
Wapewa elimu kuepusha watoto dawa za kulevya
MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini imetoa elimu kwa Umoja wa…
Category
Education policy, exam results and calendars, scholarships and opportunities for students, parents and teachers across the region.

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini imetoa elimu kwa Umoja wa…
CHAMA cha walimu (KNUT) kinataka Tume ya Kuajiri Walimu (TSC) iajiri washauri nasaha kushughulikia visa vya kujitia kitanzi na matumizi mabaya dawa za kulevya kwa walimu. TSC inasema walimu wengi wanahangaishwa na magonjwa ya akili, hali ambayo imeathiri utendakazi wao na kusambaratisha familia zao. Mwakilishi wa Kike wa Kwanza wa Kitaifa Mercy Ndung’u amesema maelfu ya walimu wanaumia lakini wao huwa wananyamaza tu. “Walimu wanahitaji huduma za ushauri popote walimu nchini. Ni huduma ya lazima ambayo inafaa kutolewa na wizara na mwaajiri ili kuokoa maisha,” Bi Ndung’u akasema katika hafla ya kuadhimisha siku 16 ya kukabili dhuluma za kijinsia mjini Bomet mwisho wa juma. “Baadhi ya changamoto za walimu huwasababisha kujihusisha na utumizi mbaya wa dawa za kulevya ili waepuke hali halisi ya maisha. Ni suala ambalo linafaa kuangaziwa na washikadau wote wa elimu nchini,” akaongeza. Kauli yake ilikaririwa na mwanachama wa Baraza Kuu la Utendaji (NEC) Alice Bor, Katibu Mtendaji wa KNUT tawi la Bomet Desmond Langat, naibu wake Jeff Bett na mwakilishi mwanamke wa KNUT tawi la Bomet Betty Langat. “Baadhi ya walimu wamejiua sababu ya msongo wa mawazo, wengine wametelekeza wajibu huku baadhi wakianza uraibu wa pombe baada ya kukosa msaada wa kisaikolojia,” akasisitiza Bw Langat. Naye Bw Bett akasema: “Walimu wanahitaji msaada kutoka kwa washikadau wote katika jamii. Hatufai kupuuza changamoto ambazo zinawakabili walimu nchini.” Walisema walimu wamekuwa wakipelekwa katika vituo vya kurekekebisha tabia nchini na wakarejea wakiwa wameimarika huku wengine wakiishia kusumbuka tena. Bi Langat alidokeza kuwa walimu wengine wanaishi bila waume ama wake sababu ya kifo ama utengano; suala ambalo anasema halifai kupuuzwa. TSC imekuwa ikikabili suala la ulevi na mafadhaiko miongoni mwa walimu kwa miaka kwa kuwa limeathiri utendakazi katika shule za umma. Tukio la hivi karibuni zaidi cha kujitia kitanzi cha mwalimu wa shule ya upili ya Kenya High jijini Nairobi. Mwili wake ulipatikana ukining’inia katika ngazi ya tenki ya maji shuleni humo mnamo Oktoba 2, 2024. Mwalimu mwingine wa shule ya upili huko Nyamira alijitia kitanzi Juni 6, 2024 baada ya kupoteza pesa katika mchezo wa kamari. Kabla ya hapo, mwalimu wa shule ya upili ya Senior Chief Musa Nyandusi – Kegati, Evans Onchari alijiua mnamo Februari 13, 2023. Katika barua aliyoacha, alisema hali mbaya ya afya ilimsukuma kusitisha maisha yake. IMETAFSIRIWA NA LABAAN SHABAAN
WATAALAMU wa kuhakiki ubora na viwango katika shule zilizo kaunti mbalimbali nchini wanamulikwa kwa utepetevu kazini. Maafisa hawa wanalaumiwa kwa mikasa ambayo imetokea katika taasisi za elimu. Wanaharakati wa masuala ya elimu kutoka Homa Bay wanataka Wizara ya Elimu iwaweke kwenye mizani maafisa hawa wa uhakiki wa ubora na viwango (QASOs). Hii ni baada baadhi ya shule hizo kuorodheshwa kuwa si salama kwa wanafunzi. Kundi hili linadai maafisa wa elimu wanakula njama na baadhi ya shule ili kuripoti kuwa taasisi hizo ni salama licha ya kubainika kuna hatari. Serikali iliamuru vitengo vya mabweni vifungwe kwenye shule za msingi 348 kote nchini. Hatua hii ilichochewa na ripoti za shule kutofikia viwango vya usalama vinavyohitajiwa. Mshirikishi wa Shirika la Elimu la Kaunti ya Homa Bay Julius Omuga alisema maafisa wa uhakiki wa ubora katika kaunti zilizoathiriwa walifeli kutekeleza majukumu yao. Bw Omuga anaarifu maafisa hawa wanafaa kubaini matatizo hata kabla ya ripoti kutolewa. “Ni kazi ya maafisa wa utathmini wa ubora kuhakikisha viwango vya juu vinadumishwa. Sehemu ya wajibu wao ni kuangazia usalama wa wanafunzi,” akasema. Amri ya kufungwa kwa shule ilitolewa baada ya mkasa wa moto kukumba shule ya Hillside Endarasha Academy katika Kaunti ya Nyeri mnamo Septemba 6, 2024. Mkasa huo ulijiri usiku wa manane na kuua wavulana 21 na kujeruhi wengine. Hapo ndipo wizara ya elimu ikaamua kukagua shule ili kutathmini iwapo wasimamizi wamefuata viwango vya usalama kwa mujibu wa sheria. Bw Omuga ameshikilia kuwa kusingekuwa na haja ya utathmini iwapo maafisa wa uhakiki wa viwango wangefanya kazi yao ipasavyo. “Iwapo wangekuwa kazini, wangetambua makosa katika baadhi ya shule na kutoa mapendekezo yanayofaa,” akatilia mkazo. Ripoti ya ukaguzi ilipendekeza kufungwa kwa shule zilizokiuka kanuni kupita kiasi. Kulingana na Bw Omuga, shule hizi hazikufaa kufungwa. Wizara ya Elimu inawahitaji maafisa wa kupima ubora kuhakikisha shule zina vifaa vya kuwezesha mazingira mazuri ya masomo. Maafisa hawa wanaelekezwa kubuni na kutekeleza sera zinazohusiana na ubora pamoja na kutoa ripoti ya walichoshuhudia kwa washikadau husika. Bw Omuga amesema maafisa hawa wanafaa kuwajibika na kutoa tahadhari mapema. “Ina maana walifeli katika kufanya kazi ipasavyo. Hatua inafaa kuchukuliwa dhidi yao,” akasisitiza. IMETAFSIRIWA NA LABAAN SHABAAN

DAR ES SALAAM; MWANAFUNZI wa fani ya mapishi kutoka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VETA) Chang’ombe,…

Na Nora Damian, Mtanzania Digital Wakati Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) kikiweka malengo ya kufikia wahitimu 13,000 ifikapo mwaka 2029 kimesema kinajivunia asilimia 95 ya wahitimu wake wanapata ajira ndani na nje ya nchi. Akizungumza Desemba 5,2024 na waandishi wa habari wakati wa mahafali ya 18 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Profesa Evaristo […]
RAIS William Ruto jana alivitaka vyuo vikuu viwaruhusu wanafunzi walio na malimbikizi ya karo kufanya mitihani ya muhula huku akikiri kwamba vyuo vikuu vingi vinatatizika kifedha. Huku akiahidi kujitolea kwa serikali kusaidia vyuo vikuu kutimiza wajibu wao wa kifedha, Rais Ruto alihusisha masaibu ya kifedha yanayovikabili vyuo vingi na kulimbikizwa kwa madeni na usumbufu uliosababishwa na mpito wa muundo mpya wa ufadhili wa elimu ya juu. "Tunapopitia mabadiliko yaliyoletwa na muundo wa ufadhili wa elimu ya juu unaozingatia wanafunzi, nahimiza vyuo vikuu kuwa na subira na kuelewana na wanafunzi. Moyo wa kuzingatia binadamu ni muhimu hasa ikizingatiwa changamoto ya ziada inayoletwa na kesi ambayo inaweza kuvuruga utekelezaji wa muundo. Kwa hivyo, natoa wito kwa vyuo vikuu viwaruhusu wanafunzi kufanya mitihani yao ya mwisho wa muhula huku vikisubiri kurejelewa kwa malipo kamili pindi tutakapopata mwelekeo kuhusu suala hilo,” akasema akiwa Machakos mjini. Rais Ruto alizungumza wakati alipoongoza mahafali ya Chuo Kikuu cha Scott Christian mjini Machakos. Makumi ya vijana walihitimu vyeti, stashahada na shahada baada ya kumaliza kozi za kilimo biashara, thiolojia, fiziolojia ya ushauri nasaha, usimamizi wa biashara na teknolojia ya habari na mawasiliano katika chuo hicho kinachohusishwa na AIC. Rais Ruto alifichua kuwa baadhi ya vyuo vikuu vinakabiliwa na tishio la kufungwa kutokana na madeni makubwa. “Leo, serikali ya Kenya inadaiwa na chuo hiki zaidi ya Sh 460 milioni,” alisema. "Najua hii imesababisha hasara kubwa kwa chuo kikuu hiki. Ndio maana nilichukua jukumu la kusuluhisha changamoto ambazo zilitatiza mfumo huo wa zamani. Mfumo wa zamani karibu ufanye vyuo vingi vifungwe. Ninafahamu kuwa chuo kikuu hiki kilifungwa kwa muda wa miezi michache. Na haikuwa sawa kwa sababu tulihusika kwa kutolipa deni kubwa la Sh 460 milioni tunalodaiwa na chuo hiki,” alisema. IMETAFSIRIWA NA BENSON MATHEKA

