Top headlines and developing stories from Tanzania, Kenya, Uganda and the wider region, gathered from the leading local and international newsrooms and updated throughout the day.
RAIS SAMIA "WAKISEMA TUNATOKA TUTAKUWEPO" - KAULI KALI KWA WANAOPANGA KUVURUGA AMANI... Rais Samia Suluhu Hassan azungumzia utayari wa vikosi na operesheni mbalimbali, akisisitiza uwepo wa mahema na…
KALAMBO, Rukwa: CCM Youth Wing (UVCCM) Deputy Chairperson, Rehema Sombi (MNEC), is expected to officially launch CCM Youth Week today, October 8, 2026, in Kalambo District, Rukwa Region. The UVCCM Youth Week is scheduled to run until October 14, 2026, bringing together young people from different parts of the country to explore common opportunities, share…
TUME ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano (NCIC) imeamuru Waziri wa Utumishi wa Umma Geoffrey Ruku na Mbunge wa Mukurweini John Kaguchia kuondoa matamshi yao yaliyodaiwa kuchochea mgawanyiko wa kikabila na kisiasa. Maagizo hayo yalitolewa huku joto la kisiasa likizidi kupanda kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027. Katika maamuzi mawili yaliyotolewa jana, Mwenyekiti wa NCIC Askofu Kepha Omae alisema matamshi ya Bw Ruku huko Tharaka Nithi yalihusu lawama za kikabila, huku ya Bw Kaguchia katika mkutano wa kisiasa Kieni, Nyeri, yakihusisha kutisha wananchi kwa misingi ya misimamo yao ya kisiasa. Kwa Bw Ruku, NCIC ililenga matamshi aliyotoa akiwa Kiang’ondi, Tharaka Nithi mwezi Julai. Tume ilisema Waziri huyo alikataa eneo la Mlima Kenya Mashariki kuchukuliwa kama “trela” ya Wakikuyu na pia akazungumzia madai kuwa baadhi ya watu wa Mlima Kenya Magharibi wanaamini Kenya ni yao. NCIC pia ilikosoa matumizi ya majina ya kikabila katika mjadala kuhusu maendeleo na uteuzi wa watu serikalini. “Kurejelea kwa jamii zao, madai kwamba watu wa Mlima Kenya Magharibi walifikiri Kenya ni yao na matumizi ya majina ya kikabila yalibadilisha malalamishi ya kitaasisi kuwa lawama za kikabila,” alisema Askofu Omae. Bw Ruku alikiri kutoa matamshi hayo alipofika mbele ya NCIC Septemba 1, lakini akasema Katiba inalinda kutambua jamii na madai ya usawa katika maendeleo na uteuzi wa watu serikalini. Alikanusha kuwa alikuwa na chuki dhidi ya watu wa jamii moja na akasema kauli yake kuhusu “kukanyaga shingo” ilikuwa lugha ya kisiasa iliyomaanisha kumshinda mpinzani kisiasa, wala si kumdhuru kimwili. Hata hivyo, NCIC ilisema wadhifa wake kama Waziri wa Serikali ulimpa ushawishi mkubwa na hivyo alipaswa kuwa mwangalifu zaidi. Tume imemwamuru Ruku kuondoa hadharani, kwa Kiswahili na Kiingereza, madai kwamba Wakikuyu wanaamini Kenya ni mali yao au wanawajibika kwa ukosefu wa usawa katika maendeleo na uteuzi. Kwa upande wa Kaguchia, NCIC ilisema matamshi yake katika mkutano wa Kieni Agosti yalivuka mipaka ya ushawishi wa kisiasa na kuwa vitisho kwa wananchi. Tume ilisema mbunge huyo aliwataka wafuasi wa Rais William Ruto, aliowataja kama wafuasi wa “Kasongo”, kutambuliwa, kufuatiliwa na kutolewa chini ya vitanda vyao. Bw Kaguchia alikamatwa Agosti 3 baada ya kuonekana katika kipindi cha Kiririmbi cha Inooro TV na baadaye kushtakiwa katika Mahakama ya Milimani kwa kosa la kutoa matamshi yanayoweza kuvuruga amani. Alipoitwa na NCIC, alipinga tafsiri ya Kiingereza ya matamshi yake ya Kikuyu, akitaka rekodi ya hotuba hiyo ichezwe na kutafsiriwa kwa Kikuyu. NCIC ilisema matamshi hayo yalikuwa na hatari ya kusababisha vitisho, kutengwa kwa watu na kudhoofisha ushiriki wa kisiasa kwa amani. Kaguchia ameagizwa kuomba msamaha hadharani na kutoa taarifa ya kusahihisha matamshi yake kwa Kikuyu, Kiswahili na Kiingereza, kwa kiwango kinacholingana na uenezaji wa hotuba yake ya awali.
RUKWA: Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (MNEC), Rehema Sombi anatarajiwa kuzindua rasmi Wiki ya Vijana wa CCM leo, Oktoba 8, 2026 Wilaya ya Kalambo, mkoani Rukwa. Wiki hiyo ya UVCCM inatarajiwa kuendelea hadi Oktoba 14, 2026, ikiwa na lengo la…
MBIO za kumtafuta mgombeaji atakayepeperusha bendera ya upinzani dhidi ya Rais William Ruto katika uchaguzi wa 2027 zinageuka vita vya kizazi, huku vijana wakitaka kuchukua nafasi ya viongozi waliotawala siasa kwa miongo kadhaa. Kwa upande mmoja kuna Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, wabunge Ndindi Nyoro (Kiharu) na Babu Owino (Embakasi East), Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya na Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi. Kwa upande mwingine kuna vigogo kama Kalonzo Musyoka wa Wiper Patriotic Front, Martha Karua wa People’s Liberation Party, Rigathi Gachagua wa Democracy for the Citizens Party (DCP) na Gavana wa Siaya James Orengo. Pia kuna kundi la wataalamu na vigogo waliotoka nje ya siasa za kawaida za uchaguzi akiwemo aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang’i, mfanyabiashara Jimi Wanjigi na aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga. Hali hii imefanya kambi ya upinzani kuwa na wagombea wengi hata kabla ya vyama kuanza rasmi mchakato wa kumteua mgombea mmoja wa urais. Wachambuzi wanasema mjadala huu hauhusu umri pekee bali pia uzoefu wa kisiasa, mtandao wa kitaifa, uungwaji mkono wa maeneo, taaluma na uwezo wa kuvutia kizazi kipya cha wapigakura. Mjadala huo umeonekana zaidi kupitia Seneta Sifuna ambaye amezindua The Equitable Party (TEP), inayotarajiwa kubadilishwa jina kuwa Linda Mwananchi Movement. Kundi lake linasukuma tiketi inayowapa vijana nafasi kubwa, jambo linaloweza kuathiri mazungumzo ya kuunda muungano mpana wa upinzani. Mbunge Babu Owino ameunga mkono azma hiyo akisema wakati umefika kwa vijana kuongoza. “Vijana wa nchi hii huambiwa kila mara kuwa wao ni viongozi wa kesho. Sasa tunasema sisi ni viongozi wa leo na wakati wetu umefika,” alisema. Hata hivyo, juhudi za vijana zinakabiliwa na ukweli kwamba vyama mbalimbali vya upinzani vina watu wanaotaka kuwania urais. Seneta wa Kitui Enoch Wambua, mshirika wa Bw Musyoka, amesema anaendelea kumuunga mkono kiongozi huyo wa Wiper, ingawa hakufunga mlango wa ushirikiano na mrengo wa Sifuna. “Ukiangalia kwa karibu, Linda Mwananchi ina watu kutoka vyama mbalimbali vya Muungano wa Upinzani. Timu hizi mbili zina lengo moja la kuhakikisha Rais Ruto anahudumu kwa muhula mmoja,” alisema. Wakati huohuo, DCP ya Bw Gachagua imeibua mvutano na \Bw Nyoro. Katibu Mkuu wa DCP John Methu alishambulia People’s Progressive Party (PPK), akiitaja kama wilibaro ndogo na kudai inalenga kuwachanganya wapigakura na kupunguza ushawishi wa DCP eneo la Mlima Kenya. Mchambuzi wa siasa Javas Bigambo alisema Bw Nyoro ana haki ya kuwania urais. “Mkenya yeyote anaweza kuwania nafasi yoyote,” alisema, akiongeza kuwa hakuna mwanasiasa au chama chenye haki ya siasa za eneo fulani. Kwa upande wake, Dkt Matiang’i ametoa wito kwa wanasiasa wa upinzani kutotafsiri ushindani wao kama uadui. “Kenya yetu ni demokrasia ya vyama vingi. Hata sisi Jubilee tunataka kiti hicho cha urais na wengine pia wanakitaka, lakini sisi si maadui,” alisema. Bw Musyoka anajipanga kama mmoja wa vigogo wanaotaka kuunganisha makundi mbalimbali ya upinzani, huku Bw Gachagua akijikita zaidi katika kuunganisha Mlima Kenya chini ya DCP. Bi Karua na Bw Orengo pia wameonyesha nia ya kuwania urais. Wataalamu wanasema changamoto kubwa kwa vijana ni kubadilisha umaarufu na ushawishi wa mitandao ya kijamii kuwa mtandao wa mashinani unaohitajika katika uchaguzi wa urais. Wakati huo huo, wagombea kama Dk Matiang’i, Bw Wanjigi na Bw Maraga wanajaribu kutumia rekodi zao za kitaaluma, utawala na utumishi wa umma kama njia mbadala ya siasa za kawaida. Seneta wa Busia Okiya Omtatah naye anajikita katika mageuzi ya Katiba, utawala wa sheria na kupunguza mamlaka makubwa ya urais. Mchambuzi Dismas Mokua anasema vita hivyo huenda visitatuliwe na umri wa wagombea bali uwezo wao wa kuunda muungano mpana unaovuka misingi ya kikabila, maeneo na vyama.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amewakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Uholanzi kuchangamkia fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana Tanzania, hususan katika sekta za uzalishaji viwandani, usindikaji wa mazao na uongezaji thamani. Akizungumza jijini The Hague, Uholanzi, Prof. Mkumbo amesema nafasi ya kimkakati ya Tanzania kijiografia, pamoja na miundombinu na…
