
Category
Top headlines and developing stories from Tanzania, Kenya, Uganda and the wider region, gathered from the leading local and international newsrooms and updated throughout the day.


By Samuel Oyadongha, Yenagoa Minister of State for Petroleum Resources (Oil), Senator Heineken Lokpobiri, has said reforms introduced by the administration of President Bola Tinubu have increased Nigeria’s crude oil production by more than 80 per cent. Lokpobiri stated this in Yenagoa, Bayelsa State, at a breakfast meeting with media friends led by Elder Asu […]

DAR ES SALAAM: VICE-PRESIDENT Deogratius Ndejembi has directed the Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) and its partners to accelerate implementation of the peri-urban electricity scheme to ensure residents in areas with rural characteristics are not disadvantaged by urban administrative boundaries. Mr Ndejembi said some communities had lifestyles and settlement patterns similar to rural areas but…

WAUMINI 16 wa Kanisa Katoliki kutoka parokia ya St Mathias Mulumba, Mikindani, Mombasa, wamefariki katika ajali ya barabarani eneo la Salama, Kaunti ya Makueni. Waumini hao walikuwa safarini kuelekea Subukia, Nakuru, kuhudhuria Siku ya Kitaifa ya Maombi) katika Madhabahu ya Kitaifa ya Subukia. Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mombasa, Martin Kivuva Musonde, alithibitisha kifo cha mahujaji hao kupitia taarifa aliyotuma kwa mapadre, watawa na waumini. “Tunasikitika kwa huzuni kubwa kutangaza kifo cha ghafla cha mahujaji 16 kutoka St Mathias Mulumba, Mikindani, katika ajali iliyotokea Salama,” alisema Askofu Kivuva. Alisema mahujaji hao walikuwa njiani kuelekea Madhabahu ya Kitaifa ya Subukia kwa ajili ya Siku ya Kitaifa ya Maombi. Askofu Kivuva aliwataka waumini kuombea roho za marehemu, familia zao, Parokia ya St Mathias Mulumba na Dayosisi ya Mombasa kwa ujumla ili wapate faraja katika kipindi hiki kigumu. “Tuombe kwa ajili ya pumziko la roho zao tunapoombea familia zao, parokia ya St Mathias Mulumba na Dayosisi nzima ili tupate faraja na utulivu kutoka kwa Bwana,” alisema. Alimalizia taarifa hiyo kwa kuwaombea marehemu, akisema: “Roho zao zipumzike kwa amani. Amina.” Kamishna wa Kaunti ya Makueni, Abdullahi Khalif, amethibitisha ajali hiyo.

KILA siku mitandao ya kijamii hujaa jumbe zinazowashauri watu kujiepusha na ndoa, kuachana na wachumba wao au kutafsiri kila mzozo kama ishara ya kuvunjika kwa uhusiano. Baadhi ya wanawake hujitokeza kwenye TikTok na majukwaa mengine kueleza jinsi wanavyoona ndoa ikiwa mzigo, huku wengine wakitumia uzoefu wao wa talaka kuwashauri walio kwenye ndoa kuwa makini na kujiandaa kwa siku ambayo mambo yataharibika. Hali hiyo imeibua swali: Je, mitandao ya kijamii inachochea migogoro katika ndoa? Mwanasaikolojia na mshauri wa ndoa Lucy Nduti anasema mitandao sasa ni chanzo cha migogoro mingi ya ndoa anayoshughulikia. Anasema tatizo ni ushauri unaotolewa na watu wasio na utaalamu, huku masuala magumu ya ndoa yakifupishwa kuwa kauli kama, “Ondoka mara moja akifanya hivi.” Bi Nduti anasema ndoa huhitaji kuangalia muktadha, mawasiliano, historia ya uhusiano, mipaka na tofauti za wahusika, mambo ambayo hayawezi kuelezwa kwa jumbe fupi mitandaoni. “Ushauri mzuri unapaswa kutoa nafasi kwa muktadha, mazungumzo na, inapohitajika, msaada wa kitaalamu,” anasema. Anasema pia tabia ya kuita kila jambo “ishara mbaya” inaweza kufanya migogoro ya kawaida ionekane kama sababu ya kuvunja ndoa. Kwa mfano, mtu anayesahau kumbukumbu ya siku muhimu au kunyamaza baada ya siku ngumu anaweza kutafsiriwa haraka kuwa ana tatizo kubwa. Mitandao pia imebadilisha jinsi watu wanavyolinganisha ndoa zao. “Tunalinganisha maisha yetu ya faragha na matukio yaliyochaguliwa na mtu mwingine kuyaonyesha hadharani. Tunaona zawadi, likizo na picha nzuri za familia, lakini hatuoni shinikizo za kifedha au mazungumzo magumu yaliyo nyuma yake,” anasema. Kwa mujibu wa Bi Nduti, hali hiyo inaweza kumfanya mtu ajiulize kwa nini ndoa yake haifanani na anazoona mtandaoni. Pia, wanandoa wanaweza kutumia muda mwingi wakiwa kwenye simu wakati wa chakula au kabla ya kulala, hivyo kupunguza mazungumzo, ukaribu na mapenzi. Hata hivyo, anasema si kila tatizo la ndoa linasababishwa na mitandao. Kwa upande wake, wakili Cosmas Mureti anasema mitandao imeanza kuonekana katika migogoro inayofikishwa mahakamani. Anasema machapisho ya mitandaoni yanaweza kutumiwa kama ushahidi wa madai kama uzinzi na ukatili katika ndoa. Hata hivyo, anatahadharisha wanandoa dhidi ya kuweka hadharani ujumbe wa kibinafsi, picha za skrini na ugomvi wao. “Watu wa nje wanaweza kuchochea mfarakano na kuvuruga juhudi za wanandoa kupatana,” anasema. Mureti pia anapinga dhana kwamba mchumba anayelinda simu yake lazima awe anaficha usaliti. “Ndoa si gereza na haiondoi haki ya mtu ya faragha,” anasema. Anasema kila wanandoa wana namna yao ya kuendesha ndoa na hawapaswi kulinganisha uhusiano wao na ndoa zinazoonyeshwa mtandaoni.

MAHAKAMA Kuu imeizuia Tume ya Huduma ya Mahakama (JSC) kuendelea kushughulikia maombi ya kuwaondoa majaji wa Mahakama ya Juu hadi kanuni za kusimamia mchakato huo ziwekwe rasmi. Majaji Charles Kariuki, Lawrence Mugambi na Bahati Mwamuye walisema Katiba inahitaji kila ombi la kumuondoa jaji liwasilishwe dhidi ya jaji mmoja mmoja na lifafanue kwa uwazi madai ya utovu wa nidhamu yanayomkabili. Walisisitiza kuwa majaji huteuliwa, huapishwa na huwajibika kibinafsi hata wanapofanya kazi kama jopo moja. Mahakama ilifutilia mbali malalamishi kadhaa yaliyowasilishwa dhidi ya majaji wa Mahakama ya Juu, yakiwemo yaliyomlenga Jaji Mkuu Martha Koome, na kuyataja kuwa batili na kinyume cha Katiba. Pia ilikataza JSC kuchukua hatua zaidi kwa msingi wa malalamishi hayo. Kesi hiyo ilitokana na malalamishi yaliyowasilishwa baada ya Mahakama ya Juu kuzuia wakili Ahmednasir Abdullahi na kampuni yake ya sheria kufika mbele ya mahakama hiyo.

