
NSSF yafikisha elimu kwa wajasiriamali Tegeta, Kawe
DAR ES SALAAMM; Lengo la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kufikisha elimu ya hifadhi ya…
Category
Education policy, exam results and calendars, scholarships and opportunities for students, parents and teachers across the region.

DAR ES SALAAMM; Lengo la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kufikisha elimu ya hifadhi ya…

WAZAZI katika Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara wametakiwa kuona umuhimu wa elimu kwa watoto kwa…

DAR ES SALAAM: MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amewataka wakuu wa shule za sekondari wilayani humo…

Ni Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ambapo leo January 6, 2024 imewatangazia wanafunzi wa stashahada watakaodahiliwa mwezi Machi (March Intake) kwamba dirisha la maombi ya mikopo ya stashahada litafunguliwa kuanzia tarehe 15/01/2025 hadi tarehe 15/02/2025. Wanafunzi wanaotarajia kuomba mikopo katika maeneo matano ya kipaumbele na wanafunzi wengine wenye udahili (admission) […] The post Dirisha La Maombi Ya Mikopo Ya Stashahada Kwa ‘March Intake’ first appeared on Millard Ayo.

DAR-ES-SALAAM : KATIBU Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa, amependekeza kuwa wafanyabiashara…
WAZAZI wengi wanakubali kuwa watoto wao wanakosa usingizi usiku na kudhani hii ni sehemu tu ya changamoto za makuzi yao. Lakini huu ndio ukweli: usingizi mzuri ni lazima kwa mtoto na unawezekana kwa kila mmoja na kuupa kipaumbele kunaweza kubadilisha maisha ya familia. Wataalam wa afya ya watoto wanasema usingizi sio tu 'kupumzika.' Kwa watoto, ni hitaji la kibayolojia ambalo huchochea ukuaji, ukuaji wa ubongo na utulivu wa kihisia. Hata hivyo, nchini Kenya, usingizi haujadiliwi kama sehemu muhimu ya afya ya mtoto. Wazazi ni wepesi kushughulikia lishe, elimu, na mazoezi, lakini usingizi mara nyingi hukosa katika orodha ya mambo muhimu kwa mtoto.Ukweli ni kwamba mtoto anayepumzika vizuri ni mtoto mwenye afya njema, mwenye furaha na anayefanikiwa zaidi—na wazazi wanaotanguliza usingizi wa watoto wao wanaboresha maisha yao wenyewe pia. Miaka ya kwanza ya maisha ya mtoto huwa ya maendeleo ya haraka ya kimwili, ya utambuzi, na ya kihisia, ambayo mengi hutokea wakati wa usingizi. Homoni za ukuaji hutolewa, ubongo huunganisha kujifunza na kumbukumbu, na mfumo wa kinga huimarishwa. Usingizi duni huvuruga michakato hii, na kusababisha masuala kama vile kuchelewa kukua, kuyumba kihisia, na kupunguza uwezo wa kujifunza. Mbali na kuathiri afya ya watoto, kukosa usingizi wa kutosha kuna athari mbaya kwa familia. Watoto wanaochoka mara nyingi huwa na hasira na hawana ushirikiano. Hili linaweza kuleta msongo wa mawazo kwa wazazi, kulegeza uhusiano na hata kusababisha uchovu. Usingizi mbaya kwa watoto ni tatizo ambalo linahitaji kushughulikiwa. Nchini Kenya, familia nyingi hukumbana na changamoto za kipekee kuhusu suala la usingizi wa watoto. Kulala chumba kimoja ni jambo la kawaida, na desturi za kitamaduni zimejikita sana. Ingawa hali hizi zinaweza kufanya kazi kwa wengine, mara nyingi husababisha usumbufu wa kulala kwa watoto na wazazi. Changamoto moja kuu ni ukosefu wa habari za kuaminika kuhusu usingizi. Wazazi wengi kwanza kurejea kwa madaktari wao wa watoto ili kupata mwongozo, ndipo wanagundua kwamba usingizi wa watoto haufai kupuuzwa kila wakati. Ingawa madaktari wa watoto ni muhimu kwa afya ya mtoto kwa ujumla, mara nyingi hawatoi mikakati ya kina, ya kibinafsi ya kulala ambayo familia zinazotatizika zinahitaji. Wakiwa wamechanganyikiwa, mara nyingi wazazi hutafuta ushauri kwa marafiki au watu wa familia, lakini ni nadra sana vidokezo wanazopata kutatua tatizo. Kinachofaa kwa mtoto mmoja huenda kisifanye kazi kwa mwingine, na kuwaacha wazazi wakihisi wamepotea zaidi. Wengine hugeukia mtandao kwa majibu, lakini ushauri unaweza kuwa mwingi na unaokinzana. Je, unapaswa kulala pamoja na mtoto au kuhimiza uhuru? Kufunza mtoto kulala ni ukatili au ni muhimu? Unajuaje kama matatizo ya usingizi ya mtoto wako ni ya kawaida au ni ishara ya tatizo kubwa zaidi? Usingizi mzuri sio bahati - ni kuhusu kuunda hali zinazofaa. Wazazi wanaweza kuanza kwa kutanguliza usingizi kwa njia ile ile wanavyotanguliza ulaji bora au mafanikio ya kitaaluma. [caption id="attachment_158474" align="alignnone" width="500"] Watoto wakifurahia. Picha|Hisani[/caption] Hapa kuna hatua chache muhimu kutoka kwa wataalamu wa afya ya watoto: 1. Weka utaratibu thabiti wa wakati wa kulala: Watoto husitawi wanapotabiri. Utaratibu wa utulivu wa wakati wa kulala kama vile kuoga kwa maji yenye joto, kusoma kitabu, na muziki wa kutuliza husaidia kuashiria kwamba ni wakati wa kupumzika. 2. Weka muda wa kulala unaolingana na umri: Watoto wadogo wanahitaji muda wa kulala mapema, mara nyingi mapema kati ya kumi na mbili na nusu na saa moja na nusu jioni. Kuchelewa kulala kwa watoto kunaweza kusababisha uchovu kupita kiasi, na kuifanya iwe ngumu kwao kutulia. 3. Unda mazingira ya kirafiki: Nafasi ya kulala inapaswa kuwa giza, tulivu na baridi kiasi. 4. Punguza muda wa kutumia vifaa vya dijitali: Mwangaza wa buluu kutoka kwenye skrini hukandamiza melatonin, homoni inayokuza usingizi. Zima vifaa angalau saa moja kabla ya kulala. Licha ya jitihada zao, wazazi wengi hujikuta wakipata shida kutekeleza mabadiliko haya au kutatua changamoto za usingizi kama vile kuamka mara kwa mara usiku au kuamka mapema. Hapa ndipo wataalamu wa usingizi wa watoto wanahitajika.“Kama mshauri wa masuala ya usingizi, mimi huwasaidia wazazi kuelewa mahitaji ya kipekee ya mtoto wao kulala na kutengeneza suluhisho inayofaa ambayo ina manufaa kwa familia. Hii sio kuhusu kuweka ratiba ngumu. Badala yake, inahusu kuwawezesha wazazi kwa maarifa na zana za kuunda tabia nzuri za kulala,” asema Dkt Mwende Kimweli, mwanasaikolojia na mtaalam wa afya watoto. Wazazi wanapotafuta usaidizi wa kitaalamu, mara nyingi hupokea mwongozo ulio wazi, unaotegemea ushahidi.“Tofauti na mapendekezo yasiyoeleweka kutoka kwa marafiki au ushauri mwingi mtandaoni, kufanya kazi na daktari hutoa mbinu mahususi zinazozingatia umri wa mtoto wako, hali ya joto na changamoto mahususi,” asema. Nchini Kenya, ambapo rasilimali za kulala kwa watoto bado ni chache, usaidizi wa kitaalamu unaweza kubadilisha hali. Kwa kutafuta msaada, wazazi wanaweza kutoka katika hali ya kukosa usingizi hadi kwenye mazoea ya amani katika muda wa majuma machache. Dkt Kimweli anasema shule, wahudumu wa afya na watunga sera wanahitaji kutambua jukumu muhimu la usingizi katika ukuaji wa mtoto. Kuelimisha wazazi kuhusu usafi wa usingizi na kuwasaidia kwa rasilimali ili kuimarisha afya ya umma. “Kwa wazazi, ujumbe ni rahisi: usingizi mzuri sio anasa-ni jambo la lazima. Kwa kutanguliza usingizi, haumsaidii mtoto wako kukua tu—unampa zana za kustawi kimwili, kihisia na kiakili.
