RAIS William Ruto jana alivitaka vyuo vikuu viwaruhusu wanafunzi walio na malimbikizi ya karo kufanya mitihani ya muhula huku akikiri kwamba vyuo vikuu vingi vinatatizika kifedha.
Huku akiahidi kujitolea kwa serikali kusaidia vyuo vikuu kutimiza wajibu wao wa kifedha, Rais Ruto alihusisha masaibu ya kifedha yanayovikabili vyuo vingi na kulimbikizwa kwa madeni na usumbufu uliosababishwa na mpito wa muundo mpya wa ufadhili wa elimu ya juu.
"Tunapopitia mabadiliko yaliyoletwa na muundo wa ufadhili wa elimu ya juu unaozingatia wanafunzi, nahimiza vyuo vikuu kuwa na subira na kuelewana na wanafunzi. Moyo wa kuzingatia binadamu ni muhimu hasa ikizingatiwa changamoto ya ziada inayoletwa na kesi ambayo inaweza kuvuruga utekelezaji wa muundo. Kwa hivyo, natoa wito kwa vyuo vikuu viwaruhusu wanafunzi kufanya mitihani yao ya mwisho wa muhula huku vikisubiri kurejelewa kwa malipo kamili pindi tutakapopata mwelekeo kuhusu suala hilo,” akasema akiwa Machakos mjini.
Rais Ruto alizungumza wakati alipoongoza mahafali ya Chuo Kikuu cha Scott Christian mjini Machakos. Makumi ya vijana walihitimu vyeti, stashahada na shahada baada ya kumaliza kozi za kilimo biashara, thiolojia, fiziolojia ya ushauri nasaha, usimamizi wa biashara na teknolojia ya habari na mawasiliano katika chuo hicho kinachohusishwa na AIC.
Rais Ruto alifichua kuwa baadhi ya vyuo vikuu vinakabiliwa na tishio la kufungwa kutokana na madeni makubwa. “Leo, serikali ya Kenya inadaiwa na chuo hiki zaidi ya Sh 460 milioni,” alisema.
"Najua hii imesababisha hasara kubwa kwa chuo kikuu hiki. Ndio maana nilichukua jukumu la kusuluhisha changamoto ambazo zilitatiza mfumo huo wa zamani. Mfumo wa zamani karibu ufanye vyuo vingi vifungwe. Ninafahamu kuwa chuo kikuu hiki kilifungwa kwa muda wa miezi michache. Na haikuwa sawa kwa sababu tulihusika kwa kutolipa deni kubwa la Sh 460 milioni tunalodaiwa na chuo hiki,” alisema.
IMETAFSIRIWA NA BENSON MATHEKA
Rais aagiza vyuo vikuu viruhusu wanafunzi wafanye mtihani
This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
EducationalTinubu: No student will be denied university education over poverty
Urges graduates to be creative, enterprising By Dayo Johnson, Akure President Bola Tinubu has assured Nigerians that no student will be denied access to tertiary education because of financial constraints. The President gave the assurance at the 37th convocation ceremony of the Federal University of Technology, Akure (FUTA), where he said the establishment of the […]
EducationalSEQUIP ilivyomfikisha Neema chuo kikuu
MBEYA: Serikali kupitia Mradi wa Kuinua Elimu ya Sekondari (SEQUIP) imeendelea kutoa fursa kwa wasichana waliokatisha masomo kutokana na changamoto mbalimbali za maisha kurejea shuleni na kuendeleza ndoto zao za elimu. Miongoni mwa wanufaika wa fursa hiyo ni Neema Andrea Usia, ambaye safari yake ya elimu ilikatizwa akiwa kidato cha pili, lakini kupitia fursa ya…
Educational892 graduates of CUHAS cadre pledge to observe ethics, dignity
MWANZA: 892 graduates of the Catholic University of Health Sciences Bugando (CUHAS) have been instructed to adhere to ethics, dignity and integrity in the provision of health services. The call was made today by the Bishop of the Catholic Diocese of Rulenge-Ngara, Mr Severine Niwemugizi, during the 19th graduation of the college held in Mwanza,…
EducationalChuka University graduate sits by himself, breaks down after no one shows up for his graduation
A Chuka University graduand broke down in tears after spending graduation day alone, as footage of him packing away a gown moved thousands of Kenyans online.