidia kupitishwa kwa Mswada wa Usimamizi wa Utulivu wa Umma wa 2025 ambao kwa sasa uko katika Bunge la Kitaifa. “Kamati ilikutana Juni 26, 2026 kuweka mpango wa kushughulikia mswada huo ambao sasa uko mbele ya Bunge la Kitaifa,” Mwanasheria Mkuu aliambia mahakama alipokuwa akiomba muda zaidi ili taratibu zote zinazohitajika kukamilishwa kabla ya sheria hiyo kupitishwa. Serikali imesema mswada huo utachukua nafasi ya Sheria ya Utulivu wa Umma na kuweka utekelezaji Ibara ya 37 ya Katiba inayolinda haki ya wananchi kukusanyika kwa amani na bila silaha, kufanya maandamano, maandamano ya kutumia mabango na kuwasilisha malalamishi. Hatua hiyo ilifuatia uamuzi wa mahakama kapata Inspekta Jenerali wa Polisi, NPS na Mwanasheria Mkuu katika na hatia ya kukaidi amri ya mahakama baada ya kushindwa kutekeleza agizo hilo ndani ya siku 90. Jaji Alfred Mabeya aliwaondolea adhabu baada ya kuzingatia maombi yao ya msamaha na hatua walizochukua kutekeleza agizo hilo. Hata hivyo, aliwataka kuwasilisha ripoti ya utekelezaji kila baada ya miezi minne. Ripoti ya kwanza inatarajiwa Januari 25, 2027, huku mahakama ikionya kuwa hatua kali za adhabu zinaweza kuchukuliwa iwapo watashindwa kutekeleza agizo hilo. Uamuzi huo unatokana na kesi iliyowasilishwa kufuatia jinsi polisi walivyoshughulikia maandamano ya kupinga serikali yaliyofanyika Kisumu, Migori na Ahero kati ya Machi na Julai 2023.
ZAIDI ya wanafunzi milioni 3.6 watafanya mitihani na tathmini za kitaifa mwaka huu huku serikali ikiweka masharti magumu kukabiliana na udanganyifu na kuhakikisha uadilifu katika mchakato huo. Waziri wa Elimu Julius Ogamba jana aliwaonya watahiniwa, wasimamizi wa vituo na wasimamizi wa mitihani dhidi ya kukiuka kanuni, akisema watakaopatikana wakifanya udanganyifu watachukuliwa hatua kali za kisheria. “Hatutakuwa na huruma kwa yeyote atakayepatikana akijihusisha na aina yoyote ya udanganyifu,” akasema Bw Ogamba wakati wa uzinduzi wa msimu wa mitihani na tathmini za kitaifa za 2026 katika jumba la Mitihani House, Nairobi. Jumla ya watahiniwa 3,634,846 wamejisajili kwa tathmini na mitihani hiyo, idadi ambayo inashinda mwaka uliopita. Wanafunzi watakaofanya mitihani ya KPSEA ni 1,380,463, ikilinganishwa na 1,298,089 mnamo 2025. Wale wa Sekondari Msingi, (KJSEA) ni 1,206,028, kutoka 1,130,679 mwaka jana, huku watahiniwa 1,048,355 wakifanya mtihani wa kidato cha nne, KCSE, kutoka 996,078 mwaka jana. KCSE inaanza Oktoba 16 kwa matayarisho kisha ing’oe nanga rasmi Oktoba 19. KJSEA na KPSEA inaanza Oktoba 26. Bw Ogamba alisema ongezeko hilo linahitaji umakinifu na rasilimali zaidi kutoka kwa maafisa wanaosimamia mitihani. Aliwataka wadau wote kufuata kanuni na kutumia mbinu mpya zilizowekwa kuboresha ufanisi na uaminifu wa mitihani. “Ni lazima tushirikiane kuhakikisha mitihani inasimamiwa kwa njia ya haki na bila udanganyifu. Hii ndiyo njia pekee ya kuweka mfumo wetu wa elimu katika ushindani wa kimataifa,” akasema. Serikali pia imeongeza makontena 48 ya kuhifadhi vifaa vya mitihani katika maeneobunge, na kufikisha idadi hiyo 701. Bw Ogamba alisema hatua zimechukuliwa kupunguza athari za mvua za El Nino, huku maafisa wa nyanjani wakipatiwa mafunzo kabla ya mitihani kuanza.
KIBAHA: COAST Region is targeting 42,000 tonnes of cashew nuts in the 2026/2027 season as authorities seek to raise production to 73,000 tonnes by 2029/2030. Coast Regional Commissioner, Mr Stanslaus Nyongo, said the targets could be achieved if farmers and other stakeholders followed agricultural experts’ advice on production, storage and marketing. “Our aim is to…
The growing participation of local investors in Tanzania’s capital market is raising the need for stronger investor education and protection, analysts have said.
UCHAGUZI mdogo wa wadi ya Migwani, Kaunti ya Kitui, umegeuka kuwa uwanja mpya wa mapambano ya kisiasa kati ya kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka na washirika wa Rais William Ruto kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Uchaguzi huo ulitokana na kujiuzulu kwa aliyekuwa Diwani wa Migwani, Harrison Maluki, ambaye aliacha wadhifa huo Agosti 6 na kuwa karani wa Bunge la Kaunti ya Kitui. Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imetangaza kuwa uchaguzi huo utafanyika Novemba 17. Bw Maluki, aliyewahi kuwa kiongozi wa wengi katika Bunge la Kaunti ya Kitui baada ya kuchaguliwa kupitia tiketi ya Wiper, sasa anaonekana kuwa karibu na baadhi ya washirika wa Rais Ruto. Hatua hiyo imezidisha mvutano kati yake na Bw Musyoka. Bw Musyoka akihutubia wafuasi wake nyumbani kwake Kitui, aliwataka wakazi kuchukua fedha zinazotolewa na wapinzani wake lakini kumpigia kura mgombea wa Wiper. “Chukueni pesa hizo lakini mpige kura kuonyesha kuwa mko tayari kuleta urais nyumbani,” akasema Bw Musyoka. Kiongozi huyo wa Wiper anataka chama chake kishinde uchaguzi huo ili kuonyesha kuwa bado kina ushawishi mkubwa katika ngome yake ya Kitui. Wanaowania tiketi ya Wiper ni aliyekuwa Diwani wa Migwani Patrick Munyithya Kani, Munywoki Mwangangi na Susan Mueni Nzoka. Hata hivyo, Wiper inakabiliwa na upinzani kutoka kwa baadhi ya washirika wake wa zamani, akiwemo Spika wa Bunge la Kaunti ya Kitui Kinengo Katisya na Bw Maluki. Wawili hao wanapinga kile wanachosema ni juhudi za chama kuzuia wapiga kura kuchagua mgombea wanayemtaka. “Wiper inapaswa kuwapa wapigakura wa Migwani nafasi ya kuchagua diwani wanayemtaka. Hatupendezwi na siasa za vyama,” alisema Bw Katisya. Kwa upande wa serikali, washirika wa Rais Ruto akiwemo Mbunge wa Mwingi Magharibi Charles Nguna na aliyekuwa Seneta wa Kitui David Musila, wanaona uchaguzi huo kama nafasi ya kuvunja ushawishi wa Bw Musyoka katika kaunti hiyo. Wanaangazia miradi ya maendeleo ya serikali kama sehemu ya kampeni zao, hasa ujenzi wa barabara ya Kwa Siku-Migwani-Mbondoni. Baadhi ya wakazi tayari wanasema miradi hiyo imebadili maisha yao. Alice Mutwa, mfanyabiashara wa mboga mwenye umri wa miaka 60, alisema uchaguzi huo utampa nafasi ya kumshukuru Rais Ruto kwa maendeleo katika eneo hilo.
A coalition of 11 civil society organisations has raised the alarm over the unexplained disruption of TikTok services in parts of northern Nigeria, describing over two weeks of institutional silence as worrying.
TANGA: PRIME Minister Dr Mwigulu Nchemba has called on Tanzanians to strengthen support for people with disabilities and vulnerable children, stressing that caring for them is a shared national responsibility. Dr Nchemba made the call yesterday during a fundraising event aimed at supporting the development and improvement of service and diakonia centres run by the…
MAADHIMISHO ya mwaka mmoja tangu kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga yamegeuka kuwa uwanja wa mapambano ya kisiasa huku wanasiasa wakitumia jina lake kujipigia debe kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Raila, aliyefariki Oktoba 15, 2025, alikuwa mmoja wa wanasiasa mashuhuri zaidi nchini na mwanzilishi wa chama cha ODM. Chama hicho kimeandaa shughuli za kisiasa za mwezi mzima za kumuenzi, huku viongozi mbalimbali wakijitahidi kujitambulisha na itikadi na sifa zake. Baadhi ya wanasiasa tayari wameanza kuchapisha na kusambaza bidhaa za kampeni zenye picha ya Raila pamoja na kauli-mbiu zao za 2027. Shughuli hizo zinaonyesha jinsi kumbukumbu ya kiongozi huyo imekuwa muhimu katika vita vya kutafuta ufuasi baada ya kifo chake. ODM inapanga kufanya mikutano Siaya, Kakamega, Garissa, Mombasa, Kajiado, Turkana na Nairobi. Ingawa mikutano hiyo imepewa jina la kumuenzi Raila, inaonekana pia inalenga kuimarisha ngome ya chama na kuhamasisha wafuasi kabla ya uchaguzi wa 2027. Chama hicho pia kinataka kutumia maadhimisho hayo kuonyesha mafanikio ya serikali ya muungano kati ya Rais William Ruto na ODM. Rais Ruto, ambaye alishirikiana na Raila katika Serikali Jumuishi baada ya maandamano ya Gen-Z ya 2024, anatarajiwa kuhudhuria hafla kuu ya kumbukumbu mjini Bondo. Hata hivyo, maadhimisho hayo yameibua pia vita vya urithi wa kisiasa wa Raila. Nairobi, Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino aliendesha hafla tofauti ya kuwasha mishumaa katika uwanja wa Jacaranda huku ODM na washirika wa serikali wakiongoza hafla ya Uhuru Park. Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, ambaye ameanzisha The Equitable Party, (TEP) pia alisema Oktoba ni mwezi muhimu kwa sababu Raila alifariki wakati huo. Bw Sifuna na viongozi wengine wa Linda Mwananchi Movement wanajiandaa kushiriki katika kinyang’anyiro cha 2027. Ndani ya familia ya Odinga, suala la mrithi wa kisiasa pia limejitokeza. Binti yake, Winnie Odinga, alitambuliwa na baadhi ya wazee wa jamii ya Luo kama mrithi wa kisiasa wa baba yake. Mama yake Ida na dada yake Rosemary walihudhuria hafla hiyo, huku Raila Odinga Junior akikosekana. Gavana wa Siaya James Orengo naye anatumia kipindi hiki kujipanga kwa uchaguzi wa 2027 na ametangaza nia ya kuwania urais. Kwa hivyo, badala ya kuwa tukio la kumkumbuka tu Raila, maadhimisho yake yamekuwa jukwaa la kujipigia debe, kujenga ushawishi na kutafuta urithi wake wa kisiasa kuelekea uchaguzi wa Agosti 2027.
HUZUNI imetanda Kiambaa, katika kijiji cha Moto, Molo, Kaunti ya Nakuru, baada ya mwanafunzi wa Kidato cha Nne kupatikana ameuawa kikatili nyumbani kwao. Joy Wangui, 18, mwanafunzi wa Shule ya Upili ya Molo, alipatikana Jumapili akiwa amelala na kulowa damu kwenye jikoni, huku kichwa chake kilichokatwa kikapatikana karibu na bafu. Polisi wameanzisha msako wa mshukiwa anayefahamika kwa familia na wakazi wa eneo hilo, ambaye alitoroka baada ya mauaji. Kamanda wa Polisi wa Molo Justus Katana alisema polisi walipokea taarifa kutoka kwa wananchi mwendo wa saa nane Jumapili kuhusu mauaji hayo. Jirani Paul Muraguri Mwangi alisema tukio hilo limewaacha wakazi wakiwa na hofu. Alisema shoka, panga na kisu, zote zilipatikana katika eneo la tukio na huenda zilitumika katika mauaji. Jirani mwengine, Charles Njenga Matendo, alisema kaka mdogo wa Wangui ndiye aliyegundua mwili wake baada ya kurejea kutoka kwa duka la familia lililokuwa karibu. Wakazi wanahofia kuwa mauaji hayo huenda yalihusiana na mzozo wa kimapenzi, ingawa polisi bado hawajathibitisha nia ya mshukiwa. Maafisa wa Idara ya Upelelezi Nchini (DCI) waliendesha uchunguzi wa kitaalamu katika eneo la tukio huku damu ikiwa bado imeonekana jikoni. Askofu Joram Nderu alimtaja Bi Wangui kama msichana mnyenyekevu, mwenye heshima na furaha aliyekuwa na matarajio mengi mema maishani.
NAIBU Rais Profesa Kithure Kindiki huenda asiwe mgombea mwenza wa Rais William Ruto katika uchaguzi mkuu wa 2027, Mbunge wa Ndia George Kariuki amedai. Bw Kariuki, ambaye ni mshirika wa karibu wa Rais Ruto, alisema Profesa Kindiki kwa sasa anashikilia wadhifa huo lakini anaweza kubadilishwa kabla ya uchaguzi. Akizungumza na redio ya Kameme, mbunge huyo alipinga madai kwamba Chama cha ODM ndicho kitatoa mgombea mwenza wa Rais Ruto. Alisema nafasi hiyo bado itaenda kwa mtu kutoka eneo la Mlima Kenya, ingawa huenda asiwe Profesa Kindiki. “ODM haitahitajika kutoa mgombea mwenza. Suala hilo litajadiliwa ili kubaini anayefaa zaidi kutoka eneo hili lenye kura nyingi,” akasema. Bw Kariuki pia alisisitiza umuhimu wa wakazi wa Mlima Kenya kubaki na umoja na kukataa mipango ya kugawanya kura za eneo hilo. Majuzi, Bw Kariuki alimvamia Profesa Kindiki akisema ameshindwa kuwatetea wakazi wa Mlima Kenya. Pia aliwakosoa Profesa Kindiki na kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua kwa kushambuliana kisiasa na kugawanya eneo hilo.
