
Category
Top headlines and developing stories from Tanzania, Kenya, Uganda and the wider region, gathered from the leading local and international newsrooms and updated throughout the day.


RIPOTI mpya ya Mdhibiti wa Bajeti imeibua wasiwasi kuhusu ongezeko la madeni katika serikali za kaunti, huku magavana wanane wa muhula wao wa kwanza wakishindwa kulipa yale ya zamani ya thamani ya zaidi ya Sh70.2 bilioni waliyorithi kutoka kwa waliowatangulia. Ripoti ya Mdhibiti wa Bajeti Margaret Nyakang’o inaonyesha kuwa madeni hayo, yanayohusu wafanyakazi, wakandarasi na wasambazaji wa bidhaa, hayajalipwa kwa zaidi ya miaka mitatu licha ya serikali za kaunti kuendelea kutumia fedha nyingi kwa mishahara na matumizi ya kawaida. Kaunti zilizoathirika zaidi ni Mombasa, Wajir, Nairobi, Kiambu, Embu, Machakos, Garissa na Taita Taveta, ambapo zaidi ya nusu ya madeni yao hayajalipwa kwa zaidi ya miaka mitatu. Kaunti ya Nairobi chini ya Gavana Johnson Sakaja inaongoza kwa deni la kihistoria la Sh49 bilioni, ikifuatwa na Kiambu iliyo na Sh3.2 bilioni, Mombasa Sh2.95 bilioni, Wajir Sh1.9 bilioni, Machakos Sh1.39 bilioni, Taita Taveta Sh1.2 bilioni, Embu Sh822.3 milioni na Garissa Sh182.98 milioni. Ripoti hiyo imechapishwa huku uchaguzi mkuu wa 2027 ukikaribia, na inaonyesha kwamba hali ya madeni katika kaunti nyingi imeendelea kuwa mbaya zaidi. Tangu uchaguzi wa 2022, kaunti zimekusanya madeni mapya yanayozidi Sh95.4 bilioni. Kaunti ya Mandera ndiyo iliyoongoza kwa madeni mapya ya Sh2.2 bilioni katika mwaka mmoja wa kifedha, ikifuatiwa na Machakos, Kilifi, Turkana, Kiambu na Meru. Kwa ujumla, serikali za kaunti zilikuwa na madeni ambayo hayajalipwa ya jumla ya Sh172.5 bilioni kufikia Juni 30, 2026. Zaidi ya nusu ya kiasi hicho kinatokana na Kaunti ya Nairobi pekee, ambayo ina madeni ya Sh86.9 bilioni. Ripoti pia imeonyesha kuwa kaunti zilitumia Sh369.9 bilioni kwa mishahara na matumizi ya kawaida katika mwaka wa fedha uliomalizika Juni 2026, huku zikielekeza Sh126.7 bilioni pekee kwa miradi ya maendeleo. Hali hiyo imesababisha baadhi ya kaunti kushindwa kutekeleza miradi muhimu. Jumla ya miradi 128 ya thamani ya Sh6.3 bilioni imekwama nchini. Nairobi inaongoza kwa miradi 57 iliyokwama ya thamani ya Sh2.24 bilioni, ikifuatiwa na Isiolo. Aidha, madeni ya mishahara na makato ya kisheria ambayo hayajawasilishwa yanakadiriwa kufikia Sh100.2 bilioni, huku zaidi ya Sh52 bilioni ya kiasi hicho ikiwa imekwama kwa zaidi ya miaka mitatu. Hali hiyo imezua hofu kuwa baadhi ya wafanyakazi wanaweza kuathiriwa wanapostaafu kwa sababu fedha zao za pensheni hazijawasilishwa inavyotakiwa. Dkt Nyakang’o ametaka serikali za kaunti kuweka kipaumbele katika kulipa madeni yaliyopo na kuongeza matumizi kwa miradi ya maendeleo badala ya kuelekeza sehemu kubwa ya mapato kwa mishahara na matumizi ya kawaida.

MOROGORO: MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Morogoro, Sheila Lukuba, amewasihi wanawake kuwa mstari wa mbele katika malezi ya watoto kwa kuwajenga katika misingi ya uzalendo ili watambue kuwa hawana nchi nyingine isipokuwa Tanzania. Lukuba ameyasema hayo katika sherehe za Siku ya Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA) zilizofanyika katika Parokia ya Mt. Fransisco wa Sales, Kata…

President Ruto issued a heartfelt statement paying tribute to his "dear friend" Chivayo, praising his energy, warmth, and conviction in Africa's potential.

KUKOSEKANA kwa Gavana wa Siaya James Orengo katika mikutano kadhaa muhimu ya viongozi wa upinzani katika siku za hivi majuzi kumezua mjadala mkubwa kuhusu hatua yake ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Kwa mwanasiasa ambaye amekuwa nguzo muhimu katika siasa za upinzani kwa miongo kadhaa, kila hatua yake au hata kutokuwepo kwake katika hafla muhimu huibua maswali mengi. Hali hiyo imefanya wengi kujiuliza iwapo Orengo anajiandaa kujiunga na muungano mpya wa kisiasa au anapanga kuanzisha mkondo wake mwenyewe. Baada ya kuwa kimya kwa muda, Orengo alijitokeza Septemba 21 wakati wa uzinduzi wa muungano mpya wa The Ukombozi Alliance, uliobadilishwa jina kutoka Azimio la Umoja One Kenya Coalition Party. Watazamaji wa kisiasa walitafsiri hatua hiyo kama ishara kwamba huenda alikuwa akijipanga kupata nafasi mpya katika upinzani. Hata hivyo, siku chache baadaye alikosekana katika kikao muhimu cha viongozi wa vuguvugu la Linda Mwananchi ambapo Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna aliidhinishwa kuwa mgombea wa urais wa muungano huo katika uchaguzi wa 2027. Kutokuwepo kwake kulionekana kuwa na uzito mkubwa kwa sababu hapo awali jina lake lilikuwa likitajwa miongoni mwa wale waliokuwa wakitazamwa kama viongozi wanaoweza kuwania nafasi ya juu katika muungano huo. Orengo pia hakuhudhuria mkutano wa kisiasa uliofanyika Narok licha ya jina lake kuwekwa kwenye mabango ya viongozi walioalikwa. Viongozi waliokuwepo ni pamoja na kiongozi wa muda wa Jubilee Fred Matiang’i na kiongozi wa People's Party of Kenya Ndindi Nyoro. Katika mahojiano maalum, Orengo aliwataka wafuasi wake kuwa watulivu huku akisema bado anaunga mkono umoja wa upinzani katika mapambano ya kuleta mabadiliko nchini. “Ninaunga mkono mapambano ya mageuzi yanayohitaji umoja na hatua za kisiasa. Wafuasi wangu wawe watulivu. Nitafafanua hatua yangu inayofuata kwa wakati unaofaa,” alisema. Ingawa hakufichua mipango yake, taarifa zinaonyesha kuwa Orengo anafikiria kufufua chama cha Liberal Democratic Party (LDP), ambacho zamani kilihusishwa na Raila Odinga na marehemu Dennis Kodhe. Kidokezo kubwa zaidi kilitolewa Jumatano alipoweka ujumbe kwenye mitandao ya kijamii akisema, “Maadhimisho ya Baba yanakaribia, jiandaeni,” akiambatisha picha ya kofia yenye rangi rasmi za LDP, yaani kijani, bluu na nyeupe. Wadadisi wa siasa wanaamini kuwa hatua hiyo huenda ikawa njia ya Orengo kujijengea nafasi mpya ya kujadiliana na makundi mbalimbali ya upinzani, yakiwemo Ukombozi Alliance na Linda Mwananchi. Chanzo cha karibu naye kinasema Orengo anaamini eneo la Nyanza linafaa kuwa na sauti yenye uzito zaidi katika siasa za upinzani. Wafuasi wake wanahisi baadhi ya viongozi ndani ya Linda Mwananchi wanajaribu kupunguza ushawishi wake. Hata hivyo, Seneta wa Kakamega Boni Khalwale amepuuzilia mbali madai ya mzozo mkubwa ndani ya vuguvugu hilo. Amesema tofauti za maoni kati ya Orengo, Sifuna na mbunge Babu Owino ni jambo la kawaida katika mfumo wa vyama vingi. Kwa sasa, hatua anayopanga Orengo bado ni siri. Lakini uchaguzi wa 2027 unapokaribia, kila ishara inaonyesha kuwa gavana huyo wa Siaya anajitayarisha kufanya uamuzi muhimu ambao unaweza kubadilisha mwelekeo wa siasa za upinzani nchini.