DAR ES SALAAM: TANZANIA Electric Supply Company Limited (TANESCO) has shortened the period for connecting new electricity customers, with some areas now receiving the service within 12 days. TANESCO Managing Director, Mr Lazaro Twange, said previously customers could wait between 30 and 90 days to be connected, depending on distance, but the period had now…
DAR ES SALAAM; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu (kulia), akiwa pamoja na Waziri wa Kazi na Kinga ya Jamii wa Jamhuri ya Kenya, Alfred Mutua (katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba, wakati wa Mkutano wa Pili wa Doha…
MRADI wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote Lamu wa thamani ya Sh2 trilioni ulikaribia kukumbwa na kizuizi cha kisheria saa chache kabla ya uzinduzi wake rasmi. Wakazi 133 waliwasilisha kesi katika Mahakama ya Mazingira na Ardhi Malindi wakitaka shughuli za mradi huo zisitishe. Wakazi hao walidai kuwa ardhi hiyo ni ya mababu zao ambao wameishi, kulima na kuendeleza eneo hilo kwa vizazi. Walilalamika kuwa serikali na waendelezaji wa mradi walianza utekelezaji bila kukamilisha tathmini ya ardhi, fidia na mpango wa kuwahamisha wakazi. Mahakama hata hivyo ilikataa kuthibitisha kesi hiyo kuwa ya dharura na kuwaagiza walalamishi kuwapa wahusika stakabadhi za kesi. Hivyo, hafla ya kuweka jiwe la msingi iliendelea Septemba 30. Siku chache baadaye, mradi huo ulikuwa tena mahakamani baada ya kesi nyingine kuthibitishwa kuwa ya dharura. Kesi hiyo inataka serikali kuweka wazi mikataba na ahadi zilizotolewa kuhusu ushiriki wa Kenya katika mradi huo. Hata hivyo, bilionea wa Nigeria Aliko Dangote alisema kesi hizo hazitamzuia kutekeleza ndoto yake ya kufanya Afrika ijitegemee katika nishati. “Ukitaka kwenda kortini kuzuia kiwanda cha Lamu, endelea. Tuko tayari. Hili ni jambo la kawaida Afrika,” alisema. Kauli hiyo inaonyesha kuwa Dangote si mgeni wa vita vya mahakama katika miradi yake mikubwa ya mafuta. Nchini Nigeria, kiwanda chake cha Lagos chenye uwezo wa kusafisha mapipa 650,000 ya mafuta kwa siku kimekumbwa na mizozo kuhusu usambazaji wa mafuta ghafi, uagizaji wa mafuta kutoka nje, kanuni za serikali na ushindani katika sekta hiyo. Kabla ya kujengwa Lekki, mradi huo ulipangwa kujengwa katika eneo la Olokola Free Trade Zone. Mpango huo ulikumbwa na changamoto za kisiasa, urasimu na mzozo kuhusu ardhi na hatimaye Dangote akahamishia mradi Lekki. Hata huko, makundi ya mazingira na wavuvi yalipinga shughuli za kuchimba mchanga na kubadilisha mazingira ya pwani, yakidai kuwa ziliathiri maeneo ya kuzaliana samaki na kuongeza mmomonyoko wa ardhi. Dangote baadaye alitia saini makubaliano na jamii 15 za eneo hilo ili kupunguza mizozo. Kampuni ilisaidia kujenga barabara, madarasa, visima, kutoa ufadhili wa masomo na mafunzo ya ufundi kwa vijana. Kiwanda chake cha Lamu kinatarajiwa kuwa na uwezo wa kusafisha mapipa 700,000 ya mafuta kwa siku na kuunda zaidi ya ajira 60,000 wakati wa ujenzi. Rais William Ruto alisema mradi huo ni zaidi ya kiwanda cha mafuta, akisema utasaidia usalama wa nishati, viwanda na biashara ya kikanda. Hata hivyo, wataalamu wanaonya kuwa kiwanda hicho hakitaondoa mara moja gharama ya mafuta nchini kwa sababu Kenya bado italazimika kuagiza mafuta ghafi kutoka nje. Rais Ruto alisema bei ya mafuta itaendelea kuathiriwa na gharama ya mafuta ghafi, usafirishaji, bima, kodi na thamani ya shilingi. Kwa upande mwingine, uwezo wa Lamu kuzalisha mafuta mengi kuliko mahitaji ya Kenya unaweza kufanya nchi kuwa muuzaji wa mafuta yaliyosafishwa kwa mataifa jirani. Hivyo, huku vita vya kisheria vikiendelea, Dangote anakabiliwa na mtihani mwingine Lamu: kuhakikisha mradi huo mkubwa unatekelezwa bila kuacha nyuma jamii zinazodai kuwa na maslahi katika ardhi hiyo.
CHAMA kipya cha The Equitable Party (TEP) kinachohusishwa na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kimeanza maandalizi ya kubadili jina na kuitwa Linda Mwananchi Movement (LMM), huku viongozi wake wakijipanga kukitumia kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Msajili wa Vyama vya Kisiasa tayari ameidhinisha mabadiliko ya majina ya maafisa wa TEP, hatua inayofungua njia kwa chama hicho kuanza mchakato wa kuitwa Linda Mwananchi. Baraza Kuu la Kitaifa la chama hicho lilikutana Jumatano na kuidhinisha mpango huo. Hatua hiyo inajiri siku chache baada ya Bw Sifuna kuzindua rasmi TEP jijini Nairobi, ambako alitambulishwa kama kiongozi wa chama hicho na kueleza mipango ya kukitumia kuelekea 2027. Katika hotuba yake ya uzinduzi mnamo Oktoba 4, Bw Sifuna alisema TEP ilipatikana baada ya juhudi za kutafuta makao mapya ya kisiasa kufuatia mzozo wake na ODM. Hata hivyo, alidokeza kuwa TEP huenda isiwe jina la mwisho la vuguvugu hilo. “Katika siku zijazo, na kwa mujibu wa uamuzi wa viongozi wakuu wa Linda Mwananchi, tutabadili jina la chama kuwa Linda Mwananchi Movement,” alisema Bw Sifuna. Aliongeza kuwa iwapo kutakuwa na vikwazo zaidi katika mchakato huo, chama kitaendelea kutumia jina la TEP. Hatua hiyo imepatia nguvu zaidi vuguvugu la Linda Mwananchi, ambalo jina lake limekuwa katika mzozo wa kisheria kati ya washirika wa Bw Sifuna na Msajili wa Vyama vya Kisiasa. Msajili aliidhinisha kuhifadhi jina Linda Mwananchi Movement Oktoba 1, kufuatia uamuzi wa Jopo la Kutatua Mizozo ya Vyama vya Kisiasa kupitia upya uamuzi wake wa awali wa kulikataa. Hata hivyo, kuhifadhiwa kwa jina hilo hakumaanishi kuwa LMM kimesajiliwa kama chama cha kisiasa. Badala yake, jina hilo limepewa muda mpya wa siku 90 ambapo waasisi wake wanaweza kukamilisha hatua zinazohitajika za usajili. Hatua hiyo inafanyika wakati muhimu kwani vyama vinavyolenga kushiriki uchaguzi wa 2027 vinapaswa kuwasilisha kwa IEBC majina na saini za maafisa wao walioidhinishwa kufikia Oktoba 15. Uamuzi wa jopo ulitokana na rufaa iliyowasilishwa na Mbunge wa Suba South Caroli Omondi, Pauline Njoki Njoroge na Faith Odhiambo baada ya Msajili kukataa majina ya Linda Mwananchi. Majina yaliyopendekezwa ni pamoja na Linda Mwananchi Alliance, Linda Mwananchi Coalition na Linda Mwananchi Party of Kenya. Jopo lilibatilisha uamuzi wa Msajili wa Agosti 7, likisema hakutoa sababu za kutosha kukataa jina hilo. Pia ilisema uhifadhi wa jina la Liberty National Democratic Alliance, maarufu kama LINDA, ulimalizika baada ya muda wa kisheria wa siku 90. Hata hivyo, bado kuna kizingiti kingine. Charles Wanyonyi amemtaka Msajili kupatia kipaumbele ombi lake la kuhifadhi jina Linda Mwananchi Party of Kenya, akisema aliliwasilisha Februari 24, 2026. Wakili wake amesema ombi hilo liliwasilishwa miezi kadhaa kabla ya yale yaliyozingatiwa na jopo. Katika uzinduzi wa TEP, Bw Sifuna alisema chama hicho kinalenga kuwapa wananchi nafasi kubwa katika siasa. Alisema vuguvugu hilo litalenga siasa zinazozingatia mawazo, uwajibikaji, huduma na Katiba, badala ya siasa zinazozunguka mtu mmoja. Bw Sifuna pia alisema vijana na wanawake watapewa nafasi kubwa katika kufanya maamuzi ya kisiasa, huku maeneo na jamii mbalimbali zikizingatiwa kwa usawa. Alisema chama hicho kiko tayari kushirikiana na viongozi wengine wa upinzani pamoja na Wakenya wanaounga misingi yake ya kisiasa.
