ZAIDI ya wanafunzi milioni 3.6 watafanya mitihani na tathmini za kitaifa mwaka huu huku serikali ikiweka masharti magumu kukabiliana na udanganyifu na kuhakikisha uadilifu katika mchakato huo.
Waziri wa Elimu Julius Ogamba jana aliwaonya watahiniwa, wasimamizi wa vituo na wasimamizi wa mitihani dhidi ya kukiuka kanuni, akisema watakaopatikana wakifanya udanganyifu watachukuliwa hatua kali za kisheria.
“Hatutakuwa na huruma kwa yeyote atakayepatikana akijihusisha na aina yoyote ya udanganyifu,” akasema Bw Ogamba wakati wa uzinduzi wa msimu wa mitihani na tathmini za kitaifa za 2026 katika jumba la Mitihani House, Nairobi.
Jumla ya watahiniwa 3,634,846 wamejisajili kwa tathmini na mitihani hiyo, idadi ambayo inashinda mwaka uliopita.
Wanafunzi watakaofanya mitihani ya KPSEA ni 1,380,463, ikilinganishwa na 1,298,089 mnamo 2025.
Wale wa Sekondari Msingi, (KJSEA) ni 1,206,028, kutoka 1,130,679 mwaka jana, huku watahiniwa 1,048,355 wakifanya mtihani wa kidato cha nne, KCSE, kutoka 996,078 mwaka jana.
KCSE inaanza Oktoba 16 kwa matayarisho kisha ing’oe nanga rasmi Oktoba 19. KJSEA na KPSEA inaanza Oktoba 26.
Bw Ogamba alisema ongezeko hilo linahitaji umakinifu na rasilimali zaidi kutoka kwa maafisa wanaosimamia mitihani.
Aliwataka wadau wote kufuata kanuni na kutumia mbinu mpya zilizowekwa kuboresha ufanisi na uaminifu wa mitihani. “Ni lazima tushirikiane kuhakikisha mitihani inasimamiwa kwa njia ya haki na bila udanganyifu. Hii ndiyo njia pekee ya kuweka mfumo wetu wa elimu katika ushindani wa kimataifa,” akasema.
Serikali pia imeongeza makontena 48 ya kuhifadhi vifaa vya mitihani katika maeneobunge, na kufikisha idadi hiyo 701.
Bw Ogamba alisema hatua zimechukuliwa kupunguza athari za mvua za El Nino, huku maafisa wa nyanjani wakipatiwa mafunzo kabla ya mitihani kuanza.
Mikakati ya kufaulisha mitihani yakamilika kwa watahiniwa 3.6m

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsAfenifere demands prosecution of sponsors of campaign violence
…Raises alarm over rising attacks ahead of 2027 elections By Adeola Badru The pan-Yoruba socio-political organisation, Afenifere, has raised the alarm over increasing political violence ahead of the 2027 general elections, calling for the arrest and prosecution of perpetrators and their sponsors. The organisation warned that the growing incidents of thuggery, intimidation and inflammatory political […]
NewsPHOTOS: First Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsFirst Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsObi woos Onitsha voters, promises jobs, better services
…Says Nigeria needs energetic president By Vincent Ujumadu The presidential candidate of the Nigeria Democratic Congress (NDC), Peter Obi, on Friday drew a large crowd in Onitsha, Anambra State, as he led members of his campaign team on a roadshow and town hall meeting in the commercial city. Obi began his visit with a stop […]