KINARA wa chama cha The Equitable Party (TEP) Edwin Sifuna amedokeza kwa mara ya kwanza, kuhusu maono yake kwa Kenya akitaja nafasi ya uchumi, uwajibikaji, udumishaji wa katiba na kupunguza ubadhirifu wa serikali, kama msingi wa azma yake ya kuwania urais 2027. Kitovu cha ajenda ya Bw Sifuna, anayoichora kuwa tofauti kabisa na mtindo wa uongozi wa Rais William Ruto, ni ahadi ya kupanua ushiriki wa umma, kuunda nafasi zaidi za kazi kwa vijana, kupunguza ushuru, kuzidisha vita dhidi ya ufisadi na kukomesha upunjaji katika serikali. Aliahidi vilevile kufanyia mageuzi sekta za elimu na afya akihoji kwamba wazazi wengi wanazidi kung’ang’ana kuwadumisha watoto wao shuleni huku wagonjwa wakikabiliwa na changamoto kupata huduma za afya licha ya utawala wa Kenya Kwanza kuzindua Bima ya Afya ya Jamii (SHIF). Iwapo atachaguliwa, Bw Sifuna ameahidi kufutilia mbali ada ya nyumba za bei nafuu na ushuru wa thamani kwa bidhaa za petroli kama sehemu ya mpango mpana wa kupunguza gharama ya maisha. Wakenya walioajiriwa kwa sasa wanachangia ada ya lazima ya asilimia 1.5 ya mishahara yao kufadhili Mpango wa Nyumba za Bei Nafuu pamoja na kiasi sawa na hicho kutoka kwa waajiri wao. Kufuta ada hiyo na SHIF vilevile kumejitokeza bayana kwenye majukwaa ya vinara kadhaa wa upinzani wanaodhamiria kumenyana na Dkt Ruto 2027. Mpango wa makazi, hata hivyo, umesalia moja kati ya miradi muhimu ya Rais Ruto. Dkt Ruto ameutaja mara kadhaa kuwa mradi maalum utakaounda mamilioni ya nafasi za kazi kwa vijana huku ukiwapa makazi bora wanajamii wenye mapato duni. Lakini Bw Sifuna anaeleza kuwa tatizo la Kenya si kukosa makazi bali ukosefu wa mapato, upuuzaji wa mambo muhimu na ufisadi na ubadhirifu miongoni mwa maafisa wa serikali. Alisema serikali atakayoongoza itajituma kusawazisha bajeti katika miezi 15 kwa kupunguza uchu wa kukopa na kuelekeza mikopo kwa sekta ya kibinafsi. Seneta huyo wa Nairobi anakadiria kuwa kati ya Sh500 bilioni na Sh1.8 trilioni huenda zikaokolewa kwa kuangamiza alichotaja kuwa ufisadi na ubadhirifu uliokolea kwenye matumizi ya serikali. Bw Sifuna anasema amekusanya kikosi cha wataalam ambacho kiko katika hatua za mwisho za kuandaa manifesto yake yenye maelezo ya kina kuhusu mpango wake. Ananuia kutumia ruwaza hiyo kama msingi wa kuwaomba kura Wakenya katika uchaguzi mkuu 2027. “Wataalamu wamenieleza kuwa inawezekana kuanzia siku ya kwanza kupunguza upunjaji serikalini na kuwapa afueni wananchi wetu kwa kupunguza kiasi sawia cha ushuru. Wananihakikishia kuwa kati ya Sh500 bilioni na Sh1.8 trilioni ni ufisadi wa kupanga kwenye bajeti.” “Wanasema ikiwa tutakabiliana kwa kujitolea na ufisadi huu uliopagiwa bajeti, inawezekana kuondoa Ada ya Nyumba, Ushuru wa Thamani kwa mafuta na umeme utakaowafaidi Wakenya wote,” alisema Bw Sifuna kwenye hotuba iliyoandikwa. Mbali na mikakati mahsusi iliyozinduliwa Jumapili alipozindua chama chake cha TEP, Bw Sifuna amehoji mara kadhaa kuwa maendeleo hayawezi kutenganishwa na uzingatiaji katiba na kuheshimu utawala wa sheria. Amekosoa miradi mikuu ya Rais Ruto, ukiwemo wa nyumba za bei nafuu, viwanja vya spoti na masoko, akiitaja mipango hiyo kuwa “vitu vinavyong’aa” visivyofaa kuwapumbaza Wakenya kusahau “alivyofeli pakubwa katika utawala wake”. Seneta huyo anasema kwamba miradi ya maendeleo haipaswi kufidia ukiukaji wa haki za binadamu wala kuhujumu nguzo za kikatiba. “Chama cha The Equitable Party hakiji kikipeperusha ufito wa miujiza utakaofuta matatizo yote nchini. Lakini tunakusudia kutoa mwongozo ambao kupitia kwao masuala haya yanaweza kusikika na kuangaziwa kupitia taasisi za kidemokrasia zinazoambatana na sheria,” alisema. Alitaja matatizo yanayowakabili wakulima na biashara ndogondogo, ikiwemo kiwango cha juu cha ushuru na gharama inayozidi kupanda ya kufanya biashara, kama masuala ambayo utawala wake utajitahidi kuangazia. Kiasi cha Sh2 bilioni kimetajawa na viongozi wa Kenya hapo mbeleni kuibwa kila siku. Februari, 2021, aliyekuwa rais wakati huo Uhuru Kenyatta aliambia Wakenya kuwa kiasi kisichopungua Sh2 bilioni huibwa kila siku, kauli iliyozua mdahalo wa umma kuhusu kiwango cha ufisadi na upunjaji wa rasilimali za umma.
Governor praises health infrastructure, security intervention BAUCHI — Bauchi State Governor, Senator Bala Abdulkadir Mohammed, has commended President Bola Ahmed Tinubu for supporting the state with critical health infrastructure and security interventions despite political differences between the Federal and Bauchi State governments. Mohammed spoke in Bauchi while receiving a Federal Government delegation led by the […]
NATION Media Group (NMG) jana ilizindua maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja katika jumba la Nation Centre, Nairobi, ikisisitiza kujitolea kwake kutoa huduma bora, uandishi huru wa habari na kuboresha huduma zake za kidijitali. Akizungumza na wafanyakazi na wasimamizi, Mkurugenzi Mkuu na Afisa Mkuu Mtendaji wa NMG Geoffrey Odundo aliwataka wafanyakazi kuwa mabalozi wa kampuni huku wakizingatia viwango vya juu vya huduma na uwajibikaji. Alisema NMG inalenga kuhudumia wasomaji na watazamaji wake kwa kuwasikiliza na kujibu mahitaji yao. Maadhimisho ya mwaka huu yanaongozwa na kaulimbiu “The Extra Mile”, huku kampuni ikisisitiza mabadiliko yake kuwa shirika linalotanguliza huduma za kidijitali.
By Luminous Jannamike ABUJA – Former Vice President and presidential candidate of the African Democratic Congress, ADC, Atiku Abubakar, has told the Federal Government that praise will not ease the hardship facing Nigerian teachers, urging it to tackle the rising cost of food, transport, rent and electricity. Atiku said teachers were being asked to keep […]
SENETA Flavio Bolsonaro amefuzu kwa raundi ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Brazil baada ya kumpiku kwa tofauti ndogo Rais wa sasa Luiz Inacio Lula da Silva katika uchaguzi mkuu. Bolsonaro, mwanawe rais wa zamani, Jair Bolsonaro, alipata asilimia 47 ya kura dhidi ya asilimia 45 za Lula. Matokeo hayo yalikuwa kinyume na utabiri wa kura za maoni, ambazo zilitarajia Lula kuongoza kwa tofauti ya karibu asilimia tatu. Sasa wawili hao watamenyana katika uchaguzi wa mwisho utakaofanyika Oktoba 25. Baada ya matokeo, Flavio alisema raia wa Brazil wanataka mabadiliko na kutangaza kile alichokiita mwisho wa enzi ya chama cha Lula cha Workers’ Party. Lula, ambaye alitarajia kushinda katika raundi ya kwanza, aliwaambia wafuasi wake kuwa kampeni mpya inaanza mara moja na akaahidi kuwaeleza wapigakura mafanikio ya serikali yake. Uchaguzi huo ulitawaliwa zaidi na masuala ya gharama ya maisha, ukosefu wa usalama na ufisadi. Licha ya kupungua kwa tatizo la uhaba wa ajira na tofauti za kimapato, Lula amekabiliwa na changamoto ya kuwashawishi wananchi wanaolalamikia gharama kubwa za maisha, madeni ya kifamilia na ongezeko la shughuli za magenge. Flavio ametumia hali hiyo kuomba kura za mabadiliko, huku Lula akipanua mipango ya ustawi wa jamii na kupendekeza msamaha wa baadhi ya madeni ya familia. Uchumi pia ulikuwa suala muhimu, huku matumizi ya serikali yakiongezeka na deni la umma kufikia zaidi ya asilimia 82 ya pato la taifa. Serikali pia ilipunguza utabiri wa ukuaji wa uchumi wa Brazil mwaka huu hadi asilimia mbili. Uchaguzi huo pia ulikumbwa na mijadala kuhusu ufisadi na madai ya kuingiliwa kutoka nje. Jair Bolsonaro, baba yake Flavio, anatumikia kifungo cha miaka 27 kwa kupanga mapinduzi baada ya kushindwa uchaguzi wa 2022. Flavio sasa anajaribu kutumia urithi wa kisiasa wa baba yake kumpinga Lula. Ingawa Rais wa Amerika, Donald Trump hajamtangaza rasmi mgombeaji anayemuunga mkono, amekuwa akimsifu Flavio na kumkaribisha Ikulu ya White House. Kwenye raundi ya pili, Brazil sasa inakabiliwa na ushindani mkali kati ya mrengo wa kushoto unaoongozwa na Lula na mrengo wa kulia unaowakilishwa na Bolsonaro. Matokeo hayo pia yanaonyesha mgawanyiko mkubwa wa kisiasa nchini Brazil, huku Flavio akifanya vizuri zaidi katika maeneo ya Kusini, Kusini-Mashariki na Kati-Magharibi, wakati Lula aliongoza katika ngome zake za Kaskazini-Mashariki pamoja na baadhi ya majimbo ya Kaskazini. Kwa upande mwingine, wapigakura waliowaunga mkono wagombeaji wengine sasa wanakuwa muhimu katika raundi ya pili. Augusto Cury alipata karibu asilimia 2.9, Renan Santos asilimia 2.2 na Ronaldo Caiado asilimia 2.2, huku wagombeaji wengine wakigawana sehemu ndogo ya kura. Ushiriki wa wapigakura pia ulikuwa suala muhimu, kwani takriban asilimia 21 ya wapigakura waliojiandikisha hawakupiga kura. Asilimia 2.93 ya kura ziliharibika na asilimia 1.84 zikawa “nyeupe” (mpigakura kutochagua mwaniaji yeyote), hali inayomaanisha kuwa sehemu kubwa ya wapigakura ambao hawakuwachagua wagombea hao wawili bado inaweza kuwa muhimu katika raundi ya mwisho. Kwa Flavio, ushindi huo wa raundi ya kwanza umempa nafasi ya kuendeleza urithi wa kisiasa wa familia ya Bolsonaro, huku Lula akilenga kuunganisha wafuasi wake na kupata kura za wagombea walioshindwa. Kwa kuwa tofauti kati yao ilikuwa chini ya asilimia mbili, kampeni ya kuelekea Oktoba 25 inatarajiwa kulenga zaidi masuala ya uchumi, usalama, ustawi wa jamii na mwelekeo wa kisiasa wa Brazil.
DAR ES SALAAM: Tanzania na Misri zitaendelea kuimarisha ushirikiano katika kukabiliana na usafirishaji haramu wa binadamu pamoja na magendo ya wahamiaji, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ayoub Mohammed Mahmoud, amesema. Amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua mafunzo ya siku tano yanayolenga kuwajengea uwezo maofisa wanaohusika na mapambano dhidi ya…
DODOMA: WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Leonard Akwilapo, amezitaka mamlaka za miji, taasisi na wananchi kuchukua hatua za maandalizi kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua za El Niño. Dk Akwilapo alitoa rai hiyo jjijini Dodoma wakati akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Makazi Duniani 2026 yaliyofanyika chini ya kaulimbiu…
DAR ES SALAAM: SERIKALI imeendelea kuweka mikakati mbalimbali ya kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, ikiwemo kuimarisha huduma za kinga, uhamasishaji na elimu kwa jamii ili kuongeza uelewa kuhusu namna ya kujikinga na magonjwa hayo. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza, Dk. Omary Ubuguyu, katika Mkutano wa 13 wa…
Tanzania continues with efforts to raise awareness on Dyslexia and this time the region is organizing a third instalment special athletics event to that effect, intending to make this year's event a springboard towards nationwide expansion from 2027 onwards.