UHABA wa vitabu vya shule za msingi unashuhudiwa nchini, baadhi ya wamiliki wa maduka ya vitabu wakisema walipokea asilimia 60 pekee ya mahitaji yao. Mkurugenzi wa duka la vitabu la Kimji Devshi, mojawapo ya wasambazaji Kaunti ya Nyeri, Bw Khilan Shah, alisema uhaba huo unawaathiri zaidi wanafunzi wa PP1 hadi Gredi ya 4. Alieleza kwamba uhaba huo unachangiwa na wachapishaji waliokabidhiwa kandarasi na serikali ambao wamechelewesha uchapishaji. “Vitabu havipatikani. Mzazi anaagiza vitabu 10 kwa darasa moja lakini tunapata vinne pekee. Bei ya vitabu vilivyoko iko juu, na hali hii inawaumiza wazazi ambao tayari wanakabiliana na gharama kubwa ya maisha,” alisema. Katika maneo mengi wauzaji vitabu walisema vitabu vya Gredi ya Tisa vipo lakini wanakumbwa na changamoto kupata vitabu vya Gredi ya kwanza hadi sita. Katika kaunti ya Murang’a, Mwenyekiti wa Kamati ya Seneti kuhusu Elimu, Bw Joe Nyutu, alisema wazazi wanapaswa kupewa muda wa kununua vitabu vya Gredi ya Tisa. “Ni kweli kuwa kufikia Jumapili, vitabu havikuwa vinapatikana kwenye soko. Serikali ilikosa sera na imeshangaza wadau wote kutokana na uhaba huo,” alisema Bw Nyutu. Mzazi kutoka Murang’a, Bi Elizabeth Soliyo alisema baadhi ya vitabu vinapatikana kwa bei ghali. Mfanyabiashara, Bw Martin Thuo, alisema kuna mkanganyiko kuhusu orodha ya vitabu vilivyoidhinishwa. IMETAFSIRIWA NA FRIDAH OKACHI
WAZAZI walio na wanafunzi katika shule 349 ambazo zilizuiwa kuwa za bweni, wametakiwa kuwahamishia katika taasisi nyingine za masomo kabla ya shule kufunguliwa Jumanne wiki ijayo kutokana na masuala ya usalama. Wizara ya Elimu iliwataka wazazi hao kuhakikisha watoto wao wanajiunga na shule tofauti baada ya ukaguzi uliofanywa kufuatia mkasa wa moto ulioua wanafunzi 21 kutoka shule ya Hillside Endarasha Academy miezi minne iliyopita kufichua masuala ya usalama katika shule hizo 349. Ukaguzi ulibaini kuwa shule nyingi za msingi za bweni zinakabiliwa na changamoto za kiusalama na miundombinu ambazo zinahatarisha maisha ya wanafunzi. Jumla ya shule 2,974 zilifanyiwa tathmini, ambapo 1,415 zilikuwa za umma na 1,659 za kibinafsi. Msongamano katika mabweni ulikuwa wa kawaida shuleni. Nafasi kati ya vitanda katika shule nyingi ilikuwa chini ya mita 1.2 kinyume na Mwongozo wa Viwango vya Usalama kwa Shule nchini Kenya (2008). Shule chache hazikuwa na walinzi/ walezi wa mabweni ya wavulana. Katika baadhi ya shule, matroni walipewa majukumu katika mabweni ya wanafunzi wa kiume. Katibu wa Elimu ya Msingi Belio Kipsang alisema serikali haitalegeza msimamo kuhusu agizo la kupiga marufuku baadhi ya shule kuwa za bweni. Alisema wazazi wa shule ambazo hazikidhi viwango vya usalama lazima wawahamishe wanafunzi hao. "Tuliambia taasisi ambazo hazikuwa zimejitayarisha vya kutosha kuwa na bweni kuacha hadi wakati huo zitakapojitayarishwa ipasavyo. Na kila shule hizo 349 ilipewa ripoti ya kueleza ilichohitaji kufanya," alisema Dkt Kipsang. Katika mahojiano na Taifa Leo, Dkt Kipsang alisema maafisa wa Wizara ya Elimu wamekagua tena baadhi ya shule. “Shule yoyote ambayo imekidhi kiwango cha maandalizi itaruhusiwa kuendelea, lakini zile ambazo haziko tayari, tumewaambia wazazi watafute shule mbadala kwa watoto wao na tumewapa muda wa kutosha, karibu miezi miwili," alisema. Dkt Kipsang alisema maafisa wa wizara kwa sasa wanajumuisha data kuhusu ni shule ngapi za bweni ambazo bado hazijatimiza viwango vya usalama. "Tuna mkutano wa wakurugenzi wetu wote wa kaunti ndogo, kaunti na maeneo leo, tutaweza kujua hali yoyote inayohitaji umakini maalum," alisema. Haya yanajiri huku wazazi wakiendelea kulalamika kuhusu hatua hiyo wakisema itakuwa changamoto na gharama kubwa kununua sare mpya, na huduma nyinginezo. Hata hivyo, Mwenyekiti wa Chama cha Kitaifa ya Wazazi Silas Obuhatsa alilaumu wazazi kwa kukosa kulazimisha bodi za usimamizi kuzingatia viwango vya usalama kabla ya shule kufunguliwa tena. IMETAFSIRIWA NA BENSON MATHEKA
OPERESHENI ya usalama katika eneo la Bonde la Ufa inayofahamika kama Maliza Uhalifu, imeangaziwa baada ya kundi la maafisa wa Huduma ya Vijana kwa Taifa (NYS) waliohusishwa kujenga shule kulalamikia kukosa kulipwa. Vijana wasiopungua 50 wa NYS wanadai jumla ya Sh3 milioni ambazo ni malimbikizi ya marupurupu yao ya miezi minne. Operesheni Maliza Uhalifu (OMU) ilizinduliwa 2013 kuangazia ukosefu wa usalama katika kaunti za Turkana, Pokot Magharibi, Elgeyo Marakwet, Baringo, Laikipia na Samburu. Iliongozwa na kikosi kinachojumuisha KDF, GSU, ASTU, polisi wa kawaida na NPRS. Maafisa hao waliojumuishwa kwenye operesheni hiyo Februari 2023, wamelalamikia kukosa kulipwa na kuongezewa muda wa kandarasi kinyume na maafikiano. Akizungumza na Taifa Leo, afisa mmoja kutoka Nakuru alifichua walihusishwa kwenye operesheni hiyo kama maafisa wenye ujuzi ili kusaidia jeshi la KDF katika ujenzi wa shule Baringo, kama sehemu ya kuzima shughuli za majangili eneo hilo na kuanzisha maendeleo. Kundi la kwanza la makurutu wa NYS lilitumwa eneo hilo kutoa huduma mbalimbali ikiwemo waashi, fundi wa mifereji, kazi za stima na nyinginezo. Afisa huyo alisema walistahili kufanya kazi kwa miezi mitatu kwa mkataba wa kulipwa marupurupu ya Sh15,000 kila mwezi. “Tulikuwa bado tunasubiri kuelekea katika maeneo yetu ya mafunzo baada ya kukamilisha mitihani yetu tulipopokea jumbe kupitia simu na kutuagiza kurejea chuoni. Tulitumwa katika operesheni kaunti hiyo ambapo KDF ilikuwa inajenga shule,” alisema afisa huyo. Waliporejea vituoni, afisa huyo alisema wahudumu wa NYS walikuwa wameitisha malipo ya Sh1,000 kila siku lakini maafisa wasimamizi wakawashawishi kuchukua nusu ya kiasi hicho. Alidai walipokea malipo ya kwanza baada ya kufanya kazi kwa miezi miwili yaliyotumwa kwa pamoja katika akaunti zao za benki mtawalia. Nakala zilizofikia Taifa Leo zinaonyesha maafisa hao walitumwa kujenga shule mbalimbali ikiwemo shule za msingi za Chesitet, Chepkesin, Kositei, Koloa, Kapindasum, Arabal, Pura, Mukutani, Sambalat, Lomelo, Chemoril na shule ya sekondari ya Kapedo. Tuliwasiliana na KDF kuhusu suala hilo lakini wakajitenga na shutuma hizo wakidai hawawajibiki kwa malalamishi ya maafisa husika.
HALI tofauti kabisa inawasubiri wazazi, shule na biashara zinazoendeshwa katika sekta ya elimu, wanafunzi watakaporejea shuleni kwa muhula wa kwanza Jumatatu, Januari 6. Kwa mara ya kwanza tangu 1985, hakutakuwa na usajili wa wanafunzi wa Kidato cha Kwanza 2025 huku mtaala wa CBC ukiingia awamu mpya baada ya mfumo wa awali wa 8-4-4 kuvunjiliwa mbali katika shule za msingi.Hakukuwa na usajili wa wanafunzi wa kidato cha kwanza 1985 baada ya muda wa elimu ya shule ya msingi kuongezewa kutoka miaka saba hadi minane, 8-4-4 ilipoanzishwa. Darasa la Nane la mwisho liliondoka shule ya msingi 2023 ambapo 2024 hakukuwa na mitihani ya Darasa la Nane (KCPE).Kundi la kwanza la CBC litajiunga na Gredi 9, ambalo ni darasa la mwisho la sekondari ya msingi iliyopo katika shule za msingi. Kutokana na hali hii, shule za sekondari zinatazamiwa kupoteza mabilioni ya fedha ambazo zimekuwa zikipokea chini ya mpango wa Elimu ya Kutwa ya Sekondari Bila Malipo (FDSE) kwa sababu zitakuwa na upungufu wa darasa moja. Kila mwanafunzi hugawiwa Sh22,244 kila mwaka za kugharamia masomo.Isitoshe, shule kadhaa zitasalia na nafasi tupu zisizotumika hali inayosubiriwa kwa hamu kufuatia malalamishi kuhusu msongamano katika shule za sekondari tangu sera ya kusajili wanafunzi wote ilipoanzishwa 2014. Hata hivyo, walimu wakuu wa shule za msingi sasa watasimamia mabilioni yaliyotengewa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za msingi. “Mambo yatabadilika sana hasa kibiashara. Kama fundi anayeunda masanduku ya shule, nimelazimika kubadilisha mbinu ya mapato kutokana na ukosefu wa biashara. Niliamua kujipanga mapema nikijua hakutakuwa tena na wanafunzi wa Kidato cha Kwanza, kwa hivyo ninaunda stovu badala yake,” anasema mfanyabiashara wa Kisumu, Richard Omollo.

