WAZIRI wa Elimu Julius Ogamba amesema serikali itakiokoa Chuo Kikuu cha Moi kisianguke.
Waziri huyo amedokeza kuwa juhudi za kufufua taasisi hiyo ziko katika hatua za mwisho na hivi karibuni, watatangazia umma kuhusu hatua zilizochukuliwa ili kurejesha shughuli za masomo katika taasisi hiyo.
Akizungumza alipokuwa akikagua jinsi mtihani wa KCSE ulivyokuwa ukiendelea Jumatatu, Novemba 18, 2024 baada ya kuzuru kaunti za Kisii na Nyamira, Bw Ogamba alisikitishwa na hali inayokikumba chuo hicho lakini akaeleza matumaini yake kuwa hivi karibuni taasisi hiyo itainuka.
“Tumeweka mpango wa kuhakikisha kuwa tunaendeleza chuo hicho. Tumebuni mkakati wa kushughulikia masuala yanayokiathiri na tutawajuza mara tu mikakati hiyo itakapokamilika,” Bw Ogamba alisema.
Mambo hayajawa sawa kwa taasisi hiyo yenye makao yake mjini Eldoret kwani imekuwa ikigonga vichwa vya habari katika siku za hivi karibuni kwa taarifa za kuvunja moyo.
Chuo hicho kimelemewa na madeni, maamuzi mabaya ya kifedha na kiutawala, nguvu kazi isiyoweza kumudiwa, miradi potovu na mengine mengi.
[caption id="attachment_163008" align="alignnone" width="300"] Waziri Julius Ogamba (kushoto) afurahia picha na walimu wakati wa kukagua mtihani wa KCSE kaunti za Kisii na Nyamira. Picha|Wycliffe Nyaberi[/caption]
Ina madeni ya zaidi ya Sh8 bilioni na wahadhiri wako kwenye mgomo, wakipinga mishahara kucheleweshwa, kutotumwa kwa malipo ya mikopo, pensheni na makato mengine ya watu wengine.
Wahadhiri hao wanataka kulipwa zaidi ya Sh8 bilioni, ikiwa ni pamoja na malimbikizo ya mishahara na fedha nyingine wanazodai kabla ya kurejea kazini.
Juhudi za kumaliza mgomo huo zimefeli huku wahadhiri hao wakishutumu uongozi wa chuo kwa kutowajali.
Kufuatia vuta nikuvute hiyo, wanafunzi ndio walioumia zaidi. Kwa sababu ya migomo isiyoisha ya wahadhiri hao, wanafunzi wanachukua miaka mingi kumaliza masomo yao katika muda unaostahili.
[caption id="attachment_163009" align="alignnone" width="300"] Waziri Ogamba katika bohari la mtihani. Picha|Wycliffe Nyaberi[/caption]
"Sio haki kwa wanafunzi kwenda chuo kikuu kwa mfano na kukaa kwa miaka tisa katika mchakato wa kufanya digrii zao. Si sawa na tunaenda kupata suluhu za muda mrefu na za kudumu kwa chuo hicho,” Bw Ogamba aliongeza.
Kamati ya Elimu ya Bunge la Kitaifa, inayoongozwa na Mbunge wa Tinderet Julius Melly ilizuru taasisi hiyo hivi majuzi na kutaka usimamizi ya chuo hicho uvunjiliwe mbali.
Kamati ilipendekeza uongozi wa taasisi hiyo uwekwe chini ya ushikilizi. Bw Ogamba alisema Wizara yake itaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha kuwa sekta ya elimu inaboreshwa.
Alisema hilo litaanza kwa kuhakikisha wanakomesha utamaduni wa kufanya udanganyifu katika mitihani. Aliwataka maafisa wanaosimamia mtihani unaoendelea kutolegeza kamba kwani mtihani huo unakaribia kufika tamati baadaye wiki hii.
Tutaokoa Chuo Kikuu cha Moi kisisambaratike, Waziri Ogamba aahidi
This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
EducationalTinubu: No student will be denied university education over poverty
Urges graduates to be creative, enterprising By Dayo Johnson, Akure President Bola Tinubu has assured Nigerians that no student will be denied access to tertiary education because of financial constraints. The President gave the assurance at the 37th convocation ceremony of the Federal University of Technology, Akure (FUTA), where he said the establishment of the […]
EducationalSEQUIP ilivyomfikisha Neema chuo kikuu
MBEYA: Serikali kupitia Mradi wa Kuinua Elimu ya Sekondari (SEQUIP) imeendelea kutoa fursa kwa wasichana waliokatisha masomo kutokana na changamoto mbalimbali za maisha kurejea shuleni na kuendeleza ndoto zao za elimu. Miongoni mwa wanufaika wa fursa hiyo ni Neema Andrea Usia, ambaye safari yake ya elimu ilikatizwa akiwa kidato cha pili, lakini kupitia fursa ya…
Educational892 graduates of CUHAS cadre pledge to observe ethics, dignity
MWANZA: 892 graduates of the Catholic University of Health Sciences Bugando (CUHAS) have been instructed to adhere to ethics, dignity and integrity in the provision of health services. The call was made today by the Bishop of the Catholic Diocese of Rulenge-Ngara, Mr Severine Niwemugizi, during the 19th graduation of the college held in Mwanza,…
EducationalChuka University graduate sits by himself, breaks down after no one shows up for his graduation
A Chuka University graduand broke down in tears after spending graduation day alone, as footage of him packing away a gown moved thousands of Kenyans online.