KAUNTI za Nairobi na Nakuru zinadaiwa Sh75.7 bilioni za mapato ambayo hayajalipwa, kiasi kinachozidi madeni yanayodaiwa na kaunti 45 zilizosalia kwa pamoja. Kiasi hicho ni zaidi ya theluthi mbili ya Sh113.3 bilioni ambazo kaunti zote 47 zinadaiwa kufikia Juni 30, 2026. Kwa mujibu wa ripoti ya utekelezaji wa serikali za kaunti ya mwaka wa kifedha wa 2025/2026 iliyoandaliwa na Mdhibiti wa Bajeti (COB) Margaret Nyakang’o, Nairobi inaongoza kwa deni la mapato la Sh59.09 bilioni, ikifuatiwa na Nakuru yenye Sh16.64 bilioni. Madeni ya Nairobi yanawakilisha asilimia 52.15 ya jumla ya mapato ambayo hayajalipwa kwa kaunti zote, huku Nakuru ikiwa na asilimia 14.69. “Mnamo Juni 30, 2026, Kaunti ya Nairobi ilikuwa na madeni ya juu zaidi ya Sh59.09 bilioni, ambayo ni asilimia 52.15 ya jumla ya mapato ambayo hayajalipwa. Kaunti ya Nakuru ilikuwa na Sh16.64 bilioni (asilimia 14.69) ya jumla ya madeni ya mapato,” inasema ripoti hiyo. Sehemu kubwa ya madeni hayo inatokana na ushuru wa ardhi, kodi za nyumba na ada nyingine, huku baadhi ya madeni yakiwa yametokana na zaidi ya miaka 10 iliyopita. Ripoti hiyo inasema hali hii inaonyesha changamoto katika ukusanyaji wa mapato, utekelezaji wa sheria na usimamizi wa fedha, jambo linalopunguza uwezo wa kaunti kutoa huduma na kugharamia maendeleo. Mtaalamu wa utawala David Ngugi alisema kurejeshwa kwa Sh113.3 bilioni kungeongeza uwezo wa kaunti kugharamia huduma muhimu na kupunguza utegemezi wao kwa serikali kuu. “Sh113.3 bilioni zinaweza kubadilisha kwa kiasi kikubwa huduma za afya katika kaunti kadhaa. Zinaweza kugharamia na kuweka vifaa katika hospitali za kisasa katika kaunti kadhaa,” akasema Bw Ngugi. “Kiasi hicho ni karibu asilimia 35 ya mgao wa fedha kwa kaunti. Pia kinaweza kugharamia miradi kadhaa mikubwa ya maji,” akaongeza Bw Ngugi. Ripoti ilisema kaunti nyingi hazijafanya juhudi za kutosha kurejesha madeni hayo, hali ambayo imezifanya kutegemea zaidi fedha kutoka serikali kuu ambazo wakati mwingine huchelewa. Nairobi, ushuru wa ardhi ndio unaochangia sehemu kubwa ya deni, huku wamiliki wa mali wakidaiwa Sh51.34 bilioni. Kaunti hiyo pia inadaiwa Sh5.64 bilioni za ada za matumizi ya maeneo ya umma, Sh440.6 milioni za kodi za nyumba na ada za vibanda vya biashara, pamoja na Sh283.7 milioni kutokana na matangazo ya nje na mabango. Kampuni ya Umeme inatajwa kama mmoja wa wanaodaiwa wakubwa, ikiwa inadaiwa Sh5.6 bilioni za ada za matumizi ya maeneo ya umma. Nakuru, deni la mapato ni zaidi ya mara tatu ya Sh5.4 bilioni ambazo kaunti hiyo ilikusanya katika mwaka wa kifedha wa 2025/2026. Ushuru wa ardhi ulikuwa Sh11.8 bilioni ya deni hilo, huku kodi za nyumba ikiwa Sh782 milioni. SHA inadaiwa Sh456.9 milioni na NHIF iliyovunjwa Sh432.9 milioni. Mombasa ilikuwa na deni la tatu kwa ukubwa la Sh13.68 bilioni, ikifuatiwa na Kiambu yenye Sh5.63 bilioni. Kaunti nyingine zenye madeni makubwa ni Kitui (Sh2.2 bilioni), Busia na Kakamega (Sh1.7 bilioni kila moja), Laikipia (Sh1.4bilioni), Kisii (Sh1.3 bilioni), na Nyeri na Bomet (Sh1.2 bilioni kila moja). Kwa mujibu wa Tume ya Ugavi wa Mapato, kaunti zina uwezo wa kukusanya angalau Sh260 bilioni kila mwaka lakini zinaendelea kukusanya chini ya Sh100 bilioni. Katika mwaka wa kifedha wa 2025/2026, kaunti zote 47 zilikusanya Sh96 bilioni kutoka Sh60 bilioni mwaka uliotangulia. Bi Nyakang’o amezishauri kaunti kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato, kutumia teknolojia na kuchukua hatua kali dhidi ya kampuni zinadaiwa ili kuongeza mapato na kupunguza utegemezi wa serikali kuu.
Minerals Minister Anthony Mavunde has ordered a technical review of levies and other statutory charges affecting small-scale miners, opening a joint Government-industry process to examine how payments are treated as minerals move from extraction through processing to sale. The review follows concerns raised by small-scale miners in Geita over the difficulty of linking payments made at earlier stages of the production chain to the same mineral consignment when it reaches another processing or regulatory point. No levy or royalty was removed at the meeting. Instead, Mr Mavunde directed the Mining Commission, small-scale mining representatives and regional authorities to examine the system and recommend ways of protecting Government revenue while making the treatment of payments clearer. The minister said the Government wanted to understand the practical concerns raised by miners before deciding whether administrative procedures needed to be changed. The review will focus partly on how mineral ownership changes along the production chain. Mining Commission officials explained that when a small-scale miner sells ore to another business, that transaction transfers ownership of the material. The buyer then processes the ore and may enter another transaction when the recovered mineral is sold, with separate statutory obligations potentially arising. Small-scale miners, however, asked the Government to examine cases where ownership does not change. Under such arrangements, a miner may extract mineral-bearing material, transport it for crushing or further processing and eventually sell the recovered gold. Their concern is that receipts issued earlier in the process may not always provide officials at subsequent stages with a clear record of payments already made in relation to the same material. Mr Mavunde consequently directed the technical team to examine whether mineral consignments can be more closely linked to their source, movement documents and payment records. One option under consideration is to identify the originating mining licence or production area and maintain a clearer connection between mineral consignments and receipts issued during transportation and processing. The technical review will also consider whether payments already made in relation to the same material can be recognised when subsequent liabilities are assessed. Mr Mavunde said the Government would first consider the legal, operational and revenue implications before making any changes. “The review must safeguard every legitimate Government entitlement while ensuring compliant small-scale mining businesses are not subjected to unnecessary administrative costs,” he said. Small-scale miners also raised concerns about moving ore between mining and processing sites, particularly where suitable treatment facilities are unavailable within a licensed area. Procedures governing the transportation of carbon used for elution were also submitted for consideration. The issue is significant given the growing contribution of small-scale mining to Tanzania’s mineral economy. Mr Mavunde said the subsector accounted for about 40 per cent of the Sh1.393 trillion collected from the mining sector during the 2025/26 financial year. The minister said the mining sector collected Sh411 billion in the first quarter of 2026/27, against a target of about Sh351 billion, equivalent to 117 per cent of the target. He said the Government was also directing 10 per cent of mining-sector collections to mineral exploration to support the identification of commercially viable deposits. FEMATA president John Bina supported the technical review, saying the financial implications should be established before any adjustments are made. Mr Mavunde said the joint team would examine charging points, receipts, mineral movements and transaction records before submitting recommendations to the Government. The review is expected to determine whether stronger traceability can provide a clearer record from the mining licence through processing to sale, while ensuring that legitimate Government revenue is protected.
MBUNGE wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Winnie Odinga, Jumamosi, alitawazwa kwa njia ya ishara na baadhi ya wazee wa jamii ya Waluo kuwa mrithi wa kisiasa wa babake marehemu Raila Odinga. Hafla hiyo ilifanyika wakati wa ibada ya kuwakumbuka wazee na wapiganaji wa zamani katika shamba la Opoda, Bondo, Kaunti ya Siaya, ambapo wazee walitumia mila kumhimiza Bi Odinga kuchukua nafasi kubwa zaidi katika siasa. Mama yake, Ida Odinga, dada yake Rosemary Odinga, wajumbe wa Baraza la Wazee wa Luo pamoja na jumla ya familia ya jumla walihudhuria hafla hiyo. Hata hivyo, kaka yake Raila Junior hakuhudhuria, huku mama yake akisema alikuwa na shughuli nyingine. “Viongozi wamesema dunia inakutaka na hawajui mustakabali wako. Ndiyo maana leo tunakutawaza uende ukapigane huko nje na kuchukua nafasi ya babako. Nyabondo (msichana kutoka Bondo), sasa wewe ndiye tunayekutegemea,” akasema Rose Otumba, mwakilishi wa kike katika Baraza la Wazee wa Luo Siaya. Bi Otumba kisha alimvisha kofia ya kitamaduni kichwani mwa Winnie, kwa njia ya mfano kumtawaza kuwa mrithi wa babake kisiasa. Hafla hiyo ilifuatiwa na nyimbo za kitamaduni za Sigweya zilizoongozwa na Jotham Ajiki, katibu wa mipango wa Baraza la Wazee wa Luo, kabla ya umati kuanza kuimba na kucheza. “Nyakawuor ana uwezo na anafaa kuwa kiongozi. Wacha nione kwa kuinua mikono wale wanaomuunga mkono,” akasema Bw Ajiki, huku umati ukimjibu kwa shangwe. Vijana waliohudhuria pia walimtaka Winnie achukue nafasi ya babake, wakisema chama kinahitaji uongozi wa kizazi kipya ili kuleta nguvu mpya. “Ida, tafadhali tupe Winnie atuongoze katika chama hiki. Tunajua Oburu ndiye anayeongoza chama kwa sasa lakini umri wake unaenda. Tupe Winnie ambaye bado ni mchanga na mwenye nguvu atuongoze,” akasema Daisy Okello Achieng, rais wa wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Jaramogi Oginga Odinga. Uungwaji huo wa wazi unaongeza kasi ya safari ya kisiasa ya Winnie. Machi, wajumbe wa ODM Nairobi walimuunga mkono kuwa naibu kiongozi wa chama. Hafla ya Jumamosi pia ilionyesha wazi tofauti ambazo huenda zimeibuka kati ya Winnie na kakake Raila Jnr. Oktoba mwaka jana, Raila Junior alichukua rasmi uongozi wa familia ya Odinga katika hafla ya kitamaduni iliyofanyika nyumbani kwao Bondo. Hafla hiyo iliongozwa na amu yake Dkt Oburu Oginga na ilihusu kukabidhiwa majukumu ya familia baada ya mazishi ya Raila. Hata hivyo, Dkt Oburu alisema wakati huo kwamba hafla hiyo ilikuwa ya kukabidhi uongozi wa familia na baraka, wala haikuhusu urithi wa kisiasa. Winnie alisema alikuwa amejitenga na shughuli za kisiasa kwa muda ili kuomboleza babake, lakini sasa kipindi hicho kimekwisha. “Watu wengi walikuwa wakiuliza Winnie ameenda wapi, lakini niliamua kuchukua muda kumuomboleza Jakom. Niliona wanajeshi wa Raila wakiwa na huzuni baada ya kifo chake na hawakutaka tena kupigana.” Ndiyo maana nilikaa kimya kwa mwaka mmoja kuomboleza, lakini sasa wakati huo umepita na ni wakati wa kusonga mbele,” akasema. Kauli yake ilionekana kuashiria mwanzo wa awamu mpya ya shughuli zake za kisiasa, ingawa alionya dhidi ya kulazimisha suala la urithi, akisema uongozi hauwezi kuchukuliwa kwa nguvu.
