MNAMO Aprili 2023, Bi Bishara Abdinoor aliingiwa na hofu alipomwona mwanae wa kiume amerejea nyumbani akimbeba mtoto wa duma.
Tineja huyo alikuwa ameshinda mchana kutwa akilisha ng’ombe katika kijiji chao cha Kursi kinachopakana na Hifadhi ya Wanyamapori ya Sabuli, alipompata mnyama huyo mdogo akiwa ametelekezwa na mamake.
Mama Abdinoor hakuwa na ufahamu kuwa ni hatia kuwa na mnyama wa porini bila leseni kutoka kwa Shirika la Wanyamapori Nchini (KWS) na hatari ambayo mwanawe aliwaletea kwa kumleta nyumbani mtoto wa duma.
“Nilitaka kumtupa mtoto huyo wa duma kwa hofu kwamba mamake angefuatilia harufu yake na aje kumchukua. Lakini mwanangu aliniomba nimruhusu amlishe kabla ya kumruhusu arejee mwituni,” akaelezea kwenye mawasiliano ya simu na Taifa Leo Dijitali.
Mahojiano hayo yalikuwa yamepangwa na Naibu Mkurugenzi anayesimamia eneo la Uhifadhi la Kaskazini Bakari Chongwa, ambapo Bi Abdinoor aliongea kupitia mkalimani.
“Mwanangu alimlisha mtoto huyo wa duma kwa chakula ambacho tuliandaa jioni hiyo; mchele kwa kitoweo cha nyama. Aidha, alimtengenezea kizimba cha kulala,” akaeleza.
Lakini familia ya Bi Abdinoor iliogopa kuwa duma huyo akiwa mkubwa angeanza kula mifugo wao, haswa mbuzi, kando na kuwashambulia watu.
Na hata baada ya kumrejesha msituni, alirejea nyumbani kwa Bi Abdinoort kila wakati, kwani alionekana kupenda chakula kilichopikwa.
“Baada ya miezi kadhaa tuliingiliana na mnyama huyo wa mwituni, alipenda watu na angetambua kila mtu katika familia yetu. Sasa tulianza kumfunga chini ya kivuli cha mti huku tukimlisha kwa hofu kwamba angewashambulia watu,” akasema.
Siku moja Afisa wa KWS anayesimamia Kaunti ya Wajir Rashid Jumale alialikwa katika redio moja inayopeperusha matangazo kwa lugha yamama, ambapo alihimiza wanajamii kuripoti visa vya wanyamapori kuingia katika makazi ya watu na hapo ndio familia iliwasiliana na KWS.
Baada ya kusikiza ushauri huo, Bw Abdinoor alituma ujumbe kwa KWS kwamba wanafuga duma ambaye walimwokoa kutoka msitu.
Bw Chongwa alimshukuru mwanamke huyo kwa kutumza mwana duma huyo sawa na mbwa au paka wake.Maafisa KWS walimchukua mnyama huyo na kumsafirisha hadi hifadhi ya Nairobi Safari Walk, ambako anatunzwa.
Familia yaishi na duma iliyemuokoa kutoka msituni
MNAMO Aprili 2023, Bi Bishara Abdinoor aliingiwa na hofu alipomwona mwanae wa kiume amerejea nyumbani akimbeba mtoto wa duma. Tineja huyo alikuwa ameshinda mchana kutwa akilisha ng’ombe katika kijiji chao cha Kursi kinachopakana na Hifadhi ya Wanyamapori ya Sabuli, alipompata mnyama huyo mdogo akiwa ametelekezwa na mamake. Mama Abdinoor hakuwa na ufahamu kuwa ni hatia kuwa na mnyama wa porini bila leseni kutoka kwa Shirika la Wanyamapori Nchini (KWS) na hatari ambayo mwanawe aliwaletea kwa kumleta nyumbani mtoto wa duma. “Nilitaka kumtupa mtoto huyo wa duma kwa hofu kwamba mamake angefuatilia harufu yake na aje kumchukua. Lakini mwanangu aliniomba nimruhusu amlishe kabla ya kumruhusu arejee mwituni,” akaelezea kwenye mawasiliano ya simu na Taifa Leo Dijitali. Mahojiano hayo yalikuwa yamepangwa na Naibu Mkurugenzi anayesimamia eneo la Uhifadhi la Kaskazini Bakari Chongwa, ambapo Bi Abdinoor aliongea kupitia mkalimani. “Mwanangu alimlisha mtoto huyo wa duma kwa chakula ambacho tuliandaa jioni hiyo; mchele kwa kitoweo cha nyama. Aidha, alimtengenezea kizimba cha kulala,” akaeleza. Lakini familia ya Bi Abdinoor iliogopa kuwa duma huyo akiwa mkubwa angeanza kula mifugo wao, haswa mbuzi, kando na kuwashambulia watu. Na hata baada ya kumrejesha msituni, alirejea nyumbani kwa Bi Abdinoort kila wakati, kwani alionekana kupenda chakula kilichopikwa. “Baada ya miezi kadhaa tuliingiliana na mnyama huyo wa mwituni, alipenda watu na angetambua kila mtu katika familia yetu. Sasa tulianza kumfunga chini ya kivuli cha mti huku tukimlisha kwa hofu kwamba angewashambulia watu,” akasema. Siku moja Afisa wa KWS anayesimamia Kaunti ya Wajir Rashid Jumale alialikwa katika redio moja inayopeperusha matangazo kwa lugha yamama, ambapo alihimiza wanajamii kuripoti visa vya wanyamapori kuingia katika makazi ya watu na hapo ndio familia iliwasiliana na KWS. Baada ya kusikiza ushauri huo, Bw Abdinoor alituma ujumbe kwa KWS kwamba wanafuga duma ambaye walimwokoa kutoka msitu. Bw Chongwa alimshukuru mwanamke huyo kwa kutumza mwana duma huyo sawa na mbwa au paka wake.Maafisa KWS walimchukua mnyama huyo na kumsafirisha hadi hifadhi ya Nairobi Safari Walk, ambako anatunzwa.

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
TravelMiss World Kufungua Milango ya Utalii
ZANZIBAR imeendelea kujitokeza kama moja ya vivutio muhimu vya utalii nchini, safari hii ikipokea ugeni wa Miss World 2026, Joheirry Molla aliyewasili visiwani humo Novemba 19, 2026, akiwa ameambatana na warembo kutoka mabara sita.
TravelAskari Tanapa, TFS mbaroni mauaji ya wabeba mkaa
KAGERA; Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera linawashikilia askari 13, wakiwemo wa wanyamapori wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), askari wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na askari mgambo, kwa tuhuma za mauaji ya watu wanne yaliyotokea Kijiji cha Kanyamika, Kata ya Karambi, Tarafa ya Kimwani, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera. Taarifa…
TravelNgorongoro scoops continental gong
ACCRA: THE Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA) has won the Excellence in Sustainable Tourism and Conservation Management Award at the Africa Business Forum & Awards 2026. The award recognises Ngorongoro’s contribution to biodiversity conservation, sustainable tourism development and the protection of its outstanding natural and cultural heritage. The awards ceremony was held in Accra, Ghana,…
TravelDk Kijaji: Mashindano makubwa gofu Afrika kufanyika Serengeti
MARA; Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Ashatu Kijaji, amesema Uwanja wa Gofu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti utawezesha Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano makubwa ya gofu ya Afrika na kimataifa, hatua inayotarajiwa kuongeza idadi ya watalii, mapato na kuitangaza nchi kupitia utalii wa michezo. Akizungumza leo Oktoba 18, 2026, wakati wa uzinduzi wa…