UZINDUZI wa ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote East Africa Petroleum Refinery and Petrochemicals cha thamani ya Sh2 trilioni umeibua mjadala kuhusu ardhi itakayotumiwa wakati wa ujenzi wa mradi huo. Rais William Ruto amesema serikali imetenga ekari 9,000 Lamu kwa mradi huo na inatafuta ekari nyingine 3,000 kadiri mradi unavyopanuka. Hivyo, jumla ya ardhi inayolengwa ni takriban ekari 12,000. Akizungumza katika Ikulu ya Mombasa Oktoba 1, 2026, Rais Ruto alisema ekari 5,000 zitatumika kuanzisha eneo maalumu la kiuchumi (SEZ), huku eneo hilo likitarajiwa pia kuwa na mji mpya. Alisema uwekezaji huo unakadiriwa kuwa sawa na asilimia 12 ya Pato la Taifa. Mradi huo unatarajiwa kuwa na uwezo wa kusafisha mapipa 700,000 ya mafuta kwa siku na kutoa nafasi za ajira 60,000 pamoja na kuchochea ukuaji wa viwanda vingine. Hata hivyo, suala la ardhi limeibua maswali kuhusu iwapo ni ya umma au kuna watu binafsi wanaoidai, namna watakavyolipwa fidia na kama thamani ya ardhi itahesabiwa kuwa sehemu ya mchango wa Kenya katika mradi huo. Wakazi 133 wa Lamu wamewasilisha kesi mahakamani wakidai kuwa sehemu ya ardhi iliyotengewa mradi huo ni ya mababu zao na wana maslahi nayo. Mahakama ya Mazingira na Ardhi imeamuru hali ya sasa katika kipande hicho cha ardhi ibaki hivyo hadi Oktoba 14, kesi hiyo itakaposikilizwa. Kesi hiyo inahusu ardhi LR No. 13061 katika eneo la Hindi/Manda Magogoni, Lamu. Hata hivyo, mahakama bado haijaamua kuhusu umiliki wa ardhi hiyo. Rais Ruto amesema ardhi inayotumiwa ni ya serikali na hakuna mtu atakayeondolewa bila fidia. Alisema iwapo kuna wakazi katika maeneo ambayo serikali itatumia kwa mradi huo, serikali ndiyo itakayowalipa fidia na si mwekezaji. “Mradi huo unatekelezwa katika ardhi ya serikali. Hakuna mtu atakayeondolewa. Lakini kama kuna wakazi katika maeneo ambayo serikali itatumia, watalipwa fidia na serikali ya Kenya,” alisema. Rais alisema haiwezekani kumwachia mwekezaji jukumu la kutafuta maelfu ya ekari na kujadiliana na wenye ardhi, akisema hilo linaweza kumfanya akate tamaa. Hata hivyo, wakazi wamekuwa wakitaka kufahamishwa eneo kamili na ukubwa wa ardhi iliyootengewa kiwanda hicho. Mohamed Rajab, katibu wa mipango wa Kililana Farmers Association, alihoji kwa nini wakazi hawakupewa maelezo kuhusu eneo kamili la mradi. Seneta aliyeteuliwa Shakila Abdalla pia alihoji kwa nini wakazi hawakuwa na taarifa kuhusu ukubwa na eneo la ardhi iliyotengwa au inayotafutwa kwa mradi huo. Baadhi ya wakazi wamehusisha mjadala huo na ununuzi wa ardhi uliofanywa awali kwa miradi ya Lapsset, wakisema masuala ya fidia bado hayajamalizika. Mjadala huo pia umefika Seneti, huku Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna akihoji kwa nini Bunge halijapewa mkataba unaoongoza uwekezaji huo. Alisema wabunge hawajui ahadi ambazo Kenya imeweka ili kuhakikisha kiwanda hicho kinajengwa. Kiongozi wa People's Party of Kenya na Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro pia ametaka serikali kufichua muundo wa umiliki, kiwango cha ardhi kinachotolewa na iwapo thamani ya ardhi hiyo itabadilishwa kuwa hisa katika mradi. “Tunatoa ardhi kiasi gani kwa kiwanda cha Dangote? Thamani yake inabadilishwa kuwa hisa? Thamani ni kiasi gani?” aliuliza. Rais Ruto amesema Kenya itatumia mali yake, ikiwemo ardhi, na Hazina ya Kitaifa ya Miundombinu kuwekeza katika mradi huo. Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka amesema uwekezaji mkubwa unapaswa kuchunguzwa ili kuhakikisha unanufaisha nchi na wananchi. Serikali imesema itahakikisha wananchi wanashirikishwa katika kila hatua ya mradi na kwamba watakaoathiriwa na upatikanaji wa ardhi watalipwa fidia. Gavana wa Lamu Issa Timamy ameunda kamati inayojumuisha taasisi zinazoshughulikia ardhi, mazingira na masuala mengine yanayohusiana na kiwanda hicho. Mshauri wa serikali na mwanauchumi Dkt David Ndii amesema wakazi walilipwa fidia mwaka 2015 baada ya serikali kutoa Sh1.3 bilioni katika awamu ya kwanza ya mradi wa Lapsset. Kwa sasa vifaa vya mradi huo vimewasili katika Bandari ya Lamu, huku mfanyabiashara Aliko Dangote akisema ujenzi utakamilika ndani ya miezi 40.

Watu 17 wamefariki papo hapo katika ajali mbaya ya barabarani iliyohusisha magari kadhaa eneo la Salama, kwenye barabara kuu ya Mombasa-Nairobi, Kaunti ya Makueni. Kamishna wa Kaunti ya Makueni, Abdullahi Khalif, amethibitisha ajali hiyo. Habari zaidi kufuata..

SENETI ya Amerika imemthibitisha mwanadiplomasia mkongwe Henry Wooster kuwa balozi mpya wa Washington nchini Kenya, hatua inayofungua njia kwa mwakilishi huyo kuanza kazi Nairobi kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027. Wooster alithibitishwa Septemba 30 kwa idhini ya pamoja ya Seneti, baada ya Kamati ya Seneti ya Mahusiano ya Kigeni kuidhinisha uteuzi wake. Rekodi rasmi ya Seneti inamtaja kama mwanachama wa ngazi ya juu wa Foreign Service mwenye cheo cha Minister-Counselor. Anachukua nafasi hiyo baada ya Meg Whitman kuondoka mwaka 2024. Tangu wakati huo, Ubalozi wa Amerika Nairobi umeongozwa na kaimu balozi huku nafasi hiyo ikiwa haina balozi aliyethibitishwa na Seneti. Uteuzi wa Wooster unakuja wakati Kenya ikijiandaa kwa uchaguzi mkuu wa Agosti 2027, jambo ambalo lilikuwa miongoni mwa masuala makuu yaliyoibuliwa wakati wa kikao chake cha kuthibitishwa Septemba 16. Akijibu maswali ya Seneta Chris Coons kuhusu namna Amerika itakavyoshughulikia uchaguzi huo, Wooster alisema Washington itafuatilia kwa karibu mchakato huo, huku kipaumbele chake kikiwa utulivu na kuepusha ghasia. Alisisitiza kuwa Amerika itasimamia haki bila kuonyesha upendeleo katika uchaguzi wa Kenya. Wooster pia alielezea Kenya kama mshirika muhimu Afrika Mashariki, akitaja ushirikiano wake katika masuala ya usalama, mapambano dhidi ya ugaidi na jukumu la maafisa wa polisi wa Kenya katika misheni ya kimataifa ya usalama nchini Haiti. Wakati wa kikao hicho, aliulizwa kuhusu uhusiano unaokua kati ya Nairobi na Beijing na iwapo hilo linaashiria Kenya kujitenga na Washington. Wooster alipinga mtazamo huo, akisema uhusiano wa Kenya na China hauongozwi na mshikamano wa kiitikadi. Kauli hiyo ilitofautiana na msisitizo wa baadhi ya maseneta kuhusu kuongezeka kwa ushawishi wa China barani Afrika. Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya Kigeni, Jim Risch, alisema Kenya ni mshirika muhimu wa Amerika lakini akaibua wasiwasi kuhusu uhusiano wake wa kidiplomasia na China pamoja na msimamo wake kuhusu Sudan. Mbali na usalama, Wooster alisema kuna nafasi ya kuimarisha ushirikiano kati ya Kenya na Amerika katika biashara, uwekezaji, afya na teknolojia. Alitaja sekta ya teknolojia nchini Kenya, mazingira ya ujasiriamali na taasisi zake kuwa maeneo ambayo yanaweza kuvutia ushirikiano zaidi wa kiuchumi kati ya nchi hizo. Kwa upande wake, Seneta Jeanne Shaheen alisema Wooster anakabidhiwa jukumu hilo wakati Kenya ikiingia kipindi cha uchaguzi na huku mustakabali wa misaada ya Amerika kwa afya na programu nyingine za maendeleo ukiwa miongoni mwa masuala yanayohitaji kushughulikiwa. Wooster ni mwanachama wa Senior Foreign Service ya Amerika. Aliwahi kuwa balozi wa Washington nchini Jordan kuanzia 2020 hadi 2023 na baadaye kushikilia nyadhifa za juu katika Wizara ya Mambo ya Nje. Amewahi kuhudumu Baghdad, Islamabad, Moscow na katika makao makuu ya NATO, pamoja na kufanya kazi katika Baraza la Usalama la Taifa la Amerika. Kabla ya kujiunga na Foreign Service, Wooster alikuwa afisa wa Jeshi la Washington. Sasa anajiandaa kuhamia Nairobi na kuanza rasmi kazi kama balozi wa Amerika nchini Kenya.