UBABE wa kudhibiti ODM umeanza kuchipuka huku viongozi wakitumia kutoonekana kwa kinara wa chama hicho Seneta Oburu Oginga katika shughuli za umma, kujijengea ushawishi ndani ya chama. Waziri wa Vyama vya Ushirika Wycliffe Oparanya, Gavana wa Kisii Simba Arati na Mwenyekiti wa ODM Gladys Wanga ni miongoni mwa viongozi ambao wamekuwa mstari wa mbele kuendesha shughuli za chama wakati Dkt Oginga bado anaugua. Mwishoni mwa wiki, wabunge Raphael Wanjala (Budalang’i), Christopher Aseka (Khwisero) na Bernard Shinali (Ikolomani), pamoja na Msemaji wa Serikali Charles Owino, walimtaka Bw Oparanya kusawazisha majukumu yake ya uwaziri na yale ya chama ili kumsaidia Dkt Oginga kuendesha ODM. “Tunataka uwe na afisi mbili, moja ya ODM ambako Dkt Oburu anafanya kazi na nyingine katika wizara yako. Tunataka utenge muda na umsaidie Dkt Oginga kufanya kazi. Tunataka utenge muda ili asilemewe na kazi. Akilemewa, tunaweza kumpoteza kwa urahisi,” akasema Bw Wanjala. Alikuwa akizungumza nyumbani kwa Bw Oparanya wakati wa ziara ya ukoo wa Kawuor, ambao ulikuwa ukoo wa marehemu Raila Odinga. Mwanawe Raila na mgombea ubunge wa Kibra, Raila Junior pamoja na mgombea ubunge wa Bondo Jaoko Oburu, mwanawe Dkt Oginga, walihudhuria hafla hiyo. Bw Wanjala pia alimtaka Bw Oparanya kuunganisha jamii za Waluo na Waluhya baada ya kifo cha Bw Raila, wakati jamii hizo zikijiweka tayari kisiasa kuelekea kwa uchaguzi mkuu wa 2027 ambapo Rais William Ruto anawania muhula wa pili, na uchaguzi wa 2032. “Tafadhali kuwa karibu sana na Oburu ili kumsaidia kiongozi wetu ambaye bado tunamhitaji licha ya umri wake mkubwa. Una uzoefu, umekuwa naibu kiongozi wa chama kwa muda mrefu na watu wako salama ukiwa karibu na Oburu,” akaongeza Bw Wanjala. Bw Owino pia aliunga pendekezo hilo, akimtaja Oparanya kuwa mwanasiasa mwenye uzoefu mkubwa zaidi katika eneo hilo na kusema uhusiano wake wa karibu na Bw Odinga kwa zaidi ya miaka 25 unamweka katika nafasi nzuri ya kumsaidia Dkt Oginga. “Umekuwa naibu kiongozi wetu wa chama kwa muda mrefu na umeachia nafasi hiyo kwa sababu wewe ni waziri, kwa hivyo usisahau kwamba bado una nafasi huko. Muunge mkono mlezi wa chama chetu. Msaidie kwa sababu hujui kitakachotokea kesho,” akasema Bw Owino. “Lazima uwe karibu sana na Dkt Oginga ili ufanye sehemu kubwa ya kazi yake. Anaendelea kuzeeka, kwa hivyo mfanyie kazi zaidi. Umetushika na sisi tutakushika mkono kwa sababu hakuna mtu mwenye cheo cha juu kukuliko katika eneo hili.” “Najua sisi watu wa Nyanza tuko tayari kuachilia nafasi yoyote katika chama na hakuna kinachotuzuia kumuunga mtu yeyote kutoka Magharibi kwa sababu mlimuunga Raila kwa miaka mingi,” akaongeza . Bw Shinali naye alisema Oparanya yuko katika nafasi nzuri zaidi ya kuwaunganisha viongozi kutoka Magharibi na Nyanza na anafaa kushirikishwa katika kuendesha shughuli za ODM. “Oparanya ndiye kiongozi mwenye uzoefu mkubwa zaidi kutoka eneo hili na ndiye atakayetuweka pamoja sisi sote kutoka Magharibi na Nyanza. Oparanya ndiye anayetuunganisha na kushikilia ODM Magharibi. Tumeona watu wa Nyanza wako pamoja nasi na wako tayari kumuunga mkono Oparanya kama mmoja wetu,” akasema Bw Shinali. Wakati Bw Oparanya akiendelea kuimarisha ngome yake, huku akitajwa kuwa miongoni mwa wanaoweza kuwa mgombea mwenza wa Rais Ruto, Bw Arati na Bi Wanga pia wamekuwa mstari wa mbele katika shughuli za ODM. Ijumaa iliyopita, Bi Wanga ambaye pia ni Gavana wa Homa Bay, aliongoza maelfu ya wafuasi wa ODM katika bustani ya Uhuru, Nairobi, katika hafla ya kuwasha mishumaa ya kumkumbuka Bw Odinga. Umati huo uliwakumbusha wengi nyakati na idadi kubwa ya watu waliohudhuria mikutano ya kisiasa ambayo Raila aliandaa katika safari yake ya kisiasa. Wiki mbili zilizopita, Bi Wanga alifanya ziara ya siku tatu katika Kajiado, Narok Kusini na Narok Kaskazini, ambako alihimiza ODM kuimarisha uungwaji mkono wake miongoni mwa jamii ya Maa. Bi Wanga anazidi kuonekana kama sura ya ODM Nyanza, huku Gavana wa Siaya James Orengo akiegemea mrengo wa Linda Mwananchi na akiwa katika harakati za kuunda chama chake. Gavana wa Kisumu Anyang’ Nyong’o, mwanasiasa mwengine mkongwe wa Nyanza, pia hashiriki sana katika shughuli za ODM, Bi Wanga akisalia sura ya chama Luo Nyanza. Prof Nyong’o aliwahi kuwa kiongozi wa ODM wakati Raila alikuwa akiwania uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika mapema mwaka jana. Bw Arati, kwa upande wake, amekuwa akiongoza shughuli za ODM wakati Dkt Oginga hayupo, hali ambayo imezua hisia kwamba sasa ni wakati wa Luo Nyanza kulipa fadhila kwa jamii ya Gusii kwa uungwaji mkono iliompa Bw Odinga kwa miaka mingi. Mji wa Kisii ulikuwa miongoni mwa maeneo yaliyoshuhudia umati mkubwa wa wafuasi wa ODM wakati wa hafla ya kuwasha mishumaa, iliyoandaliwa kwa usaidizi wa gavana huyo anayehudumu muhula wa kwanza. Bw Arati pia amekuwa akishinikiza ODM kuingia katika muungano wa kisiasa utakaohakikisha chama hicho kinapata nafasi sawa na UDA.
SIASA za vibaraka wanaodaiwa kupenyezwa na serikali zimezua hofu na kutoaminiana katika upinzani na kutishia umoja wao kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Viongozi wa upinzani sasa wana hofu kuwa serikali inaweza kupenyeza watu wake ndani ya vyama vya upinzani ili kuvuja mikakati, kuchochea migawanyiko na kuunga mkono wagombeaji wengi wa urais, kwa lengo la kumsaidia Rais William Ruto kushinda muhula wa pili. Kiongozi wa Democracy for the Citizens Party (DCP) Rigathi Gachagua tayari amedai mmoja wa viongozi wakuu wa upinzani yuko mbioni kujiunga na Rais Ruto. “Ninataka kutoa unabii leo, si kwa sababu mimi ni nabii bali kutokana na uzoefu, kuona mbali na kuelewa siasa za Kenya. Mgombeaji mmoja wa urais atatangazwa; mtu mmoja ataondoka. Mtu huyo ataondoka mwenyewe,” akasema Bw Gachagua. Akiwahutubia viongozi wa kidini jijini Boston, Amerika, aliyekuwa Naibu Rais pia alidai kuwa kuna mpango wa kupenyeza fuko katika upinzani ili kuzuia juhudi za kuunda muungano mmoja. Ingawa hakumtaja yeyote, chama cha Wiper Patriotic Front cha Kalonzo Musyoka kililazimika kukanusha madai ya mazungumzo ya siri na serikali ya Kenya Kwanza. Bw Musyoka aliripotiwa kukutana kwa siri na mwanasiasa mkongwe Johnson Muthama, mshirika wa karibu wa Rais Ruto. Mwenyekiti wa kitaifa wa Wiper Jamlek Kamau alithibitisha mkutano huo lakini akasema haukuwa wa kumshawishi Bw Musyoka kujiunga na serikali. “Ndiye nilianzisha mazungumzo na Johnstone Muthama. Hakuna wakati amekutana na kiongozi wetu wa chama kumshawishi kujiunga na serikali,” akasema Bw Kamau. Baadaye Bw Musyoka aliwaonya wanasiasa wa upinzani dhidi ya kuwa fuko wa Rais Ruto. “Ikiwa mmoja wetu atakuwa fuko wa Kasongo, atapata madhara kama ya Loti wa Biblia,” akasema. Tuhuma kama hizo pia zimekumba vuguvugu la Linda Mwananchi linalohusishwa na Seneta wa Nairobi, Edwin Sifuna. Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino, Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya, Mbunge wa Saboti Caleb Amisi na Seneta wa Kakamega Boni Khalwale wamekuwa na vyama vyao, huku Gavana wa Siaya James Orengo akisema anapanga kusajili chama kipya. Bw Natembeya na Bw Amisi wamekuwa wakivamiana kuhusu kuvuruga azma ya Bw Sifuna ya kuwania urais. Bw Amisi, kiongozi wa People’s Renaissance Movement, amesema chama chake kiliundwa kuimarisha Linda Mwananchi lakini baadaye kikaitwa fuko. “Huwa na wasiwasi kwamba baadhi ya walio karibu naye wanataka jina lake zaidi kuliko wanavyomtakia mema. Tazama vyama vya kisiasa vilivyoibuka tangu wakati huo,” akasema. Naibu kiongozi wa Jubilee Jeremiah Kioni alisema kushukiwa huko kunatumiwa na baadhi ya wanasiasa kwa maslahi ya binafsi. “Ni wale walio katika upinzani wanaoitana fuko. Hii haisaidii kuendeleza ajenda ya upinzani bali maslahi binafsi kwa kumchafua mwengine,” akasema. Mbunge wa Gatanga Edward Muriu, hata hivyo, alidai serikali ya Rais Ruto inatumia mbinu hizi kudhoofisha upinzani baada ya kupoteza uungwaji mkono katika Mlima Kenya. Mchanganuzi wa masuala ya kisiasa Profesa David Monda alisema kutoaminiana katika upinzani kutaongezeka kadri uchaguzi unavyokaribia. “Kwa hakika upinzani iko mbali kuwa na umoja. Ni ndoa ya manufaa kati ya wanasiasa wanaopinga serikali lakini wamefungwa na kutoaminiana na sintofahamu,” akasema. Aliongeza kuwa uwezo wa Rais Ruto kama kiongozi aliye mamlakani unampa nafasi nzuri ya kutumia migawanyiko ya upinzani kwa manufaa yake.
MWENDESHAJI wa bodaboda ambaye jina lake limefichwa, Paul*, amewaambia wachunguzi wa mauaji jinsi alivyohusika bila kujua katika tukio la kuuawa kwa wakili Kyalo Mbobu mnamo Septemba 9, 2025. Paul (Si jina lake kamili) amerekodi taarifa tatu kwa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), akisema alikuwa rafiki wa afisa polisi Julius Cheruiyot ambaye alimwajiri kumpeleka sehemu mbalimbali kwa malipo ya Sh3,000. Kulingana na taarifa yake, Cheruiyot alipanga mkutano na Paul na polisi mwengine katika mkahawa wa Pangani, Nairobi, asubuhi ya Septemba 10, 2025. Polisi huyo aliyetajwa kama “Afande Sang” anaaminika kuwa Inspekta Kenneth Kipkemoi Sang, ambaye ni mshukiwa mkuu katika mauaji ya Mbobu na mtafiti Victoria Mutiso. Paul alisema baadaye alimchukua Cheruiyot na kuelekea Langata Road kabla ya kusimama karibu na Galleria Mall. Baada ya saa 11.30 jioni, Cheruiyot alidaiwa kumwelekeza aingie Magadi Road. Takriban mita 50 kutoka eneo ambako Mbobu alipigwa risasi, Cheruiyot alidaiwa kumwambia asimame huku injini ya pikipiki ikiendelea kuwaka. Paul alisema hakumwona Mbobu akipigwa risasi lakini alisikia milio ya risasi kadhaa. Cheruiyot alikimbia hadi kwa pikipiki akihema na kumwamuru aondoke kwa kasi. Walirejea Pangani baada ya saa 12 jioni, ambapo Cheruiyot alidaiwa kumpa Paul salio la Sh2,000 na kumwonya asizungumzie yaliyotokea. Paul alisema alihofia kukamatwa na akabadilisha laini ya simu na kuhamia South B. Cheruiyot na Paul walikamatwa jijini Nairobi Septemba 24. Pikipiki iliyodaiwa kutumiwa katika tukio hilo pia ilipatikana. Wachunguzi wanamtuhumu Sang kuhusika katika mauaji hayo pamoja na ya Mutiso. Anaaminika kukimbilia Tanzania. Wachunguzi pia wanadai mauaji hayo yalihusishwa na mzozo wa shamba la ekari 21 Mlolongo, Kaunti ya Machakos
ASUBUHI kabla ya safari yake ya mwisho, Scholastica Ochieng alimwambia kasisi wake, Padri Patrick Maingi, kuwa kukamilisha sala za Novena kulikuwa kumempa amani ya moyoni. Baadaye siku hiyo, alijiunga na waumini wengine wa Kanisa Katoliki la St Mathias Mulumba, Mikindani, Mombasa, waliokuwa wakijiandaa kusafiri hadi Subukia, Kaunti ya Nakuru, kwa Siku ya Kitaifa ya Maombi. Scholastica na mwenzake Ann Mwanthi pia walikuwa wamelipa zaka zao siku chache kabla ya safari. “Hatuitaki kuenda mbele za Mungu tukiwa na madeni. Tunataka kumaliza madeni yetu ili tukienda, twende tukiwa na dhamira safi,” waliambia Padri Maingi. Hawakujua hayo yangekuwa miongoni mwa mazungumzo yao ya mwisho. Saa tisa alasiri Ijumaa, Padri Maingi aliwaaga mahujaji 17 wakipanda magari mawili kuelekea Subukia. “Walikuwa na furaha sana na walikuwa wakitarajia safari njema,” akasema. Miongoni mwao alikuwa Veronica Ngandi, ambaye alikuwa akijiandaa kufunga ndoa baada ya familia yake kufanya mazungumzo ya mahari Kitui. Padri Maingi alisema Veronica alipanga kuanza maandalizi ya mwisho ya harusi baada ya kurejea kutoka kwa safari hiyo. “Alikuwa anatazamia harusi yake. Aliniambia baada ya hija angeanza maandalizi lakini sasa harusi yake itakuwa mbinguni,” akasema. Sarapia, kutoka Taita Taveta, pia alikuwa na furaha kwa sababu alikuwa hajawahi kusafiri mbali na Voi. Hata hivyo, saa chache baadaye, magari hayo yalihusika katika ajali Salama kwenye barabara ya Nairobi-Mombasa na mahujaji wote 17 wakafariki. Padri Maingi alijulishwa kuhusu ajali hiyo na afisa wa trafiki John Mrei, aliyewatambua waathiriwa kutokana na kofia walizovaa zilizokuwa na jina la kanisa. Miili hiyo ilipelekwa Hospitali ya Sultan Hamud, Makueni, ambako ndugu walitambua waathiriwa 14 wanawake na wanaume watatu. Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Dayosisi ya Mombasa Dominic Kimengich alitaka barabara ya Nairobi-Mombasa ibadilishwe na ijengwe kuwa ya njia mbili, akisema eneo la Salama limekuwa hatari kwa wasafiri. Gavana wa Makueni Mutula Kilonzo Junior pia alitaka serikali ichukue hatua za haraka kuzuia vifo zaidi katika eneo hilo hatari.