MOROGORO: CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimeanza kutekeleza agizo la Makamu wa Rais la kuwawezesha vijana kupata ujuzi na uzoefu wa kazi kwa kuwaunganisha wanafunzi na wahitimu wa chuo hicho wanaoongoza kampuni na taasisi mbalimbali. Hatua hiyo inalenga kuwapa wanafunzi na wahitimu fursa ya kujifunza kutoka katika mazingira halisi ya kazi, ikiwemo uzalishaji,…
KISA cha kwanza cha Ebola nchini kilichothibitishwa Nairobi kimezua taharuki na kuchochea kaunti mbalimbali kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa huo, kufufua vituo vya kutenga wagonjwa na kuwaandaa wahudumu wa afya kukabiliana na visa vinavyoweza kujitokeza. Hatua hizo zinalenga kukagua watu na bidhaa kupitia barabara kuu, mipaka, bandari, viwanja vya ndege na vituo vya utalii, hali inayoongeza hatari ya virusi kusambaa kwa kasi endapo tahadhari hazitachukuliwa. Mombasa ni miongoni mwa kaunti zinazochukuliwa kuwa katika hatari kubwa kutokana na nafasi yake kama lango kuu la biashara ya kikanda. Ukaguzi wa madereva wa malori ya masafa marefu unatarajiwa kuanza hivi karibuni. Afisa wa kituo cha operesheni za dharura cha Port Reitz, Fatma Ali, alisema wahudumu wa afya wamewekwa katika hali ya tahadhari katika maeneo muhimu, ikiwemo Bandari ya Mombasa, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Moi na barabara zinazotumiwa na malori ya mizigo kutoka nchi jirani. “Tunapanua kampeni za kutoa elimu kwa umma kuhusu jinsi ya kujikinga na Ebola, umuhimu wa kutafuta matibabu mapema na kukabiliana na taarifa potovu zinazoweza kudhoofisha juhudi za kukabili ugonjwa huu,” alisema Bi Ali. Wahudumu wa afya pia wamefanya mazoezi ya kukabiliana na mlipuko wa Ebola, yakilenga kutenga wagonjwa, kufuatilia waliowasiliana nao, kuchukua sampuli na kukabiliana na dharura. Hata hivyo, uchunguzi wa Taifa Leo ulibaini kuwa kituo kimoja cha kutenga wagonjwa cha Port Reitz kiko katika hali isiyoridhisha, huku eneo la kuingia likiwa limezungukwa na vichaka vilivyomea. Madereva wa malori ya masafa marefu pia wamelalamika kuwa hawajahusishwa vya kutosha katika maandalizi hayo. Katibu Mkuu wa Chama cha Madereva na Makondakta wa Masafa Marefu, Roman Waema, alitaka serikali kuwashirikisha badala ya kuweka hatua zinazoweza kutatiza biashara kwenye Barabara Kuu. “Tuko hatarini. Tunasikia mengi kuhusu Ebola kwenye vyombo vya habari, ilhali tunasafiri kila siku nje ya nchi, hata DRC. Tunaomba serikali itushirikishe na kutusaidia kuchukua hatua bora za kujilinda,” alisema Bw Waema. Kaunti nyingi zimeanza kutumia tena vituo vya kutenga wagonjwa vilivyoanzishwa wakati wa Covid-19 kama vituo vya karantini vya Ebola. Homa Bay imefufua vituo kadhaa, huku Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu katika Kaunti hiyo, Amos Dulo, akisema vimekaguliwa na kuthibitishwa kuwa vinaweza kuhudumia wanaoshukiwa kuambukizwa. Vituo hivyo ni pamoja na Malela, Nyagoro, Pala Koguta, Ober, Nyangiela na Kandiege. Homa Bay iko katika eneo linalohusiana kwa karibu na Uganda kupitia Ziwa Victoria, ambako watu huvuka kati ya nchi hizo mbili, hali inayoongeza hofu ya kusambaa kwa magonjwa ya kuambukiza. Huko Eldoret, Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi (MTRH) imeanzisha kituo maalumu cha kutenga wagonjwa pamoja na kikosi cha kukabiliana na dharura. Afisa Mkuu Mtendaji wa hospitali hiyo, Dkt Philip Kirwa, alisema kituo hicho kina uwezo wa kuhudumia hadi wagonjwa 24 wanaoshukiwa kuwa na Ebola. “Kituo hicho pia hutumika kama cha wagonjwa mahututi na kina vifaa vya kisasa vya kudhibiti kusambaa kwa virusi na kuhakikisha usalama wa wahudumu wa afya,” alisema Dkt Kirwa. Katika Kirinyaga, Mkurugenzi wa Matibabu wa Kaunti, Dkt Hesbon Gakuo, alisema wodi ya kutenga wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kerugoya inaweza kuhifadhi wagonjwa 13. Aliwataka wakazi wenye homa, maumivu makali ya kichwa, kutapika, kuhara au kutokwa damu bila sababu kufika hospitalini haraka. “Tumeanzisha timu zetu za dharura na tuko tayari iwapo kutakuwa na mlipuko,” alisema. Kaunti za Nakuru, Kericho, Nyandarua, Narok na Bomet pia zimeimarisha maandalizi. Bomet imetenga vituo katika Hospitali ya Rufaa ya Longisa na hospitali za maeneo bunge. Nakuru imeshirikisha wahamasishaji wa afya ya jamii na viongozi 36 wa dini kutoa elimu kuhusu Ebola na kusaidia kubaini visa vinavyoshukiwa. Hatua hizi zimechukuliwa baada ya Wizara ya Afya kuthibitisha kisa cha kwanza cha Ebola aina ya Bundibugyo nchini. Mgonjwa huyo, raia wa Kenya aliyekuwa akiishi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), alianza kuugua akiwa DRC kabla ya kusafiri kwa barabara hadi Kampala na baadaye kwa ndege hadi Nairobi, ambako alitengwa na kupimwa na kuthibitishwa kuwa na virusi. Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza mlipuko wa Ebola Bundibugyo nchini DRC na Uganda kuwa dharura ya afya ya umma kutokana na hatari ya kusambaa kimataifa. WHO iliripoti visa 5,794 vilivyothibitishwa na vifo 2,786 kufikia Agosti 26, huku Ituri, DRC, ikiwa kitovu cha mlipuko huo. Bundibugyo ni aina ya Ebola ambayo haina chanjo au dawa maalumu iliyoidhinishwa kwa sasa, kwa mujibu wa WHO.
RAIS mstaafu Uhuru Kenyatta amejiuzulu rasmi kama mwenyekiti wa Baraza la Muungano wa Azimio la Umoja, hatua inayofungua ukurasa mpya katika juhudi za kuunda upya muungano wa upinzani kuelekea uchaguzi wa 2027. Uhuru alitangaza kujiuzulu kupitia barua ya Oktoba 5, 2026, huku muungano huo ukibadilisha jina na sasa kujulikana kama The Ukombozi Alliance (TUA). Kiongozi wa Wiper Patriotic Front, Kalonzo Musyoka, anaendesha mchakato wa kuwarai viongozi wengine wa upinzani, akiwemo kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua na Gavana wa Siaya James Orengo. Majina ya Gachagua na Orengo yalijadiliwa katika mkutano wa muungano huo Jumatano ulioongozwa na Kalonzo. “Mashauriano yanaendelea kuhusu nani atashikilia nafasi hiyo. Kwa kiasi kikubwa tumekubaliana iwe Gachagua au Gavana Orengo,” alisema afisa mmoja aliyehudhuria mkutano huo. Orengo anadaiwa kukubali kuchukua nafasi hiyo, huku jina la Gachagua likiibuka kutokana na nafasi yake katika siasa za upinzani. Juhudi za kumshawishi Gachagua zinafanyika wakati ambao DCP imekuwa ikionyesha nia ya kujenga ngome yake kisiasa kabla ya kufanya mazungumzo na vyama vingine vya upinzani. Vilevile, kundi la Linda Mwananchi linaloongozwa na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna limewahi kukataa mwaliko wa kujiunga na muungano huo. Mzozo mkubwa ni kipengele cha makubaliano ya muungano kinachotaja kiongozi wa chama kuwa mgombea wake wa urais moja kwa moja. Kalonzo aliteuliwa na Uhuru kuwa kiongozi wa muungano huo Februari, akichukua nafasi ya marehemu Raila Odinga, aliyekuwa mgombea wa urais wa Azimio katika uchaguzi wa 2022. Katika barua yake, Uhuru alisema kujiuzulu hakumaanishi ameondoka katika safari ya kisiasa ya upinzani. “Nasalia, kama kawaida, mwanachama aliyejitolea wa familia ya Azimio, tayari kuunga mkono taasisi hiyo kutoka safu za chini na kutoa ushauri nitakapohitajika,” alisema. Kalonzo alisema Uhuru amekuwa nguzo muhimu ya muungano huo na bado ni mwanachama wake. Alisema jina The Ukombozi Alliance limehifadhiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa (ORPP), huku mchakato wa kutimiza masharti ya usajili ukiendelea. Muungano huo unalenga kutumia mfumo unaofanana na ule wa NARC uliomsaidia Mwai Kibaki kushinda urais mwaka 2002. Chini ya mfumo huo, vyama vitaendelea kuhifadhi majina yao lakini kuunga mkono mgombea mmoja wa urais na ajenda ya pamoja. Mchambuzi wa siasa Prof David Monda alisema mafanikio ya mpango huo yatategemea iwapo viongozi wengine wa upinzani watakubali kujiunga na muungano huo na kumuunga mkono Kalonzo kama mgombea wa urais. Alisema hatua ya kubadili jina inalenga kuupa muungano sura mpya na kujaribu kuwavutia vijana kuelekea uchaguzi wa 2027.
WAHUDUMU wa afya wameibua wasiwasi kuhusu uwezo wa Kenya kukabiliana na Ebola baada ya kisa cha ugonjwa huo kuthibitishwa nchini, wakidai kuna upungufu wa vifaa vya kujikinga, vituo vya kutenga wagonjwa na ufuatiliaji katika maeneo ya kuingilia nchini. Mgonjwa huyo, raia wa Kenya aliyekuwa akiishi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), alifariki Oktoba 6. Hata hivyo, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilisema maandalizi ya Kenya yameimarika kutoka asilimia 66 hadi 82 kufikia Julai 2026. WHO pia ilisema Kenya imeendesha mafunzo kwa wahudumu wa afya, hasa wale wanaohusika na kukabiliana na dharura na wanaofanya kazi katika maeneo ya mipakani. Lakini Katibu Mkuu wa Muungano wa Madaktari, Wafamasia na Madaktari wa Meno Kenya (KMPDU), Dk Davji Atella, alisema hali halisi ni tofauti. Alisema kisa hicho kimezua hofu miongoni mwa wahudumu wa afya na wananchi, huku kukiwa na upungufu wa wafanyakazi. “Maandalizi hayawezi kuwa ya kufikiriwa tu, lazima yaonekane kwa vitendo. Serikali inapaswa kuweka mahitaji yote muhimu,” alisema. Naibu Katibu Mkuu wa KMPDU, Dkt Dennis Miskellah, alisema vituo vya kutenga wagonjwa lazima viwe na vifaa vya kutosha, huku wahudumu wakipewa vifaa vya kujikinga. “Tunazungumzia maandalizi gani wakati baadhi ya kaunti zinasema glavu zimeisha? Maji ya kusaidia wagonjwa walio katika hali mbaya hayatoshi. Je, tuna damu ya kutosha, hasa kwa ugonjwa kama Ebola unaosababisha kuvuja damu?” aliuliza. Katibu Mkuu wa Chama cha Maafisa wa Afya ya Umma, Mohamed Duba, alisema ufuatiliaji katika vituo vya kuingilia nchini unahitaji kuimarishwa. Alisema baadhi ya mashine za kupima joto hazifanyi kazi, huku vituo vingi vya kuingilia vikikosa vyumba vya kutenga wanaoshukiwa kuambukizwa. “Port Health haiwezi kuchukuliwa kama kazi ya pembeni. Kenya inahitaji maafisa wa afya ya umma waliohitimu, vifaa, vifaa kinga (PPE), vituo vya kutenga wagonjwa na mfumo madhubuti wa ufuatiliaji,” alisema. Duba alisema madaktari, wauguzi, wataalamu wa maabara, wataalamu wa magonjwa, na maafisa wa afya ya umma wanapaswa kufanya kazi kwa pamoja wakati wa mlipuko wa maradhi. Hata hivyo, alisisitiza kuwa ushirikiano wa wataalamu hao haumaanishi kwamba kila mmoja anaweza kufanya kazi za mwenzake, akisema kila moja inapaswa kutekeleza majukumu kulingana na taaluma na sheria zinazoiongoza. Duba pia alitaka kuwe na mfumo wazi wa kuanzishwa kwa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Kenya (KCDC), akisema taasisi hiyo inapaswa kupewa jukumu kubwa la kuzuia milipuko badala ya kusubiri magonjwa yazuke ndipo hatua zichukuliwe. “ KCDC imara inapaswa kubaini hatari mapema, kuzuia maambukizi, kuimarisha ufuatiliaji, kulinda jamii na kuratibu hatua kabla milipuko haijageuka kuwa dharura,” alisema. Alisema nguvu ya mfumo wa afya ya umma nchini haipaswi kupimwa tu kwa uwezo wa kukabiliana na milipuko inapotokea, bali pia kwa namna unavyoweza kuzuia ugonjwa usisambae na kuwa janga kubwa. Duba pia alikosoa serikali ya kitaifa kwa kushindwa kujaza nafasi za maafisa wa afya ya umma waliostaafu au kuondoka kazini. Alisema hali hiyo imewaacha wengi waliohitimu taaluma hiyo bila ajira huku mfumo wa afya ya umma ukidhoofika kutokana na uhaba wa wafanyakazi. “Hatuhitaji bajeti mpya; tunachohitaji ni kuwabadilisha wale walioondoka kazini,” alisema. Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Chama cha Afya ya Umma Kenya, Brown Ashira, alisema maafisa wa afya ya umma wamekuwa wakipuuzwa licha ya kuwa mstari wa mbele katika kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza. “Covid iliingia nchini kupitia ndege, na Ebola pia imeingia kwa njia hiyo. Historia inajirudia,” alisema. Katibu Mkuu wa Chama cha Wataalamu wa Maabara Kenya, Pius Nyakundi, pia alisema maafisa wa maabara wako katika hatari ya kuambukizwa, lakini malalamiko yao hayajapewa uzito unaostahili.
