WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Ashatu Kijaji, amefanya ukaguzi wa ukarabati mkubwa unaoendelea katika Hoteli ya Mikumi ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, hatua inayolenga kuongeza viwango vya huduma za utalii na ushindani wa hifadhi katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
Hoteli hiyo, inayomilikiwa na mwekezaji Gullam Abbasi, inafanyiwa ukarabati wa kisasa unaojumuisha uboreshaji wa vyumba, maeneo ya burudani, huduma za kimataifa, na sehemu maalum kwa watoto.Dk. Kijaji amesema uwekezaji huu ni mfano wa ushirikiano wa Serikali na sekta binafsi unaosaidia kukuza utalii, kuongeza ajira na mapato ya hifadhi.
Wizara ya Maliasili na Utalii inaendelea kushirikiana na wawekezaji binafsi kuongeza uwezo wa malazi ndani ya hifadhi zake, hatua inayotarajiwa kuongeza idadi ya watalii, muda wa kukaa hifadhini, na mapato ya uhifadhi. Hoteli ya Mikumi inatarajiwa kuwa ya kwanza ndani ya hifadhi kutoa huduma za kiwango cha kimataifa, ikiwa na vyumba 46, bwawa la kuogelea, ukumbi wa mazoezi, sauna na maeneo ya burudani kwa watoto. SOMA: Waziri Kijaji aitaka Tanapa kuongeza ubunifuThe post Dk. Kijaji aagiza ukarabati wa Hoteli Mikumi first appeared on HabariLeo.
Dk. Kijaji aagiza ukarabati wa Hoteli Mikumi

This story was originally published by Habari Leo.
Read the full story at Habari LeoRelated stories
TravelMiss World Kufungua Milango ya Utalii
ZANZIBAR imeendelea kujitokeza kama moja ya vivutio muhimu vya utalii nchini, safari hii ikipokea ugeni wa Miss World 2026, Joheirry Molla aliyewasili visiwani humo Novemba 19, 2026, akiwa ameambatana na warembo kutoka mabara sita.
TravelAskari Tanapa, TFS mbaroni mauaji ya wabeba mkaa
KAGERA; Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera linawashikilia askari 13, wakiwemo wa wanyamapori wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), askari wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na askari mgambo, kwa tuhuma za mauaji ya watu wanne yaliyotokea Kijiji cha Kanyamika, Kata ya Karambi, Tarafa ya Kimwani, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera. Taarifa…
TravelNgorongoro scoops continental gong
ACCRA: THE Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA) has won the Excellence in Sustainable Tourism and Conservation Management Award at the Africa Business Forum & Awards 2026. The award recognises Ngorongoro’s contribution to biodiversity conservation, sustainable tourism development and the protection of its outstanding natural and cultural heritage. The awards ceremony was held in Accra, Ghana,…
TravelDk Kijaji: Mashindano makubwa gofu Afrika kufanyika Serengeti
MARA; Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Ashatu Kijaji, amesema Uwanja wa Gofu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti utawezesha Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano makubwa ya gofu ya Afrika na kimataifa, hatua inayotarajiwa kuongeza idadi ya watalii, mapato na kuitangaza nchi kupitia utalii wa michezo. Akizungumza leo Oktoba 18, 2026, wakati wa uzinduzi wa…