SENETA WA Nairobi Edwin Sifuna jana alizindua rasmi chama cha The Equitable Party (TEP) atakachotumia katika uchaguzi mkuu ujao baada ya juhudi za kusajili Linda Mwananchi Movement (LMM) kukumbwa na vikwazo vingi. Katika hatua kubwa ya kuimarisha azma yake ya kuwania urais, Bw Sifuna alichukua uongozi wa chama hicho akilenga kubadilisha jina lake ili kifahamike kama Linda Mwananchi Movement. Afisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa (ORPP) mnamo Alhamisi iliidhinisha kuhifadhi jina Linda Mwananchi Movement kwa siku 90, kwa agizo la Jopo la Kutatua Migogoro ya Vyama vya Kisiasa. Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Gavana wa Siaya James Orengo, Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino, Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya, Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi na Seneta wa Kisii Richard Onyonka. TEP ilianzishwa mnamo 2022 na Mkenya anayeishi Amerika, Dkt Gilbert Marava Shanga. Viongozi waanzilishi walijiondoa baada ya mazungumzo baina yao na mrengo wa Linda Mwananchi, na kumkabidhi Bw Sifuna uongozi wa chama hicho. Uzinduzi huo ulifanyika wiki moja tu baada ya Linda Mwananchi kwa kauli moja kumwidhinisha Seneta Sifuna kuwa kiongozi wake na mgombea wake wa urais katika uchaguzi ujao. Katika hotuba yake, Bw Sifuna alizungumzia changamoto walizokumbana nazo katika juhudi za kusajili Linda Mwananchi pamoja na kufukuzwa kwao kutoka ODM. Alishutumu ORPP akisema imekuwa ikitumiwa kama chombo cha kuzuia vyama vya upinzani kufanya shughuli zao. “Tunazindua chama chetu leo kwa sababu nyumba ambayo Baba alituachia ilitekwa,” akasema Bw Sifuna, akirejelea marehemu Raila Odinga. Bw Sifuna alisema iwapo serikali itaendelea kuzuia kubadilishwa kwa jina la chama hicho, wataendelea kutumia jina la TEP hadi uchaguzi wa 2027. “Chama kitaendelea na utambulisho wake wa sasa hadi kura zipigwe 2027. Ikiwa wataendelea kuweka vikwazo kama walivyofanya awali, tutaendelea na safari yetu kwa sababu sasa tuna chama,” akaongeza. Alisema chama hicho kitalenga kurejesha imani ya Wakenya katika Katiba na utawala wa sheria, huku kikihakikisha makundi yote yanatambuliwa na kupewa nafasi sawa katika uongozi na maendeleo ya nchi. “Siwezi pekee yangu kuunda vuguvugu. Vuguvugu hili ni lenu nyote mliochagua njia ya mabadiliko na ambao mapambano na kujitolea kwenu kumetengeneza safari hii,” akasema. Bw Sifuna pia alieleza baadhi ya masuala ambayo anatarajia kushughulikia iwapo atapata nafasi ya kuongoza nchi, akitaja mzigo wa kodi unaowakabili wafanyabiashara wadogo na gharama ya juu ya kufanya biashara. Seneta huyo amekuwa akipata uungwaji mkono mkubwa katika kura za maoni, huku utafiti wa Tifa wa mnamo Julai ukionyesha kuwa angepata asilimia 15 ya uungwaji kitaifa iwapo angewania urais. Hii ilimweka nyuma ya Rais William Ruto pekee, ambaye alikuwa na asilimia 24. Bw Sifuna pia aliwaacha nyuma viongozi wengine wa upinzani, akiwemo kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka. Wakati wa uzinduzi huo, Sifuna aliwataka Wakenya wenye msimamo kama wake kujiunga na vuguvugu hilo. “Huu ni mwito wa umoja, kufanya kazi pamoja, kukua pamoja na kujenga vuguvugu litakalorejesha matumaini tuliyokuwa nayo mnamo 2010 tulipopitisha Katiba yetu. Vuguvugu hili linaanza na jambo moja rahisi; lazima serikali iwafanyie kazi wananchi,” alisema. Mbunge wa Suba Kusini, Caroli Omondi, ambaye ni msemaji wa Linda Mwananchi, alisema mipango inaendelea kubadilisha jina la chama hicho ili liakisi sura ya viongozi na wanachama wake. Gavana Orengo naye alisema yuko tayari kuunga mkono mpango wowote wa kuzuia Rais Ruto kuchaguliwa tena. “Uko mahali panapofaa, uko katika vuguvugu linalofaa na una uongozi unaofaa wa kukupeleka katika nchi ya ahadi. Tunawajibika kwa wananchi wa Kenya,” akasema Bw Orengo. Seneta Osotsi alisema walifanikiwa licha ya kile alichodai kuwa ni juhudi za serikali kuwazuia kupata chama. “Tuna jina letu, mliona walivyotutesa lakini tulienda kortini na tukawashinda,” alisema. Gavana Natembeya alisema Bw Sifuna na wenzake wanafaa kuingia katika mazungumzo na viongozi wengine wa upinzani na kukubali mgombea mmoja wa urais, akisema seneta huyo wa Nairobi ana uwezo wa kumkabili Rais Ruto. Bw Owino aliwataka viongozi hao kudumisha umoja na kuwashtumu baadhi ya viongozi wa ODM kwa kuwafukuza baada ya kutaka mabadiliko. Pia aliwataka viongozi hao kutumia uzoefu wa Gavana Orengo na kumteua kuwa mmoja wa washauri wakuu wa vuguvugu hilo.
GEITA: WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba ameitaka Wizara ya Madini kuendeleza usimamizi thabiti wa sekta ya madini ili kuongeza tija kuelekea dira ya maendeleo ya taifa 2050. Dk Mwigulu ametoa maelekezo hayo wakati akifunga Maonyesho ya Tisa ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yaliyofanyika viwanja vya Dk Samia Suluhu Hassani Manispaa ya Geita.…
Yayi praised Tinubu for projects and federal support to Ogun State, saying the president’s administration had delivered significant benefits to the state.
MOROGORO. Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew, amesema ujenzi wa Bwawa la Kidunda mkoani Morogoro, unaogharimu Sh bilioni 336, umefikia asilimia 70 ya utekelezaji. Mhandisi Kundo aliyasema hayo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo wa kimkakati, unaotekelezwa katika eneo la Ngerengere mkoani humo. Alisema kukamilika kwa bwawa hilo kutasaidia kumaliza…
Kimaiyo arap Sego aliingia katika siasa za kitaifa akiwa mwanasheria kijana mwenye matumaini makubwa, akampiku waziri Henry Kosgey katika kura za Kanu na kutwaa wadhifa wa Waziri wa Biashara. Lakini safari yake ya kisiasa ilikatizwa ghafla baada ya miezi tisa. Mnamo Januari 1988, jina la Kimaiyo arap Sego halikuwa maarufu sana nje ya Nandi. Lakini ndani ya muda mfupi, mwanasheria huyo kutoka Kapsabet alikuwa ameingia katika siasa za kitaifa kwa njia ambayo wachache walitarajia. Sego alizaliwa Septemba 1952 eneo la Kaptendon, Lessos, Nandi, katika familia ya Sylvester na Felister Sego. Baba yake alikuwa mwanajeshi wa Kings African Rifles (KAR) wakati wa Vita vya Pili vya Dunia kabla ya kustaafu na kuanza ukulima. Baada ya masomo ya msingi Kalibwani, Sego alijiunga na Kapsabet High School kwa masomo ya Ordinary Level, kisha St Mary’s Yala kwa Advanced Level. Baadaye alisomea sheria katika Chuo Kikuu cha Nairobi.Alifanya mafunzo ya uwakili katika kampuni ya Amata & Company Advocates mjini Eldoret na kufanya kazi hapo kwa takriban miaka miwili kabla ya kuanzisha kampuni yake ya uwakili mjini Kapsabet. Lakini mwaka 1983, mwanasheria huyo aliamua kuingia kwenye siasa kwa kumenyana na mwanasiasa aliyekuwa na nguvu, Henry Kosgey, katika uchaguzi wa ubunge wa Tinderet.Ilikuwa changamoto ngumu. Kosgey alipata kura 17,797 dhidi ya 1,045 za Sego.Hata hivyo, miaka mitano baadaye, mambo yalibadilika kabisa.Katika kura za mchujo za Kanu mwaka wa 1988, Sego alipata kura 14,499 huku Kosgey akipata 6,151. Kwa mujibu wa kanuni za chama wakati huo, mgombea aliyepata zaidi ya asilimia 70 ya kura za mchujo aliweza kuingia Bunge moja kwa moja.Sego akawa mbunge mpya wa Tinderet.Ushindi huo ulimfungulia mlango wa Baraza la Mawaziri. Aliteuliwa kuwa Waziri wa Biashara akiwa na umri wa miaka 32, umri ambao Kosgey alikuwa nao alipoingia serikalini.Lakini hadithi yake nzuri haikudumu.Jarida la The Weekly Review la Aprili 1989 lilieleza kuanguka kwake kisiasa kama “kupanda kwa kasi na kuanguka ghafla”, likisema matatizo yake yalianza baada ya kutofautiana na watu waliomsaidia kupata nafasi hiyo. Sego alikuwa mwanasiasa mkuu zaidi kutoka Nandi baada ya kuingia Bunge, lakini jarida hilo lilisema huenda alikadiria kupita kiasi nguvu zake za kisiasa na kupuuza ushawishi wa Mark arap Too, ambaye alikuwa akionekana kuwa mlinzi mkuu wa kisiasa Nandi. Ndani ya miezi tisa, Sego aliondolewa katika Baraza la Mawaziri na nafasi yake kuchukuliwa na mbunge mwingine wa Nandi, John Cheruiyot.Baadaye tawi la Kanu Nandi lilimlaumu kwa kutoshiriki harambee, kupuuza mikutano ya viongozi wa chama, kutoshiriki uchaguzi wa chama na kutofuatana na Rais Daniel arap Moi katika ziara zake Nandi. Sego hakujibu madai hayo kwa kuomba msamaha, jambo lililozidisha mvutano kati yake na viongozi wa chama.Wakati mmoja alikosana hadharani na Too, akimlaumu kwa kuwasaidia wapinzani wake katika juhudi za kumvua ubunge. Too naye alijibu kwa kusema malalamiko ya Sego yalikuwa “mateke ya mwisho ya farasi anayekufa”. Licha ya misukosuko hiyo, Sego aliacha alama katika Wizara ya Biashara. Alisimamia marekebisho ya Trade Licensing Act yaliyolenga kukuza viwanda vya humu nchini.Pia aliwakilisha Kenya katika mazungumzo ya biashara ya Uruguay Round chini ya GATT. Siasa za vyama vingi vilipoanza miaka ya 1990, Sego aliondoka Kanu na kujiunga na Democratic Party ya Mwai Kibaki. Uamuzi huo haukupokelewa vyema Nandi, ngome ya Kanu wakati huo.Alipokuwa akipeleka karatasi zake za uteuzi kwa uchaguzi wa 1992, alishambuliwa na umati. Alishindwa uchaguzini na baadaye akapinga ushindi wa Kosgey kama mbunge waTinderet, lakini akapoteza kesi hiyo pia.Sego alitoweka kwa muda kutoka siasa za mstari wa mbele hadi mwaka 2003 alipoingia katika mchakato wa mageuzi ya katiba kama mjumbe wa Kongamano la Kitaifa. Mwaka 2005, aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa National Anti-Corruption Campaign Steering Committee, taasisi iliyoundwa kuhamasisha umma kuhusu vita dhidi ya ufisadi.Alijiuzulu mwaka 2014 na kurejea katika taaluma yake ya uwakili.Safari ya Sego inabaki kuwa simulizi ya mwanasiasa aliyeingia Bunge kwa ushindi mkubwa, akapanda haraka hadi Baraza la Mawaziri, lakini akakutana mapema na upande mgumu wa siasa za wakati huo.
Mamdani praised and paid tribute to Nigeria’s extraordinary cultural influence across Africa and internationally. The Uganda-born mayor recalled growing up listening to Nigerian music and said he was excited to see some of the country’s stars perform.
Rais mstaafu Uhuru Kenyatta amemshambulia mrithi wake Rais William Ruto, akimtaka aache kumlaumu na badala yake kushughulikia matatizo yanayowakabili Wakenya. Akizungumza Jumamosi katika Shule ya Msingi ya Mugumo, Kaunti ya Kirinyaga, wakati wa mazishi ya Mwalimu Jackson Karua, babake kiongozi wa chama cha People's Liberation Party (PLP) Martha Karua, Bw Kenyatta alisema hana mpango wa kuwania wadhifa wowote wa kisiasa na hivyo Rais Ruto anapaswa kuelekeza nguvu zake katika kuhudumia wananchi. Uhuru alisema amekuwa akitajwa kwa majina mbalimbali na viongozi serikalini lakini hajali mashambulizi hayo ya kisiasa. “Ananiita mfadhili, kiongozi wa waasi na mlevi, lakini sijali. Anapoteza muda wake akipambana nami. Nilihudumu kwa muda wangu na ninamshukuru Mungu kwa hilo. Mimi sio mshindani wake,” alisema huku akishangiliwa na waombolezaji. Rais huyo wa mstaafu aliwakumbusha wakazi wa Mlima Kenya kwamba aliwaonya mwaka wa 2022 dhidi ya kumuunga mkono Dkt Ruto lakini walipuuzilia mbali ushauri wake. “Niliwaambia watu wetu waunge mkono Raila Odinga na Martha Karua ambao wangeweza kubadilisha nchi na kufanya kazi nzuri, lakini hawakunisikiza. Sasa wanalalamika,” alisema. Aliwataka wakazi wa eneo hilo kutorudia kosa hilo katika uchaguzi mkuu wa 2027. “Kukosea ni kawaida, lakini kurudia kosa lile lile ni jambo baya. Je, mko tayari kufanya kosa hilo kwa mara ya pili?” alihoji kwa lugha ya Gikuyu. Uhuru alimtaka Rais Ruto kusubiri uchaguzi mkuu ujao badala ya kuendelea kumlaumu kwa changamoto zinazokumba serikali yake. Alisema baadhi ya viongozi wamekuwa wakitumia jina lake kuficha mapungufu yao katika uongozi. Katika hafla hiyo, viongozi wa upinzani waliungana na kumtaka Rais Ruto kuacha kumshambulia Uhuru. Pia walisisitiza umuhimu wa umoja miongoni mwa vyama vya upinzani kabla ya uchaguzi wa 2027. Mwakilishi wa Wanawake wa Kirinyaga Njeri Maina aliwataka viongozi hao kuweka kando maslahi yao binafsi na kukubaliana kuhusu mgombea mmoja wa urais. Kauli hiyo iliungwa mkono na Uhuru ambaye alimwita tena jukwaani ili arudie wito wake. Miongoni mwa viongozi waliohudhuria mazishi hayo ni Kalonzo Musyoka, Fred Matiang’i, Edwin Sifuna, Justin Muturi, Ndindi Nyoro, Eugene Wamalwa na Martha Karua. Walimshutumu Rais Ruto kwa kile walichokitaja kuwa kuongezeka kwa ufisadi na kuzorota kwa hali ya uchumi. Bw Muturi alisema Rais Ruto anatambua kuwa anakabiliwa na upinzani mkubwa kuelekea uchaguzi ujao. Kwa upande wake, Martha Karua alisema muungano wa upinzani una azma ya kuleta mabadiliko ya uongozi nchini na kuwahimiza Wakenya kuwa wavumilivu wakisubiri hatua zinazofuata za kisiasa. Kauli za Uhuru zinajiri huku siasa za uchaguzi wa 2027 zikianza kushika kasi, na zinaonekana kuwa ishara ya kuongezeka kwa juhudi za upinzani kuunda muungano mmoja wa kumenyana na Rais Ruto katika uchaguzi huo.