—Says govt can pay between N200,000, N400,000 By Johnbosco Agbakwuru ABUJA — THE Trade Union Congress of Nigeria (TUC) on Wednesday, urged the Federal Government to improve workers’ pay immediately, rather than waiting for the next review of the national minimum wage. Briefing journalists in Abuja after its National Administrative Executive Council, NAC meeting, the […]
WATOTO wanane wameokolewa kutoka nyumbani kwa Anastacia Mumwele, mama wa mhubiri tata Paul Mackenzie, eneo la Furunzi, Malindi, Kaunti ya Kilifi, ambako inadaiwa walikuwa wakilazimishwa kufunga na kunyimwa fursa ya kwenda shuleni. Wapelelezi kutoka Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) walimkamata Bi Mumwele, nyanya wa watoto hao, wakati wa msako katika nyumba yake Jumatano alasiri. Watoto hao, wenye umri wa kati ya miaka sita na 14, walipatikana ndani ya nyumba hiyo. Watano kati yao wanaaminika kuwa watoto wa Mackenzie. Afisa mkuu wa DCI, ambaye alizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina, alisema wapelelezi walichukua hatua baada ya kupata taarifa kwamba watoto hao walikuwa wakinyimwa chakula na kulazimishwa kufuata mafundisho yanayohusishwa na imani ya Mackenzie kuhusu mwisho wa dunia. “Tulipokea taarifa kwamba nyanya yao alikuwa amewafungia watoto hao na kuwanyima chakula, hali iliyotulazimu kuchukua hatua na kuwaokoa,” afisa huyo alisema. Watoto hao walipelekwa katika Kituo cha Polisi cha Malindi, ambako maafisa wa Kitengo cha Kulinda Watoto walitarajiwa kuchukua jukumu la ustawi wao na kuwawezesha kuhamishiwa katika mazingira salama zaidi. Mwanawe Mackenzie, Dan Mackenzie, alisema aliripoti suala hilo kwa polisi baada ya baadhi ya ndugu zake na binamu zake kukataa kula. Pia alisema aligundua kuwa watoto hao hawakuwa wakienda shuleni. “Nilichukua hatua na kwenda kuripoti kwa polisi. Hali yao si mbaya, lakini walipewa chakula kabla ya kuchukuliwa na polisi,” Dan alisema katika mahojiano na Taifa Leo. Dan alidai watoto hao walikuwa wakiendelea kufuata mafundisho yanayofanana na yale yanayohusishwa na vifo vya zaidi ya watu 400 katika mauaji ya Shakahola. Afisa huyo wa DCI alisema Bi Mumwele atazuiliwa hadi atakaposhtakiwa mahakamani Alhamisi. “Tutamshtaki kwa makosa yanayohusiana na ukatili dhidi ya watoto, kuwatesa na kuwanyima watoto haki ya kupata elimu,” afisa huyo alisema. Kuokolewa kwa watoto hao kunafanyika zaidi ya miaka miwili baada ya Mackenzie kukamatwa na kushtakiwa pamoja na washtakiwa wenzake kadhaa kuhusiana na vifo vinavyohusishwa na mauaji ya Shakahola na Kwa Binzaro katika Kaunti ya Kilifi. Mackenzie anakabiliwa na mashtaka 191 ya mauaji yanayohusiana na vifo vya Shakahola. Waendesha mashtaka pia wamemshtaki kwa kosa la kuua bila kukusudia kuhusiana na vifo vingine 52 vinavyohusishwa na mauaji ya Kwa Binzaro. Pia anakabiliwa na mashtaka ya ugaidi na kueneza misimamo mikali.
DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Prof Palamagamba Kabudi, amewataka viongozi wapya wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini, kutumia falsafa ya 4Rs iliyoasisiwa na Dk Rais Samia Suluhu Hassan kama dira na nyenzo katika kutekeleza majukumu yao kwa lengo la kuimarisha demokrasia na kulisaidia…
…sets up ad hoc committee for investigation By Edwin Philip, Lafia The Nasarawa State House of Assembly has raised concerns over multiple taxation, saying the practice is imposing hardship on businesses and residents across the state. Speaker of the House, Dr Danladi Jatau, raised the concern while reading the House’s resolution on a Matter of […]
DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Profesa Palamagamba Kabudi, amevitaka vyama vya siasa kutumia fursa ya mazungumzo, ambapo amesema milango ya Serikali iko wazi na Rais Samia Suluhu Hassan yupo tayari kuwasikiliza wasiwe na hofu. Prof Kabudi amesema hayo leo, Oktoba 7, 2026, jijini Dar…
DAR ES SALAAM: Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Dorothy Semu, amesema taasisi hiyo itaendelea kuunga mkono majukwaa yanayowezesha mazungumzo, uvumilivu, ushirikishwaji, kuheshimu tofauti za kisiasa na utatuzi wa migogoro kwa njia ya amani na kisheria. Semu amesema hayo leo, Oktoba 7, 2026, jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Uongozi Mpya na Nembo…
SHEREHE iliyolenga kuwawezesha vijana, wanawake na watu wenye ulemavu mjini Homa Bay iligeuka kuwa vurugu baada ya kundi la vijana kuvamia hafla iliyohudhuriwa na Waziri wa Vyama vya Ushirika Wycliffe Oparanya na kuondoka na baadhi ya vifaa. Hafla hiyo iliandaliwa na Mbunge Mwanamke wa Homa Bay Joyce Osogo, maarufu Bensuda, katika Uwanja wa Raila Odinga. Lengo lilikuwa kupatia vikundi vifaa vya kuanzisha au kupanua biashara, huku vifaa vilivyotolewa vikijumuisha mashine za kushona, na kusaga, pampu za kuosha magari na vifaa vingine. Hafla ilipokaribia kumalizika, baadhi ya vijana waliingia uwanjani na kuanza kubeba vifaa vilivyokuwa vimepangwa kugawiwa vikundi. Oparanya alijaribu kuwatuliza bila mafanikio. “Kwa nini mnaiba vitu ambavyo vimeletwa kuwasaidia? Tumeleta vitu vingi kuwasaidia wananchi. Hakuna haja ya kuiba,” alisema. Katika tukio jingine, kikundi kilipopewa mashine, baadhi ya vijana walijaribu kuinyakua. “Linda mashine uliyopewa. Ukipoteza hii, hutapewa nyingine,” Oparanya alionya. Bensuda aliamuru baadhi ya vifaa vilivyosalia vipakiwa kwenye magari na kuwekwa mahali salama. Baadaye alidai mmoja wa waliopanga vurugu hizo ni mfanyakazi wa Serikali ya Kaunti ya Homa Bay. Viongozi wa eneo hilo walilaani tukio hilo, wakisema linaweza kuwa ishara ya kuongezeka kwa vurugu za kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027. Seneta wa Homa Bay Moses Kajwang alisema vijana hao wanapaswa kudhibitiwa mapema. “Tuna kizazi ambacho ni kigumu kukabiliana nacho. Tusipowadhibiti sasa, tutakumbana na hali ngumu baadaye,” alisema. Kamanda wa Polisi wa Homa Bay Lawrence Koilem alisema hakukuwa na ripoti rasmi ya wizi iliyowasilishwa, lakini alithibitisha kuwa polisi walifika baada ya kupata taarifa za vurugu na wakaagiza vifaa vilivyosalia kuwekwa mahali salama.
GAVANA wa Kaunti ya Isiolo, Abdi Guyo, alifika mbele ya kamati ya seneti pasipo ajenda rasmi, mwaliko wala tarehe ya kikao na kuweka utangulizi unaowapa mwanya wakuu wa kaunti kuamua kuhusu ni lini na jinsi ya kujitokeza mbele ya seneti. Gavana Guyo ambaye wakati wa kujitokeza kwake alikuwa angali chini ya kibali cha kukamatwa aliendelea kuwasilisha majibu ya usimamizi wake kwa maswali yaliyoulizwa na mkaguzi mkuu hatua ambayo ni kinyume cha sheria na kanuni za bunge. Kulingana na katiba, ajenda rasmi almaarufu Nakala ya Taratibu inapatia kamati ya bunge mamlaka ya kuketi na kuendesha shughuli zake chini ya ratiba rasmi. Kuwasilisha kiholela masuala, nakala au mjadala bila notisi ya awali ni sawa na kukiuka kanuni isipokuwa tu wanakamati wanapopitisha hoja maalum ya kufanyia marekebisho ajenda husika. Kipengee 125 cha Katiba kinatoa mwongozo maalum unaotumika na kamati ambapo shahidi (au gavana) anapaswa tu kujitokeza kufuatia mwaliko rasmi, amri kisheria au notisi inayotolewa na katibu wa kamati kwa niaba ya mwenyekiti. Gavana wa Isiolo alijiwasilisha mbele ya Kamati ya Seneti kuhusu Ukaguzi wa Hesabu za Umma (CPAC) katika kikao Jumanne wiki iliyopita badala ya kusubiri kuwasilishwa na Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja. Kwa kawaida, Inspekta Jenerali anahitajika kisheria kukamata na kuwasilisha gavana anayekaidi amri ya kufika mbele ya kamati wakati kibali cha kumkamata kinapotolewa. Gavana huyo alisusia mara kadhaa kuhudhuria vikao na kukaidi maagizo ya seneti kujibu maswali ya ukaguzi kuhusu fedha zilizotengewa kaunti ya Isiolo na kumlazimu Mwenyekiti wa CPAC, Moses Kajwang, kuamuru akamatwe mnamo Julai 2026. Alipojitokeza hata hivyo, Gavana aliomba msamaha ambapo Naibu Mwenyekiti wa CPAC, Seneta Samson Cherargei aliyeongoza kikao hicho, aliondoa kibali cha kumkamata baada ya kuthibitisha Bw Guyo amelipa faini ya Sh500,000. “Ninaomba msamaha kamati hii kwa nyakati nilizokosa kujitokeza. Kila niliposhindwa kuhudhuria niliandika barua rasmi…nimelipa faini ya Sh500,000 kwa katibu kutoka mifukoni mwangu binafsi,” alisema Gavana Guyo. Naibu Mwenyekiti wa kamati alifafanua kuhusu hali isiyo ya kawaida ya kikao hicho akihoji kwamba CPAC ilipaswa kutilia maanani masuala ya wajibikaji badala ya taratibu akinukuu sheria kuhusu haki ya kusikizwa. “Maadamu gavana amelipa faini kutoka mfukoni mwake binafsi na amejiwasilisha, gavana ameondolewa kibali cha kumkamata,” alitangaza. “Gavana unafahamu hali ya kipekee kuhusu kikao hiki. Ni kwa sababu ulikuwa chini ya kibali cha kukukamata. Ndiposa hakuna mwaliko, tarehe ya kikao na ajenda.” Seneta wa Kitui, Enoch Wambua alisema kwa kuwa mkutano na Bw Guyo haukoordheshwa kwenye ajenda ya siku hiyo, angeshirikishwa tu chini ya “shughuli nyingine yoyote,” akielezea wasiwasi kwamba magavana watarajiwa akiwa mmoja wao kama anayemezea mate ugavana, huenda wakatumia vibaya tukio hilo.
