KUTAWAZWA kwa Naibu Rais Kithure Kindiki kuwa msemaji wa Mlima Kenya kumeibua mgawanyiko katika Baraza la Wazee la Kiama Kia Ma, huku makundi mawili yakidai kuwa ndiyo yenye mamlaka halali.
Mkutano wa siri wa wazee 63 ulioitishwa Septemba 28 na mlezi wa baraza hilo, Kung’u Muigai, ulihitimisha kuwa Kiama Kia Ma, lililoanzishwa mwaka 2010, limegawanyika na kwa sasa halina mamlaka halali ya kumtawaza kiongozi yeyote hadi mzozo huo utatuliwe.
Bw Muigai alisema mkutano huo ulianza saa mbili usiku na kumalizika karibu saa nane alfajiri.
“Ilikuwa wazi kuwa Kiama Kia Ma lililoanzishwa mwaka 2010 na lililopaswa kufanya uchaguzi kila baada ya miaka minne sasa limegawanyika,” alisema.
Mzozo huo unahusishwa pia na madai ya kughushi hati za usajili wa baraza hilo. Cheti kilichodaiwa kutolewa Agosti 20, 2019 kilikataliwa na Ofisi ya Msajili wa Mashirika, iliyosema saini iliyokuwa kwenye cheti hicho haikuwa ya afisa aliyedaiwa kuitia.
Mwaka 2022, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) iliagiza Inspekta Jenerali wa Polisi kuchunguza madai ya kughushi cheti hicho na kuwasilisha ripoti.
Mzozo huo pia umehusishwa na siasa za kuelekea uchaguzi wa 2027, huku madai yakitolewa kuhusu aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua.
Hata hivyo, Gachagua amekanusha kuhusika na akawataja wazee waliomtawaza Kindiki kuwa “bandia”.
Kindiki naye amejitenga na mzozo huo, akisema sherehe hiyo ilikuwa mpango wa wazee.
“Nilikuwa mgeni wao. Wao ndio wanapaswa kujibu maswali hayo,” alisema.
Sherehe ya kumtawaza Kindiki ilifanyika katika Uwanja wa Kirigiti, Kaunti ya Kiambu, Septemba 19.
Kutawazwa kwa Kindiki kwagawanya wazee

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsAfenifere demands prosecution of sponsors of campaign violence
…Raises alarm over rising attacks ahead of 2027 elections By Adeola Badru The pan-Yoruba socio-political organisation, Afenifere, has raised the alarm over increasing political violence ahead of the 2027 general elections, calling for the arrest and prosecution of perpetrators and their sponsors. The organisation warned that the growing incidents of thuggery, intimidation and inflammatory political […]
NewsPHOTOS: First Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsFirst Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsObi woos Onitsha voters, promises jobs, better services
…Says Nigeria needs energetic president By Vincent Ujumadu The presidential candidate of the Nigeria Democratic Congress (NDC), Peter Obi, on Friday drew a large crowd in Onitsha, Anambra State, as he led members of his campaign team on a roadshow and town hall meeting in the commercial city. Obi began his visit with a stop […]