JUKWAA la Wanawake Mkoa wa Mtwara (JUWAM) limeendelea kutoa elimu kwa wanawake zaidi ya 200 kuhusu masuala mbalimbali…

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, amepongeza Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT)…

DESEMBA 9, 2024 Watanzania wanaadhimisha Miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika huku Tanzania ikifaidi matunda lukuki ya uhuru…

WANAFUNZI nchini watakiwa kutumia elimu wanayopata vyuoni na vipawa walivyonavyo kujiajiri. Hayo yamesemwa na Naibu Mkuu wa Chuo…
MAADILI ya kitaifa na kanuni za utawala kama vile uzalendo, umoja wa kitaifa, ugatuzi wa mamlaka na utawala wa sheria zinaweza kuanza kufundishwa shuleni hivi karibuni ikiwa Bunge litaidhinisha Mswada unaopendekezwa kuwa sheria. Rasimu ya Mswada Marekebisho ya Sheria za Elimu wa 2024 unalenga kurekebisha Sheria mbalimbali za elimu ili kuanzisha sayansi ya taifa kama somo la kutahiniwa kuanzia elimu ya msingi hadi elimu ya juu kama sehemu ya kuimarisha maadili ya kitaifa kwa wanafunzi mapema maishani. Mswada huo unaofadhiliwa na Mbunge wa Suba Kusini Caroli Omondi unalenga kukuza maadili na kanuni za kitaifa kama ilivyoainishwa katika Kifungu cha 10 cha katiba. "Lengo kuu la Mswada huu ni kufanyia marekebisho Sheria ya Vyuo Vikuu, 2012, Sheria ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi, 2013, Sheria ya Elimu ya Msingi, 2013 na Taasisi ya Ukuzaji Mtaala ya Kenya, 2013," unasema Mswada huo. Kwa mujibu wa ibara ya 10 ya katiba, misingi ya utawala ni pamoja na uzalendo, umoja wa kitaifa, ugatuzi wa mamlaka, utawala wa sheria na demokrasia. Pia inajumuisha utu wa binadamu, usawa, haki ya kijamii, ushirikishwaji, haki za binadamu, kutobaguliwa na ulinzi wa waliotengwa. Zaidi ya hayo, Ibara ya 10 pia inajumuisha utawala bora, uadilifu, uwajibikaji na maendeleo endelevu. Akitetea Mswada huo mbele ya kamati ya Bajeti na Matumizi, Bw Omondi alisema nchi kama vile Singapore na Uswizi ambazo zimejumuisha masomo kama hayo katika mtaala wao zina kiwango cha chini cha ufisadi, zina uwiano zaidi, na zina maendeleo ya juu kiuchumi. “Pendekezo linalenga kuinua maadili na kanuni hizi kuwa mtaala ambao utafunzwa katika viwango mbalimbali vya mfumo wetu wa elimu. Ukiangalia mashirika yote, nchi ambazo hazina elimu ya aina hii zina matatizo mengi. Hili ndilo litakalofanikisha vita vyetu dhidi ya ufisadi, vita vyetu dhidi ya ukabila, vita vyetu dhidi ya usimamizi mbovu wa kiuchumi, na kimsingi kuunda taifa moja lililojengwa juu ya maadili haya,” Bw Omondi alisema. Alisema utekelezaji wa pendekezo hilo hautakuwa ghali kwa walipa ushuru akisema faida zinazidi gharama. IMETAFSIRIWA NA BENSON MATHEKA

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Mwajiri atawajibika kutoa msaada wa elimu kwa watoto wa wafanyakazi wake wanne wenye umri kati ya miaka 3 hadi 22 (ikiwa wako shule/chuo) kwa malipo ya Sh milioni 2.5 kwa kila mmoja mwanzoni mwa mwaka.

CHUO Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas) kimesema kupitia mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi…
MAHAKAMA Kuu jijini Eldoret imempata na hatia mshukiwa mkuu wa mauaji ya mwanaharakati wa LGBT. Mahakama ilimpata Jackton Odhiambo, mpiga picha wa kujitegemea na hatia ya mauaji ya Edwin Kiptoo, almaarufu Chiloba. Mnamo Jumatano Jaji Reuben Nyakundi alitoa uamuzi wake mwaka mmoja tu baada ya mauaji hayo ya kutisha, ambayo yalizua hisia mesto kote duniani. Akitoa uamuzi wake Jaji Reuben Nyakundi alisema mshukiwa huyo alikuwa mtu wa mwisho kuonekana na marehemu ambaye alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Eldoret kabla ya mwili wake uliokuwa umeharibika kupatikana siku sita baadaye ukiwa umetupwa kando ya barabara katika Kaunti ya Uasin Gishu.. Jaji Reuben Nyakundi alisema atahukumu mshtakiwa mnamo Decemba 16, 2024. Bw Odhimabo alishtakiwa kwa kumuua Chiloba aliyekuwa akisomea shahada ya Mavazi, Mitindo na Ubunifu katika chuo cha kikuu cha Eldoret kaunti ya Uasin Gishu. Alikana kumuua Chiloba ambaye anasemekana kuwa rafikiye wa chanda na pete kati ya Desemba 31, 2022 na Januari 3, 2023, katika nyumba za makazi za Noble Breeze Apartments eneo la Chebisaas, kaunti ndogo ya Moiben. Mwili wa marehemu uligunduliwa kwenye sanduku la chuma kando ya barabara ya Kipkenyo-Kaptinga katika Kaunti Ndogo ya Kapseret mnamo Januari 3,2023. Jaji alisema kuwa Odhiambo alimdhulumu Chiloba licha ya kuwa alimtaja kuwa rafiki yake wa karibu kabla ya kupanga njama ya kifo chake ambacho alisema kilikuwa cha kikatili katika nyumba ambayo walikuwa wakiishi pamoja. Marehemu alikuwa na alama mikononi mwake ambazo ziliashiria kuwa alijaribu kujikinga akishambuliwa. Jaji alitilia mkazo kuwa ushahidi uliowasilsihwa mahamanani ulithibitisha kuwa Odhiambo alimuua Chiloba.

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema Mfuko wa Ubunifu wa Samia, umelenga kuwezesha wabunifu…

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VETA), imewataka mama na baba lishe kujiendeleza katika fani ya mapishi…

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Daniel Mushi amepokea Vyuo kumi vya Ufundi Stadi…

Na Safina Sarwatt, Kilimanjaro Wanafunzi 68 wa kike katika Shule ya Sekondari ya TPC mkoani Kilimanjaro wamepata afueni kubwa baada ya kiwanda cha sukari cha TPC kukamilisha ujenzi wa bweni jipya. Hatua hii imetatua changamoto ya kutembea umbali wa kilomita 20 kwenda na kurudi shuleni kila siku, hali iliyokuwa ikihatarisha usalama wao na kuathiri masomo. […]

Mtoto anayesoma Darasa la Tatu katika shule ya Msingi Kasota (9) Mkazi wa kijiji cha kasota Kata ya Bugulula Halmashauri ya wilaya ya Geita Mkoani humo amejeruhiwa kwa kumwagiwa mafuta ya Petrol na kuwashiwa moto sehemu mbalimbali za mwili wake na Mama yake Mzazi kwa kosa la kuiba Pesa. Akizungumza na Millardayo Siwema Kulwa ambaye […] The post Mtoto amwagiwa Petroli na kuchomwa moto kisa kuiba 800 first appeared on Millard Ayo.