Speaker of the UK House of Commons Sir Lindsay Hoyle has praised Tanzania’s role in parliamentary diplomacy and efforts to strengthen economic development and international cooperation.
DAR ES SALAAM: Dk Norga Komba, Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini China, anasema kwa mtazamo wake, utekelezaji wa Ilani ya chama hicho katika kipindi hiki unaonekana katika maeneo mbalimbali yanayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja, hususan nishati, miundombinu, uwekezaji, elimu, afya na huduma za kijamii. Katika sekta ya…
By Victor Ahiuma-Young The African Regional Organisation of the International Trade Union Confederation, ITUC-Africa, has raised the alarm over a growing decent work deficit affecting millions of young workers across the continent.The organisation, representing 18 million workers through 107 affiliated national centres in 52 countries, said young Africans are increasingly trapped in informal, unstable and […]
WAZIRI wa Afya Aden Duale amesema hakuna mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini, huku serikali ikiendelea kuwafuatilia watu 57 waliokutana na mgonjwa aliyefariki Jumanne. Duale alisema watu 10 kati ya waliofuatiliwa wamewekwa karantini jijini Nairobi huku ufuatiliaji wa wengine ukiendelea. Alisema serikali pia imejiandaa kwa uwezekano wa kuwapokea watu wanaohitaji kutengwa, huku vituo maalum vya kutenga wagonjwa vikiwa tayari. Waziri huyo alisema hatua za uchunguzi na ufuatiliaji zimeimarishwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), hasa katika Lango 16, ambako wasafiri wanaowasili kutoka nchi 10 zilizoathiriwa na Ebola wanakaguliwa zaidi. Hata hivyo, Duale alisema serikali haijafunga mipaka kutokana na tishio hilo. Alisisitiza kuwa hatua zinazochukuliwa ni za kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo na kuhakikisha watu wanaoingia nchini wanachunguzwa ipasavyo. Waziri huyo alisema ufuatiliaji wa watu waliokutana na wagonjwa au wanaoweza kuwa katika hatari unaendelea, huku mamlaka za afya zikiendelea kufuatilia hali hiyo kwa karibu. Serikali pia imeweka tayari miundombinu ya kutenga wagonjwa iwapo kutatokea hitaji la kufanya hivyo. Hatua hizo zinajiri huku mamlaka za afya zikiimarisha uangalizi katika vituo vya kuingilia nchini, hasa kwa wasafiri wanaotoka maeneo yaliyoripoti visa vya Ebola. Duale alihakikisha wananchi kuwa hakuna mlipuko wa Ebola nchini kwa sasa, huku serikali ikiendelea kuchukua tahadhari ili kuzuia ugonjwa huo kuingia na kuenea nchini.
ABIRIA mmoja amefariki baada ya kupata tatizo la kiafya akiwa ndani ya ndege ya Kenya Airways (KQ) iliyokuwa ikisafiri kutoka Nairobi kuelekea Lagos, Nigeria. Kwa mujibu wa Kenya Airways, abiria huyo alipoteza fahamu muda mfupi kabla ya ndege kutua katika Uwanja wa Kimataifa wa Murtala Muhammed, Lagos, Jumanne usiku. Shirika hilo lilisema Jumatano kwamba tukio hilo lilitokea mwendo wa saa tatu usiku kwa saa za Nigeria, takriban dakika 20 kabla ya muda uliopangwa ndege kutua. “Kenya Airways PLC inathibitisha kwamba mnamo Jumanne, Oktoba 6, 2026, ndege yetu kutoka Nairobi kuelekea Lagos ilikumbwa na hali ya dharura ya kiafya ndani ya ndege ikiwa eneo la Nigeria,” KQ ilisema. Shirika hilo lilisema abiria huyo alipatikana amepoteza fahamu takriban dakika 20 kabla ya ndege kutua Lagos. Ndege hiyo ilitua katika uwanja huo mwendo wa saa tatu na dakika arobaini na moja usiku, ambapo wahudumu wa afya waliingia ndani ya ndege kumhudumia abiria huyo. KQ ilisema hali ya abiria huyo ilizidi kuwa mbaya ndege ikiwa angani, na hivyo wafanyakazi wa ndege wakaanza taratibu za kukabiliana na dharura. Wahudumu wa ndege walitoa huduma ya kwanza huku wakijiandaa kutua Lagos, ambako wahudumu wa afya walikuwa wameandaliwa kupokea ndege hiyo. Kenya Airways iliwasilisha pole kwa familia na marafiki wa marehemu na kuomba radhi kwa usumbufu uliosababishwa na tukio hilo. “Tunatuma pole zetu za dhati kwa familia na marafiki wa marehemu na tunaomba radhi kwa usumbufu wowote ambao tukio hili huenda limesababisha. Tunaheshimu faragha na utu wa wote waliohusika,” shirika hilo lilisema. KQ ilisema inashirikiana na familia ya marehemu, mamlaka za eneo hilo na wadhibiti wa sekta ya usafiri wa anga kutoa msaada unaohitajika na kuwezesha taratibu zinazohitajika kufuatia kifo hicho. Shirika hilo halikufichua jina wala uraia wa abiria huyo. Hili si tukio la kwanza ambapo abiria wa Kenya Airways anafariki baada ya kupata dharura ya kiafya akiwa safarini. Aprili 2025, abiria mzee aliyekuwa akisafiri kwa ndege ya KQ kutoka New York kuelekea Nairobi alifariki baada ya kuugua akiwa ndani ya ndege. Ndege hiyo ilielekezwa kutua Entebbe, Uganda, ili abiria huyo apate matibabu ya dharura, lakini alitangazwa kufariki kabla ya ndege kutua. Mwaka 2022, Kenya Airways pia ilirekodi vifo vitatu vya abiria ndani ya kipindi cha takriban wiki nne katika safari kati ya Nairobi, Mombasa, New York na Casablanca. Tukio la kwanza lilitokea Agosti 22, 2022, katika ndege ya KQ003 iliyokuwa ikitoka New York kuelekea Nairobi. Abiria mmoja aliugua akiwa ndani ya ndege na safari hiyo ikaelekezwa Casablanca, Morocco. Baada ya kutua, wahudumu wa afya walimhudumia lakini wakathibitisha alikuwa amefariki. Siku 10 baadaye, Septemba 1, 2022, abiria mwingine aliyekuwa akisafiri kwa ndege ya KQ002 kutoka Nairobi kwenda New York alipatikana akiwa hajitambui na baadaye kuthibitishwa kuwa amefariki. Mnamo Septemba 14, 2022, abiria mwingine alipata matatizo makubwa ya kupumua wakati wa kupanda ndege ya KQ612 kutoka Nairobi kwenda Mombasa. Wahudumu wa afya walifika, lakini abiria huyo alifariki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA). Visa hivyo vinaonyesha changamoto ambazo mashirika ya ndege na wahudumu wa afya hukabiliana nazo pale abiria anapopata dharura kubwa ya kiafya akiwa safarini.