PWANI: WILAYA ya Mkuranga imetajwa kupiga hatua kubwa katika sekta ya elimu, ambapo idadi ya shule za msingi…

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Wilaya ya Ruangwa imepiga kasi kubwa ya maendeleo ambayo imewawezesha wakazi wa Wilaya hiyo kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za kiuchumi. Amesema kuwa Wilaya hiyo changa ilikuwa na changamoto nyingi kwenye Sekta ya Elimu, Afya, Kilimo, Miundombinu ikiwemo barabara, maji, Umeme, Uwekezaji na hata kwenye michezo “Changamoto hizi zilitufanya […] The post Rais Dkt. Samia anamchango mkubwa kwenye Maendeleo Ruangwa first appeared on Millard Ayo.
HUKU shule zikikaribia kufunguliwa, wazazi na walimu wanakumbwa na changamoto kufuatia kucheleweshwa kwa orodha ya vitabu vilivyokubaliwa rasmi kutumika kuanzia darasa la tano hadi la nane. Wazazi hao wanahofia kucheleweshwa huku na Taasisi ya Ukuzaji Mtaala (KICD), kunaaathiri kujiandaa kwa watoto wao kabla ya muhula mpya kuanza, huku nao wakikabiliwa na changamoto za kifedha. “Hatuelewi. Tunatarajiwa vipi kupanga masomo ya watoto wetu bila orodha ya vitabu?” mzazi mmoja aliuliza. Wazazi wengi hununua vitabyu wakati wa likizo. Mtaala wa Elimu na Utendaji (CBC) unategemea vifaa rasmi vya masomo ili kufanikisha malengo yake kwa wanafunzi. Bila vitabu, walimu wanakosa mwongozo wa kufanikisha ratiba za masomo, hali inayoweza kuathiri mafunzo shuleni. Wazazi hao wanahofia kuwa KICD inahatarisha elimu ya watoto, hasa wakati nchi inakumbwa na changamoto za katika utekelezaji wa CBC. Kucheleweshwa huku pia kumeziacha shule nyingi zikiwa hazijaweza kujiandaa ipasavyo, hali inayotishia kuvuruga ratiba za masomo shule zitakapofunguliwa. Wakuu wa shule wameelezea wasiwasi wao, wakionya kwamba bila kupatikana kwa vitabu vilivyokubaliwa kwa wakati, shughuli za kufundisha na kujifunza zitakumbwa na changamoto kubwa. “Hili ni kosa kubwa. CBC inategemea mwongozo uliopangiliwa vizuri, na bila vifaa hivi, tunaanza muhula kwa njia ambayo si dhabiti,” alisema mkuu mmoja wa shule. Hata hivyo, KICD imekanusha madai ya kuwa imechelewa kutoa vitabu, ikisema vitabu vinapatikana shuleni na katika maduka ya kuuza vitabu. Mkurugenzi wa KICD Prof Charles Ong’ondo, alisema vitabu vya masomo yote kuanzia masomo ya chekechea hadi darasa la tisa vipo tayari tena madukani. Lakini alikiri kuwa vitabu vya masomo ya Kilimo, Sanaa za Ubunifu, na Mafunzo ya kiufundi kwa darasa la saba na nane vilikamilishwa Desemba hii. "Vitabu hivi bado havijachapishwa, lakini vinatarajiwa kwenye maduka ifikapo Februari 2025," akasema. Prof Ong’ondo alieleza kuwa kuchelewa huko kulitokana na mchakato wa kuboresha mtaala kufuatia ripoti ya Kamati ya Rais ya Marekebisho ya Elimu iliyotolewa Agosti 2023. Kwa sasa, kuna upungufu wa vitabu vya lugha ya Kifaransa katika shule zote nchini, baada ya serikali kupeana mkandarasi biashara ya kuchapisha vitabu milioni moja vya Kifaransa ambavyo havikua vinahitajika shuleni. Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, Bi Nancy Gathungu, alisema matumizi ya fedha kwa vitabu hivi hayakuzingatia thamani yao. Hata hivyo, Prof Ong’ondo alieleza kuwa Kifaransa na lugha nyingine za kigeni si somo la lazima kwa madarasa ya kwanza hadi tisa. Shule zinazofundisha masomo haya zimeombwa kutoa taarifa kwa KICD ili kusaidia kupanga usambazaji wa vitabu.

