
Samia kuzindua sera ya elimu na mafunzo kesho
RAIS Samia Suluhu Hassan kesho anatarajia kuzindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023.…
Category
Education policy, exam results and calendars, scholarships and opportunities for students, parents and teachers across the region.

RAIS Samia Suluhu Hassan kesho anatarajia kuzindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023.…
HATUA ya kuvunja uhusiano wa kimapenzi au talaka kwenye ndoa huwa ngumu kwa wanaume ikilinganishwa na wanawake, watafiti wamebaini. Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Humboldt, Berlin Ujerumani, waligundua kuwa wanaume huthamini na wanajali sana kuwa kwenye uhusiano kuliko wanawake. Utafiti huu unayeyusha dhana ambayo imekuwepo kuwa wanawake ndio huridhika sana kuwa kwenye mapenzi kuliko wanaume. Hata hivyo, wanaume huhisi sana upweke na huathirika kabisa kisaikolojia ikilinganishwa na wanawake baada ya mapenzi kuisha kwa mujibu wa utafiti huu mpya. Kuibuka na hoja hii, wanayasansi zaidi ya 50 kutoka Chuo Kikuu cha Humboldt, walizamia na kutathmini tofauti za kijinsia kwenye mahusiano kati ya wanaume na wanawake. Wanaume baada ya ‘kuachwa’ huanza kumsaka mpenzi mwengine kwa sababu wanasaka faraja na manufaa waliyokuwa nayo kwenye penzi la zamani. “Tunafahamu kuwa wanawake hupata sapoti au ushauri wa kisaikolojia kutokana na mazingira ya kijamii. Hii ni kinyume kwa wanaume ambao hisia zao hutegemea sana kuwa katika uhusiano na wanawake,” utafiti huo unaeleza. “Kwa kifupi, uhusiano dhabiti huwa ni muhimu kisaikolojia kwa wanaume kuliko wanawake,” unaongeza. Upweke na mara nyingi kukosa manufaa ambayo yalikuwepo kabla ya kuvunjika kwa uhusiano wa kimapenzi ndio huwaponza wanaume. Pia ni rahisi wanawake kuwaendea mama, rafiki, baba, mtaalamu wa afya ya kiakili au mwanafamilia yeyote ili hisia zao zitulizwe baada ya kuvunjika kwa uhusiano. Wanaume nao mara nyingi hujitenga na kuendelea na maisha yao huku wakiumia ndani kwa ndani bila kumwaga mtama kwa yeyote. “Ni jambo ambalo limekuwepo tangu utotoni katika jamii kuwa wanawake wapo radhi kuzungumzia matatizo yao na kusaidiana kihisia, kuliko wanaume. Utafiti huu unaongezea kwa zile za nyuma ambazo zimeweka wanaume kama wenye nguzo katika uhusiano na hujali hatima ya mapenzi kuliko wanawake. Tafiti za awali pia zimeonyesha kuwa kuwa kwenye uhusiano huimarisha afya ya kiakili kwa wanaume. Hii ndiyo maana wanaume ambao wapo kwenye ndoa, imebainika huwa hawazeeki mapema wakilinganishwa na makapera.

SERIKALI imeiwezeshaTaasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) Sh bilioni 21.8 kwa kipindi cha miaka minne ili kutekeleza…
ZAIDI ya wavulana 200 kutoka Shule ya Upili ya Wavulana ya AIC Cheplaskei walihatarisha maisha yao baada ya kutembea mwendo wa kilomita 20 hadi Makao Makuu ya Kaunti ya Uasin Gishu jijini Eldoret kupinga mpango wa kumhamisha mwalimu wao mkuu waliyemtaja kama mzazi stadi na msimamizi bora. Wanafunzi hao waliojawa na ghadhabu walitembea kwa zaidi ya kilomita 20 kutoka Cheplaskei, kaunti ndogo ya Kesses hadi jijini Eldoret walishutumu baadhi ya wanachama wa bodi ya usimamizi kwa kuendeshwa na ukabila kupanga njama ya kuhamisha mwalimu wao mkuu kwa madai ya kuwa anatoka katika kabila jingine. [caption id="attachment_167056" align="alignnone" width="1504"] Wanafunzi wa Cheplaskei A.I.C Boys waliotembea kwa umbali wa kilomita 20 usiku kulalamikia kuhamishwa kwa mwalimu mkuu. Picha|Jared Nyataya[/caption] “Lengo letu ni kufaulu katika elimu hatujali mkuu wetu anatoka katika kabila gani, baadhi ya wafadhili wa shule yetu wameungana kupanga njama za uhamisho wa mkuu wetu mpya kwa manufaa ya baadhi ya wasimamizi wa shule yetu, iwapo watashawishi uhamisho wa mwalimu mkuu hatutakubali kukaa darasani,” alisema mmoja wa wanafunzi hao alipokuwa akihutubia Mkurugenzi wa Elimu Kaunti ya Uasin Gishu John Thiringi. Kwa pamoja walitaka naibu mwalimu mkuu pamona mhasibu wa shule wahamishwe badala ya mwalimu mkuu. Walidai kuwa wanaotaka mwalimu mkuu kuhamishwa hawapendi sera yake ya kutaka walimu kukamilisha silabasi kwa wakati hasa kwa watahiniwa wa Kidato cha Nne. Wanafunzi hao ambao hawakuwahi kuhudhuria masomo tangu Jumatatu walifanya maandamano mafupi katika shule hiyo na kusababisha uharibifu wa mali. Kwa pamoja walisema wanaridhishwa zaidi na Mwalimu Mkuu wao wa sasa, Bw Nathan Oguye ambaye amechukua nafasi ya mwalimu mkuu mstaafu George Oloo. Bw Thiringi aliwaomba kurudi shuleni huku akiahidi kushughulikia matakwa yao. Wanafunzi hao walirejeshwa shuleni kwa mabasi sita kutoka shule mbalimbali katika kaunti ya Uasin Gishu.
Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Iringa Bw. Reginaldo Msendekwa amefungua mafunzo kwa walimu wa sayansi na hisabati na kuwataka washiriki hao kwenda kuyatumia mafunzo hayo kuimarisha taaluma hususani matumizi ya TEHAMA shuleni. Akifungua mafunzo hayo Januari, 25 2025 katika chuo cha Ualimu Kleruu kilichopo katika Manispaa ya Iringa amewaasa washiriki hao kwenda kuyatumia mafunzo watakayoyapata […] The post Walimu waaswa matumizi ya Tehama mashuleni first appeared on Millard Ayo.
Na Mwandishi Wetu Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu CPA Amos Makalla leo tarehe 27 Januari 2025 ameanza ziara ya siku mbili Visiwa vya Pemba akianzia Kusini Pemba . Makalla akiwa kusini Pemba amefanya ukaguzi wa Miradi ya kimkakati akianzia Shule ya Kisasa na ya Mfano ya Ole sekondari iliyopo […]
Nimepokea taarifa ya vifo vya watoto wetu wa Businda sekondari kwa masikitiko makubwa. Naomba kuwapa pole sana wazazi, walezi, walimu, wanafunzi wa shule ya sekondari Businda na ndugu wote waliguswa na msiba huu mkubwa Vifo vya vijana wetu vimetushtua sana wana Bukombe wote Tunawaombea faraja familia zote zilizofikwa na msiba huu aidha, tunawaombea uponyaji wa […] The post Dkt Biteko atoa pole kwa Wanabukombe kufuatia tukio la radi first appeared on Millard Ayo.
Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu CPA Amos Makalla leo tarehe 27 Januari 2025 ameanza ziara ya siku mbili Visiwa vya Pemba akianzia Kusini Pemba . Makalla akiwa kusini Pemba amefanya ukaguzi wa Miradi ya kimkakati akianzia Shule ya Kisasa na ya Mfano ya Ole sekondari iliyopo jimbo la Chake […] The post Mwenezi Makalla akagua miradi ya kimkakati mkoa wa Kusini Pemba first appeared on Millard Ayo.
Imeelezwa kuwa Kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia imesaidia na kuibua Migogoro na changamoto za kisheria Elfu 9 na 69 toka mwaka 2023 ilipoanzishwa ambapo kampeni hiyo imekuwa Mkombozi kwa wananchi kutatuliwa migogoro kisheria pamoja na kupewa elimu hiyo. Hayo yameelezwa na Mwakilishi wa Naibu Waziri Mkuu ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa […] The post Migogoro 9069 yaibuliwa katika kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia tangu 2023 first appeared on Millard Ayo.
BARAZA la Kitaifa la Mtihani Kenya (Knec) limetangaza kuanza kwa usajili wa watahiniwa wa Gredi 6, kuanzia Januari 27 hadi Februari 28, 2025. Watahiniwa wa Gredi 6 hufanya Tathmini ya Elimu ya Shule ya Msingi Kenya (KPSEA) mwishoni mwa shule ya msingi, kabla ya kujiunga na shule ya Sekondari Msingi. Katika taarifa, Afisa Mkuu Mtendaji wa Knec David Njengere alisema kuwa watahiniwa lazima watimize vigezo vyote. Alionya kuwa kusajili watahiniwa hewa ni kosa, jambo ambalo linaweza kusababisha kufutwa kwa usajili wa shule zinazohusika. "Wanafunzi wote walio katika Gredi 6 watasajiliwa upya kwa tathmini hiyo kupitia tovuti ya usajili ya KPSEA ambayo itafikiwa kati ya Januari 27 na Februari 28 2025," alisema. Wanafunzi katika Gredi 6 wanahitajika kujiandikisha kwa KPSEA, tathmini iliyoundwa ili kutathmini umahiri wao kabla ya kujiunga na Sekondari Msingi. Mchakato huo unahusisha kuthibitisha maelezo muhimu, ikiwa ni pamoja na majina, vyeti vya kuzaliwa na hati nyingine muhimu, ili kuhakikisha usahihi wa usajili. “Marekebisho ya data ya wasifu wa mtahiniwa lazima yafanywe wakati wa usajili ili kuhakikisha usahihi wa habari zilizowasilishwa ikiwa ni pamoja na mpangilio sahihi wa majina ya wanafunzi kama yalivyoandikwa katika vyeti vyao vya kuzaliwa, jinsia, mwaka wa kuzaliwa, uraia, chaguo la elimu ya dini na wenye mahitaji maalum na walemavu,” alisema. Dkt Njengere pia aliagiza uhamisho wa watahiniwa ukamilishwe kabla ya kufungwa kwa tovuti ya usajili mnamo Februari 28, 2025, ili kuhakikisha mchakato wa usajili unafanyika kwa uwazi. "Hakuna uhamisho utakaoruhusiwa baadaye, zaidi mchakato wa uhamisho lazima ufanyike mtandaoni, ili kuepuka kurudiwa kwa watahiniwa,” alisema. Zaidi ya hayo, alisema kuwa shule zilizo na watahiniwa chini ya watano hazitaruhusiwa kusajili watahiniwa wa KPSEA 2025 kama vituo huru. “Shule zilizo na chini ya wanafunzi 5 hazitaruhusiwa kusajili watahiniwa wa KPSEA 2025 kama vituo huru vya kutathmini. Shule kama hizi zinashauriwa kuwasiliana na wakurugenzi wa elimu wa kaunti zao ili kutambua vituo vya kutathmini vya Knec vilivyo na zaidi ya watahiniwa 5 kwa usajili wa wanafunzi wao,” akasema. IMETAFSIRIWA NA BENSON MATHEKA