AFRIKA bado inaagiza dawa nyingi inazotumia kutoka nje ya bara, hali inayoziacha nchi kama Tanzania katika utegemezi wa minyororo ya kimataifa ya usambazaji, wakati serikali mbalimbali barani humo zikiongeza juhudi za kujenga uwezo wa kuzalisha dawa ndani ya nchi. Changamoto hiyo inaonekana wazi Tanzania, ambako uzalishaji wa dawa nchini bado uko chini sana ya mahitaji…
BRAZIL: ZANZIBAR’S young football stars have landed in Brazil, ready to fly the flag at the PQCUPBRASIL 2026 youth tournament. The 18-player Zanzibar Spice Boys U-13 squad arrived early today at Belo Horizonte/Confins–Tancredo Neves International Airport ahead of the tournament, which runs from October 10-15 in Minas Gerais. Led by delegation head Ambassador Abdulsamad Abdulrahim,…
Kwa zaidi ya miongo miwili, Tanzania imekuwa ikitegemea kwa kiasi kikubwa ufadhili wa kimataifa katika kuendesha baadhi ya huduma muhimu za afya, hasa mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI. Miongoni mwa washirika wakubwa ni Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR), ambao kwa miaka mingi umechangia upatikanaji wa huduma za…
TANZANIA inakabiliwa na changamoto ya kuendeleza baadhi ya huduma muhimu za afya baada ya mabadiliko katika ufadhili wa Marekani kuibua wasiwasi kuhusu uendelevu wa programu za kupambana na Virusi vya Ukimwi (VVU), matibabu, huduma za maabara na huduma zinazotolewa kwa jamii. Kwa zaidi ya miongo miwili, Marekani kupitia Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani…
…No case in Nigeria, agency says By Chioma Obinna The Nigeria Centre for Disease Control and Prevention, (NCDC) yesterday heightened vigilance across the country following confirmation of an imported case of Ebola disease caused by the Bundibugyo virus in Kenya.The development has raised concerns over the risk of international importation of the disease into Nigeria […]
MWANAMKE mmoja katika Kaunti ya Homa Bay alikamatwa na kuzuiliwa na polisi baada ya uchunguzi kumhusisha na mauaji ya mumewe ambayo awali alikuwa ameenda kuripoti katika kituo cha polisi. Rose Akoth alifika katika Kituo cha Polisi cha Ndiru Jumatatu akidai kuwa mumewe, John Okoko, alikuwa ameuawa na watu wasiojulikana. Hata hivyo, maelezo aliyotoa yaliibua maswali na kuwafanya maafisa wa usalama kuanza kumchunguza kwa kina. Mwili wa Okoko, mwenye umri wa miaka 42, ulipatikana ukiwa umetupwa kwenye kichaka katika Kijiji cha Kadibuoro, Kaunti ya Homa Bay, Jumapili. Polisi wanasema uchunguzi wao ulionyesha kuwa mauaji hayo yalifanyika nyumbani kwake kabla ya mwili kuhamishwa na kutupwa eneo ulikopatikana. Kwa mujibu wa polisi, Okoko aliuawa akiwa amelala ndani ya nyumba yake baada ya kupigwa kwa kifaa kizito. Baada ya mauaji hayo, washukiwa walioshiriki walidaiwa kuusafisha mwili huo bafuni, kumvisha nguo nyingine na baadaye kuubeba umbali wa takriban kilomita moja hadi kichakani. Kamanda wa Polisi wa Rangwe, Magdalene Chebet, alisema Akoth awali alidai kuwa mumewe alikuwa ameenda kukutana na mkulima aliyekuwa amemwahidi miche ya mpunga kabla ya kuuawa na mtu asiyejulikana. Alipoulizwa maswali zaidi na kuombwa kuwaongoza maafisa hadi nyumbani kwake, polisi waligundua ushahidi uliobadilisha mwelekeo wa uchunguzi. Madoa ya damu yalipatikana kwenye kuta za chumba cha kulala na kwenye kitanda cha wanandoa hao. “Ushahidi huo ulitosha kuonyesha kuwa marehemu aliuawa ndani ya nyumba,” alisema Chebet. Baada ya kuhojiwa zaidi, Akoth alidaiwa kuwahusisha mwanawe mwenye umri wa miaka 24 na mwanaume mwingine mwenye umri wa miaka 36 kuwa washirika katika mauaji hayo. Habari za kukamatwa kwa washukiwa hao ziliwashtua wakazi wa eneo hilo ambao hapo awali walidhani Okoko alikuwa ameuawa na watu wasiojulikana. Wakazi wenye hasira walimvamia mshukiwa huyo wa miaka 36 kabla ya polisi kuingilia kati na kumuokoa. Polisi wamesema bado hawajabaini sababu ya mauaji hayo. Washukiwa wote watatu wanazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Ndiru wakisubiri kufikishwa mahakamani, huku mwili wa Okoko ukihifadhiwa katika mochari ya Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Homa Bay kwa uchunguzi wa maiti
IDARA ya usalama katika Kaunti ya Lamu inachunguza kutoweka kwa zaidi ya vijana 50 wanaoaminika kuvuka hadi nchi jirani ya Somalia kujiunga na kundi la kigaidi la Al-Shabaab. Kamishna wa Kaunti ya Lamu, Bw Stephen Sangolo, alithibitisha kutoweka ghafla kwa vijana hao mapema mwezi uliopita. Ripoti za kutoweka kwao zilianza kuibuka siku chache kabla na baada ya sherehe za awamu ya 137 za Maulid kisiwani Lamu. Sherehe hizo zilifanyika Septemba 9 hadi 12.Baadhi ya vijana waliotoweka walikuwa miongoni mwa waliosafiri kutoka visiwa mbalimbali vya Lamu kufika kwenye mji wa kale wa Lamu kuhudhuria tamasha hizo za kila mwaka. Vijiji ambapo vijana wameripotiwa kutoweka kwa wingi ni vile vya kisiwa cha Pate, kaunti ndogo ya Lamu Mashariki, ikiwemo Siyu, Shanga-Rubu, Faza, Kizingitini, Tchundwa, Mbwajumwali na Myabogi. “Tuko na ripoti za ujasusi kuwahusu vijana wapatao 50 wa Lamu waliovuka kisiri kuingia nchini Somalia. Baadhi ya wanafamilia tayari wamefika kwenye vituo vyetu vya polisi kupiga ripoti kuhusu watu wao kutoweka. Usalama umeimarishwa kila upande, ikiwemo sehemu za mpakani kama vile Kiunga wakati tukiwatafuta waliotoweka,” akasema Bw Sangolo. Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Lamu, Bw Shadrack Ruto, pia alithibitisha kutoweka ghafla kwa vijana hao karibu mwezi mmoja uliopita sasa. Bw Ruto alionya kuhusu kuwepo kwa maajenti wa makundi ya kigaidi ambao wamekuwa wakiendeleza usajili wa vijana kujiunga na Al-Shabaab maeneo ya Lamu. Maajenti hao wamekuwa wakitumia njia za kijanja kuwasajili vijana, ikiwemo kuwaahidi kazi na mishahara mikubwa, ambazo Bw Ruto alizitaja kuwa za uongo.Pia aliionya jamii dhidi ya kuwaamini baadhi ya wanaowaendea na kutangamana nao kwa kujidai kuwa wanachama wa mashirika ya wahisani yanayotiliwa shaka.“Kuna watu wanaojidai kuleta misaada na fedha za kusaidia jamii. Baadaye wananyemelea vijana wasiokuwa na ajira. Wanawatenga na kuwaahidi kazi, vyeo vikubwa na mishahara minono. Wanawapokeza vijana hao mafundisho ya itikadi kali kabla ya kuwavukisha Somalia. Tuko macho kukabili uozo huo,” akasema Bw Ruto.Wakuu hao wa usalama waliwashauri wazazi kufuatilia kwa karibu mienendo ya watoto wao na kuchunguza kazi wanazoahidiwa ili kuepusha vijana wasijipate mtegoni.Kutoweka kwa vijana 50 katika hali tatanishi kunajiri wakati ambapo Lamu imeshuhudia kuimarika kwa usalama kufuatia kuzinduliwa kwa oparesheni inayoendelea msituni Boni mnamo Septemba 2015. Oparesheni hiyo iliyoanzishwa na serikali kuu, inadhamiria kuwasaka na kuwamaliza magaidi wa Al-Shabaab wanaoaminika kujificha ndani ya msitu mkuu wa Boni.Juni 2014, magaidi wa Al-Shabaab kutoka Somalia, wakiwa wamejihami kwa silaha hatari, walivamia mji wa Mpeketoni na viunga vyake, ambapo waliua watu zaidi ya 90, wengi wao wakiwa ni wanaume kwa usiku mmoja.Magari na nyumba kadhaa ziliteketezwa kwenye uvamizi huo ambao hadi leo unazingatiwa kuwa miongoni mwa mashambulio mabaya zaidi ya kigaidi kuwahi kushuhudiwa nchini.
DAR ES SALAAM: AGE-BASED lending restrictions should be reviewed to give financially capable older customers greater consideration for credit, with borrowers’ financial position and repayment capacity also taken into account, an Absa Bank Tanzania customer has said. Long-serving Absa customer Hilary Biduga, who operates businesses in the tourism and transport sectors, made the remarks during…
WASHUKIWA 1,827 wamekamatwa nchini kwa tuhuma za kuhusika katika uhalifu wa magenge kati ya Januari na Agosti mwaka huu, huku 729 wakipatikana na hatia. Kati ya kesi hizo, 716 bado ziko mahakamani huku serikali ikiongeza msako dhidi ya makundi hayo kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027.Idara ya Serikali ya Usalama wa Ndani na Utawala wa Kitaifa, imetambua magenge na makundi 109 ya wahalifu nchini, idadi ambayo imeongezeka kutoka 89 yaliyotangazwa kuwa haramu kupitia Gazeti la Serikali Nambari 10427 la mwaka 2016.Katibu wa Usalama wa Ndani, Dkt Raymond Omollo, alisema serikali haitawalenga watu wanaotekeleza uhalifu pekee, bali pia viongozi, wafadhili na wanaoendesha shughuli za makundi hayo.Trans Nzoia inaongoza kwa idadi ya washukiwa waliokamatwa ikiwa na 491, ikifuatiwa na maeneo mengine yaliyoathiriwa na vitendo vya magenge. Kwa mujibu wa serikali, magenge hayo yanaweza kutumiwa wakati wa uchaguzi kuvuruga mikutano, kuwatisha wapinzani, kushambulia na kusababisha ghasia.Katibu wa Usalama wa Ndani, Raymond Omollo, alisema serikali haitawalenga watu wanaotekeleza uhalifu pekee, bali pia viongozi, wafadhili na wanaoendesha shughuli za makundi hayo.“Wale wanaoajiri, kufadhili au kuongoza makundi hayo watawajibishwa pamoja na wanaotekeleza ghasia,” alisema.
SUALA la nani atakayevishwa urithi wa kisiasa wa marehemu Raila Odinga limeingia sura mpya baada ya bintiye Winnie Odinga kutawazwa kuwa mrithi wa kisiasa wa baba yake. Winnie, ambaye ni mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), alitawazwa Jumamosi katika hafla iliyohudhuriwa na mama yake Ida Odinga pamoja na wazee na washirika wa familia. Hata hivyo, kutokuwepo kwa kaka yake, Raila Odinga Junior, kulifanya tukio hilo kuzua maswali kuhusu mwelekeo wa familia kuelekea uchaguzi wa 2027. Raila Junior alisema hakujua kuhusu hafla hiyo na akasisitiza kuwa tayari anaendelea kujenga safari yake ya kisiasa. Siku hiyo hiyo, Raila Junior na Jaoko Oburu, mwanawe kiongozi wa ODM Oburu Oginga, walimtembelea Waziri wa Ushirika Wycliffe Oparanya nyumbani kwake Mabole, Kakamega. Katika ziara hiyo, Oparanya aliunga mkono azma ya Raila Junior kuwania ubunge Kibra na Jaoko kuwania kiti cha Bondo. Matukio hayo mawili yaliyofanyika siku moja yameonyesha jinsi familia hiyo inavyokabili suala nyeti la urithi wa kisiasa baada ya kifo cha kiongozi huyo. Winnie amekuwa akishinikizwa na baadhi ya wafuasi wa marehemu baba yake kuchukua nafasi ya mbele katika siasa kuelekea 2027. Kiti cha useneta Nairobi kimetajwa kuwa mojawapo ya nafasi anazoweza kuwania. Wafuasi hao wanamtaja Winnie kama mtu aliyekuwa karibu na kampeni za baba yake kwa miaka mingi na aliyeshiriki katika kazi za ubunifu, mawasiliano na matumizi ya teknolojia katika kampeni zake. Baada ya kutawazwa, Winnie alisema alikuwa amejitenga na siasa kwa muda ili kuomboleza kifo cha baba yake. “Watu wengi walikuwa wakiuliza nilikoenda lakini niliamua kuchukua muda kumuomboleza Jakom. Niliona askari wa Raila walivunjika moyo alipofariki na hawakutaka tena kupigana. Ndiyo maana nilikaa kimya kwa mwaka mmoja kuomboleza, lakini sasa muda huo umeisha na ni wakati wa kusonga mbele,” alisema. Winnie pia alizungumzia umuhimu wa wazee katika masuala ya urithi, akisema madaraka hayapaswi kunyakuliwa kwa nguvu. “Cheo au nafasi si kitu cha kuchukuliwa kwa nguvu. Wazee wana jukumu la kuhifadhi na kulinda jamii, kwa hivyo lazima tuamue njia inayotufaa,” alisema. Kwa upande wake, Raila Junior alisema analenga kujijengea jina kisiasa badala ya kutegemea jina la baba yake. “Ninazingatia kujenga taaluma yangu ya kisiasa kama Raila Junior, Raila Kembo. Nina matumaini nitafanikiwa. Sitategemea tu jina la Baba wala kupigana kuidhinishwa na mtu,” alisema. Alisema pia alikuwa na shughuli nyingine siku hiyo na hakujua kuhusu hafla ya kutawazwa kwa dada yake. Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Luo, Odungi Randa, alisema hakuwa kwenye hafla hiyo na angezungumza na wazee waliohudhuria kabla ya kutoa msimamo. Hata hivyo, mzee Jotham Ajiki, ambaye ni katibu wa baraza hilo, alisema hakuwa na sababu ya kuomba msamaha kwa sababu alialikwa nyumbani kwa Ida bila kujua yaliyokuwa yamepangwa. “Niliitwa na Mama Ida kwa hafla hiyo na nikaelekezwa nilichopaswa kufanya. Siwezi kuomba msamaha kwa kilichotokea kwa sababu nilikuwa mgeni wa Mama,” alisema. Wakati huo huo baadhi wamemtaka Ida Odinga kutoa mwelekeo kuhusu nafasi ya familia ndani ya ODM. Bw,Jaramogi Ogana, alisema wanataka familia ikubaliane kuhusu mtu mmoja wa kuwakilisha urithi huo ili kuepusha migongano. “Tunataka mkubaliane mtoe mtu mmoja kwa sababu hatutaki mgongano na tutamuunga mkono,” alisema.