WADAU mbalimbali wanaofanya shughuli za kupinga ukatili wa kijinsia mkoani Mtwara wamesema, wanaendelea kutoa elimu kwa jamii na…
WIZARA ya Elimu inaomba Wakenya watoe maoni yao kuhusu mfumo mpya wa ufadhili wa elimu vyuoni. Wakenya wanatakiwa kupendekeza njia ya kuboresha mfumo huo ambao umeibua utata tangu uanzishwe. Katibu wa Idara ya Elimu ya Vyuo na Utafiti Dkt Beatrice Inyangala amesema kamati inayokusanya maoni iko tayari kuwasikiliza wananchi. “Serikali imejitolea kuwapa wanafunzi elimu nafuu na inayofaa wakati wote. Ni kwa sababu hii kamati iliundwa kuangazia masuala yaliyoibuliwa kuhusiana na mfumo wa ufadhili wa elimu vyuoni,” akasema. Kulingana na Wizara ya Elimu, mfumo mpya unahakikisha kuwa kila mwanafunzi anasaidiwa kwa kutumia kigezo cha uhitaji kutegemea na mshahara wa familia. Kuliibuka cheche kali na maandamano kutoka kwa Wakenya baada ya mfumo wa ufadhili kuwaweka wanafunzi katika kundi lisilofaa huku wengine wakiteta walipokea msaada mdogo zaidi kuliko waliotarajia. Ilibidi serikali iunde kamati ya kukusanya maoni na kupendekeza marekebisho. Jopo hilo linajumuisha viongozi wa wanafunzi, makamu chansela wa vyuo, wahadhiri na wataalamu wengine pamoja na wananchi wa kawaida. “Hii ni serikali ambayo husikiliza na tumewasikia. Tutaendelea kuwasikiliza,” akasema Dkt Inyangala. Katibu huyu amesema malalamishi ya wanafunzi yanaweza kutumwa kwa wakuu wa vyuo na viongozi wa wanafunzi. “Tunategemea mawazo yenu ya ubunifu kuboresha mfumo wa ufadhili ili ukithi mahitaji ya kila mmoja,” alisema mnamo Ijumaa alipohudhuria hafla ya kufuzu katika Chuo Kikuu cha Tom Mboya mjini Homa Bay. Alitetea mfumo huo akisema ulianzishwa kusaidia wanafunzi na wazazi kutegemea hali za kiuchumi za familia. “Lengo lake lilikuwa kusambaza fedha za kutosha kwa vyuo vikuu kuimarisha viwango vya elimu,” akaongeza akisema mfumo huo ulitekelezwa kikamilifu katika mwaka wa kwanza kabla ya malalamishi kuibuka. Mfumo huu ulianzishwa mnamo Mei 3, 2023 na umekumbwa na pingamizi baada ya wanafunzi wengi kutengewa migao midogo. Utaratibu wa ufadhili kwa wanafunzi wa vyuo unahusisha mseto wa ufadhili kutoka kwa serikali, mikopo na karo. Rais William Ruto alibuni kamati ya wanachama 129 mnamo Septemba 16, 2024 kupiga msasa mfumo huo kwa kipindi cha angalau wiki nane. Imetafsiriwa na Labaan Shabaan

BARAZA la Mtihani Tanzania NECTA limepanda miti ,zaidi ya 2000 katika shule tano za msingi katika Jiji la…
CHAMA cha Walimu wa Shule za Upili na Vyuo vya Kadri (KUPPET) tawi la Kisii kimekashifu hatua ya Baraza la Mitihani ya Kitaifa nchini (KNEC) kwa kuwazuia baadhi ya walimu waliokuwa wanajiandaa kusahihisha mitihani ya kitaifa ya shule za sekondari (KCSE) mwaka huu wasihusike na zoezi hilo. Katibu Mtendaji wa KUPPET eneo la Kisii Joseph Abincha amedai kuwa agizo la KNEC linaenda kinyume na kanuni za kimataifa za leba. Akizungumza katika hafla ya mazishi ya mmoja wa wanachama eneo la Bomachoge Borabu, Bw Abincha aliomba Waziri wa Elimu Julius Migos Ogamba atathmini uamuzi wa KNEC. “Kwamba kuna shule zinazoshukiwa kuhusika katika wizi wa mitihani, haiwezekani walimu waliokuwa nyumbani wakati wa mitihani waadhibiwe,” akasema Bw Abincha. “Walimu hawa walikuwa wanangoja mwezi Desemba ufike ili waanze kusahihisha mitihani hiyo. Ninamwomba waziri wa elimu akabili KNEC na kubadilisha uamuzi huu,” akaongeza. Baraza la mitihani lilichukua hatua hii inayoibua mzozo mkali na walimu baada ya shule wanakofunzia walimu hao huko Kisii kuripotiwa kuwa na visa vya udanganyifu katika mitihani iliyokamilika juma lililopita. Makumi ya visa vya udanyanyifu wa mitihani viliripotiwa katika kipindi cha mwezi mmoja wa mitihani ya kila mwaka ya KCSE. Mnamo Novemba 22, walimu wanne wa shule ya upili ya Bobamba iliyoko Gucha, Kaunti ya Kisii, walitiwa mbaroni kwa kuhusishwa na wizi. Kabla ya hapo, walimu 13 walikamatwa kwa tuhuma sawia katika shule ya sekondari ya Nyamninia, Kaunti ndogo ya Gem-Yala mnamo Novemba 11 na kufikishwa kizimbani.

WATU 23 wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi la Shule ya Msingi Salem kugongana na gari la Jeshi la…

NAIBU Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Vijana Mkoa wa Ruvuma (CCM), Judith Kapinga ameahidi kutoa…