Na Nora Damian, Mtanzania Digital Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Profesa Bonaventure Rutinwa amewahimiza Watanzania kujifunza lugha ya Kichina na kupata ujuzi juu ya utamaduni na mila zake. Amesema tayari Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetangaza Kichina kuwa miongoni mwa lugha za kigeni kufundishwa katika shule za msingi […]

MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala amewataka wananchi mkoani humo kujitokeza kwa wingi kupata elimu na…

UTOAJI wa elimu ya kisheria kwa wananchi mkoani wa Mtwara kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama…

Shirika la Haki Elimu, kwa kushirikiana na serikali ya Canada kupitia taasisi ya Global Affairs Canada, limezindua Mradi wa Mageuzi ya Usawa wa Kijinsia katika Elimu (MMUKE). Mradi huu utagharimu Dola za Canada Milioni 4.5 (takribani Shilingi Bilioni 7.8 za Kitanzania). Lengo lake kuu ni kuboresha mazingira ya elimu, hasa kwa wasichana, kwa kuhakikisha miundombinu […] The post “Haki Elimu yatoa Bil.7 kukabiliana na vitendo vya Ukatili Kwa watoto Mashuleni” first appeared on Millard Ayo.
SHULE za umma kote nchini zinakabiliwa na hali ngumu kifedha baada ya serikali kuchelewa kutoa fedha kabla ya muhula wa kwanza kuanza ilivyokuwa imeahidi. Ucheleweshaji huo umeweka zaidi ya shule za Msingi za umma 23,000 na karibu shule 10,000 za sekondari katika hali mbaya ya kifedha, na hivyo kulazimu nyingi kukopa kukidhi shughuli za kimsingi. Hii inafuatia kutotimizwa kwa ahadi ya Waziri wa Elimu Julius Ogamba kuwa pesa hizo zingetolewa kabla ya shule kufunguliwa, huku Waziri wa Fedha John Mbadi akitoa hahakikisho kuwa fedha za muhula wa kwanza zingetolewa ndani ya wiki ahadi ambayo haijatimizwa. “Wiki ijayo Hazina itatoa Sh48.8 bilioni ambayo ni asilimia 50 ya mgao wa mwaka huu kufadhili mfumo wetu wa elimu,” alisema Waziri Mbadi mnamo Januari, 17, 2025. Mwenyekiti wa Kitaifa wa Chama cha Walimu Wakuu wa Shule za Msingi nchini Kenya (KEPSHA) Johnson M. Nzioka ameeleza wasiwasi wake kuhusu matatizo ya kifedha yanayokabili shule za umma, akisema kucheleweshwa kwa fedha kumeongezea presha wasimamizi wa shule. Bw Nzioka alilalamika kuwa serikali haijatimiza ahadi yake jambo ambalo limeacha shule nyingi na changamoto tele. “Serikali ilituhakikishia kwamba fedha zingetolewa kabla ya muda kuanza, lakini haikuwa hivyo, tuliahidiwa fedha zingetolewa ndani ya wiki moja, bado wiki imegeuka mwezi, sasa hivi shule zinaendeshwa kwa mkopo, na hii inaathiri pakubwa ari ya walimu na ubora wa elimu,” alisema. Kulingana na Bw Nzioka, shule za msingi za umma zinatatizika kukidhi mahitaji ya kimsingi, ikiwa ni pamoja na kulipa wauzaji bidhaa na kudumisha huduma muhimu. Walimu pia wanateseka. “Serikali inatarajia shule zifanyeje? Tulifunga shule bila fedha jam,bo ambalo ni aibu. Wauzaji wanakuja ofisini kwetu wakitaka malipo,” akasema Bw Nzioka. Aliomba serikali kuharakisha kutoa fedha ili kuzuia hali kuwa mbaya zaidi akisema kuna umuhimu wa kuwa na mkakati endelevu wa kuhakikisha fedha zinatolewa kwa wakati. Alionya kuwa tatizo la fedha lililopo sasa linaweza kusababisha madhara ya muda mrefu kwa sekta ya elimu. “Hatuwezi kuendelea kufanya kazi namna hii, shule ziko katika hali mbaya na imani katika mfumo wa elimu inapungua, tunahitaji hatua za haraka,” akasema Bw Nzioka. Mwalimu mkuu mmoja katika kaunti ya Bungoma alieleza hali mbaya ya shule katika eneo hilo kutokana na ukosefu wa rasilimali muhimu na usaidizi kutoka kwa serikali. "Sijui jinsi serikali inataka tufanye kazi kwa sababu hakuna vitabu, hatuna hata lango, na walinzi wawili walijiuzulu. Niko kwa shida kwa sababu walimu hawana hata chaki. Inabidi wachangie pesa ili tununue chakula cha mchana. Ni aibu kusema,” alisema. Mwenyekiti wa Chama cha Wakuu wa Shule za Sekondari Kenya (KESSHA) Willy Kuria ameitaka Wizara za Fedha na Elimu kulipa malimbikizi ya Sh64 bilioni ambazo haijalipa kwa muda wa miaka minne. Alisema kuwa shule nyingi zinadaiwa kuanzia Sh20 milioni hadi Sh70 milioni, huku baadhi ya wakuu wa shule wakiaibishwa na wauzaji bidhaa. “Serikali lazima iachilie Sh64 bilioni kusaidia shule kulipa madeni. Tunatatizika kulipa madeni na bili kama vile za maji na umeme,” akasema Bw Kuria.
Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital SHULE Sekondari Feza Boys imejivunia uwekezaji iliyofanya katika kumuandaa mwanafunzi kuwa bora baada ya kufaulisha wanafunzi wote kwa kupata daraja la kwanza katika mtihani wa Taifa wa kidato cha nne ulifanyika mwaka 2024, huku zaidi ya asilimia 65 wakipata division 1.7. Hayo ameyasema Makamu Mkuu wa Shule ya FEZA Boys, […]