BAADA ya kuchukua tahadhari kwa miezi kadhaa, Wizara ya Afya jana ilithibitisha kisa cha kwanza cha Ebola aina ya Bundibugyo nchini Kenya. Wizara ilisema mgonjwa huyo aliyekuwa raia wa Kenya alifariki Jumatatu usiku na hatua zimechukuliwa kwa kuzingatia taratibu za kiafya. Waziri wa Afya Aden Duale alisema Jumanne kuwa mwanamume huyo alikuwa ameishi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa miaka saba, ambako aliugua takriban mwezi mmoja uliopita na kutibiwa katika hospitali kadhaa. Mgonjwa huyo alisafiri kwa barabara kutoka DRC hadi Kampala, Uganda, kabla ya kupanda ndege ya Jambojet 8523 kuelekea Nairobi. Alifika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) saa saba mchana Jumamosi, Oktoba 3, na kufanyiwa ukaguzi wa kawaida wa afya katika kituo cha afya cha uwanja huo kabla ya kupitia taratibu za uhamiaji. Jamaa na rafiki walimchukua JKIA kwa gari aina ya Toyota Fielder na kumpeleka katika hospitali moja jijini Nairobi, ambako alitengwa haraka katika chumba maalum katika kitengo cha dharura kabla ya kuhamishiwa kituo cha kutengwa wagonjwa cha East Wing. Alifika hospitalini akiwa na homa, baridi, uchovu mwingi, udhaifu, maumivu ya misuli, maumivu wakati wa kumeza, maumivu ya koo na kutokwa na damu chini ya ngozi katika maeneo aliyodungwa sindano. Madaktari walishuku alikuwa na homa ya virusi inayosababisha kutokwa na damu kutokana na dalili na historia yake ya safari nchini DRC. Sampuli zake zilipimwa katika Maabara ya Kitaifa ya Virusi na maabara ya Kenya Medical Research Institute (KEMRI), na zote zikathibitisha kuwa alikuwa na Ebola aina ya Bundibugyo. Mgonjwa huyo alipatiwa matibabu ya kumsaidia, lakini alifariki. Mazishi yake yalipangwa kufanyika Jumanne kwa kuzingatia taratibu salama na zenye heshima za mazishi ya waathiriwa wa Ebola. Wizara imetambua watu 28 waliowasiliana na marehemu, wakiwemo jamaa na wahudumu wa afya waliomhudumia. Duale alisema pia abiria 23 na wahudumu wanne waliokuwa katika ndege moja na marehemu wanafuatiliwa huku mipango ya kuwaweka walio katika hatari karantini ikiendelea. “Kenya imekuwa katika hali ya tahadhari ya juu tangu mlipuko huu ulipoanza Mei 2026,” alisema Duale. Kufikia Jumanne, Wizara ilikuwa imewapima wasafiri 652,584 na kuchunguza sampuli 267 katika maabara tano. Aidha, wahudumu 4,971 wa afya katika ngazi ya kitaifa na kaunti wamefunzwa kuhusu kinga na udhibiti wa Ebola. “Ni kipimo kimoja pekee ambacho kimepatikana kuwa cha Ebola,” taarifa ya Wizara ilisema. Duale aliwataka Wakenya kutokuwa na hofu, akisema mifumo yote ipo tayari kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo. Aliwashauri wananchi kunawa mikono mara kwa mara, kutumia dawa za kusafisha mikono na kuepuka mawasiliano ya karibu na wagonjwa wanaotoka katika nchi zilizo na maambukizi. Wananchi wenye dalili wanashauriwa kutafuta matibabu katika vituo vya afya vinavyotambuliwa na kutoa taarifa kuhusu wagonjwa wanaowajua. Wizara pia imewaagiza wahudumu wa afya kuzingatia viwango vya juu vya kuzuia na kudhibiti maambukizi. Wananchi wanaweza kupata taarifa kupitia majukwaa rasmi ya Wizara au kupiga simu ya bila malipo 719.
“Democracy is not merely a form of government. It is primarily a mode of associated living, of conjoint communicated experience.” — John Dewey The reactions to my recent article, “Election Without Political Parties: Outlook Towards 2027”, have been several, and they raised important questions that deserve further examination. If political parties in Nigeria are losing […]
AZMA ya Edwin Sifuna ya kuwania urais inaonekana kuingia katika kipindi chake kigumu zaidi. Kilichoanza kama harakati yenye nguvu na umoja chini ya Linda Mwananchi sasa kimeanza kugeuka mgawanyiko na kuibua misafara tofauti ya kisiasa. Kila kikosi kikuu kilichoonekana kuwa tayari kuunga mkono mradi wa urais wa vuguvugu hilo sasa kinaonekana kujenga utambulisho wake wa kisiasa. Swali si tena ikiwa Linda Mwananchi ina nyufa, bali ikiwa Sifuna atastahimili kuziziba nyufa hizo kabla ya uchaguzi wa 2027. Kuibuka na kuimarika kwa vyama vinavyohusishwa na wanasiasa kama Babu Owino, James Orengo, Caleb Hamisi, Boni Khalwale, George Natembeya, Eugene Wamalwa na Rigathi Gachagua kunazua maswali mazito. Je, wanajiandaa kwa mazungumzo ya kisiasa, wanajilinda dhidi ya kusalitiwa, au ni ishara ya kutokuaminiana ndani ya upinzani? Uamuzi wa Sifuna kukumbatia The Equitable Party (TEP) dakika za mwisho unaibua maswali chungu nzima. Je, ulikuwa mkakati uliopangwa kwa makini au anajaribu kupakata kivuli baada ya kushindwa kuifanya Linda Mwananchi kuwa chombo chake cha urais? Muda sasa unakuwa silaha ya kisiasa. Muda wa usajili, uteuzi wa wagombea na mipango ya miungano unakaribia, je, Sifuna ataweza kumudu suitafahamu ya kisiasa na kiuchaguzi kwa muda mrefu? Ikiwa TEP itakuwa chombo chake, je, jina, utambulisho na maana ya kisiasa ya TEP vinaweza kubadilishwa kuwa Linda Mwananchi kwa haraka? Zaidi ya hayo,Sifuna yuko tayari kubeba gharama kubwa ya kifedha na kiutawala ya kuipa TEP msukumo wa kitaifa uliokuwa umeanza kuhusishwa na Linda Mwananchi? Umaarufu wa mikutano na mitandao ya kijamii hauwezi moja kwa moja kugeuka kuwa kura, mawakala, ofisi, vifaa vya kampeni na mtandao wa vituo vya kupigia kura. Sifuna kuwauliza wenzake na wafuasi wake ikiwa wako tayari kwenda naye hadi “mwisho wa safari” au kumwacha kunaonyesha shinikizo la kisiasa linalomkabili. Anapaswa kuponya migawanyiko ya Linda Mwananchi, kujenga msingi wa kitaifa, kukijenga chama chake, kuwaunganisha viongozi wa upinzani na kuwashawishi Wakenya kuwa anaweza kumpa Rais William Ruto ushindani wa kweli. Ingawa baadhi ya wafuasi wake wanahisi kuwa jina Sifuna pekee linatosha kusisimua wananchi na kupata kura, anacho kibarua kutafuta fedha za kampeni na kujadiliana na viongozi wakuu ambao huenda nao wana matarajio ya urais au nafasi kubwa za kisiasa. Zaidi ya yote, lazima awajengee imani kwamba kumuunga mkono hakutakuwa kujitoa mhanga kisiasa. Je, Sifuna alielewa kikamilifu mzigo uliomsubiri kabla ya kutangaza azma yake ya urais? Mihemko ya kisiasa inaweza kuleta taswira ya umoja, hasa wakati wa mikutano mikubwa, kauli mbiu na umaarufu mitandaoni vinapotafsiriwa kama vidokezo vya kupata ushindi. Ndoto ya Sifuna bado haijafa, lakini njia imekuwa ngumu zaidi. Adui wake mkubwa kisiasa huenda sirais Ruto, bali mgawanyiko ndani ya upinzani wenyewe. Takribani ionozi wote wa upinzani wanakariri umuhimu wa kuungana na kumteua mwaniaji mmoja kuwania urais. Je, watakapofanya hivyo watampa Sifuna nafasi hiyo? Iwapo hawezi kubadilisha kutokuaminiana kuwa mazungumzo, vyama pinzani kuwa muungano na shauku ya kisiasa kuwa hamasa ya kitaifa, ndoto ya Linda Mwananchi inaweza kukumbana na anguko la mapema. Je, Sifuna ataweza kuwaunganisha vigogo waliokuwa wameahidi kutembea naye, kabla hawajaamua kutembea kivyao?
