BARAZA la Kitaifa la Mtihani Kenya (Knec) limetangaza kuanza kwa usajili wa watahiniwa wa Gredi 6, kuanzia Januari 27 hadi Februari 28, 2025.
Watahiniwa wa Gredi 6 hufanya Tathmini ya Elimu ya Shule ya Msingi Kenya (KPSEA) mwishoni mwa shule ya msingi, kabla ya kujiunga na shule ya Sekondari Msingi.
Katika taarifa, Afisa Mkuu Mtendaji wa Knec David Njengere alisema kuwa watahiniwa lazima watimize vigezo vyote.
Alionya kuwa kusajili watahiniwa hewa ni kosa, jambo ambalo linaweza kusababisha kufutwa kwa usajili wa shule zinazohusika.
"Wanafunzi wote walio katika Gredi 6 watasajiliwa upya kwa tathmini hiyo kupitia tovuti ya usajili ya KPSEA ambayo itafikiwa kati ya Januari 27 na Februari 28 2025," alisema.
Wanafunzi katika Gredi 6 wanahitajika kujiandikisha kwa KPSEA, tathmini iliyoundwa ili kutathmini umahiri wao kabla ya kujiunga na Sekondari Msingi.
Mchakato huo unahusisha kuthibitisha maelezo muhimu, ikiwa ni pamoja na majina, vyeti vya kuzaliwa na hati nyingine muhimu, ili kuhakikisha usahihi wa usajili.
“Marekebisho ya data ya wasifu wa mtahiniwa lazima yafanywe wakati wa usajili ili kuhakikisha usahihi wa habari zilizowasilishwa ikiwa ni pamoja na mpangilio sahihi wa majina ya wanafunzi kama yalivyoandikwa katika vyeti vyao vya kuzaliwa, jinsia, mwaka wa kuzaliwa, uraia, chaguo la elimu ya dini na wenye mahitaji maalum na walemavu,” alisema.
Dkt Njengere pia aliagiza uhamisho wa watahiniwa ukamilishwe kabla ya kufungwa kwa tovuti ya usajili mnamo Februari 28, 2025, ili kuhakikisha mchakato wa usajili unafanyika kwa uwazi.
"Hakuna uhamisho utakaoruhusiwa baadaye, zaidi mchakato wa uhamisho lazima ufanyike mtandaoni, ili kuepuka kurudiwa kwa watahiniwa,” alisema.
Zaidi ya hayo, alisema kuwa shule zilizo na watahiniwa chini ya watano hazitaruhusiwa kusajili watahiniwa wa KPSEA 2025 kama vituo huru.
“Shule zilizo na chini ya wanafunzi 5 hazitaruhusiwa kusajili watahiniwa wa KPSEA 2025 kama vituo huru vya kutathmini. Shule kama hizi zinashauriwa kuwasiliana na wakurugenzi wa elimu wa kaunti zao ili kutambua vituo vya kutathmini vya Knec vilivyo na zaidi ya watahiniwa 5 kwa usajili wa wanafunzi wao,” akasema.
IMETAFSIRIWA NA BENSON MATHEKA
KNEC yaanza kusajili watahiniwa wa KPESA, na haya ndiyo masharti
This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
EducationalTinubu: No student will be denied university education over poverty
Urges graduates to be creative, enterprising By Dayo Johnson, Akure President Bola Tinubu has assured Nigerians that no student will be denied access to tertiary education because of financial constraints. The President gave the assurance at the 37th convocation ceremony of the Federal University of Technology, Akure (FUTA), where he said the establishment of the […]
EducationalSEQUIP ilivyomfikisha Neema chuo kikuu
MBEYA: Serikali kupitia Mradi wa Kuinua Elimu ya Sekondari (SEQUIP) imeendelea kutoa fursa kwa wasichana waliokatisha masomo kutokana na changamoto mbalimbali za maisha kurejea shuleni na kuendeleza ndoto zao za elimu. Miongoni mwa wanufaika wa fursa hiyo ni Neema Andrea Usia, ambaye safari yake ya elimu ilikatizwa akiwa kidato cha pili, lakini kupitia fursa ya…
Educational892 graduates of CUHAS cadre pledge to observe ethics, dignity
MWANZA: 892 graduates of the Catholic University of Health Sciences Bugando (CUHAS) have been instructed to adhere to ethics, dignity and integrity in the provision of health services. The call was made today by the Bishop of the Catholic Diocese of Rulenge-Ngara, Mr Severine Niwemugizi, during the 19th graduation of the college held in Mwanza,…
EducationalChuka University graduate sits by himself, breaks down after no one shows up for his graduation
A Chuka University graduand broke down in tears after spending graduation day alone, as footage of him packing away a gown moved thousands of Kenyans online.