Naibu Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Vijana Mkoa wa Ruvuma (CCM), Mhe.Judith Kapinga ameahidi kutoa kompyuta 139 katika Shule za Msingi 139 zilizopo Halmashauri ya wilaya ya Mbinga Vijijini ili kuchochea kasi ya ukuaji wa Elimu katika wilaya hiyo. Mhe. Kapinga ametoa ahadi hiyo Novemba 28, 2024 wakati wa hafla ya uwekaji […] The post Shule za msingi 139 Mbinga kupewa kompyuta first appeared on Millard Ayo.
MJUKUU wa aliyekuwa Rais Daniel Moi, Collins Kibet, amelegeza msimamo wake kuhusu malezi ya watoto wake na kupendekeza hatua za kuhakikisha watoto hao wananufaika na mali ya familia yake. Hii inafuatia mzozo wa muda mrefu wa kisheria kuhusu madai yake ya kupuuza majukumu yake kama mzazi. Bw Kibet ambaye anakabiliwa na kesi ya kutotii amri ya mahakama iliyotolewa Juni 2022, aliwasilisha mapendekezo Novemba 27 ya kuwatunza watoto hao wawili na akaeleza nia yake ya kuwatambulisha watoto hao, ili wanufaike na baadhi ya manufaa anayostahili kutokana na uhusiano wake na familia ya Moi. Ameahidi kuwasajili katika Shule maarufu ya Kabarak na kulipia gharama zao za matibabu kupitia Kituo cha Huduma za Afya cha Kabarak. Mjukuu huyo wa Moi anataka pia aruhusiwe kuwaona watoto pamoja na kuwa nao wakati wa likizo za shule. “Mshtakiwa atahakikisha watoto wanasajiliwa katika Shule ya Kabarak kwa elimu yao. Atashughulikia mahitaji ya matibabu ya watoto kupitia Kituo cha Huduma za Afya cha Kabarak na wazazi wote wawili wawe na uwezo wa kuwafikia watoto wakati wa likizo za shule,” akasema Bw Kibet kwenye mawasilisho mahakamani. Bw Kibet pia anataka mama wa watoto hao Gladys Jeruto Tagi, kudumisha malezi halisi ya watoto. Anapendekeza wazazi wote wawili wachangie gharama za chakula, mavazi na burudani wanapokuwa na watoto. Haya yanajiri baada ya mahakama kumwita Bw Kibet aeleze ni kwa nini asiadhibiwe kwa kukosa kutii amri ya kumtaka kutoa Sh 1.6 milioni kila mwaka kwa mahitaji ya watoto wake, ikiwa ni pamoja na elimu, matibabu na burudani. Maagizo hayo yalitolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Bw Benjamin Limo, baada ya Bi Tagi kumshutumu Bw Kibet kwa kupuuza majukumu yake kama mzazi. Mzozo huo uliongezeka na kusababisha Bw Kibet kukamatwa na kufungwa jela kwa wiki moja mnamo Septemba. Hukumu hiyo iliondolewa baadaye. Katika utetezi wake, Bw Kibet ambaye ni mwana wa Jonathan Toroitich, alijitaja kuwa maskini na anayekumbwa na msongo wa mawazo.Alisema hana kazi, hana mahali pa kuishi na anategemea wasamaria wema. Alisema matatizo yake yalianza baada ya kupoteza watu wa karibu wa familia yake akiwemo mama yake, baba yake, babu na shangazi yake ambao walikuwa wakimjali. Hakimu Mwandamizi, Bw Kipkurui Kibet, alimwagiza Bi Tagi kujibu ombi la Kibet kabla ya kesi hiyo kutajwa Januari 15, 2025. IMETAFSIRIWA NA BENSON MATHEKA
Mwanangu nakupigia, ni mamako kijijini, Sababu nakuambia, mambo si mema nyumbani, Nasema mwenzio dia, karudi tena sokoni! Jamani rudi nyumbani, mwanangu unagongewa! Ukiwa huko Malindi, maliyo yashangiliwa, Ajapo leo Muhindi,asaliyo ajigawa, Nimeona mengi kundi,mamako nimepagawa! Jamani rudi nyumbani, mwanangu unagongewa! Unapotua usiku, kwake naye ni mchana, Amejigeuza kuku, chumbani hatuwi tena, Ninayoyaona huku,mwanangu yasinya sana, Jamani rudi nyumbani, mwanangu unagongewa! Kugongewa ni lazima, lakini hino mezidi, Kama mama yaniuma,mkeo ndiye hasidi, Mwana tena ninasema,usinywe hino likwidi, Jamani rudi nyumbani, mwanangu unagongewa! Inazima yangu simu,yabidi nikome miye, Mwanangu haya fahamu,mke wako tena siye, Tayari anayo sumu,mtazame tena yeye, Jamani rudi nyumbani, mwanangu unagongewa! DOMIANO ADIBA ONYANGO. MALENGA ADIBA JINA KUBWA. BUDALANGI, BUSIA. Mirumbe nimehitimu! Naanza Bismillahi, kwa jina lake Jalia, Alhamdulilahi, siku leo mewadia, Sisi sote twafurahi, Rabana katujalia Nashukuru Mkawini, Mirumbe nimehitimu! Chereko leo chereko, Mirumbe natabasamu, Chereko najipa heko, dua naitakadamu, Nachanua kwa kicheko, Mirumbe nimehitimu, Nashukuru Maulana, Mirumbe nimehitimu! Kila refu lina ncha, japo elimu bahari, Kwa jino hata ukucha, nimekua jemedari, Mapozi napiga picha, kumbukumbu ya safari, Nashukuru Rahmani, Mirumbe nimehitimu! Nawashukuru wazazi, ndugu zangu na jamaa, Kujituma waziwazi, mnione nikipaa, Mola awape mbawazi, hakika mlinifaa, Nashukuru Maulana, Mirumbe nimehitimu! Nanyi siwaweki kando, wahadhiri wajanjuzi, Somo lenu kama jando, limevuvia ujuzi, Wino huno wa upendo, na thawabu za Mwenyezi, Namshukuru Wadudi, Mirumbe nimehitimu! Tamati nakata wino, kuyamaliza muhali, Kichwa hadi kisigino, maleba yapamba mwili, Bendi zapigwa piano, na mahadhi yakubali, Nashukuru Maulana, Babu miye nimefuzu! MIRUMBE P NICKSON "USTADHI BABU KIJANA" Siku itafika Siku moja itafika,milango itafunguka, Ije mvua ya masika,tuendako tutafika, Kudura zake Rabuka,juu yetu zitashuka, Hiyo ndiyo siku moja,tutakayofanikiwa. Siku moja itafika, njaa itatutoroka, Na vyakula vitalika, pia vinywaji kunyweka, Ima siku ikifika, hasidi taaibika, Hiyo ndiyo siku moja, tutakayofanikiwa. Siku moja itafika, lawama zitasitika, Na kero zitaondoka, kubezwa kutapunguka, Hiyo siku ikifika, kwa wazi tutasifika, Hiyo ndiyo siku moja, tutakayofanikiwa. Siku moja itafika, tutakuwa watukuka, Tukishapata baraka, kotekote tutawika, Mkono wake Rabuka, utatugusa hakika, Hiyo ndiyo siku moja, tutakayofanikiwa. Siku moja itafika, jua kutwa litawaka, Wenzi wetu watacheka, nyuso hazitavimbika, Majukwaa wataweka, ili sisi kusikika, Hiyo ndiyo siku moja, tutakayofanikiwa. Siku moja itafika, hata mwisho napofika, Hili nalo nahakika, walokesha kutucheka, Wakiijenga mipaka, kikomoni watafika Hiyo ndiyo siku moja, tutakayofanikiwa ABUTHWALIB LUKUNGU. ABU MALENGA MKALITUSI. CHUO KIKUU CHA RONGO, CHAWAKIRO. Wanawake wasidhulumiwe Malenga natanguliza, naomba yenu makini, Kuna jambo natangaza, kwenu nasema usoni, Kwa siku lajiongeza, lakuwa uhayawani, Wanawake wana haki, wasidhulumiwe kamwe. Mwasema eti hasira, zachochea hayo yote, Sasa ona ni hasara, zatupata sisi wote , Hofu wanayo hadhira, dhuruma maisha yote, Wanawake wana haki, wasidhulumiwe kamwe. Juzi 'likuwa Wanjiku, uovu akafanyiwa, Sitaki kuweka shuku, kifo kilikusudiwa, Watazamwa kama kuku, dhuruma ikidaiwa, Wanawake wana haki, wasidhulumiwe kamwe. Wanawake wana haki, si vita kila uchao, Tusiwalete hamaki, pia wao wana zao, Tusiwafanye fariki, na tunataka mazao, Wanawake wana haki, wasidhulumiwe kamwe. Kalamu yalia wino, naomba mimi kusita, Tuishi kwa upendano, ili tutoe matata, Tulete ushikamano, tusuluhishe kuteta, Wanawake wana haki, wasidhurumiwe kamwe. SAMUEL MUNGAI MALENGA MHENGA CHUO KIKUU CHA MURANG'A Heshima Watoto nawausia, ya muhimu kusikia, Yale nitawaambia, yanaweza kukufaa, Na heshima ukijua, kwa maisha utapaa, Ukiwa nayo heshima, mbali nayo utafika. Heshima nayo maana, popote ukitembea, Na Mungu anakuona, ni vizuri kusikia, Hivyo basi ni maana, heshima kuzingatia, Ukiwa nayo heshima, mbali nayo utafika. Ukiwa hata shuleni, heshimu wako mwalimu, Utapenya maishani, uwe mtu wa muhimu, Nawasaha sikizeni, usije kujilaumu, Ukiwa nayo heshima, mbali nayo utafika. Kumbuka