WATOTO wanane wameokolewa kutoka nyumbani kwa Anastacia Mumwele, mama wa mhubiri tata Paul Mackenzie, eneo la Furunzi, Malindi, Kaunti ya Kilifi, ambako inadaiwa walikuwa wakilazimishwa kufunga na kunyimwa fursa ya kwenda shuleni.
Wapelelezi kutoka Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) walimkamata Bi Mumwele, nyanya wa watoto hao, wakati wa msako katika nyumba yake Jumatano alasiri.
Watoto hao, wenye umri wa kati ya miaka sita na 14, walipatikana ndani ya nyumba hiyo. Watano kati yao wanaaminika kuwa watoto wa Mackenzie.
Afisa mkuu wa DCI, ambaye alizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina, alisema wapelelezi walichukua hatua baada ya kupata taarifa kwamba watoto hao walikuwa wakinyimwa chakula na kulazimishwa kufuata mafundisho yanayohusishwa na imani ya Mackenzie kuhusu mwisho wa dunia.
“Tulipokea taarifa kwamba nyanya yao alikuwa amewafungia watoto hao na kuwanyima chakula, hali iliyotulazimu kuchukua hatua na kuwaokoa,” afisa huyo alisema.
Watoto hao walipelekwa katika Kituo cha Polisi cha Malindi, ambako maafisa wa Kitengo cha Kulinda Watoto walitarajiwa kuchukua jukumu la ustawi wao na kuwawezesha kuhamishiwa katika mazingira salama zaidi.
Mwanawe Mackenzie, Dan Mackenzie, alisema aliripoti suala hilo kwa polisi baada ya baadhi ya ndugu zake na binamu zake kukataa kula.
Pia alisema aligundua kuwa watoto hao hawakuwa wakienda shuleni.
“Nilichukua hatua na kwenda kuripoti kwa polisi. Hali yao si mbaya, lakini walipewa chakula kabla ya kuchukuliwa na polisi,” Dan alisema katika mahojiano na Taifa Leo.
Dan alidai watoto hao walikuwa wakiendelea kufuata mafundisho yanayofanana na yale yanayohusishwa na vifo vya zaidi ya watu 400 katika mauaji ya Shakahola.
Afisa huyo wa DCI alisema Bi Mumwele atazuiliwa hadi atakaposhtakiwa mahakamani Alhamisi.
“Tutamshtaki kwa makosa yanayohusiana na ukatili dhidi ya watoto, kuwatesa na kuwanyima watoto haki ya kupata elimu,” afisa huyo alisema.
Kuokolewa kwa watoto hao kunafanyika zaidi ya miaka miwili baada ya Mackenzie kukamatwa na kushtakiwa pamoja na washtakiwa wenzake kadhaa kuhusiana na vifo vinavyohusishwa na mauaji ya Shakahola na Kwa Binzaro katika Kaunti ya Kilifi.
Mackenzie anakabiliwa na mashtaka 191 ya mauaji yanayohusiana na vifo vya Shakahola. Waendesha mashtaka pia wamemshtaki kwa kosa la kuua bila kukusudia kuhusiana na vifo vingine 52 vinavyohusishwa na mauaji ya Kwa Binzaro.
Pia anakabiliwa na mashtaka ya ugaidi na kueneza misimamo mikali.
Watoto wanane waliokuwa wakifunga waokolewa kutoka nyumba ya mamake pasta Mackenzie

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsAfenifere demands prosecution of sponsors of campaign violence
…Raises alarm over rising attacks ahead of 2027 elections By Adeola Badru The pan-Yoruba socio-political organisation, Afenifere, has raised the alarm over increasing political violence ahead of the 2027 general elections, calling for the arrest and prosecution of perpetrators and their sponsors. The organisation warned that the growing incidents of thuggery, intimidation and inflammatory political […]
NewsPHOTOS: First Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsFirst Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsObi woos Onitsha voters, promises jobs, better services
…Says Nigeria needs energetic president By Vincent Ujumadu The presidential candidate of the Nigeria Democratic Congress (NDC), Peter Obi, on Friday drew a large crowd in Onitsha, Anambra State, as he led members of his campaign team on a roadshow and town hall meeting in the commercial city. Obi began his visit with a stop […]