DAR ES SALAAM: The National Examinations Council of Tanzania (NECTA) has reported a significant improvement in the Form…
MIAKA sita tangu mwalimu Peter Tabichi kushinda tuzo ya mwalimu bora duniani, mwalimu mwingine kutoka nchini Kenya ameteuliwa kuwania tuzo hiyo ya hadhi. Bw Dominic Orina, ambaye ni mwalimu wa kilimo katika Shule ya Msingi ya Kugerwet, inayopatikana katika eneobunge la Konoin, katika kaunti ya Bomet ni miongoni mwa walimu 50 wa mwisho katika uteuzi huo. Mshindi wa tuzo hiyo iliyoanzishwa miaka minane iliyopita, hukirimiwa Sh129 milioni kutokana na ubunifu wao ambao huchangia kwa njia za kipekee katika kazi yao. Akiongea na Taifa Leo baada ya uteuzi wake, Bw Orina aliwataka Wakenya kumuombea ili aibuke mshindi. “Ndugu zangu Wakenya, nitilie dua ili niitwae zawadi hii. Ikiwa nitatangazwa mshindi, ushindi wangu hautakuwa wangu pekee bali kwa nchi yetu nzima,” Orina alisema. Tangu alipoajiriwa katika Shule ya Kugerwet mwaka 2017, Bw Orina aliwaongoza wanafunzi wake kuanzisha mradi wa ukuzaji mboga na ufugaji sungura. Alifanikisha hili kufuatia ufufuzi wa chama cha 4K shuleni humo. Kutokana na kauli mbiu ya chama hicho ya Kuungana, Kufanya na Kusaidia Kenya, mwalimu huyo amefanikiwa kuwajenga wanafunzi hao kuwa na moyo wa kujitegemea na kuzalisha mboga kwa wingi kwa matumizi yao shuleni na nyumbani. Bw Orina ambaye ni mzawa wa kaunti ya Nyamira, anafahamika sana mitandaoni kutokana na kazi yake ya kukuza mboga kwenye magunia na karatasi za plastiki. Mwaka 2020, mwalimu mwingine wa Kenya Linah Anyango naye alikuwa miongoni mwa washindani wengine 50 walioteuliwa kuwania taji hiyo. Bw Orina vilevile, amekuwa akitumia mitandao ya kijamii kuwarai wahisani kuwanunulia sare baadhi ya wanafunzi wake wanaotoka katika familia zisizojiweza.

MAOFISA Uchaguzi mkoani Mtwara wamepatiwa mafunzo juu ya uendeshaji na usimamizi wa zoezi la uboreshaji wa daftari la…

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo ikiongozwa na Mwenyekiti Husna Sekiboko imekutana na Uongozi…
WANAUME wakongwe ambao hunywa sharubati ya zabibu (grape juice) wanapunguza uwezekano wa kuandamwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume, Utafiti umebaini. Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Tianjin, Kaskazini mwa China, walisema kuwa wanaume ambao walikunywa sharubati ya zabibu mara tano kwa siku au hata zaidi kwa wiki, walipunguza tatizo la kukosa hamu wakati wa tendo la ndoa. Wanaume 300 wenye tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume walihusishwa na wengine 300 ambao wako sawa. Ilibainika kuwa wale waliokunywa sharubati ya zabibu kwa zaidi ya mara tano waliimarisha uweledi wao wa kusakata ngoma chumbani kuliko jinsi ambavyo walikuwa hapo awali. Ukosefu wa nguvu za kiume ni tatizo ambalo huwakumba sana wanaume wazee hasa wenye umri wa miaka 60 na zaidi. Kwa mujibu wa takwimu kutoka Taasisi ya Kitaifa ya Kenya, asilimia 95 za wanaougua ugonjwa wa moyo huwa wana tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. “Sharubati ya zabibu haina kemikali hatari na ina madini ambayo yana manufaa kiafya. Ile ya zabibu nyekundu ni nzuri zaidi kwa sababu ina kemikali ambazo zinazuia seli muhimu kuharibiwa,” utafiti huo ulioendeshwa na kikosi cha wataalamu na watafiti wakiongozwa na Liwei Wua ulieleza. Watafiti hao pia walichunguza umuhimu wa sharubati ya nyanya, matunda, machungwa, limau na paipai lakini ile ya zabibu ndiyo ilipatikana kuwa na manufaa kwa waliopungukiwa na hamu ya kufanya mapenzi. Aidha watafiti pia walichunguza maziwa na aina mbalimbali za soda lakini bado wakapata sharubati ya zabibu ndiyo huwasaidia wanaume kuongeza ashiki. Wakati wa utafiti huo, ilipatikana sharubati nyekundu ya zabibu pia husaidia kuepesha magonjwa ya moyo kwa kuimarisha usambazaji wa damu mwilini kwa kuzuia mishipa kuzibwa kwa mafuta.
Mpenzi hajali mahitaji yangu ingawa ana pesa nyingi. Ajabu ni kwamba tukiwa maskani za starehe huwa anatumia pesa nyingi, sio kwangu tu bali kwa marafiki zake. Ananipenda kweli? Mpenzi wako amekuonyesha wazi kuwa ni mgumu wa kutoa pesa. Hayo ni maumbile yake na usitarajie kuwa atabadilika. Akikuoa hali hiyo inaweza kuleta ugomvi kati yenu. Fanya uamuzi unaofaa. Niolewe kwa sababu ya mimba au nibaki shule? Mimi ni mwanafunzi wa shule ya upili. Mpenzi wangu amenipachika mimba na yuko tayari kunioa. Lakini wazazi wangu wamekataa, wanasisitiza nirudi shule baada ya kujifungua. Nahofia ataniacha. Usikubali kukatiza masomo kwa sababu ya ndoa. Umekuwa shuleni kwa miaka mingi na itakuwa hasara kwako na kwa wazazi wako kuachia njiani. Fuata ushauri wa wazazi. Kama mpenzi wako hawezi kusubiri ni heri muachane. Mama ananikwamilia hata niolewe Nina mpenzi na anataka kunioa. Lakini mamangu anapinga kwa sababu mimi ndiye mtoto wake wa pekee. Anaogopa kuachwa peke yake. Nifanyeje? Hatua ya mamako inaonyeshawazi kwamba anajali maslahi yake kuliko yako. Endelea na mipango yako na umhakikishie utakuwa ukimtembelea. Ameniacha kwa simu Mpenzi wangu amevunja uhusiano wetu baada ya miezi mitatu tu. Alifanya hivyo kupitia simu akaniambia nimsahau. Sikutarajia hatua yake hiyo, nina maumivu makali moyoni. Ni haki ya mtu kuchagua kupenda ama kutopenda. Mpenzi wako amekueleza wazi kwamba hakutaki na huwezi kumbadili nia. Heshimu uamuzi wake na uendelee na maisha yako.
MOTO mkubwa uliozuka umechoma sehemu ya jengo la Gandhi Wing katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Jengo hilo ambalo linatambuliwa mno na ambalo lina afisi za wahadhiri, vyumba vya masomo na afisi zingine nyingi za usimamizi wa kimasomo liligubikwa na moto mkali ambao ulionekana hata kwa umbali. Muda mfupi baadaye, zimamoto waliwasili na video za wapita njia zilionyesha zimamoto hao wakipambana kudhibiti miale mikali. Afisa wa mawasiliano John Orindi amethibitisha kufikia wakati wa kuandika taarifa hii kwamba moto huo umedhibitiwa ingawa chanzo bado hakijabainika.