KENYA imezindua rasmi ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta na bidhaa za petroli cha Dangote East Africa Petroleum Refinery and Petrochemicals SEZ katika Kaunti ya Lamu, mradi unaotarajiwa kugharimu takriban Sh2 trilioni. Shughuli ya uwekaji jiwe la msingi iliongozwa na Rais William Ruto katika Bandari ya Lamu jana na kuhudhuriwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, Rais wa Benin Romuald Wadagni na Rais wa Togo Jean-Lucien Savi de Tové. Mwekezaji mkuu wa mradi huo, bilionea wa Nigeria Aliko Dangote, pia alikuwepo. Rais Ruto alisema mradi huo ni hatua muhimu katika juhudi za Afrika za kujitegemea kiuchumi kwa kusindika rasilimali zake badala ya kuziuza kama malighafi. “Mradi huu ni zaidi ya kiwanda cha kusafisha mafuta. Ni uwekezaji katika usalama wa kawi, ukuaji wa viwanda na ushirikiano wa kikanda. Ni thibitisho kuwa Afrika sasa inaweza kufadhili, kujenga na kuongeza thamani ya bidhaa zake hapa nyumbani,” alisema Rais Ruto. Aliongeza kuwa kwa muda mrefu Afrika imekuwa ikitoa malighafi huku mataifa mengine yakinufaika kwa kuzisindika, kuzitengeneza na kupata ajira pamoja na mapato yanayotokana nazo. Kwa mujibu wa Rais, Kenya ilitumia zaidi ya Sh530 bilioni mwaka uliopita kuagiza bidhaa za mafuta kutoka nje, hali inayoonyesha umuhimu wa kuwa na uwezo wa kuzalisha bidhaa hizo ndani ya eneo hili. “Lazima tuzalishe zaidi ya tunachotumia. Lazima tuongeze thamani ya bidhaa tunazozalisha na kupunguza kutegemea bidhaa zinazoagizwa kutoka nje,” alisema. Rais Museveni aliunga mkono maono hayo akisema viwanda vitasaidia kufungua fursa mpya za kiuchumi katika eneo la Afrika Mashariki. Alitumia mfano wa msimamo wa Uganda wa kutotuma madini ya chuma kusindikwa nje ya nchi ili kusisitiza umuhimu wa kuongeza thamani ya rasilimali ndani ya nchi husika. Kiongozi huyo pia alitoa wito wa kuharakishwa kwa muungano wa Afrika Mashariki ili kurahisisha biashara, uwekezaji na uhamaji wa wafanyakazi katika ukanda huu. “Tunapaswa kuwa na Shirikisho la Afrika Mashariki ambapo wananchi wanaweza kuvuka mipaka kwa urahisi na kufanya kazi popote katika eneo hili,” alisema. Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alisema hatua ya Afrika kutegema pakubwa masoko ya nje umefanya bara hili kukumbwa na misukosuko ya bei na changamoto za ugavi wa bidhaa muhimu. Alisema kiwanda cha Lamu kitasaidia kuleta huduma za usindikaji wa mafuta karibu na soko la Afrika Mashariki na kupunguza gharama ya kupata bidhaa za petroli. “Kadri viwanda na idadi ya watu vinavyoongezeka, mahitaji ya mafuta nayo yanaongezeka. Mradi huu utakuwa na mchango mkubwa katika sehemu hii ya bara,” alisema. Bilionea Aliko Dangote alisema mradi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 40 ijayo na utakuwa mfano wa kile ambacho Waafrika wanaweza kufanikisha wanaposhirikiana. Alisema Afrika imebarikiwa kwa rasilimali nyingi lakini inaendelea kupoteza mapato kwa kuuza malighafi na kuagiza bidhaa zilizotengenezwa. “Lazima Afrika ijitosheleze. Hatupaswi kutegemea nchi nyingine kwa bidhaa muhimu. Asilimia 94 ya dawa tunazotumia zinaagizwa kutoka nje. Tunahitaji kujenga viwanda vyetu na kuimarisha uzalishaji wa ndani,” alisema. Dangote aliongeza kuwa kundi lake linapanga kuwekeza zaidi katika sekta mbalimbali za Afrika ifikapo mwaka 2030, zikiwemo madini, viwanda, bandari na kawi. Mradi wa Lamu unatarajiwa kuwa msingi wa maendeleo ya mji mkubwa wa viwanda unaozunguka bandari hiyo. Pia utaongeza mahitaji ya huduma za usafirishaji, uhandisi, ujenzi, makazi na kawi huku ukifungua maelfu ya nafasi za kazi. Viongozi waliohudhuria hafla hiyo walisisitiza kuwa maendeleo ya Afrika yatapatikana kupitia ongezeko la viwanda, usindikaji wa rasilimali ndani ya bara na ushirikiano wa kikanda unaolenga kuboresha maisha ya wananchi na kukuza uchumi wa mataifa ya Afrika.

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limepata nafasi ya pili kati ya Mashirika ya Umma ya Huduma na Biashara 306, kwa utendaji bora katika usimamizi wa fedha (Best Financial Management Performance – Commercial Entities). Tuzo hiyo imekabidhiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, Septemba 30, 2026, jijini Arusha, katika kikao…

CHAMA cha Orange Democratic Movement (ODM) kesho kitazindua rasmi shughuli za mwezi mzima za kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha mwanzilishi wake, Raila Amolo Odinga, kupitia hafla ya kuwasha mishumaa kote nchini. Hafla hiyo itaanza saa kumi na mbili jioni huku Wakenya wakihimizwa kuwasha mishumaa popote walipo kwa heshima ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya. Mwenyekiti wa Kitaifa wa ODM, Gladys Wanga, alisema hafla kuu jijini Nairobi itafanyika katika Bustani ya Uhuru kuanzia saa tisa alasiri. Maeneo mengine yatakayoshuhudia shughuli hizo ni Treasury Square mjini Mombasa, Kisumu Central Square na makao makuu ya Kaunti ya Kajiado. Shughuli hizo zinaashiria mwanzo wa kile ODM imeita “Mwezi wa Baba”, mwezi maalum wa kukumbuka maisha, uongozi na mchango wa Raila katika siasa za Kenya. ODM inasema maadhimisho hayo yanalenga kuwapa Wakenya nafasi ya kutafakari maisha ya Raila aliyefariki nchini India Oktoba 15, 2025 akiwa na umri wa miaka 80. Baada ya hafla ya mishumaa, shughuli hizo zitaendelea katika maeneo mbalimbali nchini. Mnamo Oktoba 9 kutakuwa na mkutano mkubwa wa kumbukumbu Kakamega huku shughuli za kifamilia zikifanyika kati ya Oktoba 10 na 15 kabla ya ibada kuu ya kumbukumbu katika Kang’o Ka Jaramogi, Bondo, siku ya Oktoba 15. Shughuli hizo pia zitafanyika Garissa, Pwani, Kajiado na Turkana kabla ya kuhitimishwa kwa mkutano mkubwa wa kumbukumbu jijini Nairobi Oktoba 31. ODM imesema maadhimisho hayo hayalengi tu kuomboleza kiongozi huyo wa zamani bali pia kukumbuka maadili aliyosimamia. Katika maisha yake ya kisiasa, Raila alijulikana kwa kupigania katiba mpya, demokrasia ya vyama vingi, ugatuzi na ushiriki mpana wa wananchi katika masuala ya utawala. Chama hicho kimewahimiza wafuasi wake kutumia mwezi huo kujitolea upya katika misingi na maono aliyoyaacha Raila huku kikitafakari mustakabali wake wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027.

KAUNTI ya Lamu ilikuwa katika ulinzi mkali wa kijeshi jana wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote East Africa Petroleum Refinery kinachotarajiwa kugharimu Sh2 trilioni. Kuanzia Jeti Kuu ya Mokowe, ambayo ndiyo lango kuu la kuingia Kisiwa cha Lamu, hadi eneo la Kililana katika Bandari ya Lamu ambako hafla hiyo ilifanyika, kulikuwa na uwepo mkubwa wa maafisa wa usalama kutoka vikosi mbalimbali. Hatua hizo za usalama zilianza kuonekana Jumanne wakati maandalizi ya mwisho ya hafla hiyo yalipokuwa yakiendelea. Maeneo ya Mokowe, Hindi, Mpeketoni, Kisiwa cha Lamu na Bandari ya Lamu yalishuhudia msururu wa maafisa wa usalama waliokuwa wakiratibu operesheni maalum kwa ajili ya kuwapokea viongozi wa mataifa mbalimbali. Rais William Ruto alikuwa mwenyeji wa hafla hiyo iliyohudhuriwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, viongozi wengine wa Afrika pamoja na bilionea wa Nigeria Aliko Dangote ambaye ndiye mwekezaji mkuu wa mradi huo. Jana asubuhi, anga ya Kisiwa cha Manda na maeneo ya mradi wa Lapsset ilikuwa na shughuli nyingi za ndege za kijeshi na polisi zilizokuwa zikifanya doria za mara kwa mara. Helikopta hizo zilikuwa zikihakikisha usalama wa viongozi waliokuwa wakiwasili kupitia Uwanja wa Ndege wa Manda Bay na Uwanja wa Ndege wa Manda. Baharini pia hali ilikuwa tofauti. Maji ya Bahari Hindi kuanzia Mji wa Lamu hadi Kililana yalikuwa chini ya ulinzi mkali. Meli za Jeshi la Wanamaji la Kenya pamoja na boti za kasi za usalama zilifanya doria mfululizo kuzuia vyombo vya majini visivyoidhinishwa kusogea karibu na eneo la hafla. Meli kubwa ya kijeshi pia ilionekana ikiwa imetia nanga baharini. Nchini kavu, maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF), polisi wa kukabiliana na fujo (GSU) na mashirika mengine ya usalama waliweka vizuizi vya ukaguzi katika barabara kuu zinazoelekea bandari ya Lamu. Katika lango kuu la kuingia bandarini, wageni wote walilazimika kuthibitisha vitambulisho vyao na kukaguliwa kwa kina kabla ya kuruhusiwa kuingia. Licha ya hatua hizo kali za usalama, hali ndani ya eneo la hafla ilikuwa ya shangwe huku viongozi wa jamii, vijana na wageni kutoka ndani na nje ya nchi wakikusanyika kushuhudia uzinduzi wa mradi huo mkubwa. Hali ya usafiri wa anga pia ilikuwa ya kipekee huku helikopta zikifika mfululizo bandarini zikibeba viongozi na wajumbe mbalimbali. Saa sita na dakika ishirini na mbili mchana, Rais Ruto akiwa pamoja na Rais Museveni na Waziri Mkuu Abiy Ahmed walishika koleo na kuchota udongo kuashiria kuanza rasmi kwa ujenzi wa mradi huo. Muda mfupi baadaye, ndege za kijeshi za KDF zilifanya maonyesho maalum angani kuonyesha kuwa eneo hilo lilikuwa salama kwa uwekezaji mkubwa wa kimkakati kama huo. Katika hotuba yake, Bw Dangote alifichua baadhi ya matukio yaliyotokea wakati Rais Ruto na mkewe Rachel Ruto walipotembelea kiwanda chake cha kusafisha mafuta mjini Lagos, Nigeria. Alisema Mama wa Taifa alionyesha hamu kubwa ya kujifunza kuhusu mchakato wa usindikaji wa mafuta kiasi kwamba alionekana kama mwanafunzi wa uhandisi wa kemikali. Dangote pia alimpongeza Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo kwa mchango wake katika miradi yake ya awali ya viwanda nchini Nigeria. Wakati huo huo, wafanyabiashara wa Lamu walinufaika pakubwa kutokana na hafla hiyo. Hoteli nyingi zilijaa wageni huku biashara za mikahawa, vituo vya mafuta, usafiri na huduma nyingine zikirekodi ongezeko kubwa la wateja.

Orodata Science has flagged persistent infrastructure, water supply, staffing and accessibility challenges affecting primary healthcare centres across Nigeria, particularly facilities located in hard to reach communities.