By Rotimi Ojomoyela ADO-EKITI — Senate Leader, Senator Opeyemi Bamidele, has said sustained investment in basic education is critical to producing well-rounded citizens, professionals and responsible leaders for national development. Bamidele spoke in Iyin-Ekiti during the inauguration of the renovated Government Science College, Iyin-Ekiti, which he renovated at a cost of over N200 million. He […]
By Esther Onyegbula For the Ugwu family, identifying Chinyere Susan Rosemary was a moment they never imagined they would experience.At a mortuary in Enugu, surrounded by the cold finality of death and in the presence of the suspect and three police officers investigating the case, the family searched for something familiar in a body that […]
By Ndahi Marama North East Governors Forum, NEGF, yesterday, raised the alarm over what it described as the seeming neglect of the Mambilla Hydro power plant and called on Federal Government to expedite action on the completion and take-off of the plant.Rising from its 13th Regular meeting in Maiduguri, the Borno State capital, NEGF, in […]
Mwaka mmoja baada ya kifo cha Raila Odinga, Chama cha Orange Democratic Movement (ODM) kinamkumbuka huku kikikabiliwa na swali ambalo halijapata jibu la wazi hadi sasa. Swali hilo limezidi kuwa muhimu chama hicho kikijiandaa kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha Raila mnamo Oktoba 15, 2026, huku makundi mbalimbali ya kisiasa yakitoa tafsiri tofauti kuhusu urithi wake wa kisiasa. ODM, chini ya uongozi wa kaka yake Raila, Oburu Oginga, imeandaa shughuli za mwezi mzima chini ya kaulimbiu ‘Mwezi wa Baba’. Shughuli hizo zitahitimishwa kwa ibada ya kumbukumbu katika makazi ya familia ya Odinga huko Bondo. Rais William Ruto anatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo. Hata hivyo, maandalizi hayo yamefichua tofauti kati ya viongozi wa ODM na familia ya Raila. Familia hiyo imekuwa ikiandaa ratiba yake ya maadhimisho na kusisitiza kuwa hafla hiyo inapaswa kuwaleta pamoja wote walioguswa na maisha ya Raila badala ya kuwa shughuli ya chama pekee. “Hatutaki iwe siku ya kujitenga au kuwekewa vizuizi,” alisema Winnie Odinga, binti ya Raila, akitaka kumbukumbu ya baba yake ihusishe watu wote.Kifo cha Raila mwezi Oktoba 2025 kilichochea mzozo kuhusu mwelekeo wa kisiasa wa ODM. Oburu alithibitishwa kuwa kiongozi wa chama, lakini kundi lililoongozwa na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna lilipinga ushirikiano wa karibu kati ya ODM na serikali ya Rais Ruto. Mzozo huo ulihusisha kuondolewa kwa Sifuna kama Katibu Mkuu wa chama. Baada ya malalamiko mbalimbali kuwasilishwa katika Mahakama ya Migogoro ya Vyama vya Kisiasa, hatua ya awali ya kumuondoa ilibatilishwa kwa kukiuka haki ya kusikilizwa. Hata hivyo, chama kiliruhusiwa kuanzisha upya mchakato wa kinidhamu. Mnamo Septemba, mahakama hiyo ilithibitisha kuondolewa kwa Sifuna, ikisema alipata nafasi ya kutosha kujitetea.Seneta Godfrey Osotsi aliunga mkono Sifuna na baadaye akaondolewa katika nafasi yake ya naibu kiongozi wa chama. Wawili hao walipoteza pia baadhi ya nyadhifa zao bungeni na tangu wakati huo wamekuwa viongozi wakuu wa vuguvugu la Linda Mwananchi, linalopinga ushirikiano wa ODM na serikali.Mabadiliko makubwa zaidi katika ODM yameonekana katika uhusiano wake na Rais Ruto. Viongozi wa chama wamekumbatia ushirikiano na rais na wameashiria kuwa watamuunga mkono katika uchaguzi wa 2027.Oburu amesema ODM haitasimamisha mgombea wake wa urais, akidai kuwa ushirikiano huo ni wa kuendeleza makubaliano ya kisiasa yaliyofikiwa Raila akiwa hai.“ODM na UDA si wapinzani, ni washirika katika serikali jumuishi,” alisema Ruto wakati wa ziara yake Nyanza hivi majuzi. Hata hivyo, tafiti za maoni zinaonyesha wengi wa Wakenya hawajaridhishwa na mpangilio huo. Utafiti wa TIFA ulionyesha asilimia 52 ya Wakenya wanapinga Serikali Jumuishi huku asilimia 30 pekee wakiiunga mkono. Miongoni mwa wafuasi wa ODM, asilimia 74 waliunga mkono msimamo wa Linda Mwananchi dhidi ya asilimia 20 waliounga mkono kundi la Linda Ground linalohusishwa na Oburu.Vuguvugu la Linda Mwananchi sasa limepanuka zaidi ya mzozo wa ndani ya ODM na linajitokeza kama chombo kipya cha upinzani. Sifuna, Osotsi, Gavana wa Siaya James Orengo na Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino ni miongoni mwa viongozi wanaosisitiza kuwa ODM inapaswa kubaki chama huru cha upinzani.Mnamo Septemba, vuguvugu hilo lilimwidhinisha Sifuna kuwa mgombea wake wa urais katika uchaguzi wa 2027. Utafiti wa Infotrak ulionyesha asilimia 24 ya Wakenya walijitambulisha zaidi na Linda Mwananchi, huku asilimia 27 wakiunga mkono Serikali Jumuishi. Vuguvugu hilo lilipata uungwaji mkono mkubwa miongoni mwa vijana na katika maeneo ya Magharibi, Nairobi na Nyanza. Kwa ODM, kumbukumbu ya kwanza ya kifo cha Raila ni zaidi ya hafla ya maombolezo. Ni fursa ya kuenzi maono yake kuhusu ugatuzi, uwajibikaji, haki za kijamii, ugavi sawa wa rasilimali na mageuzi ya kidemokrasia, huku chama kikitetea ushirikiano wake na serikali ambayo Raila alipinga kwa miaka mingi. Kwa upande wa Linda Mwananchi, urithi huo unatafsiriwa kama mwito wa kuendeleza upinzani huru.Familia ya Raila imejaribu kuweka maadhimisho hayo mbali na mvutano huo wa kisiasa. “Tunahitaji maadhimisho ya kwanza yawape watu nafasi yao na Baba, kumkumbuka, kumuomboleza, kusherehekea maisha yake na kuheshimu safari waliyotembea pamoja naye,” familia ilisema. Hicho ndicho kinachoonekana kuwa kinaya kikubwa cha kumbukumbu ya kwanza ya Raila. Mwanasiasa aliyetumia maisha yake kujenga mojawapo ya vyama vinavyotambulika zaidi nchini ameacha nyuma chama kilichogawanyika kuhusu mwelekeo wake wa baadaye. Swali sasa si jinsi ODM itakavyomkumbuka Raila pekee, na ikiwa chama hicho kinaweza kuwashawishi wafuasi wake kwamba siasa zake za baada ya Raila bado zinaendana na misingi aliyojitolea kujenga maisha yake yote.
UCHAGUZI mkuu wa mwaka 2027 unapokaribia, juhudi za wanasiasa na wafanyabiashara wa siasa kutafuta vyama vya kisiasa zimegeuza mazingira ya siasa nchini kuwa uwanja wenye ushindani mkali, huku zaidi ya vyama 100 vikiwa vimesajiliwa. Baadhi ya wanasiasa tayari wamenunua na kubadilisha sura ya vyama vilivyokuwepo huku wengine wakiharakisha kusajili vyama vipya. Hali hiyo imeibua maswali kuhusu nafasi halisi ya vyama vya kisiasa katika demokrasia ya Kenya. Wachanganuzi wa siasa wanasema vyama vingi vya sasa havijajengwa juu ya misingi ya itikadi au sera za muda mrefu, bali vinatumika kama vyombo vya muda vya uchaguzi vinavyowapa viongozi nafasi ya kupata tiketi za moja kwa moja, kushawishi maamuzi na kujiongezea nguvu kisiasa. Kwa mujibu wa Profesa XN Iraki wa Chuo Kikuu cha Nairobi, umiliki wa chama cha kisiasa sasa umegeuka kuwa biashara yenye faida kubwa. “Kumiliki chama nchini Kenya sasa ni ishara ya hadhi na chanzo cha mapato. Wakati wa uteuzi wa wagombea, vyeti vya uteuzi hutolewa kwa malipo. Wanaotaka kuwania nyadhifa hulipa ada kubwa za uteuzi na hivyo vyama kuwa vituo vya kutengeneza fedha,” anasema. Profesa Iraki anaongeza kuwa vyama vingi hutumika kwa uchaguzi mmoja tu kabla ya viongozi wake kuvitelekeza baada ya kufanikisha malengo yao. “Mara nyingi mwenye chama hutumia chama kama matatu. Akifika anapotaka, hushuka na kukiacha,” anasema. Mwanasheria na mchambuzi wa siasa Steve Kabita anakubaliana na mtazamo huo. Anasema kumiliki chama huwapa wanasiasa uhakika wa kushiriki meza ya mazungumzo ya miungano pamoja na kuwalinda dhidi ya migogoro ya uteuzi. “Kiongozi wa chama huwa na ushawishi mkubwa katika mazungumzo ya kisiasa. Wanasiasa wengi huepuka hatari ya kunyimwa tiketi kwa kuanzisha au kumiliki vyama vyao wenyewe,” anasema. Aidha, anasema chama kinaweza kuwa chanzo cha fedha kupitia Hazina ya Vyama vya Kisiasa inayofadhiliwa na walipa kodi. Vyama vinavyotimiza masharti ya sheria hupokea fedha za umma kulingana na idadi ya kura na viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi uliopita. Lakini wataalamu wanaonya kuwa hali hiyo inaweza kudhoofisha demokrasia. Profesa Tom Nyamache wa Chuo Kikuu cha Turkana anasema vyama vinapogeuzwa biashara, sera na manifesto hupoteza maana. “Vyama vinapokuwa kipaumbele cha faida binafsi, itikadi husukumwa pembeni na manifesto hubaki ahadi zisizo na uzito,” anasema. Aliyekuwa Mbunge wa Mukurwe-ini Kabando wa Kabando pia anaonya kuwa Kenya inahitaji vyama imara vinavyoweza kuunganisha wananchi kitaifa badala ya vyombo vinavyotumiwa kusukuma maslahi ya mtu mmoja. Homa ya kuanzisha vyama imeongezeka huku viongozi kadhaa wakijiandaa kwa uchaguzi wa 2027. Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna tayari amehifadhi jina la chama cha Linda Mwananchi huku Gavana wa Siaya James Orengo naye akitangaza mpango wa kuzindua chama chake. Miongoni mwa vyama vipya vilivyosajiliwa ni Democracy for Citizens Party (DCP) ya aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, pamoja na vyama vingine kadhaa vinavyojiandaa kushiriki uchaguzi ujao. Wanasiasa wengine kama Kawira Mwangaza, Ndindi Nyoro, Babu Owino na George Natembeya pia wamehusishwa na ununuzi au uongozi wa vyama vipya huku wakijiweka tayari kwa uchaguzi wa 2027. Kwa sasa, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa inaonyesha kuna vyama 101 vilivyosajiliwa kikamilifu na vingine zaidi ya 30 vikiwa katika hatua ya usajili wa muda. Msajili wa Vyama vya Kisiasa John Cox Lorionokou tayari ameonya kuwa atafanya ukaguzi wa makao makuu na matawi ya vyama hivyo ili kubaini vinavyotimiza matakwa ya sheria. Amesema vyama visivyo na ofisi katika angalau kaunti 24 vinaweza kuzuiwa kushiriki uchaguzi wa 2027. Na uchaguzi unapokaribia, inaonekana kuwa usajili wa vyama vipya hauchochewi tu na demokrasia au itikadi za kisiasa, bali pia na tamaa ya nguvu, pesa na ushawishi. Hali hiyo imegeuza vyama vya kisiasa kuwa bidhaa inayotafutwa kwa bidii na wanasiasa wanaotaka kujihakikishia nafasi katika siasa za baada ya 2027. Zaidi ya hayo, wimbi la kuanzishwa kwa vyama vipya limeibua hofu kuhusu mustakabali wa mfumo wa vyama vya kisiasa nchini. Wataalamu wanaonya kuwa bila mageuzi ya kina, Kenya inaweza kujikuta ikiwa na mamia ya vyama ambavyo vipo kwa jina pekee bila kuwa na ushawishi wa kweli kwa wananchi. Sheria ya Vyama vya Kisiasa inaeleza kwamba jukumu la chama si kusimamisha wagombeaji pekee wakati wa uchaguzi. Vyama vinapaswa pia kuandaa sera za umma, kuelimisha wapigakura kuhusu masuala ya kitaifa, kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika uongozi na kusaidia kuendesha serikali. Hata hivyo, wachambuzi wanasema vyama vingi havitimizi wajibu huo na vinaonekana tu wakati wa kampeni. Kumbukumbu za zinaonyesha kuwa miongoni mwa vyama vipya ni Democracy for Citizens Party (DCP) kinachohusishwa na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, pamoja na We Alliance Party na National Economic Development Party. Vingine ni People's Forum for Rebuilding Democracy, Nationalists Patriotic Party, Vision for Development Alliance (VIDA), Msingi wa Taifa na United Patriotic Movement inayohusishwa na Seneta wa Kakamega Boni Khalwale.
