Kamati yajadili upatikanaji vitabu vya kufundishia, kujifunzia
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo ikiongozwa na Mwenyekiti Husna Sekiboko imekutana na Uongozi…
The post Kamati yajadili upatikanaji vitabu vya kufundishia, kujifunzia appeared first on HabariLeo.
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo ikiongozwa na Mwenyekiti Husna Sekiboko imekutana na Uongozi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na kujadili hali ya upatikanaji wa vitabu vya kufundishia na kujifunzia.
Wizara imetoa taarifa ya hali ya uchapaji na usambazaji vitabu, mafanikio na changamoto zilizojitokeza na hivyo Kamati kuagiza wizara kuangalia namna bora ya kuondoa changamoto ili vitabu vipatikane kwa wakati.
Viongozi wa Wizara walioshiriki kikao hicho ni Naibu Waziri, Omari Kipanga, Naibu Katibu Mkuu Dk Charles Mahera na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Elimu Tanzania, Dk Aneth Komba.
The post Kamati yajadili upatikanaji vitabu vya kufundishia, kujifunzia appeared first on HabariLeo.