By Henry Umoru ABUJA — Presidential candidate of the Nigeria Democratic Congress, NDC, in the 2027 election, Peter Obi, has raised concerns over the conditions at the Ramin Kura Internally Displaced Persons, IDP, camp in Sokoto State, saying as many as 10 displaced persons are forced to share a room. Obi, a former governor of […]

SENETA wa Nairobi, Edwin Sifuna, amepata ushindi mkubwa kisiasa baada ya Jopo la Kusuluhisha Migogoro ya Vyama vya Kisiasa kubatilisha uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Kisiasa uliozuia kuhifadhiwa kwa jina Linda Mwananchi Movement (LMM). Jopo hilo liliamua kwamba chama cha Liberty National Democratic Alliance (LINDA) hakikuwa kimesajiliwa kikamilifu wala kwa muda, na kwamba kuhifadhi jina lake kulikofanywa Novemba 15, 2024 kuliisha muda wake kisheria baada ya siku 90. Wanachama wa jopo hilo walisema kuwa mara muda wa kuhifadhi unapokwisha bila mwombaji kuendelea na hatua zinazohitajika za usajili, haki ya jina hilo hupotea moja kwa moja na haiwezi kufufuliwa kupitia uamuzi wa kiutawala. Mgogoro huo ulianza baada ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa kukataa ombi la kuhifadhi jina la Linda Mwananchi Movement lililowasilishwa na Mbunge wa Suba Kusini Caroli Omondi, mwanaharakati Pauline Njoroge na rais wa zamani wa Chama cha Wanasheria Kenya (LSK) Faith Odhiambo. Watatu hao wanahusishwa na mrengo unaoungwa mkono na Bw Sifuna. Walipinga uamuzi huo wakisema kuwa jina la Linda Mwananchi Movement ni tofauti kabisa na Liberty National Democratic Alliance na hivyo halikupaswa kuzuiwa. Jopo lililoongozwa na wakili Gad Gathu lilikubaliana nao na kuamuru Msajili wa Vyama vya Kisiasa kufikiria upya ombi hilo ndani ya siku saba. Hata hivyo, uamuzi huo haujasajili chama kipya moja kwa moja bali umerejesha maombi hayo kwa msajili kwa hatua zaidi. Katika uamuzi wake, jopo hilo lilisema sheria hairuhusu kulazimisha waombaji kutaja waasisi wa chama katika hatua ya kuhifadhi jina. Zaidi ya hayo jopo liliondoa stakabadhi zote zilizowasilishwa na LINDA katika kesi hiyo, likisema chama hicho hakikuwa na uwezo wa kisheria kushiriki kwa sababu hakijasajiliwa rasmi. Jopo lilibaini kuwa majina ya Liberty National Democratic Alliance na Linda Mwananchi Movement hayafanani kwa muundo, matamshi wala maana. Lilisema neno “Linda” ni neno la Kiswahili lenye maana yake ya kawaida, ilhali LINDA ni kifupi cha majina ya chama kingine. Majaji waliongeza kuwa Msajili alikuwa ameruhusu vyama vingine kutumia maneno kama “Liberty”, “National”, “Democratic” na “Alliance”, hivyo kukataa jina la Linda Mwananchi kulikuwa kinyume na kanuni za usawa na haki katika utoaji wa huduma za umma. Kutokana na sababu hizo, baraza lilitangaza kuwa uamuzi wa Msajili uliotolewa Agosti 7, 2026 haukuwa halali na kuagiza ombi la Linda Mwananchi Movement lichunguzwe upya kwa mujibu wa sheria. Aidha, jopo lilichunguza suala la uhifadhi wa jina la LINDA na kubaini kuwa chama hicho hakikuwasilisha kwa wakati fomu rasmi ya kuomba usajili wa muda kama inavyotakiwa na sheria. Kulingana na uamuzi huo, jina hilo lilikuwa limehifadhiwa kwa siku 90 pekee kuanzia Novemba 15, 2024. Msajili wa Vyama vya Kisiasa alikiri kuwa hakukuwa na ombi rasmi lililowasilishwa ndani ya muda huo. Hata barua iliyotumwa Februari 4, 2025 haikutosheleza mahitaji ya kisheria. Kwa msingi huo, jopo liliamua kuwa uhifadhi wa jina la LINDA ulikuwa umefutika kisheria na haukuweza kutumiwa kuzuia waombaji wengine kutafuta jina la kisiasa linalofanana kwa neno “Linda”.

He said Tinubu’s absence from August 30 to September 29, amid insecurity and other challenges, raised questions about the President’s leadership and communication with Nigerians.

By Nwabueze Okonkwo ONITSHA — Founder of the Movement for the Actualisation of the Sovereign State of Biafra (MASSOB), Chief Ralph Uwazuruike, has said the concerns raised by the late Biafran leader, Chief Chukwuemeka Odumegwu Ojukwu, about Nigeria remain relevant 66 years after independence. Uwazuruike made the assertion in a statement issued on his behalf […]

MAHAKAMA ya Rongo imehukumu mwanamke mmoja kutoka Kaunti ya Migori kifungo cha miaka 25 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kujaribu kumuua mke mwenza kwa kumwagia asidi usoni katika shambulio lililomuacha na majeraha makubwa ya kudumu. Hakimu Mkuu wa Rongo, Chrisphine Orwo, alimpatia Margaret Atieno Otieno adhabu hiyo baada ya kupata kuwa alimshambulia Alfine Anyango mnamo Novemba 25, 2024, katika eneo la Saria, Kaunti Ndogo ya Awendo. Mahakama iliambiwa kuwa saa moja na nusu jioni siku hiyo, Alfine alikuwa akihudumia wateja katika kibanda chake wakati Margaret, ambaye ni mke mwenza wake, alipowasili. Awali hakukuwa na dalili yoyote ya hatari. Hata hivyo, muda mfupi baadaye Margaret alimmiminia kemikali kali usoni. Ndani ya muda mfupi uso wake ulianza kuvimba huku kemikali hiyo ikiteketeza mgongo na matiti yake. Kutokana na maumivu makali, alianguka chini na kuanza kupiga mayowe kuomba msaada. Binti yake mkubwa, Brenda Atieno Otieno, alieleza kuwa alikuwa akimpelekea mama yake chakula alipokutana na Margaret akitoka dukani akiwa amebeba jagi chini ya mkono. Dakika chache baadaye alisikia mayowe na kukimbilia eneo hilo ambapo alimkuta mama yake akiwa ameungua vibaya usoni. Mfanyakazi mmoja wa familia hiyo, Victor Otieno, naye alishuhudia tukio hilo na kusema Margaret alitorokea msituni baada ya kuona watu wakifika eneo la tukio. Mwathiriwa alipelekwa katika Zahanati ya Dede kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Migori. Baadaye alihamishiwa Hospitali ya Misheni ya Ombo na kisha Hospitali ya Kisii Chiron ambako alifanyiwa upasuaji maalumu wa kurekebisha ngozi. Katika utetezi wake, Margaret alikana mashtaka na kudai kuwa kulikuwa na ugomvi baada ya kutukanwa na mke mwenza wake. Hata hivyo, mahakama ilitupilia mbali maelezo hayo na kuamua kuwa upande wa mashtaka ulithibitisha kesi bila shaka yoyote. Hakimu Orwo alisema majeraha aliyopata Alfine yalikuwa ya kutishia maisha na yalimuacha na ulemavu pamoja na kasoro ya kudumu usoni. Ingawa sheria inaruhusu kifungo cha maisha kwa kosa hilo, hakimu aliamua kumpa Margaret kifungo cha miaka 25 gerezani na siku 14 za kukata rufaa.

By Rotimi Ojomoyela ADO-EKITI — There was drama in the early hours of Wednesday in Ado-Ekiti as staff and students of the Federal University, Oye-Ekiti (FUOYE) mobilised to the residence of the Vice-Chancellor, Prof. Joshua Ogunwole, after policemen reportedly arrived there in an attempt to arrest him. The Vice-Chancellor had raised the alarm after policemen […]

VIONGOZI wanne wa Afrika wameungana na Rais William Ruto na mfanyabiashara Aliko Dangote katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote cha Sh2 trilioni Lamu. Viongozi hao ni Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, Rais Romuald Wadagni wa Benin na Rais Jean-Lucien Savi de Tové wa Togo. Hafla hiyo inaashiria kuanza kwa ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta na bidhaa za petroli pamoja na eneo maalum la kiuchumi la viwanda katika Kaunti ya Lamu. Mradi huo una thamani ya Sh2 trilioni na unatarajiwa kuwa miongoni mwa uwekezaji mkubwa zaidi wa sekta binafsi katika Afrika Mashariki. Mbali na viongozi hao, mataifa mengine ya eneo hili pia yaliwakilishwa katika hafla hiyo, kuonyesha umuhimu wa mradi huo kwa sekta ya nishati na uchumi wa kanda. Kiwanda hicho kinatarajiwa kuongeza uwezo wa Afrika Mashariki katika kusafisha mafuta, kupunguza kutegemea bidhaa za petroli zinazoagizwa kutoka nje na kuchochea shughuli za viwanda. Mradi huo pia unatarajiwa kuimarisha nafasi ya Lamu kama kitovu cha biashara, nishati na usafirishaji katika ukanda wa Afrika Mashariki. Uwepo wa viongozi kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika unaonyesha kuwa mradi huo hauonekani kama uwekezaji wa Kenya pekee, bali una umuhimu kwa soko la kikanda la bidhaa za mafuta na petroli.

