WAUMINI 16 wa Kanisa Katoliki kutoka parokia ya St Mathias Mulumba, Mikindani, Mombasa, wamefariki katika ajali ya barabarani eneo la Salama, Kaunti ya Makueni.
Waumini hao walikuwa safarini kuelekea Subukia, Nakuru, kuhudhuria Siku ya Kitaifa ya Maombi) katika Madhabahu ya Kitaifa ya Subukia.
Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mombasa, Martin Kivuva Musonde, alithibitisha kifo cha mahujaji hao kupitia taarifa aliyotuma kwa mapadre, watawa na waumini.
“Tunasikitika kwa huzuni kubwa kutangaza kifo cha ghafla cha mahujaji 16 kutoka St Mathias Mulumba, Mikindani, katika ajali iliyotokea Salama,” alisema Askofu Kivuva.
Alisema mahujaji hao walikuwa njiani kuelekea Madhabahu ya Kitaifa ya Subukia kwa ajili ya Siku ya Kitaifa ya Maombi.
Askofu Kivuva aliwataka waumini kuombea roho za marehemu, familia zao, Parokia ya St Mathias Mulumba na Dayosisi ya Mombasa kwa ujumla ili wapate faraja katika kipindi hiki kigumu.
“Tuombe kwa ajili ya pumziko la roho zao tunapoombea familia zao, parokia ya St Mathias Mulumba na Dayosisi nzima ili tupate faraja na utulivu kutoka kwa Bwana,” alisema.
Alimalizia taarifa hiyo kwa kuwaombea marehemu, akisema: “Roho zao zipumzike kwa amani. Amina.”
Kamishna wa Kaunti ya Makueni, Abdullahi Khalif, amethibitisha ajali hiyo.
17 waliofariki ajalini Salama ni mahujaji wakielekea Subukia, aeleza Askofu

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsAfenifere demands prosecution of sponsors of campaign violence
…Raises alarm over rising attacks ahead of 2027 elections By Adeola Badru The pan-Yoruba socio-political organisation, Afenifere, has raised the alarm over increasing political violence ahead of the 2027 general elections, calling for the arrest and prosecution of perpetrators and their sponsors. The organisation warned that the growing incidents of thuggery, intimidation and inflammatory political […]
NewsPHOTOS: First Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsFirst Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsObi woos Onitsha voters, promises jobs, better services
…Says Nigeria needs energetic president By Vincent Ujumadu The presidential candidate of the Nigeria Democratic Congress (NDC), Peter Obi, on Friday drew a large crowd in Onitsha, Anambra State, as he led members of his campaign team on a roadshow and town hall meeting in the commercial city. Obi began his visit with a stop […]