DUKA la jumla la Quickmart Jumanne lilimsimamisha kazi mmoja wa meneja wake na kuomba msamaha kuhusu tukio la mteja aliyekuwa amenunua maziwa kudhulumiwa.
Kupitia taarifa, usimamizi wa supamaketi hiyo ulisema kuwa umemsimamisha kazi meneja wa tawi lake la Buruburu ambaye anatuhumiwa kwa kumpiga mteja, kisa kilichozua ghadhabu za Wakenya. Video iliyosambaa mitandano ilionyesha baadhi ya wateja wakidai kuwa wamewahi kuhangaishwa na meneja huyo.
Kutokana na kusambaa kwa video hiyo, kumekuwa na wito kuwa Wakenya wasusie supamaketi hiyo huku wengine wakitaka waheshimiwe na kusaka uwajibikaji kutoka kwa Quickmart.
“Tunawapa kipaumbele wateja wetu na heshima kwa kila mteja anayeingia mlango wetu. Tunasikitisha kilichofanyika na kumwomba msamaha mteja aliyeathirika pamoja na yeyote ambaye alikerwa na tukio lenyewe,” ikasema taarifa ya Quickmart.
“Punde tu baada ya kufahamishwa kuhusu tukio hilo, tulichukua hatua kwa kumsimamisha mfanyakazi wetu aliyehusika huku tukiendeleza uchunguzi na asasi husika,” ikaongeza taarifa hiyo.
Quickmart ilitoa ufafanuzi zaidi kuwa imemfikia mteja aliyedhulumiwa na kumwomba msamaha kisha kuahidi kushirikiana naye wakati wa uchunguzi. Vilevile ilisema inamakinikia kuwa na mazingira maridhawa ya utendakazi kwa wafanyakazi na wateja wake.
Kwenye video iliyosambaa mitandaoni, mteja huyo alisimulia kuwa pamoja na ndugu yake, walijijazia maziwa baada ya kukosa mhudumu na wakalipa kisha kupewa risiti.
Walipokuwa wakiondoka walikabiliwa kwa nini walijijazia maziwa hayo ambapo vuta ni kuvute ilifuata kisha meneja huyo akachukua risiti yao na kuirarua.
Meneja huyo aliwashangaza zaidi kwa kudai wawili hao walikuwa wameiba lita 57 za maziwa kisha kuwazuiliwa kwenye hifadhi ya supamaketi na kuwapiga.
“Tuliingiwa na wasiwasi na meneja huyo alituzuilia kisha akaanza kutupiga pamoja na ndugu yangu. Tulipomuuliza kwa nini alikuwa akitupiga, alikataa kujibu,” akasema mteja huyo.
Wawili hao kisha walipelekwa Kituo cha polisi cha Buruburu lakini baba yao alikuwa tayari huko na wakawaachiliwa.
Quickmart yaomba msamaha, yachunguza madai ya mteja kudhulumiwa

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
TravelMiss World Kufungua Milango ya Utalii
ZANZIBAR imeendelea kujitokeza kama moja ya vivutio muhimu vya utalii nchini, safari hii ikipokea ugeni wa Miss World 2026, Joheirry Molla aliyewasili visiwani humo Novemba 19, 2026, akiwa ameambatana na warembo kutoka mabara sita.
TravelAskari Tanapa, TFS mbaroni mauaji ya wabeba mkaa
KAGERA; Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera linawashikilia askari 13, wakiwemo wa wanyamapori wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), askari wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na askari mgambo, kwa tuhuma za mauaji ya watu wanne yaliyotokea Kijiji cha Kanyamika, Kata ya Karambi, Tarafa ya Kimwani, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera. Taarifa…
TravelNgorongoro scoops continental gong
ACCRA: THE Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA) has won the Excellence in Sustainable Tourism and Conservation Management Award at the Africa Business Forum & Awards 2026. The award recognises Ngorongoro’s contribution to biodiversity conservation, sustainable tourism development and the protection of its outstanding natural and cultural heritage. The awards ceremony was held in Accra, Ghana,…
TravelDk Kijaji: Mashindano makubwa gofu Afrika kufanyika Serengeti
MARA; Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Ashatu Kijaji, amesema Uwanja wa Gofu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti utawezesha Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano makubwa ya gofu ya Afrika na kimataifa, hatua inayotarajiwa kuongeza idadi ya watalii, mapato na kuitangaza nchi kupitia utalii wa michezo. Akizungumza leo Oktoba 18, 2026, wakati wa uzinduzi wa…