KUTAWAZWA kwa Naibu Rais Kithure Kindiki kuwa msemaji wa Mlima Kenya kumeibua mgawanyiko katika Baraza la Wazee la Kiama Kia Ma, huku makundi mawili yakidai kuwa ndiyo yenye mamlaka halali. Mkutano wa siri wa wazee 63 ulioitishwa Septemba 28 na mlezi wa baraza hilo, Kung’u Muigai, ulihitimisha kuwa Kiama Kia Ma, lililoanzishwa mwaka 2010, limegawanyika na kwa sasa halina mamlaka halali ya kumtawaza kiongozi yeyote hadi mzozo huo utatuliwe. Bw Muigai alisema mkutano huo ulianza saa mbili usiku na kumalizika karibu saa nane alfajiri. “Ilikuwa wazi kuwa Kiama Kia Ma lililoanzishwa mwaka 2010 na lililopaswa kufanya uchaguzi kila baada ya miaka minne sasa limegawanyika,” alisema. Mzozo huo unahusishwa pia na madai ya kughushi hati za usajili wa baraza hilo. Cheti kilichodaiwa kutolewa Agosti 20, 2019 kilikataliwa na Ofisi ya Msajili wa Mashirika, iliyosema saini iliyokuwa kwenye cheti hicho haikuwa ya afisa aliyedaiwa kuitia. Mwaka 2022, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) iliagiza Inspekta Jenerali wa Polisi kuchunguza madai ya kughushi cheti hicho na kuwasilisha ripoti. Mzozo huo pia umehusishwa na siasa za kuelekea uchaguzi wa 2027, huku madai yakitolewa kuhusu aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua. Hata hivyo, Gachagua amekanusha kuhusika na akawataja wazee waliomtawaza Kindiki kuwa “bandia”. Kindiki naye amejitenga na mzozo huo, akisema sherehe hiyo ilikuwa mpango wa wazee. “Nilikuwa mgeni wao. Wao ndio wanapaswa kujibu maswali hayo,” alisema. Sherehe ya kumtawaza Kindiki ilifanyika katika Uwanja wa Kirigiti, Kaunti ya Kiambu, Septemba 19.
DAR ES SALAAM: THEMinister for Energy Dr Juma Zuberi Homera has launched new customer service systems for the Tanzania Electric Supply Company (TANESCO), alongside an improved Customer Service Charter aimed at ensuring both large and small customers receive faster and more convenient services. Launching the systems in Dar es Salaam on October 6, 2026, Dr…
ARUSHA; Spika wa Bunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu amesema Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) si fursa pekee ya Wabunge kukutana kama wawakilishi wa Mabunge, bali pia ni wakati muhimu wa kutathmini jinsi mabunge yanavyoweza kukidhi matarajio ya wananchi na kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika jamii. Spika amesema hayo leo wakati…
“The crash of military aircraft in Nigeria under the Tinubu administration is a serious national issue that again raises questions on the subjects of equipping as well as welfare of our military and other security agencies under this administration, despite the enormous resources at its disposal,” Ihediwa said.
TANZANIA inakabiliwa na changamoto ya kuhakikisha mikataba ya madini inalinda maslahi ya Taifa kwa muda mrefu, wakati ushindani wa kimataifa wa rasilimali za madini barani Afrika ukiendelea kuongezeka. Mikataba ya madini ina nafasi muhimu katika kuamua nani anadhibiti uzalishaji, madini yatachakatwa wapi, Serikali itapata kiasi gani cha mapato na ni kwa kiwango gani shughuli za…
KILIMANJARO: Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umetunukiwa Cheti cha ISO 9001:2015 cha Mfumo wa Usimamizi wa Ubora na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), hatua inayolenga kuimarisha ubora wa huduma kwa wanachama, waajiri na wadau. Cheti hicho kimetolewa baada ya NSSF kukamilisha mchakato wa uhakiki na ithibati ya mfumo wake wa usimamizi wa…
The order on October 2 suspended provisions that industry players warned would raise the cost of doing business, deter foreign investment and drive cargo to rival ports.
Wizara ya Afya imethibitisha kisa cha kwanza cha ugonjwa wa Ebola nchini Kenya, huku mgonjwa aliyekuwa akiugua akifariki Jumatatu usiku mjini Nairobi. Waziri wa Afya Aden Duale alisema Jumanne, Oktoba 6, kuwa mgonjwa huyo alikuwa ametoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kupitia Uganda, kabla ya kuwasili Nairobi. Duale alisema mgonjwa huyo alikuwa akiishi na kufanya kazi DRC kwa miaka saba na alianza kuugua takriban mwezi mmoja uliopita. Alitibiwa katika hospitali kadhaa nchini humo kabla ya kusafiri kwa barabara kupitia Uganda kurejea Kenya. “Wizara ya Afya inawafahamisha wananchi kwamba imethibitisha kisa cha kwanza kilichoingizwa nchini cha ugonjwa wa Ebola aina ya Bundibugyo,” alisema Duale. Mgonjwa huyo baadaye alipanda ndege ya Jambojet iliyokuwa na abiria 23 na wahudumu wanne, na kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) Jumamosi, Oktoba 3, saa saba mchana. Alifanyiwa ukaguzi wa kawaida wa afya JKIA kabla ya kupita katika kituo cha uhamiaji. Baadaye alichukuliwa moja kwa moja kutoka uwanja huo na jamaa na marafiki kwa gari aina ya Toyota Fielder na kupelekwa Nairobi Hospital, ambako alitengwa katika chumba maalum. Alikuwa na dalili zikiwemo homa, baridi, uchovu mwingi, udhaifu, maumivu ya misuli, maumivu wakati wa kumeza na kutokwa na damu chini ya ngozi. “Kwa kuzingatia dalili na historia yake ya safari, madaktari walishuku homa ya virusi na kuchukua sampuli kwa uchunguzi, ambazo zilithibitisha kuwa alikuwa na Ebola,” Duale alisema. Sampuli hizo zilifanyiwa vipimo katika Maabara ya Kitaifa ya Virusi na Kenya Medical Research Institute (KEMRI), na taasisi zote mbili zikathibitisha maambukizi. Mgonjwa huyo alipatiwa matibabu ya kumsaidia kupunguza madhara ya ugonjwa huo, lakini alifariki Jumatatu saa tano na nusu usiku. Duale alisema maandalizi ya mazishi salama na yenye heshima yanaendelea, huku mazishi yakipangwa kufanyika baadaye Jumanne kwa kuzingatia taratibu za mazishi ya waathiriwa wa Ebola. Wizara imetambua watu 28 waliokuwa wametangamana na marehemu, wakiwemo jamaa na wahudumu wa afya waliomhudumia. Serikali pia inawatafuta abiria wengine 23 na wahudumu wanne waliokuwa katika ndege moja na marehemu. Duale alisema wahudumu 4,971 wa afya katika ngazi ya kitaifa na kaunti wamefunzwa kuhusu kinga na udhibiti wa Ebola. Alisema serikali pia imejulisha Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu kisa hicho. “Mifumo yote iko tayari kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu,” Duale alisema.
MIILI tisa ya waumini wa Kanisa Katoliki la St Mathias Mulumba, Mikindani waliofariki katika ajali ya barabarani eneo la Salama, Kaunti ya Makueni, imesafirishwa hadi Mombasa kuhifadhiwa huku mipango ya mazishi ikianza. Miili hiyo imehifadhiwa katika mochari ya Hospitali ya Jocham, Mombasa, baada ya kuwasili saa chache baada ya usiku wa manane kuamkia Jumatatu. Waathiriwa hao walikuwa miongoni mwa mahujaji waliofariki baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali kwenye barabara kuu ya Nairobi-Mombasa Jumamosi, ambapo watu 17 walipoteza maisha. Walikuwa wakisafiri kuelekea Madhabahu ya Subukia, Nakuru, kwa ajili ya Siku ya Kitaifa ya Maombi. Bw Martin Obwaka, aliyeongoza jamaa na marafiki walioenda hadi Salama kuchukua miili hiyo, alisema waliwasili Mombasa mwendo wa saa kumi usiku wa kuamkia Jumatatu. Bw Obwaka alisema walihakikisha miili hiyo imehifadhiwa ipasavyo kabla ya kuondoka katika saa kumi na mbili asubuhi. Rekodi za hospitalini zinaonyesha kuwa, miili hiyo iliwasili ikiwa katika magari matatu ya kusafirisha maiti. “Nilirekodi magari haya matatu ya kubeba maiti. Yalileta miili ya waathiriwa wa ajali ya Salama,” alisema mfanyakazi wa hospitalini. Baadaye msafara ulielekea hadi Kanisa Katoliki lililo Mikindani kwa ajili ya sala. Miili hiyo itasalia katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Jocham huku familia na kanisa zikiendelea na maandalizi ya mazishi. Mbunge wa Jomvu, Bw Badi Twalib, alisema Rais William Ruto alimpigia simu baada ya ajali hiyo na kuahidi kusaidia familia zote zilizopoteza wapendwa wao katika maandalizi ya mazishi. “Rais Ruto alinipigia simu binafsi kama mbunge wa eneo hili kufuatia msiba huu. Pia ameahidi kusaidia familia zote 17 zilizopoteza wapendwa wao katika ajali hiyo ya barabarani. Baadhi yao watasafiri hadi Nyanza, Ukambani na eneo la Kati, kwa hivyo tunamshukuru Rais kwa msaada wake. Huu ungekuwa mzigo mkubwa kwa familia, na tunamshukuru Kiongozi wa Nchi,” alisema Bw Twalib. Akizungumza katika Kanisa Katoliki la St Mathias Mulumba, Mikindani, Jumapili, Bw Twalib alisema Rais alimpa Katibu katika Wizara ya Mambo ya Ndani, Dkt Raymond Omollo, jukumu la kuhakikisha familia hizo zinapata msaada unaohitajika. Alisema Dkt Omollo anawasiliana na Kamishna wa Kaunti ya Mombasa, Mohamed Noor, ili kuratibu maandalizi hayo. Bw Noor alithibitisha kuwa serikali ya kitaifa itasaidia katika maandalizi ya mazishi ya mahujaji wote 17. Viongozi wa Mombasa waliungana kuwafariji familia zilizopoteza wapendwa wao katika ajali hiyo. Gavana wa Mombasa, Bw Abdulswamad Nassir, alifichua kuwa mwili mmoja pekee kati ya 17 ulikuwa bado haujatambuliwa kufikia Jumapili. Bw Nassir alisema anashirikiana na gavana mwenzake wa Makueni, Bw Mutula Kilonzo, kuratibu uchunguzi wa miili yote. Alihakikishia familia na kanisa kuwa serikali ya kaunti pia ingewasaidia katika mchakato huo. “Msijali kuhusu chochote. Tutagharimia kila kitu. Mungu awapunguzie maumivu yenu,” alisema. Spika wa Seneti, Bw Amason Kingi, alitaka uchunguzi wa kina ufanywe kuhusu ajali hiyo, akisema waliohusika kuisababisha wanapaswa kuwajibishwa kisheria. Aliwataka maafisa katika mamlaka husika kubaini chanzo cha ajali hiyo na kuhakikisha familia zilizofiwa zinapata haki.
Tanzania imetakiwa kuhakikisha ukuaji wa sekta ya madini mkakati unaenda sambamba na kuongeza thamani, ujenzi wa viwanda, ulinzi wa mazingira na ushiriki wa Watanzania ili rasilimali hizo ziwe kichocheo cha maendeleo ya muda mrefu ya taifa. Tanzania ina madini mbalimbali yanayohitajika katika minyororo ya kimataifa ya uzalishaji, yakiwemo grafaiti, nikeli, kobalti, lithiamu na madini adimu,…