WAZEE katika Kaunti ya Lamu wamelalamikia kusahaulika kwa elimu ya watu wazima, almaarufu ngumbaru.
Wazee hao wamedai kwamba katika miaka ya hivi majuzi, serikali na Wizara ya Elimu imeipa kipaumbele utekelezaji wa mtaala mpya wa CBC ilhali ngumbaru haikumbukwi.
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Lamu, Mohamed Mbwana, alishikilia kuwa elimu ya watu wazima ni kiungo muhimu kwenye mipango ya maendeleo ya taifa lolote lile. Alisema elimu hiyo ni muhimu kupewa uzito sawa na elimu nyinginezo zinazotiliwa mkazo.
[caption id="attachment_164948" align="alignnone" width="1828"] Wanafunzi wakihudhuria darasa katika kituo cha mafunzo ya watu wazima cha Kapserton Adult Basic Education Centre eneo la Kipkaren Celian mjini Nandi mnamo 2013. PICHA | MAKTABA[/caption]
Bw Mbwana alieleza kutoridhishwa kwake na jinsi wazee wengi Lamu bado hawajui kusoma na kuandika, hali ambayo inawaathiri kimaisha na hivyo pia kuathiri maendeleo ya kitaifa.
“Elimu ya ngumbaru ililetwa nchini kusudi likiwa ni kuleta nuru hasa kwa wengine wetu ambao tulidhania hatutajua kusoma au kuandika maishani. Mimi binafsi imenisadia pakubwa.
“Ila miaka ya sasa hatujaona tena msukumo wa elimu ya watu wazima. Utasikia kote mkazo ukiwekwa kwa mtaala wa CBC. Sisi wazee mumetuweka wapi? Lazima mtuzingatie pia. Ni muhimu elimu ya ngumbaru itiliwe mkazo pia,” akasema Bw Mbwana.
[caption id="attachment_164949" align="alignnone" width="2000"] Wanafunzi wa Sekondari Tangulizi wakati wa somo ndani ya maabara ya sayansi katika Shule ya Msingi ya Bomu eneo la Changamwe mjini Mombasa, mnamo Januari 2024. PICHA | KEVIN ODIT[/caption]
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Elimu katika Kaunti ya Lamu, Bw Zachary Mutuiri, aliwataka wazee wajiandikishe kupokea elimu hiyo akisisitiza kuwa serikali inaithamini.
Alisema elimu ya ngumbaru inaendelea na akawataka wazee wenye kiu ya elimu hiyo kujitokeza.
“Wanaolalamika huenda hawajajitokeza wazi kujisajili kupokea mafunzo ya ngumbaru. Elimu ya ngumbaru ipo Lamu. Wazee hata wana afisa wao maalumu.
“Ningewasihi wenye kiu ya elimu hiyo wajitokeze na watahudumiwa,” akasema Bw Mutuiri.
Kassim Shee, 75, mzee wa Kizingitini, Lamu Mashariki, anataja kutojua kusoma na kuandika kuwa kikwazo kikubwa katika harakati za kuimarisha huduma za jamii nchini. Anasema ari yake ni kutafuta hiyo elimu ya ngumbaru kwani miaka ya ujana wake hakuweza kukanyaga darasani.
Kinachomtia wasiwasi ni mahali pa kuipata elimu hiyo, akidai kuwa kwao Kizingitini hajaona kituo chochote au mwalimu wa ngumbaru wa kuwawezesha kuipata elimu wanayotafuta.
[caption id="attachment_164951" align="alignnone" width="2000"] Watahiniwa wenye umri wa watu wazima na wa kibinafsi baada ya kumaliza mtihani wa mwisho wa KCPE 2015 katika Shule ya Msingi ya Nyamasaria mjini Kisumu. PICHA | MAKTABA[/caption]
“Nina kiu ya elimu niliyoiacha miaka mingi iliyopita. Nataka kurudi darasani ila hawa walimu au vituo vya ngumbaru hatuvioni tena. Serikali ifanye juhudi kutuanzishia upya mpango huo. Wasitusahau,” akasema Bw Shee.
Kwa upande wake, Bi Khadija Hussein, 56, anasema hatua ya wanawe na wajukuu wake kuongea Kiingereza mfululizo kila wanapokaa naye kunamfanya kuwa na msukumo wa kutaka kurudi darasani, asome na kuifahamu vyema lugha hiyo.
“Sitaki kusengenywa mimi. Watoto na wajukuu zangu wanapoongea Kingereza nyumbani ninahisi upweke. Siwezi kuchangia kwa sababu sijui hata kinachozungumziwa. Na ndiyo sababu nataka nirudi ngumbaru, nisome ili nijue angalau neno moja moja la Kiingereza,” akasema Bi Hussein.
Wakongwe walia ngumbaru imesahaulika CBC ikipewa kipaumbele
This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
EducationalTinubu: No student will be denied university education over poverty
Urges graduates to be creative, enterprising By Dayo Johnson, Akure President Bola Tinubu has assured Nigerians that no student will be denied access to tertiary education because of financial constraints. The President gave the assurance at the 37th convocation ceremony of the Federal University of Technology, Akure (FUTA), where he said the establishment of the […]
EducationalSEQUIP ilivyomfikisha Neema chuo kikuu
MBEYA: Serikali kupitia Mradi wa Kuinua Elimu ya Sekondari (SEQUIP) imeendelea kutoa fursa kwa wasichana waliokatisha masomo kutokana na changamoto mbalimbali za maisha kurejea shuleni na kuendeleza ndoto zao za elimu. Miongoni mwa wanufaika wa fursa hiyo ni Neema Andrea Usia, ambaye safari yake ya elimu ilikatizwa akiwa kidato cha pili, lakini kupitia fursa ya…
Educational892 graduates of CUHAS cadre pledge to observe ethics, dignity
MWANZA: 892 graduates of the Catholic University of Health Sciences Bugando (CUHAS) have been instructed to adhere to ethics, dignity and integrity in the provision of health services. The call was made today by the Bishop of the Catholic Diocese of Rulenge-Ngara, Mr Severine Niwemugizi, during the 19th graduation of the college held in Mwanza,…
EducationalChuka University graduate sits by himself, breaks down after no one shows up for his graduation
A Chuka University graduand broke down in tears after spending graduation day alone, as footage of him packing away a gown moved thousands of Kenyans online.