Wanawake na Wafanyakazi wa mkoa wa Dar es salaam kupitia wilaya ya Ubungo wametakiwa kuendelea kujiunga kwenye Vyama mbalimbali vyenye kutoa fursa mbalimbali ikiwepo kupata elimu namna ya kujikomboa na kuweza kutatua changamoto mbalimbali zikiwemo za kiuchumi na kijamii. Kauli hiyo imesemwa leo na Mwenyekiti wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi wilaya ya Ubungo na […] The post Wanawake Wafanyabiashara na Wafanyakazi wamekutana na kujadili kukuza uchumi wao first appeared on Millard Ayo.

Mamlaka ya mapato Tanzania TRA Mkoa wa Tanga imewatembelea na kutoa shukrani kwa walipa Kodi upande wa Shule za sekondari wilayani Lushoto Mkoani hapa. Akizungumza mara baada ya kuwatembelea walipa Kodi wa Shule ya Sekondari Mazinde Juu na Shule ya Sekondari Kifungiro Girl’s Naibu Kamishna Huduma wa za Kiufundi TRA Bw.TedFrank Sirlikuwasha ambaye amemwakilisha Kamishna […] The post “TRA Mkoa wa Tanga wawapongeza walipa Kodi wa Shule na Vinywaji” first appeared on Millard Ayo.

Mtangazaji wa Clouds Media na Mwenyekiti Tasisi ya “Babuu Cancer Foundation” Sedou Mandingo maarufu “Babuu wa kitaa” ameandaa matembezi ya furaha yatakayofanyika December 28 2024 Jijini Mwanza yakilenga kutoa elimu ya Saratani. Babuu akiwa ameongozana na Wataalamu wa Afya, amezungumza na Waandishi wa Habari Jijini Mwanza, ameeleza kuwa Kampeni yake ya ‘Happy Walk’ ina lenga […] The post Babu wa kitaa aandaa matembezi ya furaha yatakayofanyika December 28 2024 Mwanza first appeared on Millard Ayo.

Mahakama ya China imetoa hukumu ya kifo iliyositishwa kwa mtu mmoja aliyejeruhi zaidi ya watoto kumi na wawili kwa kugonga gari lake kwenye umati wa watu nje ya shule ya msingi katikati mwa China kwa kile kilichosemekana ni kutokukubaliana na talaka kati yake na mkewe. Watu 30, wakiwemo watoto 18 wa shule, walijeruhiwa katika kisa […] The post Mwanamume Mchina aliyefanya shambulio baada ya talaka ahukumiwa kifo first appeared on Millard Ayo.

Mkuu wa mkoa wa Katavi Bi. Mwanamvua Mrindoko amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka watoto shule pindi msimu mpya wa masomo unapoanza Januari 13, 2025 ambapo mkoa wa Katavi una jumla ya wanafunzi 13,887 watakaojiunga na shule za sekondari. Mkuu huyo wa mkoa wa Katavi ametoa rai hiyo wakati akizungumza na waandishi wa Habari ofisini […] The post Wanafunzi 13,887 wanatarajiwa kujiunga na shule za sekondari Katavi 2025 first appeared on Millard Ayo.

Japan inachukua mipango ya hatua kuelekea kufanya maisha ya Mwezi kuwa ukweli,ambapo Chuo Kikuu cha Kyoto na kampuni kubwa ya ujenzi ya Kajima Corp wakishirikiana kuunda makazi ya mwezi ambayo hutoa mvuto bandia, vyombo vya habari vya ndani viliripoti Jumapili. Mradi wa “Neo Lunar Glass” unalenga kuunda muundo wa paraboloid wenye uwezo wa kuiga hali […] The post Japan yaanza mipango ya kuweka maisha halisi kwenye mwezi first appeared on Millard Ayo.

Zaidi ya Watu milioni Mbili(2.5) nchini wamefikiwa na elimu ya uhifadhi na Utunzaji wa rasilimali za maji ambayo wamepatiwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Shahidi wa Maji. Akizungumza katika hafla maalum ya kuwatunuki vyeti baadhi ya Wadau wa maji iliyofanyika Mjini Morogoro Mkurugenzi wa Shirika hilo Abel Dugange amesema kundi hilo limekuwa muhimu hasa […] The post Shahidi wa Maji wawafikiwa Watu Milion 2.5 elimu ya utunzaji vyanzo vya maji first appeared on Millard Ayo.