Maafisa kutoka TBS na ZBS wakitoa elimu kwa wajasiriamali juu ya umuhimu wa kuwa na alama ya ubora katika maonesho ya 11 ya biashara yanayoendelea visiwani Zanzibar. The post TBS watoa elimu kwa Wajasiriamali Zanzibar (picha) first appeared on Millard Ayo.

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema serikali itawasilisha mabadiliko ya Sheria ya Elimu Na…

WAKATI jana wanafunzi kote nchini wakianza muhula mpya wa masomo, hali ni tofauti kwa Shule ya Sekondari ya…

Idadi ya watu waliouawa huko Gaza kwenye mashambulizi mabaya ya Israeli katika eneo la Palestina ni kubwa zaidi kuliko takwimu zilizoripotiwa na mamlaka ya afya ya eneo hilo, watafiti katika chuo kikuu cha afya nchini Uingereza wamegundua. Katika utafiti uliopitiwa na rika uliochapishwa Alhamisi katika jarida la The Lancet, watafiti katika Chuo cha London School […] The post Idadi ya vifo Gaza inaweza kuwa 41% juu kuliko takwimu rasmi :utafiti first appeared on Millard Ayo.
WAFANYAKAZI 43 katika shule ya jamii ya Gatoto eneo la Mukuru kwa Reuben, Embakasi Kusini wamebaki katika hali ya sintofahamu kuhusu hatma yao baada ya wasimamizi wa awali chini ya mpango wa Gatoto Intergrated Development Programme kuondolewa. Mfanyakazi mmoja ambaye hakutaka kutajwa alisema kuna wasiwasi mkubwa kuhusu mishahara yao. Alisema walimu waliosajiliwa na TSC walifanya mkutano na mwalimu mkuu mpya na kuonywa dhidi ya kufanya maamuzi ya haraka ya kujiuzulu. “Hadi sasa, hatujui ni nani atatulipa, ingawa uongozi mpya umetuhakikishia. Ninajiuliza tu jinsi na lini nitapata mshahara wangu,” alisema mfanyakazi huyo. [caption id="attachment_166234" align="alignnone" width="640"] Baadhi ya wazazi na wakazi wakiandamana kupinga kugeuza shule hiyo na kuwa ya umma. Picha|Fridah Okachi[/caption] Mfanyakazi huyo alisema wasiwasi uliongezeka zaidi baada ya walimu watano kutumwa na TSC. “Walimu wawili tayari wameondoka bila hata kuwasilisha barua za kujiuzulu. Wengine wengi wanazingatia kuondoka,” aliongeza mfanyakazi mwingine. Suala lingine linaloisumbua shule ni ukosefu wa chakula cha kutosha kwa walimu na wanafunzi. Alibainisha mabadiliko makubwa ambayo yamewalazimisha walimu na wanafunzi kutegemea mgao mdogo wa chakula, ambao huenda ukaisha hivi karibuni. Hii ikitokana na magunia 50 ya mahindi yaliyosalia. “Sasa hakuna kiamsha kinywa kwa walimu na wanafunzi. Tunapata tu uji saa nne asubuhi na sehemu ndogo ya chakula aina ya githeri mchana,” alilalamika mfanyakazi huyo. Mabadiliko hayo yanaathiri wazazi na wanafunzi ambao walikuwa wakinufaika na ufadhili wa elimu chini ya GIDP. Ruth Ndunge, mama wa watoto sita, alieleza huzuni yake kuhusu jinsi ya kusomesha wanawe watatu ambao wako shule za sekondari. Alifichua watatu hao, walilipiwa karo baada ya kufanya vizuri katika mitihani yao ya shule ya msingi. [caption id="attachment_166236" align="alignnone" width="640"] Bango katika shule ya Jamii ya Gatoto, mtaa wa Mukuru. Picha|Fridah Okachi[/caption] “Watoto wangu hawajarudi shule kwa sababu hakuna mtu wa kulipa karo yao. Unaponiona nikilia, ni kwa sababu nimezidiwa na wasiwasi,” alitirirkwa kwa machozi. Mfaidi mwingine ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Maseno Bw Victor Achula. Bw Achula alilaumu hatua ya serikali ya kuchukua shule hiyo, akisema inaweza kuathiri ufadhili wa masomo yake. “Huu ni mwaka wangu wa tatu chuoni, lakini sasa sijui itakuwaje kwani waliokuwa wakilipa karo yangu tayari wamejiondoa,” alisema. Mwenyekiti wa bodi GIDP Bw Felix Mwangangi, alikosoa Wizara ya Elimu kufanya mabadiliko hayo bila kuwahusisha. “Wizara ya Elimu haikutuma mawasiliano rasmi kuhusu kuifanya shule kuwa taasisi ya umma. Shule kwa sasa ina wanafunzi 1,000, na akiba ya chakula kitadumu kwa wiki mbili pekee,” alisema. [caption id="attachment_166237" align="alignnone" width="640"] Lango kuu la Shule ya Jamii ya Gatoto, mtaa wa Mukuru, Embakasi Kusini, Januari 9, 2025. Picha|Fridah Okachi[/caption] Taifa Dijitali ilithibitisha kuwa shughuli za masomo zinaendelea kama kawaida chini ya uongozi mpya wa mwalimu mkuu Margret Kimani, ambaye anadai alitumwa na Tume ya Huduma za Walimu (TSC). Bi Kimani, aliyekataa kuzungumza zaidi, alisema shule iko imara. Chifu wa eneo hilo, Bw David Ndirangu, aliyempokea mwalimu mkuu mpya, alithibitisha kuwa shule sasa iko chini ya udhibiti wa serikali. “Kuna utawala mpya, na mambo bado yanatulia. Ninavyojua, serikali imetuma walimu saba. Serikali haiwezi kutoa fedha kwa miradi ya kibinafsi, kwa hivyo mwalimu mkuu mpya ameanza shughuli ya kufungua akaunti mpya,” alisema. Hata hivyo, Afisa wa Elimu wa Kaunti Ndogo ya Embakasi Kusini, Bi Mary Kimeu, alikataa kutoa maoni.
MGOGORO wa chuo kikuu cha Moi bado haujaisha huku Muungano wa Wahadhiri wa Vyuo Vikuu (UASU na vyama vya wafanyakazi wengine chuoni wakianza tena kususia kazi na kushutumu wasimamizi wa chuo hicho kwa kukosa kuheshimu mkataba wa kurejea kazini. Wakizungumza na wanahabari mjini Eldoret Jumatatu, Januari 13, 2025, maafisa wa UASU waliapa kurejea barabarani mara moja huku wakidai mshahara wao wa Desemba. "Tuliwasiliana na wasimamizi wa Chuo Kikuu cha Moi pamoja na maafisa wa wizara ambao walikubaliana kwamba wafanyakazi wa chuo kikuu cha Moi watalipwa mishahara yao ya Desemba leo la sivyo tunarudi mgomoni," alisema Dkt Busolo Wegesa Katibu Mkuu UASU chuo cha Moi. Dkt Busolo alishutumu chuo kikuu kwa mawasiliano duni ambayo yamechangia changamoto zinazokumba chuo hicho. Hata hivyo, Dkt Busolo alisema kulipa mishahara ya mwezi Desemba kutafungua njia ya majadiliano zaidi ili kubaini sababu ya kwa nini chuo hicho kimeshindwa kutekeleza makubaliano kati ya uongozi na UASU kuhusu jinsi ya kuanza tena kazi katika chuo hicho. "Tumezungumza na maafisa wa wizara ya elimu kuhusu jinsi ya kufanya kazi pamoja na usimamizi wa Chuo Kikuu cha Moi, na wakati wa majadiliano wizara ilikubali kuwa mishahara ya wafanyakazi wa chuo kikuu cha Moi itatolewa leo na mara tu tutakapolipwa hapo ndipo tutakapojua hatua inayofuata na jinsi ilivyo sasa hakuna kazi inayoendelea katika chuo hiki,” akasema Bw Wegesa. Maoni yake yaliungwa mkono na katibu wa KUSU tawi la chuo hicho Mary Chepkwemoi aliyesema kuwa wafanyakazi wa chuo hicho wamepoteza imani na usimamizi kutokana na kushindwa kwa chuo hicho kutimiza ahadi za awali. Bi Chepkwemoi alisema wafanyakazi wameapa kutorejea kazini hadi chuo kitekeleze vipengele vyote vya makubaliano ya kurejea kazini. "Kutokana na kutokuwa na imani na usimamizi wa chuo kikuu tunarejea kugoma na haswa ikiwa mshahara wetu wa Desemba hautawekwa katika benki zetu na zaidi ni lazima chuo kitekeleze fomula ya kurejea kazini kwa jumla," alisema Bi Chepkwemoi. Mwishoni mwa mwezi Novemba 2024, wafanyakazi wa chuo hicho walisitisha mgomo ambao ulikuwa umedumu miezi mitatu baada ya kuafikia mwafaka na utawala wa chuo hicho.
WIKI moja tu baada ya shule kufunguliwa kwa muhula wa kwanza, walimu wakuu wameanza kuwatuma nyumbani wanafunzi wenye masalio ya karo. Hii ni baada ya Serikali kukosa kutuma shuleni pesa za ufadhili wa shughuli za masomo, hali ambayo imewaacha walimu wakuu katika hali ngumu kuendesha shughuli za shule za umma. Maafisa wa Chama cha Walimu wa Shule za Upili (Kessha), wakiongozwa na mwenyekiti wa kitaifa Willy Kuria walisema wanachama wao hawana jingine ila kuwatuma nyumbani wanafunzi. Walimu wakuu walianza kufanya hivyo Ijumaa wiki jana wakisema hawana fedha za kuendeshea shughuli za masomo. “Hatukupewa pesa za kutosha mwaka jana… kulikuwa na upungufu wa Sh7000 kwa kila mwanafunzi. Na kila mwaka kumekuwa na upungufu wa kiasi sawa na hicho. Kwa miaka mitano sasa serikali tunaidai serikali jumla ya Sh64 bilioni kuashiria kuwa shule zinakabiliwa na mzigo wa madeni,” akasema Bw Kuria. Mwenyekiti huyo wa chama cha KESSHA alisema shule zilipofunga mwishoni mwa muhula wa tatu mwkaa jana, shule hizo hazikuwa zimewalipa Walimu walioajiriwa na Bodi za Shule, kutokana na ukosefu wa pesa. Kwa mfano, Shule ya Upili ya Murang’a yenye jumla ya wanafunzi 1, 800 inazongwa na mzigo wa deni la Sh20 milioni za malipo ya umeme, maji na vifaa vingine vya masomo ilivyowasilishiwa na wafanyabiashara kwa mkopo. “Madeni yetu yamekuwa yanaongezeka kwa sababu huwa tunalipa kidogo kidogo kutokana na changamoto za kifedha. Tumekuwa tukilipa baadhi ya madeni haya wanafunzi wa kidato cha kwanza wanaporipoti. Lakini serikali inapokosa kutoa pesa za ufadhili wa masomo, huku tukiwa hatujui ni lini pesa hizo zitatolewa nasi hatuna uhakika wa kulipa malimbikizi ya mishahara,” Bw Kuria akasema. Bw Kuria alisema, ambaye ni pia ndiye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Upili ya Murang’a alisema hali ni ngumu kwa sababu Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza hawakusajiliwa kutokana na mpango unaoendelea kuwa kuondolea mbali mfumo wa elimu wa 8-4-4 kutoa nafasi kwa mtaala wa Umilisi na Utendaji (CBC). Mwaka jana, 2024, hakukuwa na watahiniwa wa Mtihani wa Darasa la Nane (KCPE), ishara kwamba hakuwa na uteuzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu. Kundi la mwisho la wanafunzi waliofanya KCPE wako katika kidato cha pili mwaka huu. Mfumo wa Elimu wa 8-4-4 ulianzishwa 1985 ambapo wanafunzi walikuwa wakisoma kwa miaka minne katika shule za msingi, miaka minne katika shule za upili na miaka minne katika vyuo vikuu. Kinyume na mfumo huo, mtaala wa CBC unatilia mkazo zaidi ujuzi, unafuata mfumo wa 2-6-3-3-3. Kwa hivyo, mojawapo za sababu zinazochangia shule za upili kukumbwa na changamoto za kifedha ni ukosefu wa usajili wa wanafunzi wapya. “Shule za mabweni hutegemea usajiliwa wa wanafunzi wa kidato cha kwanza kupata pesa zaidi lakini mwaka huu hazijapata pesa hizo na ndio maana zinakumbwa na changamoto za kifedha,” Bw Kuria akaeleza. Alisema shule za upili za kutwa ndizo zimeathiriwa zaidi kwa sababu zinategemea fedha kutoka kwa serikali kuendeshea shughuli zao ikizingatiwa kuwa hazitozi karo zozote.