UHUSIANO wa mfanyabiashara Wicknell Chivayo na mkewe wa kwanza, Sonja Louise Madzikanda, ulivunjika mwanzoni mwa 2024 na kugeuka kuwa mzozo mkubwa wa mamilioni ya pesa kortini. Madzikanda, mwenye umri wa miaka 34 na mama wa watoto wawili wa Chivayo, alitangaza kutengana na mumewe huku akiwasilisha kesi kuhusu mali ya mamilioni ya dola, magari ya kifahari na haki ya kuwaona watoto wao. Stakabadhi za kesi katika Mahakama Kuu zinaonyesha kuwa Madzikanda alidai malipo ya Sh3.2 bilioni, matunzo ya kila mwezi ya Sh5.1 milioni na Sh130 milioni kila mwaka kwa likizo na burudani. Pia alitaka apewe malezi kamili ya watoto wao wawili huku Chivayo akipewa muda mdogo wa kuwaona. Chivayo naye aliwasilisha kesi ya dharura akitaka kuruhusiwa kuwaona watoto, akidai Madzikanda alikuwa “akimnyima fursa ya kuwaona” licha ya juhudi zake za kutatua mzozo huo kwa amani. Wawili hao walifunga ndoa ya kitamaduni Julai 2017 na wana watoto wawili walio chini ya miaka 10. Katika taarifa yake kortini, Madzikanda alisema ndoa hiyo ilikuwa imevunjika kabisa, akitaja madai ya uzinzi, unyanyasaji wa kihisia na kutelekezwa. Hata hivyo, Aprili mwaka huu, Mahakama Kuu ya Zimbabwe iliidhinisha makubaliano yaliyofikiwa na wawili hao, ambapo Chivayo alikubali kulipa Sh649 milioni kwa matunzo ya watoto wao. Kati ya fedha hizo, Sh285 milioni zilikuwa tayari zimelipwa, huku salio la Sh363 milioni likipaswa kulipwa ndani ya siku 30. Fedha hizo ziliwekwa katika akaunti ya benki iliyodhibitiwa na Madzikanda. Lengo lilikuwa fedha hizo ziwekezwe na kuzalisha faida itakayogharamia mahitaji ya watoto baadaye. Kwa miezi 12 ya kwanza, Chivayo alitakiwa kuendelea kugharamia maisha ya watoto huku Madzikanda akiunda hazina hiyo. Baada ya hapo, gharama hiyo ingelipwa kutokana na faida ya uwekezaji. Lakini makubaliano hayo hayakumaliza mzozo mpana kuhusu utajiri wa Chivayo. Madzikanda alikuwa amedai mali kadhaa ikiwemo nyumba Zimbabwe na Afrika Kusini, magari ya kifahari na maslahi katika biashara zinazohusishwa na Chivayo. Magari yaliyotajwa ni Rolls-Royce Spectre, Rolls-Royce Ghost mbili, Rolls-Royce Phantom, Range Rover, Mercedes-Benz V-Class na Mercedes-Benz Maybach. Pia alitaja ndege ya kibinafsi na kampuni zikiwemo Intratek, WMC Trading, IMC Communications, Trintas Petroleum na Eldo. Mali aliyodai ilijumuisha ardhi Gletwyn, nyumba katika Rikitayi Villas, Ballantyne Park, Harare, na nyumba katika DaVinci Suites, Sandton, Johannesburg. Aidha, alitaka watoto wahakikishiwe elimu, matibabu na mahitaji yao mengine, pamoja na bajeti ya dola milioni moja kila mwaka kwa likizo na burudani. Kilichoidhinishwa na mahakama ni mpango wa Sh649 milioni kwa matunzo na uwekezaji wa watoto. Madzikanda pia alibaki na watoto, huku Chivayo akipewa nafasi ya kuwa nao kwa wiki moja kamili kila mwezi, wikendi na likizo za umma kwa zamu. Katika wiki ya kuwaona, Chivayo alitakiwa kuwepo mwenyewe na hakuruhusiwa kukabidhi majukumu yake ya mzazi kwa watu wengine. Mzozo huo ulikuwa bado mahakamani wakati Chivayo na mkewe wa pili walipofariki katika ajali ya helikopta Jumatano usiku. Pia kulikuwa na mvutano kuhusu uhalali wa ndoa yao ya kitamaduni. Madzikanda alisema ndoa hiyo ilithibitishwa na malipo ya mahari na hivyo alikuwa na haki ya kudai sehemu ya mali iliyopatikana wakati wa ndoa. Hata hivyo, mawakili wa Chivayo walidai ndoa hiyo haikuwa imesajiliwa rasmi na hivyo Madzikanda hakuwa na haki ya baadhi ya madai yake. Mawakili hao pia walidai Madzikanda alikuwa amemaliza uhusiano huo alipompa Chivayo gupuro Februari 2024. Katika mila za Kishona, gupuro ni ishara inayotolewa mbele ya mashahidi au familia kuashiria kuvunjika kwa ndoa. Madzikanda alipinga hoja hiyo akisema uhusiano huo haukuweza kuvunjwa kwa kitendo hicho pekee na kwamba mahakama ilipaswa kuamua. Juni 2026, Chivayo alijaribu kuondoa madai ya mali na mali nyingine kutoka kwa kesi hiyo, lakini Mahakama Kuu ilikataa ombi lake na kumtaka alipe gharama ya kesi. Jaji Fatima Maxwell alisema Chivayo alikuwa tayari amekubali kumlipa Madzikanda Sh649 milioni na kwamba makubaliano waliyotia saini yaliacha suala la kuvunjwa kwa ndoa yao liamuliwe katika kesi kuu. Kabla ya mzozo huo, Madzikanda alikuwa mhasibu mjini Harare, aliwahi kufanya kazi katika kampuni ya Ernst & Young na alikuwa na shughuli zake za kibiashara. Haijulikani wawili hao walikutana vipi. Tangu kifo cha Chivayo Jumatano, Madzikanda hajatoa taarifa yoyote ya umma iliyothibitishwa kuhusu kifo chake.

VUGUVUGU la kisiasa la Linda Mwananchi linaloongozwa na Seneta wa Nairobi, Edwin Sifuna, limepata afueni baada ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa kuidhinisha jina la chama hicho kwa muda wa siku 90. Hata hivyo, hatua hiyo imeibua changamoto mpya za kisiasa na kiutawala ambazo zinaweza kuchelewesha uzinduzi wa chama hicho. Msajili wa Vyama vya Kisiasa alitoa kibali hicho kufuatia uamuzi wa Jopo la Kutatua Migogoro ya Vyama vya Kisiasa ulioagiza ombi la Linda Mwananchi Movement (LLM) kupitiwa upya. Uamuzi huo ulijiri siku chache kabla ya tarehe ambayo viongozi wa vuguvugu hilo walikuwa wametaja kuzindua rasmi chama chao. Seneta wa Vihiga, Godfrey Osotsi, ambaye ni mmoja wa viongozi wa Linda Mwananchi, hakuthibitisha tarehe mpya ya uzinduzi na kusema wananchi wataarifiwa kwa wakati ufaao. Lakini kibali hicho kimefungua mjadala mkubwa kuhusu mwelekeo wa kisiasa wa kundi hilo. Swali kuu ni iwapo Bw Sifuna atatumia Linda Mwananchi kama chama kipya kabisa au atachukua moja ya vyama ambavyo washirika wake wamesajili kama njia mbadala. Kwa muda, viongozi wa kundi hilo walikuwa wakichunguza uwezekano wa kutumia vyama vilivyosajiliwa tayari baada ya jina la Linda Mwananchi kukataliwa hapo awali. Mojawapo ni United Democratic Party (UDP), chama kilichohusishwa na marehemu Cyrus Jirongo na ambacho kina uhusiano na Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya. Hata hivyo, mpango huo umekwama kutokana na pingamizi kutoka kwa baadhi ya maafisa wa chama hicho waliopinga mabadiliko ya uongozi na mipango ya kukigeuza kuwa chombo cha kisiasa cha Bw Sifuna katika uchaguzi mkuu wa 2027. Mahakama pia ilizuia kwa muda hatua ya kutangaza kiongozi mpya au mgombea urais kupitia chama hicho. Wadadisi wa siasa sasa wanasema Bw Sifuna analazimika kuamua haraka ikiwa ataendelea kujenga Linda Mwananchi kama chama kipya au kuachana na mchakato huo na kutumia mojawapo ya vyama vilivyopo. Changamoto nyingine ni kwamba viongozi mbalimbali wa chama hicho tayari wamepata vyama vyao binafsi. Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino ana chama cha Mwananchi Party, Mbunge wa Saboti Caleb Amisi ameanzisha People's Renaissance Movement, huku Seneta wa Kakamega Boni Khalwale akiwa na United Patriotic Movement (UPM) kilichosajiliwa kikamilifu. Kwa upande mwingine, Gavana wa Siaya James Orengo amechukua uongozi wa Liberal Democratic Party (LDP), chama chenye historia kubwa ya kisiasa nchini kutokana na uhusiano wake wa zamani na Raila Odinga. Kuibuka kwa vyama hivi kumefanya hali kuwa tata zaidi. Wachambuzi wanasema viongozi hao lazima waamue ikiwa vyama vyao vitasalia huru, vitaungana chini ya mwavuli mmoja au vitakuwa washirika katika muungano wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Sheria ya vyama vya kisiasa pia inaweka masharti magumu kwa chama kipya kusajiliwa kikamilifu. Mbali na kupata usajili wa muda, chama lazima kiwe na wanachama wasiopungua wapigakura 1,000 katika zaidi ya nusu ya kaunti za Kenya, pamoja na kuonyesha uwakilishi wa kikabila, kijinsia na makundi maalum. Vuguvugu hilo pia linakabiliwa na muda mfupi wa kutimiza masharti hayo kwani jina la Linda Mwananchi limehifadhiwa kwa siku 90 pekee. Wakati huohuo, madai ya umiliki wa jina hilo bado yanaendelea. Charles Wanyonyi amedai kuwa aliomba kusajili chama chenye jina la Linda Mwananchi Party of Kenya mapema zaidi kuliko kundi la Bw Sifuna na ametaka ombi lake kupewa kipaumbele. Mbali na suala la chama, kundi hilo pia linakabiliwa na changamoto ya uongozi. Hivi majuzi viongozi wake walimteua Bw Sifuna kuwa mgombea wao wa urais, lakini Bw Orengo, ambaye pia alikuwa ametangaza kuwania tiketi hiyo, hakuhudhuria mkutano huo. Hatua yake ya kuchukua LDP imezua maswali kuhusu mustakabali wa Linda Mwananchi. Wengine wanahisi kuwa chama hicho kinaweza kuwa jukwaa kuu la Bw Sifuna, huku wengine wakiamini vuguvugu hilo litaishia kuwa muungano wa vyama kadhaa vinavyounganishwa na lengo la kisiasa la pamoja. Kwa sasa, ushindi wa kisheria wa kupata jina la Linda Mwananchi umeondoa kikwazo kimoja pekee. Changamoto kubwa inayomkabili Bw Sifuna na washirika wake ni kuamua ni mfumo upi wa kisiasa utakaounganisha maslahi ya viongozi ambao tayari wanaanza kujijengea vyama vyao kuelekea uchaguzi wa 2027.