Jitihada Za Serikali ya awamu ya Sita ni kuhakikisha sekta ya elimu inaboreshwa na kutolewa kwa nadharia na Vitendo zaidi ili kuwarahisishia Wahitimu kuweza kujiajiri pindi wakimaliza masomo yao. Zaidi ya Wanafunzi 200 wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya kutokea Ndaki ya usanifu Majengo na Teknolojia ya Majenzi (coACT) wamefanya mafunzo ya Usanifu […] The post Zaidi ya wanafunzi 200 wajengewa uwezo kwa vitendo first appeared on Millard Ayo.
NI pigo kuu kwa Serikali ya Rais William Ruto baada ya Mahakama kuu kufutilia mbali mfumo mpya wa ufadhili wa masomo katika vyuo vikuu ikisema unabagua na kukandamiza haki wanafunzi kupata elimu muwafaka. Akitangaza mfumo huu mpya uliozinduliwa na Serikali ya Kenya Kwanza unakiuka Katiba na haki ya watoto kupata elimu iliyo na ushindani katika lingo za kimataifa, Jaji Enock Chacha Mwita alisema matumaini na matarajio ya wanafunzi yalitiwa kiza. Jaji Mwita alisema elimu ndicho kiungo muhimu zaidi katika ustawi wa kila nchi na kwanba ni jukumu ya Serikali kuhakikisha wanafunzi wamepokea elimu bora itakayowawezesha kubobea taaluma wanazohitimu. Jaji Mwita alikubaliana na walalamishi walioishtaki serikali kwamba mfumo huu mpyawa kufadhili elimu katika vyuo vikuu umesababisha mtafuruku mkubwa katika fani ya elimu. Jaji huyo alisema mfumo huu wa ufadhili wa elimu ya juu uliwatwika wazazi mzigo mzito wa kugharamia elimu ya wanao ambayo inapasa kugharamiwa na Serikali. Mahakama ilikubaliana na Tume ya Kitafa ya Kutetea Haki za nadamu (KHRC), Elimu Bora Working Group na Miungano ya vyama vya wanafunzi kwamba mfumo huu unakinzana na Katiba kwamba serikali ifadhili masomo ya wanafunzi katika nyanja zote kwenye vyuo vikuu , taasisi za masomo ya anuai na kiufundi (TVETs). “Mfumo huu mpya kufadhili elimu katika vyuo vikuu unakinzana na Katiba na unawabagua wanafunzi ambao wako na haki ya kupata elimu bora,”Jaji Mwita alisema. Jaji huyo alisema Katiba imeipa serikali jukumu la kufadhili elimu katika vyuo vikuu na vyuo vya kiufundi. Alisema mwongozo wa serikali wa kuwajukumisha wazazi kugharamia elimu ya wanao ni “ukiukaji wa hali ya juu ya katiba na haki za watoto kupata elimu kwa ufadhili wa serikali.” Jaji Mwita alisema wanafunzi kutoka familia sisizo na uwezo kifedha na wamehitimu kusoma taaluma zinazofadhiliwa kwa gharama ya juu wamebaguliwa. Alisema lazima kuwe na usawa na haki itendeke kwa wote wanaofaulu kujiunga na vyuo vikuu. Jaji Mwita alisema matarajio ya wanafunzi kujiunga na vyuo vikuu kusoma taaluma waliohitimu yalikuwa yamedidimia. Kabla ya mfumo huu kupitishwa na kuanza kutekelezwa , Jaji Mwita alisema haukupata uungwaji mkono na wananchi kwa kukumbatia maoni yao. Jaji huyo alisema katiba imeshauri kwamba kabla ya mwongozo wowote ule au sheria yoyote ile lazima maoni ya wananchi yashirikishwe kabla ya kupitishwa na kuanza kutumika. “Mchango wa umma kabla ya sheria au mwongozo kupitishwa lazima ushirikishwe,”Jaji Mwita alisema, huku akiongeza “maoni ya wananchi hayakushirikisha kabla ya kuanza kutumika.” Baada ya maoni ya wananchi kusikika ilipasa bunge la kitaifa kuyajadili na kuyatathmini kabla ya sheria hiyo ya ufadhili wa masomo kufanyiwa mageuzo. 'Ilipasa sheria hii na mfumo huu mpya wa ufadhili masomo uchangiwe na wananchi kabla ya kuanza kutekelezwa,” Jaji Mwita alisema. Katika kesi hiyo iliyowasilishwa kortini mwaka uliopita, KHRC na mashirika hayo mengine yaliomba mahakama kuu iufutilie mbali mfumo huu hautilii maanani kamwe maslahi ya wanafunzi kutoka familia maskini. Pia walalamishi walisema mfumo huu umezua mtafaruku katika uteuzi wa wananchi wanaojiunga na vyuo vya anuai na kiufundi (TVETs) kwa vile hakukuwa na mwelekeo kutoka taasisi ya uteuzi wa wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu (KUCCPS). Pia KHRC ilisema “utaratibu wa utoaji mikopo ya ufadhili wa elimu ya juu haueleweki, umekumbwa na hali ya suinto fahamu na umekiuka sheria.’’ Jaji Mwita aliombwa afutilie mbali mfumo huu na kutupilia mbali tetezi za wizara ya elimu. Mnamo Oktoba 3, 2024, Mahakama ilitoa agizo la muda kusitisha utekelezaji wa mfumo huu mpya wa ufadhili ya elimu vyuo vikuu.

Matumizi ya simu za mkononi yatapigwa marufuku katika shule za msingi na sekondari kote nchini Brazil ikiwa sheria iliyopitishwa hivi karibuni na Bunge la Congress na itaidhinishwa na Rais Luiz Inacio Lula da Silva, vyombo vya habari vya ndani viliripoti Alhamisi. Sheria hiyo, iliyoundwa kushughulikia athari mbaya za simu za mkononi kwa afya na elimu […] The post Brazil yapiga marufuku matumizi ya simu za mkononi shuleni first appeared on Millard Ayo.

Watoto kadhaa wamekufa wakati wa mkanyagano siku ya Jumatano katika maonyesho ya watoto yaliyoandaliwa kusini magharibi mwa Nigeria, mamlaka ilisema. Kisa hicho kilitokea katika Shule ya sekondari ya Kiislamu huko Basorun, Jimbo la Oyo, karibu na kitovu cha kiuchumi cha Lagos. Vikosi vya usalama vilihudhuria eneo la tukio na kuwakamata waandaaji wa hafla hiyo, gavana […] The post Watoto kadhaa nchini Nigeria wamekufa kwenye mkanyagano Nigeria first appeared on Millard Ayo.

The post Wadau wajadili Elimu ya Ualimu appeared first on HabariLeo.
UTAFITI mpya umefichua kwamba uvutaji sigara kuanzia utotoni unaongeza hatari ya kukumbwa na maradhi ya moyo mapema maishani. Aidha, utafiti huo umeonyesha kwamba watoto wengi wanaoanza kuvuta tumbaku katika umri wa miaka 10 au katika umri wa kubalehe, huendelea kufanya hivyo hata baada ya kutimu miaka ya ishirini. Watafiti walifuatilia watoto 1,931 waliozaliwa miaka ya tisini kuanzia walipokuwa na umri wa miaka 10 hadi walipofika miaka 24. Mwanzoni mwa utafiti huo, ni asilimia 0.3 pekee ya watoto waliokuwa wakivuta sigara katika umri wa miaka 10, lakini idadi hii iliongezeka na kufikia asilimia 26 walipofika katikati ya miaka 20. Takriban thuluthi tatu ya wale walioanza kuvuta sigara utotoni au katika umri wa kubalehe, waliendelea hadi mwanzoni mwa utu uzima. Matumizi ya kila mara ya tumbaku kuanzia umri wa miaka 10 kuendelea hadi miaka 24, yalihusishwa na asilimia 52 ya visa vya uharibifu wa moyo mapema maishani, ambapo matatizo haya yalikuwa pamoja na moyo kuvimba, moyo kupunguza uwezo wa kujilegeza, na shinikizo la damu, kufikia miaka 24. Baada ya kuhusisha hatari zingine kama vile shinikizo la damu, uzani mzito kupindukia, moyo kuvimba na ulegevu, vichochezi vya moja kwa moja vya tumbaku vinavyosababisha moyo kuvimba kati ya umri wa miaka 17 na 24 vilikuwa asilimia 30. Tafiti za awali kwa watu wakomavu zimeonyesha kwamba uvutaji sigara kuanzia umri wa kubalehe, huongeza hatari ya maradhi ya moyo kufikia umri wa makamo. Hata hivyo, hakuna utafiti wa awali ambao ulichanganua ishara za mapema za uvutaji tumbaku kuanzia utotoni, kwa moyo. “Ni hatari sana kuanza kuvuta sigara katika umri huu mdogo, huku visa vya ongezeko la idadi ya vijana walio katika umri wa kubalehe wanaovuta sigara za kieletroniki. Bidhaa za sigara hizi huwa na viungo hatari kwa mapafu, na pia husababisha hitilafu kwenye mapigo ya moyo, hali ambayo yaweza kusababisha uharibifu wa kiungo hiki. Wanaotumia sigara za kieletroniki pia bila kujua wanajiweka hatarini,” asema Andrew Agbaje, profesa mshiriki katika Chuo Kikuu cha Eastern Finland. “Utafiti huu unaonyesha kwamba mbali na kusababisha hatari ya kukumbwa na maradhi ya moyo baadaye maishani, uvutaji sigara katika umri wa kubalehe, unasababisha uharibifu wa kudumu kwenye misuli ya moyo,” alisema Emily Bucholz, Profesa msaidizi katika Kitivo cha udaktari cha Chuo Kikuu cha Colorado School of Medicine. Utafiti huo, ambao ni ushirikiano kati ya chuo kikuu vya Bristol na Exeter, nchini Uingereza na Chuo Kikuu cha Eastern Finland, ulichapishwa kwenye jarida la the Journal of the American College of Cardiology (JACC).