KUELEKEA kuanza safari ya mageuzi katika sekta ya elimu, Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua Sera ya Elimu…

UYUI, Tabora: WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) imeendelea na kampeni yake ya nyumba kwa nyumba ya kutoa elimu…
SASA watahiniwa ambao walikosa kufanya Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne (KCSE), kutokana na sababu mbalimbali, wataweza kuufanya mtihani huo katikati mwa mwaka. Hii ni baada ya Wizara ya Elimu kutangaza kuwa KCSE hiyo ya katikati mwa mwaka, itafanyika mwezi wa Julai. Akitangaza matokeo ya KCSE ya 2024, Alhamisi, Januari 9, 2025, Waziri wa Elimu Julius Migos Ogamba alisema hatua hiyo imechukuliwa kuimarisha ubora wa mfumo wa mitihani ya kitaifa. “Kuanzia mwaka huu, na baada ya kufanya mashauriano na wadau, ningependea kutangaza kuwa Baraza la Kitaifa la Mitihani Nchini (KNEC) limeanzisha mtihani wa KCSE ya katikati mwa mwaka utakaofanywa Julai kila mwaka,” akaeleza katika makao makuu ya KNEC, Nairobi. “Mtihani huo utalenga watahiniwa ambao wangependa kurudia KCSE baada ya kutoridhishwa na matokeo waliyopata na wale waliokosa kufanya mtihani huo baada ya kuugua au kukumbwa na changamoto zisizotarajiwa,” Bw Ogamba akaeleza. Waziri aliongeza kuwa KCSE hiyo ya katikati mwa mwaka pia inalenga watu wazima ambao wangetaka kupata cheti cha mtihani huo. Bw Ogamba pia aliongeza kuwa hatua hiyo inalenga kuwafaidi wanafunzi wenye mahitaji mbalimbali huku ikihakikisha kuwa wote wanapata elimu kwa usawa na urahisi. Katika miaka ya nyuma, watahiniwa waliokosa kufanya KCSE, baada ya kusajiliwa, kutokana na sababu mbalimbali katika vile ugonjwa, walilazimika kusubiri hadi mwaka unaofuatia kuufanya mtihani huo. Aidha, wale ambao walitaka kurudia KCSE baada ya kupata gredi isiyowaridhisha pia walilazimika kurudia masomo katika kidato cha nne na kuufanya mtihani huo mwaka mmoja baadaye. Kawaida, mtihani wa KCSE hufanywa mara moja mwishoni mwa mwaka.

