TRA yawataka wafanyabiashara kuendelea kutatua changamoto bila kufunga maduka
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa wito kwa wafanyabiashara kuendelea kushirikiana na mamlaka hiyo na kutatua changamoto zinazowakabili bila migomo wala kufunga maduka ili kukuza sekta ya biashari. Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipakodi kutoka mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) makao makuu, Richard Kayombo wakati akizungumza na wafanyabiashara mbalimbali katika […]
The post TRA yawataka wafanyabiashara kuendelea kutatua changamoto bila kufunga maduka first appeared on Millard Ayo.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa wito kwa wafanyabiashara kuendelea kushirikiana na mamlaka hiyo na kutatua changamoto zinazowakabili bila migomo wala kufunga maduka ili kukuza sekta ya biashari.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipakodi kutoka mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) makao makuu, Richard Kayombo wakati akizungumza na wafanyabiashara mbalimbali katika maeneo yao ya biashara mjini Njombe.
“Ushirikiano wetu utatuwezesha kufika mahali tunapopataka bila mivutano,kugoma wala kufunga maduka kwasababu tunajenga nyumba moja”amesema Kayombo
Awali akizungumza na mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amesema, TRA imejiwekea malengo ya kukusanya kodi zaidi ya shilingi Trilioni 3.4 nchini kwa kipindi cha mwezi Disemba mwaka huu,hivyo wapo mkoani Njombe kwa ajili ya kuhimiza jambo hilo ili kuhakikisha wanapata mapato ya kutosha.
“Kwa mwezi huu lengo ni Trilioni 3.4 na ni lengo kubwa kuliko miezi mingine yote kwa hiyo hatuwezi kulifikia bila ya ushirikino, tuhamasishane ili tuweze kulitimiza,” alisema Kayombo.
Kayombo ametumia fursa hiyo kuwataka wafanyabiashara nchini kulipa kodi kwa hiari ili kuiwezesha serikali kutekeleza miradi ya maendeleo na uendeshaji wa shughuli za kiserikali kwa ujumla.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Kissa Kasongwa akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amesema serikali itaendelea kuhimiza wafanyabiashara na wananchi kulipa kodi.
“Lengo ni kuwaleta pamoja wafanyabiashara na kuondoa manung’uniko kwa hiyo watu wanalipa kodi ya hiyari yao, wanalipa kodi wakiwa na amani kwamba wanachangia kitu kwenye nchi yao,” alisema Kissa.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Halmashauri ya Mji Njombe, Eliud Pangamawe alisema pamoja na adha nyingine ambazo zinaikabili sekta hiyo lakini wao wanasisitiza mahusiano pamoja na kuhamasisha wafanyabiasha waendelee kulipa kodi.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Richard Kayombo yupo mkoani Njombe akiendelea na ziara yake ya kutembelea maduka mbalimbali pamoja na kuzungumza na wafanyabiashara kupitia mikutano ya wazi ili kuhakikisha lengo la makusanyo ya serikali linatimia.
The post TRA yawataka wafanyabiashara kuendelea kutatua changamoto bila kufunga maduka first appeared on Millard Ayo.