IMF yapongezwa kwa kubuni miradi mbalimbali

Milard Ayo
Published: Dec 17, 2024 07:14:55 EAT   |  Educational

Mwanajumuiya wa Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM) (Alumni) Abdulmajid Nsekela amempongeza Mkuu wa chuo hicho Profesa Josephat Lotto na timu yake kutokana na kubuni mikakati mbalimbali kwa ajili ya kuboresha elimu nchini. Nsekela ameyazungumza hayo wakati wa hafla ya chakula cha jioni ya wanafunzi waliosoma zamani katika chuo hicho ,iliofanyika usiku wa kuamkia leo […]

The post IMF yapongezwa kwa kubuni miradi mbalimbali first appeared on Millard Ayo.

Mwanajumuiya wa Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM) (Alumni) Abdulmajid Nsekela amempongeza Mkuu wa chuo hicho Profesa Josephat Lotto na timu yake kutokana na kubuni mikakati mbalimbali kwa ajili ya kuboresha elimu nchini.

Nsekela ameyazungumza hayo wakati wa hafla ya chakula cha jioni ya wanafunzi waliosoma zamani katika chuo hicho ,iliofanyika usiku wa kuamkia leo jijini Dodoma.

Nsekela amesema mkakati wa kushawishi wanafunzi wapende somo la hisabati lakini pia kukifahamu chuo hicho ni mzuri kutokana na kwamba utaongeza wigo wa wanafunzi kujiunga na chuoni hapo kusoma kozi mbalimbali zinazotolewa.

Aidha alisema wao kama Alumni watashirikiana pamoja na IFM ili kuhakikisha chuo hiko kinazidi kutanua wigo wa utoaji elimu ndani na nje ya nchi ili kuzalisha wataalamu wengi wa masuala ya fedha.

“Nampongeza mkuu wa chuo kutokana na kubuni mikakati mbalimbali ya kuboresha chuo hiko,”alisema Nsekela.

Kuhusu fedha milioni 52.8 zinazohitajika kwa ajili ya mkakati wa kupeleka conter book shuleni ili kushawishi wanafunzi kupenda kusoma hisabati na kuifahamu IFM,Nsekela aliendesha harambee kwa Alumni hao,ambapo ahadi zilipatikana shilingi milioni 36,huku fedha tasilimu zilipatikana shilingi milioni nane.

Kwa upande wa Mkuu wa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM),Profesa Josephat Lotto amewaomba Alumni waliosoma katika chuo hiko,ambao wapo katika ofisi mbalimbali,kuhakikisha wanawasimamia wanafunzi wanaoenda kufanya mafunzo kwa vitendo ili kupata uzoefu,badala ya kuwatuma kukoroga chai na kubeba mafaili.

Profesa Lotto amesema wanafunzi hao wanapoenda katika ofisi mbalimbali kwa ajili ya kufanya mafunzo kwa vitendo ya fani walizosomea wengi wanaishia kutumwa mafaili na kukoroga chai jambo linalopelekea kushindwa kupata kile alichokusudia na kurudi chuoni akiwa hana kitu.

“Hili suala linasikitisha sana kwa sababu wanafunzi wanarudi chuoni wakiwa hawajapata kitu,naomba nyie kama alumni mliopo katika ofisi mbalimbali kuwasaidia wanafunzi hao ili wakihitimu waweze kuajirika au kujiajiri wao wenyewe,”alisema Profesa Lotto.

  

The post IMF yapongezwa kwa kubuni miradi mbalimbali first appeared on Millard Ayo.