NAIBU Rais Profesa Kithure Kindiki huenda asiwe mgombea mwenza wa Rais William Ruto katika uchaguzi mkuu wa 2027, Mbunge wa Ndia George Kariuki amedai.
Bw Kariuki, ambaye ni mshirika wa karibu wa Rais Ruto, alisema Profesa Kindiki kwa sasa anashikilia wadhifa huo lakini anaweza kubadilishwa kabla ya uchaguzi.
Akizungumza na redio ya Kameme, mbunge huyo alipinga madai kwamba Chama cha ODM ndicho kitatoa mgombea mwenza wa Rais Ruto. Alisema nafasi hiyo bado itaenda kwa mtu kutoka eneo la Mlima Kenya, ingawa huenda asiwe Profesa Kindiki.
“ODM haitahitajika kutoa mgombea mwenza. Suala hilo litajadiliwa ili kubaini anayefaa zaidi kutoka eneo hili lenye kura nyingi,” akasema.
Bw Kariuki pia alisisitiza umuhimu wa wakazi wa Mlima Kenya kubaki na umoja na kukataa mipango ya kugawanya kura za eneo hilo.
Majuzi, Bw Kariuki alimvamia Profesa Kindiki akisema ameshindwa kuwatetea wakazi wa Mlima Kenya. Pia aliwakosoa Profesa Kindiki na kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua kwa kushambuliana kisiasa na kugawanya eneo hilo.
Dai huenda Ruto akamtema Kindiki kabla ya 2027

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsAfenifere demands prosecution of sponsors of campaign violence
…Raises alarm over rising attacks ahead of 2027 elections By Adeola Badru The pan-Yoruba socio-political organisation, Afenifere, has raised the alarm over increasing political violence ahead of the 2027 general elections, calling for the arrest and prosecution of perpetrators and their sponsors. The organisation warned that the growing incidents of thuggery, intimidation and inflammatory political […]
NewsPHOTOS: First Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsFirst Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsObi woos Onitsha voters, promises jobs, better services
…Says Nigeria needs energetic president By Vincent Ujumadu The presidential candidate of the Nigeria Democratic Congress (NDC), Peter Obi, on Friday drew a large crowd in Onitsha, Anambra State, as he led members of his campaign team on a roadshow and town hall meeting in the commercial city. Obi began his visit with a stop […]