MWAKA mmoja baada ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, tofauti za kimya kimya zimeanza kujitokeza kati ya familia yake na chama cha Orange Democratic Movement (ODM) kuhusu jinsi ya kuhifadhi na kuenzi urithi wake wa kisiasa na kitaifa. Mvutano huo umeonekana wazi zaidi katika maandalizi ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo chake Oktoba 15. Huku familia ya Raila ikisisitiza shughuli ziongozwe na familia, ODM imeandaa maadhimisho yake ya mwezi mzima chini ya kaulimbiu ya “Mwezi wa Baba”. Hali hiyo imeibua maswali kuhusu nani ana mamlaka ya kuzungumzia urithi wa Raila na iwapo kumbukumbu zake zinapaswa kuhusishwa zaidi na ODM, chama alichoongoza kwa zaidi ya miongo miwili, au kuwasilishwa kama urithi wa kitaifa unaovuka mipaka ya siasa za vyama. Tofauti hizo zilidhihirika zaidi Ijumaa familia ya Raila ilipokosa kuhudhuria hafla ya kuwasha mishumaa iliyoandaliwa na ODM katika Bustani ya Uhuru jijini Nairobi. Raila Odinga Junior pekee ndiye aliyeshiriki hafla ya chama hicho iliyofanyika Mombasa. Akiwahutubia wafuasi, Raila Junior alionekana kuweka wazi msimamo wake kuhusu chama cha kisiasa alichoacha babake. “Leo ni siku ya kumkumbuka Baba Raila Amolo Odinga na kama Raila Junior, ningependa kusisitiza jambo moja, chama ambacho Baba alituachia ni ODM,” alisema. Pia aliwaonya vijana dhidi ya kuvutiwa na miungano mipya ya kisiasa. “Najua kuna watu wanaokimbia huku na kule, lakini nataka kuwaambia vijana kwamba si kila king’aacho ni dhahabu,” alisema. Kauli hizo zinajiri huku baadhi ya washirika wa zamani wa Raila wakiongozwa na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna wakihusishwa na juhudi za kuunda chama kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Kwa sasa ODM ni sehemu ya serikali jumuishi inayoongozwa na Rais William Ruto, mpangilio ambao Raila aliunga mkono kabla ya kifo chake. Hata hivyo, baadhi ya washirika wake wa zamani wameonekana kuunga mkono mirengo mipya ya kisiasa. Mivutano hiyo ilionekana wazi zaidi baada ya Mwakilishi wa Wanawake wa Kisumu Ruth Odinga kukosoa maandalizi ya ODM ya maadhimisho hayo. Kupitia mtandao wa kijamii, alisema baadhi ya viongozi wa chama wanaonekana kutumia kumbukumbu za Raila kwa manufaa yao badala ya kumuenzi ipasavyo. ODM ilitangaza mpango wake wa “Mwezi wa Baba” mnamo Septemba 10, ukianza kwa hafla za kuwasha mishumaa kote nchini Oktoba 2 na kuendelea na shughuli mbalimbali katika maeneo tofauti ya nchi mwezi mzima. Maelfu ya wafuasi walishiriki hafla hizo katika Nairobi, Kisumu, Mombasa na maeneo mengine. Hata hivyo, hakuna mwanafamilia wa karibu wa Raila aliyejitokeza katika hafla ya Nairobi. Wakati huo huo, familia imeunda Kamati ya Kitaifa ya Kumbukumbu ya Raila Amolo Odinga inayoongozwa na Profesa Adams Oloo huku Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo akiwa naibu mwenyekiti. Profesa Oloo amesisitiza mara kadhaa kwamba shughuli zinazoandaliwa na familia ni tofauti na zile za kisiasa za ODM. Amesema Mama Ida Odinga ataongoza rasmi hafla ya kuwasha mishumaa Oktoba 14 saa kumi na mbili jioni, siku moja kabla ya kilele cha maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kifo cha Raila. Kwa mujibu wa Profesa Oloo, Wakenya watahimizwa kuwasha mishumaa popote walipo. Kamati hiyo ilizinduliwa rasmi na Mama Ida Odinga Septemba 17 na imepewa jukumu la kuratibu shughuli zote za kitaifa za kumuenzi Raila. Aidha, Oktoba 14 kutakuwa na hafla ya kimataifa ya kuwasha mishumaa katika eneo la Kang’o Ka Jaramogi, Bondo, ambako Raila amezikwa karibu na kaburi la babake, Jaramogi Oginga Odinga. Kilele cha kumbukumbu za umma kitafanyika Oktoba 15 katika Uwanja wa Migwena Cultural and Sports Ground, Bondo. Wakati huo huo, serikali pia inashiriki kikamilifu maandalizi hayo. Makaburi maalum ya kumbukumbu ya Raila yanajengwa Kang’o Ka Jaramogi na yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi Oktoba 7 katika hafla ya kitaifa itakayohudhuriwa na wageni wachache kutokana na nafasi finyu. Naibu Mkuu wa Wafanyakazi katika afisi ya Rais, Josephat Nanok, alisema hafla hiyo itaandaliwa kwa heshima za kijeshi sawa na zile zinazotolewa kwa viongozi wa kitaifa waliowahi kushikilia nyadhifa za juu serikalini. Huku familia ikijitahidi kuweka maadhimisho hayo mbali na siasa za vyama, ODM nayo imeendelea na ratiba yake ya shughuli mbalimbali, zikiwemo mikutano ya kisiasa na maadhimisho katika Kakamega, Garissa, Pwani, Kajiado na Turkana. Wachunguzi wa siasa wanaona mgawanyiko huo kama ishara ya changamoto mpya kuhusu nani atakayelinda na kufafanua urithi wa Raila Odinga, mwanasiasa aliyekuwa mmoja wa viongozi mashuhuri zaidi katika historia ya siasa za Kenya. Ingawa pande zote zinadai zinalenga kumuenzi Raila, tofauti za mbinu kati ya familia yake na ODM zinaonyesha kwamba mjadala kuhusu mwelekeo wa kisiasa na kihistoria wa urithi
Parents of the 20 abducted prospective National Youth Service Corps members, PCMs, were thrown into profound sadness, yesterday, leading them to appeal to the Olubadan of Ibadanland, Oba Rashidi Ladoja, to assist in rescuing their children from the kidnappers’ den.
Cornelius Korir, 41, anaamini yuko hai baada ya kukosa nafasi katika gari lililowabeba waumini 17 wa Kanisa Katoliki la St Mathias Mulumba, Parokia ya Mikindani, waliofariki katika ajali mbaya eneo la Salama. Korir, baba wa watoto watatu, alipanga kusafiri pamoja na waumini wenzake kuhudhuria Siku ya Kitaifa ya Maombi katika madhabahu ya Subukia. Hata hivyo, alivunjika moyo alipoambiwa kuwa gari walilokuwa wametengewa tayari lilikuwa limejaa.Kutokana na azma yake ya kushiriki maombi hayo, Chama cha Wamishonari wa Kikatoliki tawi la Mikindani kilimpa fedha za kukata tikiti ya usafiri wa umma. Alielekea katika afisi za Dreamline na kufanikiwa kuhifadhi nafasi.Baadaye jioni, akiwa kanisani kwa misa, alipata habari kuwa nafasi moja ilikuwa imepatikana katika gari la waumini. Hata hivyo, tayari alikuwa amenunua tikiti yake.“Nilikuwa tayari nimekata tikiti, kwa hivyo wakaamua kumpatia mtu mwingine nafasi hiyo,” alisema. Korir alisafiri kivyake na kufika salama Subukia. Alipofika ndipo alipopokea simu kutoka kwa mwenyekiti wa jumuiya yake akimfahamisha kuwa gari la waumini wenzake lilikuwa limepata ajali mbaya eneo la Salama.“Nilishtuka sana. Nilikuwa nimefika tu Subukia nilipoambiwa wenzangu wamefariki katika ajali,” alisema. Wingu la simanzi limetanda katika Kanisa Katoliki la St Mathias Mulumba, Parokia ya Mikindani, Mombasa, baada ya waumini 17 waliokuwa wakielekea Subukia, Kaunti ya Nakuru, kuhudhuria siku ya kitaifa ya maombi kufariki katika ajali ya barabarani eneo la Salama kwenye barabara kuu ya Mombasa-Nairobi. Waathiriwa hao waliondoka Mombasa wakiwa na matumaini ya kushiriki ibada ya kiroho, lakini safari yao ikakatizwa ghafla walipohusika katika ajali iliyojumuisha magari kadhaa katika eneo la Mlima Kiu. Kwa mujibu wa polisi, ajali hiyo ilitokea majira ya saa moja usiku baada ya lori lililokuwa likielekea Mombasa kujaribu kupita magari mengine katika sehemu ya kupanda mlima. Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Mukaa, Hussein Abduba, alisema lori hilo liligonga magari kadhaa baada ya dereva wake kuingia katika njia ya magari yanayokuja kutoka upande mwingine.“Lori hilo liligonga magari kadhaa baada ya dereva kujaribu kuyapita magari mengine kwenye njia ya kupanda mlima,” alisema. Habari za mkasa huo zilipowafikia waumini wa St Mathias Mulumba, mamia yao walifika kanisani kuthibitisha huku wengine wakianza safari ya kuelekea Sultan Hamud kutambua miili ya wapendwa wao. Padre Kizito Iloka alisema kanisa limepoteza waumini 17 katika ajali hiyo na kwamba, miili yao ilihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Sultan Hamud. “Tuko hapa kuwaombea waumini wetu waliofariki katika ajali ya barabarani walipokuwa njiani kwenda Subukia. Tumepoteza waumini 17,” alisema.Katika misa maalumu ya maombi, Padre Augustine Lape aliwataka waumini kuwa na nguvu huku wakikabiliana na mshtuko wa msiba huo. “Jambo muhimu zaidi tunashughulikia kwa sasa ni jinsi ya kukabiliana na mshtuko huu kwa sababu hii ni habari ya kushtua. Chini ya uongozi wa Askofu Mkuu Martin Kivuva na Askofu Mkuu Mteule Dominic Kimengich, tutaendelea kutoa msaada wa kiroho kwa familia zilizoathirika,” alisema. Padre huyo pia aliomba hatua zaidi zichukuliwe kuzuia ajali za barabarani ambazo zimeendelea kuangamiza maisha ya Wakenya wengi kila mwaka.Miongoni mwa walioguswa zaidi na msiba huo ni Bi Sarah Nashivanda, 20, aliyempoteza mama yake. Kwa machozi, alisema mazungumzo yao ya mwisho yalifanyika saa mbili usiku kabla ya ajali.“Aliniambia walikuwa katika maombi na angenipigia simu asubuhi baada ya kufika Subukia. Hiyo ndiyo ilikuwa mara yangu ya mwisho kuzungumza naye. Kabla ya kuondoka aliniambia nijitunze na niwe salama,” alisema. Naye Sheila Rose, aliyempoteza shangazi yake Scholastica Ochieng, alisema bado haamini kwamba mkutano wao wa wiki hiyo ulikuwa wa mwisho. Marehemu ameacha watoto wawili.
MISRI:MAKAMU wa Rais wa Tanzania Deogratius Ndejembi, amesema Afrika ina sera, mikakati na makubaliano mazuri ya maendeleo, lakini sasa inapaswa kuongeza kasi ya utekelezaji ili rasilimali na fursa zilizopo barani humo ziweze kuleta manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi. Amesema hayo leo, Oktoba 3, 2026, akimwakilisha Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwenye Jukwaa la…
HUZUNI na ghadhabu zimetanda katika kijiji cha Mugambaciura, Kaunti ya Kirinyaga, kufuatia kifo cha mwanamke mjamzito aliyedaiwa kusukumwa kutoka kwa gari la polisi lililokuwa likiendeshwa baada ya yeye na mumewe kushindwa kutoa hongo ya Sh1,000 iliyodaiwa na maafisa wa polisi. Bi Catherine Mwende, ambaye alikuwa mjamzito wa miezi ya mwisho, alifariki papo hapo pamoja na mtoto aliyekuwa tumboni baada ya kuanguka barabarani. Mumewe, Anthony Muturi, alipata majeraha mikononi na miguuni lakini alinusurika. Kulingana na Bw Muturi, mkasa huo ulitokea Ijumaa walipokuwa wakielekea shambani kuvuna miraa. Akiwa pamoja na mkewe, alisema gari la polisi lilisimama na maafisa waliokuwa ndani wakawapa lifti hadi walikokuwa wakielekea. Hata hivyo, walipofika karibu na walikokusudia kushuka, mambo yalibadilika ghafla. Bw Muturi alisema walipowaomba maafisa hao wasimamishe gari ili washuke, walidai walipe Sh1,000 kama ishara ya shukrani kwa lifti waliyopewa. “Walipotusimamisha mwanzoni hawakutuambia kuwa tulihitajika kulipia safari hiyo. Tulishangaa walipoanza kutudai pesa tulipofika tunakokwenda,” alisema Muturi. Kwa mujibu wake, yeye na mkewe waliwaeleza polisi kuwa hawakuwa na fedha hizo, jambo lililosababisha mabishano makali. Ndipo, kwa mujibu wa madai yake, maafisa hao waliwasukuma kutoka kwenye gari hilo lililokuwa bado likiendeshwa. Mwende alianguka kifudifudi barabarani na kufariki pamoja na mtoto wake ambaye alikuwa hajazaliwa. Muturi, ambaye alitibiwa hospitalini na kuruhusiwa kurejea nyumbani, sasa anataka serikali kuhakikisha uchunguzi wa kina unafanywa na waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria. “Nimepoteza mke wangu na mtoto wangu ambaye alikuwa hajazaliwa. Maafisa waliohusika wanapaswa kuwajibishwa,” alisema kwa huzuni. Kisa hicho kimezua hasira miongoni mwa wakazi wa eneo hilo, ambao wamewashutumu maafisa wa polisi kwa kuwadhulumu wananchi kwa kisingizio cha kuwapa lifti. Mchungaji Ephantus Mwangi alisema ikiwa madai hayo yatathibitishwa, basi hatua kali za kisheria zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya maafisa wote waliohusika. “Kama wakazi tunataka haki itendeke. Polisi wanaopatikana na hatia lazima wawajibishwe kwa mujibu wa sheria,” alisema. Baada ya tukio hilo, wakazi wenye hasira walifunga barabara ya Piai-South Ngariama wakipinga kile walichokitaja kuwa ukatili wa polisi. Pia walifukuza maafisa wa usalama waliofika eneo hilo kuchukua mwili wa marehemu. Hali ya taharuki ilitawala huku waandamanaji wakitaka hatua za haraka zichukuliwe dhidi ya maafisa wanaohusishwa na kisa hicho. Baadhi ya wakazi walidai kuwa matukio ya maafisa wa polisi kudai fedha kutoka kwa watu wanaowapa lifti yamekuwa yakitokea mara kwa mara. “Majuzi tu tulipewa lifti na kisha tukaombwa tulipe Sh500,” alisema mkazi mmoja, Alfred Muthomi. Lawrence Mugo, mwendesha bodaboda aliyefika eneo la tukio muda mfupi baada ya ajali hiyo, alisema alishtushwa na hali aliyokuta. “Sikuamini nilichokiona. Mwanamke alikuwa ameaga dunia huku mwanamume akiwa amejeruhiwa vibaya kando ya barabara,” alisema. Aliyekuwa Naibu Gavana wa Kirinyaga, Peter Ndambiri, amelaani tukio hilo na kuitaka Idara ya Polisi kufanya uchunguzi usioegemea upande wowote ili ukweli ujulikane. Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Mwea Mashariki, Henry Gitonga, alisema uchunguzi umeanzishwa kubaini kilichotokea na kuwataka wakazi kuwa watulivu wakati mamlaka zikichunguza madai hayo. Tukio hilo limeibua maswali mazito kuhusu mienendo ya baadhi ya maafisa wa usalama na uhusiano wao na wananchi.