DAR ES SALAAM: KATIKA kuboresha kiwango cha utoaji elimu na kutengeneza mazingira bora na rafiki ya kusomea na…

DAR ES SALAAMM; Lengo la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kufikisha elimu ya hifadhi ya…

WAZAZI katika Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara wametakiwa kuona umuhimu wa elimu kwa watoto kwa…

DAR ES SALAAM: MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amewataka wakuu wa shule za sekondari wilayani humo…

Ni Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ambapo leo January 6, 2024 imewatangazia wanafunzi wa stashahada watakaodahiliwa mwezi Machi (March Intake) kwamba dirisha la maombi ya mikopo ya stashahada litafunguliwa kuanzia tarehe 15/01/2025 hadi tarehe 15/02/2025. Wanafunzi wanaotarajia kuomba mikopo katika maeneo matano ya kipaumbele na wanafunzi wengine wenye udahili (admission) […] The post Dirisha La Maombi Ya Mikopo Ya Stashahada Kwa ‘March Intake’ first appeared on Millard Ayo.

DAR-ES-SALAAM : KATIBU Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa, amependekeza kuwa wafanyabiashara…
WAZAZI wengi wanakubali kuwa watoto wao wanakosa usingizi usiku na kudhani hii ni sehemu tu ya changamoto za makuzi yao. Lakini huu ndio ukweli: usingizi mzuri ni lazima kwa mtoto na unawezekana kwa kila mmoja na kuupa kipaumbele kunaweza kubadilisha maisha ya familia. Wataalam wa afya ya watoto wanasema usingizi sio tu 'kupumzika.' Kwa watoto, ni hitaji la kibayolojia ambalo huchochea ukuaji, ukuaji wa ubongo na utulivu wa kihisia. Hata hivyo, nchini Kenya, usingizi haujadiliwi kama sehemu muhimu ya afya ya mtoto. Wazazi ni wepesi kushughulikia lishe, elimu, na mazoezi, lakini usingizi mara nyingi hukosa katika orodha ya mambo muhimu kwa mtoto.Ukweli ni kwamba mtoto anayepumzika vizuri ni mtoto mwenye afya njema, mwenye furaha na anayefanikiwa zaidi—na wazazi wanaotanguliza usingizi wa watoto wao wanaboresha maisha yao wenyewe pia. Miaka ya kwanza ya maisha ya mtoto huwa ya maendeleo ya haraka ya kimwili, ya utambuzi, na ya kihisia, ambayo mengi hutokea wakati wa usingizi. Homoni za ukuaji hutolewa, ubongo huunganisha kujifunza na kumbukumbu, na mfumo wa kinga huimarishwa. Usingizi duni huvuruga michakato hii, na kusababisha masuala kama vile kuchelewa kukua, kuyumba kihisia, na kupunguza uwezo wa kujifunza. Mbali na kuathiri afya ya watoto, kukosa usingizi wa kutosha kuna athari mbaya kwa familia. Watoto wanaochoka mara nyingi huwa na hasira na hawana ushirikiano. Hili linaweza kuleta msongo wa mawazo kwa wazazi, kulegeza uhusiano na hata kusababisha uchovu. Usingizi mbaya kwa watoto ni tatizo ambalo linahitaji kushughulikiwa. Nchini Kenya, familia nyingi hukumbana na changamoto za kipekee kuhusu suala la usingizi wa watoto. Kulala chumba kimoja ni jambo la kawaida, na desturi za kitamaduni zimejikita sana. Ingawa hali hizi zinaweza kufanya kazi kwa wengine, mara nyingi husababisha usumbufu wa kulala kwa watoto na wazazi. Changamoto moja kuu ni ukosefu wa habari za kuaminika kuhusu usingizi. Wazazi wengi kwanza kurejea kwa madaktari wao wa watoto ili kupata mwongozo, ndipo wanagundua kwamba usingizi wa watoto haufai kupuuzwa kila wakati. Ingawa madaktari wa watoto ni muhimu kwa afya ya mtoto kwa ujumla, mara nyingi hawatoi mikakati ya kina, ya kibinafsi ya kulala ambayo familia zinazotatizika zinahitaji. Wakiwa wamechanganyikiwa, mara nyingi wazazi hutafuta ushauri kwa marafiki au watu wa familia, lakini ni nadra sana vidokezo wanazopata kutatua tatizo. Kinachofaa kwa mtoto mmoja huenda kisifanye kazi kwa mwingine, na kuwaacha wazazi wakihisi wamepotea zaidi. Wengine hugeukia mtandao kwa majibu, lakini ushauri unaweza kuwa mwingi na unaokinzana. Je, unapaswa kulala pamoja na mtoto au kuhimiza uhuru? Kufunza mtoto kulala ni ukatili au ni muhimu? Unajuaje kama matatizo ya usingizi ya mtoto wako ni ya kawaida au ni ishara ya tatizo kubwa zaidi? Usingizi mzuri sio bahati - ni kuhusu kuunda hali zinazofaa. Wazazi wanaweza kuanza kwa kutanguliza usingizi kwa njia ile ile wanavyotanguliza ulaji bora au mafanikio ya kitaaluma. [caption id="attachment_158474" align="alignnone" width="500"] Watoto wakifurahia. Picha|Hisani[/caption] Hapa kuna hatua chache muhimu kutoka kwa wataalamu wa afya ya watoto: 1. Weka utaratibu thabiti wa wakati wa kulala: Watoto husitawi wanapotabiri. Utaratibu wa utulivu wa wakati wa kulala kama vile kuoga kwa maji yenye joto, kusoma kitabu, na muziki wa kutuliza husaidia kuashiria kwamba ni wakati wa kupumzika. 2. Weka muda wa kulala unaolingana na umri: Watoto wadogo wanahitaji muda wa kulala mapema, mara nyingi mapema kati ya kumi na mbili na nusu na saa moja na nusu jioni. Kuchelewa kulala kwa watoto kunaweza kusababisha uchovu kupita kiasi, na kuifanya iwe ngumu kwao kutulia. 3. Unda mazingira ya kirafiki: Nafasi ya kulala inapaswa kuwa giza, tulivu na baridi kiasi. 4. Punguza muda wa kutumia vifaa vya dijitali: Mwangaza wa buluu kutoka kwenye skrini hukandamiza melatonin, homoni inayokuza usingizi. Zima vifaa angalau saa moja kabla ya kulala. Licha ya jitihada zao, wazazi wengi hujikuta wakipata shida kutekeleza mabadiliko haya au kutatua changamoto za usingizi kama vile kuamka mara kwa mara usiku au kuamka mapema. Hapa ndipo wataalamu wa usingizi wa watoto wanahitajika.“Kama mshauri wa masuala ya usingizi, mimi huwasaidia wazazi kuelewa mahitaji ya kipekee ya mtoto wao kulala na kutengeneza suluhisho inayofaa ambayo ina manufaa kwa familia. Hii sio kuhusu kuweka ratiba ngumu. Badala yake, inahusu kuwawezesha wazazi kwa maarifa na zana za kuunda tabia nzuri za kulala,” asema Dkt Mwende Kimweli, mwanasaikolojia na mtaalam wa afya watoto. Wazazi wanapotafuta usaidizi wa kitaalamu, mara nyingi hupokea mwongozo ulio wazi, unaotegemea ushahidi.“Tofauti na mapendekezo yasiyoeleweka kutoka kwa marafiki au ushauri mwingi mtandaoni, kufanya kazi na daktari hutoa mbinu mahususi zinazozingatia umri wa mtoto wako, hali ya joto na changamoto mahususi,” asema. Nchini Kenya, ambapo rasilimali za kulala kwa watoto bado ni chache, usaidizi wa kitaalamu unaweza kubadilisha hali. Kwa kutafuta msaada, wazazi wanaweza kutoka katika hali ya kukosa usingizi hadi kwenye mazoea ya amani katika muda wa majuma machache. Dkt Kimweli anasema shule, wahudumu wa afya na watunga sera wanahitaji kutambua jukumu muhimu la usingizi katika ukuaji wa mtoto. Kuelimisha wazazi kuhusu usafi wa usingizi na kuwasaidia kwa rasilimali ili kuimarisha afya ya umma. “Kwa wazazi, ujumbe ni rahisi: usingizi mzuri sio anasa-ni jambo la lazima. Kwa kutanguliza usingizi, haumsaidii mtoto wako kukua tu—unampa zana za kustawi kimwili, kihisia na kiakili.