SERIKALI za kaunti zimefungua akaunti nyingine 1,411 zamdhibiti katika mwaka uliomalizika Juni 2026, hatua iliyoongeza idadi ya akaunti zinazodaiwa kuendeshwa kinyume cha sheria hadi 6,503. Ripoti mpya ya Mdhibiti wa Bajeti (CoB) inaonyesha idadi hiyo iliongezeka kutoka akaunti 5,092 zilizokuwapo kufikia Juni 2025, licha ya juhudi za serikali za kuimarisha usimamizi wa fedha za umma na kupunguza matumizi ya akaunti zisizoidhinishwa. Ongezeko hilo linajiri huku wizara ya fedha ikiendelea na mpango wa kuhamishia kaunti zote katika mfumo wa Akaunti Moja ya Hazina (Treasury Single Account-TSA), unaolenga kuweka fedha zote za serikali chini ya usimamizi wa pamoja ili kuimarisha uwazi na udhibiti wa matumizi. Kwa miaka kadhaa, taasisi za usimamizi wa fedha zimekuwa zikionya kuhusu ongezeko la akaunti za kibiashara zinazotumiwa na kaunti, zikisema hali hiyo inatoa hatari ya matumizi mabaya ya fedha za umma na kudhoofisha uwajibikaji. Kulingana na Kanuni za Usimamizi wa Fedha za Umma kwa Serikali za Kaunti, akaunti za kaunti zinapaswa kuendeshwa kupitia Benki Kuu ya Kenya (CBK). Akaunti katika benki za kibiashara zinaweza kufunguliwa tu kwa idhini maalum. Isitoshe, nakala za idhini hizo zinapaswa kuwasilishwa kwa Mdhibiti wa Bajeti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ili kuthibitisha uhalali wa akaunti hizo. Mdhibiti wa Bajeti Margaret Nyakang’o amesema kaunti nyingi hazijawasilisha stakabadhi hizo, jambo linalozua mashaka kuhusu uhalali wa maelfu ya akaunti zinazotumika. “Ukosefu wa nakala za barua za idhini kwa ofisi ya Mdhibiti wa Bajeti unapunguza uwezo wa kuthibitisha uhalali, madhumuni na ukamilifu wa akaunti za benki za kibiashara zinazotumiwa na kaunti,” alisema katika ripoti yake. Kaunti ya Pokot Magharibi ndiyo iliongoza kwa kufungua akaunti nyingi zaidi mpya baada ya kuongeza 235. Siaya ilifuata kwa akaunti 217, Nyeri 208, Migori 153 na Kajiado 120. Aidha, baadhi ya kaunti zina jumla kubwa ya akaunti za kibiashara, ikiwemo Kitui iliyo na akaunti 328, Machakos 307 na Bungoma 294. Wizara ya Fedha inaamini mfumo wa TSA utasaidia kuunganisha fedha za serikali mahali pamoja na kurahisisha ufuatiliaji wa mapato, matumizi na salio la fedha za umma. Mpango huo ulianza kutekelezwa Julai 2026 huku kaunti zote 47 zikitarajiwa kuhamia hatua kwa hatua katika mfumo huo mpya. Serikali ina matumaini kuwa mageuzi hayo yatapunguza kugawanya fedha katika akaunti nyingi na kuimarisha usimamizi wa rasilimali za umma. Ripoti hiyo pia inajiri wakati kaunti nyingi zinaendelea kukabiliwa na madeni ambayo hayajalipwa, kuchelewesha malipo kwa wanakandarasi na viwango vya chini vya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Wataalamu wa fedha za umma wanaonya kuwa usimamizi duni wa fedha unaweza kuathiri utoaji wa huduma muhimu kwa wananchi.

MAHAKAMA ya Mazingira na Ardhi imeamuru ardhi yenye thamani ya takriban Sh25 milioni jijini Mombasa ambayo ilitwaliwa kinyume cha sheria na mwanasiasa wa zamani mwaka 1994 irejeshwe kwa umma. Ardhi hiyo inayojulikana kama Machakos Street ilikuwa sehemu ya hifadhi ya barabara ya umma, lakini baadaye ikapewa marehemu Ezekiel Luyali Liyai kujenga nyumba za makazi. Kwa sasa eneo hilo linatumika kama maegesho ya magari. Mahakama ilibaini kuwa taratibu za kisheria zilizohitajika kufuatwa kabla ya kufungwa kwa barabara ya umma hazikuzingatiwa kabla ya ardhi hiyo kutolewa. Jaji alisema hakukuwa na ushahidi wowote wa matangazo rasmi ya serikali kuchapishwa kuarifu umma kuhusu nia ya kufunga barabara hiyo. “Pia hakukuwa na rekodi sahihi za pingamizi zozote kutoka kwa wamiliki wa ploti jirani,” ilisema mahakama. Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) ilieleza mahakama kuwa ardhi hiyo ilikuwa sehemu ya hifadhi ya barabara iliyokuwa chini ya Manispaa ya Mombasa na ilikusudiwa kutumiwa na umma. Kulingana na EACC, ardhi hiyo ilipatiwa marehemu Liyai mwaka 1994 kwa njia isiyo halali kupitia David Kalume Randu na Ahmed Mwidhani, waliokuwa Karani wa Mji na Meya wa manispaa hiyo mtawalia. Tume hiyo ilisema maafisa hao walitumia vibaya mamlaka yao na kukiuka wajibu wao wa kulinda mali ya umma kwa kurahisisha ugavi wa ardhi hiyo kinyume cha sheria. Hata hivyo, Bw Mwidhani alikanusha madai hayo na kusema hakuhusika moja kwa moja katika ugavi wa ardhi. Alidai kuwa jukumu hilo lilikuwa la mhandisi wa manispaa ambaye alikuwa afisa wa kiufundi mwenye mamlaka ya kushauri baraza kuhusu masuala ya ardhi. Mahakama ilisema hakukuwa na ushahidi kwamba ugavi huo uliidhinishwa na baraza la manispaa au wizara husika. Jaji aliamua kuwa ugavi wa ardhi hiyo mwaka 1994 ulikuwa haramu na wa ulaghai na ikaagiza Msajili Mkuu wa Ardhi afute usajili uliotolewa Septemba 1, 1994 na kuzuia familia ya Liyai au maajenti wao kuuza, kuhamisha au kufanya shughuli yoyote kuhusu ardhi hiyo.

KILA asubuhi, Margaret Santa Thoya, 26, hufika katika hifadhi ya maiti ya Hospitali ya Malindi akiwa na mkoba uliojaa vipodozi, brashi za nywele na vifaa vya urembo. Tofauti na wataalamu wengi wa urembo, kazi yake ni kuwapamba maiti ili waonekane nadhifu na wenye hadhi kabla ya kuagwa na familia zao. Margaret hutafuta familia zilizofiwa na kuwapa huduma ya kupamba nywele na uso wa wapendwa wao waliofariki. Kazi hiyo humpa kati ya Sh1,500 na Sh7,000 kwa kila mteja kulingana na huduma inayohitajika. Kwa miaka minne sasa, amekuwa akifanya kazi hiyo ambayo wengi huiona kuwa ya kipekee na ya kutisha. Hata hivyo, anasema changamoto kubwa si maiti bali jinsi jamii inavyomchukulia. “Watu wengi hawataki kuhusishwa nami kwa sababu nashughulika na maiti. Wengine huniita ‘Maggie wa Mochari’ na wanaume wengi huogopa hata kuzungumza nami,” anasema. Margaret anasema taaluma hiyo imeathiri maisha yake ya kijamii na nafasi yake ya kupata mchumba. Watu wengi humtenga kutokana na imani kwamba mtu anayeshughulika na maiti hubeba mkosi au nguvu zisizoeleweka. Baada ya kumaliza darasa la nane mwaka 2016, Margaret alikosa karo ya kuendelea na masomo. Alifanya kazi za mjengo na za nyumbani kabla ya kujiunga na sekta ya urembo kupitia rafiki aliyekuwa na saluni. Baadaye, wenyeji wa kijiji chake walimuomba awasaidie kutengeneza mwili wa mwanamke aliyekuwa amefariki. Alikubali, akaenda katika mochari na kupamba nywele za marehemu huyo. Kazi yake iliwavutia wengi na hapo ndipo safari yake katika taaluma hiyo ilipoanza. Mwanzoni hata familia yake ilipinga kazi hiyo. Mama na dada zake walikuwa wakimtaka kuoga na kubadilisha nguo nje ya nyumba kila alipotoka mortuary. Hata hivyo, baada ya muda walielewa kuwa kazi hiyo ni halali na ndiyo chanzo chake cha mapato. Margaret si peke yake. Samson Karisa, 35, pia huwa anahudumia maiti kwa kuwatengeneza na hata kurekebisha nyuso za waliopata majeraha mabaya katika ajali. Karisa hutumia nta na vifaa maalumu kufunika majeraha ili familia isiogope mwili wa marehemu wakati wa kuuaga. Hutoza kati ya Sh1,000 na Sh5,000 kutegemea ugumu wa kazi. Licha ya kazi hiyo kumsaidia kujikimu, Karisa anasema mama yake, mke wake na watoto wake hawajui anachofanya. Alihamia Malindi kutoka Kilifi ili kuficha taaluma yake kutokana na hofu ya kutengwa na jamii. Mwenyekiti wa Chama cha Ushauri wa Kisaikolojia nchini tawi la Lamu, Andrew Masama, anasema ubaguzi dhidi ya watu wanaoshughulika na maiti unatokana na imani za kitamaduni na hofu ya kifo. Anasema jamii nyingi za Kiafrika huhusisha kifo na mikosi, jambo linalowafanya watu kuogopa wale wanaofanya kazi karibu na marehemu. “Hawa ni wataalamu kama wengine na wanastahili kuheshimiwa kwa huduma wanazotoa kwa familia zilizofiwa,” amesema Masama. Licha ya changamoto hizo, Margaret na Karisa wanasema wataendelea na kazi yao kwa sababu huwa wanasaidia familia kuwaaga wapendwa wao kwa heshima na amani.

