WATAALAMU wa masuala ya lishe sasa wanasema kuwa ulaji wa mara kwa mara wa nyama chemsha una maadhara ya kiafya.
Wataalamu hao sasa wanasema kuwa nyama ya ng'ombe iliyochemshwa inayopendwa na wengi ina kiwango kikubwa cha mafuta.
Joy Ouma, mtaalamu wa lishe aliyesajiliwa katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan, anasema nyama ya ng'ombe, kwa jumla, ina viwango vya juu vya mafuta ambayo yanaweza kusababisha ongezeko la kolesterol.
"Japo nyama ya ng'ombe ina protini na madini, wasiwasi hutokea inapotumiwa kupita kiasi, kwani nyama hiyo inapochemshwa, basi watu wanaikula sana," akasema mtaalamu Ouma.
Kepha Nyanumba, mtaalamu wa lishe aliyeidhinishwa kutoka Nairobi, anaongeza kuwa mara nyingi watu hudharau madhara ya kiafya ya kula kiasi kikubwa cha nyama, bila kujali jinsi inavyopikwa.
"Nyama ya ng'ombe ya kuchemsha inaweza kuonekana kama chaguo bora zaidi ikilinganishwa na kukaanga au kuchomwa, lakini bado ina kiasi kikubwa cha mafuta, hasa katika sehemu ndogo kama vile mbavu. Mafuta haya yanaweza kujilimbikiza mwilini baada ya muda na kuchangia kiwango cha juu cha kolesterol jambo ambalo huongeza hatari ya magonjwa ya moyo na mishipa ya damu,” anasema.
Bi Ouma anaonya kwamba ulaji wa mara kwa mara wa nyama kama hiyo inaweza kuongeza kolesterol ambayo ni hatari sana kwa mwili. Viwango vya juu vya mafuta mwilini huongeza hatari ya ugonjwa wa moyo.
"Watu wengi wanadhani kuwa nyama ya ng'ombe ya kuchemsha ni bora kwa sababu haijakaangwa, lakini kiwango cha mafuta kinabaki kuwa wasiwasi. Kula nyama ya ng'ombe mara kwa mara au kwa sehemu kubwa kunaweza kusababisha maadhara makubwa ya kiafya ya muda mrefu," anasema.
Hatari nyingine iliyopuuzwa ni uwezekano wa kupata kuwa mfugo ulikuwa ukiugua kabla ya kuchinjwa kwani inaathiri watu walio na matatizo ya figo.
Nyama ya ng'ombe ina protini nyingi, na ulaji wa vyakula vyenye protini nyingi kwa wingi unaweza kusumbua figo, na kufanya figo kufura au hata ugonjwa sugu wa figo.
"Unapokula nyama ya ng'ombe kupita kiasi, figo zako hufanya kazi kwa muda wa ziada ili kuondoa sumu hizi, ambazo baada ya muda zinaweza kusababisha uharibifu, haswa kwa watu ambao tayari wana matatizo ya figo," asema Bi Ouma.
Bw Nyanumba anaongeza kuwa wale walio na historia ya familia ya ugonjwa wa figo au matatizo mengine ya msingi wanapaswa kuwa waangalifu Zaidi.
"Ulaji wa nyama mara kwa mara unaweza kuathiri utendakazi wa figo kwa watu ambao tayari wako katika hatari. Ni muhimu kula aina vingine vya chakula vilivyo nap rotini ili kuzuia ugonjwa wa figo," anasema.
IMETAFSIRIWA NA WINNIE ONYANDO
Tambua kwa nini nyama chemsha ina madhara licha ya kupendwa na walinda afya
This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
EducationalTinubu: No student will be denied university education over poverty
Urges graduates to be creative, enterprising By Dayo Johnson, Akure President Bola Tinubu has assured Nigerians that no student will be denied access to tertiary education because of financial constraints. The President gave the assurance at the 37th convocation ceremony of the Federal University of Technology, Akure (FUTA), where he said the establishment of the […]
EducationalSEQUIP ilivyomfikisha Neema chuo kikuu
MBEYA: Serikali kupitia Mradi wa Kuinua Elimu ya Sekondari (SEQUIP) imeendelea kutoa fursa kwa wasichana waliokatisha masomo kutokana na changamoto mbalimbali za maisha kurejea shuleni na kuendeleza ndoto zao za elimu. Miongoni mwa wanufaika wa fursa hiyo ni Neema Andrea Usia, ambaye safari yake ya elimu ilikatizwa akiwa kidato cha pili, lakini kupitia fursa ya…
Educational892 graduates of CUHAS cadre pledge to observe ethics, dignity
MWANZA: 892 graduates of the Catholic University of Health Sciences Bugando (CUHAS) have been instructed to adhere to ethics, dignity and integrity in the provision of health services. The call was made today by the Bishop of the Catholic Diocese of Rulenge-Ngara, Mr Severine Niwemugizi, during the 19th graduation of the college held in Mwanza,…
EducationalChuka University graduate sits by himself, breaks down after no one shows up for his graduation
A Chuka University graduand broke down in tears after spending graduation day alone, as footage of him packing away a gown moved thousands of Kenyans online.