UHABA wa vitabu vya shule za msingi unashuhudiwa nchini, baadhi ya wamiliki wa maduka ya vitabu wakisema walipokea asilimia 60 pekee ya mahitaji yao. Mkurugenzi wa duka la vitabu la Kimji Devshi, mojawapo ya wasambazaji Kaunti ya Nyeri, Bw Khilan Shah, alisema uhaba huo unawaathiri zaidi wanafunzi wa PP1 hadi Gredi ya 4. Alieleza kwamba uhaba huo unachangiwa na wachapishaji waliokabidhiwa kandarasi na serikali ambao wamechelewesha uchapishaji. “Vitabu havipatikani. Mzazi anaagiza vitabu 10 kwa darasa moja lakini tunapata vinne pekee. Bei ya vitabu vilivyoko iko juu, na hali hii inawaumiza wazazi ambao tayari wanakabiliana na gharama kubwa ya maisha,” alisema. Katika maneo mengi wauzaji vitabu walisema vitabu vya Gredi ya Tisa vipo lakini wanakumbwa na changamoto kupata vitabu vya Gredi ya kwanza hadi sita. Katika kaunti ya Murang’a, Mwenyekiti wa Kamati ya Seneti kuhusu Elimu, Bw Joe Nyutu, alisema wazazi wanapaswa kupewa muda wa kununua vitabu vya Gredi ya Tisa. “Ni kweli kuwa kufikia Jumapili, vitabu havikuwa vinapatikana kwenye soko. Serikali ilikosa sera na imeshangaza wadau wote kutokana na uhaba huo,” alisema Bw Nyutu. Mzazi kutoka Murang’a, Bi Elizabeth Soliyo alisema baadhi ya vitabu vinapatikana kwa bei ghali. Mfanyabiashara, Bw Martin Thuo, alisema kuna mkanganyiko kuhusu orodha ya vitabu vilivyoidhinishwa. IMETAFSIRIWA NA FRIDAH OKACHI
WAZAZI walio na wanafunzi katika shule 349 ambazo zilizuiwa kuwa za bweni, wametakiwa kuwahamishia katika taasisi nyingine za masomo kabla ya shule kufunguliwa Jumanne wiki ijayo kutokana na masuala ya usalama. Wizara ya Elimu iliwataka wazazi hao kuhakikisha watoto wao wanajiunga na shule tofauti baada ya ukaguzi uliofanywa kufuatia mkasa wa moto ulioua wanafunzi 21 kutoka shule ya Hillside Endarasha Academy miezi minne iliyopita kufichua masuala ya usalama katika shule hizo 349. Ukaguzi ulibaini kuwa shule nyingi za msingi za bweni zinakabiliwa na changamoto za kiusalama na miundombinu ambazo zinahatarisha maisha ya wanafunzi. Jumla ya shule 2,974 zilifanyiwa tathmini, ambapo 1,415 zilikuwa za umma na 1,659 za kibinafsi. Msongamano katika mabweni ulikuwa wa kawaida shuleni. Nafasi kati ya vitanda katika shule nyingi ilikuwa chini ya mita 1.2 kinyume na Mwongozo wa Viwango vya Usalama kwa Shule nchini Kenya (2008). Shule chache hazikuwa na walinzi/ walezi wa mabweni ya wavulana. Katika baadhi ya shule, matroni walipewa majukumu katika mabweni ya wanafunzi wa kiume. Katibu wa Elimu ya Msingi Belio Kipsang alisema serikali haitalegeza msimamo kuhusu agizo la kupiga marufuku baadhi ya shule kuwa za bweni. Alisema wazazi wa shule ambazo hazikidhi viwango vya usalama lazima wawahamishe wanafunzi hao. "Tuliambia taasisi ambazo hazikuwa zimejitayarisha vya kutosha kuwa na bweni kuacha hadi wakati huo zitakapojitayarishwa ipasavyo. Na kila shule hizo 349 ilipewa ripoti ya kueleza ilichohitaji kufanya," alisema Dkt Kipsang. Katika mahojiano na Taifa Leo, Dkt Kipsang alisema maafisa wa Wizara ya Elimu wamekagua tena baadhi ya shule. “Shule yoyote ambayo imekidhi kiwango cha maandalizi itaruhusiwa kuendelea, lakini zile ambazo haziko tayari, tumewaambia wazazi watafute shule mbadala kwa watoto wao na tumewapa muda wa kutosha, karibu miezi miwili," alisema. Dkt Kipsang alisema maafisa wa wizara kwa sasa wanajumuisha data kuhusu ni shule ngapi za bweni ambazo bado hazijatimiza viwango vya usalama. "Tuna mkutano wa wakurugenzi wetu wote wa kaunti ndogo, kaunti na maeneo leo, tutaweza kujua hali yoyote inayohitaji umakini maalum," alisema. Haya yanajiri huku wazazi wakiendelea kulalamika kuhusu hatua hiyo wakisema itakuwa changamoto na gharama kubwa kununua sare mpya, na huduma nyinginezo. Hata hivyo, Mwenyekiti wa Chama cha Kitaifa ya Wazazi Silas Obuhatsa alilaumu wazazi kwa kukosa kulazimisha bodi za usimamizi kuzingatia viwango vya usalama kabla ya shule kufunguliwa tena. IMETAFSIRIWA NA BENSON MATHEKA
OPERESHENI ya usalama katika eneo la Bonde la Ufa inayofahamika kama Maliza Uhalifu, imeangaziwa baada ya kundi la maafisa wa Huduma ya Vijana kwa Taifa (NYS) waliohusishwa kujenga shule kulalamikia kukosa kulipwa. Vijana wasiopungua 50 wa NYS wanadai jumla ya Sh3 milioni ambazo ni malimbikizi ya marupurupu yao ya miezi minne. Operesheni Maliza Uhalifu (OMU) ilizinduliwa 2013 kuangazia ukosefu wa usalama katika kaunti za Turkana, Pokot Magharibi, Elgeyo Marakwet, Baringo, Laikipia na Samburu. Iliongozwa na kikosi kinachojumuisha KDF, GSU, ASTU, polisi wa kawaida na NPRS. Maafisa hao waliojumuishwa kwenye operesheni hiyo Februari 2023, wamelalamikia kukosa kulipwa na kuongezewa muda wa kandarasi kinyume na maafikiano. Akizungumza na Taifa Leo, afisa mmoja kutoka Nakuru alifichua walihusishwa kwenye operesheni hiyo kama maafisa wenye ujuzi ili kusaidia jeshi la KDF katika ujenzi wa shule Baringo, kama sehemu ya kuzima shughuli za majangili eneo hilo na kuanzisha maendeleo. Kundi la kwanza la makurutu wa NYS lilitumwa eneo hilo kutoa huduma mbalimbali ikiwemo waashi, fundi wa mifereji, kazi za stima na nyinginezo. Afisa huyo alisema walistahili kufanya kazi kwa miezi mitatu kwa mkataba wa kulipwa marupurupu ya Sh15,000 kila mwezi. “Tulikuwa bado tunasubiri kuelekea katika maeneo yetu ya mafunzo baada ya kukamilisha mitihani yetu tulipopokea jumbe kupitia simu na kutuagiza kurejea chuoni. Tulitumwa katika operesheni kaunti hiyo ambapo KDF ilikuwa inajenga shule,” alisema afisa huyo. Waliporejea vituoni, afisa huyo alisema wahudumu wa NYS walikuwa wameitisha malipo ya Sh1,000 kila siku lakini maafisa wasimamizi wakawashawishi kuchukua nusu ya kiasi hicho. Alidai walipokea malipo ya kwanza baada ya kufanya kazi kwa miezi miwili yaliyotumwa kwa pamoja katika akaunti zao za benki mtawalia. Nakala zilizofikia Taifa Leo zinaonyesha maafisa hao walitumwa kujenga shule mbalimbali ikiwemo shule za msingi za Chesitet, Chepkesin, Kositei, Koloa, Kapindasum, Arabal, Pura, Mukutani, Sambalat, Lomelo, Chemoril na shule ya sekondari ya Kapedo. Tuliwasiliana na KDF kuhusu suala hilo lakini wakajitenga na shutuma hizo wakidai hawawajibiki kwa malalamishi ya maafisa husika.
HALI tofauti kabisa inawasubiri wazazi, shule na biashara zinazoendeshwa katika sekta ya elimu, wanafunzi watakaporejea shuleni kwa muhula wa kwanza Jumatatu, Januari 6. Kwa mara ya kwanza tangu 1985, hakutakuwa na usajili wa wanafunzi wa Kidato cha Kwanza 2025 huku mtaala wa CBC ukiingia awamu mpya baada ya mfumo wa awali wa 8-4-4 kuvunjiliwa mbali katika shule za msingi.Hakukuwa na usajili wa wanafunzi wa kidato cha kwanza 1985 baada ya muda wa elimu ya shule ya msingi kuongezewa kutoka miaka saba hadi minane, 8-4-4 ilipoanzishwa. Darasa la Nane la mwisho liliondoka shule ya msingi 2023 ambapo 2024 hakukuwa na mitihani ya Darasa la Nane (KCPE).Kundi la kwanza la CBC litajiunga na Gredi 9, ambalo ni darasa la mwisho la sekondari ya msingi iliyopo katika shule za msingi. Kutokana na hali hii, shule za sekondari zinatazamiwa kupoteza mabilioni ya fedha ambazo zimekuwa zikipokea chini ya mpango wa Elimu ya Kutwa ya Sekondari Bila Malipo (FDSE) kwa sababu zitakuwa na upungufu wa darasa moja. Kila mwanafunzi hugawiwa Sh22,244 kila mwaka za kugharamia masomo.Isitoshe, shule kadhaa zitasalia na nafasi tupu zisizotumika hali inayosubiriwa kwa hamu kufuatia malalamishi kuhusu msongamano katika shule za sekondari tangu sera ya kusajili wanafunzi wote ilipoanzishwa 2014. Hata hivyo, walimu wakuu wa shule za msingi sasa watasimamia mabilioni yaliyotengewa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za msingi. “Mambo yatabadilika sana hasa kibiashara. Kama fundi anayeunda masanduku ya shule, nimelazimika kubadilisha mbinu ya mapato kutokana na ukosefu wa biashara. Niliamua kujipanga mapema nikijua hakutakuwa tena na wanafunzi wa Kidato cha Kwanza, kwa hivyo ninaunda stovu badala yake,” anasema mfanyabiashara wa Kisumu, Richard Omollo.