MAAFISA wa upelelezi wamepanua msako wa Inspekta Kenneth Kipkemoi Sang hadi Tanzania baada ya juhudi za kumkamata nchini Kenya kugonga mwamba. Inspekta Sang, ambaye ni mkuu wa Kituo cha Polisi cha Nderi katika Kaunti ya Kiambu, amekuwa akitafutwa tangu kuuawa kwa Dkt Victoria Mutiso mjini Nairobi mnamo Julai 29 mwaka huu. Wachunguzi wanaamini ndiye kiungo muhimu kati ya maafisa wa polisi wanaoshukiwa kutekeleza mauaji ya Dkt Mutiso na wakili Kyalo Mbobu pamoja na watu wanaodaiwa kufadhili uhalifu huo. Wiki iliyopita, timu ya maafisa wa polisi ilifika Busia kufuatia taarifa za kijasusi zilizoonyesha kuwa Sang alikuwa amejificha eneo hilo. Hata hivyo, walipofika katika nyumba aliyokuwa akidaiwa kuishi, hawakumpata. Pia hakupatikana katika hoteli moja ambayo taarifa zilionyesha alikuwa akitembelea kupata chakula. Nyumba hiyo ni ya mmoja wa jamaa zake ambaye alihojiwa na baadaye kuachiliwa bila mashtaka. Ingawa Sang alikuwa bado akitumia nambari yake ya simu inayojulikana, wachunguzi wanasema alikuwa akiiwasha kwa muda mfupi ili kuwasiliana na baadhi ya watu wanaochunguzwa kuhusiana na mauaji hayo. Wachunguzi wanasema mshukiwa huyo amekuwa akiwasiliana kwa kiwango kidogo sana na familia na marafiki wa karibu, jambo ambalo limefanya iwe vigumu kufuatilia alipo. Alhamisi iliyopita, polisi waliwakamata maafisa wawili wa polisi na waendeshaji wawili wa bodaboda kuhusiana na mauaji ya wakili Mbobu. Uchunguzi wa simu zao ulionyesha kuwa mmoja wa maafisa hao alikuwa akiwasiliana na Sang mara kwa mara. Matokeo hayo yameimarisha imani ya wachunguzi kuwa Sang huenda alivuka mpaka na kuingia Tanzania baada ya kukwepa operesheni ya polisi karibu na mpaka wa Kenya na Uganda. Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI), Mohammed Amin, amesema Inspekta Sang anahusishwa na mauaji yote mawili. Aidha, uchunguzi umebaini kuwa Konstebo Julius Cheruiyot, anayeshukiwa kumuua wakili Mbobu, alikuwa akifanya kazi chini ya usimamizi wa Sang. Polisi pia walipata bastola aina ya Ceska iliyokuwa imekabidhiwa Cheruiyot siku ambayo wakili huyo aliuawa. Uchunguzi wa kitaalamu wa silaha hiyo ulithibitisha kuwa ndiyo iliyotumika katika mauaji hayo. Wakati huo huo, DCI ilimkamata mshukiwa mwingine, Maritim Kimutai, kuhusiana na mauaji ya Dkt Mutiso. Kimutai atafunguliwa mashtaka pamoja na Rose Mbithe, Angela Mulwa, Chris Mulwa na Konstebo Elijah Kibelion Kimoi. Wote watano walifikishwa katika Mahakama Kuu jana kusomewa mashtaka. Kwa sasa, timu ya maafisa wa DCI na Interpol inaendelea na operesheni nchini Tanzania huku ikisaka aliko Inspekta Sang, ambaye sasa anaonekana kuwa mtu muhimu zaidi katika kufichua mtandao unaodaiwa kuhusika na mauaji hayo mawili yaliyotikisa nchi.

KIONGOZI wa ODM Dkt Oburu Oginga amerejea nchini baada ya kukaa nchini Uingereza kwa takriban wiki tatu akipata matibabu, wakati chama hicho kinajiandaa kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha kakake, Raila Odinga. Dkt Oburu alirejea Ijumaa, Septemba 25, na chama kikathibitisha kurejea kwake siku iliyofuata. Kurejea kwake kunatokea huku ODM ikipanga shughuli za mwezi mzima kumuenzi Raila, aliyeaga dunia Oktoba 15, 2025 nchini India. Mpango huo unaojulikana kama “Mwezi wa Baba” utaanza Oktoba 2 kwa zoezi la kitaifa la kuwasha mishumaa, kabla ya mikutano na shughuli za kumbukumbu katika maeneo mbalimbali. Shughuli hizo zitafikia kilele kwa mkutano mkubwa Nairobi Oktoba 31. Mkutano mkubwa wa kumbukumbu utafanyika Kakamega Oktoba 9, huku familia ya Raila ikiongoza shughuli za Oktoba 10 hadi 15 zitakazofikia kilele katika ibada ya kumbukumbu huko Kang’o Ka Jaramogi, Bondo. Baadaye, ODM imepanga mikutano Garissa Oktoba 17, Pwani Oktoba 18 na 19, Kajiado Oktoba 21 na Turkana kati ya Oktoba 23 na 25, kabla ya hitimisho Nairobi Oktoba 31. Dkt Oburu alipokuwa Uingereza, Mwenyekiti wa ODM Gladys Wanga aliongoza shughuli za chama, zikiwemo za kisiasa Nyanza. Kurejea kwake sasa kunampa nafasi ya kuongoza chama katika kipindi ambacho ODM inakabiliwa na mjadala kuhusu mwelekeo wake baada ya kifo cha Raila. Wakati huo huo, familia ya Raila imeunda kamati yake ya kitaifa inayoongozwa na Prof Adams Oloo kuratibu shughuli za kumbukumbu. Familia imesema maadhimisho hayo ni ya Wakenya wote walioguswa na maisha ya Raila. Mpango wa familia unaingiliana kwa kiasi na ratiba ya ODM, hali ambayo imeibua mjadala kuhusu uratibu wa shughuli hizo. Kurejea kwa Dkt Oburu pia kunatokea wakati ODM ikikabiliwa na tofauti za kisiasa kuhusu uhusiano wake na serikali ya Rais William Ruto na viongozi wanaounga mkono upinzani. Dkt Oburu amekuwa akitetea ushirikiano wa ODM na UDA chini ya serikali jumuishi, huku baadhi ya viongozi wa ODM wakifuata mwelekeo tofauti. Mwezi Agosti, alihusisha ushirikiano wa ODM na UDA na kuendeleza ajenda ya Raila.

JUHUDI za washirika wa Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kupata chama cha United Democratic Party (UDP) kama jukwaa la kuwania urais mwaka 2027 zimepata pigo jipya baada ya viongozi wakuu wa chama hicho kuwasilisha malalamishi rasmi kupinga mabadiliko ya uongozi na mpango wa kukibadilisha rangi. Mvutano huo umeibuka siku chache kabla ya Oktoba 3, tarehe ambayo washirika wa Sifuna wanatarajiwa kutangaza rasmi chama atakachotumia katika safari yake ya kuwania urais. Malalamishi mawili yaliyowasilishwa kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa (ORPP) Septemba 28 sasa yameibua maswali mazito kuhusu uhalali wa hatua zinazolenga kuunda upya chama hicho kufuatia kifo cha mwanzilishi wake na aliyekuwa kiongozi wa chama, Cyrus Jirongo, mnamo Desemba 2025. Katika malalamishi ya kwanza, Makamu Mwenyekiti wa UDP Adow Mohammed Abukar amepinga taarifa za kuteuliwa kwa Mukasa Mwambu Muliro kuwa kiongozi wa muda wa chama. Bw Abukar amesema muundo mpya wa uongozi unaoripotiwa haujatambuliwa na viongozi waliochaguliwa kihalali katika mkutano wa mwisho wa wajumbe wa kitaifa wa chama uliofanyika Februari 24, 2022. Ametaka Msajili wa Vyama vya Kisiasa, John Cox Lorionokou, kubaini ni chombo gani cha chama kilichotoa idhini ya uteuzi huo, kikao hicho kilifanyika lini na wapi, nani walihudhuria na ikiwa kulikuwa na idadi ya wajumbe wa kutosha kufanya maamuzi hayo. Pia anataka msajili athibitishe kuwepo kwa kumbukumbu rasmi na azimio lililoidhinisha mabadiliko hayo ya uongozi. Malalamishi ya pili yaliwasilishwa na mwanachama wa Baraza Kuu la Kitaifa la UDP (NEC), Manasse Kuria Kweya, ambaye pia aliwahi kuwa msaidizi binafsi wa marehemu Jirongo. Katika barua yake, Bw Kweya anahoji hatua zinazochukuliwa kuhusiana na urithi wa uongozi wa chama, nafasi ya viongozi waliopo na mipango ya kubadilisha jina, nembo na rangi za UDP. Kwa mujibu wa katiba ya chama hicho, Bw Kweya anasema kuwa baada ya kiongozi wa chama kufariki au kujiuzulu, mwenyekiti wa kitaifa ndiye anayepaswa kuchukua nafasi ya kaimu kiongozi wa chama hadi uchaguzi maalumu ufanyike ndani ya mwaka mmoja. Kutokana na hilo, amehoji kwa nini mwenyekiti wa sasa wa chama hajachukua nafasi hiyo kama inavyoelekezwa wazi katika katiba. “Kuna mwenyekiti wa kitaifa aliye madarakani. Ni muhimu kufafanuliwa ni kwa msingi gani wa kikatiba hajachukua jukumu ambalo limetajwa wazi katika kifungu husika cha katiba ya chama,” amesema. Pingamizi hizo zinatatiza mpango uliotangazwa na Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya wa kugeuza UDP kuwa jukwaa la kisiasa la Sifuna kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Baada ya kifo cha Jirongo katika ajali ya barabarani kwenye eneo la Karai katika barabara kuu ya Nairobi-Nakuru, chama hicho kimekuwa kikivutia wanasiasa wanaotafuta vyama vilivyosajiliwa tayari kutumia katika uchaguzi ujao. Bw Kweya anasema mabadiliko ya uongozi hayawezi kufanywa kwa kuwateua viongozi wapya bila kufuata masharti ya katiba ya chama. Pia amehoji hatma ya aliyekuwa Naibu Mwenyekiti wa Taifa, akitaka kufahamishwa ikiwa alijiuzulu, aliondolewa au nafasi hiyo ilitangazwa wazi kwa njia halali. Mbali na mzozo wa uongozi, malalamishi hayo pia yanapinga mpango wa kubadilisha jina, nembo na rangi za UDP. Kweya anataka ushahidi kwamba Baraza Kuu la Kitaifa la chama lilijadili na kuidhinisha mabadiliko hayo kwa mujibu wa taratibu zote zinazotakiwa. Anahitaji maelezo kuhusu tarehe ya kikao, ajenda, waliohudhuria, idadi yao, mijadala iliyofanyika na azimio rasmi lililopitishwa. Kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Kisiasa, chama kilichosajiliwa kikitaka kubadilisha jina, katiba, viongozi, nembo au rangi, lazima kimjulishe msajili ambaye naye anatakiwa kuchapisha taarifa hiyo katika Gazeti Rasmi la Serikali na vyombo vya habari vya kitaifa. Wakati hayo yakijiri, washirika wa Sifuna wamekuwa wakitafuta kwa muda chama kitakachotumika katika kampeni zake za urais. Hapo awali walijaribu kubadilisha jina la UDP kuwa Ukombozi People’s Party, lakini Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa ilikataa ombi hilo kwa maelezo kuwa jina hilo linafanana na lile la The Ukombozi Alliance inayohusishwa na kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka. Kukataliwa kwa ombi hilo kulilazimisha kundi la Sifuna kutafuta mbinu mbadala. Hata hivyo, kiongozi mmoja wa timu yake amenukuliwa akisema kuwa seneta huyo bado hajafichua chama atakachotumia na kwamba ndiye atakayetangaza mwenyewe wakati ufaao. Wakati huo huo, vuguvugu la Linda Mwananchi tayari limemuidhinisha Sifuna kuwa mgombea wake wa urais. Uamuzi huo ulifikiwa katika mkutano uliowahusisha viongozi kadhaa akiwemo Natembeya, Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi, Seneta wa Kakamega Boni Khalwale, Seneta wa Kisii Richard Onyonka, Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino na Mbunge wa Suba Kusini Caroli Omondi. Hata hivyo, Gavana wa Siaya James Orengo hakuhudhuria mkutano huo na hapo awali alikuwa amesisitiza kuwa wanaotaka kugombea urais wanapaswa kupitia mchakato wa wazi wa uteuzi badala ya mmoja wao kupitishwa moja kwa moja. Sasa macho yote yanaelekezwa kwa Msajili wa Vyama vya Kisiasa ambaye atalazimika kuamua ikiwa mabadiliko yanayopendekezwa ndani ya UDP yanafuata katiba ya chama na sheria za nchi. Uamuzi huo unaweza kuwa muhimu kwa mustakabali wa kampeni za Sifuna. Ikiwa washirika wake watafanikiwa kudhibiti mifumo ya kikatiba ya UDP, chama hicho kinaweza kuwa jukwaa lake la urais mwaka 2027. Lakini ikiwa viongozi wanaopinga hatua hizo watashikilia usukani wa chama, basi Sifuna atalazimika kutafuta chama kingine au kuanzisha mkondo mpya wa kisiasa.