pia nyumbani, kuzingatia heshima, Heshimu baba nyumbani, mkumbuke pia mama, Nawaambia jamani, usiweze kulalama, Ukiwa nayo heshima, mbali nayo utafika. Ni ujumbe nimesema, kwa watoto wasikie, Wasikie yale mema, heshima wazingatie, Nimefika kaditama, ujumbe uwafikie, Ukiwa nayo heshima, mbali nayo utafika. MALENGA KITONGOJINI, LIONEL ASENA VIDONYI TONGAREN, NDALU Naiokoa semia! Naomba mnisamehe ,nisowaitika simu, Si ati nipo sherehe,eti nimezima simu, Siwezi enda sherehe,wa mtihani msimu, Naiokoa semia,hilo nomba muelewe. Baba nawe mama yangu, nomba msiwe na hofu, Nipo tu chumbani mwangu, semia yanipa hofu, Mkononi simu yangu, nafungua pidihefu, Naiokoa semia,hilo nomba muelewe! Sitaki nije kufeli, nina magumu masomo, Ndio maana silali, siishiriki migomo, Taniruzuku Jalali ,nijapo fika kikomo, Naiokoa semia, hilo nomba muelewe. Msinitumie jumbe, sina muda wa kujibu, Nimejua nyie kumbe,ndinyi mnaniharibu, Na macho niyafumbue, nisiwaone karibu , Naiokoa semia, hilo nomba muelewe! Nijapo tua mzigo, natia dua kwa Mola, Mambo siwe mbagombago, niiitimishe makala, Sherehe zipa kisogo, ,nisijegeuka fala, Naiokoa semia, hilo nomba muelewe! JAPHETH NZOMO ZAO LA HEKIMA CHAKIMUT Sigara Namaliza mshahara,tena unanipa shida, Namaliza mshahara,kuzilipa zako ada, Namaliza mshahara,ninatoa ushuhuda, Sigara wewe sigara,I wapi yako faida? Unanipea madhara,mwilini kikuhifafadhi, Unanipea madhara,yakunifisha maradhi , Unazidisha madhara,yakunishushia hadhi, Sigara wewe sigara,niipi yako faida? Nikuvutapo sigara,unanipa kikohozi, Nikuvutapo sigara,yani dobera maozi, Nikuvutapo sigara,ninatukana wazazi, Sigara wewe sigara,niipi Sasa faida? Nikuvutapo sigara,ninawaza ubakaji, Nikuvutapo sigara,ninakuwa mkabaji, Nikuvutapo sigara,nafanya nisotaraji, Sigara wewe sigara, niipi yako faida? Umenifanya fukara, mavazi ni matambara, Umenifanya fukara,nadra Mimi kung’ara, Umenifanya fukara,kila kitu ni hasara, Sigara wewe sigara,niipi yako faida? Nenda ongea sigara, pamoya rafiki zako, Nenda ongea sigara, Bangi hadi na tobako, Nenda ongea sigara, wambe na gura mliko, sigara wewe sigara, Lau hauna faida ! Nakutaliki sigara, kwa kuwa huna msada , Nakutaliki sigara, nakana zako Ibada , Nakutaliki sigara, Tena sitakupa muda, Sigara wewe sigara, Lau hauna faida ! SAM MTSUFA MALENGA MCHANGA MALINDI Naisifu Longa Longa La ngomani likigonga,tu tayari kusikiza, Kiswahili tunabonga, Taifani twatukuza, Nyie kwetu ni wahenga kila neno mnaguz,a Kongoleni Longalonga, Kiswahili kutujuza. Kwenye lugha nyi bwenyenye, mwatukosha runingani, Mgusapo ndipo penye, twaipenda burudani, Hamfanyi kenyekenye, mambo yeni si utani, Kongoleni Longalonga,Kiswahili kutujuza. Kwenu upo ufanisi, Kiswahili kukitunza, Bila shaka tunahisi lugha yetu taikuza, Siwashike ibilisi,mkaanza kupuuza, Kongoleni Longalonga,Kiswahili kutujuza. Munene nipe nikupe,yatutoa bumbuwazi, Nawe Nuhu situtupe,shairini tenda kazi, Tawaganda kama kupe,nyie chai si andazi, Kongoleni Longalonga,Kiswahili kutujuza. Kikomoni natuia,na uchafu ninakoga, Samiati mechambua,kwetu sisi kuwa mboga, Nyoyo zetu twafungua,twasema bila yoga, Kongoleni Longalonga,Kiswahili kutujuza. CHARLES WAMBUA TAVETA
WANAFUNZI zaidi ya 20 kutoka familia maskini, mtaa wa Kawangware walifanya sherehe ya kufunzu kuashiria kukamilisha mtihani wa Kidato cha Nne baada ya kufadhiliwa miaka minne na Shirika la Every Girls Count (EGC). Kulingana na Shirika hilo, lilijitolea kusaidia wanafunzi hao ambao walishindwa kujiunga shule na hivyo kuwalipia karo katika shule za kutwa. Wanafunzi hao ambao walipata alama zaidi ya 350 katika mtihani wa darasa la nane, walipewa fursa ya kujiunga na shule za kutwa. Esther Achieng ambaye alijawa na furaha kwa kuvalia gauni, alisema aliepuka kurejea kijijini kuungana na mamake mzazi baada ya mfadhili kumtafutia nafasi na kujiunga na shule kutwa ya Upili ya Dagoretti. [caption id="attachment_163668" align="alignnone" width="2560"] Mkurugenzi wa Shirika la Every Girl Counts Emmanuel Katana akiongeza na wanafunzi 20 kutoka shule za kutwa wakiwa wamevalia magauni baada ya mtihani wa Kidato cha Nne 2024, KCSE. Picha|Fridah Okachi[/caption] “Nafurahi kukamilisha masomo yangu bila tatizo kama wenzangu mtaani. Nilipopata barua ya kujiunga na Kidato cha Kwanza nje ya Nairobi, niliona ndoto yangu imetimia. Wazazi walikuwa wameshindwa kulipa karo kwa sababu nilikuwa na ndugu wengine katika shule za upili na mmoja chuo kikuu,” alisema Achieng. Aliongeza kuwa wazazi wake walishindwa kulipa karo hiyo, babake ambaye ni bawabu akitegemea mshahara wa Sh12,000 pekee kukimu maisha ya familia, naye mamake akisalia mashambani. Kando na Achieng, Damaria Bocheni ambaye ni yatima alifahamu kuwa atarejeshwa mashambani na mjombaye pindi tu matokeo ya mtihani wa darasa la nane yalipotangazwa. Wasiwasi ulimjaa Bocheni kwa kuwa mjombaye alitegemea kibaru cha mjengo. “Nilifululiza hadi katika afisi za kusaidia wasichana. Mlezi wangu ndiye alikuwa mama na baba kwa wanawe na pia kwangu. Alinifahamisha hana uwezo wa kunisomesha licha ya kupata alama zaidi ya 300,” alidokeza Bocheni. Mkurugenzi wa Shirika la Every Girl Counts Bw Emmanuel Katana alisema walisherehekea wanafunzi hao ambao walipatwa na changamoto wakati mgumu wa Covid-19 (mwaka 2020-2021) na mafuriko wakiwa darasa la nane na pamoja na mafuriko katika mwaka 2024. [caption id="attachment_163669" align="alignnone" width="2560"] Mwazilishi wa Shirika la Every Girl Counts akizungumza katika sherehe ya kufunzu kwa wanafunzi hao wa Kidato cha Nne, KCSE. Picha|Fridah Okachi[/caption] “Naamini mtoto wa kike akipewa elimu, jamii inaimarika. Hapo mbeleni kulikuwa na shida ya kupelekwa shuleni. Hivi sasa, katika mtaa wa Kawangware mzazi akiwa na msichana na mvulana wanaofaa kujiunga na shule ya upili, iwapo ana uwezo wa kusomesha mtoto mmoja, mvulana atapewa kipaumbele,” alisema Bw Katana. Mwazilishi wa shirika la EGC, Bi Renee Cook alisema mradi huo unalenga kutoa fedha za elimu kwa ajili ya kuwasomesha mtoto wa kike hadi shule ya upili wanaoishi katika mazingira magumu jijini Nairobi. Bi Cook alisema kuwa japo elimu nchini Kenya ni tofauti na nchi ya Amerika, alitaka serikali kubadilisha mbinu na kuhakikisha kila mwanafunzi anajiunga na shule ya upili na kumaliza. “Najua kunaweza kuwa na upungufu wa bajeti kwa serikali kutoa chakula cha mchana kwa mwanafunzi, na hapo ndipo tunapoingia kusaidia familia na kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula.” Hadi kufikia sasa wanafunzi 80 kutoka mtaa huo wamepewa fursa ya kusoma katika shule ya upili, wanaofanya bora katika mtihani huo wa kitaifa wa kidato cha nne wakiendelea hadi chuo kikuu.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 27, 2024 ameshiriki katika zoezi la upigaji kura kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji, kwenye kituo cha Shule ya Msingi Nandagala, Ruangwa, Lindi Novemba 27, 2024. Akizungumza baada ya kupiga kura ambapo aliongozana na Mkewe Marry Majaliwa, Waziri Mkuu amewapongeza wakazi wa eneo hilo kujitokeza kwa […] The post Waziri Mkuu apiga kura kijijini kwake Nandagala first appeared on Millard Ayo.

