WAHADHIRI na wafanyakazi wengine wa vyuo vikuu vya umma wamekataa pendekezo jipya la serikali kuhusu Mkataba wa Makubaliano ya Kazi (CBA) wa miaka ya 2025 hadi 2029, wakisema halikidhi matakwa yao.
Mzozo huo unahusisha tofauti kubwa kati ya madai yaliyowasilishwa na vyama vya wafanyakazi vya UASU, KUSU na KUDHEIHA na mapendekezo yaliyotolewa na Baraza la Vyuo Vikuu vya Umma (IPUCCF), linalowakilisha waajiri.
Vyama hivyo vilipendekeza nyongeza kubwa ya mishahara na marupurupu mbalimbali. UASU, kwa mfano, ilitaka mishahara ya msingi iongezwe kwa kiwango cha kati ya asilimia 36 na 68 kulingana na daraja la kazi. Pia ilipendekeza nyongeza ya asilimia 57 ya marupurupu ya nyumba, ya usafiri ya hadi Sh60,000 kwa baadhi ya daraja na ya maprofesa ya Sh80,000.
Aidha, chama hicho kilitaka marupurupu ya vitabu ya kati ya Sh65,000 na Sh90,000 kwa mwaka, ya likizo ya hadi Sh70,000 pamoja na bima ya matibabu, meno na macho.
Hata hivyo, waajiri walipendekeza ongezeko la chini zaidi. Baada ya kupitia chaguo mbalimbali, IPUCCF ilipendekeza mishahara iongezwe kwa asilimia mbili kila mwaka katika kipindi cha miaka minne ya CBA. Hii inatafsiriwa kuwa nyongeza ya jumla ya asilimia 8.25 pekee kufikia mwaka 2029.
Katibu Mkuu wa UASU, Dkt Constantine Wasonga, alisema vyama vya wafanyakazi havikushirikishwa kikamilifu katika kufikia uamuzi huo.
“Hatuwezi kupewa kiwango cha mwisho halafu tuelezwe tukubali. Maafikiano ya pamoja yanahitaji mazungumzo ya kweli,” alisema.
Mwenyekiti wa KUSU, Dkt Charles Mukhwaya, alisema wafanyakazi wamechoshwa na mazungumzo yasiyozaa matunda.
“Hatuwezi kuendelea kuzunguka katika jambo moja milele. Ikiwa haki zetu hazitazingatiwa, tuko tayari kwenda barabarani kudai tunachostahili,” alisema.
Kwa upande wake, KUDHEIHA imesema pendekezo la sasa halikidhi matarajio ya wafanyakazi na haiwapi nafasi ya kupanda madaraja kazini.
Mgomo wa wahadhiri wachacha, wakataa dili ya serikali

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsAfenifere demands prosecution of sponsors of campaign violence
…Raises alarm over rising attacks ahead of 2027 elections By Adeola Badru The pan-Yoruba socio-political organisation, Afenifere, has raised the alarm over increasing political violence ahead of the 2027 general elections, calling for the arrest and prosecution of perpetrators and their sponsors. The organisation warned that the growing incidents of thuggery, intimidation and inflammatory political […]
NewsPHOTOS: First Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsFirst Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsObi woos Onitsha voters, promises jobs, better services
…Says Nigeria needs energetic president By Vincent Ujumadu The presidential candidate of the Nigeria Democratic Congress (NDC), Peter Obi, on Friday drew a large crowd in Onitsha, Anambra State, as he led members of his campaign team on a roadshow and town hall meeting in the commercial city. Obi began his visit with a stop […]