HANGZHOU, China
TUKIO la kushangaza na la aibu lilishuhudiwa katika mji huu baada ya jombi kunaswa kwenye video akining’inia kwenye roshani ya hoteli akiwa amevaa boksa pekee.
Inasemekana mwanaume huyo alikuwa akijaribu kutoroka kupitia dirisha ili asionekane baada ya kudaiwa kufumaniwa akila uroda chumbani na mke wa mtu.
Walioshuhudia walisema mwanaume huyo aliteleza na kujikuta akining’inia juu ya roshani ya hoteli, akishindwa kupanda wala kushuka.
Video za tukio hilo zilisambaa kwa kasi mitandaoni na kusababisha kicheko na kejeli kutoka kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.
Hatimaye, maafisa wa zimamoto waliingilia kati na kumshusha salama.
Polisi walisema hakuna aliyekamatwa, lakini tukio hilo limeacha maswali mengi kuhusu uhusiano wa siri na maamuzi hatari yanayochukuliwa baada ya kufumaniwa katika michepuko.
Kalameni kwenye fumanizi akwama dirishani akitoroka
HANGZHOU, China TUKIO la kushangaza na la aibu lilishuhudiwa katika mji huu baada ya jombi kunaswa kwenye video akining’inia kwenye roshani ya hoteli akiwa amevaa boksa pekee. Inasemekana mwanaume huyo alikuwa akijaribu kutoroka kupitia dirisha ili asionekane baada ya kudaiwa kufumaniwa akila uroda chumbani na mke wa mtu. Walioshuhudia walisema mwanaume huyo aliteleza na kujikuta akining’inia juu ya roshani ya hoteli, akishindwa kupanda wala kushuka. Video za tukio hilo zilisambaa kwa kasi mitandaoni na kusababisha kicheko na kejeli kutoka kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii. Hatimaye, maafisa wa zimamoto waliingilia kati na kumshusha salama. Polisi walisema hakuna aliyekamatwa, lakini tukio hilo limeacha maswali mengi kuhusu uhusiano wa siri na maamuzi hatari yanayochukuliwa baada ya kufumaniwa katika michepuko.

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
TravelMiss World Kufungua Milango ya Utalii
ZANZIBAR imeendelea kujitokeza kama moja ya vivutio muhimu vya utalii nchini, safari hii ikipokea ugeni wa Miss World 2026, Joheirry Molla aliyewasili visiwani humo Novemba 19, 2026, akiwa ameambatana na warembo kutoka mabara sita.
TravelAskari Tanapa, TFS mbaroni mauaji ya wabeba mkaa
KAGERA; Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera linawashikilia askari 13, wakiwemo wa wanyamapori wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), askari wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na askari mgambo, kwa tuhuma za mauaji ya watu wanne yaliyotokea Kijiji cha Kanyamika, Kata ya Karambi, Tarafa ya Kimwani, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera. Taarifa…
TravelNgorongoro scoops continental gong
ACCRA: THE Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA) has won the Excellence in Sustainable Tourism and Conservation Management Award at the Africa Business Forum & Awards 2026. The award recognises Ngorongoro’s contribution to biodiversity conservation, sustainable tourism development and the protection of its outstanding natural and cultural heritage. The awards ceremony was held in Accra, Ghana,…
TravelDk Kijaji: Mashindano makubwa gofu Afrika kufanyika Serengeti
MARA; Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Ashatu Kijaji, amesema Uwanja wa Gofu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti utawezesha Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano makubwa ya gofu ya Afrika na kimataifa, hatua inayotarajiwa kuongeza idadi ya watalii, mapato na kuitangaza nchi kupitia utalii wa michezo. Akizungumza leo Oktoba 18, 2026, wakati wa uzinduzi wa…