KENYA leo inaingia katika hatua muhimu ya sekta ya kawi huku ikianza rasmi ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta kinachotarajiwa kugharimu takriban Sh2 trilioni. Mradi huo unaopangwa kujengwa katika Bandari ya Lamu unatajwa kuwa mkubwa zaidi wa aina yake Afrika Mashariki na unatarajiwa kubadilisha sekta ya mafuta nchini na kufanya Kenya kuwa kitovu cha kawi katika eneo hili. Gharama ya mradi huo ni sawa na takriban asilimia 12 ya Pato la Taifa la Kenya la mwaka 2025, lililofikia Sh17.58 trilioni, kwa mujibu wa Shirika la Kitaifa kuhusu Takwimu Kenya (KNBS). Kiwanda hicho kinatarajiwa kuwa na uwezo wa kusafisha mapipa 700,000 ya mafuta ghafi kwa siku, kiwango sawa na uwezo wa kiwanda cha Dangote kilichoko Lagos, Nigeria. Wiki iliyopita, Rais William Ruto alitembelea kiwanda hicho cha Dangote nchini Nigeria kabla ya hafla ya kuanza ujenzi wa mradi wa Lamu. Kiwanda cha Dangote, ambacho ni kikubwa zaidi Afrika kwa kutumia mfumo mmoja wa kusafisha mafuta, kimegeuka kuwa kituo kikubwa cha viwanda kinachozalisha petroli, dizeli na mafuta ya ndege kwa soko la Nigeria na mataifa mengine. Baada ya ziara hiyo, Rais Ruto alisema kiwanda cha Nigeria kina uwezo wa kusafisha mapipa 700,000 ya mafuta ghafi kwa siku na kuzalisha zaidi ya lita 100 milioni za petroli, dizeli na mafuta ya ndege kila siku. Alisema mradi huo pia umejengwa ukiwa na miundombinu mikubwa, ikiwemo kilomita 120 za mabomba ya chini ya bahari yanayotumika kusafirisha mafuta ghafi kutoka kwenye meli hadi kiwandani. Mradi wa Lamu unalenga kutumia mfano huo kuimarisha uzalishaji wa mafuta nchini na kupunguza kutegemea bidhaa za petroli kutoka nje. Kiwanda hicho kinatarajiwa kuhudumia Kenya pamoja na nchi jirani kama Ethiopia, Uganda, Tanzania, Sudan Kusini na Burundi. Aidha, waendelezaji wa mradi huo wanatarajia kutumia mafuta ghafi yanayochimbwa nchini Kenya pamoja na kutoka mataifa jirani, yakiwemo Sudan Kusini. Mradi huo pia unatarajiwa kutoa ajira nyingi. Rais Ruto amesema unaweza kuzalisha hadi ajira 60,000 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja wakati wa ujenzi na kikianza kufanya kazi. Mbali na mafuta, kiwanda hicho kinatarajiwa kuchochea viwanda vingine, vikiwemo vya kemikali na mbolea “Mradi huu utabadilisha sekta ya mafuta nchini na katika eneo hili, kuhakikisha upatikanaji wa mafuta, kuimarisha usalama wa kawi, kuongeza uzalishaji viwandani na kuunda ajira 60,000,” Rais Ruto alisema. Maandalizi ya ujenzi tayari yameanza. Mwishoni mwa wiki, meli MV Da Yang Bai He ilitia nanga katika Bandari ya Lamu ikiwa na zaidi ya tani 2,900 za vifaa vya ujenzi na mizigo ya mradi. Ujenzi wa kiwanda hicho unatarajiwa kuchukua kati ya miezi 30 na miaka minne baada ya uzinduzi. Kampuni ya Engineers India Limited (EIL) kutoka India, ambayo ilihusika katika ujenzi wa kiwanda cha Dangote nchini Nigeria, imepewa mkataba wa karibu Sh58 bilioni, kuwa mshauri mkuu wa usimamizi wa mradi wa Lamu. EIL ilisema kiwanda hicho kitakuwa cha kisasa na kitasaidia kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya mafuta katika Afrika Mashariki. Kampuni hiyo pia ilisema mradi huo utasaidia kupunguza kutengemea bidhaa za mafuta kutoka nje na kuimarisha usalama wa kawi katika ukanda huu. Kiwanda cha Dangote nchini Nigeria kiligharimu karibu Sh2.6 trilioni, na sasa kinafanya kazi kikamilifu. Dangote pia amepanga kuongeza uwezo wake wa kusafisha mafuta hadi mapipa 1.4 milioni kwa siku ifikapo 2029. Kwa Kenya, mradi wa Lamu unalenga kuiga mafanikio hayo katika pwani ya Afrika Mashariki, huku ukifungua nafasi kwa shughuli zaidi za viwanda na biashara zinazohusiana na mafuta. Iwapo utakamilika kama ulivyopangwa, kiwanda hicho kitakuwa mojawapo ya miradi mikubwa zaidi ya uwekezaji binafsi kuwahi kufanywa Afrika Mashariki.

KILIMANJARO: NAIBU Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, ameitaka sekta binafsi kuongeza uwekezaji katika usafiri wa anga ili kuimarisha huduma, kuongeza ushindani na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa. Kihenzile ametoa wito huo wakati akikagua maendeleo ya maboresho yanayoendelea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ikiwemo Jengo la Watu Mashuhuri la Uhuru, ambalo…

The High Court’s Dar es Salaam Sub-Registry will deliver its judgment on November 6, 2026, in the treason case against Chadema national chairman Tundu Lissu. The trial, which has lasted about a year, concluded on Tuesday, September 29, after the prosecution and defence presented their final submissions before a three-judge panel. Mr Lissu is charged under Section 39(2)(d) of the Penal Code, Revised Edition 2022, with allegedly showing intent to threaten the Government. The prosecution alleges that on April 3, 2025, Mr Lissu, while in Tanzania, made statements and published material online that incited the public to prevent the 2025 General Election. The prosecution cited statements in which Mr Lissu allegedly said the opposition would prevent the election, mobilise rebellion and “disrupt” the polls in pursuit of political change. The case is being heard by Justices Dunstan Ndunguru, who chairs the panel, James Karayemaha and Ferdinand Kiwonde. Mr Lissu presented his final submissions from September 23 to 28, arguing that the prosecution had failed to prove the charge based on the evidence presented in court. The prosecution presented its final submissions on September 29, arguing that it had met the required legal threshold. State Attorney Nassoro Katuga said evidence from 17 prosecution witnesses, together with evidence from five defence witnesses, had established the charge beyond reasonable doubt. “We submit that the Republic has proved the charge beyond reasonable doubt and ask the court to find that the accused committed the offence,” Mr Katuga told the court. He said the prosecution’s sole objective had been to prove the charge under the provision, which he described as a new legal provision being applied for the first time in the case. Justice Ndunguru thanked the parties and members of the public who attended the proceedings. He also referred to disruptions caused by ringing mobile phones during the hearing, saying the judges had not been provoked into invoking Section 114 of the Penal Code. He said the court needed time to consider the lengthy evidence and final submissions, particularly because the case involved a charge being heard under the provision for the first time. “Therefore, we will deliver the judgment on November 6, 2026,” Justice Ndunguru said.

Says 2027 polls must not be compromised By Adesina Wahab Senator Iyabo Obasanjo has raised the alarm over what she described as renewed threats to her life following an attack on a campaign gathering of the Peoples Democratic Party (PDP) in Abeokuta, Ogun State, on Monday. Obasanjo, the PDP candidate for Ogun Central Senatorial District […]

The council said it had mobilised public servants across the country for a three day warning strike if the Federal Government failed to address the issues raised in its letter to President Bola Tinubu before the deadline.

