MJUKUU wa aliyekuwa Rais Daniel Moi, Collins Kibet, amelegeza msimamo wake kuhusu malezi ya watoto wake na kupendekeza hatua za kuhakikisha watoto hao wananufaika na mali ya familia yake.
Hii inafuatia mzozo wa muda mrefu wa kisheria kuhusu madai yake ya kupuuza majukumu yake kama mzazi.
Bw Kibet ambaye anakabiliwa na kesi ya kutotii amri ya mahakama iliyotolewa Juni 2022, aliwasilisha mapendekezo Novemba 27 ya kuwatunza watoto hao wawili na akaeleza nia yake ya kuwatambulisha watoto hao, ili wanufaike na baadhi ya manufaa anayostahili kutokana na uhusiano wake na familia ya Moi.
Ameahidi kuwasajili katika Shule maarufu ya Kabarak na kulipia gharama zao za matibabu kupitia Kituo cha Huduma za Afya cha Kabarak.
Mjukuu huyo wa Moi anataka pia aruhusiwe kuwaona watoto pamoja na kuwa nao wakati wa likizo za shule.
“Mshtakiwa atahakikisha watoto wanasajiliwa katika Shule ya Kabarak kwa elimu yao. Atashughulikia mahitaji ya matibabu ya watoto kupitia Kituo cha Huduma za Afya cha Kabarak na wazazi wote wawili wawe na uwezo wa kuwafikia watoto wakati wa likizo za shule,” akasema Bw Kibet kwenye mawasilisho mahakamani.
Bw Kibet pia anataka mama wa watoto hao Gladys Jeruto Tagi, kudumisha malezi halisi ya watoto. Anapendekeza wazazi wote wawili wachangie gharama za chakula, mavazi na burudani wanapokuwa na watoto.
Haya yanajiri baada ya mahakama kumwita Bw Kibet aeleze ni kwa nini asiadhibiwe kwa kukosa kutii amri ya kumtaka kutoa Sh 1.6 milioni kila mwaka kwa mahitaji ya watoto wake, ikiwa ni pamoja na elimu, matibabu na burudani.
Maagizo hayo yalitolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Bw Benjamin Limo, baada ya Bi Tagi kumshutumu Bw Kibet kwa kupuuza majukumu yake kama mzazi.
Mzozo huo uliongezeka na kusababisha Bw Kibet kukamatwa na kufungwa jela kwa wiki moja mnamo Septemba. Hukumu hiyo iliondolewa baadaye.
Katika utetezi wake, Bw Kibet ambaye ni mwana wa Jonathan Toroitich, alijitaja kuwa maskini na anayekumbwa na msongo wa mawazo.Alisema hana kazi, hana mahali pa kuishi na anategemea wasamaria wema.
Alisema matatizo yake yalianza baada ya kupoteza watu wa karibu wa familia yake akiwemo mama yake, baba yake, babu na shangazi yake ambao walikuwa wakimjali.
Hakimu Mwandamizi, Bw Kipkurui Kibet, alimwagiza Bi Tagi kujibu ombi la Kibet kabla ya kesi hiyo kutajwa Januari 15, 2025.
IMETAFSIRIWA NA BENSON MATHEKA
Mjukuu wa Moi alegeza msimamo, akubali kuwajibikia masuala ya ulezi wa wanawe
This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
EducationalTinubu: No student will be denied university education over poverty
Urges graduates to be creative, enterprising By Dayo Johnson, Akure President Bola Tinubu has assured Nigerians that no student will be denied access to tertiary education because of financial constraints. The President gave the assurance at the 37th convocation ceremony of the Federal University of Technology, Akure (FUTA), where he said the establishment of the […]
EducationalSEQUIP ilivyomfikisha Neema chuo kikuu
MBEYA: Serikali kupitia Mradi wa Kuinua Elimu ya Sekondari (SEQUIP) imeendelea kutoa fursa kwa wasichana waliokatisha masomo kutokana na changamoto mbalimbali za maisha kurejea shuleni na kuendeleza ndoto zao za elimu. Miongoni mwa wanufaika wa fursa hiyo ni Neema Andrea Usia, ambaye safari yake ya elimu ilikatizwa akiwa kidato cha pili, lakini kupitia fursa ya…
Educational892 graduates of CUHAS cadre pledge to observe ethics, dignity
MWANZA: 892 graduates of the Catholic University of Health Sciences Bugando (CUHAS) have been instructed to adhere to ethics, dignity and integrity in the provision of health services. The call was made today by the Bishop of the Catholic Diocese of Rulenge-Ngara, Mr Severine Niwemugizi, during the 19th graduation of the college held in Mwanza,…
EducationalChuka University graduate sits by himself, breaks down after no one shows up for his graduation
A Chuka University graduand broke down in tears after spending graduation day alone, as footage of him packing away a gown moved thousands of Kenyans online.