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa wito kwa wafanyabiashara kuendelea kushirikiana na mamlaka hiyo na kutatua changamoto zinazowakabili bila migomo wala kufunga maduka ili kukuza sekta ya biashari. Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipakodi kutoka mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) makao makuu, Richard Kayombo wakati akizungumza na wafanyabiashara mbalimbali katika […] The post TRA yawataka wafanyabiashara kuendelea kutatua changamoto bila kufunga maduka first appeared on Millard Ayo.

Mwanajumuiya wa Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM) (Alumni) Abdulmajid Nsekela amempongeza Mkuu wa chuo hicho Profesa Josephat Lotto na timu yake kutokana na kubuni mikakati mbalimbali kwa ajili ya kuboresha elimu nchini. Nsekela ameyazungumza hayo wakati wa hafla ya chakula cha jioni ya wanafunzi waliosoma zamani katika chuo hicho ,iliofanyika usiku wa kuamkia leo […] The post IMF yapongezwa kwa kubuni miradi mbalimbali first appeared on Millard Ayo.

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na taifa kwa ujumla limepata sifa kubwa kwa miaka ya hivi karibuni kwenye suala la utafiti ukiwemo wa kumtumia panya namna ya kutafuta na kubaini vilipuzi na mabomu yalitotengwa ardhini. Miongoni mwa panya hao ni Magawa aliyesifika kusaidia kugunduliwa kwa zaidi ya mabomu 108 ya kutegwa ardhini nchini […] The post Chuo Kikuu cha Sokoine chamuenzi panya Magawa first appeared on Millard Ayo.
WAZEE katika Kaunti ya Lamu wamelalamikia kusahaulika kwa elimu ya watu wazima, almaarufu ngumbaru. Wazee hao wamedai kwamba katika miaka ya hivi majuzi, serikali na Wizara ya Elimu imeipa kipaumbele utekelezaji wa mtaala mpya wa CBC ilhali ngumbaru haikumbukwi. Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Lamu, Mohamed Mbwana, alishikilia kuwa elimu ya watu wazima ni kiungo muhimu kwenye mipango ya maendeleo ya taifa lolote lile. Alisema elimu hiyo ni muhimu kupewa uzito sawa na elimu nyinginezo zinazotiliwa mkazo. [caption id="attachment_164948" align="alignnone" width="1828"] Wanafunzi wakihudhuria darasa katika kituo cha mafunzo ya watu wazima cha Kapserton Adult Basic Education Centre eneo la Kipkaren Celian mjini Nandi mnamo 2013. PICHA | MAKTABA[/caption] Bw Mbwana alieleza kutoridhishwa kwake na jinsi wazee wengi Lamu bado hawajui kusoma na kuandika, hali ambayo inawaathiri kimaisha na hivyo pia kuathiri maendeleo ya kitaifa. “Elimu ya ngumbaru ililetwa nchini kusudi likiwa ni kuleta nuru hasa kwa wengine wetu ambao tulidhania hatutajua kusoma au kuandika maishani. Mimi binafsi imenisadia pakubwa. “Ila miaka ya sasa hatujaona tena msukumo wa elimu ya watu wazima. Utasikia kote mkazo ukiwekwa kwa mtaala wa CBC. Sisi wazee mumetuweka wapi? Lazima mtuzingatie pia. Ni muhimu elimu ya ngumbaru itiliwe mkazo pia,” akasema Bw Mbwana. [caption id="attachment_164949" align="alignnone" width="2000"] Wanafunzi wa Sekondari Tangulizi wakati wa somo ndani ya maabara ya sayansi katika Shule ya Msingi ya Bomu eneo la Changamwe mjini Mombasa, mnamo Januari 2024. PICHA | KEVIN ODIT[/caption] Hata hivyo, Mkurugenzi wa Elimu katika Kaunti ya Lamu, Bw Zachary Mutuiri, aliwataka wazee wajiandikishe kupokea elimu hiyo akisisitiza kuwa serikali inaithamini. Alisema elimu ya ngumbaru inaendelea na akawataka wazee wenye kiu ya elimu hiyo kujitokeza. “Wanaolalamika huenda hawajajitokeza wazi kujisajili kupokea mafunzo ya ngumbaru. Elimu ya ngumbaru ipo Lamu. Wazee hata wana afisa wao maalumu. “Ningewasihi wenye kiu ya elimu hiyo wajitokeze na watahudumiwa,” akasema Bw Mutuiri. Kassim Shee, 75, mzee wa Kizingitini, Lamu Mashariki, anataja kutojua kusoma na kuandika kuwa kikwazo kikubwa katika harakati za kuimarisha huduma za jamii nchini. Anasema ari yake ni kutafuta hiyo elimu ya ngumbaru kwani miaka ya ujana wake hakuweza kukanyaga darasani. Kinachomtia wasiwasi ni mahali pa kuipata elimu hiyo, akidai kuwa kwao Kizingitini hajaona kituo chochote au mwalimu wa ngumbaru wa kuwawezesha kuipata elimu wanayotafuta. [caption id="attachment_164951" align="alignnone" width="2000"] Watahiniwa wenye umri wa watu wazima na wa kibinafsi baada ya kumaliza mtihani wa mwisho wa KCPE 2015 katika Shule ya Msingi ya Nyamasaria mjini Kisumu. PICHA | MAKTABA[/caption] “Nina kiu ya elimu niliyoiacha miaka mingi iliyopita. Nataka kurudi darasani ila hawa walimu au vituo vya ngumbaru hatuvioni tena. Serikali ifanye juhudi kutuanzishia upya mpango huo. Wasitusahau,” akasema Bw Shee. Kwa upande wake, Bi Khadija Hussein, 56, anasema hatua ya wanawe na wajukuu wake kuongea Kiingereza mfululizo kila wanapokaa naye kunamfanya kuwa na msukumo wa kutaka kurudi darasani, asome na kuifahamu vyema lugha hiyo. “Sitaki kusengenywa mimi. Watoto na wajukuu zangu wanapoongea Kingereza nyumbani ninahisi upweke. Siwezi kuchangia kwa sababu sijui hata kinachozungumziwa. Na ndiyo sababu nataka nirudi ngumbaru, nisome ili nijue angalau neno moja moja la Kiingereza,” akasema Bi Hussein.
PICHA ina thamani sawa na idadi ya maneno 1, 000, na Yiyi Wang anakiri haya kupitia kipaji chake cha sanaa. Kinda huyu mwenye umri wa miaka 17, ana mapenzi ya mazingira na yaliyomo kupitia uchoraji. Kipenzi cha mimea na wanyama, Yiyi msichana mwenye asili ya China, huzungumza upendo wake kwa mazingira kupitia sanaa. “Sanaa haielezei hadithi pekee, ila pia inaonyesha na kutoa hisia, na jumbe,” anasema msanii huyu anayetoka Beijing, China. Kwake picha na michoro, inaelezea lugha ambayo maneno yasingeweza. Akiwa mwanafunzi wa Shule ya Upili China, Yiyi huvutiwa na mazingira kiasi cha kutoa hamasisho kuhusu wanyamapori na mimea kwa kutumia michoro. [caption id="attachment_164806" align="aligncenter" width="300"] Yiyi Wang akiwa na babake, akielezea kuhusu talanta yake katika sanaa. PICHA|SAMMY WAWERU[/caption] Kwa sasa, ni mwanafunzi wa madarasa ya juu (senior student), mwaka wa pili Beijing High School’s International Department. Mapenzi yake katika sanaa, yalianza akiwa mchanga kiumri, babake Tan Wang, akifichua kwamba alikuwa akichora kwenye jukwaa lolote alilokutana nalo. “Akiwa na miaka mitano, alionyesha ari ya sanaa na kwa siku angelala saa tano pekee kwa sababu ya kufanya uchoraji,” Wang akaambia Akilimali kwenye mahojiano ya kipekee Jijini Nairobi. Wang na bintiye, walikuwa wamezuru Kenya majuzi ambapo walipata fursa ya kutembelea Mbuga ya Kitaifa ya Wanyamapori Nairobi. Yiyi alivutiwa zaidi na twiga na nguruwe wa mwituni (warthog), viumbe anaohoji hajawahi kuwaona ana kwa ana. Anaridhishwa na mila itikadi za Kiafrika, mapenzi anayosema yalichochewa na hadithi kuhusu Bara Afrika alizosimuliwa na babake aliporejea China, akiwa mchanga. [caption id="attachment_164807" align="aligncenter" width="300"] Yiyi Wang na babake, Tan Wang walikuwa wamezuru Kenya majuzi. PICHA|SAMMY WAWERU[/caption] Wang alikuwa akifanya kazi Afrika. “Kila aliporejea nyumbani, alikuwa akija na michoro kutoka kwa wasanii wa Kiafrika, ambayo ilifanya nivutiwe na mila za Afrika,” Yiyi akasema. Mwongo mmoja baadaye, sasa amegeuza aliyoshuhudia babake na kuwasimulia kuwa sanaa yake mwenyewe. Kinachomfurahisha zaidi, Yiyi anasema ni uwezo wake kuwasilisha lugha na hisia za wanyama kupitia michoro. Aidha, anakumbuka utangamano na mbwa kipenzi chake anayesema hakuelewa alichotaka alipobweka. “Huenda alitaka maji, huenda chakula.” Yiyi anasema muhimu ni utangamano kati ya binadamu na wanyama, wawe wa nyumbani au pori. “Husikitika sana kuona makao ya wanyamapori yakivamiwa kupitia uharibifu wa mazingira, hasa misitu,” anasema. Huku akiendelea kunoa makali katika sanaa shuleni, ana imani atayapalilia zaidi katika chuo kikuu. Kwenye safari ya uchoraji, kinachomridhisha zaidi ni kuunganisha wasanii wa Afrika na masoko ya China. Julai 2024, licha ya umri wake mdogo, aliandaa hafla ya wasanii kutoka Afrika kuuza michoro yao China. [caption id="attachment_164808" align="aligncenter" width="300"] Yiyi Wang Julai 2024 aliandaa hafla Beijing China, ambapo alitumia jukwaa la maonyesho hayo kupiga jeki wachoraji kutoka Barani Afrika. PICHA|SAMMY WAWERU[/caption] Ikiwa na kaulimbiu ‘Sillage African Folk Artists Charity Art Sale’, ilivutia wasanii 13 na kuegemea michoro yenye mada; itikadi na mila za Kiafrika. “Ilishirikisha kina mama waliovalia mavazi ya Kiafrika, nyimbo na ala za muziki, ikiwa ni pamoja na wanyamapori tajika Barani Afrika,” Yiyi anafafanua. Hata ingawa haikuwa rahisi kuandaa maonyesho hayo, anasema alisaidiwa na babake, marafiki na hata walimu wake. Alitumia mitandao ya kijamii kama vile Instagram, Youtube, Facebook na Tiktok, kusaka wachoraji. Hafla hiyo, Yiyi alikusanya zaidi ya Yuan 30, 000 sawa na kima cha Sh543, 000 thamani ya Kenya, hela alizotumia kupiga jeki wachoraji kutoka Afrika kwa kuwanunulia vifaa vya kuchora na hata kulipia wengine karo kunoa bongo katika sanaa. Ana imani ataendelea kutumia weledi wake kuinua wasanii wa Kiafrika. Akiwa raibu wa kahawa ya Kenya, kufikia sasa amezuru nchi za Kenya na Misri, Barani Afrika.