By Ozioruva Aliu BENIN CITY – PROMINENT journalist, activist and lawyer, Richard Akinnola, on Friday expressed concern about the current state of the judiciary in Nigeria and said that it was more independent and fearless under the military era than under the democratic dispensation. He said that even though there are a number of judges […]

Demands review of long-distance NYSC postings By Adeola Badru IBADAN — The National Association of Nigerian Students (NANS), Southwest Zone D, has raised concern over alleged ransom demands of up to ₦50 million for some prospective National Youth Service Corps (NYSC) members abducted while travelling from Ibadan to their orientation camps. The association also called […]

African start-ups raised $2 billion in the first half of 2026, representing a 67 percent growth compared to a year earlier.

DODOMA: WAZIRI wa Ujenzi, Masanja Kadogosa, amesema atashirikiana kwa karibu na viongozi na watumishi wa wizara hiyo kuhakikisha miradi inayotekelezwa katika Sekta ya Ujenzi inatekelezwa kwa weledi na ufanisi, kwa lengo la kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali katika kuendeleza miundombinu nchini. Kadogosa ameyasema hayo leo, Oktoba 2, 2026, katika Ofisi za Wizara ya Ujenzi, Mtumba…

Thousands of rural residents will have their electricity connection fees covered under a new financing scheme involving Tanzania Electric Supply Company (Tanesco) and CRDB Bank, as the government seeks to make electricity more accessible to households and businesses. Under the programme, rural and village residents who cannot afford the connection fee will have the Sh27,000 cost paid by CRDB Bank without having to repay the money. Urban residents will instead access loans of up to Sh320,000 from CRDB to cover the cost of connecting their homes to electricity, which they will repay gradually. The programme, launched yesterday, Friday, October 2, 2026, operates under the slogan “Kila Kaya Itawaka” (Every Household Will Have Electricity). Speaking after launching the initiative, Vice President Deogratius Ndejembi said the government was seeking to ensure electricity reached every Tanzanian because of its role in supporting economic activities and improving household welfare. He also challenged Tanesco, CRDB and other financial institutions to explore a system that would allow customers to borrow electricity credit through mobile money and banking platforms. He said such a system could help households that run out of electricity credit but do not have immediate cash to continue accessing the service. “Just as mobile networks allow people to borrow airtime, we should find a way for people to borrow electricity and repay it later,” Mr Ndejembi said. He suggested that a customer who borrowed electricity worth Sh2,000 could repay Sh2,100, with the additional Sh100 serving as the cost of the service. “If it is possible with mobile networks, it is also possible here so that every Tanzanian can have access to electricity while the borrowing limit increases as they continue repaying,” he said. Mr Ndejembi said the government had also recognised that some urban areas had living conditions similar to rural communities and should therefore benefit from the lower connection fee. “There are areas that are officially urban but look like villages. The people living there have rural conditions, yet they are required to pay Sh320,000 to connect to electricity. To achieve our goals, such a person should pay Sh27,000,” he said. He said Tanzania had made significant progress in expanding electricity access, with all 12,318 villages now connected to electricity. Energy Minister Juma Homera said the government would ensure that its plans and strategies were implemented to achieve universal electricity access. Tanesco managing director Lazaro Twange said the utility currently had more than 6.4 million customers and was expected to connect 1.7 million new customers annually. He said achieving the target required adequate infrastructure, reliable electricity supply and partnerships that could address financial barriers faced by some customers. “Some customers cannot afford the connection costs. To address this, partnerships are necessary, which is why CRDB is supporting the initiative,” Mr Twange said. He said rural and small-settlement residents would receive the Sh27,000 connection subsidy without repayment, while urban customers requiring Sh320,000 would access loans through CRDB. CRDB managing director Abdulmajid Nsekela said the bank had joined the initiative because not every Tanzanian could afford the cost of connecting to electricity. He said the partnership was intended to support households and businesses and contribute to the objectives of Tanzania Development Vision 2050. The programme initially covers five districts, with CRDB targeting to support electricity connections for 500,000 Tanzanians annually. Mr Nsekela said electricity would also allow rural businesses to extend their operating hours and improve productivity. Chairperson of the Parliamentary Standing Committee on Energy and Minerals Subira Mgalu said MPs, village leaders and street leaders would help identify households with the greatest need for the programme. Chamwino District Commissioner Janeth Mayanja said the initiative would provide an opportunity for people who had been unable to connect to electricity despite power infrastructure reaching their areas. Nyasa District Commissioner Peres Magiri said all villages in the district had electricity, but only 150 of its 421 hamlets were connected, making the programme important in expanding access. Dar es Salaam Regional Commissioner Albert Chalamila said the region had about 5.3 million people according to the 2022 Population and Housing Census, with Dar es Salaam and Pwani jointly consuming more than 800 megawatts, driven by industries and other economic activities.

The Peoples Democratic Party, PDP, in Cross River State, Friday raised the alarm over alleged gun attacks by hoodlums on its consultative meetings in Calabar South Local Government Area, which left three persons injured and several vehicles damaged.

The U.S. Citizenship and Immigration Services (USCIS) will introduce new fees for the EB-5 Immigrant Investor Program from November 30, 2026.

DAR ES SALAAM: MAKAMU wa Rais, Deogratius Ndejembi, amesema Mpango wa Ufadhili wa Uunganishaji Umeme kwa Wananchi unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Benki ya CRDB, utarahisisha upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi wa mijini na vijijini na kuongeza fursa za maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Akizungumza leo Oktoba 2,…

DAR ES SALAAM: THE Tanzanian Vice President, Deogratius Ndejembi, has witnessed the signing and launch of a landmark financing scheme aimed at helping more Tanzanians access electricity, through a partnership between Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) and CRDB Bank. The signing ceremony was held on October 2, 2026, at the Julius Nyerere International Convention Centre…

GEITA; Jeshi la Polisi mkoani Geita linamshikilia Faustine Zakaria, ambaye ni kinyozi kwa tuhuma za kuharibu kwa makusudi fedha halali za Tanzania kinyume na sheria za nchini. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Safia Jongo, ametoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari na kueleza kuwa Faustine alionekana akitenda kosa hilo…

Ethiopia and Eritrea have severed diplomatic relations as renewed fighting in Ethiopia’s northern Tigray region raises fears of a wider conflict in the Horn of Africa. The diplomatic rupture followed Ethiopia’s decision on Thursday to close its embassy in Asmara and expel 10 Eritrean diplomats, including the country’s chargé d’affaires and diplomats accredited to the […]

KILIMANJARO; Serikali ya Tanzania imeendelea kuchukua hatua madhubuti kuimarisha na kuinua vyama vya ushirika nchini, kwa lengo la kuhakikisha vinaendeshwa kwa uwazi, uadilifu na uwajibikaji na vinawanufaisha wananchi, hususan wakulima. Kupitia usimamizi wa Mrajis wa Vyama vya Ushirika Taifa, Serikali imeendelea kutafuta suluhisho la changamoto zinazovikabili vyama vya ushirika, ikiwemo migogoro, madeni ya muda mrefu,…

KIGOMA: Serikali imezitaka kamati za maafa katika mikoa na wilaya nchini kuchukua tahadhari mapema dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Niño, ikiwemo kutambua maeneo hatarishi na kuwaandaa wananchi kuondoka kabla ya maafa kutokea. Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Watu wenye Ulemavu, Lina Kitosi, amesema kuchukua tahadhari…

DAR ES SALAAM: Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila hulaza wagonjwa kati ya watano na saba wenye kiharusi kila siku, hali inayodhihirisha ukubwa wa tatizo hilo na umuhimu wa jamii kuongeza uelewa kuhusu ugonjwa huo. Daktari Bingwa Bobezi wa Magonjwa ya Ubongo na Mishipa ya Fahamu kutoka hospitalini hapo, Dk Brighton Mushengezi, amesema kiharusi kinaendelea kuwa changamoto…

By Providence Ayanfeoluwa Tension is mounting in Igando Peace Estate Phase IV as residents raise alarm over persistent illegal dumping of refuse at a government-closed dumpsite adjacent to their community. The site, located near Lanre Bus-Stop along the Isheri-Igando Expressway, was officially decommissioned by the Lagos State Government years ago. However, residents say waste transport […]

Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo Mutahi Kagwe amewataka wakulima nchini kutumia teknolojia, huduma za kidijitali na mbinu za kilimo zinazozingatia mabadiliko ya tabianchi ili kukabiliana na hali ya hewa isiyotabirika, gharama kubwa ya uzalishaji na kupungua kwa rutuba ya ardhi. Akizungumza Jumatano wakati wa ufunguzi rasmi wa Maonesho ya 125 ya Kimataifa ya Biashara ya Nairobi katika Uwanja wa Jamhuri, Kagwe alisema teknolojia inaweza kuwasaidia wakulima kufanya maamuzi bora kuhusu mazao ya kupanda, wakati wa kupanda, pembejeo za kutumia na masoko ya kuuza mazao yao. Alisema mustakabali wa sekta ya kilimo hautategemea serikali pekee bali ushirikiano kati ya wakulima, watafiti, wawekezaji, sekta ya binafsi pamoja na serikali za kitaifa na kaunti. Maonesho hayo ya siku saba yaliyoanza Septemba 28 na yatakamilika Oktoba 4 yamewaleta pamoja wakulima, wafugaji, watafiti na kampuni za teknolojia kuonyesha ubunifu mbalimbali chini ya kaulimbiu ya kuendeleza kilimo kinachozingatia tabianchi kwa ukuaji endelevu wa uchumi. Baadhi ya teknolojia zinazoonyeshwa ni matumizi ya Akili Unde (AI), droni, vifaa vya unyunyuzaji, mashine za kilimo, mifugo bora, teknolojia za afya ya mifugo na mbegu za mazao yanayostahimili ukame. Kagwe alisema mabadiliko ya tabianchi, gharama kubwa ya uzalishaji na mahitaji mapya ya soko yanawalazimu wakulima kubadilisha mbinu zao za uzalishaji. Alionya kuwa ukame na mafuriko yanayosababishwa na tabianchi yanagharimu uchumi wa Kenya kiasi kikubwa kila mwaka kupitia hasara ya mazao, mifugo na masoko. Alisema serikali inaimarisha huduma za kidijitali katika sekta ya kilimo ikiwemo usajili wa wakulima, huduma za nyanjani, bima na upatikanaji wa pembejeo. Kulingana naye, takriban wakulima 8.9 milioni tayari wamesajiliwa katika mfumo wa kitaifa wa usimamizi wa taarifa za kilimo. Waziri huyo pia alisisitiza umuhimu wa kupima afya ya udongo kabla ya kutumia mbolea. Alisema asilimia 63 ya udongo nchini una kiwango kikubwa cha asidi, hali inayopunguza uzalishaji. “Ni makosa kutumia pembejeo bila kufanya uchunguzi wa kisayansi wa hali ya udongo,” alisema. Wakati huo huo, serikali imeanzisha mradi wa kitaifa wa uchunguzi wa udongo kwa njia za kidijitali kwa ushirikiano na Shirika la Utafiti wa Kilimo na Mifugo Kenya (KALRO). Kagwe aliongeza kuwa serikali inawekeza katika afya ya mifugo, mbegu bora, uzalishaji wa maziwa na upanuzi wa masoko ya nyama na bidhaa nyingine za mifugo ili kuongeza mapato ya wakulima. Aliwataka wakulima, wawekezaji na wadau wengine kutumia maonesho hayo kuunda ushirikiano na kupanua matumizi ya teknolojia zinazoweza kuongeza uzalishaji wa chakula na kuboresha mapato katika sekta ya kilimo.

MAHAKAMA ya Mazingira na Ardhi imeamuru Serikali ya Kaunti ya Mombasa kuwalipa zaidi ya wakazi 200 wa eneo la Mwakirunge fidia ya Sh350 milioni kutokana na ukiukaji wa haki yao ya kuishi katika mazingira safi na salama uliosababishwa na uchafuzi kutoka jaa la taka eneo hilo. Katika uamuzi wake, Jaji Lucas Naikuni alisema wakazi hao, wakiongozwa na mwanaharakati wa mazingira Ainea Ragen, walithibitisha kuwa jaa hilo limekuwa likasababisha madhara ya muda mrefu kwa maisha yao. Jaji huyo alibaini kuwa Serikali ya Kaunti ya Mombasa pamoja na Mamlaka ya Kitaifa ya Kusimamia Mazingira (NEMA) walishindwa kuchukua hatua za kutosha kuzuia na kudhibiti uchafuzi wa mazingira unaotokana na shughuli za jaa la Mwakirunge. “Jaaa la Mwakirunge limekuwepo kwa muda mrefu na bado linaendelea kufanya kazi hadi leo. Hivyo basi haki ya wakazi ya kuishi katika mazingira safi na yenye afya inaendelea kukiukwa,” alisema jaji huyo. Mahakama ilisema ushahidi uliowasilishwa ulionyesha kuwa hatua na uzembe wa maafisa ulisababisha madhara ya kimazingira na kukiuka Kifungu cha 42 cha Katiba, kinachohakikisha kila mtu ana haki ya mazingira safi na yenye afya. Mbali na fidia hiyo, mahakama pia imeamuru kaunti hiyo kuanza mara moja ujenzi wa ukuta wa simiti kuzunguka jaa hilo. Ukuta huo unatakiwa kuwa na urefu wa angalau mita sita, uwe na milango salama ya kuingilia na kutoka. Kaunti imepewa muda wa miezi 12 kukamilisha kazi hiyo na pia kuweka walinzi wa kutosha pamoja na mfumo wa kudhibiti watu wanaoingia katika eneo hilo. Aidha, mahakama imeagiza serikali ya kaunti kuandaa na vifaa vya kisasa vya kuchoma taka vinavyokidhi viwango vya kimataifa vya afya na usalama. Hata hivyo, jaji alikataa ombi la wakazi kutangaza kipande hicho cha ardhi ya ekari 50 kuwa ardhi ya jamii, uamuzi uliomaanisha kuwa jaa hilo halitahamishwa kwa sasa.

DAR ES SALAAM: A SEEDLING in a nursery is a promise. A living forest is proof. For years, the environmental response to tobacco curing in Tanzania has followed a familiar equation: wood is consumed, therefore trees must be planted. Millions of seedlings have been raised, nurseries established and woodlots promoted. Yet the harder question remains:…

DODOMA: TUME ya Utumishi wa Walimu (TSC) imewataka walimu wote nchini kuisoma, kuielewa na kuitekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, hususan nguzo ya pili inayohusu uwezo wa watu na maendeleo ya jamii. Nguzo hiyo inalenga kujenga taifa lenye watu wenye ujuzi, maarifa na uwezo wa kukabiliana na ushindani katika dunia inayobadilika kwa kasi. Wito…

KAUNTI ya Lamu imeandika historia mpya baada ya Uwanja wa Ndege wa Manda kupokea safari za ndege za kimataifa kwa mara ya kwanza, hatua inayotarajiwa kufungua fursa mpya za biashara, utalii na uwekezaji kufuatia uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Kiwanda cha Kusafisha Mafuta cha Dangote cha Shilingi trilioni mbili. Mnamo Jumatano, ndege aina ya Boeing 737-800 iliyombeba Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ilitua katika uwanja huo saa nne na dakika arubaini na nne asubuhi. Ndege nyingine zilifika kutoka Nigeria, Ethiopia na Uganda, jambo lililoashiria kuimarika kwa hadhi ya Lamu katika mtandao wa usafiri wa anga wa Afrika Mashariki. Sherehe ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi huo mkubwa pia ilileta ndege za kifahari zikiwemo Gulfstream G500 na G600, Embraer Legacy 600 pamoja na Global Express 900. Helikopta kadhaa nazo zilitua katika eneo la Bandari ya Lamu. Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Kenya (KAA) ilisema kupokelewa kwa ndege hizo ni ishara kuwa Lamu sasa inaingia katika jukwaa la kimataifa. Mafanikio hayo yamechangiwa na ukarabati wa njia ya kurukia ndege yenye urefu wa kilomita mbili na upana wa mita 30. Waziri wa Uchukuzi Davis Chirchir alisema serikali imeboresha miundombinu ya uwanja huo na ina mpango wa kuujenga upya kabisa ili kuendana na mahitaji ya baadaye ya eneo la Lapsset na mji mkuu mpya unaotarajiwa kukua Lamu. “Lamu itakuwa mji ambao wengi hawakuwahi kufikiria wangeuona katika maisha yao. Uchumi wake utabadilika pamoja na ule wa Kenya na eneo lote,” alisema Chirchir. Wadau wa biashara wanaamini mradi wa Dangote utachochea ukuaji mkubwa wa uchumi wa eneo hilo. Rais wa Chama cha Kitaifa cha Wafanyabiashara na Viwanda Kenya (KNCCI), Dkt Erick Rutto, alisema nafasi za kazi zaidi ya 60,000 zinazotarajiwa kuundwa wakati wa ujenzi zitafungua fursa nyingi kwa wenyeji. Alisema sekta za biashara, uvuvi, makazi na huduma zitanufaika kutokana na ongezeko la wafanyakazi na wageni watakaomiminika Lamu. Gavana wa Lamu Issa Timamy alihakikisha kuwa serikali ya kaunti itashirikiana kikamilifu na wawekezaji ili kuhakikisha mradi huo unafanikiwa. Aliwahimiza wakazi kupata ujuzi utakaowasaidia kupata ajira zinazotarajiwa kuibuka. Hata hivyo, aliwataka wawekezaji kuhakikisha mazingira, mikoko, fukwe na urithi wa kitamaduni wa Lamu unalindwa ipasavyo. Kwa upande wake, bilionea wa Nigeria Aliko Dangote aliahidi kuwa mradi huo utatekelezwa kwa kuzingatia viwango vya juu vya kulinda mazingira huku ukiwafaidi wananchi wa Kenya na Afrika Mashariki. Rais William Ruto alisema Lamu, ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikionekana kama eneo lililosahaulika kutokana na idadi ndogo ya wakazi, sasa itakuwa kitovu kipya cha maendeleo ya taifa. Kwa mujibu wa takwimu za sensa ya mwaka 2019, Lamu ndiyo kaunti yenye idadi ndogo zaidi ya watu nchini, ikikadiriwa kuwa na wakazi 175,705 mwaka 2025. Hata hivyo, uwekezaji mkubwa unaoingia katika eneo hilo unatarajiwa kubadilisha sura ya uchumi wake kwa miaka ijayo.

