UCHUNGUZI kuhusu ajali ya helikopta ya uokoaji iliyotokea katika Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA) umeanza kwa lengo la kubaini chanzo cha ajali hiyo iliyotokea juzi na kusababisha vifo vya watu watano.
Hayo yamesemwa na Mhifadhi Mkuu wa Huduma za Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA), Musa Kuji alipokuwa akiwapa taarifa waandishi wa habari kuhusu tukio hilo mjini Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro.”Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana na maofisa wa mamlaka zinazohusika na usafiri wa angani kwa maana ya TCAA na nyingine zinazohusiana na shughuli hizo wako katika eneo la tukio ili kuendelea na uchunguzi,” alisema.
Kwa mujibu wa Kamishna Kuji, ajali hiyo ilitokea katika eneo la kambi ya barafu lenye urefu wa meta 4,673 kutoka usawa wa bahari ambalo ni sehemu ya Mlima Kilimanjaro. “Ajali hii ilihusisha helikopta ya uokoaji kutoka kwa Kampuni ya KiliMedair na kusababisha vifo vya watu watano akiwemo mwanamke mmoja,” alisema.
Amewataja waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni rubani wa helikopta hiyo mkazi wa Kata ya Soweto katika Manispaa ya Moshi, Constantin Mazonde (42). “Wengine ni Davis Plos (30) mtalii kutoka Jamhuri ya Czech, Anna Plosova (30) mtalii kutoka Jamhuri ya Czech, Jimmy Daniel (32) daktari kutoka kampuni ya uokoaji ya KiliMedair mkazi wa Kata ya Rau, Manispaa ya Moshi na Innocent Mmbaga mwongoza watalii mkazi wa Jiji la Moshi,” alisema.
Kuji amesema kuwa mawasiliano kati ya mamlaka husika nchini na ubalozi wa Czech nchini tayari yameanza ili utambuzi wa ziada wa wageni waliofariki uweze kukamilika na kukamilisha taratibu nyingine zinazohusiana na msiba wa watu hao ambao waliingia nchini kama watalii. SOMA: ‘Ningekuwepo kwenye ajali iliyomuua Sokoine’The post Uchunguzi waanza helikopta iliyoua watano Kilimanjaro first appeared on HabariLeo.
Uchunguzi waanza helikopta iliyoua watano Kilimanjaro

This story was originally published by Habari Leo.
Read the full story at Habari LeoRelated stories
TravelMiss World Kufungua Milango ya Utalii
ZANZIBAR imeendelea kujitokeza kama moja ya vivutio muhimu vya utalii nchini, safari hii ikipokea ugeni wa Miss World 2026, Joheirry Molla aliyewasili visiwani humo Novemba 19, 2026, akiwa ameambatana na warembo kutoka mabara sita.
TravelAskari Tanapa, TFS mbaroni mauaji ya wabeba mkaa
KAGERA; Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera linawashikilia askari 13, wakiwemo wa wanyamapori wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), askari wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na askari mgambo, kwa tuhuma za mauaji ya watu wanne yaliyotokea Kijiji cha Kanyamika, Kata ya Karambi, Tarafa ya Kimwani, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera. Taarifa…
TravelNgorongoro scoops continental gong
ACCRA: THE Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA) has won the Excellence in Sustainable Tourism and Conservation Management Award at the Africa Business Forum & Awards 2026. The award recognises Ngorongoro’s contribution to biodiversity conservation, sustainable tourism development and the protection of its outstanding natural and cultural heritage. The awards ceremony was held in Accra, Ghana,…
TravelDk Kijaji: Mashindano makubwa gofu Afrika kufanyika Serengeti
MARA; Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Ashatu Kijaji, amesema Uwanja wa Gofu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti utawezesha Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano makubwa ya gofu ya Afrika na kimataifa, hatua inayotarajiwa kuongeza idadi ya watalii, mapato na kuitangaza nchi kupitia utalii wa michezo. Akizungumza leo Oktoba 18, 2026, wakati wa uzinduzi wa…