SERIKALI imeunda kikosi cha asasi mbalimbali ili kuharakisha utekelezaji wa agizo la Mahakama Kuu linalohitaji kuwekwa kwa kanuni mpya za kusimamia maandamano ya umma na mienendo ya polisi.
Kikosi hicho kinajumuisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wizara ya Usalama wa Ndani, Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS), Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu (KNCHR), Tume ya Huduma kwa Polisi (NPSC), Mamlaka Huru ya Usimamizi wa Polisi (IPOA) pamoja na mashirika mengine.
Hatua hiyo ilibainika wakati mahakama ilipopewa taarifa kuhusu utekelezaji wa uamuzi wa Machi 25, 2026, ulioitaka serikali kuchapisha kanuni za maandamano, maandamano ya kutumia au kupita barabarani na matumizi ya nguvu ya polisi dhidi ya waandamanaji kwa muda wa siku 90.
Agizo hilo lilielekezwa kwa Inspekta Jenerali wa Polisi, NPS na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Mahakama iliambiwa kuwa kamati hiyo imeandaa mpango wa utekelezaji na pia inasaidia kupitishwa kwa Mswada wa Usimamizi wa Utulivu wa Umma wa 2025 ambao kwa sasa uko katika Bunge la Kitaifa.
“Kamati ilikutana Juni 26, 2026 kuweka mpango wa kushughulikia mswada huo ambao sasa uko mbele ya Bunge la Kitaifa,” Mwanasheria Mkuu aliambia mahakama alipokuwa akiomba muda zaidi ili taratibu zote zinazohitajika kukamilishwa kabla ya sheria hiyo kupitishwa.
Serikali imesema mswada huo utachukua nafasi ya Sheria ya Utulivu wa Umma na kuweka utekelezaji Ibara ya 37 ya Katiba inayolinda haki ya wananchi kukusanyika kwa amani na bila silaha, kufanya maandamano, maandamano ya kutumia mabango na kuwasilisha malalamishi.
Hatua hiyo ilifuatia uamuzi wa mahakama kapata Inspekta Jenerali wa Polisi, NPS na Mwanasheria Mkuu katika na hatia ya kukaidi amri ya mahakama baada ya kushindwa kutekeleza agizo hilo ndani ya siku 90.
Jaji Alfred Mabeya aliwaondolea adhabu baada ya kuzingatia maombi yao ya msamaha na hatua walizochukua kutekeleza agizo hilo. Hata hivyo, aliwataka kuwasilisha ripoti ya utekelezaji kila baada ya miezi minne.
Ripoti ya kwanza inatarajiwa Januari 25, 2027, huku mahakama ikionya kuwa hatua kali za adhabu zinaweza kuchukuliwa iwapo watashindwa kutekeleza agizo hilo.
Uamuzi huo unatokana na kesi iliyowasilishwa kufuatia jinsi polisi walivyoshughulikia maandamano ya kupinga serikali yaliyofanyika Kisumu, Migori na Ahero kati ya Machi na Julai 2023.
Serikali mbioni kuandaa sheria mpya za maandamano nchini

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsAfenifere demands prosecution of sponsors of campaign violence
…Raises alarm over rising attacks ahead of 2027 elections By Adeola Badru The pan-Yoruba socio-political organisation, Afenifere, has raised the alarm over increasing political violence ahead of the 2027 general elections, calling for the arrest and prosecution of perpetrators and their sponsors. The organisation warned that the growing incidents of thuggery, intimidation and inflammatory political […]
NewsPHOTOS: First Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsFirst Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsObi woos Onitsha voters, promises jobs, better services
…Says Nigeria needs energetic president By Vincent Ujumadu The presidential candidate of the Nigeria Democratic Congress (NDC), Peter Obi, on Friday drew a large crowd in Onitsha, Anambra State, as he led members of his campaign team on a roadshow and town hall meeting in the commercial city. Obi began his visit with a stop […]