Lawyers, human rights advocates and child protection experts have raised concerns over a rise in the number of children among convicted prisoners in Tanzania, calling for greater use of rehabilitation and alternatives to imprisonment.

ARUSHA: RAIS wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dk Tulia Ackson, amesema mageuzi yaliyofanywa ndani ya jumuiya hiyo yamewezesha mabunge kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia bila kulazimika kuchagua jambo moja pekee. Dk Tulia amesema hayo leo jijini Arusha mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kushiriki mkutano wa IPU, akieleza kuwa mabadiliko hayo ni miongoni…

WABUNGE wametishia kufanya mabadiliko yatakayoweka vizuizi kwa uhuru wa vyombo vya habari kutokana na uchapishaji wa madai ambayo hayajathibitishwa kuhusu ukiukaji wa taratibu za uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027. Wabunge hao walitaka Baraza la Habari Kenya (MCK) kuchukua hatua dhidi ya vyombo vya habari wanavyolaumu kwa kuwapotosha wananchi kupitia taarifa kuhusu maandalizi ya uchaguzi ujao. Kwa mujibu wa wabunge hao, baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikichapisha madai yasiyo na ushahidi kuhusu mfumo wa uchaguzi, jambo ambalo linaweza kudhoofisha imani ya wananchi katika matokeo ya uchaguzi na hata kuchochea vurugu. Wakilenga hasa shirika la habari la Standard Group, walidai kuwa limekuwa likitumia majukwaa yake kuendeleza ajenda za kisiasa kupitia taarifa zake za uchaguzi. Hata hivyo, katika toleo lake la Septemba 30, Standard Group ilisema haitatishwa wala kulegeza msimamo wake katika kutekeleza majukumu ya uandishi wa habari. “Kiwango chochote cha vitisho hakitatuzuia kuendelea kutekeleza uandishi wa habari wa hali ya juu. Hatutatishwa wala kulazimishwa kunyamaza,” ilisema kampuni hiyo katika taarifa. Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Kitaifa, Junet Mohamed, alisema ingawa uhuru wa vyombo vya habari unalindwa na Katiba, kuna wajibu wa kuhakikisha wananchi wanapata taarifa za kweli. “Sote tunatambua uhuru wa vyombo vya habari, lakini hakuna uhuru wa kueneza propaganda zinazowapotosha Wakenya. Kila mwaka tunapitisha bajeti ya MCK lakini taasisi hiyo inaendelea kutazama bila kuchukua hatua,” alisema mbunge huyo wa Suna Mashariki. Alisema madai yasiyothibitishwa kuhusu uchaguzi wa 2027 yanaweza kuwafanya wananchi kukosa imani na matokeo ya uchaguzi. Kwa upande wake, Mbunge wa Homa Bay Town, Peter Kaluma, alitaka hatua kali zichukuliwe dhidi ya vyombo vya habari vinavyosambaza taarifa za kupotosha. “Tukiacha hali hii iendelee, tunaweza kujikuta tukifuata mkondo uliosababisha mauaji ya kikabila nchini Rwanda mwaka 1994. Tunahitaji hatua kali na hata uhuru wa vyombo vya habari unaweza kuwekewa mipaka,” alisema. Naibu Spika wa Bunge la Kitaifa, Gladys Boss, alisema madai ya mara kwa mara kuhusu wizi wa kura yanaweza kusababisha taharuki na vurugu baada ya uchaguzi. “Tunapoanza kueneza madai kwamba mfumo wa uchaguzi una mianya, wananchi wataacha kuamini matokeo ya mwisho na hali hiyo inaweza kusababisha machafuko,” alisema. Bi Boss pia alipinga madai kuwa uchaguzi uliopita uliibwa, akisema aliwahi kushiriki katika uhakiki wa matokeo kwa niaba ya Mahakama ya Juu alipokuwa Msajili Mkuu wa Idara ya Mahakama. Wakati huo huo, mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Erastus Ethekon, alikanusha madai yaliyosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba tume hiyo imekuwa ikisajili raia wa Uganda kuwa wapigakura nchini Kenya. Bw Ethekon alisema tume imepokea kwa masikitiko taarifa hizo ambazo hazina ushahidi na ambazo zinaweza kudhoofisha imani ya umma katika uadilifu wa uchaguzi. “Hakuna mtu, kundi au taasisi ambayo imewasilisha ushahidi wa kuaminika unaothibitisha madai hayo ya ukiukaji wa sheria,” alisema. Aliongeza kuwa ikiwa ushahidi wa kweli utawasilishwa, IEBC itachukua hatua za kinidhamu na za kisheria dhidi ya yeyote atakayebainika kuhusika.

CHANGAMOTO mpya imeibuka kuhusu umiliki wa jina la chama cha kisiasa cha Linda Mwananchi, huku Bw Charles Wanyonyi akidai kuwa ombi lake la kusajili jina hilo lilitangulia lile linalohusishwa na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kwa zaidi ya miezi mitatu. Kupitia mawakili wake, Bw Wanyonyi ameandikia Msajili wa Vyama vya Kisiasa akitaka ombi lake lililowasilishwa Februari 24, 2026 lipewe kipaumbele, akisema haliwezi kuondolewa na muombaji aliyefuata baadaye. Hatua hiyo imejiri siku moja baada ya Jopo la Kutatua Mizozo ya Vyama vya Kisiasa kubatilisha uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Kisiasa wa kukataa ombi la washirika wa Bw Sifuna la kusajili jina la Linda Mwananchi Movement (LMM). Mahakama ilikubali rufaa iliyowasilishwa na Mbunge wa Suba Kusini Caroli Omondi, mwanaharakati Pauline Njoroge na rais wa zamani wa Chama cha Wanasheria Kenya (LSK) Faith Odhiambo. Jopo hilo liliagiza Msajili achunguze upya ombi lao ndani ya siku saba. Kulingana na stakabadhi za kesi, waombaji hao walikuwa wamependekeza majina sita yanayojumuisha maneno “Linda Mwananchi”. Majina hayo ni Linda Mwananchi Alliance, Linda Mwananchi Alliance of Kenya, Linda Mwananchi Coalition, Linda Mwananchi Party, Linda Mwananchi Party of Kenya na Linda Mwananchi People’s Party. Barua ya Oktoba 1 kutoka kwa kampuni ya mawakili ya Wanzau, Odhiambo & Associates inaonyesha kuwa Bw Wanyonyi aliwasilisha ombi la kusajili jina la “Linda Mwananchi Party of Kenya” mnamo Februari 24, 2026, ilhali kundi la Omondi, Njoroge na Odhiambo liliwasilisha ombi lao Juni 4. “Mteja wetu aliwasilisha ombi lake zaidi ya miezi mitatu kabla ya waombaji wengine. Kipaumbele kinachotokana na ombi hilo hakiwezi kuondolewa kisheria na ombi la baadaye lenye jina sawa au linalofanana kwa kiasi kikubwa,” mawakili hao walisema. Wamemtaka Msajili kushughulikia na kuhifadhi jina hilo kwa niaba ya Bw Wanyonyi, wakinukuu Kifungu cha 4B cha Sheria ya Vyama vya Kisiasa. Awali, ombi la Bw Wanyonyi lilikataliwa kwa madai kuwa lilifanana na kaulimbiu iliyohifadhiwa ya “Linda Mkenya, Boresha Kenya” pamoja na sababu za maslahi ya umma. Hata hivyo, hakukata rufaa dhidi ya uamuzi huo katika mahakama hiyo. Katika uamuzi wake, mahakama ilisema Msajili hakutoa maelezo ya kutosha kuhusu sababu za maslahi ya umma zilizotumiwa kukataa ombi la kundi la Bw Sifuna. Jopo hilo pia lilichunguza chama cha Liberty National Democratic Alliance (LINDA) na kubaini kuwa hakikuwa chama kilichosajiliwa kikamilifu wala kwa muda. Mahakama ilisema uhifadhi wa jina la LINDA uliisha moja kwa moja baada ya siku 90 tangu ombi lake la Novemba 2025. Pia ikabaini kuwa Msajili hakuwa na mamlaka ya kufufua uhifadhi huo kupitia barua ya Agosti 14, 2026. Aidha, jopo hilo lilikataa hoja kwamba jina la Linda Mwananchi linafanana na kifupi cha LINDA. Lilisema “Linda” ni neno la Kiswahili linalomaanisha kulinda au kutetea, huku LINDA ikiwa kifupi cha Liberty National Democratic Alliance. Mahakama iliongeza kuwa hakukuwa na msingi wa kuzuia usajili wa Linda Mwananchi Movement kwa misingi ya kufanana kwa majina. Ilibatilisha uamuzi wa Msajili wa Agosti 7 na kuagiza ombi la kusajili Linda Mwananchi Movement na kifupi chake LMM lichunguzwe upya ndani ya siku saba. Hata hivyo, barua ya Oktoba 1 sasa imetoa changamoto mpya kwa msajili kuamua kati ya ombi la awali la Bw Wanyonyi na agizo la mahakama la kushughulikia upya ombi la washirika wa Bw Sifuna.