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Wilson Mahera amewataka Maafisa Uthibiti Ubora wa Wilaya…

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania (HESLB) inakaribisha timu ya maofisa sita kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu na Masomo ya Zambia (HELSB) kwa ziara ya mafunzo ya siku tano. Katika ujumbe wake wa kuukaribisha Jumatatu, Novemba 25, 2024 katika Ofisi za HESLB jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji […] The post Dkt Bill Kiwia akutana na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu na Masomo ya Zambia (HESLB) first appeared on Millard Ayo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego ameipongeza Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) katika mpango wao wa kukuza somo la Hisabati kwa shule za Singida akisema kuwa ni mfano bora na ubunifu ambapo Taasisi hiyo inaufanya kukuza elimu hapa nchini. Ameyasema hayo hapo jana wakati wa Mahafali ya 22 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) […] The post RC Singida awapa tano Uhasibu first appeared on Millard Ayo.

WADAU wa mziki nchini wamesema upo umuhimu wa wasanii wa mziki nchini kupatiwa elimu ya uwekezaji ili iwasaidie kutumia vizuri vipato vyao vinavyotokana na kazi hiyo hasa pale shughuli zao hizo zinapofikia ukomo. Walitoa kauli hiyo jana Dar es Salaam, katika hafla iliyowakutanisha wasanii hao kwa ajili ya kuwapatia elimu ya namna ya kutumia […] The post Walichokifanya ‘’Mdundo’ wadau wa muziki wafunguka “elimu itolewe, vipato viongezeke” first appeared on Millard Ayo.

Katika mahafali ya 16 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa yaliyoongozwa na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar…
NI pigo kwa baadhi ya walimu watahini nchini baada ya Baraza la kitaifa la mitihani nchini (KNEC) kuwatumia jumbe za kuwataka kutoshiriki zoezi la kusahihisha mitihani. Walimu hao hawakuelezwa sababu ya KNEC kuwatumia jumbe hizo wiki hii licha ya wao kupokea barua za mwaliko hapo awali. Taifa Leo imebaini kwamba walimu wote waliopokea jumbe za KNEC za kutohudhuria zoezi la usahihishaji ni wale ambao shule zao zilipatikana kuwa na dosari fulani wakati mitihani ya KCSE ilipokuwa ikiendelea. Hatua ya KNEC imezua tumbojoto miongoni mwa walimu wakuu wa shule nyingi za sekondari nchini. Mtihani wa kidato cha nne ulikamilika rasmi Ijumaa Novemba 22, 2024. Serikali ilikuwa imeweka mipango kabambe kuzuia udanganyifu . Mojawapo ya mikakati hiyo ni karatasi za maswali kuwa na jina la mwanafunzi, nambari ya usajili ya mwanafunzi pamoja na jina na nambari fiche ya shule. Hatua hizi zilisaidia kupunguza usambazaji wa mitihani mtandaoni. Vile vile hatua ya walimu watahini kutoka shule zilizohusishwa na dosari kwa njia moja au nyingine kuzuiliwa kusahihisha ni njia moja Baraza la mitihani limechukua kuzuia kuendeleza udanganyifu. Usahihishaji wa mitihani ya KCSE unatarajiwa kuanza rasmi juma lijalo.

KIASI cha Sh bilioni 26 kinatarajia kutumika kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi…
UTANYIMWA haki ya kulea mtoto wako iwapo wewe ni mraibu wa dawa za kulevya na ikithibitisha una mazoea ya kuwanyanyasa, sheria ya watoto inasema. Kulingana na sheria hiyo,watoto walio na umri wa chini ya miaka 10, ni mama zao wanaopatiwa haki ya malezi isipokuwa kama imethibitishwa kuwa hawezi kuwalea kutokana na masuala kama vile unyanyasaji, kuwatelekeza, wana ugonjwa wa akili usiotibika, au ni waraibu wa dawa za kulevya. Nchini Kenya, sheria kuhusu malezi ya mtoto zinapatikana katika Sheria ya Watoto ya 2022, ambayo inabainisha haki na wajibu wa wazazi, walezi, na serikali kuhusiana na watoto. Masuala ya malezi ya mtoto mara nyingi hutokea wazazi wanapotengana au kuachana. Sheria nchini Kenya inatambua kwamba maslahi ya mtoto ni muhimu katika uamuzi wowote ambao anahusika. Wakati wa kufanya uamuzi kuhusu ni nani anapaswa kuishi na kumlea mtoto, mahakama huzingatia mambo mbalimbali hasa umri wa mtoto, afya yake na na uwezo wa mzazi wa kukidhi mahitaji ya mtoto. Katika baadhi ya matukio, mtoto anaweza kuruhusiwa kuamua anayetaka kuishi naye kati ya baba na mamake iwapo ana umri wa kutosha. Katika sheria, malezi ya mtoto ni uhusiano kati ya mzazi au mlezi na mtoto. Sheria inafafanua haki na wajibu wa mzazi kufanya maamuzi kuhusu malezi ya mtoto. Inajikita kuhakikisha anaishi mahali pazuri, salama na anaweza kupata elimu Mahakama inaweza kugawanywa malezi ya mtoto kwa baba na mama wakitengana: Malezi ya pamoja yanamaanisha kwamba wazazi wote wawili wana haki ya kufanya maamuzi kuhusu maisha ya mtoto wao, malezi ya pekee yanamaanisha kwamba ni mzazi mmoja tu ndiye ana haki ya kufanya maamuzi kuhusu maisha ya mtoto wake. Kutwikwa jukumu la malezi ya mzazi mmoja, ina maana kwamba mzazi mmoja ataishi na mtoto na kuwa mlezi mkuu na mtoa maamuzi. Hata hivyo, asiyetwikwa jukumu hili, awe baba au mama, anaweza kupatiwa haki ya kumuona na kumtembelea mtoto mara kwa mara. Mahakama inaweza pia kuweka au kuidhinisha mpangilio maalum wa malezi ambapo wahusika, kupitia mpatanishi au wakili, wanakubaliana jinsi wanavyotaka kushiriki malezi. Ni muhimu kutambua kwamba maamuzi ya malezi yanaweza kurekebishwa ikiwa kuna mabadiliko makubwa katika hali zinazoathiri ustawi wa mtoto. Ni muhimu kusisitiza kuwa katika kuamua kuhusu malezi, mahakama huzingatia maslahi bora ya mtoto. Sheria ya Watoto, 2022 inatwika mahakama mamlaka ya kutoa haki ya kutunza watoto kulingana na ukweli na ushahidi uliopo ili kuhakikisha suluhu bora zaidi kwa maisha na usalama wa mtoto. Sababu nyingine ambayo inazingatiwa ni hali ya maisha ya kila mzazi na uwezo wao wa kuandaa mazingira ya nyumbani yenye utulivu kwa mtoto. Hii ni pamoja na mambo kama vile tabia ya mzazi na hali ya makazi ili kuepuka kumweka mtoto katika mazingira yanayoweza kumdhuru. Mahakama inaweza pia kuzingatia historia yoyote ya unyanyasaji au kutelekezwa na mzazi yeyote, pamoja na historia yoyote ya uhalifu. Sheria inayosimamia malezi ya mtoto nchini Kenya inatambua kwamba wazazi wote wawili wana haki sawa za malezi, lakini mahakama inaweza kutoa haki kwa mzazi mmoja iwapo mzazi mwingine atapatikana kuwa hafai au hawezi kuweka mazingira salama na thabiti kwa mtoto.

SHILINGI bilioni 26 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Kampasi…