MOSHI: Baadhi ya madereva wa mabasi katika Stendi Kuu ya Mabasi Moshi, mkoani Kilimanjaro, wamegoma kutoa huduma za usafiri kwa saa kadhaa kupinga mfumo wa kukatwa pointi za leseni kwa makosa ya barabarani, wakidai kuwa utaratibu huo unawaongezea mzigo wa kiuchumi licha ya baadhi ya makosa hayo kutozwa faini. Madereva hao pia wanaitaka Serikali kuweka…

VYUO VIKUU vya umma vinaendelea na juhudi za dharura kutafuta suluhu ya mzozo wa Mkataba wa Pamoja wa Kazi (CBA) kabla ya wahadhiri kutekeleza tishio lao la kugoma ndani ya siku chache zijazo. Chama cha Wahadhiri wa Vyuo Vikuu (UASU) kimesisitiza kuwa notisi yake ya mgomo bado ipo na kwamba wahadhiri watasusia kazi Oktoba 2, 2026 ikiwa mazungumzo kuhusu CBA mpya ya kipindi cha 2025 hadi 2029 hayatapiga hatua za kuridhisha. Katika Chuo Kikuu cha Nairobi, wasimamizi wameanza tena mashauriano na viongozi wa vyama vya wafanyakazi pamoja na Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC) ili kutatua masuala yaliyosalia kuhusu mikataba ya awali ya wafanyakazi. Chuo hicho kinasema kilikamilisha mazungumzo ya CBA ya miaka 2017 hadi 2021 na vyama vitatu vinavyotambuliwa rasmi, ambavyo ni UASU, KUSU na KUDHEIHA, mwezi Aprili mwaka huu. Baada ya mazungumzo hayo, mikataba hiyo iliwasilishwa kwa SRC kwa ushauri kabla ya kusajiliwa rasmi. Hata hivyo, SRC ilieleza wasiwasi wake kuhusu baadhi ya marupurupu yaliyopendekezwa, yakiwemo ya nyumba, likizo, vitabu, maprofesa, matibabu ya meno na macho, pamoja na marupurupu ya wafanyakazi wanaoshikilia nyadhifa mbalimbali. Kutokana na hali hiyo, SRC ilitaka chuo hicho kurekebisha baadhi ya vipengele au kuwasilisha ushahidi unaoonyesha kuwa marupurupu hayo yanaweza kugharamiwa kwa njia endelevu. Wakati huo huo, vyuo vikuu vya umma vimeeleza kuwa havina uwezo wa kifedha wa kufadhili CBA mpya bila msaada wa ziada kutoka Wizara ya Fedha. Viongozi wa vyuo hivyo wanasema taasisi hizo tayari zinakabiliwa na upungufu wa zaidi ya Sh100 bilioni kutokana na fedha ambazo serikali haijatoa kikamilifu chini ya mfumo mpya wa ufadhili wa wanafunzi. Mwenyekiti wa Kamati ya Makamu wa Vyuo Vikuu vya Umma, Profesa Daniel Mugendi, amesema ukosefu wa fedha umeweka vyuo katika hali ngumu ya kutekeleza majukumu ya kawaida ya masomo, wafanyakazi na shughuli za uendeshaji. Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa UASU, Dkt Constantine Wasonga, amesema vyuo haviwezi kutegemea karo ya wanafunzi kufadhili mishahara ya wahadhiri. Amesisitiza kuwa serikali ndiyo inapaswa kutoa fedha maalum za kutekeleza CBA mpya.

DAR ES SALAAM: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ameziagiza kampuni zinazokusanya na kusafirisha taka katika eneo la Tabata Liwiti, Mtaa wa Mfaume, Wilaya ya Ilala, kuacha mara moja utupaji wa taka ovyo na kuzitaka kuzipeleka katika dampo lililotengwa, ikiwemo Pugu. Chalamila amesema wananchi wanalipia huduma ya ukusanyaji na usafirishaji wa taka,…

WATETEZI wa haki za kiraia wamewasilisha kesi katika Mahakama Kuu wakitaka taasisi za usimamizi wa fedha za umma zizuiwe kuidhinisha matumizi ya serikali za kaunti yanayozidi kiwango cha asilimia 35 ya mapato kinachoruhusiwa kutumiwa kwa mishahara na marupurupu ya wafanyakazi. Walalamishi hao, akiwemo Laban Omusundi pamoja na mashirika ya Ignite Kenya na Sheila Kendi, wanadai kuwa Mdhibiti wa Bajeti, Wizara ya Fedha, Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC), Seneti na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wameshindwa kutekeleza sheria licha ya ripoti za ukaguzi kuonyesha ukiukaji huo kwa miaka kadhaa.Katika kesi hiyo, wanataka mahakama itangaze kuwa matumizi yoyote ya fedha za kaunti yanayozidi kiwango cha asilimia 35 ni kinyume cha Katiba na sheria za usimamizi wa fedha za umma. Pia wanataka taasisi hizo ziagizwe kuchukua hatua za kuhakikisha hitaji hili linatekelezwa kikamilifu.Jaji Julius Nang’ea aliidhinisha kesi hiyo kuwa ya dharura na kuagiza walalamishi kuwasilisha stakabadhi za kesi kwa washtakiwa mara moja. Hata hivyo, hakutoa maagizo ya muda waliyokuwa wameomba.Mzozo huo unahusu Kanuni ya 25(1)(b) ya Sheria ya Usimamizi wa Fedha za Umma kwa Serikali za Kaunti ya mwaka 2015, ambayo inaelekeza kuwa mishahara na marupurupu ya wafanyakazi wa kaunti hayafai kuzidi asilimia 35 ya jumla ya mapato ya kaunti. Walalamishi wanasema kiwango hicho kiliwekwa kulinda uthabiti wa kifedha na kuhakikisha angalau asilimia 65 ya mapato ya umma yanatumiwa katika maendeleo na utoaji wa huduma kwa wananchi.Kwa mujibu wa ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, serikali za kaunti zilitumia Sh207.99 bilioni kwa mishahara na marupurupu katika mwaka wa kifedha wa 2023/24, sawa na asilimia 45 ya mapato yao yote. Ripoti hiyo ilionyesha kuwa ni kaunti chache sana zilizofanikiwa kuzingatia kiwango kilichowekwa kisheria.Taarifa za hivi majuzi pia zinaonyesha kuwa kaunti 42 zilitumia kati ya asilimia 37 na 63 ya mapato yao kwa mishahara na marupurupu katika miezi tisa hadi Juni 2026. Kwa kipindi hicho, kaunti hizo zilitumia Sh171.36 bilioni kwa mishahara dhidi ya mapato ya Sh386.59 bilioni. Walalamishi wanaonya kuwa ongezeko la matumizi ya mishahara limeathiri utoaji wa huduma muhimu kama afya, maji, usafi wa mazingira, kilimo na ujenzi wa barabara. Wanasema hali hiyo imechangia kukwama kwa miradi ya maendeleo, uhaba wa dawa hospitalini, kucheleweshwa kwa malipo ya wasambazaji na kuongezeka kwa madeni ya kaunti.Kesi hiyo, ambayo imetaja kaunti zote 47 kama wahusika wenye maslahi, itatajwa tena mahakamani Oktoba 12 kwa maelekezo zaidi

The United States has praised Nigeria’s response to recent attacks in the Middle Belt, urging the government to maintain efforts to safeguard communities in Plateau State.

DAR ES SALAAM: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewataka viongozi katika maeneo mbalimbali kutekeleza kwa vitendo maelekezo ya Serikali, hususan kuhusu usafi na utunzaji wa mazingira, akisisitiza kuwa hawapaswi kusubiri kukumbushwa mara kwa mara kuhusu wajibu wao. Chalamila ametoa kauli hiyo leo wakati wa ziara yake Wilaya ya Kinondoni, ambapo alitembelea…

TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imepanua usajili wa Wakenya wanaoishi ughaibuni kutoka nchi 12 hadi 26, hatua inayolenga kuwapa Wakenya wengi zaidi nafasi ya kushiriki uchaguzi mkuu wa Agosti 2027. Wakati huo huo, tume hiyo imekanusha madai kwamba inasajili raia wa nchi jirani kuwa wapigakura nchini Kenya. Mwenyekiti wa IEBC Erastus Ethekon amesema Wakenya wanaoishi ughaibuni wana haki ya kushiriki uchaguzi kama sehemu ya wajibu wao wa kikatiba. “Tume imeidhinisha mchakato wa kutambua nchi zaidi ili kuongeza idadi ya Wakenya wanaoshiriki uchaguzi kutoka nchi za nje. Usajili utaanza baada ya kuzinduliwa kwa awamu ya pili ya Usajili Endelevu wa Wapigakura,” akasema Bw Ethekon. Usajili wa Wakenya walio nje ya nchi ulianza katika nchi chache wakati wa uchaguzi wa 2013 na kuongezwa katika chaguzi zilizofuata, hadi kufikia nchi 12 katika uchaguzi wa 2022. Bw Ethekon alisema hatua hiyo inazingatia Kifungu cha cha Katiba kinachotaka usajili wa Wakenya wanaoishi nje ya nchi uendelee ili watimize haki yao ya kushiriki uchaguzi. Alisema usajili wa wapigakura walioko nje ya nchi si mchakato wa siri au usio rasmi, bali ni jukumu la IEBC lililotambuliwa na Katiba na linalotekelezwa kupitia mifumo maalumu chini ya usimamizi wa tume. Alikanusha pia madai kwamba IEBC inawasajili raia wa Uganda kuwa wapigakura, akisema madai hayo yanaweza kudhoofisha imani ya umma katika uadilifu na usalama wa uchaguzi. Bw Ethekon alisema hadi sasa hakuna mtu, shirika au kikundi kilichowasilisha ushahidi wa kuaminika kuhusu madai ya ukiukaji wa sheria au ubadhirifu. Alisema iwapo ushahidi wa kuaminika utawasilishwa, tume itachukua hatua zinazofaa, ikiwemo uchunguzi wa makosa ya jinai na kuwafikisha wahusika mahakamani.

A senior official of the Democratic Republic of the Congo’s ruling party was beaten to death on Sunday after appearing on a radio programme to raise awareness about the Ebola outbreak, according to a party representative.

By Edwin Phillip, Lafia LAFIA — The Vice Chancellor of the Federal University of Lafia (FULafia), Prof. Mohammed Isa Kida, has raised concern over the impact of insecurity on student enrolment, saying fear of kidnapping and other criminal activities is forcing some students to stay away from the institution. Kida disclosed this on Monday during […]

Flip-flops, inadequate protective equipment and limited safety training among some fuel station workers are not simply individual shortcomings but signs of gaps in a system meant to protect people working in hazardous environments.

