Maofisa wapewa elimu ya uchaguzi

Habari Leo
Published: Jan 17, 2025 12:26:56 EAT   |  Educational

MAOFISA Uchaguzi mkoani Mtwara wamepatiwa mafunzo juu ya uendeshaji na usimamizi wa zoezi la uboreshaji wa daftari la…

The post Maofisa wapewa elimu ya uchaguzi appeared first on HabariLeo.

MAOFISA Uchaguzi mkoani Mtwara wamepatiwa mafunzo juu ya uendeshaji na usimamizi wa zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linalotarajiwa kuanza mkoani humo Januari 28, 2025 na kumalizika Februari 3, mwaka huu.

Akizungumza leo mkoani Mtwara wakati wa mafunzo hayo,  Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Rufani, Jacobs Mwambegele amesema ni matarajio ya tume kipitia mafunzo hayo kila mmoja wao atapata ujuzi wa kutosha kutekeleza majukumu hayo.

Aidha mafunzo hayo yamehusisha namna ya ujazaji wa fomu pamoja na matumizi ya mfumo wa kuandikisha wapiga kura ili kuwezesha uelewa wa pamoja utakaowapa fursa ya kutumiwa kwa ufasaha mfumo huo pamoja na vifaa vingine vya kuandikisha wapiga kura.

“Nawasihi muwe na ushirikiano mzuri na wa karibu na tume wakati wote mtakapokuwa mnatekeleza majukumu yenu na ikiwa mnahitaji ufafanuzi au maelekezo yoyote  msisite kuwasiliana na tume,”amesisitiza Mwambegele.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Ofisa Mwandikishaji kutoka Jimbo la Newala Vijijini Magreth Liponda amesema wamejiandaa vizuri kulipokea zoezi hilo na kulifanikisha kwa kiwango kikubwa ikiwemo kuhamasisha wananchi ili wajitokeze kwa wingi katika zoezi hilo.

Ofisa mwandikishaji kutoka Jimbo la Nanyamba, Zefrin Mwende “Mafunzo tumeyapokea vizuri na tunaahidi kwenda kulitekeleza vizuri  sana”

Aidha mafunzo hayo yamehusisha mratibu wa uandikishaji mkoa wa mtwara, maofisa waandikishaji, maofisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya jimbo, maofisa uchaguzi,  maofisa ugani na maofisa TEHAMA wa halmashauri.

Aidha zoezi hilo linaenda sambamba na kauli mbiu inayosema ‘Kujiandikisha kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora’.

The post Maofisa wapewa elimu ya uchaguzi appeared first on HabariLeo.