HUZUNI imetanda Kiambaa, katika kijiji cha Moto, Molo, Kaunti ya Nakuru, baada ya mwanafunzi wa Kidato cha Nne kupatikana ameuawa kikatili nyumbani kwao.
Joy Wangui, 18, mwanafunzi wa Shule ya Upili ya Molo, alipatikana Jumapili akiwa amelala na kulowa damu kwenye jikoni, huku kichwa chake kilichokatwa kikapatikana karibu na bafu.
Polisi wameanzisha msako wa mshukiwa anayefahamika kwa familia na wakazi wa eneo hilo, ambaye alitoroka baada ya mauaji.
Kamanda wa Polisi wa Molo Justus Katana alisema polisi walipokea taarifa kutoka kwa wananchi mwendo wa saa nane Jumapili kuhusu mauaji hayo.
Jirani Paul Muraguri Mwangi alisema tukio hilo limewaacha wakazi wakiwa na hofu. Alisema shoka, panga na kisu, zote zilipatikana katika eneo la tukio na huenda zilitumika katika mauaji.
Jirani mwengine, Charles Njenga Matendo, alisema kaka mdogo wa Wangui ndiye aliyegundua mwili wake baada ya kurejea kutoka kwa duka la familia lililokuwa karibu.
Wakazi wanahofia kuwa mauaji hayo huenda yalihusiana na mzozo wa kimapenzi, ingawa polisi bado hawajathibitisha nia ya mshukiwa.
Maafisa wa Idara ya Upelelezi Nchini (DCI) waliendesha uchunguzi wa kitaalamu katika eneo la tukio huku damu ikiwa bado imeonekana jikoni.
Askofu Joram Nderu alimtaja Bi Wangui kama msichana mnyenyekevu, mwenye heshima na furaha aliyekuwa na matarajio mengi mema maishani.
Huzuni na hasira mwanafunzi wa kidato cha nne akiuawa kwa kukatwa kichwa

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsAfenifere demands prosecution of sponsors of campaign violence
…Raises alarm over rising attacks ahead of 2027 elections By Adeola Badru The pan-Yoruba socio-political organisation, Afenifere, has raised the alarm over increasing political violence ahead of the 2027 general elections, calling for the arrest and prosecution of perpetrators and their sponsors. The organisation warned that the growing incidents of thuggery, intimidation and inflammatory political […]
NewsPHOTOS: First Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsFirst Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsObi woos Onitsha voters, promises jobs, better services
…Says Nigeria needs energetic president By Vincent Ujumadu The presidential candidate of the Nigeria Democratic Congress (NDC), Peter Obi, on Friday drew a large crowd in Onitsha, Anambra State, as he led members of his campaign team on a roadshow and town hall meeting in the commercial city. Obi began his visit with a stop […]