KIFO cha mfanyabiashara maarufu wa Zimbabwe, Wicknell Chivayo, katika ajali ya helikopta Septemba 30 kimefunga sura ya maisha ya mtu ambaye kwa miaka mingi alijijengea sifa ya kuwa karibu sana na baadhi ya viongozi wenye ushawishi mkubwa zaidi barani Afrika. Ingawa alikuwa raia wa Zimbabwe mwenye asili ya Eswatini, Chivayo alionekana kuwa raia wa Afrika nzima. Kupitia mitandao yake ya kijamii, mara kwa mara alionekana akiwa katika ikulu mbalimbali, mikutano ya viongozi wakuu, sherehe za kifahari na hafla za watu mashuhuri. Alikuwa maarufu kwa maisha ya anasa. Magari ya Rolls-Royce, Range Rover, ndege binafsi, helikopta, saa za thamani kubwa na mavazi ya wabunifu maarufu yalikuwa sehemu ya maisha yake. Lakini zaidi ya mali hiyo, kilichovutia wengi ni uwezo wake wa kupata nafasi karibu na marais, wafalme na wafanyabiashara wakubwa wa Afrika. Kwa mashabiki wake, Chivayo alikuwa mfano wa mtu aliyeinuka kutoka hali ya kawaida hadi utajiri mkubwa. Walimuona kama mfadhili aliyesaidia watu wengi kwa mali yake. Kwa wakosoaji wake, alikuwa mfano wa uhusiano wa karibu kati ya wafanyabiashara na viongozi wa kisiasa, jambo ambalo lilizua maswali kuhusu chanzo cha utajiri wake na jinsi alivyopata ushawishi mkubwa. Safari yake haikuwa rahisi. Mwaka 2005, Mahakama Kuu ya Zimbabwe ilimhukumu kifungo cha miaka mitano gerezani baada ya kupatikana na hatia katika kesi ya ulanguzi wa fedha iliyohusisha zaidi ya Sh6.6 milioni. Hata hivyo, baadaye alikata rufaa na hukumu hiyo ikabatilishwa. Baada ya kutoka gerezani, alijijenga upya katika ulimwengu wa biashara. Alianzisha kampuni ya Intratrek Zimbabwe, iliyojihusisha na miradi ya nishati na miundombinu. Kupitia kampuni hiyo, alipata kandarasi kubwa zilizompa umaarufu nchini Zimbabwe. Hata hivyo, shughuli zake za biashara hazikukosa migogoro. Alikabiliwa na mashtaka kadhaa kuhusiana na mradi wa nishati ya jua wa Gwanda. Mwaka 2019 mahakama ilifutilia mbali mashtaka hayo, jambo lililompa ushindi mkubwa wa kisheria. Na biashara zake zilivyokua, ndivyo mtandao wake wa viongozi ulivyopanuka. Nchini Zimbabwe alihusishwa kwa karibu na Rais Emmerson Mnangagwa. Pia alionekana akiwa karibu na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Mfalme wa Eswatini Mswati III, Rais wa Nigeria Bola Tinubu, Rais wa Zambia Hakainde Hichilema, Rais wa Msumbiji Daniel Chapo, na aliyekuwa Rais wa Malawi Peter Mutharika. Nchini Kenya, uhusiano wake na Rais William Ruto ulivutia hisia nyingi. Chivayo alizuru Kenya mara kadhaa na kupigwa picha akiwa Ikulu na rais huyo. Mwezi Agosti, alisambaza video iliyomuonyesha Rais Ruto akiendesha gari kumsindikiza kuelekea helikopta yake baada ya kuhudhuria hafla ya harusi ya kitamaduni ya binti ya rais, Charlene Ruto, huko Kilgoris, Narok. Baada ya kifo chake, Rais Ruto alimuomboleza Chivayo kama rafiki wa karibu. Chivayo mwenyewe alikuwa amesisitiza kuwa urafiki wao ulitokana na imani, ushauri na heshima, na si biashara au zabuni za serikali. Lakini kilichomfanya kuwa maarufu zaidi kwa wananchi wa kawaida ni ukarimu wake. Aligeuza utoaji zawadi kuwa sehemu ya maisha yake ya kila siku. Aliwapa wanamuziki, viongozi wa dini, marafiki, mawakili na watu mbalimbali magari ya kifahari pamoja na fedha nyingi. Katika maadhimisho ya miaka 83 ya kuzaliwa ya Rais Mnangagwa, Chivayo alitoa magari 10 ya Toyota Land Cruiser pamoja na ambulansi. Mara nyingi alisema kuwa ukarimu wake ulitokana na maisha magumu aliyopitia utotoni. Hata siku ya mwisho wa maisha yake aliendelea na utamaduni huo. Asubuhi ya Septemba 30, aliandika katika mitandao ya kijamii kuwa angewapa washirika wake wa muda mrefu zawadi za magari ya kifahari na mamia ya maelfu ya dola za Amerika kama ishara ya shukrani kwa urafiki wao. Saa chache baadaye, helikopta aliyokuwa akisafiria pamoja na mkewe Lucy “Lulu” Muteke ilianguka na kuua wote waliokuwa ndani. Maisha yake binafsi pia yalikuwa na misukosuko. Mahusiano yake ya zamani na Sonja Madzikanda, ambaye walizaa watoto wawili, yaliishia katika vita mahakamani kuhusu mali na matunzo ya watoto. Baadaye alimuoa Lucy Muteke mwaka 2025, ambaye alikuwa naye katika safari yake ya mwisho. Kwa wengi, Chivayo atasalia kuwa mfanyabiashara aliyefanikiwa, mfadhili na mtu aliyefungua milango ya urafiki na viongozi wa juu zaidi Afrika. Kwa wengine, atakumbukwa kama ishara ya ukaribu kati ya utajiri mkubwa na nguvu za kisiasa. Licha ya maoni hayo tofauti, hakuna shaka kwamba alikuwa mmoja wa wafanyabiashara waliovutia mijadala mikubwa zaidi barani Afrika. Kifo chake kimeacha maswali mengi kuhusu urithi wake, utajiri wake na nafasi yake katika siasa na biashara Afrika. Hata baada ya kuaga dunia, jina la Wicknell Chivayo linaendelea kujadiliwa na kuibua mitazamo tofauti kuhusu maisha yake ya kipekee.

IRINGA: Zikiwa zimepita mbili tu baada ya kurejea nchini kutoka China alikokuwa katika ziara ya kikazi kwa muda wa wiki tatu, Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Jackson Kiswaga, amekutana na kula chakula pamoja na wanafunzi 145 wenye mahitaji maalumu wanaolelewa na kusoma katika shule ya msingi Kipera iliyopo jimboni mwake. Kiswaga amesema ameamua kutumia muda…

By Victor Ahiuma-Young The African Regional Organisation of the International Trade Union Confederation, ITUC-Africa, has raised concerns over the Nigeria–United States critical minerals framework, warning that Nigeria must ensure its mineral wealth contributes directly to the country’s development rather than creating another form of economic dependency.In a statement by its General Secretary, Akhator Joel Odigie, […]

U.S. Secretary of State Marco Rubio has congratulated Nigeria on its 66th Independence Anniversary, describing the country as vital to Africa’s stability and economic growth.

The former Anambra State governor also referenced the recent death of 37 young people, while raising concerns over hunger and Nigeria’s infant and maternal mortality rates.

MWANAMME mmoja na mwanamke walifariki katika matukio ya kusikitisha Kaunti ya Migori baada ya mzozo uliodaiwa kuhusisha deni la Sh700 kugeuka vurugu na hasira za wananchi. Tukio hilo lilitokea katika Kijiji cha Kamunga, ambapo Mercela Anyango aliondoka nyumbani kwake asubuhi ya Septemba 30 kwenda kudai pesa alizokuwa akidaiwa na jirani yake, Oburu Owino. Kwa mujibu wa mumewe, Kennedy Onyango Juma, mkewe alikuwa amemweleza kwamba angeenda nyumbani kwa Owino kudai pesa hizo ili kulipa baadhi ya bili za familia. Baadaye Juma aliporudi kutoka sokoni Awendo na kukuta nyumba ikiwa tupu, aliamua kumfuata mkewe nyumbani kwa jirani huyo. Hata hivyo, alipofika hakuwakuta wawili hao. “Niliamini angekuwa bado huko kwa sababu alikuwa amenieleza kuwa angeenda kudai deni hilo,” alisema Juma. Alipokuwa akirejea nyumbani, alikumbana na tukio la kutisha la mwili wa mkewe ukiwa umetupwa katika shamba la miwa karibu na eneo hilo. Kifo hicho kiliwashtua wakazi wa kijiji ambao walikusanyika haraka baada ya habari kusambaa. Hasira ziliongezeka na wakazi wakamtafuta Owino, ambaye walimtaja kuwa mshukiwa mkuu. Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Uriri, Ali Bashir, alisema maafisa walipokea taarifa kuwa kundi la wananchi wenye ghadhabu lilikuwa linamtafuta Owino. Baadaye ilibainika kuwa alikuwa ameenda Soko la Uriri. Huko ndipo wananchi walimfuata na kumshambulia na kumuua kabla ya polisi kufika eneo la tukio. Kamanda Bashir alikosoa vikali hatua ya wananchi kujichukulia sheria mkononi, akisema uchunguzi wa awali haukuwa umebaini ushahidi wowote kumhusisha Owino moja kwa moja na kifo cha Anyango. “Ukweli kwamba mwili ulipatikana karibu na nyumba yake haumfanyi kuwa muuaji. Hilo linaweza kuthibitishwa tu baada ya uchunguzi kukamilika,” alisema. Afisa huyo alisema mzozo wa deni ungeweza kutatuliwa kwa amani kupitia usaidizi wa chifu, naibu chifu au wazee wa kijiji badala ya kusababisha umwagikaji wa damu.

