MAHAKAMA Kuu jijini Eldoret imempata na hatia mshukiwa mkuu wa mauaji ya mwanaharakati wa LGBT.
Mahakama ilimpata Jackton Odhiambo, mpiga picha wa kujitegemea na hatia ya mauaji ya Edwin Kiptoo, almaarufu Chiloba.
Mnamo Jumatano Jaji Reuben Nyakundi alitoa uamuzi wake mwaka mmoja tu baada ya mauaji hayo ya kutisha, ambayo yalizua hisia mesto kote duniani.
Akitoa uamuzi wake Jaji Reuben Nyakundi alisema mshukiwa huyo alikuwa mtu wa mwisho kuonekana na marehemu ambaye alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Eldoret kabla ya mwili wake uliokuwa umeharibika kupatikana siku sita baadaye ukiwa umetupwa kando ya barabara katika Kaunti ya Uasin Gishu..
Jaji Reuben Nyakundi alisema atahukumu mshtakiwa mnamo Decemba 16, 2024.
Bw Odhimabo alishtakiwa kwa kumuua Chiloba aliyekuwa akisomea shahada ya Mavazi, Mitindo na Ubunifu katika chuo cha kikuu cha Eldoret kaunti ya Uasin Gishu.
Alikana kumuua Chiloba ambaye anasemekana kuwa rafikiye wa chanda na pete kati ya Desemba 31, 2022 na Januari 3, 2023, katika nyumba za makazi za Noble Breeze Apartments eneo la Chebisaas, kaunti ndogo ya Moiben.
Mwili wa marehemu uligunduliwa kwenye sanduku la chuma kando ya barabara ya Kipkenyo-Kaptinga katika Kaunti Ndogo ya Kapseret mnamo Januari 3,2023.
Jaji alisema kuwa Odhiambo alimdhulumu Chiloba licha ya kuwa alimtaja kuwa rafiki yake wa karibu kabla ya kupanga njama ya kifo chake ambacho alisema kilikuwa cha kikatili katika nyumba ambayo walikuwa wakiishi pamoja.
Marehemu alikuwa na alama mikononi mwake ambazo ziliashiria kuwa alijaribu kujikinga akishambuliwa.
Jaji alitilia mkazo kuwa ushahidi uliowasilsihwa mahamanani ulithibitisha kuwa Odhiambo alimuua Chiloba.
Mshukiwa wa mauaji ya mwanaharakati wa LGBTQ Chiloba apatikana na hatia
This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
EducationalTinubu: No student will be denied university education over poverty
Urges graduates to be creative, enterprising By Dayo Johnson, Akure President Bola Tinubu has assured Nigerians that no student will be denied access to tertiary education because of financial constraints. The President gave the assurance at the 37th convocation ceremony of the Federal University of Technology, Akure (FUTA), where he said the establishment of the […]
EducationalSEQUIP ilivyomfikisha Neema chuo kikuu
MBEYA: Serikali kupitia Mradi wa Kuinua Elimu ya Sekondari (SEQUIP) imeendelea kutoa fursa kwa wasichana waliokatisha masomo kutokana na changamoto mbalimbali za maisha kurejea shuleni na kuendeleza ndoto zao za elimu. Miongoni mwa wanufaika wa fursa hiyo ni Neema Andrea Usia, ambaye safari yake ya elimu ilikatizwa akiwa kidato cha pili, lakini kupitia fursa ya…
Educational892 graduates of CUHAS cadre pledge to observe ethics, dignity
MWANZA: 892 graduates of the Catholic University of Health Sciences Bugando (CUHAS) have been instructed to adhere to ethics, dignity and integrity in the provision of health services. The call was made today by the Bishop of the Catholic Diocese of Rulenge-Ngara, Mr Severine Niwemugizi, during the 19th graduation of the college held in Mwanza,…
EducationalChuka University graduate sits by himself, breaks down after no one shows up for his graduation
A Chuka University graduand broke down in tears after spending graduation day alone, as footage of him packing away a gown moved thousands of Kenyans online.