PWANI: WILAYA ya Mkuranga imetajwa kupiga hatua kubwa katika sekta ya elimu, ambapo idadi ya shule za msingi…

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Wilaya ya Ruangwa imepiga kasi kubwa ya maendeleo ambayo imewawezesha wakazi wa Wilaya hiyo kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za kiuchumi. Amesema kuwa Wilaya hiyo changa ilikuwa na changamoto nyingi kwenye Sekta ya Elimu, Afya, Kilimo, Miundombinu ikiwemo barabara, maji, Umeme, Uwekezaji na hata kwenye michezo “Changamoto hizi zilitufanya […] The post Rais Dkt. Samia anamchango mkubwa kwenye Maendeleo Ruangwa first appeared on Millard Ayo.
HUKU shule zikikaribia kufunguliwa, wazazi na walimu wanakumbwa na changamoto kufuatia kucheleweshwa kwa orodha ya vitabu vilivyokubaliwa rasmi kutumika kuanzia darasa la tano hadi la nane. Wazazi hao wanahofia kucheleweshwa huku na Taasisi ya Ukuzaji Mtaala (KICD), kunaaathiri kujiandaa kwa watoto wao kabla ya muhula mpya kuanza, huku nao wakikabiliwa na changamoto za kifedha. “Hatuelewi. Tunatarajiwa vipi kupanga masomo ya watoto wetu bila orodha ya vitabu?” mzazi mmoja aliuliza. Wazazi wengi hununua vitabyu wakati wa likizo. Mtaala wa Elimu na Utendaji (CBC) unategemea vifaa rasmi vya masomo ili kufanikisha malengo yake kwa wanafunzi. Bila vitabu, walimu wanakosa mwongozo wa kufanikisha ratiba za masomo, hali inayoweza kuathiri mafunzo shuleni. Wazazi hao wanahofia kuwa KICD inahatarisha elimu ya watoto, hasa wakati nchi inakumbwa na changamoto za katika utekelezaji wa CBC. Kucheleweshwa huku pia kumeziacha shule nyingi zikiwa hazijaweza kujiandaa ipasavyo, hali inayotishia kuvuruga ratiba za masomo shule zitakapofunguliwa. Wakuu wa shule wameelezea wasiwasi wao, wakionya kwamba bila kupatikana kwa vitabu vilivyokubaliwa kwa wakati, shughuli za kufundisha na kujifunza zitakumbwa na changamoto kubwa. “Hili ni kosa kubwa. CBC inategemea mwongozo uliopangiliwa vizuri, na bila vifaa hivi, tunaanza muhula kwa njia ambayo si dhabiti,” alisema mkuu mmoja wa shule. Hata hivyo, KICD imekanusha madai ya kuwa imechelewa kutoa vitabu, ikisema vitabu vinapatikana shuleni na katika maduka ya kuuza vitabu. Mkurugenzi wa KICD Prof Charles Ong’ondo, alisema vitabu vya masomo yote kuanzia masomo ya chekechea hadi darasa la tisa vipo tayari tena madukani. Lakini alikiri kuwa vitabu vya masomo ya Kilimo, Sanaa za Ubunifu, na Mafunzo ya kiufundi kwa darasa la saba na nane vilikamilishwa Desemba hii. "Vitabu hivi bado havijachapishwa, lakini vinatarajiwa kwenye maduka ifikapo Februari 2025," akasema. Prof Ong’ondo alieleza kuwa kuchelewa huko kulitokana na mchakato wa kuboresha mtaala kufuatia ripoti ya Kamati ya Rais ya Marekebisho ya Elimu iliyotolewa Agosti 2023. Kwa sasa, kuna upungufu wa vitabu vya lugha ya Kifaransa katika shule zote nchini, baada ya serikali kupeana mkandarasi biashara ya kuchapisha vitabu milioni moja vya Kifaransa ambavyo havikua vinahitajika shuleni. Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, Bi Nancy Gathungu, alisema matumizi ya fedha kwa vitabu hivi hayakuzingatia thamani yao. Hata hivyo, Prof Ong’ondo alieleza kuwa Kifaransa na lugha nyingine za kigeni si somo la lazima kwa madarasa ya kwanza hadi tisa. Shule zinazofundisha masomo haya zimeombwa kutoa taarifa kwa KICD ili kusaidia kupanga usambazaji wa vitabu.

Wanawake na Wafanyakazi wa mkoa wa Dar es salaam kupitia wilaya ya Ubungo wametakiwa kuendelea kujiunga kwenye Vyama mbalimbali vyenye kutoa fursa mbalimbali ikiwepo kupata elimu namna ya kujikomboa na kuweza kutatua changamoto mbalimbali zikiwemo za kiuchumi na kijamii. Kauli hiyo imesemwa leo na Mwenyekiti wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi wilaya ya Ubungo na […] The post Wanawake Wafanyabiashara na Wafanyakazi wamekutana na kujadili kukuza uchumi wao first appeared on Millard Ayo.

Mamlaka ya mapato Tanzania TRA Mkoa wa Tanga imewatembelea na kutoa shukrani kwa walipa Kodi upande wa Shule za sekondari wilayani Lushoto Mkoani hapa. Akizungumza mara baada ya kuwatembelea walipa Kodi wa Shule ya Sekondari Mazinde Juu na Shule ya Sekondari Kifungiro Girl’s Naibu Kamishna Huduma wa za Kiufundi TRA Bw.TedFrank Sirlikuwasha ambaye amemwakilisha Kamishna […] The post “TRA Mkoa wa Tanga wawapongeza walipa Kodi wa Shule na Vinywaji” first appeared on Millard Ayo.