Waziri mkuu wa Albania amesema huenda nchi hiyo ikafikiria kufanya “uamuzi mkali” wa kuzipiga marufuku kabisa TikTok na Snapchat kufuatia mauaji ya mwanafunzi wa shule ya msingi mwenye umri wa miaka 14 na mwanafunzi mwingine katika mji mkuu wa Tirana. Katika taarifa baada ya mkutano wa Baraza la Mawaziri, Edi Rama alisisitiza kwamba kifo cha […] The post Albania yajipanga kupiga marufuku kabisa TikTok na Snapchat first appeared on Millard Ayo.
ALIYEKUWA Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, ameibua mdahalo muhimu kuhusu nafasi ya lugha kwenye siasa za kinyang’anyiro cha Uenyekiti wa Tume ya Muungano wa Afrika (AUC). Ingawa Afrika ina ndimi nyingi, bara bado limegawanyika kwa vigezo na misingi ya lugha za watawala wa kikoloni. Kuna nchi zinazotumia Kiingereza (Anglofoni), Kifaransa (Frankofoni) na Kireno (Lusofoni). Akizungumza jijini Addis Ababa, Ethiopia mnamo Novemba 10,2024, Bw Odinga alisema, Afrika bado inatatizwa na chembechembe za ukoloni mamboleo unaoendelezwa na lugha za kigeni. Mataifa mengi ya Afrika bado yanatumia lugha za kikoloni kwa ajili ya mawasiliano, shughuli za kiuchumi na hata ufundishaji katika mifumo ya elimu. Hali hii ni bayana hasa ikizingatiwa kwamba uhuru wa Afrika yamkini ni wa ‘bendera’. Mifumo yetu ya kiuchumi, kiutawala na hata elimu imejengwa kwenye amara za kikoloni. Je, Afrika imefanya juhudi zozote za kimaksudi kuibomoa miundomsingi ya kikoloni – hasa kuhusiana na lugha? Jibu ni ndio. Mwandishi Ngugi wa Thiong’o, ambaye huziona lugha za kigeni kama nyenzo za kuimarisha ukoloni, ameshiriki sana uanaharakati wa kutetea lugha za kiasili – hasa Gikuyu na Kiswahili. Falsafa ya Ngugi ni kwamba: “Ikiwa unajua lugha zote ulimwenguni, na ukawa hujui lugha yako ya mama au lugha inayosheheni utamaduni wako, huo ni utumwa.” Katika kitabu chake – Moving the Centre: The Struggle for Cultural Freedoms (James Carrey, 1993), Ngugi anajishughulisha na suala la ‘uhamishaji wa kitovu sumbufu’ (problematic centre) kuwili. Kwanza, baina ya, na ndani ya mataifa.
WATAALAMU wa masuala ya lishe sasa wanasema kuwa ulaji wa mara kwa mara wa nyama chemsha una maadhara ya kiafya. Wataalamu hao sasa wanasema kuwa nyama ya ng'ombe iliyochemshwa inayopendwa na wengi ina kiwango kikubwa cha mafuta. Joy Ouma, mtaalamu wa lishe aliyesajiliwa katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan, anasema nyama ya ng'ombe, kwa jumla, ina viwango vya juu vya mafuta ambayo yanaweza kusababisha ongezeko la kolesterol. "Japo nyama ya ng'ombe ina protini na madini, wasiwasi hutokea inapotumiwa kupita kiasi, kwani nyama hiyo inapochemshwa, basi watu wanaikula sana," akasema mtaalamu Ouma. Kepha Nyanumba, mtaalamu wa lishe aliyeidhinishwa kutoka Nairobi, anaongeza kuwa mara nyingi watu hudharau madhara ya kiafya ya kula kiasi kikubwa cha nyama, bila kujali jinsi inavyopikwa. "Nyama ya ng'ombe ya kuchemsha inaweza kuonekana kama chaguo bora zaidi ikilinganishwa na kukaanga au kuchomwa, lakini bado ina kiasi kikubwa cha mafuta, hasa katika sehemu ndogo kama vile mbavu. Mafuta haya yanaweza kujilimbikiza mwilini baada ya muda na kuchangia kiwango cha juu cha kolesterol jambo ambalo huongeza hatari ya magonjwa ya moyo na mishipa ya damu,” anasema. Bi Ouma anaonya kwamba ulaji wa mara kwa mara wa nyama kama hiyo inaweza kuongeza kolesterol ambayo ni hatari sana kwa mwili. Viwango vya juu vya mafuta mwilini huongeza hatari ya ugonjwa wa moyo. "Watu wengi wanadhani kuwa nyama ya ng'ombe ya kuchemsha ni bora kwa sababu haijakaangwa, lakini kiwango cha mafuta kinabaki kuwa wasiwasi. Kula nyama ya ng'ombe mara kwa mara au kwa sehemu kubwa kunaweza kusababisha maadhara makubwa ya kiafya ya muda mrefu," anasema. Hatari nyingine iliyopuuzwa ni uwezekano wa kupata kuwa mfugo ulikuwa ukiugua kabla ya kuchinjwa kwani inaathiri watu walio na matatizo ya figo. Nyama ya ng'ombe ina protini nyingi, na ulaji wa vyakula vyenye protini nyingi kwa wingi unaweza kusumbua figo, na kufanya figo kufura au hata ugonjwa sugu wa figo. "Unapokula nyama ya ng'ombe kupita kiasi, figo zako hufanya kazi kwa muda wa ziada ili kuondoa sumu hizi, ambazo baada ya muda zinaweza kusababisha uharibifu, haswa kwa watu ambao tayari wana matatizo ya figo," asema Bi Ouma. Bw Nyanumba anaongeza kuwa wale walio na historia ya familia ya ugonjwa wa figo au matatizo mengine ya msingi wanapaswa kuwa waangalifu Zaidi. "Ulaji wa nyama mara kwa mara unaweza kuathiri utendakazi wa figo kwa watu ambao tayari wako katika hatari. Ni muhimu kula aina vingine vya chakula vilivyo nap rotini ili kuzuia ugonjwa wa figo," anasema. IMETAFSIRIWA NA WINNIE ONYANDO