CHUO cha Uhasibu Arusha(IAA) kimeagizwa kutanua wigo wa elimu katika nchi za Afrika Mashariki(EAC) na Nchi za Kusini…

MAKAMU wa Rais, Dk Philip Mpango amesema ili kuinua viwango vya tafiti za vyuo nchini, vyuo vya elimu…

Na Nora Damian, Mtanzania Digital Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wametakiwa kusoma vitabu mbalimbali kutoka China kikiwemo kinachozungumzia dhana ya utawala bora ili kujifunza namna nchi hiyo ilivyoendelea. Ushauri huo umetolewa Desemba 11,2024 na Mkurugenzi Mtanzania wa Taasisi ya Confucius Chuo Kikuu cha Dar es Salaam inayofundisha lugha ya Kichina, Profesa […]
GAVANA wa Nairobi, Johnson Sakaja ametaja usambazaji wa mlo wa Sh5 kwa siku kwa kila mwanafunzi kama mojawapo ya sera anazojivunia. Bw Sakaja amesema mpango huo unaoendeshwa chini ya programu ya Dishi na County, unaendelea kuvutia watoto kujiunga na shule katika gatuzi lake. Mradi huo wa kaunti, ulizinduliwa Agosti 2023 na mwaka mmoja baadaye, Gavana Sakaja anasema umeandikisha ufanisi. Alisema umeleta tabasamu kwa watoto wanaotoka familia zisizojiweza kimapato. Unalenga wanafunzi wa shule za umma za msingi pekee Nairobi. Aidha, kila mwanafunzi hutoa Sh5 kwa siku. “Inaridhisha kuona chini ya programu ya Dishi na County kila mwanafunzi anapata chakula cha Sh5 kwa siku,” Sakaja akasema mnamo Alhamisi, Desemba 12 wakati wa maadhimisho ya Jamhuri 2024. Hafla hiyo ya kitaifa ilifanyika Uhuru Grounds, na iliongozwa na Rais William Ruto. Bw Sakaja alisema mradi wa Dishi na County umewafaa mamia na maelfu ya watoto, hasa katika mitaa ya mabanda Nairobi ambao kwao kupata chakula huwa kibarua. Programu hiyo, hata hivyo, imekuwa ikikosolewa, Wakenya wakimtaka Sakaja kutafuta suluhu ya kudumu kwa wenyeji Nairobi.
WANAUME huwa hawafanyi hila kwamba wamefika kilele wakati wa mahaba ikilinganishwa na wanawake, watafiti wamebaini. Utafiti uliochapishwa kwenye jarida linaloangazia masuala ya ngono, ulisema wanawake wengi ndio hudanganya wanaume kuwa wamefika kilele wakati wa tendo la ndoa. “Tulibaini kuwa wanawake, watu wenye jinsia mbili (huntha), na kuwa na wapenzi wengi, ni sababu ambazo zinahusishwa na tabia ya wapenzi kudanganya kuwa wamefikia kilele wakati wanaposhiriki ngono,” sehemu ya utafiti huo inaeleza. Aidha utafiti huo uligundua watu ambao wapo kwenye uhusiano wa wazi ndio walikuwa na tabia ya kudanganya kufika kileleni. Wale ambao wapo kwenye ndoa au uhusiano wa kudumu iligunduliwa hawakuwa sana na tabia hiyo ya kuchukiza. Vilevile waliokuwa na tabia hiyo ya ukora, ni wale ambao hawakuwa wakiridhika na uhusiano ambao wapo, hawakuwa wakiridhishwa na wapenzi wao na pia walikuwa wakisumbuliwa na msongo wa mawazo kuhusu masuala mbalimbali maishani. Wanaume na wanawake ambao walikuwa wakishiriki hadaa hiyo hata hivyo, walikuwa na sababu tofauti baada ya kuachana na tabia hiyo. Wanaume walisema penzi lao lilikuwa limeimarika na sasa walikuwa wakifurahia tendo la ndoa. Baadhi walisema waliachana na wapenzi wao kwa hivyo hawakuwa wakishiriki ngono kabisa. Wanawake nao walisema hawakuona haja ya kuwahadaa wapenzi wao na wakaridhika na maisha bila kufika kilele wakati wa mapenzi. Utafiti uliofanywa hapo awali ulionyesha kuwa kibayolojia wanawake wakati mwingine hupata ugumu wa kufikia kilele wakati wa mapenzi. Hii ndiyo maana baadhi yao hawamakinikii suala hilo huku wanaume wanapogundua hilo, hujilaani kuwa hawajawaridhisha kitandani. “Tunaamini kuwa ikija katika wapenzi kufika kilele wakishiriki ngono, mazungumzo ni jambo ambalo ni muhimu sana,” akasema Dkt Silvia Pavan kutoka Chuo Kikuu cha Copenhagen.