RAIS William Ruto jana alihitimisha ziara yake ya siku nane katika eneo la Pwani kwa ahadi mpya za kutatua tatizo sugu la ukosefu wa ardhi miongoni mwa wakazi huku akionya mabwanyenye wanaomiliki ardhi bila kuitumia. Hata hivyo, idadi ndogo ya hati miliki zilizotolewa Kaunti ya Mombasa imeibua maswali kuhusu kasi ya utatuzi wa migogoro ya ardhi katika eneo hilo. Mombasa ilipokea hati miliki 4,360 pekee, idadi ndogo ikilinganishwa na kaunti nyingine za Pwani. Kwale ilipokea hati 94,175, Kilifi ikapata 36,826 huku Taita Taveta ikipewa hati 31,318. Kaunti za Lamu na Tana River zilipokea jumla ya hati 22,770. Maeneo ya Mombasa kama Zum Zum, Katani, Kwa Bulo na Aldina yameendelea kukwama kutokana na kesi mahakamani na kutopatikana kwa idhini kutoka kwa wamiliki wa ardhi walioko nje ya eneo hilo. Akizungumza katika uwanja wa Mama Ngina Waterfront, Mombasa, Rais alisema serikali haitaruhusu maelfu ya wakazi kufurushwa kutoka mashamba ambayo wameishi kwa miaka mingi. “Hatutakubali tamaa ya baadhi ya mabwanyenye wanaozuia juhudi za kutatua dhuluma za kihistoria za ardhi katika Pwani. Tuko tayari kufanya mazungumzo lakini hatutaruhusu wananchi kufurushwa,” alisema. Rais alihitimisha ziara yake Lamu ambapo aligawa hati miliki 20,189 kwa wakazi wa maeneo mbalimbali. Hafla hiyo pia ilitumiwa kuhimiza wakazi kuunga mkono mradi wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote pamoja na eneo maalum la viwanda kwa gharama ya Sh2 trilioni. Rais alisema serikali imetenga Sh7.5 bilioni kujenga nyumba 3,000 kwa wafanyakazi watakaoajiriwa katika kiwanda hicho. “Tunataka wafanyakazi watakaokuja kufanya kazi hapa wapate makazi bora na mazingira mazuri ya kazi,” alisema. Waziri wa Madini na Uchumi wa Bahari, Ali Hassan Joho, alisema mradi huo unaweza kubadilisha kabisa uchumi wa Pwani, ukanda ambao umekuwa ukilalamikia kutengwa kwa miaka mingi. Naye Gavana wa Lamu, Issa Timamy, alisema wenye ardhi halali watakaoathiriwa na mradi huo watapata fidia. Waziri wa Ardhi, Alice Wahome, alisema utoaji wa hati miliki utawapa maelfu ya wakazi umiliki rasmi wa ardhi zao na kumaliza migogoro ya muda mrefu. Hata hivyo, huku wakazi wa Lamu wakisherehekea kupokea hati miliki, maelfu ya wakazi wa Mombasa bado wanasubiri migogoro ya ardhi kutatuliwa ili waweze kupata nyaraka zao.
WAHADHIRI na wafanyakazi wengine wa vyuo vikuu vya umma wamekataa pendekezo jipya la serikali kuhusu Mkataba wa Makubaliano ya Kazi (CBA) wa miaka ya 2025 hadi 2029, wakisema halikidhi matakwa yao. Mzozo huo unahusisha tofauti kubwa kati ya madai yaliyowasilishwa na vyama vya wafanyakazi vya UASU, KUSU na KUDHEIHA na mapendekezo yaliyotolewa na Baraza la Vyuo Vikuu vya Umma (IPUCCF), linalowakilisha waajiri. Vyama hivyo vilipendekeza nyongeza kubwa ya mishahara na marupurupu mbalimbali. UASU, kwa mfano, ilitaka mishahara ya msingi iongezwe kwa kiwango cha kati ya asilimia 36 na 68 kulingana na daraja la kazi. Pia ilipendekeza nyongeza ya asilimia 57 ya marupurupu ya nyumba, ya usafiri ya hadi Sh60,000 kwa baadhi ya daraja na ya maprofesa ya Sh80,000. Aidha, chama hicho kilitaka marupurupu ya vitabu ya kati ya Sh65,000 na Sh90,000 kwa mwaka, ya likizo ya hadi Sh70,000 pamoja na bima ya matibabu, meno na macho. Hata hivyo, waajiri walipendekeza ongezeko la chini zaidi. Baada ya kupitia chaguo mbalimbali, IPUCCF ilipendekeza mishahara iongezwe kwa asilimia mbili kila mwaka katika kipindi cha miaka minne ya CBA. Hii inatafsiriwa kuwa nyongeza ya jumla ya asilimia 8.25 pekee kufikia mwaka 2029. Katibu Mkuu wa UASU, Dkt Constantine Wasonga, alisema vyama vya wafanyakazi havikushirikishwa kikamilifu katika kufikia uamuzi huo. “Hatuwezi kupewa kiwango cha mwisho halafu tuelezwe tukubali. Maafikiano ya pamoja yanahitaji mazungumzo ya kweli,” alisema. Mwenyekiti wa KUSU, Dkt Charles Mukhwaya, alisema wafanyakazi wamechoshwa na mazungumzo yasiyozaa matunda. “Hatuwezi kuendelea kuzunguka katika jambo moja milele. Ikiwa haki zetu hazitazingatiwa, tuko tayari kwenda barabarani kudai tunachostahili,” alisema. Kwa upande wake, KUDHEIHA imesema pendekezo la sasa halikidhi matarajio ya wafanyakazi na haiwapi nafasi ya kupanda madaraja kazini.
Spika wa Bunge la Kitaifa, Moses Wetang’ula, amesema serikali inaendelea kuwekeza katika maendeleo ya miundombinu na kuimarisha usalama katika Kaunti ya Marsabit ili kufungua fursa za kiuchumi na kuboresha maisha ya wakazi wa eneo hilo. Akizungumza katika hafla ya kuchangisha fedha za elimu eneo la Mugur E Serima, Marsabit, Wetang’ula alisema serikali imepiga hatua katika kupambana na ukosefu wa usalama kupitia ushirikiano na jamii za eneo hilo. Alisema maeneo ya mashinani na yaliyotengwa kwa muda mrefu yanapaswa kunufaika kwa usawa kutokana na miradi ya maendeleo ya kitaifa kwa kuwa sehemu kubwa ya rasilimali za nchi hupatikana nje ya miji mikubwa. Kwa mujibu wa Spika huyo, kuboresha barabara na miundombinu mingine kutachochea biashara, kuvutia wawekezaji na kuunganisha jamii mbalimbali za Marsabit. Aliongeza kuwa usalama thabiti utawawezesha wakazi kutumia kikamilifu rasilimali zilizopo katika kaunti hiyo. Wetang’ula alitaja maendeleo yaliyopatikana chini ya utawala wa Rais William Ruto, ikiwemo miradi ya barabara, afya na elimu pamoja na uwekezaji mkubwa kama mradi wa Sh2 trilioni wa Lamu wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote. Pia alisema serikali itaajiri walimu 24,000 zaidi mwaka huu, huku maeneo ya mazingira magumu yakipewa kipaumbele ili kuhakikisha usawa wa fursa za elimu nchini. Naye Katibu wa Utawala na Afisa Mkuu wa Uhasibu katika Huduma ya Kitaifa ya Polisi, Bernice Lemedeket, aliwashukuru viongozi wanaounga mkono elimu ya mtoto wa kike. “Tumefanikiwa katika taaluma zetu kwa sababu tulibaki shuleni. Tunapaswa kuona watoto wengi kutoka jamii zilizotengwa wakifanya vyema katika masomo,” alisema. Gavana wa Marsabit, Mohamud Mohamed Ali, alisema serikali yake imetoa ufadhili kamili wa masomo kwa zaidi ya wanafunzi 10,000 tangu mwaka 2018. “Hatutumii misingi ya ukoo katika kutoa ufadhili wa elimu. Sheria zimebadilika lakini hilo halimaanishi tuache kuwekeza katika elimu,” alisema. Gavana huyo pia alitangaza kumuunga mkono Rais Ruto katika uchaguzi wa 2027, akisema upinzani hauna ajenda wala viongozi wenye uwezo wa kuongoza taifa. Mbunge wa Laisamis, Joseph Lemasolai Lekuton, alimshukuru Wetang’ula kwa kuendelea kuunga mkono jamii zilizotengwa na kuhimiza umoja ili kuchochea maendeleo zaidi katika eneo hilo. Kwa upande wake, Katibu wa Wizara ya Ustawi wa Viwanda, Dkt Juma Mukhwana, alisema serikali imepata mafanikio makubwa ya maendeleo na kuwataka Wakenya kuendelea kuunga mkono ajenda yake ya maendeleo.
Rubani mwenza wa ndege ya Flydubai iliyokuwa ikielekea Israel alijaribu kuteka ndege hiyo baada ya kumshambulia rubani kwa shoka akiwa angani, mwendesha mashtaka mkuu wa Falme za Kiarabu amesema. Ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka Dubai kuelea Tel Aviv ikiwa na zaidi ya abiria 170. Takribani saa mbili na nusu baada ya kuondoka, ilianza kushuka kwa kasi umbali wa karibu futi 17,000, hali iliyozua hofu kubwa miongoni mwa abiria. Rubani mkuu, Kapteni Smit Machchhar, ambaye alijeruhiwa katika shambulio hilo, alisema alijikuta amelala sakafuni akiwa amejeruhiwa alipogundua ndege ilikuwa ikipoteza mwelekeo. “Nilijiambia lazima nijaribu mara ya mwisho kufungua mlango kutoka ndani,” alisema, hatua iliyowaruhusu baadhi ya abiria kuingia kwenye chumba cha marubani na kusaidia kudhibiti hali. Baada ya mshambuliaji kushindwa nguvu, marubani wawili wa akiba waliokuwa ndani ya ndege walifanikiwa kuitua salama nchini Saudi Arabia. Mamlaka za UAE zimesema uchunguzi unaendelea kubaini chanzo na sababu za tukio hilo. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema mshukiwa huyo ni raia wa Oman. Vyombo mbalimbali vya habari vimemtaja kuwa Hamam al-Hammami. Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Amerika, alipokuwa akifanya kazi katika shirika la ndege la Oman Air, aliondolewa kwenye mafunzo ya urubani kutokana na wasiwasi kuhusu misimamo yake mikali ya kidini. Netanyahu alisema baada ya kushindwa kutekeleza mpango wake, mshukiwa huyo aliendelea kupiga kelele akisema, “Niueeni, niueeni.” Aliongeza kuwa dalili zinaonyesha mshukiwa alikuwa na nia ya kuangusha ndege hiyo. Abiria mmoja, Almog Itali, alisema alihisi ndege ikishuka kwa kasi. “Ghafla, ndege ilianza kushuka kwa nguvu kubwa kwa sekunde kadhaa kabla ya kutulia na kisha kuanza tena kushuka,” alisema. Kwa mujibu wa Rais wa Israel Isaac Herzog, mwanamke mmoja Mwisraeli aliyekuwa ndani ya ndege ndiye aliyegundua mtafaruku uliokuwa ukiendelea kwenye chumba cha marubani na kupiga kamsa. Abiria kadhaa waliingia ndani ya chumba hicho na kufanikiwa kumzuia mshambuliaji aliyekuwa akijaribu kuharibu vifaa vya kuongoza ndege. Kapteni Machchhar amelazwa hospitalini Abu Dhabi na ameripotiwa kuwa katika hali nzuri na anaendelea kuimarika. Serikali ya India pia imethibitisha kuwa afya yake inaendelea kuimarika baada ya kujeruhiwa katika tukio hilo ambalo limetajwa kuwa liliepusha janga kubwa la angani.