Donald Trump alimteua Linda McMahon, Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa World Wrestling Entertainment [WWE], Jumanne kuongoza Idara ya Elimu. Akimuelezea McMahon kama “mtetezi mkali wa Haki za Wazazi,” Trump alisema katika taarifa yake: “Tutarudisha Elimu MAREKANI, na Linda ataongoza juhudi hizo.” McMahon ni mwenyekiti mwenza wa timu ya mpito ya Trump kabla ya kurejea kwake […] The post Trump amteua mwanzilishi wa ligi ya mieleka kuwa waziri wa Elimu first appeared on Millard Ayo.
ALIYEKUWA Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, ameibua mdahalo muhimu kuhusu nafasi ya lugha kwenye siasa za kinyang’anyiro cha Uenyekiti wa Tume ya Muungano wa Afrika (AUC). Ingawa Afrika ina ndimi nyingi, bara bado limegawanyika kwa vigezo na misingi ya lugha za watawala wa kikoloni. Kuna nchi zinazotumia Kiingereza (Anglofoni), Kifaransa (Frankofoni) na Kireno (Lusofoni). Akizungumza jijini Addis Ababa, Ethiopia mnamo Novemba 10,2024, Bw Odinga alisema, Afrika bado inatatizwa na chembechembe za ukoloni mamboleo unaoendelezwa na lugha za kigeni. Mataifa mengi ya Afrika bado yanatumia lugha za kikoloni kwa ajili ya mawasiliano, shughuli za kiuchumi na hata ufundishaji katika mifumo ya elimu. Hali hii ni bayana hasa ikizingatiwa kwamba uhuru wa Afrika yamkini ni wa ‘bendera’. Mifumo yetu ya kiuchumi, kiutawala na hata elimu imejengwa kwenye amara za kikoloni. Je, Afrika imefanya juhudi zozote za kimaksudi kuibomoa miundomsingi ya kikoloni – hasa kuhusiana na lugha? Jibu ni ndio. Mwandishi Ngugi wa Thiong’o, ambaye huziona lugha za kigeni kama nyenzo za kuimarisha ukoloni, ameshiriki sana uanaharakati wa kutetea lugha za kiasili – hasa Gikuyu na Kiswahili. Falsafa ya Ngugi ni kwamba: “Ikiwa unajua lugha zote ulimwenguni, na ukawa hujui lugha yako ya mama au lugha inayosheheni utamaduni wako, huo ni utumwa.” Katika kitabu chake – Moving the Centre: The Struggle for Cultural Freedoms (James Carrey, 1993), Ngugi anajishughulisha na suala la ‘uhamishaji wa kitovu sumbufu’ (problematic centre) kuwili. Kwanza, baina ya, na ndani ya mataifa.
CHAMA cha Kitaifa cha Walimu (KNUT) kimeomba Tume ya Huduma kwa Walimu (TSC) kurejesha utambuzi wa Kaunti ya Kajiado kama eneo lenye mazingira magumu ya utendakazi. Hii itawawezesha walimu katika kaunti hiyo kulipwa marupurupu ya kuhudumu katika mazingira magumu sawa na wenzao wanaofanya kazi katika maeneo kame (ASAL). Akiongea alipohudhuria mkutano wa kila mwaka wa Knut tawi la Kajiado, Katibu Mkuu wa chama hicho Collins Oyuu alisema walimu wanaofundisha Kajiado wanapitia changamoto nyingi kutokana na mazingira magumu wanayofanyia kazi. “Kajiado ingali eneo lenye ugumu kwa wafanyakazi wakiwemo walimu. Lakini inasikitisha kuwa TSC iliondoa Kajiado kutoka orodha ya kaunti ambako mazingira ya utendakazi ni magumu,” akasema Bw Oyuu. Katibu huyo Mkuu pia aliilaumu TSC kuwa kukosa kuwatuma walimu wa kutosha katika maeneo kame, akisema hiyo inaathiri viwango vya elimu. Bw Oyuu aliitaka tume hiyo iajiri walimu zaidi kuwezesha kifikiwa kwa idadi hitajika ya walimu kwa mujibu wa viwango vilivyowekwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Elimu na Utamaduni (UNESCO). “Tunaitaka serikali iajiri walimu zaidi ili kupunguza kero ya uhaba wa walimu wa kutosha kote nchini. Inasikitisha kuwa katika baadhi ya shule mwalimu mmoja anawafunza watoto 70 badala ya wanafunzi 45, kulingana na viwango vya Unesco,” Bw Oyuu akasema. Katibu wa Knut katika Kaunti ya Kajiado Elie Korinko alisema shule zilizoko maeneo ya mijini zina walimu wengi kupita kiasi ilhali zile zilizoko mashambani zinakumbwa na uhaba mkubwa wa walimu. “TSC inafaa kudumisha usawa wakati wa usambazaji wa walimu. Shughuli hii haistahili kuyumbishwa kwa manufaa ya maeneo fulani pekee huku maeneo mengine yakiumia,” akasema. “Kwa hivyo, tunaitaka TSC kuendesha shughuli ya kutumwa kwa walimu kwa njia inayozingatia usawa na uwazi,” akaongeza. Mapema mwaka huu, TSC ilitekeleza mpango wa usawazishaji ili kutoa nafasi kwa makundi yaliyobaguliwa katika sekta ya elimu kupata haki. Waliofaidi ni walimu kutoka makabila madogo yaliyotengewa, wanaoishi na ulemavu na walimu kutoka maeneo yaliyosalia nyuma kimaendeleo. Aidha, kaunti nyingine zaidi zilijumuishwa kwenye orodha ya zile zenye mazingira magumu ya utendakazi.
Hujambo shangazi? Kuna tatizo limeingia katika ndoa yangu. Mume wangu haniamini. Mara nyingi nisipokuwa nyumbani hufikiria nina mwanamume mwingine. Sijawahi kwenda nje ya ndoa na tabia yake hiyo inaniudhi sana. Nifanyeje? Mume wako anasumbuliwa na wivu. Hawezi kukufungia nyumbani ili usionekane na wanaume wengine. Endelea kumhakikishia uaminifu wako kwake. Hatimaye atathibitisha huna mambo mengine nje ya ndoa kisha atatulia. Nimempenda mubaba Nina umri wa miaka 18 na ninasoma katika shule ya upili. Nimependana na mwanaume wa miaka 35 na ameahidi kunioa. Je, ni makosa? Hayo ni makosa makubwa. Wewe bado ni mdogo sana, huna uwezo wa kuelewa mapenzi. Utaharibu maisha yako. Mwambie mwanaume huyo asubiri umalize masomo. Msupa ninayempenda anadai dume linalozuru kwake ni rafiki tu, ila siamini! Za kwako shangazi. Nampenda mwanamke jirani yangu na nimeona dalili kuwa yeye pia ananitaka. Lakini kuna mwanamume ambaye nimempata kwake mara kadhaa. Aliniambia ni rafiki tu lakini siamini. Nishauri. Ni jambo la kawaida kwa wanaume kadhaa kumtaka mwanamke mmoja. Mwanamke huyo ndiye ataamua ni nani anayemfaa kati yako na huyo mwanamume mwingine. Kama kweli unampenda, usife moyo. Anataka kurudi ila mimi sina nafasi yake tena moyoni Nilitofautiana na mpenzi wangu kuhusu mambo fulani na tukaachana. Tangu hapo amekuwa akinipigia simu akitaka turudiane na mimi sitaki. Naomba ushauri wako. Mwanamume huyo ameonyesha nia ya kufufua uhusiano wenu. Kama umeamua huwezi kurudiana naye, sidhani unahitaji ushauri wangu. Mwambie wazi kwamba humtaki ili aondoe mawazo yake kwako.

SERIKALI na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu wameombwa kuendelea kuboresha sekta ya elimu nchini ili kujenga nchi…
WAZIRI wa Elimu Julius Ogamba amesema serikali itakiokoa Chuo Kikuu cha Moi kisianguke. Waziri huyo amedokeza kuwa juhudi za kufufua taasisi hiyo ziko katika hatua za mwisho na hivi karibuni, watatangazia umma kuhusu hatua zilizochukuliwa ili kurejesha shughuli za masomo katika taasisi hiyo. Akizungumza alipokuwa akikagua jinsi mtihani wa KCSE ulivyokuwa ukiendelea Jumatatu, Novemba 18, 2024 baada ya kuzuru kaunti za Kisii na Nyamira, Bw Ogamba alisikitishwa na hali inayokikumba chuo hicho lakini akaeleza matumaini yake kuwa hivi karibuni taasisi hiyo itainuka. “Tumeweka mpango wa kuhakikisha kuwa tunaendeleza chuo hicho. Tumebuni mkakati wa kushughulikia masuala yanayokiathiri na tutawajuza mara tu mikakati hiyo itakapokamilika,” Bw Ogamba alisema. Mambo hayajawa sawa kwa taasisi hiyo yenye makao yake mjini Eldoret kwani imekuwa ikigonga vichwa vya habari katika siku za hivi karibuni kwa taarifa za kuvunja moyo. Chuo hicho kimelemewa na madeni, maamuzi mabaya ya kifedha na kiutawala, nguvu kazi isiyoweza kumudiwa, miradi potovu na mengine mengi. [caption id="attachment_163008" align="alignnone" width="300"] Waziri Julius Ogamba (kushoto) afurahia picha na walimu wakati wa kukagua mtihani wa KCSE kaunti za Kisii na Nyamira. Picha|Wycliffe Nyaberi[/caption] Ina madeni ya zaidi ya Sh8 bilioni na wahadhiri wako kwenye mgomo, wakipinga mishahara kucheleweshwa, kutotumwa kwa malipo ya mikopo, pensheni na makato mengine ya watu wengine. Wahadhiri hao wanataka kulipwa zaidi ya Sh8 bilioni, ikiwa ni pamoja na malimbikizo ya mishahara na fedha nyingine wanazodai kabla ya kurejea kazini. Juhudi za kumaliza mgomo huo zimefeli huku wahadhiri hao wakishutumu uongozi wa chuo kwa kutowajali. Kufuatia vuta nikuvute hiyo, wanafunzi ndio walioumia zaidi. Kwa sababu ya migomo isiyoisha ya wahadhiri hao, wanafunzi wanachukua miaka mingi kumaliza masomo yao katika muda unaostahili. [caption id="attachment_163009" align="alignnone" width="300"] Waziri Ogamba katika bohari la mtihani. Picha|Wycliffe Nyaberi[/caption] "Sio haki kwa wanafunzi kwenda chuo kikuu kwa mfano na kukaa kwa miaka tisa katika mchakato wa kufanya digrii zao. Si sawa na tunaenda kupata suluhu za muda mrefu na za kudumu kwa chuo hicho,” Bw Ogamba aliongeza. Kamati ya Elimu ya Bunge la Kitaifa, inayoongozwa na Mbunge wa Tinderet Julius Melly ilizuru taasisi hiyo hivi majuzi na kutaka usimamizi ya chuo hicho uvunjiliwe mbali. Kamati ilipendekeza uongozi wa taasisi hiyo uwekwe chini ya ushikilizi. Bw Ogamba alisema Wizara yake itaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha kuwa sekta ya elimu inaboreshwa. Alisema hilo litaanza kwa kuhakikisha wanakomesha utamaduni wa kufanya udanganyifu katika mitihani. Aliwataka maafisa wanaosimamia mtihani unaoendelea kutolegeza kamba kwani mtihani huo unakaribia kufika tamati baadaye wiki hii.

Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe mkoani Njombe Erasto Mpete ameagiza wamiliki na wasimamizi wa shule za kulea watoto (Day care) kuzingatia miongozo ya uanzishaji wa shule hizo ikiwa ni pamoja na majengo kuto kuwa na wapangaji wengine ili kuimarisha ulinzi wa watoto. Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wazazi kwenye mahafali ya kwanza […] The post Njombe TC wataka wazazi kuona umuhimu wa kupeleka watoto kwenye shule za malezi (Chekechea) first appeared on Millard Ayo.