WAZIRI wa Afya Aden Duale amezua mdahalo mitandaoni baada ya kusema atawahamasisha Wasomali kutoka Somalia kumuunga mkono Rais William Ruto katika uchaguzi mkuu wa 2027. Akizungumza katika mkutano na wanachama wa Muungano wa jamii ya Wasomali jijini Mombasa, Bw Duale alisema ana uzoefu wa zaidi ya miaka 25 katika siasa na amehudumu katika serikali za marais wa zamani Mwai Kibaki na Uhuru Kenyatta pamoja na Rais Ruto. Alisema uzoefu huo umemwezesha kutofautisha jinsi serikali hizo tatu zilivyoshughulikia Waislamu na jamii ndogo nchini. Bw Duale alikosoa operesheni za kiusalama zilizofanywa wakati wa utawala wa Kibaki na Kenyatta, akisema vijana Waislamu waliuawa katika Msikiti wa Musa, Mombasa, kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi. “Lazima tuseme ukweli. Watoto wetu waliuawa kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi. Kenya ni ya kila mtu na sisi si wageni katika nchi hii. Tulizaliwa hapa, sisi ni wafugaji, Waislamu, watu wa Kaskazini Mashariki na Pwani na Kenya ni yetu,” akasema. “Ikiwa unafikiri wafugaji na Waislamu ni watalii, basi utapata mshangao mkubwa.” Akaongeza. Bw Duale alisema serikali ya Ruto imeondoa vikwazo vilivyowakabili Wasomali na Waislamu kupata vitambulisho, pasipoti na vyeti vya kuzaliwa. Alisema hapo awali waliotuma maombi ya kupata stakabadhi hizo walikabiliwa na ukaguzi wa kiusalama kutoka taasisi mbalimbali. “Watoto wetu walichunguzwa na kuulizwa maswali kutoka hapa hadi Ethiopia, lakini leo Mungu alitupa Rais Ruto ambaye ameleta usawa,” akasema. “Rais Ruto alipoondoa ukaguzi huo, walisema alikuwa akileta watu kutoka Somalia. Sasa nataka kusema wazi kwamba tutawaleta Wasomali kutoka Somalia.” Bw Duale aliwataka Waislamu kumuunga mkono Rais Ruto kwa muhula mwingine, akisema serikali yake imewapa nafasi zaidi katika nyadhifa za juu. Alisema pia ushirikiano wa sasa kati ya ODM na UDA katika serikali Jumuishi utasaidia kuhakikisha Rais Ruto anachaguliwa tena 2027.

UHUSIANO wa kimapenzi uliodumu miaka minne kati ya mwanamume raia wa Uholanzi na mwanamke Mkenya umeishia kortini kuhusiana na zawadi ikiwemo Sh2.2 milioni anazosema alituma kujenga boma walilopaswa kuishi pamoja baada ya kufunga ndoa. Hata hivyo, mwanamke huyo Bi SL anasema pesa hizo alipewa kwa hiari kama zawadi walipokuwa wakichumbiana na kukanusha kuahidi kuolewa na raia huyo wa kigeni, Bw BD, wala kujenga boma naye. Kiini cha mvutano huo kinadaiwa kuwa ahadi ya ndoa ambayo haikutimizwa, mwanamume mwingine kuishi katika nyumba husika, polisi kuhongwa na kupigania kurejeshewa hela. Mgogoro huo umebadilika kutoka uhusiano wa kimapenzi uliotibuka kuwa kesi ya uhalifu ambapo Bi SL anashutumiwa kudanganya na kupata hela kupitia ujanja katika kesi ambapo Bw BD anaitisha kulipwa Sh2.4 milioni kwa jumba la ghorofa tatu kutoka kwa SL eneo la Vikwathani, Bamburi, Mombasa. Mahakama Kuu Ijumaa ilipuuzilia mbali jaribio la SL kusimamisha kesi ya uhalifu, ikiacha mashtaka ya uhusiano, hela na mali kushughulikiwa katika kesi iliyowasilishw mbele ya korti za hakimu. Kulingana na Bi SL, uhusiano ulianza baada ya Bw BD kumfuata kupitia jamaa wa familia kuanzia 2019. Alimwelezea kama raia wa Uholanzi anayezuru Kenya mara moja kwa mwaka. Kuanzia mwishoni mwa 2020 hadi 2023 katikati, alisema BD alimtumia kupitia M-Pesa, aghalabu Sh100, Sh200 au Sh1,000 kwa kadi ya simu au chamcha kama “mpenzi wake mtarajiwa.” Alisema Sh70,000 zilitumwa kwa mazishi ya baba yake BD huku fedha nyingine zikitumika kuweka paa nyumba yake Likoni. Alisema walikutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza mwishoni mwa 2022. “Korti hii haiwezi kuchukua hatua kwa ushahidi ambapo upande mmoja unasema upo lakini umeamua kutowasilisha,” alisema Jaji Ngaah Jairus. Jaji alikanusha hoja kuwa mzozo huo unahusu tu uhusiano uliotibuka au suala la mali. “Iwe pesa zilikuwa zawadi au zilipatikana kupitia ulaghai ndiyo aina ya suala halisi, ambalo ni sharti korti itoe uamuzi kulihusu baada ya kusikiza ushahidi utakaopigwa msasa kupitia kuhoji,” alisema jaji.

ARUSHA: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ametoa wito kwa viongozi wa taasisi za umma kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na badala yake kuelekeza fedha katika kuwawezesha vijana kwa kuwajengea uwezo na uzoefu. Ndejembi ameyasema hayo leo Septemba 28, 2026, katika hafla ya kufungua Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi…

KAHAMA: Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba, ametoa maagizo kwa wamiliki na mameneja wa migodi nchini kuhakikisha wanaboresha maeneo ya uchimbaji wa madini, hususan upande wa maduara, uwekaji wa mtingi na vyoo, ili kuhakikisha usalama kabla ya mvua za El Nino zinazotabiriwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuanza kunyesha.…

DAR ES SALAAM: ZAIDI ya watu 300, wakiwemo vijana, viongozi wa Serikali, watunga sera, wataalamu wa afya, mashirika ya kiraia na wadau wa maendeleo, wanatarajiwa kushiriki Mkutano wa Young and Alive Summit 2026 unaolenga kutoa nafasi kwa vijana kujadili changamoto zao na kushiriki katika kutafuta suluhisho. Mkutano huo utafanyika kuanzia Oktoba 11 hadi 14, mwaka…

DAR ES SALAAM: Serikali imesisitiza umuhimu wa kusimamia uadilifu, usahihi na ukweli katika mnyororo wa taarifa, hasa katika kipindi hiki ambacho teknolojia ya kidijitali imeongeza kasi ya upatikanaji na usambazaji wa habari. Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upatikanaji wa Taarifa (IDUAI), kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa…

MOROGORO: SERIKALI imesema inatambua kuwa vyama vya ushirika na saccos nchini vina mchango mkubwa katika kukuza uchumi kwa wananchi na kwa kupitia Saccos wanaweza kuweka akiba, kupata mikopo kwa masharti nafuu , kukuza biashara na kuimarisha ustawi wa familia. Naibu Waziri wa Fedha, Mhandisi Mshamu Munde, amesema hayo akifungua mkutano mkuu wa 13 wa mwaka…

KENYA imepewa leseni ya kutengeneza dawa mpya ya kumeza ya kuzuia maambukizi ya ukimwi, hatua inayoiweka miongoni mwa nchi tatu Afrika zitakazozalisha dawa hiyo kwa ajili ya masoko ya Afrika. Kampuni ya dawa ya Merck imetoa leseni ya kuzalisha toleo la bei nafuu la Alimatravir, dawa inayotarajiwa kumezwa mara moja kwa mwezi. Nchini Kenya, dawa hiyo itatengenezwa na Kampuni ya Universal Corporation. Hatua hiyo inatajwa kuwa ya kihistoria kwani watengenezaji wa dawa barani Afrika wamehusishwa katika mchakato wa uzalishaji wa dawa ya HIV tangu mwanzo. Utafiti wa awamu ya tatu unaoendelea Kenya, Uganda na Afrika Kusini unahusisha wanawake vijana na unatarajiwa kukamilika mwaka ujao. “Afrika inabeba robo ya mzigo wa magonjwa duniani. Tunatengeneza chini ya asilimia sita ya vifaa vya matibabu tunavyohitaji na asilimia moja ya chanjo tunazotumia.” akasema Rais William Ruto, katika hotuba iliyosomwa na Waziri wa Afya Aden Duale katika mkutano wa pembeni wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Alisema janga la Covid-19 lilionyesha madhara ya kutegemea minyororo ya usambazaji kutoka nje. “Watu wetu walilipa gharama ya minyororo ya usambazaji ambayo hatukuimiliki. Hatutapitia hali hiyo tena,” akasema. Rais Ruto pia alisema Afrika sasa ina fursa ya kutengeneza dawa zake badala ya kusubiri kuzinunua kutoka nje. “Kiwanda kisichokuwa na wanunuzi si sekta ya viwanda. Ni jengo la gharama kubwa,” alisema. Merck inasema dawa hiyo inaweza kugharimu dola tano (Sh650) kwa mtu kwa mwaka. Dkt Nicholas Muraguri alisema ushirikiano huo utasaidia Afrika kuimarisha uzalishaji wa dawa, ajira na usambazaji. “Ushirikiano huu si wa kusambaza dawa pekee, unahusu kubadilisha mfumo wa usawa katika afya duniani,” akasema. Alisema tatizo la kuzuia maambukizi ya ukimwi si ukosefu wa sayansi, bali gharama na kupungua kwa ufadhili wa programu za afya.

IRINGA: Ujenzi wa nyumba ya muhudumu wa afya katika Zahanati ya Usolanga, wilayani Iringa unatarajiwa kupiga hatua baada ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, Arif Abri, kuchangia mabati 30. Pamoja na msaada huo utakaosaidia kuimarisha mazingira ya utoaji wa huduma kwa wananchi wa kijiji hicho na maeneo ya jirani, kada huyo wa CCM…

GEITA: SERIKALI imejizatiti kuimarisha utafiti wa kina wa jiofizikia kutoka takribani asilimia 16 ya sasa hadi angalau kufikia asilimia 50 ya eneo lote la nchi ifikapo mwaka 2030. Mpango huo unalenga kuongeza mchango wa sekta ya madini katika pato la taifa ambapo hadi mwaka 2025/26 mchango wa sekta ya madini umefikia asilimia 10 huku ikichangia…

The Dar es Salaam Water Supply and Sanitation Authority (Dawasa) has identified more than 20 areas where water infrastructure could be affected by heavy El Niño rains expected in Dar es Salaam and Coast regions.

TABORA: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) National Executive Committee Secretary for Politics and International Relations, Ms Rabia Hamid, has called on persons with disabilities, young people and other social groups to utilise government loans provided through local authorities to improve their economic wellbeing. Speaking in Tabora over the weekend during a meeting attended by party leaders,…