JARIBIO la kampuni ya Oilmax Ventures kupinga zabuni ya uchapishaji wa karatasi za kura za Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) limegonga mwamba baada ya Mahakama Kuu kubaini kuwa kampuni hiyo ilichelewa kuwasilisha kesi yake. Kampuni hiyo ilitaka kubatilisha uamuzi wa Bodi ya Ukaguzi wa Ununuzi wa Umma (PPARB) iliyoidhinisha masharti ya zabuni hiyo, yakiwemo yale yanayohusu uzoefu wa uchapishaji wa karatasi za kura na uwezo wa kifedha wa kampuni zilizoshindana. Hata hivyo, Jaji William Musyoka alitupilia mbali kesi hiyo kwa misingi ya kiufundi baada ya kubaini kuwa Oilmax ilikosa kutii muda uliowekwa na mahakama. Kampuni hiyo ilikuwa imepewa siku tatu kuwasilisha kesi kamili baada ya kupata ruhusa ya kufanya hivyo. Badala yake, hati za kesi ziliwasilishwa Septemba 15, siku tano baada ya muda huo kuisha. Kutokana na hali hiyo, IEBC iliomba mahakama ifunge faili ya kesi hiyo. Katika uamuzi wake, Jaji Musyoka alisema migogoro ya zabuni za umma huhitaji kushughulikiwa kwa haraka kwa sababu sheria inataka kesi zikamilishwe ndani ya siku 45. “Wakati ni jambo muhimu sana katika kesi za ukaguzi wa zabuni za umma,” alisema jaji huyo. Oilmax ilijitetea kwa kudai kuwa mfumo wa kielektroniki wa mahakama wa Case Tracking System (CTS) ulikuwa na hitilafu wakati ilipojaribu kuwasilisha stakabadhi zake Septemba 10. Lakini mahakama haikukubaliana na hoja hiyo. Jaji alisema upande mwingine katika kesi hiyo uliweza kuwasilisha stakabadhi zake siku hiyo hiyo kupitia mfumo huo. Aidha, alihoji ni kwa nini kampuni hiyo ilichukua siku tano kugundua kuwa stakabadhi zake hazikuwa zimepakiwa kwenye mfumo. Kampuni hiyo pia iliomba muda wa ziada wa kuwasilisha kesi, ikilaumu wakili wake na matatizo ya mfumo wa kielektroniki. Hata hivyo, mahakama ilisema ombi hilo lilitolewa baada ya dosari hiyo kubainika na hivyo halikustahili kukubaliwa. Chanzo cha mzozo huo ni zabuni iliyotangazwa na IEBC Agosti 11 ya uchapishaji wa karatasi za kura, rejista ya wapigakura, fomu za matokeo ya uchaguzi na vifaa vingine vya uchaguzi. Oilmax ilipinga sharti la kwamba mkandarasi lazima awe amewahi kukamilisha angalau mikataba miwili ya uchapishaji wa karatasi za kura zilizo na alama za usalama, ikiwemo mmoja ulioshughulikia angalau karatasi 150 milioni katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Kampuni hiyo pia ilikosoa masharti ya kifedha yaliyowataka waombaji kuwa na mauzo ya angalau Sh 6 bilioni kwa mwaka na uwezo wa kupata fedha taslimu za Sh10 bilioni. Hata hivyo, PPARB iliamua kuwa masharti hayo yalifaa kutokana na ukubwa wa zabuni hiyo, ambayo IEBC inakadiria itahitaji uchapishaji wa karatasi za kura takriban milioni 168. Kwa uamuzi wa Mahakama Kuu, changamoto ya Oilmax dhidi ya zabuni hiyo sasa imefikia kikomo bila hoja zake kuu kusikilizwa.

"On this day, I call for the rule of law to be applied fairly in every case. The continued detention of Sheikh Sani Khalifa Zaria and Mallam Nasir Ahmad El-Rufai raises questions about due process that the authorities must answer," he said.

DAR ES SALAAM: Katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kuimarisha usafi na utunzaji wa mazingira, Kampuni ya TotalEnergies Tanzania kwa kushirikiana na Arena Recycling Ltd imezindua mradi wa ukusanyaji na urejelezaji wa taka za plastiki jijini Dar es Salaam. Mradi huo unalenga kupunguza athari za taka za plastiki katika mazingira, huku zikikusanywa na kuongezewa…

RUKWA: Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkansi, Manispaa ya Sumbawanga na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa, Jacqueline Mzindakaya, wamefurahishwa na jitihada za Serikali za kuimarisha huduma za afya, huduma za uchunguzi na matibabu. Hatua hiyo itasaidia kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto, baada ya Zahanati za Chala na King’ombe kupatiwa na…

DAR ES SALAAM: TAIFA Stars Head Coach Miguel Gamondi has praised his players for fighting like “warriors” in their 1-1 draw against Madagascar, saying their spirited second-half display underlined the identity his technical bench is building for Tanzania. Stars endured a difficult first half at Stade d’Honneur de Meknes, where Madagascar controlled much of the…

Rais William Ruto ameomboleza kifo cha mfanyabiashara mashuhuri wa Zimbabwe, Wicknell Chivayo, pamoja na mkewe Lucy Muteke, waliokuwa miongoni mwa watu sita waliofariki baada ya helikopta waliyokuwa wakisafiria kuanguka nchini Zimbabwe Jumatano jioni. Katika ujumbe wake wa rambirambi, Rais Ruto alimtaja Chivayo kama rafiki wa karibu na kusema kifo chake cha ghafla ni pigo kubwa kwa familia yake, marafiki na watu wote waliomfahamu. “Nimesikitishwa sana na kifo cha kusikitisha cha rafiki yangu Wicknell Chivayo, pamoja na mkewe Lucy Muteke na watu wengine waliopoteza maisha katika ajali hiyo ya helikopta nchini Zimbabwe,” alisema Rais Ruto. Aliongeza kuwa Chivayo atakumbukwa kwa urafiki wake, uchangamfu wake na imani yake kubwa katika uwezo wa bara la Afrika kufanikiwa kiuchumi. “Wicknell alikuwa rafiki wa karibu ambaye aligusa maisha ya watu wengi. Nitamkumbuka kwa urafiki wake, nguvu zake na imani yake katika mustakabali wa bara letu,” alisema. Rais pia alituma rambi rambi kwa familia za waliofariki, Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa na wananchi wa Zimbabwe. Ajali hiyo ilitokea karibu saa kumi na moja jioni katika eneo la Marondera Rural, mashariki mwa mji mkuu wa Zimbabwe, Harare. Mamlaka nchini humo zilisema watu wote sita waliokuwa ndani ya helikopta hiyo walifariki dunia. Msemaji wa serikali ya Zimbabwe, Nick Mangwana, alisema ndege hiyo ilikuwa imebeba mfanyabiashara maarufu, abiria wengine watatu na marubani wawili. Kwa mujibu wa familia yake, Chivayo na mkewe walikuwa miongoni mwa walioangamia. Taarifa hiyo ilithibitishwa na msemaji wa familia, Herbert Chivayo. Kifo chake kinafunga ghafla ukurasa wa maisha ya mmoja wa wafanyabiashara waliotajika zaidi nchini Zimbabwe. Chivayo alikuwa mwanzilishi wa kampuni ya Intratrek Zimbabwe na alihusishwa na miradi mikubwa ya nishati na miundombinu, ikiwemo Mradi wa Nishati ya Jua wa Gwanda. Nchini Kenya, Chivayo alijulikana kutokana na ukaribu wake na Rais Ruto. Mwezi Agosti alizua mjadala baada ya kuchapisha video iliyomuonyesha Rais akimsindikiza kwa gari kuelekea uwanja wa helikopta katika makazi yake ya Kilgoris, Kaunti ya Narok. Mfanyabiashara huyo pia alikuwa rafiki wa karibu wa Rais Mnangagwa na alionekana mara kwa mara akiwa na viongozi wakuu wa kisiasa barani Afrika. Licha ya sifa zake za ukarimu na michango kwa michezo, dini na burudani, shughuli zake za biashara na uhusiano wake wa kisiasa pia zilivuta uchunguzi wa umma mara kwa mara. Kifo chake sasa kinaacha pengo kubwa katika nyanja za biashara, siasa, michezo na shughuli za kijamii nchini Zimbabwe.

DAR ES SALAAM: MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeishauri Serikali kuchukua hatua za kuridhia na kuweka katika sheria za ndani mikataba ya kimataifa inayolenga kulinda watu dhidi ya kutoweka kwa kulazimishwa na vitendo vingine vya kikatili au vya udhalilishaji vinavyoendelea katika jamii. Akizungumza kupitia tamko kwa vyombo vya habari, Mratibu wa…

GEITA: THE Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO) in collaboration with Geita Gold Mining Limited (GGML) have launched a major energy infrastructure project that will connect GGML’s operations directly to Tanzania’s national grid, bypassing the Mpomvu substation in Geita. Funded by TANESCO and developed following a feasibility study jointly undertaken by the two companies, the…

FROM REFORM TO PROSPERITY: INDEPENDENCE DAY ADDRESS TO THE NATION BY HIS EXCELLENCY, PRESIDENT BOLA AHMED TINUBU, GCFR, 1ST OCTOBER 2026 My fellow Nigerians, Sixty-six years ago today, our flag was raised, for the first time, over a free and sovereign nation. Since then, we have journeyed together as one nation, bound by our collective […]