Chuo Kikuu cha Sokoine chamuenzi panya Magawa

Milard Ayo
Published: Dec 16, 2024 12:55:30 EAT   |  Educational

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na taifa kwa ujumla limepata sifa kubwa kwa miaka ya hivi karibuni kwenye suala la utafiti ukiwemo wa kumtumia panya namna ya kutafuta na kubaini vilipuzi na mabomu yalitotengwa ardhini. Miongoni mwa panya hao ni Magawa aliyesifika kusaidia kugunduliwa kwa zaidi ya mabomu 108 ya kutegwa ardhini nchini […]

The post Chuo Kikuu cha Sokoine chamuenzi panya Magawa first appeared on Millard Ayo.

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na taifa kwa ujumla limepata sifa kubwa kwa miaka ya hivi karibuni kwenye suala la utafiti ukiwemo wa kumtumia panya namna ya kutafuta na kubaini vilipuzi na mabomu yalitotengwa ardhini.

Miongoni mwa panya hao ni Magawa aliyesifika kusaidia kugunduliwa kwa zaidi ya mabomu 108 ya kutegwa ardhini nchini Cambodia na mchango wake unaruhusu jamii nchini Cambodia kuishi, kufanya kazi na kucheza bila hofu ya kupoteza maisha au kiungo.

Kwa kutambua mchango wake mnamo Septemba 2020, Shirika la Matibabu ya Wanyama la Uingereza lisilokuwa la kiserikali (PDSA), lilimtunza panya Magawa kutoka Tanzania medali ya dhahabu.

Tuzo hiyo ni kutokanana ushujaa wake kwa kujitolea kwake kuokoa maisha ya watu kupitia kazi yake ya kubaini ma bomu yaliyotegwa ardhini nchini Cambodia.

Kwa mujibu wa Taasisi isiyo ya Kiserikali inayofundisha Panya Kutatua Matatizo ya Kibinaadamu (APOPO), imeeleza kuwa Magawa alifunzu mitihani yake mwaka 2016.

The post Chuo Kikuu cha Sokoine chamuenzi panya Magawa first appeared on Millard Ayo.