The post Tanzania mabingwa shule za Afrika CECAFA appeared first on HabariLeo.

Watoto wawili wa familia moja ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi katika halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe wanadaiwa kubakwa na kuambukizwa virusi vya ukimwi (VVU) na baba yao wa kufikia. Victor Nyato ni mwenyekiti wa mtaa wanapoishi watoto hao na mama yao ambao mmoja anasoma darasa la pili mwenye umri wa miaka […] The post Baba adaiwa kubaka na kuwaambukiza VVU watoto wa kufikia first appeared on Millard Ayo.

Samwel Swai :DAR ES SALAAM: KWA mara ya pili Chuo Kikuu cha Dr es Salaam (UDSM), kimepokea msaada…

WAHITIMU wa Chuo cha Ustawi wa Jamii wametakiwa kutumia elimu waliyoipata kuwa fursa ya ajira. Akizungumza wakati wa…

Wadau wa elimu wakiwemo Camfed wametakiwa kuendelea kushirikiana na wadau wengine na serikali katika programu zake zenye lengo la kusaidia watoto hasa wakike kwenye suala la elimu kwa kuongeza kasi na uwekezaji wa sera mpya iliyoboreshwa. Hayo yamesemwa na Ernest Hinju Mkurugenzi msaidizi elimu ya watu wazima na elimu maalumu kwenye mkutano mkuu wa mwaka […] The post Wadau wa elimu Watakiwa kushirikiana kuunga mkono serikali first appeared on Millard Ayo.

Naibu katibu Mkuu Wizara ya elimu sayansi na teknolojia Prof Daniel Mushi amesema ili nchi ipige hatua kimaendeleo ni lazima kutumia tenkolojia ambayo inamchango mkubwa Katika kuleta mabadiliko nchini na duniani kwa ujumla. Porofesa Mushi ameyasema hayo wakati akizungumza katika kongamano la tatu la kimataifa la vyuo vya elimu ya juu vya ndani na nje […] The post Teknolojia kuchangia Maendeleo ya nchi. first appeared on Millard Ayo.

UJENZI wa majengo ya mabweni na jengo la utawala katika Taasisi ya Sayansi za Baharini (IMS) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), iliyopo Buyu visiwani Zanzibar umefikia asilimia 50 kukamilika. Ukiwa unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Agosti 2025 na kuanza kutumika, ujenzi huo ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa […] The post Ujenzi wa majengo mapya IMS Zanzibar wafikia asilimia 50 first appeared on Millard Ayo.

Shule ya Msingi Mazola, iliyopo katika kijiji cha Mazola, kata ya Doda, wilaya ya Mkinga, imepata afueni kubwa baada ya kukabidhiwa matundu ya vyoo 12 vilivyojengwa kwa msaada wa Shirika la World Vision kwa kushirikiana na serikali. Ujenzi huo umegharimu shilingi milioni 86.4 na unalenga kuboresha mazingira ya elimu kwa wanafunzi wa shule hiyo. Mkuu […] The post “World Vision imekabidhi matundu 12 ya vyoo shule ya msingi Mazola Wilayani Mkinga Tanga” first appeared on Millard Ayo.

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda amesema kuwa Masomo ya Maendeleo (Development Studies) yanapaswa kusaidia…

Na Safina Sarwatt, Moshi Zaidi ya wanafunzi 1,000 kutoka familia zenye mazingira duni wamefaidika na mpango wa ufadhili wa masomo ulioanzishwa na Kiwanda cha Sukari TPC Moshi kupitia taasisi yake ya Foundation for Community Transformation in Kilimanjaro (FTK). Mpango huu, ulioanza mwaka 2012, umewezesha wanafunzi wa maeneo yanayozunguka kiwanda hicho kuendelea na masomo yao ya […]

TIMU ya wasichana chini ya miaka 15 imeanza mashindano ya Ubingwa wa Shule za Afrika inayofanyika Uganda kwa…
HULDAH Momanyi Hiltsley, mzawa wa kwanza wa Kenya aliyeweka historia kwa kushinda kiti katika uchaguzi wa Amerika anatazamiwa kurejea nchini kwa ibada ya shukrani na hafla nyinginezo. Bi Momanyi atakuwa Kenya kwa siku nane kabla ya kurejea Marekani kujiandaa kwa uapisho wake utakaofanyika mwakani. Aliandikisha historia baada ya kuchaguliwa katika Bunge la Wawakilishi la Minnesota, Wilaya ya 38A katika uchaguzi wa Novemba. Mwakilishi huyo Jumatatu alisema atatua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) Jumanne, Desemba 10, 2024 saa tano asubuhi. Baada ya kuwasili, anatarajiwa kupamba hafla katika Chuo Kikuu cha Daystar leo jioni, ambapo atatoa hotuba kuu katika mkutano ambao utakuwa na mazungumzo kuhusu dhuluma za kijinsia. Mama huyo wa watoto wawili alisema kuwa atafanya vikao vingine vinavyolenga kuwatia moyo Wakenya kwamba wanaweza kufikia mambo makuu ikiwa watakuwa na ari na azma kama yeye. Mwakilishi huyo pia alifichua kwamba amepokea mwaliko rasmi wa kuungana na viongozi wengine kusherehekea sherehe za mwaka huu za Jamhuri Dei katika bustani ya Uhuru jijini Nairobi mnamo Alhamisi. Baada ya sherehe hizo ambazo zitaadhimisha miaka 60 ya Kenya kuwa Jamhuri, Huldah atasafiri hadi nyumbani kwao katika kaunti ya Nyamira, ambapo sherehe yake ya shukrani itafanyika. Hafla ya kurejea kwake nyumbani itaandaliwa kwa ushirikiano na serikali ya kaunti ya Nyamira na itafanyika katika Shule ya Upili ya Nyambaria siku ya Ijumaa. Akiongea kuhusu ujio wake, Bi Momanyi alisema alifurahishwa na upendo alioonyeshwa kutoka kwa Wakenya baada ya kumshinda Brad Olson wa Republican kwenye wadhifa huo. Alinyakua kiti hicho kwa tiketi ya chama cha Democratic-Farmer-Labour.

SERIKALI imeshauriwa kutumia vizuri rasilimaliwatu ili kuendelea kuimarisha uchumi. Mhadhiri wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha…